Moja ya maagizo ambayo Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake alipowatuma kwenda kuhubiri injili mbali, lilikuwa ni kutokulipisha fedha katika huduma yoyote watakayoitoa, hali kadhalika kutokubeba chochote katika safari yao. Yaani wasiwe na maandalizi yoyote ya njiani, Lakini mwishoni kabisa mwa maagizo yake aliyasema maneno haya “maana mtenda kazi astahili posho lake”.. Sasa swali linakuja Je hili posho ni lipi alilostahili huyu mtandakazi ili hali ameitwa atoe bure?
Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake”.
Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake”.
JIBU: Posho aliyostahili ni ile ambayo Bwana Yesu mwenyewe atampa katika kazi ya injili anayoipeleka, kwa kupitia watu wakarimu ambao Bwana Yesu mwenyewe atawagusa moyo huko waendako aidha kwa kuwapa maji, au chakula, au nguo, na wakati mwingine hata fedha.
Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Bwana Yesu anaweza kumtunza mtumwa wake, katika mazingira yoyote atakayomtuma. Na ndiyo maana mwishoni kabisa akawaambia maneno haya;
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
Ni kufunua kuwa hatupaswi kuwa na wasiwasi wa maandilizi yoyote ya huduma ya Kristo, pale ambapo hatuna chochote, Bwana anataka tuwe wepesi (SIMPLE), tusijali sana tutakula nini, tutavaa nini huko tuendako, kesho tutatolea wapi nauli ya kurudi, hilo jambo Bwana hataki sisi kama watumwa wake tulifikirie, kwasababu ameahidi kabisa ikiwa tunatenda kazi yake kiuaminifu, basi tumestahili posho yake, hivyo anza kutumika.
Lakini haimaanishi kuwa, wakati wote, hata kama unacho, ndio ujifanye hauna, hapana, bali, upo wakati wewe kama mtumishi wa Mungu utabarikiwa na utakuwa navyo vya kuendea huko katika ziara, hivyo vitumie hivyo, Na ndio maana wakati mwingine Bwana aliwaambia wajibebe fimbo ya njiani, na kujifungia viatu, wakati sehemu nyingine kama tuliyosoma hapo juu aliwakataza.(Marko 6:8-9)
Kwahiyo, kwa vyovyote vile, Bwana atatutunza, ilimradi tunamtumkia yeye kwa uaminifu. Tusiwe na wasiwasi na huduma yake, Haleluya..
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
ANGALIENI MWITO WENU.
WITO WA MUNGU HAUVUKI NENO LAKE.
MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.
HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU
Rudi nyumbani
Print this post
Kuna makundi mawili ya WACHAWI!.
1. Wachawi wa kawaida wanaojulikana; wanaopaa na Nyungo, na kuloga na kuwanga!. Hawa wanamharibia mtu Maisha yake ya kimwili tu, kufanya mtu awe na kasoro fulani fulani za kimwili, au kimaisha.
2. Manabii wa Uongo: Hili ni kundi la Pili la wachawi!, ambalo ni hatari sana kuliko hilo la kwanza!.. kundi hili haliwalogi watu kimwili bali kiroho.. yaani kazi yake ni kumsababisha mtu aukose uzima wa milele kwa kuiacha Imani au kwa kutoijua imani.
Hili kundi la Pili, ndiyo lile Mtume Paulo alilolizungumzia katika kitabu cha Wagalatia na lile Bwana alilotuambia tujihadhari nalo.
Wagalatia 3:1 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? 2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 3 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? BAADA YA KUANZA KATIKA ROHO, MNATAKA KUKAMILISHWA SASA KATIKA MWILI?”
Wagalatia 3:1 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?
2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
3 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? BAADA YA KUANZA KATIKA ROHO, MNATAKA KUKAMILISHWA SASA KATIKA MWILI?”
Na Bwana Yesu alituonya tujihadhari na kundi hilo la Pili, Zaidi ya lile la kwanza.
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali”.
Manabii wa uongo ni wachawi wanaologa roho, ambao wamevaa mavazi ya karama za Mungu, wanajiita wachungaji, waalimu, wainjilisti, waimbaji, wahubiri n.k lakini katika utu wao wa ndani ni waharibifu wa roho za watu!.
Hawa hawatakuonea wivu wewe kwa Maisha mazuri hapa duniani, tena watakuhubiria hayo!, watakupaka na mafuta, na kukulisha chumvi, na udongo ilimradi tu, upate mafanikio, wala hawataona wivu wewe kuzaa Watoto, wala hawatakuonea wivu wewe kufurahi duniani, kama lile kundi la kwanza, ambalo halitaki ufanikiwe hapa duniani.
