(Masomo maalumu yahusuyo Sadaka na Matoleo)
Angalizo: Masomo haya hayana lengo ya kuhimiza matoleo, (Au kuwaweka watu katika mitego ya kutoa) bali yana lengo la kutoa elimu sahihi ya kiMungu juu ya faida za kumtolea Mungu kwa njia yeyote ile.
Na wajibu wa kumtolea Mungu si wa waumini (au washirika tu peke yao) bali wa kila mtu ikiwemo wainjilisti, wachungaji, maaskofu, wazee wa kanisa, mitume, waimba kwaya na wengine wote. Hivyo ni muhimu pia kujifunza mambo haya, ili tupate faida (Isaya 48:17)
2Wakorintho 9:11 “mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, UMPATIAO MUNGU SHUKRANI KWA KAZI YETU. 12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali HUZIDI SANA KUWA NA FAIDA KWA SHUKRANI NYINGI APEWAZO MUNGU;”
2Wakorintho 9:11 “mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, UMPATIAO MUNGU SHUKRANI KWA KAZI YETU.
12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali HUZIDI SANA KUWA NA FAIDA KWA SHUKRANI NYINGI APEWAZO MUNGU;”
Nataka uone hilo neno.. “HUZIDI SANA KUWA NA FAIDA”… Maana yake ni kwamba pamoja na faida hiyo iliyotajwa hapo ya “kuwatimizia watakatifu riziki zao”..lakini pia Faida iliyo kubwa kupita yote ni hiyo kwamba “MUNGU ATAPEWA SHUKRANI NYINGI”.
Unawasaidia mayatima, wale mayatima watamshukuru MUNGU SANA KWA KILE WALICHOKIPOKEA… Na ndicho Mungu anachokihitaji sana.. SHUKRANI… shukrani.
Unaweza kuona kama shukrani ni jambo dogo!.. lakini kwa MUNGU ni jambo kubwa…
Mungu anapendezwa na shukrani kuliko maombi mengi tuyapelekayo mbele zake… Unaweza kutumia lisaa limoja kumshukuru tu MUNGU kwa mema yake na ukapata faida kubwa kuliko kupeleka mahitaji orodha ya mahitaji kwa muda huo.. (Shukrani ni darasa pana sana na lenye faida kubwa sana kiroho).
Na hapa Neno la Mungu linasema kuwa “shukrani atakazopewa MUNGU kutoka kwa wale waliopokea, basi hizo ni faida kubwa”.
Mtu akimshukuru Mungu kwaajili ya kile ulichotoa, hiyo ni faida kubwa kwako, Maskini akimshukuru Mungu kwaajili ya kile ulichotoa hiyo ni faida kubwa kwako, Mtumishi wa Mungu akimshukuru Mungu kwaajili kile ulichotoa hiyo ni faida kubwa kwako, Yatima akimshukuru Mungu kwaajili kile ulichotoa hiyo ni faida kubwa kwako, Mnyonge akimshukuru Mungu kwaajili ya kile ulichotoa hiyo ni faida kubwa kwako.
2Wakorintho 9:11 “mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, UMPATIAO MUNGU SHUKRANI KWA KAZI YETU. 12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu”.
12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Shukrani ni nini kibiblia?
Mistari ya biblia kuhusu shukrani.
HUNA SHIRIKA NAMI.
SI KWA FAIDA YA MWENYEZI, BALI KWA FAIDA YETU.
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
Rudi Nyumbani
Print this post
Swali: Kwanini tutoe sadaka? Na Je ni lazima kutoa sadaka?..Na mtu asipotoa sadaka ni dhambi?
Jibu: “Utoaji” (uwe wa sadaka au wa kitu kingine chochote) ni wajibu wa kila “Mwamini”.. Mtu ambaye si mtoaji bado hana badiliko la kweli ndani yake!…na wala Mungu hayupo ndani yake.
Sasa kwanini tunatoa sadaka? Na kwanini mtu ambaye si mtoaji hana Mungu ndani yake?
Jibu, Tunatoa sadaka kwasababu Mungu naye ni Mtoaji (vyote tunavyonufaika navyo ni yeye katupa bure bila gharama). Na kwanini Mungu awe mtoaji na sisi tuwe watoaji?.. Ni kwasababu tumeumbwa kwa sura na Mfano wake! (Mwanzo 1:26).
Kama mtu hatoi maana yake ule mfano wa Uungu ndani yake haupo kwasababu Mungu sifa yake kuu ni utoaji!.. Ametoa uzima bure, ametoa maisha bure Zaidi sana ametupa uzima wa milele bure kupitia kumtoa mwanawe wa pekee (Yohana 3:16) na mambo mengine mengi.. Hivyo na sisi ni lazima tuwe kama yeye…ndivyo maandiko yanavyotuambia.
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Na kutoa ni “Wajibu” Zaidi ya “Agizo”.. Mtu anayejua wajibu wake, hakumbushwi kumbushwi, halazimishwi lazimishwi wala hasukumwi sukumwi.. Anatimiza wajibu wake kwasababu anajua pia ni kwa faida yake.
Ukiona utoaji ni sheria ngumu kwako, kwamba unaona uchungu kumtolea Mungu.. au unaona kama unafilisika, au unaonewa au unadhulumiwa wahi kutafuta msaada kutoka kwa BWANA, Mlile mwambie aiondoe hiyo roho ndani yako kwasababu ndio roho ile ile iliyokuwa ndani ya Kaini alipoona kumtolea Mungu sehemu ya kwanza ya vitu vyake ni hasara kubwa!.. na kwasababu anasukumwa sukumwa na sheria ya utoaji, akalazimika kumtolea Mungu sehemu hafifu na sadaka zake na hivyo zikakataliwa.
