Category Archive maswali na majibu

Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

SWALI: 2Timotheo 3:7, ina maana gani inaposema;

wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.


JIBU: Katika kitabu cha 2Timotheo sura ya tatu(3), kuanzia mstari 1-9. Kinaeleza sifa za watu watakaozuka katika siku za mwisho.  Tabia ambazo hapo mwanzo hazikuwepo. Sasa ukisoma pale utaona zimeorodheshwa baadhi ikiwemo kutokea watu wenye kupenda fedha, watu wakali, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu,..na nyinginezo

Lakini ipo sifa nyingine inatajwa pale, kuwa litazuka kundi la watu wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..ndio hao ambao anaeleza sasa mbeleni, wanajifunza sikuzote ila wasiweze kuufikia ujuzi wa kweli.

Tusome;

2 Timotheo 3:5-9

[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

[6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;

[7]wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

[8]Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

[9]Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.

Maana ya ujuzi;

Ujuzi maana yake ni ufanisi au kukifanya kitu kwa utashi wote. Mtu anaweza akafanya jambo lakini akiwa hana ujuzi nalo litakuwa ni kituko kama sio hasara kabisa. Kwamfano mtu atasema, mimi naweza kujenga (na hajasomea ujenzi). Hivyo akaenda kununua tofali na kuanza kupandisha, unajua ni nini kitamkuta? kwasababu hajui kanuni za ujenzi anaenda  kufanana na yule mtu aliyejenga nyumba yake juu ya machanga.

Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa watu, hawakuufikia huo ujuzi wa kweli, kwasababu walikuwa na nia zao wenyewe za tofauti na sio ya Kristo, walilenga kuwakusanya wanawake waliokuwa na mizigo ya dhambi, kama daraja lao, na hifadhi yao ya kihuduma, ili watumize malengo yao. Sasa Kwa urefu wa tabia za wanawake hao bofya link hii  uwasome >>> Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?

Lakini huo ujuzi wa kweli ni upi?

ujuzi wa kweli ni UTAUWA/ UTAKATIFU. Mtu anayefikia kilele cha kuifahamu kweli ya Kristo huishia katika utakatifu wa kweli. Tunalisoma hilo katika;

Tito 1:1

[1]Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ‘ujuzi wa kweli’ ile iletayo utauwa;

Umeona ujuzi wa kweli, lazima ulete utauwa.

Lakini watu hawa walikuwa na mfano wa utauwa lakini walizikana nguvu zake kimatendo, ndio maana hawakufikia..waliitwa wakristo lakini wakristo jina, waliitwa mitume, wainjilisti, manabii, waalimu, watakatifu, lakini nia zao zipo penginepo. Walikuwa na elimu za vyuoni, wanajua kuyachambua maandiko, na vifungu vyote, lakini maisha ya utakatifu yapo mbali na wao.

Ndilo linalotendeka leo hii, maarifa tuliyonayo kuhusu Mungu ni mengi, zaidi hata watu wa kale, tuna wingi wa vyuo vya theolojia, na makanisa, na mafudisho mengi. Lakini maisha ya wengi hayamwakisi Kristo katika utakatifu wa kweli.

ndio hili neno linatimia,

wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli

Ni swali la kujiuliza na sisi, je! wokovu wetu umefikia ujuzi wa kweli? Kumbuka hizi ni siku za mwisho, mafundisho uliyonayo yanakusukuma kwenye nini? FUATA UTAKATIFU.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Maana ya Mathayo 6:34 ‘Yatosha kwa siku maovu yake’ 

SWALI: Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema.. “Yatosha kwa siku maovu yake”.

Mathayo 6:34

[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.


JIBU: Bwana, hataki tuwe na hofu ya vitu vya huko mbeleni (ambavyo bado havijafikiwa), si mpango wa Mungu tubebe mizigo mingi kwa wakati mmoja, kwasababu hatujaumbiwa asili hiyo, ndio maana hata katika ile sala ya Bwana tunasema; utupe “siku kwa siku” rikizi yetu.

Hasemi utupe riziki ya “mwaka mzima” kana kwamba tukikosa vyote leo hatutaishi.. bali siku kwa siku..

Kwanini iwe hivyo?

Sasa katika hali yetu ya kibinadamu tunajua kabisa mihangaiko yetu, taabu zetu, shughuli zetu za kila siku, mara nyingi huwa haziwi safi kama tunavyotarajia, wakati mwingine kama sio kujikwaa, basi tunakutana na mambo mengi pia ya kukosesha yasiyompendeza Mungu. Hayo ndio maovu yake.