Manabii wa uongo!, wenyewe hawana shida na wewe kufanikiwa.. wenyewe wanashida moja tu kwako!.. kwamba USIURITHI UZIMA WA MILELE!!!!. Hilo tu!!
Hebu tujifunze kwa nabii mmoja wa uongo katika biblia, (aliyekuwa mchawi wa roho za watu), na kisha tutapata kujifunza zaidi…
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, MCHAWI, NABII WA UONGO, Myahudi jina lake BAR-YESU; 7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, MTU MWENYE AKILI. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), AKASHINDANA NAO, AKITAKA KUMTIA YULE LIWALI MOYO WA KUIACHA ILE IMANI”.
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, MCHAWI, NABII WA UONGO, Myahudi jina lake BAR-YESU;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, MTU MWENYE AKILI. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), AKASHINDANA NAO, AKITAKA KUMTIA YULE LIWALI MOYO WA KUIACHA ILE IMANI”.
Umeona hapo kazi ya huyo mchawi (aliye nabii wa uongo) ni ipi?.. Haikuwa kumwangia na kumloga Sergio asiwe Tajiri, au asiwe na akili, au asiwe na Watoto, bali ilikuwa ni KUMTIA MOYO WA KUIACHA IMANI YA BWANA YESU!!!.
Ndugu, Manabii wa uongo hata leo wanafanya kazi hiyo hiyo!.. wanashikiria biblia, wanahubiri, na wana majina ya kikristo (kama huyu Bar-Yesu) na mbaya zaidi wanatoa mpaka pepo, lakini ndani yako ni wauaji wa roho!!..
Kaka/Dada usifurahie kufarijiwa na mhubiri anayekuambia kuwa mambo yote ni sawa na huku hayaoni maisha yako yaliyojaa uzinzi, usifarijiwe na mchungaji yeyote, au nabii, au mwalimu, au padri, anayekuambia kuwa wewe ni mtoto wa Mungu, unayependwa na ilihali wewe ni mwizi, ni mlevi, ni muabudu sanamu, ni mgomvi, ni mtu wa hasira, ni mtu wa kutosamehe, ni mtu wa vinyongo na mtazamaji pornography, ni mtu wa kujichua ni mtu wa kuvaa na kutembea nusu uchi.. Tambua kuwa wewe bado hujawa mtoto wa Mungu katika hiyo hali ya dhambi uliyopo.
Jua huyo mchungaji au mwalimu anayekufundisha hivyo, hakupeleki kwenye Imani, bali anakutoa kwenye Imani..
Hiyo ndio kazi kubwa ya manabii wa Uongo!. KUKUFANYA UKAE MBALI NA ILE KWELI, AU USIIELEWE KABISA!!. Na ubaya ni kwamba hawa manabii wa uongo, WENGI WAO wanaujua ukweli! Lakini kwasababu wapo kwaajili ya kazi waliotumwa na baba yao (ibilisi), basi ndio wanaendelea kuwapotosha watu makusudi..
Neno la Mungu linasema..
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Itafute kweli yote ya Neno la Mungu..na JIHADHARI NA MANABII WA UONGO!..
Bwana Yesu anarudi na hizi ni siku za Mwisho.
Maran atha!
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10 WHATSAPP-Group
Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
Jibu: Biblia haitupi andiko la moja kwa moja kuwa uchongaji wa ndevu au nywele ni dhambi. Hilo hasaa linategemea na nia, au kiwango , au mtindo. Hapo ndipo yaweza kuwa rahisi kuhukumu kama ni dhambi au la!. Kwamfano mwingine amenyoa kawaida, kisha kwa kumalizia akapenda kuzichonga kwa lengo la kuzifanya ziwe katika mpangilio wake bora lakini hana nia nyingine yoyote, hiyo sio dhambi.
Lakini mwingine anaweka ndevu au nywele zake katika mitindo, fulani mfano tu watu wa kiulimwengu, mfano anachonga pembeni, kisha katikati anaacha kimchirizi kidogo cha nywele (kiduku), utajiuliza huyu mtu nia yake ni nini? Sisi tumeambiwa, Nuru yetu iangaze mbele za watu, ili watakapoona matendo yetu wamtukuze Baba yetu wa mbinguni.. Lakini wewe kama mkristo, unayechonga nywele kwa mitindo hiyo, ni nuru gani unaangaza?