Mungu anayekupa pumzi na maisha bure unaonaje uchungu kumtolea sehemu ya kumi tu! Na sehemu 9 zilizosalia zibaki kwako?.. Huoni kuna shida kama unaona uchungu kwa hicho kidogo?..
Mungu unayekanyaga ardhi yake bure, unayevuta hewa yake bure tangu umezaliwa, unayefurahia jua lake bure bila kulipia hata mia, na wakati huo huo unawalipa tanesco fedha nyingi kwa kukupatia tu kanuru kadogo wakati wa usiku.. Huyo Mungu akupaye hayo yote, unamwonea uchungu na hata kumwibia, na ukiambiwa kuhusu kumtolea unaona unafilisiwa na kudhulumiwa, utaachaje kuwa kama KAINI WEWE!!. Moyo wako hauwezi kuwa kwa MUNGU Kamwe!, haijalishi utakuwa unaomba sana wewe bado utakuwa mnafiki.
Usikwepe kumtolea Mungu na tena ifanye kuwa ni wajibu, na si Agizo wala Amri!. Na madhara ya kutomtolea Mungu (kukwepa wajibu) yanapatikana katika Mathayo 25:41-46
+255789001312 au +255693036618
Kwanini Sadaka ya Kaini ilikataliwa? (Mwanzo 4:5).
SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.
Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?.
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?
Rudi nyumbani
Swali: Kwanini sadaka ya Kaini ya Mazao ilikataliwa na ile ya Habili ya wanyama ilikubaliwa? Je ni kwamba “wanyama” ni bora kuliko “mazao” mbele za Mungu?
Jibu: Turejee,
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.
Sababu ya sadaka ya Kaini kukataliwa si kwasababu Mungu anapendezwa sana na wanyama kuliko mazao.. LA! Zaidi sana Mazao yanaweza kuwa bora kuliko wanyama kwasababu hayahusishi umwagaji wa damu.
Lakini sababu kuu ya Sadaka ya Kaini kukataliwa ni hiyo tunayoisoma katika mstari wa 3 na wa 4..
“Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta WAZAO WA KWANZA wa wanyama wake na SEHEMU ZILIZONONA za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;”
Habili alileta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona… Lakini Kaini hakupeleka sehemu za kwanza za mazao yake!..bali alipeleka sehemu dhaifu, kama ni mahindi pengine alipeleka yale yaliyoharibika haribika, kama ni matikiti alipeleka yale yaliokaribia kuoza! N.k..na zile njema na nzuri aliona zinamfaa yeye na si Mungu anayempa pumzi, na uhai na maisha.
Hivyo alimfanya Mungu wapili katika mali zake, na Mungu naye akamfanya wa pili mbele ya ndugu yake Habili.
Lakini Mungu ni wa upendo, huwenda alifanya vile kwa kukosa maarifa.. hivyo alimwonya na kumfundisha njia iliyobora ya kutoa sadaka ili sadaka yake ikubaliwe kama ya nduguye, lakini kwa kiburi alishupaza shingo, na akaenda kumwua ndugu yake, ikawa dhambi kubwa sana kwake.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. 8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “
Ni jambo gani tunajifunza hapo?
Jambo kuu tunalojifunza ni kuwa Mungu anaziangalia sadaka zetu, na kupitia hizo anatuhukumu nazo!.. Maandiko yanasema “hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakapokuwepo (Mathayo 6:21)”.. Kama hazina yako ya kwanza haipo kwa Mungu, na Moyo wako hauwezi kuwa kwa Mungu, na ndicho kilichokuwa kwa Kaini.. Hazina yake kamilifu haikuwa kwa Mungu ndio maana hata Moyo wake haukumwelekea Mungu baada ya pale.
Lakini kama sehemu ya kwanza ya Hazina yako (sadaka) ipo kwa Mungu hata moyo wako utakuwa kwa Mungu..
Na kama unataka kujipima kama moyo wako kweli upo kwa Mungu “jiangalie utoaji wako”..(Hicho ndio kipimo kirahisi sana cha kujitambua wewe ni mtu wa namna gani).. Kwasababu hiyo basi ni dhambi kubwa sana kukwepa matoleo, haihitaji elimu kubwa kufahamu hilo….mtolee Bwana Zaka, mtolee Bwana sehemu zilizonona wala usimwibie, na moyo wako utakuwa kwake na utabarikiwa pia.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?
SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
(Masomo maalumu yahusuyo matoleo na sadaka).
Karibu tujifunze bible, Neno la Mungu wetu lililo mwanga wa Njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zab. 119:105).
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa Sadaka katika agano jipya, na shetani anafanya kila awezalo kuwazuia watu wasitoe sadaka kwa Mungu, kwani anaijua Nguvu iliyopo katika sadaka kwa mkristo.
Na moja ya njia anayotumia kuwafanya watu wasimtolee Mungu, ni kuwanyanyua watu/watumishi wake ambao watalichafua eneo hilo kwa aidha kuwalazimisha watu, au kuwatapeli, au kutumia uongo kwa kivuli cha biblia.
Na mtu aliye dhaifu kiimani, akishaona kasoro hizo basi moja kwa moja anakata shauri au anaadhimia kutotoa kabisa sadaka mahali popote kwa kuamini kuwa ni utapeli tu ndio unaoendelea, hivyo adui anakuwa ameshinda juu ya huyo mtu katika eneo la utoaji.