Tunakutana na watukanaji, na wazinzi, na waharibifu, wenye mizaha, wasumbufu, n.k. hivyo kiuhalisia katika mambo yetu mema, maovu pia hutokea. Hivyo kitendo cha kuyataabikia sana ya mbeleni, tafsiri yake ni kuwa tunayaleta na maovu yake pia leo. Na matokeo yake tutalemewa na maovu kichwani Na kujikuta tunamkosea Mungu.

Bwana anataka tupambane kwanza na yale ya leo, ya kesho tutapewa nguvu ya kushindana nayo. Kwa tafsiri nyingine ikiwa wewe ni wa kubeba mambo mengi ya mbeleni, dhambi itakulemea na kukushinda.

Yatosha kwa siku maovu yake.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?

Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

HAMJAFAHAMU BADO?

Rudi Nyumbani

Print this post

Munyu ni nini? (Wakolosai4:6).

Jibu: Turejee..

Wakolosai 4:6 “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea MUNYU, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.

“Munyu” ni kiswahili kingine cha “chumvi”. Neno hili limeonekana mara moja tu katika biblia..

Hivyo hapo maandiko hayo yanaweza kusomeka hivi…

“Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea CHUMVI, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.

Sasa swali; Maneno yaliyokolea Munyu/chumvi ndio maneno gani?.

Kabla ya kuyaangalia haya maneno hebu tujifunze matumizi ya chumvi.

Mbali na kwamba chumvi ni kiungo cha kuongeza ladha ya chakula, lakini pia ilitumika kwaajili ya kuhifadhia vitu ili visiharibike.

Enzi za zamani hakukuwa na friji kama tulizo nazo sasa, hivyo kitu pekee kilichotumika kuhifadhia chakula ambacho hakijapikwa ilikuwa ni chumvi?.

Kwahiyo chakula kilichotiwa chumvi kilidumu muda mrefu, na kitu kingine chochote..

Soma zaidi kuhusu Agano la chumvi hapa》》Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)

Sasa tukirudi katika “maneno” ni hivyo hivyo… “maneno yaliyokolea chumvi/munyu” mbali na kwamba ni maneno yaliyokolea ladha za kiroho..Lakini pia ni “maneno yenye kidumu muda mrefu”…yasiyopita!

Ni maneno yenye kidumu si mengine zaidi ya yale yenye kutangaza habari za uzima wa milele.

Ni maneno yenye kutangaza tumaini lililopo ndani ya YESU..maneno yenye kumpa mtu hamasa ya kumtumikia Mungu ili awe na nafasi katika ule mji mtakatifu..

Ni maneno yote yaliyonenwa na YESU mwenyewe…

Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

Lakini maneno yasiyo na munyu ni yale yote yenye kunia na kutukuza mambo ya duniani ambayo yapo leo na kesho hayapo..

Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 

14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.

Bwana atusaidie maneno yetu yakolee munyu daima.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

IMANI YENYE MATENDO

Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)

Ninyi ni chumvi ya dunia, Andiko hilo lina maana gani?

HAMJAFAHAMU BADO?

JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA,

SWALI:  Naomba kufahamu maana ya unabii unaozungumzia taifa la Tiro (Isaya 23). Kwamba litafanya ukahaba na falme zote ulimwenguni kisha utajiri wake utakuwa wakfu kwa Bwana. Tafsiri yake ni nini?

Isaya 23:17-18 inasema..

[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.

18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.


JIBU: Ukianza kusoma toka mstari wa kwanza wa hiyo sura ya ishirini na tatu (23), utaona Mungu anazungumzia adhabu, aliyoitoa kwa hilo taifa la Tiro lililokuwa na utajiri na mali nyingi kutokana na biashara zake lilizofanya na dunia nzima. Hata kuyakosesha na mataifa mengine, kwa bidhaa zake. Na jambo hilo Mungu akalihesabu kama ni ukahaba, hivyo akalipiga na kuliangusha kabisa likawa si kitu tena kwa muda wa miaka sabini(70). 

Ni mfano tu, mataifa yanayokosesha ulimwengu sasa, kwa kuuza bidhaa ambazo ni machukizo kwa Mungu, utakuta taifa linazalisha nguo za mitindo ya nusu uchi, na kuyauzia mataifa mengine, au linatengeneza sinema zenye maudhui za kizinzi na kuyasambazia mataifa mengine yaliyokuwa na maadili.. Huo ndio mfano wa ukahaba ambao taifa la Tiro lilikuwa linafanya.