Hali kadhalika tumeambiwa tusiifuatishe namna ya dunia hii (Warumi 12:1).
Hatuna budi kufahamu kuwa miili yetu ni makao ya Mungu, mwenyewe, hivyo lolote tunalolifanya ni lazima tujiulize kwanza mwenye hekalu anapendezwa na huu mtindo ninaomwekea, ikiwa amani ya Kristo ipo ndani yako na una ujasiri wote kumuhubiri Kristo katika hali hiyo fanya, lakini ikiwa hakuna amani, acha mara moja.
1Wakorintho 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Je kwa mkristo aliyeokoka, ni dhambi kunyoa ndevu zake?
NGUVU YA MNADHIRI WA BWANA.
Kwanini ndugu wanaokaa pamoja wawe kama mafuta ya Haruni?
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
WhatsApp
Kupoza ni nini?
Jibu: “Kupoza” ni Kiswahili kingine cha neno “kuponya”. Hivyo badala ya kutumia neno kuponya, linaweza kutumika neno “kupoza” likawa na maana ile ile. (kama vile neno mtu na mwanadamu inavyoweza kuwa na maana moja).
Bwana Yesu aliwapa Mitume wake uwezo wa kupoza wagonjwa kupitia jina lake.
Marko 6:12 “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 13 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, WAKAWAPOZA”.
Marko 6:12 “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.
13 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, WAKAWAPOZA”.
Na uwezo huo haukuishia tu kwa wale mitume 12, bali aliendelea hata watumishi wengine wengi waliomwamini Bwana Yesu kama akina Stefano na akina Barnaba, na Paulo.
Matendo 28:8 “Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na KUMPOZA. 9 Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja WAKAPOZWA”.
Matendo 28:8 “Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na KUMPOZA.
9 Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja WAKAPOZWA”.
Na uwezo huo haukuishia tu kwa wakristo wa kanisa la Kwanza, bali hata leo uwezo huo Bwana katupa, wote tumwaminio pale tunapokwenda kuhubiri injili..
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 POZENI WAGONJWA, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”.
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 POZENI WAGONJWA, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”.
Na si katika kuhubiri tu!.. bali hata popote pale tutakapokuwepo, uwezo huo utakuwa nasi..
Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”.
Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”.
Yesu, anafanya miujiza hata leo!.
LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
Ramli ni elimu ya ufalme wa giza, wanayotumia waganga na wenye mapepo ya utambuzi katika kutabiri mambo yajayo, hivyo mtu yeyote anayetumia elimu hiyo kutabiri mambo yajayo, mtu huyo anapiga ramli.
Na watu walipiga ramli aidha kwa njia ya kutumia viganja vya mikono, au kwa kutumia viungo vya Wanyama.
Katika agano la kale, Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli wasipige ramli ya aina yoyote ile, baadhi walitii na wengi hawakutii, bali waliendelea kupiga ramli na kufanya mambo mengine mabaya…jambo lililowafanya watolewe kutoka katika nchi yao na kupelekwa Babeli na Ashuru utumwani.
2Wafalme 17:16 “Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali. 17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, WAKAPIGA RAMLI, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake 19 Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe. 20 BASI BWANA AKAKIKATAA KIZAZI CHOTE CHA ISRAELI, AKAWATESA, NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WENYE KUWATEKA NYARA, HATA ALIPOKWISHA KUWATUPA, WATOKE MACHONI PAKE”.
2Wafalme 17:16 “Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.
17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, WAKAPIGA RAMLI, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake
19 Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe.
20 BASI BWANA AKAKIKATAA KIZAZI CHOTE CHA ISRAELI, AKAWATESA, NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WENYE KUWATEKA NYARA, HATA ALIPOKWISHA KUWATUPA, WATOKE MACHONI PAKE”.
Lakini swali la kujiuliza, je ni kweli Ramli ina matokeo yoyote??..Kwamba mtu akienda kwa mganga na kupiga ramli ili ajue kesho yake itakuwaje, ni kweli atatabiriwa sahihi mambo yajayo?.
Jibu ni la!.. Shetani kamwe hajui kesho kutatokea nini, kama vile mwanadamu asivyojua kesho ni nini kitatokea. Mwenye uwezo wa kujua kesho ni Mungu peke yake!, kwasababu yeye ndio MWANZO na MWISHO, fahamu zake hazina mipaka.
Lakini shetani anachoweza kufanya ni kupanga jambo leo ambalo anatumaini kuwa kesho litatokea. Kwahiyo mtu anayekwenda kwa mganga, akitaka kujua kesho yake itakuwaje..shetani atakachokifanya ni kumpangia huyo mtu kesho yake, jinsi itakavyokuwa.