Lakini jambo ni moja tu!.. SADAKA INA NGUVU, na kila MKRISTO (pasipo kujali wadhifa wake, iwe mchungaji au mwanafunzi) NI LAZIMA AJIFUNZE KUTOA SADAKA ili KUFUNGUA MILANGO YA BARAKA na KUONDOA VIKWAZO.
Sasa zipo faida nyingi za SADAKA, lakini leo nataka tuizungumzie hii moja, ambayo ni muhimu sana kuijua…Nayo si nyingine Zaidi ya “KUHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU”. Si kila madhabahu inaharibiwa kwa kuomba tu!, la! Nyingine ni lazima zihusishe matoleo/Sadaka.
Hebu tusome habari ya Gideoni kidogo.
Waamuzi 6:25 ”kawa usiku uo huo Bwana akamwambia, MTWAE NG’OMBE WA BABA YAKO, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI, aliyo nayo baba yako, UKAIKATE ASHERA ile iliyo karibu nayo; 26 UKAMJENGEE BWANA, MUNGU WAKO, MADHABAHU juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; UKAMTWAE YULE NG’OMBE WA PILI NA KUMTOA AWE SADAKA YA KUTEKETEZWA, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata”
Waamuzi 6:25 ”kawa usiku uo huo Bwana akamwambia, MTWAE NG’OMBE WA BABA YAKO, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI, aliyo nayo baba yako, UKAIKATE ASHERA ile iliyo karibu nayo;
26 UKAMJENGEE BWANA, MUNGU WAKO, MADHABAHU juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; UKAMTWAE YULE NG’OMBE WA PILI NA KUMTOA AWE SADAKA YA KUTEKETEZWA, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata”
Hapo kuna hatua 4 Gideoni alizoambiwa na Mungu azifanye, ambazo zimebeba funzo kubwa..
1.MTWAE NG’OMBE WA BABA
Kwanini Amtwae Ng’ombe wa Baba yake?.. Kwasababu madhabahu ile ya baali ilikuwa imemshika sana baba yake (ilikuwa na nguvu juu ya nyumba ya baba yake yote). Ikifunua kuwa na sisi tunapotaka kushughulika na madhabahu za mababa, ni lazima tutafute sadaka kwajili yao, tena zile zinazowagusa kama hiyo ya Gideoni.
2. UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI.
Baada ya Gideoni kumtwaa Ng’ombe wa baba yake, hatua iliyofuata ni kuangusha ile madhababu ya baali na ashera iliyomshika baba yake (kwa kuivunja vunja na kuiponda ponda). Na sisi baada ya kuandaa sadaka hatua inayofuata ni kuzivunja hizo madhabahu kwa damu ya YESU kwa njia ya maombi na kwa KUZIONDOA KABISA KIMWILI KAMA ZINAONEKANA..
Kama kuna miti fulani inatumika kiibada hapo ulipo unaikata, kama ni mazindiko yamewekwa juu ya dari unayaondoa, wala usiogope, na tena wakati mwingine usimwambie mtu..wewe yaondoe kimya kimya kama alivyofanya Gideoni..ukienda kutafuta ruhusa hawatakuruhusu..zaidi utanyanyua vita vikali..
Gideoni angeenda kumpa kwanza taarifa baba yake kwamba ile madhabahu ya baali anaenda kuivunja baba yake asingemwelewa kabisa, kwani zile roho zilikuwa zimemshika baba yake na alikuwa anaiogopa sana ile miungu.. Vile vile madhabahu za mababa/na mababu zimewashika na kuwaogopesha wanaoziabudu.
Hivyo wewe vaa ujasiri kuwasaidia, kwani baada ya hapo watamshukuru Mungu wako kwa mambo yatakayofanyika baada ya hapo.
3.UKAMJENGEE BWANA MADHABAHU.
Baada ya Gideoni kuvunja ile madhabahu akaijenga madhabahu ya BWANA pale pale. Na sisi baada ya maombi na kusafisha kila uchafu..tunalisimamisha jina la Bwana mahali pale, kwa kuanzisha ibada, au kanisa…Wengi baada ya maombi hakuna tena kinachoendele, jambo ambalo ni la hatari sana!..
Ni lazima jina la Bwana liendelee kutamkwa mahali pale, ili madhabahu ya adui isisimamishwe tena, kama ni nyumbani au kijijini. (Maombi ya asubuhi na jioni lazima yafanyike, vile vile nyakati za kujifunza Neno la Mungu lazima ziendelee, na watu waendelee kumtafuta Mungu).. Sio kuomba tu na kuacha!.
4. UKAMTOE NG’OMBE KUWA SADAKA.
Baada ya Gideoni kujenga madhabahu akamtoa yule Ng’ombe wa baba yake awe sadaka na hapo ndipo ukawa mwisho wa Nguvu ya ile madhabahu ya baali kutenda kazi…ikamwachia baba yake moja kwa moja, hata alipokuja na kusikia kuwa ile madhabahu ya ashera imevunjwa na mwanae wala hakuogopa kwani tayari vifungo vya uoga vilikuwa vimeshamwachia…. na hata yeye (Gideoni) naye pia alifunguliwa kwa ujumla.. Na hapo ndio ukawa mwanzo wa ushujaa wa Gideoni!.
