Agano la kale lina jumla ya mistari 23,145, na mistari 7957 kwenye agano jipya. Kuleta jumla ya mistari 31,102 kwa biblia nzima.
Ambapo tukileta katika eneo la wastani ni sawa na kusema biblia ina mistari 26 kwa sura.
Washirikishekishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia ina sura na milango mingapi?
Je kumwimbia Mungu kwa kucheza ni sahihi kibiblia?
Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Rudi Nyumbani
SWALI:Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini?
Tunaona Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili, Mungu alimpa adhabu kwa kumwambia maneno haya;
Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Lakini tukiendelea kusoma tunaona, Kaini anamlilia Mungu na kumwambia adhabu yangu ni kali sana, haichukuliki, kila mahali nitakapoenda nitakuwa mtu wa kuuliwa, ndipo Mungu akamuhakikisha ulinzi kwa kumwekea alama. Kama tunavyosoma kwenye vifungu vinavyofuata;
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga
Swali linakuja hii alama ni ipi?
Lakini kabla ya kufahamu alama yenyewe ni nini ni vizuri ukaelewa maana ya adhabu aliyopewa ya kuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Fungua hapa ufahamu tafsiri yake >>>> UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.
Hivyo tukirudi kwenye swali alama ni ipi?
Zipo nadharia nyingi, lakini tujifunze kwanza baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa adhabu ile Kaini aliitambua kabisa ilihusu kutengwa na fadhili na uso wa Mungu kabisa. Na mahali popote pasipo na mkono wa Mungu hapana usalama wowote, ni sawa na mwili unaokosa kinga, kila ugonjwa unaopita pale utaushambulia, hata yale maradhi madhaifu kabisa,. Ndicho alichokigundua Kaini alijua pasipo Mungu duniani hata kwa sehemu ndogo, haiwezekaniki kuishi, chochote chenye uhai atakuweza tu, wanyama watakuweza, mapepo yatakuweza. Ndio maana ya kauli yake hiyo ‘kila anionaye ataniua’.
Lakini Mungu akamuhakikishia usalama, kwa kumwekea alama, ili yoyote akimwona asimuue Kaini. Sasa kufikiri alama hiyo ni mchoro(tattoo) Fulani mwilini, si rahisi kumfanya mtu asidiriki kumuua, kwani mchoro hauzuii mtu kuangamizwa.
Lakini kufikiria alama iliwekwa katika eneo la ki-mwonekano (ukubwa), au eneo la kuongezewa sifa/ufanisi Fulani uliotofauti na wengine yaweza kuwa jambo la kweli.
Kwanini?
Tunaweza kuona baada ya pale sifa za uzao wa Kaini jinsi zilivyokuwa, walikuwa ni watu wavumbuzi, watu wa elimu (Mwanzo 4:20-22) lakini pia Hodari na wengine wao wenye maumbo makubwa (Mwanzo 6:4),. Kwahiyo sikuzote tunafahamu hata sasa walio na uwezo mkubwa wa kielimu na kiteknolojia si rahisi kuwaweza kivita, hata iweje. Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, walikuwa ni wakulima tu na wafugaji. Hawakuwa na ujuzi mwingi ijapokuwa walikuwa ni uzao wa Mungu.
Kwahiyo wana wa Kaini, waliitawala dunia, hawakuwa watu dhaifu dhaifu, na yoyote ambaye angejaribu kumuua mmojawapo, kisasi kingemrudia mara saba, kwa nguvu tu walizokuwa nazo, ijapokuwa hawakuwa na Mungu maishani mwao.
Si jambo la ajabu Mungu kumuhakikisha ulinzi mtu mwovu, leo hii wengi watasema Bwana mbona wenye dhambi ndio wanaofanikiwa, mbona waovu ndio wenye nguvu duniani, wapo salama, ndio wenye mavumbuzi makubwa. Fahamu kuwa hiyo ni alama yao. Ambayo ilianzia tokea mbali kwa Kaini. Kwasababu wangekuwa waovu, halafu pia wanyonge, wangeishije kwenye hii dunia.