Isaya 23:15

[15]Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba. 

Lakini baadaye Mungu alilirudia tena, na kuruhusu lifanikiwe, kama pale mwanzo. Likajikusanyia tena utajiri mwingi sana kwa biashara zake.. Lakini Kwasababu halikutubu, kitabia  Mungu akalipiga kwa namna nyingine kwa kuzuia utajiri wao wasiule au kwa lugha nyingine hazina zao zisitunzwe kwa maendeleo yao, Bali Bwana atazizuia zije kutumika  kwa kazi yake yeye mwenyewe na watu wake.

Na unabii huo ulikuja kutimia..

ndio maana ya huo mstari wa 18, unaosema..

[18]Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. 

Hii ni kufunua nini?

Kufanikiwa kwake mwovu, kunatimiza makusudi mawili la kwanza ni aidha kwenda kujiangamiza mwenyewe (Mithali 1:32, Zab 92:7), au kumkusanyia mtu mwingine mwenye haki.

biblia inasema..

Mithali 28:8

[8]Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. 

Watu wengi wanaofanikiwa isivyo halali,mara nyingi mali zao, hula wengine..Ndicho alichokifanya Mungu kwa taifa la Tiro. 

Ni kutufundisha pia fedha na dhahabu ni mali ya Bwana. Yeye ana uwezo wa kuzuia na kuachilia, anauwezo wa kuwapa watu wake hazina za gizani ambazo hawajazisumbukia, kwa ajili ya kazi yake.

Hivyo kumbuka Bwana akufanikishapo, tembea na Kristo, kinyume na hapo, mambo hayo mawili yanaweza kukukuta, aidha mafanikio hayo yazidi kukuangamiza ufe uende kuzimu, au yaliwe na watu wengine kabisa wema usiowajua na kazi yako ikawa bure.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Masomo mengine:

Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?

Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)

Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?

Print this post

Sheshaki ni wapi? (Yeremia 25:26)

Swali: Sheshaki inayotajwa katika Yeremia 25:26  ilikuwa ni wapi?


Jibu: Turejee..

Yeremia 25:26 “na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na MFALME WA SHESHAKI atakunywa baada yao.

27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu”.

“SHESHAKI” ni jina lingine la Taifa la “Babeli”. Kama vile “YESHURUNI” ilivyo jina lingine la Taifa la Israeli.

Kumbukumbu 33:26 “Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake”.

Soma pia Kumbukumbu 32:15 na Isaya 44:2, utaona Zaidi kuhusu Yeshuruni, na kwa urefu Zaidi fungua hapa >> Yeshuruni ni nani katika biblia?

Na vivyo hivyo na “Babeli”, jina lake lingine aliitwa “Sheshaki”… Majina haya yalitumika mara nyingi kwenye mashairi na methali za kiyahudi. Utalisoma jina hilo tena katika Yeremia 51:41, ambapo imetaja kwa uwazi kuwa ni Babeli.

Yeremia 51:41 “Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa! Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa! Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa katikati ya mataifa.

42 Bahari imefika juu ya Babeli, Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.

43 Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu ye yote, Wala hapiti mwanadamu huko”.

Je Umeokoka?.. kama bado unasubiri nini?..

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:

Babeli ni nchi gani kwasasa?

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

UFUNUO: Mlango wa 18

Rudi Nyumbani

Print this post

Kisonono kinachozungumziwa katika Mambo ya Walawi 15:2 ni kipi?

Jibu: Turejee..

Walawi 15:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2 Haya, semeni na wana wa Israeli, mkawaambie, Mtu ye yote atakapokuwa na kisonono kimtokacho mwilini mwake, atakuwa najisi kwa ajili ya kisonono chake.

3 Na unajisi wake katika kisonono chake ni huu; kama mwili wake unachuruzika kisonono chake, au kama kisonono chake kimezuiwa mwilini mwake, ni unajisi wake.

4 Kitanda cho chote akilaliacho mwenye kisonono kitakuwa najisi; na kitu cho chote ambacho akiketia kitakuwa najisi”.

Moja ya magonjwa yaliyotajwa kwenye biblia ni pamoja na huu wa “kisonono” lakini kisonono hiki ni Zaidi ya hiki tukujuacho ambacho kipo mingoni mwa magonjwa ya zinaa (Maarufu kama Gonorrea).