Kwamfano mtu anakwenda kwa mganga kutaka kujua kama kesho atatembelewa na wageni au la!.. na yule mganga akamtabiria na kumwambia kwamba kesho atatembelewa na wageni, na tena akawataja na majina, na muda watakaokuja.. Na kweli kufikia hiyo kesho, hao wageni wakaja kama alivyotabiriwa jana.
Sasa hapo sio kwamba huyo mganga, kimiujiza kapelekwa kesho na kuona matukio yake. Bali anachokifanya ni kutuma mapepo, ambayo yatakwenda kuwaingia hao watu aliowataja na kuwashawishi wamtembelee huyo mtu katika huo muda aliopanga yeye siku ya kesho.
Kwahiyo hao wageni na wenyewe kama hali zao za kiroho zipo chini, basi wataingiliwa na hayo mapepo na kesho kwa kujua au kutokujua wanajikuta wanakwenda safari ambayo hawajaitegemea, ili kutimiza ubashiri wa huyo mganga!.
Kwahiyo wote wanaopiga ramli, ndio kitu wanachofanyiwa na shetani (wanatengenezewa matukio) pasipo wao kujua, wakidhani wanaambia mambo yajayo. Hiyo ndio sababu Bwana aliwakataza na anatukataza Watoto wake hata leo, tujiepushe na Ramli na aina yoyote ile pamoja na ushirikina, kwasababu zinaasisiwa na shetani, baba wa Uongo. (Yohana 8:44).
Shetani angekuwa anajua mambo yajayo (future), basi angejua hata siku ya unyakuo ni lini, lakini hajui chochote!. Anachojua kiufasaha ni mambo yaliyopita tu!, kwasababu tayari ni matukio ambayo yameshatokea, jambo ambalo pia lipo ndani ya uwezo wetu sisi wanadamu kujua mambo yaliyopita, lakini si kujua mambo yajayo.
Kwahiyo unapokwenda kwa mganga kupiga ramli kutaka kujua kesho yako, fahamu kuwa ni umeenda kwa shetani kutengenezewa kesho yako na si kuambiwa kesho yako, Utatengenezewa vifo na shetani, utatengenezewa mikosi, na shida, na vile vile utatengenezewa baraka bandia ambazo mwisho wake ni laana.
Ukitaka kuijua kesho yako itakuwaje soma Neno la Mungu..Hilo ndio litakupa unabii kamili na wa uhakika wa kesho yako jinsi itakavyokuwa.
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?
Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
Jibu: Tusome..
1 Timotheo 3:8 “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, SI WATU WA KUTUMIA MVINYO SANA, si watu wanaotamani fedha ya aibu”.
Kufuatia mstari huu wengi wamejikuta wamezama katika ulevi. Pasipo kujua msingi wa andiko hili kwa undani.
Tukisoma maandiko pasipo msaada wa Roho Mtakatifu tutajikuta tunaangamia badala ya kuponyeka..
2 Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; KWA MAANA ANDIKO HUUA, BALI ROHO HUHUISHA”.
Umeona?..andiko linaweza KUUA!!, shetani alijaribu kulitumia Andiko kumwangamiza Bwana Yesu kule jangwani wakati anajaribiwa.. “Alimwambia, jitupe chini kwakuwa imeandikwa (Mathayo 4:6-7)”..Lakini kwasababu Bwana alikuwa amejaa Roho Mtakatifu aliweza kutambua hila za shetani, na kumshinda.
Kwahiyo tukirudi katika hilo andiko linalosema kuwa Mashemasi wasiwe watu wa kutumia mvinyo sana, ni vizuri kujua muktadha wa andiko hilo, ili tusije tukafanya makosa katika kupambanua maandiko.
Sasa ili tuelewe vizuri andiko hilo maana yake ni nini, hebu twende mbele kidogo mpaka mlango wa 5, wa kitabu hicho hicho cha 1Timotheo. (Tafadhali zingatia maneno yaliyoainishwa kwa herufi kubwa).
1 Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo KIDOGO, kwa ajili ya TUMBO lako, na MAGONJWA yakupatayo mara kwa mara”.
Hapa tunaona Mtume Paulo kwa kuongozwa na Roho anamwambia Timotheo asitumie maji tu, bali na Mvinyo, (Na mvinyo wenyewe si mwingi bali KIDOGO).