Vile vile na sisi tunapomaliza maombi na kuhitimisha kuvunja madhabahu…Ile sadaka inapaswa itumike kujenga kanisa la pale, au kuimarisha ibada za pale, ikiwa na maana kwamba kama fedha basi zitumike kununua biblia, au vitabu vya nyimbo, au kama ni kiwanja kimetolewa kama sadaka basi kitumike kujenga kanisa ili watu wa Mungu waendelee kumwabudu Mungu wa kweli pale.
Lakini ikiwa hakuna namna ya wewe kufika mahali pale ambapo madhabahi hizo zimesimamishwa, aidha kutokana na umbali.. basi baada ya maombi toa sadaka katika madhabahu nyingine yoyote ya Mungu aliye hai na italeta matokeo yale yale. Lakini kumbuka USIOMBE TU, BILA KUTOA!..TOA TOA TOA!!!!!
MADHABAHU NI NINI?
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
UDHAIFU WA SADAKA!
Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
Jibu: Tusome..
Walawi 22:21 “Na mtu awaye yote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au SADAKA YA MOYO WA KUPENDA, katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote”.
Sadaka ya Moyo wa kupenda, ni sadaka ambayo wana wa Israeli walimtolea Mungu wao wenyewe kwa kupenda (yaani pasipo kuagizwa wala masharti).
Zilikuwepo sadaka zilizokuwa na sababu, kwa mfano sadaka ya Shukrani, tayari sadaka hiyo inatolewa kwa lengo la kushukuru, kutokana na mambo fulani ambayo mtu kafanyiwa na Mungu.
Lakini sadaka ya Moyo wa kupenda, haikuwa na sababu yoyote nyuma yake… ni mtu tu anapenda kumtolea Mungu kwasababu amependa tu kufanya hivyo..na wala si kwasababu Mungu kaagiza.
Mfano wa sadaka hiyo ni ile ambayo baadhi ya wana wa Israeli waliipeleka mbele za Bwana wakati wa ujenzi wa Maskani ya Bwana.
Wakati huo Mungu hakuwaagiza wana wa Israeli wachangie gharama za ujenzi huo wa maskani ya Mungu…lakini baadhi ya watu waliguswa na kumtafuta Musa na kudhamiria kubeba gharama za kazi hiyo kwa mapenzi yao wenyewe…
Kutoka 35:29 “Wana wa Israeli WAKALETA SADAKA ZA KUMPA BWANA KWA MOYO WA KUPENDA; wote, waume kwa wake, AMBAO MIOYO YAO ILIWAFANYA KUWA WAPENDA KULETA KWA HIYO KAZI, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa”.
Kutoka 35:21 “Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu”.
Soma pia Kutoka 25:2 na 2Nyakati 29:31.
Swali ni je! katika Agano jipya bado tunazo sadaka kama hizi?..
Jibu ni Ndio! Bado Zipo na ndizo zinazompendeza Bwana, na tunazopaswa kutoa.
Utauliza katika agano jipya tunasoma wapi hayo…??.
2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”.
Umeona sadaka ya Moyo wa kupenda ni sadaka Bwana anayoikubali.
Je na wewe unayo desturi ya kumtolea Bwana kwa moyo wa kupenda au kwa sababu tu ya shinikizo fulani?.
Kamwe usiache kumtolea Mungu, lakini katika kumtolea hakikisha unamtolea kwa Moyo.
Sadaka ya namna hii ni sadaka bora na inayompendeza Mungu
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.
YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.
Katika biblia (Agano la kale), kimiminika kilichokuwa kinatolewa sadaka ni “Divai” na si kitu kingine,
Walawi 23:13 “Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na SADAKA YAKE YA KINYWAJI ITAKUWA NI DIVAI, robo ya hini”.
Unaweza kuona pia sadaka hii ya Kinywaji ikitajwa katika kitabu cha Kutoka 29:40, Kutoka 30:9, na Walawi 23:18, Hesabu 6:15, Hesabu 15:6 na Hesabu 28:17..
Sasa swali linakuja kwanini IWE DIVAI na si kitu kingine?
Sasa Sadaka ya kinywaji (Divai) iliyokuwa inapelekwa katika madhabahu haikuwa kwa kazi ya Ulevi, bali kwa matumizi ya Nishati.
Katika sheria za Musa, Bwana aliagiza pia wana wa Israeli watoe sadaka ya kinywaji, ambayo ilikuwa ni DIVAI. Na divai hiyo ilipelekwa kwa kuhani, na kuhani aliingia nayo ndani ya hema, na kuitwaa sehemu ndogo ya ile Divai, na kisha kuimimina juu ya madhahabu Pamoja na unga mwembamba, na kuwasha moto juu yake.
Asili ya sadaka hii ni wapi?
Matoleo ya sadaka ya kinywaji yalianzia kwa Yakobo kipindi alipotokewa na Mungu kule Betheli, kama vile sadaka ya Zaka ilivyoanzia kwa Ibrahimu kipindi anakutana na Melkizedeki na hatimaye ikaja kuwa sheria kwa Israeli yote. Vivyo hivyo na sadaka ya kinywaji.
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.
15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Sasa Sadaka ya Kinywaji inawakilisha nini katika Agano jipya?
Sadaka ya kinywaji katika Agano jipya inawakilisha damu ya YESU, ambayo ilimwagika/kumiminwa kwaajili yetu, mara moja tu! (kumbuka damu ya Yesu, inafananishwa na Divai), Bwana Yesu alilisema hilo wazi..
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Umeona hapo! Kile kikombe (Divai) kilikuwa ni Damu ya Yesu iliyotiririka na iliyomwagika pale Kalvari, na ni ufunuo wa Ile sadaka ya kinywaji ambayo ilikuwa inamiminwa juu ya madhabahu. Na pia ni ufunuo wa meza ya Bwana.
Bwana Yesu akubariki
Maran atha!
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.
BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?
Haya ni maswali 8 maarufu yahusuyo Zaka.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?,
2. Je fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?,
4. Je fedha ya mkopo inatolewa fungu la 10?.
5. Je Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni.?
6. Je kama nimepokea mshahara ambao haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa.kila.siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka?
8. Je! Fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi kimaandiko?.Na je kuna ulazima wowote wa kulipa zaka?
Tukianza na swali la kwanza.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?(Zaka).
Jibu: Kila mtu aliyeokoka ana wajibu wa kutoa fungu la 10. Haijalishi umri wake, jinsia yake?, au hali yake ya kiuchumi.
Maana yake kama unafanya kazi ya mikono au haufanyi, ni lazima kutoa fungu la 10 (yaani kulipa zaka).
2. Fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
Fungu la 10 linatolewa katika faida na si mtaji. Mfano una mtaji wa laki moja, na kazi unayoifanya imakupa faida kwa siku sh. Elfu kumi. Hapo zaka utatoa kutoka katika hiyo faida uliyoipata na si. Kutoka katika mtaji ulionao (maana yake kiasi cha zaka unachopaswa utoe hapo kwa siku ni sh. Elfu moja).
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?
Kama zawadi hiyo uliyopewa utaifanya kuwa mtaji, basi hutaitolea zaka, lakini utatoa katika faida huo mtaji utakayoizalisha. Lakini kama zawadi hiyo matumizi yake ni kama ya mshahara wa kawaida..yaani katika kujihudumia kwa chakula, makazi au malazi, basi utaitolea zaka.
Na vile vile kama hufanyi kazi yoyote, au bado hujapata kazi, chochote kitakachofika mkononi mwako kwaajili ya mahitaji yako, hicho utakitolea zaka.
4. Je fedha ya mkopo, tunaitolea zaka?
Kama mkopo uliochukua ni kwa lengo la mtaji wa biashara, hupaswi kuutolea zaka, bali utatoa zaka katika faida utakayoipata kutoka katika mkopo huo.
Lakini kama mkopo ulioupokea ni kwa lengo la kujihudumia kimaisha kama chakula, mavazi au malazi (Huo ni kama mshahara, hivyo unapaswa uutolee zaka).
5. Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni moja.?
Jibu: Zaka utatoa kutoka katika hiyo milioni moja na si kutoka katika hiyo laki 7, maana yake kiasi cha zaka hapo kitakuwa ni sh. Laki moja kila mwezi.
6. Je kama nimepokea mshahara/Zawadi ambayo haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
Jibu: Kama ng’ombe huyo utamfanya kuwa mtaji, hautamtolea zaka, isipokuwa faida utakazozipata kutoka katika shughuli hiyo, utaitolea zaka (maana yake kama utafanya biashara ya kuuza maziwa, faida utakayoipa kupitia maziwa hayo, utalipa zaka).
Lakini kama utamtumia kwaajili ya kitoweo, hapo huna budi kutafuta thamani ya ngombe huyo na kutoa sehemu ya 10, maana yake kama ng’ombe ana thamani ya milioni moja basi utatoa laki moja kama zaka, au kama hutaweza kupata thamani hiyo, basi utaitoa sehemu ya 10 ya nyama kama zaka.
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa kila siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka mwaka?
Jibu: Ndio! Lakini kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Mfano unaweza ukawa unapata faida ndogo, ambayo mahesabu ya zaka yake yanakuwa ni chini ya sh.50, sasa huwezi kutoa sh 40 au 20 au 10 kama zaka kila siku, kwasababu hata matumizi ya hizo sarafu hayapo!.Kwahiyo suluhisho ni kufanya mahesabu ya kiasi kinachopatikana kwa wiki au mwezi, na kulipa kwa pamoja.
Vile vile hakuna ratiba maalumu ya kimaandiko ya wakati wa kulipa zaka..maana yake kama mtu atachagua kulipa kila mwisho wa wiki, hafanyi dhambi, mwingine kila mwisho wa mwezi hakosei, mwingine kila mwisho wa miezi mitatu pia afanyi makosa, ilimradi analipa kiasi chote kwa uaminifu. (Lakini ni vizuri zaidi kulipa mapema, ili kuzuia mlundikano wa madeni..lakini kila mtu anao ustaarabu wake, ambao yeye anauwezo wa kuumudu).
8. Je fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi?..kwa mayatima, kanisani, kwa mtumishi wa Mungu au wapi?.
Ili kupata kupata jibu la swali hili kwa urefu unaweza kufungua hapa >>>> NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
Bwana atubariki.
JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?
Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?
KITABU CHA UKUMBUSHO
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
WhatsApp
Sadaka ya amani, ilikuwa ni sadaka inayotolewa kwa Mungu kutokana na amani mtu aliyoipata; Tofauti na ambavyo ingeweza kutafsirika kuwa ni sadaka ambayo mtu angeitoa kwa Mungu ili kupatana naye! (yaani kurejesha amani na Mungu), lakini sivyo, haikuwa na maana hiyo!.
Wana wa Israeli walitoa aina hii ya sadaka, pale ambapo ndani yao walipata amani. Na amani hiyo ilitokana na Mungu kuwafanyia jambo Fulani zuri katika Maisha yao labda kuwafanikisha, au kuponywa magonjwa au kupatanishwa na maadui zao n.k.
Hivyo kutokana na amani hiyo walimtolea Bwana sadaka ya kumshukuru, ndio iliyojulikana kama sadaka ya Amani. (Na sadaka Hii ilikuwa ni sadaka ya hiari na haikuwa ya amri, maana yake mtu hakulazimishwa kumtolea Mungu, ni kwajinsi atakavyojisikia yeye, kama ameona kuna sababu ya kumshukuru Mungu kwa amani basi alimtolea, kama aliona hakuna sababu basi aliacha!, hakulazimishwa).
Tofauti na sadaka nyingine ambazo mtu akipeleka mbele za Bwana, kama ni ng’ombe au mbuzi au kondoo au njiwa, mnyama yule anakuwa anateketezwa wote juu ya madhabahu baada ya kuchunwa, lakini sadaka hii ya Amani ilikuwa tofauti kidogo!, kwani baada ya mtu kumleta mbele za Bwana katika hema, kuhani alimchuna yule mnyama, na kutoa baadhi ya viungo vichache vya ndani tu!, ambavyo ni FIGO, MAFUTA YAFUNIKAYO MATUMBO, na KITAMBI KILICHOPO KATIKA INI. Na viungo hivyo ndivyo alivyokuwa anaviteketeza juu ya madhahabu, sehemu iliyobakia yaani nyama ya mwili, ilikuwa ni kwaajili ya makuhani, na mara chache sana iliteketezwa kwa moto.
Walawi 3:1 “Na matoleo yake kwamba ni SADAKA ZA AMANI; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana. 2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. 3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo, 4 NA FIGO ZAKE MBILI, NA MAFUTA YALIYOSHIKAMANA NAZO, YALIYO KARIBU NA KIUNO, NA HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, PAMOJA NA HIZO FIGO; HAYO YOTE ATAYAONDOA. 5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana”.
Walawi 3:1 “Na matoleo yake kwamba ni SADAKA ZA AMANI; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana.
2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,
4 NA FIGO ZAKE MBILI, NA MAFUTA YALIYOSHIKAMANA NAZO, YALIYO KARIBU NA KIUNO, NA HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, PAMOJA NA HIZO FIGO; HAYO YOTE ATAYAONDOA.
5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana”.
Sadaka hii inatufundisha nini sisi watu wa agano jipya?
Je inatufundisha na sisi tukachune ng’ombe na kuwatoa sadaka ya kuteketezwa?.. La!, haitufundishi hivyo, bali inatufundisha kuzijali Fadhili za Bwana.
Kama Bwana amekupa amani katika Taifa unaloishi huna budi kumshukuru kwa matoleo yako kwa chochote kile angalau kila mwaka au kila mwezi..(Hiyo ni sadaka ya amani kwako kwa Bwana, usipomtolea hutendi dhambi ila pia hupati thawabu).
Vile vile kama Bwana kakupa Amani na nyumba yako, au ndoa yako..basi mshukuru kwa chochote, mtolee sadaka hiyo ya amani, naye ataona umemheshimu, na utapata baraka.
Kama Bwana amekupa amani mahali unapoishi, au unapofanyia kazi, au unapomtumikia yeye.. basi mtolee sadaka ya Amani, sadaka ya namna hiyo inaugusa sana moyo wa Mungu kwasababu anaona unazithamini Fadhili zake.
Na eneo lingine lolote la Maisha yako ambalo unaona umepata amani kwalo, mtolee chochote yeye.. Na kipeleke kwenye nyumba ya Mungu.
Na katika matoleo kumbuka jambo hili siku zote!, sadaka za amani zinapelekwa kwenye nyumba ya Bwana au kwenye utumishi wa Bwana, usipeleke kwa maskini, wala kwa ombaomba barabarani!!..
Israeli kulikuwa na maskini wengi, lakini Bwana alimwagiza Musa na Haruni kuwa wawaambie Israeli wote wapeleke sadaka zao NYUMBANI KWAKE!..sio kwamba Mungu alikuwa hawaoni maskini!, aliwaona lakini alikuwa na sababu kubwa kwanini awaambie wapeleke nyumbani kwake!.. Ni kwasababu nyumbani kwake ndipo kunapotoka uzima!, ndipo ibada za kuwaombea Israeli wote zinapofanyika!, (ikiwemo na maskini ndani yake), ndipo walipokuwepo makuhani wa Bwana ambao muda wote wanafanya kazi ya Mungu, kuwapatanisha na kuwarejesha kwa Mungu wao!. Pasipo ile hema kuwepo ya kufanya upatanisho, Israeli ingeshafutika kitambo..Hiyo ndio maana Bwana alisema sadaka zote ziende pale, ili ule utumishi wa ukuhani uendelee kuwepo, usife wala kupotea.
Hivyo ukiwa na chochote tofauti na sadaka ya shukrani, wapelekee maskini, na wasiojiweza mitaani, lakini sadaka! Ipeleke madhabahuni kwa Bwana!..itakuletea matokeo makubwa Zaidi.
Usianze kusema, wala kufikiri sadaka yako inaliwa na wachungaji!, hiyo sio kazi yako, mwachie Bwana yeye anajua kushughulika na madhahabu yake, aliwaadhibu wana wa Eli waliokuwa makuhani kwa kuidharau sadaka ya Bwana, pasipo kusaidiwa na mtu, atashughulika na viongozi wa namna hiyo hiyo siku hizi za mwisho, lakini wewe uliyetoa hutakuwa na hatia, thawabu yako ipo pale pale.