Kamwe usiitamani alama ya Kaini, usitamani kulindwa ndani ya uovu, kwasababu utadumu kwa kitambo tu, baadaye utaangamizwa kama ilivyokuwa kwa hawa, katika gharika. Yesu alitoa mfano wa magugu na ngano katika shamba, kama tunavyoifahamu ile habari, wale wakulima walitaka kwenda kuyang’oa magugu shambani ili waziache ngano. Lakini mwenye shamba akasema waache vyote vikue pamoja mpaka siku ya mavuno, ndipo yatakusanywa na kutupwa motoni.
Na tafsiri ya mfano ya ule mfano akasema shamba ni ulimwengu, na ngano ni wana wa ufalme, lakini magugu ni wana wa ibilisi, na wavunaji ni malaika. Kuonyesha duniani yapo mapando ya aina mbili, na yote yatashiriki mbolea, maji, matunzo yote kutoka kwa Mungu, na kimsingi magugu huwa ndio mepesi kustawi kwa haraka kuliko ngano.
Jiulize na wewe ambaye unastarehe katika dhambi na hauoni madhara yoyote, unaelekea wapi? Hujui umetiwa alama kwa muda, nguvu zako, utajiri wako, mafanikio yako, zaidi ya watu wa Mungu, usidhani ndio umebarikiwa unathamini na Mungu. lakini wakati utafika kuzimu utaiona. Embu kubali sasa kuwa mwana wa ufalme, kwa kumaanisha kutubu dhambi, na kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili akuondolee deni la dhambi uwe mtakatifu mbele zake kwa damu yake, akuepushe na hukumu inayokuja .
Ikiwa upo tayari kuokoka leo. Fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Nitamjuaje nabii wa Uongo?
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.(Opens in a new browser tab)
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Mithali alikuwa nani?
Sulemani mwana wa Daudi, anajitaja mwenyewe kama mwandishi, katika mwanzo kabisa wa kitabu hiki
Mithali 1:1 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu
Kitabu hichi kinakadiriwa kuandikwa miaka mia tisa (900) kabla ya Kristo.Ni kitabu kilichojaa maneno ya hekima na kanuni, maagizo ya rohoni, vilevile maonyo mbalimbali yanayohusiana na maisha ya kawaida, pamoja na maarifa na mafunzo yaliyo katika vitu vya asili.
Mithali 1-22:16, Iliandikwa na Sulemani mwenyewe.
Kuanzia Mithali 22:17-24:34, zilizojulikana kama kitabu cha Tatu, huwenda ziliandikwa na wengine lakini zikakusanywa na Sulemani mwenyewe.
Lakini Kuanzia Mithali 25-29, biblia inatuambia ziliandikwa na Sulemani, lakini watu wa mfalme Hezekia ndio waliozirekodi.
Na Mithali 30, Ambacho hujulikana kama kitabu cha Tano. Kiliandikwa na Aguri bin Yake.
Lakini Mithali 31 ambacho ni cha mwisho, kiliandikwa na mfalme Lemueli.
Japo wanazuoni wengine husema Aguri bin yake na Lemueli, yalikuwa ni majina mengine ya Sulemani.
Kwa vyovyote, kitabu hichi kwa sehemu kubwa kimeandikwa na Sulemani. Ndio maana hujulikana kama kitabu cha Sulemani. Lakini pia hatuna uhakika asilimia zote hekima zote ziliandikwa na yeye mwenyewe, kufuata na hao watu wawili wa mwisho wasiojulikana.
Kwa urefu wa chambuzi wa kitabu hichi fungua link hii >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Hizi ni baadhi ya fafanuzi ya hekima tuzisomazo katika kitabu hicho
Maana ya Mithali 21:17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;
Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;
Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;
Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?
Nini maana ya Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;
Je! Sulemani alienda mbinguni?
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Wafalme alikuwa nani?
Biblia haijaweka bayana aliyekuwa mwandishi wa kitabu hiki, lakini kufuatana na hadithi za kiyahudi huaminika kuwa nabii Yeremia ndiye alikuwa mwandishi wa vitabu hivi viwili vya wafalme.
Kitabu hichi kinaeleza kwa kina tawala za kifalme Kuanzia Mfalme Sulemani, na kugawanyika kwa taifa la Israeli pande mbili, hadi kuanguka kabisa kwa taifa lote la Israeli kwa kuchukuliwa utumwani Ashuru na Babeli. Miongoni mwa Wafalme wapo waliosimama vema, lakini pia wapo wengi waliolikosesha taifa la Israeli, Wa kwanza alikuwa ni Yeroboamu ambaye ndiye aliyeupokea ufalme uliogawanyika yeye aliunda sanamu na kuzisimamisha kaskazini na kusini mwa Israeli, ili waisraeli wakamwabudu Mungu huko. Machukizo ambayo yaliendelea hivyo kwa muda mrefu, ijapokuwa zilikuja kuondolewa hizo sanamu na mfalme aliyeitwa Yosia, lakini bado hasira ya Mungu haikupoa kwa mambo mengi mabaya waliyokuwa wanayatenda wana wa Israeli, Hadi walipofikia hatua ya kuhamishwa.
Kwa urefu wa uchambuzi wa vitabu hivi waweza fungua hapa upate kujisomea >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Je! Wewe umepokea wokovu wa Roho yako kwa Kristo Yesu? Kama ni la! Basi wakati ndio huu wa kufanya geuko la dhati, moyoni mwako. Ikiwa upo tayari basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.
Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).(Opens in a new browser tab)
WhatsApp
Mwandishi wa kitabu cha Filemoni
Kitabu cha Filemoni ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika akiwa kifungoni Rumi. Waraka huu alimuandikia Filemoni mtu ambaye alimgeuza yeye mwenyewe katika injili yake. Baadaye akawa mtendakazi katika utumishi wa Bwana, katika nyumba yake mwenyewe. Na kuwa Baraka kwa watakatifu wengi huko Kolosai.
Filemoni 1:2 “na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako”
Kilichomsukuma hasaa mtume Paulo kuandika waraka huo ilikuwa ni kwa mtendakazi wake mpya aliyemzaa katika Kristo aliyeitwa Onesmo ambaye hapo mwanzo alikuwa ni mtumwa wa Filemoni aliyemwibia vitu vyake na kukimbia. Kwamba sasa ampokee na kumchukulia kama mtendakazi mwenzao, kwasababu ametubu na anafaa kwa utumishi. Kwa urefu wa mafunzo yaliyo ndani ya kitabu hichi cha Filemoni, Fungua hapa, ujifunze kwa kina >>>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.
Je! Umempokea Kristo maishani mwako?
Kama ni la! Basi wakati ndio huu, bofya hapa kwa mwongozo wa namna ya kumpokea Kristo maishani mwako. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)
Kijeshi kushindwa kumtambua adui yako mpaka adui yako anajitambulisha kwako tena mbele ya macho yako ni ishara kubwa ya kushindwa mapambano.
Ndivyo ilivyokuwa kwa wale askari, walipofika na ujasiri wao mwingi, wakiwa na wazo la kumkamata mlengwa wao, tunaona mambo yalikuwa ni tofauti, kwasababu viashiria na matarajio yaliyokuwa kichwani mwao, hayakuweza kumfunua ni nani miongoni mwao ndiye mlengwa, huwenda wengine walidhani hayupo amekimbilia mapangoni kama Daudi. Lakini Yesu baada ya kuona wanahangaika sana ndipo akawauliza mnamtafuta nani.. Na wao kwa ujasiri wakajibu Yesu Mnazareti.. Yesu akasema ni mimi hapa! Tusome;
Yohana 18:3-8
[3]Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
[4]Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta?
[5]Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
[6]Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.
[7]Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.
[8]Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
Hivyo kibinadamu kwa taarifa hizo za ghafla nguvu lazima zikuishie, na kunyong’onyea ujikutapo kwenye mazingira kama hayo. Ni mfano tu wa ile habari ya Elisha (2Wafalme 6:8-23), Mfalme wa Shamu alituma majeshi kwenda kumkamata kwasababu alikuwa anatoa siri za ufalme wake kwa mfalme wa Israeli. Na hiyo ikapelekea washindwe sana mbele ya wayahudi. Lakini tunaona walipomfuata Elisha, alimwomba Mungu jeshi zima lipigwe upofu wasimtambue. Ndipo Elisha akalipeleka hilo jeshi katikati ya mji. Na baadaye akaomba wafumbiliwe macho, wakafumbuliwa wakagundua kumbe adui yao ndiye aliyekuwa kiongozi wao wa mbele.
Nguvu ziliwaishia kujikuta katikati ya maadui zao, wakifahamu kinachofuata ni kifo. Lakini Elisha hakuagiza wauliwe, bali aliwaombea kwa mfalme wapewe chakula wale wanywe kisha waondoke. Ndipo walipoondoka, hawakurudi tena kuwasumbua Israeli kwa kipindi kirefu. Kwasababu waliwapaliwa makaa ya moto kichwani.
Inamfunua Kristo kwa wakati ule, maadui zao walipofika pale bustanini, hakuwaua kwasababu alikuwa na uwezo huo, lakini alipokatwa sikio, mmojawapo wa wale askari alikuwa radhi kumponya, (kumfanyia huduma).
Na zaidi sana alikuwa tayari kuondoka na wale askari kuuawa nao, jambo ambalo Elisha hakufanya. Ili tu yeye afe taifa zima lipone..ni upendo wa namna gani huu usioweza kuelezeka aliuonyesha!.
Na kwa kifo chake hawakupona wayahudi tu, bali mpaka ni sisi watu wa mataifa kwa vizazi vyote, tumepona. Utukufu na heshima ni zake milele na milele.
Kwa hitimisho ni kuwa wale askari waliorudi nyuma wakaanguka chini, haikuwa bure hure, yote hiyo ilikuwa ni kufuatana na mwitikio wa Yesu kwao ambao hawakuutazamia.
Ni kutufundisha kuwa mawazo ya Mungu, sio mawazo yetu, rehema zake na fadhili zake na huruma zake ni nyingi kiasi ambacho kinaweza kumfanya mwanadamu aanguke na kutetemeka, kwa mwitikio wake mkuu wa upendo kwa wenye dhambi.
Je! Umempokea Kristo? Kumbuka lengo lake ni kukuvuta ili usiangukie hukumu. Okoka leo
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)
Waraka wa kwanza na ule wa pili wa timotheo,mtume Paulo aliuandika akiwa gerezani kama mfungwa Rumi.
Kwa urefu wa maelezo ya nyaraka Paulo alizoziandika akiwa gerezani, fungua hapa >>> Je ni nyaraka zipi mtume Paulo aliziandikia gerezani?
Lakini swali linakuja je Timotheo alikuwa wapi kwa wakati huo nyaraka hizo mbili zinaandikwa. Jibu ni kwamba alikuwa Efeso. Tunalithibitisha hilo kwa maneno ya Paulo mwenyewe. Tusome;
1Timotheo 1:3 Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
Amen
Vihekalu vya fedha vya Artemi vilikuwaje? (Matendo 19:24).
MAMBO NANE (8), AMBAYO WEWE KAMA KIONGOZI UTAIGWA.(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Wagerasi ni watu waliokuwa wanaishi katika mji ulioitwa Gerasi ambao ulikuwa kusini mashariki mwa bahari ya Galilaya. (Tazama kwenye picha)
Ulikuwa ni moja ya miji ya Nchi ya Dekapoli. Nchi ya watu wa mataifa.
ndio kule ambako Yesu alivuka na kukatana na wale watu waliokuwa vichaa wakali, akawafungua.
Marko 5:1-3
[1]Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. [2]Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; [3]makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;
[1]Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.
[2]Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;
[3]makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;
Urefu wa habari hii fungua hapa >>ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.
Mathayo 8:28-34, na Luka 8:26-39.
Ni nini ambacho Bwana anataka tujifunze kwa hawa wagerasi?