Na ni kwasababu gani atumie mvinyo?..je! ni kwasababu ya burudani, au kujisisimua?? au kujiliwaza??, au kupunguza mawazo???…jibu ni la!..Bali ni kwasababu ya TUMBO na MAGONJWA, yampatayo mara mwa mara.
Maana yake mvinyo huo ulitumika kwa ajili la Matibabu ya magonjwa..na si kwaajili ya ulevi au kujisisimua..ndio maana hapo Paulo anamalizia kwa kusema KIDOGO..kiasi ambacho hakiwesi kumlewesha mtu, kwasababu ukitumika mwingi, utavuka lengo la matibabu, na kumfanya mtu alewe.
Na mvinyo uliokuwa unatumika, kwa matumizi ya matibabu, haukuwa kila aina ya mvinyo tu!..bali uliokuwa unatumika ni DIVAI tu!. Zamani Divai ilitumika kwa matumizi mengi, ikiwemo matibabu ya tumbo na sio tumbo tu bali hata majeraha.. Tunaweza kulithibitisha hilo katika ile Habari ya msamaria mwema.
Luka 10:33 “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.
Luka 10:33 “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.
Sasa Paulo kama alivyomuasa hapo Timotheo (ambaye ni askofu wa makanisa )kwamba ATUMIE MVINYO KIDOGO (Zingatia hili neno KIDOGO!!) kwa ajili ya tumbo na magonjwa ya mara kwa mara, na si burudani, ndio hivyo hivyo anawaasa mashemasi na maaskofu wengine kwamba na wao wasiwe watu wa kutumia mvinyo nyingi (maana yake watumie kidogo)..kwaajili ya magonjwa ambayo yatakuwa yanawapata mara kwa mara.
Kwasababu madhara ya kutumia mvinyo nyingi ni kulewa. Na maandiko yanasema ulevi ni dhambi.
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”.
Sasa swali la kujiuliza ni je, hata leo tunapopatwa na magonjwa ya tumbo, au majeraha ya mwili tutumie Divai kujitibu?.
Jibu ni la!.. Sasahivi tunayo madawa mengi, yanayotibu tumbo na majeraha kwa ukamilifu wote. Ni sehemu chache sana za dunia zilizosalia zinazotumia njia hiyo ya matumizi ya divai kidogo kwaajili ya tiba ya tumbo au vidonda.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba ULEVI NI DHAMBI, na walevi wote hawataurithi uzima wa milele.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ULEVI, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
21 husuda, ULEVI, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Kama bado hujampokea Yesu, kumbuka hizi ni siku za Mwisho, kama bado ni mzinzi, au MLEVI, au mtukanaji, au mwizi, au muuaji, tambua kuwa upo hatarini!..hivyo suluhisho ni kumpokea Yesu ili akuoshe dhambi zako na kukusafisha.
Je! ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?
Je tunaruhusiwa kutumia vidonge wakati wa kufunga?
Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Je! mabalasi Bwana Yesu aliyoyatumia kugeuzia maji kuwa divai, yalitumika tu kwa kazi hiyo?
SWALI: Biblia ina maana gani kusema maneno haya kwa habari ya mitume?
Matendo 5:13 “hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;”
JIBU: Tusome habari hiyo tena;
Matendo ya Mitume 5:12-16 [12]Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; [13]na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha; [14]walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; [15]hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao. [16]Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
Matendo ya Mitume 5:12-16
[12]Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
[13]na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;
[14]walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;
[15]hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.
[16]Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
Japokuwa Mungu alidhihirisha uweza mwingi na maajabu kwa mikono ya mitume, lakini kulikuwa na aina maisha/ mwenendo ambao haukuwa mwepesi kwa watu wengine kuufuata kama wao.
Na ndio maana maandiko yanasema hapo “hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao, japokuwa walikuwa wanawaadhimisha, yaani wanawaonea fahari kama maaskari wa Bwana, waaminifu.
Na mwenendo wenyewe ambao uliwafanya watu wasiweze kufuatana nao, ndio huo wa kutokuogopa vifo, mapigo, mabaraza ya makuhani, mashutumu, na sura za watu.
Ikumbukwe kuwa mitume walipoitwa hawakutumwa kwanza nchi za mbali bali waliagizwa waanzie kwanza pale pale Yerusalemu ambapo palikuwa na ukinzani mkubwa sana kutoka kwa wafalme na viongozi wa kidini,
na cha hatari zaidi mitume walikuwa wanaongozwa kwenda kuhubiri katika hekalu lile lile ambalo, Kristo alipindua meza zao, hata baadaye tena Petro na Yohana walipofungwa, kwasababu ya kuhubiria watu, mule hekaluni..utaona malaika aliwatoa na kuwaaagiza warudi kule kule hekaluni kuhubiri.