Hivyo usisikilize uongo wa shetani uliozagaa kila mahali unaosema..nikipata sadaka napeleka kwa mayatima na ombaomba, kwasababu wachungaji ni wahuni!! Utajipunguzia thawabu zako!..Toa sehemu nyingine na kuwapa hao, lakini sadaka yako ambayo itaambatana na shukrani na maombi, ipeleke madhabahuni kwa Bwana. (HIYO NI KULINGANA NA NENO LA MUNGU!!).
Bwana atusaidie tuzijali Fadhili za Bwana.
Maran atha
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18
Katika Agano la kale zilikuwepo aina za sadaka mbali mbali, ambazo Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wazitoe, ilikuwepo sadaka ya Amani, sadaka ya dhambi, sadaka ya kuinuliwa, kadhalika ilikuwepo sadaka ya kutikiswa na nyingine nyingi. Leo tutaitazama hii sadaka ya kutikiswa kwa ufupi na ujumbe wake katika roho.
Awali ya yote ikumbukwe kuwa makuhani peke yao ndio waliopewa dhamana na Mungu ya kutumika katika nyumba yake, na ndio waliopewa dhamana ya kufanya shughuli zote za kikuhani, ikiwemo kupokea sadaka kutoka kwa watu, walizomletea Bwana. Sadaka hizo zilikuwa za aina tofauti tofauti, zilikuwepo za wanyama, zilikuwepo za ndege kama njiwa, zilikuwepo pia za nafaka kama ngano, unga na nafaka nyingine.
Endapo Mtu akileta sadaka yake ya mnyama kama kondoo, basi alimleta kwa kuhani, kisha kuhani atamchinja Yule kondoo na kuichukua damu yako, ambayo hiyo ndiyo itakuwa kwaajili ya upatanisho wa Yule mtu, kisha viungo baadhi atavichoma juu ya madhabahu ndani ya Hema au hekalu mbele za Bwana, na sehemu ya nyama iliyobakia ambayo haijachomwa, Mungu aliruhusu Kuhani huyo iwe yake yeye na familia yake (Ndio mshahara wake). Makuhani walikuwepo wengi wanaofanya kazi hizo, na walikuwa wanafanya kazi hizo kwa zamu.
Na sadaka ya unga, ilikuwa ni hivyo hivyo, kiwango kidogo kilichomwa juu ya madhabahu mbele za Bwana na kiwango kilichobakia kilikuwa ni kwaajili ya Makuhani waliohudumu katika nyumba ya Bwana, Sadaka zote za dhambi na hatia ndio zilikuwa zinatolewa kwa utaratibu huo.
Sasa sadaka ya Kutikiswa ilikuwa ni tofauti kidogo, Kwani baada ya sadaka kupokelewa na Kuhani, kama ni Nafaka au Mnyama. Basi kuhani alichukua kwanza sehemu ndogo ya sadaka hiyo na kuinyanyua juu na kisha KUIPUNGA HEWANI MBELE ZA BWANA, kwa mfumo wa KUITIKISA TIKISA, Kisha baada ya hapo ataishusha chini, na kuendelea na hatua nyingine za kutekekeza baadhi ya viungo juu ya madhabahu, na sehemu iliyobakia ni riziki yao.
Sadaka ya kutikishwa ilihusisha aina zote za sadaka, yaani za Wanyama, ndege pamoja na Nafaka. Sasa sio kila sadaka wana wa Israeli walizokuwa wanazileta zilitikiswa namna hiyo mbele za Bwana, la! Bali ni baadhi tu!.
Walawi 7:28 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,29 Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa Bwana, atamletea Bwana matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani;30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa SADAKA YA KUTIKISWA MBELE YA BWANA.31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na cha wanawe.32 Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani.33 Katika wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake.34 Kwa maana, HICHO KIDARI CHA KUTIKISWA, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.”.
Walawi 7:28 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
29 Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa Bwana, atamletea Bwana matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani;
30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa SADAKA YA KUTIKISWA MBELE YA BWANA.
31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na cha wanawe.
32 Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani.
33 Katika wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake.
34 Kwa maana, HICHO KIDARI CHA KUTIKISWA, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.”.
Mistari mingine inayozungumziwa sadaka hiyo ya kutikiswa ni Kutoka 29:27,Walawi 8:27, Walawi 9:21, Walawi 10:14, Hesabu 6:20, Hesabu 8:11, na Hesabu 8:18.
Sadaka hiyo imebeba ujumbe gani kwetu?
Mungu aliruhusu baadhi za sadaka zitolewe kwa njia ya kawaida na nyingine zitolewe kwa njia hiyo ya kunyanyuliwa juu na kutikiswa tikiswa, (yaani kuipungia hewani)
Kutufundisha kuwa na sisi hatuna budi kuzitofautisha sadaka zetu, Sadaka ya kumshukuru Mungu kwa matendo aliyokufanyia mwaka mzima, au mwezi mzima, au jinsi alivyokuokoa na majaribu makuu haiwezi kuwa sawa na sadaka ya kawaida unayomtolea siku zote, Ya shukrani ni lazima iwe ya juu kidogo, na uitangaze mbele zake, kwasababu ya matendo makuu aliyokufanyia, ni lazima iambatane na kuinyanyua mikono yako juu na kumwimbia kwa kumshukuru, na kumtukuza, Sadaka ya namna hiyo inapendeza zaidi mbele za Mungu wetu..