Mistari mingine iliyotaja ugonjwa huo ni (Walawi 22:14 na Hesabu 5:2)

Kisonono kilichozungumzwa katika biblia ni mjumuiko wa magonjwa yote yanayosababisha kutokwa na uchafu katika njia za haja ndogo (kwa jinsia zote), yawe yanasababishwa na zinaa, au yasiyosababishwa na zinaa….na uchafu huo ni pamoja na (usaha, damu au mchanganyiko).

Kwahiyo katika biblia mtu yeyote aliyetokwa na chochote kati ya hivyo katika viungo vyake vya uzazi alihesabika kuwa na kisonono na alikuwa najisi mpaka atakapopona ugonjwa huo (hawezi kukusanyika katika kusanyiko la Bwana, na alikuwa anatengwa).

Lakini je hata sasa mtu wa namna hii anapaswa kutengwa?

Katika agano jipya hakuna agizo la kuwatenga wagonjwa wa aina yoyote, au wanawake walio katika mzunguko wa hedhi. Wote wanaweza kukusanyika katika nyumba ya Mungu (kwasababu kimtokacho mtu katika mwili hakimtii unajisi, bali kile kimtokacho kutoka moyoni, ndicho kinachomtia mtu unajisi, sawasawa na Marko 7:20-22).

Marko 7:20  “Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

21  Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22  wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23  Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.

Ikiwa mtu huyo amejitakasa moyoni kwa viwango vya kustahili kumfanyia Mungu ibada, hata akiwa na maradhi mwilini, bado ibada yake itapokelewa na Bwana.

Ikiwa kisonono mtu alichokipata ni matokeo ya zinaa, huyu mtu anapaswa atubie kwanza zinaa yake aliyoifanya kwa kumaanisha kuacha hiyo dhambi (kwa ufupi aokoke), na baada ya toba akiwa katika hatua za kutafuta uponyaji, anaweza kujumuika na wengine katika majumuiko ya kumwabudu Mungu.

Vile vile ikiwa ameupata kwa njia nyingine isiyohusisha zinaa, atajitakasa nafsi yake kwa toba na rehema kwa makosa mengine na atajiunga na wengine katika kumwabudu Mungu.

Mwisho: Mshahara wa dhambi ni mauti..ikimbie dhambi, na sehemu salama ya kukimbilia ili upate msaada ni msalabani, kwasababu msaada kamili upo msalaban, Kama hujampokea Bwana YESU upo hatarini…na hauwezi kushindana na dhambi.

Ni heri leo ukayasalimisha maisha yako kwake, na yeye atakuokoa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?

Tatizo la Bawasiri kibiblia

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.

Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?

Rudi Nyumbani

Print this post

kiaramu ni lugha gani? je ilizungumzwa na Yesu?

Kati ya lugha tatu ambazo zinaonekana katika uandishi wa biblia Kiaramu (Aramaic), ni mojawapo nyingine zikiwemo Kiebrania na kiyunani.

Sehemu kubwa ya agano la kale imeandikwa katika lugha ya Kiebrania na maeneo machache machache sana yalikuwa na maandishi ya kiaramu, (Ezra 4:8 – 6:18, Danieli 2: 4 – 7:28)

 Lakini katika agano jipya sehemu kubwa imeandikwa katika lugha ya kiyunani (kigiriki), na mahali pachache pachache kuna maandishi ya kiaramu.

Hivyo lugha hii haipo kwa sehemu kubwa katika biblia

Je chimbuko la hii lugha ni wapi?. 

Ni lugha iliyozungumzwa na watu walioitwa Waaramu, ambao lugha yao ilienea kwenye mataifa mbalimbali ambayo kwasasa ni nchi za Lebanoni, Syria, Yordani, Iraq, na Uturuki, na sehemu nyingine za mashariki ya kati. Ni lugha ambayo ilikuwa na nguvu sana zamani za falme   kama Ashuru, na ufalme wa Uajemi. 

Enzi za Bwana wetu Yesu Kristo, lugha hii ilizungumzwa pia maeneo ya Israeli hususani katika miji ya Galilaya, ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alilelewa. Huku kiyahudi ikiwa ni lugha ya asili, kidini na kisiasa.

Hivyo lugha kuu ya Bwana ilikuwa ni hii kiaramu, japokuwa alizungumza pia kiyahudi.