Matendo ya Mitume 5:18-21
[18]wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; [19]lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, [20]Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu. [21]Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
[18]wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
[19]lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,
[20]Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
[21]Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha.
Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
Unaona, Hata wakati kanisa linapitia dhiki Yerusalemu, na kuwafanya watakatifu wote watawanyike, ni mitume peke yao waliendelea kubaki Yerusalemu.
Matendo ya Mitume 8:1
[1]Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.
Hivyo kwa utumishi wa namna hiyo wa kuhatarisha maisha, haikuwa vyepesi kwa watu wengi, kuufuata..japokuwa watu walikuwa pamoja nao bega bega, wakifurahia ushujaa wao, wakitamani waendelee kumtumikia Mungu kwa ujasiri, injili ienee.
Jambo kama hilo tunaliona pia katika huduma ya Bwana Yesu..
Biblia inasema wengi wa wakuu wa kidini walimuamini lakini hawakuweza kumkiri kwasababu ya hofu wa watu..
Yohana 12:42
[42]Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.
Watu wengi hawakuweza kuambata na Yesu katika mapito yake lakini aliaminiwa na wengi.
Hii ni kufunua nini kwa watumishi wa Mungu?
Ikiwa umeitwa kama mtumishi wa Mungu..Ni lazima maisha yako yajikite katika utumishi wa Mungu kwelikweli, yaani viwango vyako vya kujikana lazima viwe juu zaidi ya watu wengine..
Ndivyo Mungu atakavyokutumia na ndivyo watu watakavyokuadhimisha kama ilivyokuwa kwa mitume.
Chachu yetu ni lazima izidi ya watu wengine. Bwana atusaidie sana.
THAWABU ZA SIRI, ZA WATAKATIFU MBINGUNI.
SIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, BALI MAFARAKANO.
KWANINI MITUME WAMUULIZE BWANA FARAGHANI?
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Ulafi ni nini kibiblia?
Kupatiliza ni neno lenye maana ya “kupiga/kuadhibu ”..mfano badala ya kusema “fulani, kapigwa na Mungu, unaweza kusema fulani kapatilizwa na Mungu”
Lakini swali la kujiuliza ni je!..Mungu huwa anapiga watu (anapatiliza)?
Jibu ni ndio!. Huwa anatoa adhabu, anawapatiliza waovu vile vile na wema endapo wakitoka nje ya mstari.
Lakini siku zote adhabu za Mungu lengo lake ni ili sisi tutubu na si kutukomoa au kutukomesha, kama sisi wanadamu tunavyokomeshana.
Tunapopatwa na majanga tofauti tofauti, ni ili tutubu tuache njia zetu mbaya na tulitafute kusudi la Mungu juu ya maisha yetu. Na pale tunapopata ufahamu na kugeuka kuiacha ile njia mbaya tuliyokuwa tunaiendea basi moja kwa moja, Bwana anaondoa yale mapatilizo na kutupatia mema.
Mfano wa mtu aliyepigwa baada ya kuliacha kusudi la Mungu ni nabii Yona.Yeye alidhani kuacha kuitii sauti ya Mungu ataendelea kuwa salama!…kumbe kinyume chake ndio anazidi kuielekea ile hatari.
Akajikuta amekaa tumboni mwa samaki siku 3, bila kula wala kunywa.
Vile vile Bwana anawapatiliza Waovu hata kizazi cha tatu na cha nne..
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; NAWAPATILIZA wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”.
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; NAWAPATILIZA wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”.
Umeona?..ukiabudu sanamu, kama babu yako au kama baba yako au bibi yako au mama yako…Bwana atakupatiliza wewe mzao wake kama na wewe utaendelea na kuabudu sanamu kama wao.
Vile vile na wakristo wote waliomwamini Yesu wamepewa mamlaka na nguvu za kuvamia kambi za adui katika ulimwengu wa roho na kupatiliza (kupiga) kila kazi zote za giza, na kuyaacha huru mateka..
Tunaweza kuyasoma hayo katika…
2 Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 6 tena TUKIWA TAYARI KUPATILIZA maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
2 Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
6 tena TUKIWA TAYARI KUPATILIZA maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
Na tunazipiga/patiliza Ngome za Adui kwa KUOMBA, KUHUBIRI na KUSOMA NENO.