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?
Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?
Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
Jibu: Tusome kuanzia juu kidogo,
Mathayo 6:1“ Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:1“ Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Kwa namna ya kawaida haiwezekani kufanya jambo mkono wako mmoja usiwe na mawasiliano ufanyalo mkono wako wa pili, Kwasababu mwili wako wote umeungamanishwa na kuwa kitu kimoja. Kwahiyo Bwana Yesu alipotoa huo mfano hakumaanisha kuwa tutafute namna ambayo wakati tunatoa sadaka mkono wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kulia. Bali alitumia huo mfano kama kionjo tu!. Ambacho kingetusaidia kuelewa kwa kina anachotaka kumaanisha.
Kwamba sadaka zetu ziwe za siri za hali ya juu, zisiwe za kutangaza tangaza, kiasi kwamba hata wewe mwenyewe kwenye nafsi yako (mwili wako) huitangazi tangazi…Unakuwa unaitoa na kuisahau..
Luka 18:10 “ Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; HUTOA ZAKA KATIKA MAPATO YANGU YOTE. 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. 14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; HUTOA ZAKA KATIKA MAPATO YANGU YOTE.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.
Sasa sio kwamba huyo mtoza ushuru hapo juu, hakuwa anatoa zaka, au sadaka.. Alikuwa anazitoa, pengine zaidi hata ya huyo Farisayo, lakini kila alipotoa katika nafsi yake anakuwa anazisahau, hajinyanyui mbele za Mungu, wala hazitaji taji mbele za Mungu, kila siku anajiona kama hajamtolea, anakuwa hazihesabu, anajiona kama bado ana deni kubwa la kumtolea Mungu…. Hivyo hiyo ikamfanya awe wa haki zaidi kuliko ya yule Farisayo, ambaye alikuwa anajiinua inua katika nafsi yake.
Lakini zama hizi ni kinyume chake, hebu mtu amtolee Mungu sadaka Fulani, labda kiwango Fulani cha fedha, utaona jinsi atakavyotangaza kwa watu, atawejiwekea mazingira kila mtu ajue, na hata wakati mwingine kunung’unika nung’unika, anapoona jambo Fulani halipo sawa (kila mara utasikia anataja..sadaka zetu zinafanyiwa hichi au kile!!).. na hata akifaulu hilo (akawa hanung’uniki), utaona anavyojinyanyua kila siku mbele za Mungu katika sala zake.. Akisali utasikia, mwezi uliopita nilikutolea sadaka hii!..wiki iliyopita nikakutolea tena.. jambo hilo atalirudia rudia mara nyingi…kila sadaka anayotoa anaihesabu na anaona ni kama anamnufaisha Mungu kwa sadaka zake na wala si kama ni wajibu wake.
Lakini wakati huo huo yupo mwingine ambaye hawezi kupitisha wiki, hajamtolea Mungu sadaka nono, na kila anapopiga magoti mbele za Mungu anajiona kama hajawahi kumtolea chochote. Sadaka aliyoitoa wiki iliyopita hata haikumbuki! (Huyo ndio mfano wa mtu yule anayetoa sadaka ambayo hata mkono wake mmoja haujui ifanyacho mkono wake wa pili).
Hivyo Neno hilo ni kutufundisha tu, jinsi ya kuenenda mbele za Mungu, ili tupate thawabu, tufahamu kuwa tunapomtolea Mungu, au tunapowapa vitu watu, tusijionyeshe mbele za watu wala mbele za Mungu, Ukishatoa sahau kama umetoa, zaidi ya yote tutafute kumtolea tena na tena.. Ndivyo tutakavyopata thawabu kutoka kwa Mungu, lakini kinyume cha hapo, Bwana Yesu alisema, tumekwisha kupata thawabu zetu.
Bwana atubariki na kutusaidia.
Kumbuka, kama unaisikia injili leo na kuipinga, kama unahubiriwa uache uzinzi, na hutaki kuamua kuacha makusudi, kama unahubiriwa uache ulevi, na wizi na mambo yote machafu hutaki na unatafuta kumtolea Mungu sadaka, biblia inasema “kutii ni bora kuliko dhabihu (1Samweli 15:22)”.. na pia inasema…
Mhubiri 5:1 “Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya”.
Na pia inasema “Sadaka ya wasio haki ni chukizo;..(Mithali 15:8)” Na tena…
Kumbukumbu 23: 8 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.
Usichukue mshahara wako wa kazi ya Bar na kumpelekea Mungu, ukidhani inamfurahisha sana hiyo sadaka.. Yeye anaihitaji roho yako ipate wokovu na si fedha yako. Sadaka ni matokeo ya shukrani, sasa utamshukuru vipi mtu ambaye umemkataa moyoni mwako?..si utakuwa ni mnafiki na kumfanya ahuzunike juu yako?.
Hivyo kama hujampokea Yesu, leo unayo nafasi, kabla ya kufikiria kwenda kumtolea Mungu, fikiria kwanza kuondoa roho ya uasherati, ulevi, kujichua, wizi na nyinginezo ndani yako. Baada ya hapo ndipo fikiria kwenda kumtolea Mungu, na unapomtolea hakikisha hujinyanyui mbele zake.
NGUVU YA SADAKA.
2Samweli 24:1-14,inasema ni jambo la kutisha kuangukia katika mkono wa Bwana je! inakinzana na Waebrania 10:31?.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.