Baadhi ya maneno ya kiaramu ambayo yananukuliwa moja kwa moja kutamkwa na Bwana Yesu ni haya; (japo yapo na pia mengine)

Marko 5:41 “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka”. 

Marko 7:34 “akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. 

Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Maneno mengine ni kama “Hosana” (lenye maana ya okoa sasa), Mathayo 21:9

“Aba” (Marko 14:36), lenye maana ya Baba.

Lakini pia swali la kujiuliza ni nini sababu ya Bwana Yesu, kuipenyeza lugha hii katika baadhi ya matukio?

jibu ni kuwa hakuna jambo la muhimu sana katika hiyo lugha, isipokuwa ni maongozo  ya Roho Mtakatifu ndani yake kwa wakati huo. Kama tu sehemu nyingine alipoongozwa kutema mate chini atengeneze tope apake mtu machoni ili apone. 

Hivyo Bwana Yesu alikuwa ni mtu aliyetega sikio kuisikia sauti ya Roho. Vivyo hivyo na sisi, misukumo mbalimbali yaweza kuja ndani yetu. Wakati mwingine hutaomba kwa akili, utaomba kwa kunena kwa lugha, utaomba kwa nyimbo, utaomba kwa kuugua na kulia, kwa jinsi Roho atakavyokusukuma ndani.

Ni kutuonyesha kuwa Bwana hakuwa na fomula fulani pekee katika kutenda kazi, alitegemea maongozo ya Roho Mtakatifu.

Vivyo hivyo na sisi tunapojawa Roho vema. Atatugusa kwa namna mbalimbali na hivyo tutatimiza makusudio yake vizuri, katika jina lake kuu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

SEMA KWA LUGHA NYINGINE.

ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Print this post

Nini maana “Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa”?

Swali: Katika Luka 19:26, kwanini Bwana YESU aseme kila mwenye kitu atapewa na yule asiye na kitu atanyang’anywa?, na kwanini isiwe kinyume chake?..kwasababu hilo ni kama jambo la kikatili, kumnyang’anya mtu kile kidogo alicho nacho.

Jibu: Turejee mstari huo..

Luka 19:24 “Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.

25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.

26 Nawaambia, KILA ALIYE NA KITU ATAPEWA, BALI YULE ASIYE NA KITU ATANYANG’ANYWA HATA ALICHO NACHO”.

Ni kweli tukisoma kwa tafakari za kawaida (za kimwili) ni kama jambo la kikatili, kumpokonya mtu kile kidogo alichonacho, lakini mstari huo hauhusu mambo ya mwilini bali ya rohoni (kwamba maskini anyang’anywe kidogo alicho nacho na apewe tajiri..La! hiyo sio maana ya huo mstari).

Ili tuelewe vizuri, turejee ule mfano wa Mzabibu katika Yohana 15:1-2, Neno la Mungu linasema..

Yohana 15:1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

2  KILA TAWI NDANI YANGU LISILOZAA HULIONDOA; NA KILA TAWI LIZAALO HULISAFISHA, ILI LIZIDI KUZAA”.

Kwa wale wakulima wanaelewa lengo la kuondoa yale matawi yasiyozaa matunda ni nini?.

Kusudi au lengo la kuondoa yale matawi yasiyozaa na kubakisha yale yanayozaa peke yake katika shina la mti ni kudhibiti matumizi mabaya ya chakula yatokayo katika mizizi kulekeka katika matawi.

Chakula kitokacho ardhini, na kupanda katika matawi ya mti, kama matawi yale yapo kumi (10) na kati ya hayo manne (4) ndiyo yenye kuzaa na (6) yaliyosalia hayazai, ni kwamba kile chakula kitokacho kwenye mizizi na kuelekea kwenye matawi hayo, kitajigawanya kulingana na idadi ya matawi yaliyopo.. na hivyo yale matawi manne (4) yazaayo yatapokea chakula kidogo, na yale (6), yatapokea kingi.

Sasa matokeo yake ni kwamba yale matawi manne (4) yazaayo yatazaa kwa kiwango kidogo kwasababu ya kiasi kidogo cha chakula yapokeayo, na yale mengine sita yasiyozaa yatakuwa yanapokea chakula cha bure ambacho hakiyasaidii matawi hayo, hivyo uzalishaji wa ule mti UTAKUWA HAFIFU, endapo ukiendelea kubaki na yale matawi yasiyozaa.. (mti utaonekana una matawi mengi na mkubwa lakini matunda machache).