Maran atha!.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp group:Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
KWANINI UPIGE MISHALE CHINI?
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
Yapo maombi ya namna tofauti tofauti, lakini yote ni lazima yaangukie katika mojawapo ya makundi haya Matano (5).
Wengi hawafahamu kama sifa zetu ni maombi yanayojitegemea kwa Mungu, haya ni maombi yanayomwasilia Mungu katika mfumo wa nyimbo, halikadhalika pia kwa kumwadhimisha kwa matendo yake makuu aliyoyafanya kwa kuzungumza kwa vinywa vyetu.. ndio maombi ya kwanza yenye nguvu. Tunapomsifu Mungu katika Roho na kweli, ni Zaidi ya maombi mengine yote tunayoweza kuyapeleka kwake.,
Biblia inasema Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;(1Nyakati 16:29), Na pia Mataifa yote yamsifu yeye. Mambo mengi, na vifungo vingi huwa vinafunguka, pale tu tunapomsifu Mungu kwa kumaanisha katika Roho na kweli, Kwasababu ni maombi yanayouvuta uwepo wa Mungu kwa haraka sana juu ya mtu, Na ndio maana ibada zote lazima zitanguliwe na maombi haya.
Ni maombi ya kuwaombea wengine, Zaidi ya kwako mwenyewe. Kuwaombea watakatifu, kuwaombea, wanyonge, kuliombea taifa, viongozi, hata maadui zako n.k. Haya ni maombi ambayo yanampendeza Mungu sana. Danieli alifunga na kuomba kwa ajili ya taifa lake Israeli, na dhambi zao, Na Mungu akamsikia akamrehemu (Danieli 9:1-27).
Bwana Yesu alipokuwa duniani, sehemu kubwa ya maombi yake ilikuwa ni kutuombea sisi (Yohana 17) hivyo akasema pia, tuombeane sisi kwa sisi ili tupate kuponywa (Yakobo 5:16). Ikiwa na maana wengi hawawezi kuokoka/kufunguliwa wenyewe, ikiwa sisi hatutawaombea, Na pale maombi haya yanapokuwa ya muda mrefu (ya dua), basi huwa yana nguvu Zaidi, kupelekea kutupa kibali cha kupendwa na Mungu, kama ilikuwa kwa Danieli.
Ni maombi ya kupeleka haja zetu kwa Mungu, ikiwemo, kumwomba Roho wake, rizki, amani, furaha, uponyaji, kibali, fursa, gari n.k. Bwana Yesu alisema pia, tuombapo tuombe Bwana atupe rizki zetu,(Mathayo 6:11). Na pia alisema tuombe nasi tutapewa. Haya ndio maombi yanayojulikana na kuombwa na watu wengi sana.
Luka 11:11 “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? 12 Au akimwomba yai, atampa nge? 13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Luka 11:11 “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Ni maombi muhimu kwa kila mwanadamu, ni maombi ya wakati wote, ya asubuhi, ya mchana, na jioni, tunamshukuru Mungu, kwa uhai, afya, chakula, makazi, Malazi, familia,
Wakolosai 3:15 inasema “….tena iweni watu wa shukrani.”. Ulishawahi kushukuriwa kwa wema Fulani uliomtendea mtu, ukaona hali unayojisikia ndani ya moyo wako kwa shukrani ile..Ndivyo ilivyo kwa Mungu anapoona Sio kila majira tunaenda kumpelekea tu mahitaji yetu..Bali wakati mwingine tunamkaribia kumshukuru kwa vile anavyotufanyia. Inampendeza sana moyo. Na wakati mwingine kupelekea hata kupewa vile vilivyosalia, kwasababu tunaonyesha kuthamini neema yake.
Ni maombi ya kushindana, na nguvu za giza, kwa mamlaka ya rohoni tuliyopewa katika damu ya Yesu, Hapa tunatangaza ushindi, na pia kutamka kwa Imani katika Neno la Mungu. Yapo mambo mengine ibilisi hawezi kuyaachia kirahisi rahisi. Hivyo inahitaji kukemea, kuamuru, kuvunja, na kubomoa, kwa Imani.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Hivyo kama watakatifu tukijifunza kutumia aina hizi tano za maombi, bila kupuuzia hata moja, basi, tutakuwa ni askari wazuri sana katika roho.
Shalom
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA
LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.
Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1)
Warumi 5:20 “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; NA DHAMBI ILIPOZIDI, NEEMA ILIKUWA NYINGI ZAIDI”.
Ili tuweze kuelewa vizuri labda tujifunze katika mfano mmoja au miwili ya kimaisha.