Ni watu ambao walithamini, hazina zao, mali zao, utajiri wao, zaidi ya kufunguliwa kwao, ndio maana mara tu walipoona nguruwe wao wamekufa wote, jambo hilo liliwafanya wawe na hofu, na hiyo ikawapelekea kumsihi Yesu aondoke katika nchi yao, asije akaleta hasara zaidi.
hawakuona wokovu ule mkuu uliowafikia, waliona hasara waliyopata. Hiyo ni mbaya sana, kwa urefu ya jambo hilo pitia hili somo.
Kamwe usiwe mgerasi.
Bwana akubariki
HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
2Timotheo 4:21 “Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia”
Mtume Paulo ni mtu aliyetambua kuwa kustawi kwa huduma yake kunategemea sana sapoti ya watendazi wenzake wengine wenye ni moja na yeye. Hivyo tunasoma wakati akiwa Rumi kama mfungwa, alimwandikia waraka mwanawe Timotheo, aiharakishe huduma yake, ili amfuate kule Rumi wasaidiane katika huduma kabla ya wakati wa bariki kuanza.
“Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi”.
Paulo alijua mazingira yanaweza kukawiisha kusudi la Mungu. Hivyo alitambua kuwa mtu akiongeza jitihada anaweza kukamilisha mambo yake mapema kabla mazingira Fulani hayajamuathiri kutenda kusudi lingine la Mungu.
Kwa ukanda waliokuwa, ilikuwa ni ngumu sana, meli kusafiri nyakati za baridi kwasababu ya barafu baharini, hivyo safari zote za majini zilisitishwa kwa miezi kadhaa mpaka baridi itakapoisha ndipo safari zianze tena, Paulo aliliona hilo akatambua ni jambo la asili haliwezi kuepukika kwa kufunga na kuomba, isipokuwa kwa kupangilia tu ratiba vizuri.
Hii ni kutufundisha sisi, tufahamu kuwa mazingira Fulani, au nyakati Fulani zisizo rafiki sana huwa zinapita, au zitakuja mbele yetu ambazo zinaweza zikawa ni kikwazo cha utumishi kwa sehemu Fulani.
Kwamfano wakati wa baridi kwako, unaweza kuwa ni wakati wa ndoa. Kama wewe ni kijana hujaoa/ hujaolewa, unanafasi sasa ya kumtumikia Mungu kwa uhuru wote. Titahidi sana kufanya hivyo sasa, kwasababu nafasi hiyo inaweza ikapungua kwa sehemu uingiapo katika majukumu ya kindoa. Usipojitahidi sasa kujiwekea msingi mzuri kwa Mungu wako, utataabika sana kuujenga huo uwapo kwenye ndoa.
Wakati wa baridi unaweza ukawa ni kipindi cha kazini au masomoni. Ikiwa bado hujapata kazi, au upo likizo kazini au shuleni, embu tumia vema wakati wako, kuongeza kitu kikubwa katika ufalme wa Mungu, kwasababu shughuli zitakapokulemea, kuujenga tena huo msingi itakuwia ngumu sana, na kama ikiwezekana yaweza kukuchukua wakati mrefu. Uwapo ‘free’ usilale, bali tumia sasa kuongeza mikesha, maombi ya masafa marefu, kusoma biblia yote.
Wakati wa baridi waweza kuwa uzee. Kwa jinsi umri unavyokwenda ndivyo uwezo wa mwili wako unavyopungua, Hivyo utengenezapo mambo yako mapema na Bwana, basi wakati huo ukikukuta hautakuathiri sana, kwasababu tayari yale ya msingi uliyopaswa uyafanye umeshayafanya mapema, uzeeni ni kumalizia tu.
Zipo nyakati nyingi za baridi. Chunguza tu maisha yako ujue wakati wako wa baridi unafika lini na ni upi, kisha jitahidi sana, kuwekeza kwa Mungu sasa, kimaombi, kiusomaji Neno, na kiuinjilisti.
MCHE MWORORO.(Opens in a new browser tab)
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
Je ni wakina nani ambao hawataonja mauti mpaka siku ya kuja Bwana?
(Opens in a new browser tab)Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)Rudi Nyumbani
Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu katika kujifunza Neno la Mungu. Leo tutaona mambo Makuu sita (6), ambayo Mungu anatumia kuondoa uovu ndani ya mtu, na kumfanya awe mtakatifu kabisa kama yeye alivyo. Ikiwa wewe umemfuata Kristo basi tarajia mambo haya matano atayatumia katika maisha yako, kukukamilisha.
Tukianza na
Kumbuka sisi sote tulizaliwa na deni la dhambi. Hivyo tulistahili hukumu ya mauti, (Warumi 6:23), Lakini deni hilo lilikuja kulipwa na Bwana wetu Yesu kwa kifo chake pale msalabani (Warumi 5:8). Kumwagika kwa damu yake, sote tumepokea “msamaha wa dhambi” bure kwa neema. Hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kukubaliwa na Mungu, kwa uweza wake mwenyewe. Kwahiyo damu ya Yesu imekuwa hatua ya kwanza ya sisi kukubaliwa na Mungu.
Sasa tunaweza kupokea msamaha kweli, tukasemehewa, lakini dhambi bado ikawepo ndani yetu. Na hilo sio kusudu la Mungu atusemehe tu, halafu atuache tuendelee kuwa watumwa wa dhambi ndani kwa ndani. Si lengo la Mungu, hata mtu mwenye upendo wa dhati wa Yule aliyekosewa naye, anapoona amemsamehe, huwa hamwachi tena kesho arudie kosa lile lile ili, amsamehe, hapana, bali humwonyesha njia ya kuepuka makosa ili yeye mwenyewe aweze kusimama kwa ujasiri mbele zake. Na ndivyo ilivyo kwa Mungu mara baada ya kupokea msamaha wa dhambi, huyo mtu anaanza hatua ya utakaso wa Mungu ambao sasa hufanywa na Roho Mtakatifu aliyeingia ndani yake, Ndio hapo inakuja hatua ya pili,
Biblia inasema Neno ni kama maji, ambayo yanasafisha.
Waefeso 5:26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Umeona, Kristo hulisafisha kanisa lake, kwa Neno, ndio maana wewe kama mtu uliyempokea Yesu, Ni lazima uwe na juhudu nyingi sana za kusoma Neno la Mungu kila siku, usikie maonyo, fundisho, agizo, njia, (2Timotheo 3:16), Na kwa jinsi unavyojifunza sana, ndivyo unavyosafishwa moyo wako na roho yako, hatimaye unaanza kujiona mtu ambaye huna hatia ndani yako. Na hapo ndipo unapojikuta unaacha baadhi ya mambo uliyokuwa unafanya huko nyuma. Kumbuka biblia uliyonayo sio kitambulisho cha mkristo au pambo la mkoba, bali ni maji hayo ya kukusafisha, hivyo oga kila siku, uwe msafi. Kwasababu usipofanya hivyo utakuwa mchafu tu sikuzote.
Kwa kawaida sio kila uchafu hutoka kwa maji, mwingine huitaji moto ili kuundoa. Kwamfano ukiupata mwamba wenye dhahabu ndani yake ukipitisha maji huwezi toa uchafu uliogandamana nao,hivyo wale wafuaji, wanaupitisha kwenye moto, kisha unayeyuka na baada ya hapo uchafu na dhahabu hujitenga kisha wanaikusanya dhahabu. Ndivyo ilivyo na Mungu kwa watoto wake. Upo moto ambao wewe kama mwana wa Mungu ni lazima tu utapitishwa hata iweje, kuondoa mambo sugu yaliyogandamana na wewe yasiyoweza kutoka kwa Neno tu bali kwa hatua ya kimaisha, ndio huo unaoitwa “ubatizo wa moto”. Mfano wa huu ndio ule uliompata mfalme Nebukadreza (Danieli 4), kukaa miaka saba maporini kula majani ili tu aondolewe kiburi ndani yake. Ni aina Fulani ya maisha ambayo kwako yatakuwa kama moto, lakini mwisho wake hukuletea faida ya roho yako.
1Petro 1:6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Zipo tabia nyingine ambazo Mungu anaona mwanawe anakuwa nazo kwa ujinga tu, hivyo, ili kuundoa ujinga huo, haihitaji maji wala moto, bali kiboko. Anapoona unafanya jambo Fulani kwa makusudi na alishakukataza hapo awali fahamu pia kiboko kitapita juu yako.
Waebrania 12:6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Waebrania 12:6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Biblia inasema pia..
Mithali 22:15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Yohana mbatizaji kwa uvuvio wa Roho aliandika maneno haya kuhusu Bwana Yesu..
Mathayo 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Mathayo 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Yesu akija kwako, fahamu kuwa mkononi ameshika pepeto pia, na wewe utawekwa juu yake, Anajua kabisa ulipo wewe makapi pia yapo, uliyotoka nayo huko shambani (ulimwenguni), hivyo ili kukutenga nayo, ataanza kukupepeta, kama vile ngano, utarushwa juu, utashushwa chini, utarushwa juu utashushwa chini, huwezi kuachwa utulie, lengo ni kuhakikisha makapi yote yanapeperushwa na upepo, iwe ni watu, vitu, utaona tu unapelekwa mbele, unarudishwa nyuma..baadaye akishaona ni ngano tu imebakia chini, hapo ndipo anapokuacha, unaanza kuona ushwari. Hii ilimkuta Ibrahimu, Bwana anamtoa Uru, anampeleka kaanani, mara anakimbilia Misri, mara anarudisha, lakini baadaye Mungu alimpa pumziko, baada ya kuona wote waliokuwa wameshikamana naye hawapo naye.
Usishangae kutokuwa na utulivu katika nyakati fulani za maisha yako wokovu, wakati Fulani unafanikiwa, halafu unarudi chini, wakati Fulani unapata amani kotekote, gafla inaondoka, unapata, ghafla tena unapoteza, tulia tu, kuwa na amani ndani ya Kristo, utakuwa tu, imara, wala hiyo misukosuko haitakuwepo tena, ni kwanini iwe hivyo? Ni kwasababu makapi yanapeperushwa na upepo.
Kaa ukifahamu Yesu anajulikana pia kama tabibu,(Marko 2:17) na anajua maovu mengine unayoyafanya yanatokana na magonjwa na majeraha ya rohoni, anajua hali yako ilivyo hivyo anachokifanya ni kukutibu yeye mwenyewe, ndio hapo unashangaa tu mwingine anatokwa na mapepo yaliyokuwa yanamsumbua na kumpelekea kutenda dhambi mwingine anapona udhaifu fulani, uliokuwa unamfanya amkosee Mungu, mwingine anapokea faraja, amani, utulivu usio wa kawaida, anashangaa kuona tofauti kubwa ya sasa na hapo kabla. Hili nalo mtu aliyempokea Kristo ataliona kwenye maisha yake. Na atimaye anakuwa mwema yeye tu mwenyewe, asukumwi tena na presha ya dhambi fulani. Kwasababu tabibu mkuu ameshamponya, ambaye akikuweka huru, unakuwa huru kwelikweli.
Ufunuo 3:18
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na DAWA ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
Hivyo, wewe kama mwana wa Mungu, tambua yote hayo yatapita katika sehemu Fulani ya maisha yako. Usidhani kusafishwa tu na damu ya Yesu ndio basi, utatakaswa na hiyo ni katika maisha yako yote. Haiwezekani mtu aliyeokoka ambaye amepokea Roho maisha yake yote awe Yule Yule wa zamani, hizo sio kanuni za wokovu, wala sio kusudi la Mungu. Ukubali utakaso, au usiwe mkristo kabisa. Kwasababu hivi viwili huenda sambamba wala haviwezi kutenganishwa. Huo ndio upendo wa Mungu.
Utukufu na heshima ni vyake milele na milele.
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> hhttps://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
(Opens in a new browser tab)UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
Ipi tofuati kati ya UTAKATIFU na UKAMILIFU?