Sasa kutatua hilo tatizo wakulima, huwa wanayaondoa yale matawi yasiyozaa ili yasiendelee kutumia chakula cha bure, na matokeo ya kuyaondoa kwa kuyakata yale matawi yasiyozaa, na kubakisha yale yazaayo peke yake, ni kwamba kile chakula chote kitokacho ardhini hakitapotea bali kitaenda moja kwa moja kwa yale matawi yazaayo..

Na matokeo yake yale matawi yazaayo yatapokea virutubisho vingi na kusababisha kuzaa Zaidi..Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba uwepo wa matawi yasiyozaa katika shina ni uharibifu kwa yale matawi mengine yazaayo..

Na hiyo ndiyo sababu ya Bwana YESU kusema, “KILA ALIYE NA KITU ATAPEWA, BALI YULE ASIYE NA KITU ATANYANG’ANYWA HATA ALICHO NACHO”.. maana yake KILA TAWI LINALOZAA LITAONGEZEWA NGUVU NA LILE LISILOZAA HATA KILE KIDOGO LIPOKEACHO LITANYANG’ANYWA (LITAKATWA).

Mathayo 3:10 “Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.

Ikiwa umepata Neema ya kusikia injili lakini unaichezea, hutaki kuzaa matunda ya haki kuwa makini sana, kuna hatari mbele yako!!

Ikiwa umepata Neema ya kusikia Injili na hutaki kubadilika miaka nenda rudi, uko vile vile, kuwa makini!!

Luka 13:6 “Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.

7  Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?

8  Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;

9  nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate”.

Ikiwa umepewa Karama/huduma na hutaki kuitumia, ipo vile vile kuwa makini sana!!.. hiyo Neema itaondolewa kwako na kupewa mtu mwingine ambaye atazaa matunda.

Mathayo 25:24  “Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

25  basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

26  Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27  basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28  Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29  Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa”.

Bwana akubariki, na Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TAWI LIZAALO HULISAFISHA ILI LIZIDI KUZAA.

SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.

Rudi Nyumbani

Print this post

yubile ni nini kwenye maandiko?

Yubile, wengine huiita yubilei, au yubilii.

Ni mwaka wa hamsini (50), katika kalenda ya miaka ya kiyahudi. Mungu aliwaagiza wana wa Israeli, wahesabu miaka saba, kisha waizidishe mara saba,  7×7=49.

Na ule  unaofuata wa 50, uliitwa mwaka wa yubile.

Ni mwaka ambao Mungu aliwaagiza wapumzike kabisa, hawakuruhusiwa kupanda wala kuvuna. Kwa miaka miwili mfululizo(yaani mwaka wa 49 na ule wa 50), kwasababu ule wa 49 ni sabato ya kila mwaka wa 7, ndio maana miaka miwili inatokea hapo. Sasa swali la kujiuliza wangewezaje kuishi miaka yote miwili bila kufanya kazi? Jibu ni kwamba Mungu aliwabariki mara dufu katika mwaka wa 48, hivyo wakafanikiwa kukusanya vingi vya kuwatosha miaka yote hiyo miwili ijayo bila kazi.

Lakini pia ulikuwa ni mwaka wa kusamehe madeni sambamba na hilo ulikuwa mwaka pia wa kuwaachilia huru watumwa.

Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda.

9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.

10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.

11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.

12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.  13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake.

14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;

15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe

Yubile, ilifunua  kazi ya msalaba baadaye. Kwani Bwana wetu Yesu ndiye aliyekuja kutimiza kazi  hii rohoni.

Kwanza ndani yake tunapokea pumziko kamili la utumwa wa dhambi. Pili tunasamehewa deni zetu (dhambi zetu), Na Tatu tunafanywa huru, katika vifungo vya shetani. Yaani Magonjwa na mapepo.

Huo ndio mwaka wa Bwana uliokubaliwa, ndio Yubile yetu halisi.

lakini pia sisi kama waamini katika mwenendo wetu, tuna mambo ya kujifunza tuipatazampo Yubile?.

Kwanza ni umuhimu wa kupumzika, kuahirisha mambo yetu kupata muda na Mungu. Si tupate tu siku moja kwa wiki kuwa karibu na Mungu. Wakati mwingine Mungu anataka kipindi kirefu. Wewe kama mfanyakazi, au umejiajiri, jiwekee utaratibu baada ya kipindi fulani uwe na likizo ndefu ambayo unaitenga kwa Mungu wako,kuutafuta uso wake, ni muhimu sana.

pili tunajifunza kusamehe watu madeni yao. Si kila tunayemdai lazima atulipe, fikiria juu ya hilo. Yesu alisema achilieni nanyi mtaachiliwa. Hujui ni wapi na wewe sikumoja utakwama, na utatamani.uachiliwe.

na mwisho kuwapa uhuru watumwa wetu ikiwa wewe ni mwajiri, fikiria kuwa mfanyakazi wako anahitaji pumziko refua, mpatie, bila kumpunguzia mshahara wake. Bwana ataona umeitunza yubilee yake pia kimwili. Na sio kufanya kumbukizi ya ndoa, au kuzaliwa, hiyo sio yubilei.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

SIKUKUU YA VIBANDA.

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

Rudi Nyumbani

Print this post

Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume.

Kitabu cha Matendo ya mitume hakimtaji moja kwa moja mwandishi wake, lakini tunaweza kumtambua, kutokana na utambulisho wake mwanzoni mwa waraka huo, kwamba ni LUKA. Kwasababu waraka huu aliulekeza kwa mtu mmoja aliyeitwa Theofilo, ambaye anamtaja pia alimtumia waraka wa kwanza uliozungumzia habari za Yesu tangu mwanzo hadi siku alipochukuliwa juu, na huu si mwingine zaidi ya waraka wa Luka. Soma  Luka. (1:1-3)

Ndio maana inaaminika aliyeandika waraka huu ni Luka.

Matendo 1:1  Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha,

2  hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua;

3  wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.

Kitabu hichi cha matendo ya mitume, kama jina lake linavyojieleza kinaeleza hasaa jinsi mitume wa Bwana walivyoanza kulitekeleza lile agizo kuu la Yesu alilowaambia wakahubiri injili kwa kila kiumbe. Tangu Yerusalemu, uyahudi, samaria na dunia nzima.

Kinatufundisha jinsi Roho Mtakatifu alivyowaongoza hadi kukamilisha jukumu hilo la injili ulimwenguni mwote kwa mafanikio makubwa.

Na mambo ambayo tunajifunza kwao ni haya:

Umoja: Hawakuwa na nia tofauti tofauti, bali moja ya Kristo, walikubali kudumu katika fundisho la mitume bila shuku yoyote. Walifanya yote kwa ushirikiano kwasababu vitu vyote waligawana kama kila mtu alivyokuwa na hitaji lake.

Matendo 4:32  Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.

Mashauri ya pamoja:  Hata mahali ambapo hakukueleweka vema, au kutokea kwa mikanganyiko waliweza kukaa katika Baraza la wazee na mitume, kutafakari kwa pamoja ndipo hekima ya Roho ikaamua yawapasayo kutenda.(Matendo 15: 1-21).Ndio maana hawakuwa na madhehebu.

Furaha ya Roho: Kanisa lilifurahia ibada, na imani ndani ya Kristo. Sio la watu ambao walisukumwa kufanya majukumu yao, bali wote waliona ni raha kumfuata Kristo kwa moyo mweupe.

Matendo 2:46  Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe

Maombi: Mara nyingi walidumu katika maombi,  hekaluni, na manyumbani mwao (Watendo 1:14)

Upendo: Walipendana, Waliweza kuwa na vitu vyote shirika, hawakubaguana, wala kuwa na ubinafsi kiasi kwamba hakukuwa na yoyote aliyekuwa na mahitaji ndani ya kanisa.

Matendo 2:44  Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45  wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja

Uvumilivu: Walipitia dhiki, wengine wapigwa mawe, waliburutwa, lakini hawakuitupilia mbali imani, kinyume chake ndio injili walizidi kuihubiri.

Matendo 8:1,4

 1  Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume…..4  Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.Hivyo hayo ni baadhi ya mambo ambayo na sisi tunaweza kujifunza katika kanisa la mwanzo.

Je! Umeokoka?

Kama bado unasubiri nini? Kumbuka hizi ni siku za mwisho. Tubu dhambi zao leo, mwamini Yesu, ukabatizwe akusamehe dhambi zako, Ikiwa utapenda kupata msaada huo wa kumpokea Kristo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?

Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Wafalme

Rudi Nyumbani

Print this post