Swali: Sheshaki inayotajwa katika Yeremia 25:26 ilikuwa ni wapi?
Jibu: Turejee..
Yeremia 25:26 “na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na MFALME WA SHESHAKI atakunywa baada yao. 27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu”.
Yeremia 25:26 “na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na MFALME WA SHESHAKI atakunywa baada yao.
27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu”.
“SHESHAKI” ni jina lingine la Taifa la “Babeli”. Kama vile “YESHURUNI” ilivyo jina lingine la Taifa la Israeli.
Kumbukumbu 33:26 “Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake”.
Soma pia Kumbukumbu 32:15 na Isaya 44:2, utaona Zaidi kuhusu Yeshuruni, na kwa urefu Zaidi fungua hapa >> Yeshuruni ni nani katika biblia?
Na vivyo hivyo na “Babeli”, jina lake lingine aliitwa “Sheshaki”… Majina haya yalitumika mara nyingi kwenye mashairi na methali za kiyahudi. Utalisoma jina hilo tena katika Yeremia 51:41, ambapo imetaja kwa uwazi kuwa ni Babeli.
Yeremia 51:41 “Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa! Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa! Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa katikati ya mataifa. 42 Bahari imefika juu ya Babeli, Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake. 43 Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu ye yote, Wala hapiti mwanadamu huko”.
Yeremia 51:41 “Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa! Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa! Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa katikati ya mataifa.
42 Bahari imefika juu ya Babeli, Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.
43 Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu ye yote, Wala hapiti mwanadamu huko”.
Je Umeokoka?.. kama bado unasubiri nini?..
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:
Babeli ni nchi gani kwasasa?
Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
UFUNUO: Mlango wa 18
Rudi Nyumbani
Print this post