Umewahi kujiuliza ni kwanini gharama za usafiri wa Umma zipo chini, kuliko zile za usafiri binafsi?. Leo hii ukisafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine, kwa kutumia basi la umma, utaona gharama zipo chini, kuliko ukitumia usafiri wako binafsi.
Sasa ni kwasababu gani iko hivyo?..Ni kwasababu mnapokuwa wengi mnachangia zile gharama, na hivyo kusababisha nauli kuwa ndogo kwa kila mmoja, lakini ukiwa peke yako itakubidi ubebe wewe gharama zote za usafiri, Maana yake badala ya kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma kwa Tsh. Elfu 20, utajikuta unatumia laki 2 kwa safara hiyo hiyo, endapo utatumia usafiri binafsi.
Kwahiyo kwa ufupi tunaweza kusema “wenye uhitaji wa kusafiri wanapokuwa wengi, basi kunakuwa na neema ya punguzo la bei)”.
Au umewahi kujiuliza ni kwanini baadhi ya dawa au chanjo za magonjwa sugu ambayo yanaathiri watu wengi kwa wakati mmoja, kama Kifua kikuu, Ukimwi, au CORONA yanatolewa bure bila malipo?..si kwasababu madawa hayo ni ya gharama za chini, la! Ni ya gharama kubwa sana, lakini kwasababu yana waathiri watu wengi kwa wakati mmoja, nchi inafanya juhudi dawa hizo zipatikane bila malipo, ili hasara isiwe kubwa kwa taifa!..
Hivyo itaingia gharama ya kuyanunua madawa hayo kwa bei ya juu, na kuyagawa bure kwa wananchi!.
lakini laiti kama magonjwa hayo yangekuwa yanawaathiri watu wachache tu!, basi yangepatikana kwa gharama zile zile za juu tu!
Vivyo hivyo katika Imani, dhambi ya mtu mmoja pekee isingetosha kumleta Kristo ulimwenguni.. Kwasababu gharama ya kumwokoa mwanadamu ni kubwa sana si ndogo!. (Mungu kumtoa mwana wake wa pekee si gharama ndogo!). 1Wakorintho 7:23 “Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu”. Soma pia 1Petro 1:18.
Hivyo ilibidi wakosaji tuwe wengi, ili Neema nayo iwe nyingi!!…iweze kupatikana bure!! Hiyo ndiyo sababu kwanini Kristo hakuja ulimwenguni siku ile ile Adamu alipoasi.. Bali alikuja miaka mingi baadaye..
Warumi 5:16 “…….kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; BALI KARAMA YA NEEMA ILIKUJA KWA AJILI YA MAKOSA MENGI, IKALETA KUHESABIWA HAKI”.
Hiyo ndio sababu pia kwanini kanuni ya kuupokea wokovu imerahisishwa namna hii!.. Ni kitendo tu cha KUMWAMINI Bwana YESU, na KUTUBU!, kwa kudhamiria kuacha dhambi, na KUBATIZWA katika ubatizo sahihi, na KUPOKEA ROHO MTAKATIFU. Basi!.. Ukiifuata hiyo kanuni, utakuwa umeupokea Wokovu kamili, na umeipokea Neema ya Mungu katika Maisha yako.
Itii injili leo, inapokuonya juu ya uvaaji wako mbaya, juu ya vimini unavyovaa na wigi unazovaa, juu ya wanja unaoupaka, juu ya lipstick unazotumia, juu ya suruali unazozivaa, juu ya mitindo yote ya kidunia uliyo nayo.. juu ya ulevi wako, na anasa na utukanaji ulionao!. Tubu leo na kuitii injili, kabla ya ule mwisho kufika..
Ukiyadharau maneno ya Mungu ya Uzima yanayokuonya leo, utafika wakati utatamani wokovu utaukosa.. na wakati huo, upo karibu kufika, wakati mlango wa neema utakuwa umefungwa!.. kitakachokuwa kimesalia ni hukumu ya ziwa la Moto!.
Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?.
Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?.
Kama hujampokea Yesu na kubatizwa na ungehitaji kumpokea leo na kubatizwa, basi tumia namba hizo hapo chini, kuwasiliana nasi ili tukusaidie juu ya hilo, pale mahali ulipo. Au tafuta kwa bidi mahali popote ambapo utaweza kupata msaada huo mapema sana kabla mambo hayajaharibika Zaidi.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
KAMA SI YESU, HABARI YETU INGEKUWA IMEISHA ZAMANI SANA.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU.