Category Archive Uncategorized @sw-tz

Mierebi ni Nini kwenye biblia? (Isaya 15:7)

Mierebi ni aina ya miti inayostawi Mahali palipo na maji maji, Mahali pengine popote haistawi. Tazama mwonekano wake kwenye picha juu.

Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hili;

Mambo ya Walawi 23:40

[40]Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.

Isaya 44:2-5

[2]BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.

[3]Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;

[4]nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.

[5]Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.

Soma pia Ayubu 40:22, na Isaya 15:7

Kama tunavyosoma hapo Bwana aliwaagiza Wana wa Israeli watumie matawi yake kama kitu Cha shangwe katika sikukuu ya vibanda..Pindi wanapokusanyika wayanyanyue juu wamwimbie Bwana nyimbo za furaha. Lakini bado tunaona sifa ya mti huu ni kuwa karibu na vijito vya maji.

Vivyo hivyo na watu wa Mungu Rohoni, Bwana anawaona kama mierebi yake, miti inayostahili kumsifu Bwana..Kwasababu ndani yao mito ya maji ya uzima inatiririka.. lakini wengine ambao hawana Kristo ni sawa na miti mikavu tu.

Na matokeo ya kukosa mito ya uzima ndani yako ni wewe kufanyika makao ya mapepo kwasababu mapepo ndio Yanakaa sehemu isiyo na maji.

Soma

Mathayo 12:43-45

[43]Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. [44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. [45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.

Umeona? Unasubiri nini usimpe Bwana Yesu maisha Yako? Huna Raha, Wala Tumaini, Wala faraja unapokuwa nje ya Kristo. Okoka Leo Bwana ayaponye maisha Yako.

Ikiwa upo tayari kuchukua uamuzi huo wa kuokoka na kufanyika Mwerebi mzuri wa Bwana basi fungua hapa Kwa ajili ya mwongozo huo>>

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mretemu ni mti gani?

Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?

Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

NUNUA MAJI YA UZIMA.

Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).

Rudi nyumbani

Print this post

Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako (Mithali 27:23)

Haya ni Mafundisho maalumu Kwa ajili ya watumishi, ikiwa wewe ni kiongozi, askofu, mwalimu, mchungaji, mtume, mwinjilisti, unayesimama mahali fulani katika kulitazama kundi la Bwana, au jamii ya watu waliookoka, basi mafundisho haya ni maalumu kwako.

Biblia inasema;

Mithali 27:23

[23]Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;  Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.

Mchungaji Bora sikuzote anatambua ni wajibu wake kuwa karibu na mifugo yake wakati mwingi. Ili Kuhakikisha Mahali wanapolala ni salama, wanaogeshwa Kila wakati, wanapata chakula Bora, afya zao pia ni njema na wanachungwa Mahali salama.

 Kwamfano kama mchungaji akiwa Hana desturi ya kwenda zizini. Tunajua mifugo Kwa kawaida Huwa Haijui kujisafisha yenyewe, matokeo yake ni kwamba lile zizi litajaa vinyesi na mwisho wa siku watapata magonjwa na kufa, na hasara inaangukia kwa mchungaji?

Vilevile akiiachia mifugo yake ianze kujichunga yenyewe, inaenda popote iwezavyo kujitafutia chakula, bila shaka itapotea, kama sio kuibiwa, au kuliwa na wanyama wakali, au kula vitu visivyostahili.

Hivyo utaona ni sharti Mahali palipo na mifugo, hapapaswi kukosekana mchungaji hata kidogo. Hii inatufundisha sisi tulio watumishi, kuhakikisha tunafahamu Hali mbalimbali za watu wale tunaowaongoza.

Tunawajibu wa kuwapa chakula kizuri kitakachowakuza (yaani Neno la Mungu lisiloghoshiwa), tuna wajibu wa kuwalinda kiroho, dhidi ya mafundisho potofu na mitego ya ibilisi, Kwa kuwaonya na kuwakemea pale inapobidi wavukapo mipaka.

Tuna wajibu wa kuwaombea, tunawajibu wa kuwafariji na kuzijali Hali zao za mwilini katika maisha Yao ya kawaida.

Hivyo wewe kama kiongozi ikitokea upo mbali na kundi lako, usikawie sana, ukaliacha kundi lako ma-miezi na ma-miaka,bila kujua maendeleo yao, ukadhani kwamba litaweza kujichunga lenyewe, hiyo ni hatari..ni heri uwe mtu wa kwenda na kurudi, kwenda na kurudi… lakini pia ukiwa karibu nalo usiwe mlegevu kupeleka jicho lako Kila eneo la maisha Yao ya kiroho na ya kimwili, kuangalia ni wapi Pana mapungufu au  shida..ili kuondoa kasoro hizo, Ili kundi la Bwana listawi kama vile yeye atakavyo.

Ndio maana ya hili andiko Mithali 27:23 “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;  Na kuwaangalia sana ng’ombe zako”.

Ni wajibu wako kufanya hivyo, kwa hiari yako mwenyewe na sio kama unalazimishwa;

1 Petro 5:2

[2]lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Kwanini Nuhu alimlaani Kaanani badala ya mtoto wake Hamu,

EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.

FANYA KAMA UONAVYO VEMA.

ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

Rudi nyumbani

Print this post

Tatizo la maumivu ya mgongo kibiblia.

Je mgongo kuuma kunasababishwa na nini?

Kama maumivu ya mgongo si kutokana na umri, au ugonjwa uliopo ndani ya mwili wako sasa, au si kutokana na ajali uliyoipata au hali uliyopo sasa kama Ujauzito n.k?. Na umejaribu kutafuta kila suluhisho kwa madaktari bila mafanikio yoyote..basi fahamu kuwa huenda kuna ujumbe  kutoka kwa Bwana unaopaswa kuujua nyuma ya huo ugonjwa, na ukisha ujua na kuchukua hatua basi ugonjwa wako huo utaondoka mara moja.

Tusome maandiko yafuatayo..

Mithali 10:13 “Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu”

Mithali 19:29 “Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu”

Mithali 26:3 “Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu”.

Yatazame maisha yako je! Yamejaa mizaha?, yamejaa udunia? Je maneno yako yamejaa upumbavu?.. Kama hekima imepungua ndani yako, na mizaha imezidi katika maisha yako, basi huenda maumivu ya mgongo wako ni ujumbe kutoka kwa Mungu  kwamba utubu na kugeuka. Na ukishatubu kwa kumaanisha kabisa kubadili njia zako, basi BWANA atakuponya mara moja!

Lakini kama njia zako na midomo yako ni ya hekima, basi fahamu kuwa ni mashambulizi umepokea kutoka kwa adui, lakini habari njema ni kwamba Yupo Mkuu wa uzima aliyeteswa kwaajili yetu, YESU KRISTO, mwombe huyo kwa Imani naye atakuponya kikabisa kabisa. Au wasiliana nasi kwa namba tajwa hapo chini, tuweze kukuombea kwa jina la Bwana Yesu Kristo naye atakuponya.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Tatizo la Bawasiri kibiblia

Tatizo la kuvimba miguu kibiblia

TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA

JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?

Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).

Rudi nyumbani

Print this post

TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi

Mafundisho maalumu Kwa ajili ya watumishi wa Mungu.

Huu ni mwendelezo wa mafundisho maalumu Kwa ajili watumishi wa Mungu, ikiwa wewe ni Mchungaji, mwalimu, mtume, askofu,Nabii, au mtu yoyote unayemtumikia Mungu katika nafasi yoyote kanisani au kwenye huduma basi mafundisho haya yatakufaa sana.

Wakati ule Yakobo alipodhamiria kwenda kukutana na ndugu yake Esau baada ya kutengana naye Kwa muda mrefu..maandiko yanasema walifurahi sana walipoonana kule nyikani. Na baada ya mazungumzo Yale kuisha,  sasa ikiwa ni wakati wao wa kuondoka pale nyikani walipokutana waelekee Kaanani.

Na kama tunavyosoma habari tunaona ndugu yake Esau alimshurutisha wasafiri pamoja naye. Ndipo Yakobo akamwambia Esau kuwa jambo hilo ni gumu kwake..kwasababu ya Hali ya makundi mbalimbali na watu na mifugo aliyokuwa nayo..Tusome..

Mwanzo 33:12-17

[12]Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia.

[13]Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng’ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.

[14]Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.

[15]Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu.

[16]Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri.

[17]Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.

Ni nini cha kujifunza hapo?

Yakobo alilitambua kundi analolichunga, alijua kuwa wapo watoto wachanga ndani yake, na mifugo pia michanga, Ambayo haijazoezwa kupelekwa mkiki mkiki, kwani ikilazimishwa kufanywa hivyo itakufa yote njiani. Hivyo akaomba muda wa kusafiri wake uongezwe, kusudi kwamba ayakokote taratibu taratibu mpaka yatakapofika kule Shekemu alipokuwa anapakusudia. Pengine mwendo wa siku moja tu ikamgharimu mwezi.

Tofauti na Esau yeye alikuwa na watu wa vita tu,watu walio hodari, Lakini Yakobo alikuwa na makundi yote. Na hivyo kwenda nayo taratibu taratibu ilimgharimu .

Hii ni kutufundisha asili ya msimamizi wa kweli, kwanza hulijali kundi lake, pia anakuwa tayari kuchukuliana na vile vyombo dhaifu. Kwasababu sio wote katika kanisa watakuwa na mwendo kama wa kwao, SI wote watakuwa wepesi kustahimili vishindo kama baadhi yao. Hivyo wewe kama kiongozi ni lazima ujifunze kuendana na makundi yote kama Musa kule jangwani, ili kisipotee chochote. Maana yake ni kuwa usiwe na haraka ya kufikisha kundi Mahali Fulani Kwa jinsi utakavyo, vinginevyo utawaua wengine.

Yakobo alipaita mahali pale Sukothi, kwasababu ndipo alipowajengea makundi yake vibanda. Na wewe pia jenga Sukothi yako.

Bwana akubariki.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

TOFAUTI YA MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU NI IPI?

Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?

MAFUNDISHO YA NDOA.

MIGAWANYO MINNE (4), YA HUDUMA YA YESU.

Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

Rudi nyumbani

Print this post

Tatizo la kuvimba miguu kibiblia

Biblia inasema nini kuhusiana na kuvimba miguu na miguu kuuma?

Kama miguu imevimba na hujui chanzo, wala madaktari hawaoni tatizo…basi huenda ni Mungu anataka kusema na wewe jambo, ambalo ukilirekebisha basi tatizo hilo linaweza kukuisha moja kwa moja..

Hebu tusome maandiko yafuatayo katika biblia..

Nehemia 9:19  “hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; NGUZO YA WINGU haikuwaondokea wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala NGUZO YA MOTO haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonyesha njia watakayoiendea. 

20 Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.

21 Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala MIGUU YAO HAIKUVIMBA

Wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Nguzo ya Wingu, Na nguzo ya Moto ambayo ni ufunuo wa ROHO MTAKATIFU juu yao, ambaye aliwaongoza kama ROHO MWEMA, katika njia yao..

Ikiwa na maana kuwa njia waliyokuwa wanaiendea ilikuwa ni njia sahihi waliyoongozwa na Roho wa Mungu ndio maana miguu yao HAIKUVIMBA!, lakini wangeenda njia nyingine tofauti na hiyo ya Roho Mwema, basi ni wazi kuwa miguu yao Ingevimba, hata kama wangekuwa hawatembei, wamekaa tu, bado ingevimba.

Kwahiyo na wewe kama unaona miguu yako imevimba, na hujui chanzo na wala huoni dalili ya kupona, huenda upendo wa Mungu unakukumbusha kuwa umtafute Roho Mtakatifu, kwani yeye ndiye atakayeyaongoza maisha yako ya kiroho, maumivu hayo ni ishara ya upendo wa Mungu kwako kutaka kukupa zawadi ya Roho wake Mtakatifu, akuongoze katika njia sahihi.

Sasa utampataje Roho Mtakatifu?

Utampata kwa kanuni ifuatayo..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.

Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA

TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.

HUNA SHIRIKA NAMI.

Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?

Vihekalu vya fedha vya Artemi vilikuwaje? (Matendo 19:24).

MWANAMKE, BINTI, MAMA ( Sehemu ya 1)

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini samaki wasio na mapezi na magamba hawakuruhusiwa kuliwa?

Mambo ya Walawi 11:9-12

[9]Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.

[10]Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu,

[11]watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.

[12]Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.

Mapezi ya samaki, ni vile vitu kama mbawa ngumu zenye mfano wa miiba  zinazokaa Kwa juu, au pembeni au nyuma mwa mwili wa samaki.Ukitazama samaki kama perege, sato au sangara utaona mapezi Yao.Na faida za mapezi hayo ni kuwa yanasaidia kuogelea, kuelea vema kwenye maji, kukunja Kona, kuongeza kasi na kusimama au kugeuka Kwa haraka.

Halikadhalika samaki waliokuwa na magamba ndio tu walioruhusiwa kuliwa. Na magamba yaliwasaidia kujilinda na maadui au wadudu wavamiaji kwenye mwili. Kwani ngozi ya samaki ni laini hivyo isipofunikwa na magamba magumu kama yale, meno makali ya maadui yanapopita ni rahisi kujeruhiwa, Yanakaa kama dirii kifuani mwa askari.

Lakini si samaki wote walikuwa na haya mapezi na magamba, Bali wengine hawakuwa nayo mfano wa Hawa ni kama kambale, papa, pomboo, pwezi.

Sasa Kwanini viumbe hivyo vikatazwe kuliwa na ufunuo wake ni upi Rohoni?

Kama tunavyofahamu agano la kale ni kivuli Cha agano jipya, sio kwamba viumbe hivyo vikiliwa vitamkosesha mtu mbingu, au vitamnajisi roho , hapana. Bali vilifanywa vile kwa makusudi ili kutupitishia sisi ujumbe wa Rohoni katika agano letu jipya. Kwamba na sisi kama tutafanana na mojawapo wa viumbe hivyo Rohoni basi tunakuwa najisi mbele za Mungu.

Samaki mwenye magamba ni mwenye ulinzi wa kutosha dhidi ya mashambulizi ya maadui. Na sisi tunapokosa ulinzi wa Rohoni mfano wa yule askari anayezungumziwa katika Waefeso 6, mwenye dirii ya haki kifuani, ngao ya Imani mkononi na chepeo ya wokovu kichwani. Tunakuwa ni wadhaifu, kiasi Cha kutoweza simama mbele ya adui yetu shetani. Hivyo ni kuhakikisha kuwa umesimama imara katika wokovu wako, lakini pia utambue haki uliyopewa katika  msalaba wa Yesu Kristo na Imani Yako timilifu ndani ya wokovu wako. Hapo utakuwa umejidhatiti vya kutosha mfano wa samaki mwenye gamba gumu, au mamba aliyefunikiwa na ngozi yenye gamba.

Ayubu 41:13 “Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?  14 Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.  15 Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri.  16 Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati.  17 Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa”

Vilevile samaki aliyekuwa na mapezi alikuwa ni mwepesi kukatiza katika maji. Ni sawa na mabawa Kwa ndege, au miguu na kwa mtu. Hivyo na sisi katika ulimwengu huu wa dhambi ili tusionekane kuwa najisi tuvae mapezi yetu ambayo maandiko yanasema .Ndio ule utayari wa kuihubiri injili.

Waefeso 6:15

[15]na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

Tusienende Kama watu wasio na kusudi maalumu la kufanya duniani, tuvae utayari, ndio mapezi yetu tutembee ulimwengu kote kiuhubiri/ kushuhudia habari njema.Kwasababu tukikosa haya, siku ile ya mwisho, tutatengwa samaki wema na waovu..Kisha wale waovu watatupwa nje.

Mathayo 13:47  ‘Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;

48  hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. 49  Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki’

Tusiwe samaki najisi.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Injili iliyopo kwa Samaki aina ya Eeli.

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)

Lumbwi ni nini katika biblia?

Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.

Je! Ni dhambi kumpiga au kumuua mnyama bila sababu yoyote?

Manyoyota ni nini (Ayubu 37:6)

Rudi nyumbani

Print this post

Neno vuruvuru linamaanisha nini katika biblia?

JIBU: Kibiblia ni neno linalomaanisha “mvurugano” au “mvurugiko”

Neno hilo utalisoma katika kifungu hiki;

Isaya 17:13 “Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.  14 Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang’anya mali zetu”.

Hapo ni Bwana anawahakikishia watu wake ulinzi madhubuti dhidi ya adui zao. Anasema mambo matatu yatawakumba hao wanaojaribu kuwaangamiza watu wa Mungu.

La kwanza,watakemewa  na kukimbia mbali sana: Ni kama wakati wa washami kipindi cha nabii Elisha, Bwana alipowasikilizisha kelele za majeshi wakakimbia wakashindwa hata kuchukua na nyara zao nyuma(2Wafalme 7).

La pili ni “ watafanana na makapi mbele ya upepo: Kwa kawaida ngano inapopepetwa yale makapi huwa yanarushwa na upepo mbali sana, ndivyo watakavyofanywa waadui wa watoto wa Mungu wanapokaribiwa, watatoweka ghafla.

Na la tatu anasema  watakuwa kama mavumbi ‘vuruvuru’ mbele ya tufani: Kwa kawaida upepo  mkali wa kisulisuli au tufani  inapopita juu ya ardhi iliyokuwa kavu, ule upepo wake mkali unatabia ya kuvuruga mavumbi, na kuyafanya yaruke hewani yasambae tu ovyo vyo, na hiyo husababishia hali ya hewa kuchafuka sana. Hivyo, Bwana anasema, ndivyo itakavyokuwa kwa  watu hao, watavurugwa, kiasi cha kutokuelewana, kila mmoja atakuwa na lake, ni kuchanganyikiwa tu, Ndio maana ya hilo andiko.

Lakini ni nini Bwana anataka tujifunze?

Ni kwamba tuwapo ndani Kristo, hatuna haja ya kuwa  na hofu, kwasababu shetani na majeshi yake, yatakutana kwanza na jeshi la Bwana kabla ya kutufikia  sisi. Ndicho Elisha alichomwambia Gehazi, kwamba  jeshi letu ni kubwa kuliko la kwao.

Hivyo mtakatifu yoyote unayedumu katika wokovu (usio wa mdomo bali wa roho), ulinzi huu unao. Lakini kinyume chake ni  kweli ikiwa upo nje ya Kristo, huna ulinzi wowote kwa Bwana, na matokeo yake shetani anaweza kufanya lolote atakalo juu yako, hata kukuua.

Swali ni Je! Umeokoka?

Kama bado na upo tayari kufanya hivyo sasa basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo was ala hiyo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

Je! Sulemani alienda mbinguni?

Nini maana ya uvuvio?

MZUNGUKO WAKO NI UPI?

Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?

Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)

Manyoyota ni nini (Ayubu 37:6)

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Nuhu alimlaani Kanaani badala ya mtoto wake Hamu,

SWALI: Kwanini Nuhu alimlaani Kanaani badala ya mtoto wake Hamu, ambaye ndiye aliyekuwa na makosa?


JIBU: Ni kweli kama tunavyosoma katika maandiko, pindi ambapo Nuhu amelima shamba lake la mizazibu akaaanda divai nyingi akanywa akalewa mpaka akalala uchi hadharani, tunaona mtoto wake mmoja aliyeitwa Hamu alipomuona hakuchukua hatua stahiki kumsitiri Baba yake

Lakini wale watoto wake wawili (yaani Yafethi na Shemu) walipomwona baada ya kuambiwa na Hamu, hawakutaka kutazama bali walichukua mavazi yao mabegani Kisha wakaenda kinyume nyume wakamfunika Baba Yao. 

Nuhu alipopata taaarifa, aliyoyafanya mwanawe wa mwisho alimlaani, lakini laana yake haikuwa Kwa Hamu Moja Kwa Moja Bali Kwa mtoto wake aliyeitwa Kaanani..Sasa swali ni je Kwanini afanye hivyo Kwa Kaanani mjukuu wake, angali kitendo kimetendwa na Hamu.

Mwanzo 9:20-25

[20]Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; [21]akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. [22]Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. [23]Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. [24]Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. [25]Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

Ipo mitazamo mingi katika jambo hilo, wapo wengine wanaomini kuwa Shemu alikuwepo na mwanaye huyo mkubwa Kaanani, na huwenda yeye naye alipuuzia kumsitiri Babu yake, au alifanya jambo baya kwake,  wengine wanasema Hamu tayari alikuwa amebarikiwa na Mungu hivyo Baba yake asingeweza Tena kumlaani mtu ambaye amebarikiwa (Mwanzo 9:1),ndio maana laana akaisogeza kwa mjukuu wake.

Wengine wanaaanimi aliposema alaaniwe Kaanani, ni lugha tu iliyomaanisha pia “Baba wa kaanani”

Lakini ni vema tukaona muktadha wa uandishi wote, ikumbukwe kuwa aliyekiandika kitabu hicho ni Musa, na tunafahamu hatma ya taifa la Israeli, ilikuwa si katika mataifa yote duniani, bali pale Kaanani. Hivyo, ulikuwa ni unabii, wa Nuhu, kuonyesha moja wa uzao Shemu uitwao kaanani utalaaniwa. Hivyo tunapokuja kusoma juu ya anguko la wenyewe wa taifa lile, walivyoangamizwa na kuteketezwa na taifa la Israeli, ni kutukumbusha kuwa tayari Kaanani ilikuwa imeshalaaniwa tangu zamani, kuangamizwa kwao na maovu yao ni matokeo ya laana iliyotajwa zamani.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kanaani ni nchi gani kwasasa?

Nchi ya Nodi ambayo Kaini alikimbilia ndio nchi gani kwasasa?(Mwanzo 4:16).

Wakaanani walikuwa ni watu gani?

saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?

Rudi nyumbani

Print this post

Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)

SWALI: Mjombakaka ni nani kwenye maandiko?


JIBU: Neno hilo tunalipata kwenye vifungu hivi;

Walawi 11:29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake,

Katika agano la kale, Mungu alitoa maagizo ya wanyama wanaopaswa kuliwa na wale wasiopaswa kuliwa. Na mmoja wa viumbe vilivyokatazwa kuliwa alikuwa ni mjombakaka.

Mjombakaka kama lilivyotumika hapa kwenye maandiko ni Kobe, na aina zake zote.

Walioorodheshwa katika vifungu hivyo ni wanyama wasio na mabawa, tofauti na wale wa kwenye Mambo ya walawi 11:20-23 wenye mabawa, ambao wote kwa pamoja wamewekwa katika kundi la viumbe najisi ambavyo haviruhusiwa kushikwa au kuliwa, kwasababu “vinatambaa” yaani matumbo yao yakiburuta chini.

Lakini Mungu aliruhusu visiliwe sio kwasababu za kiafya kama wengi wanavyodhani. Hapana, kwani hata sasa zipo jamii nyingi zinakula baadhi ya wanyama hao na wanaishi bila matatizo yoyote ya kiafya, bali walikatazwa kutokana na tabia walizobeba, ambazo zinafunua jambo la kiroho ambalo mtu akiwa nalo, basi anaweza kuonekana najisi mbele za Mungu.

Kwamfano, walikatazwa kula wanyama wasiocheua, kama nguruwe. Mnyama asiyecheuwa hana sifa ya kuhifadhi chakula na kukirejesha tena mdomo kukitafuna kisha kukimeza tena kama ng’ombe. Kufunua kuwa tukiwa watu tusioweza kukumbuka fadhili za Mungu alizotutendea nyuma, tukiwa watu wa kusikia tu Neno halafu baada ya hapo ndio imeisha hatulitendei kazi, sisi mbele za Mungu tunaonekana kama viumbe najisi.

Halikadhalika na hapa, wanyama hawa walionekana najisi, kwasababu wanatambaa, matumbo yao yanagusa chini. Nyoka alipolaaniwa aliambiwa kwa matumbo atakwenda. Ikiwa na maana haikuwa ni mapenzi ya Mungu viumbe vyake vitambae, tengeneza picha mwanadamu angekuwa anatembea huku tumbo lake likiburuta chini, angekuwa mdhaifu kiasi gani.?

Vivyo hivyo rohoni, hatupaswi kutambaa, bali kukimbia. Mashindano tuliyowekewa mbele yetu sio hata ya kutembea, bali kukimbia kabisa,

1Wakorintho 9:24 “ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate”.

Hivyo hupaswi kuwa mlegevu, ukijiona upo katika ukristo ule ule miaka nenda miaka rudi, huna jambo jipya uliloliongeza katika ufalme wa Mungu, au uliloliongeza ni dogo kulinganisha na muda uliodumu kwenye wokovu wako basi ujue kuwa unatambaa na hivyo Mungu anakuhesabu kama mmoja wa wanyama najisi.

Hivyo tujitahidi tusiwe wakristo wa namna hii, onyesha bidii kwa Mungu, itende kazi ya Mungu kwa karama uliyowekewa ndani yako. Kila siku jiulize ni jambo gani jipya nimeliongeza kwa Mungu wangu. Kwasababu ukumbuke kuwa kila mmoja atatolea hesabu talanta yake aliyopewa na Mungu siku ile. Je wewe umeongeza nini kwenye ufalme wa Mungu?

Bwana atupe nguvu ya kulitendea kazi Neno lake.

Shalom.

Angalia chini maana ya wanyama wengine kibiblia.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Lumbwi ni nini katika biblia?

JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.

Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?

Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

HAKUONA MAHALI PA KUTUA KWA WAYO WA MGUU WAKE.

Nyamafu ni nini?

Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?

Rudi nyumbani

Print this post

USHUJAA WA ROHONI HAUANGALII UZOEFU WAKO.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Nakukaribisha tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu.

Leo nataka tujifunze asili ya ushujaa wa rohoni, ambao wakati mwingine tunadhani mpaka tuwe na uzoefu ndio tuweze kufanya makuu kwa Mungu. Wakati Fulani Taifa la Israeli liliingia katika hali mbaya ya njaa isiyokuwa ya kawaida, mpaka kufikia hatua ya baadhi ya watu kuchinja watoto wao na kuwala (2Wafalme 6:28-29),  Na hiyo ilikuwa ni kwasababu ya kuzungukwa na maadui zao wenye nguvu kwa muda mrefu walioitwa washami. Hivyo wakashindwa kuingiza au kutoa chochote ndani ya mji kwa muda usiokuwa mchache.

Hivyo hali ikawa mbaya sana, mfalme akafunga mji, hawajui cha kufanya, watu wamepaniki, wanakula vitu visivyopaswa kuliwa, kiasi kwamba hata ‘mavi ya njiwa’ tu yalikuwa yanauzwa kama chakula. Tengeneza picha taifa kubwa kama hilo, linakumbwa na janga la njaa kali namna hiyo, hadi askari wake wazoefu wa vita, wanatetemeka na kujificha ndani ya mji, kwasababu walijua wakitoka tu ni kifo.

Na ndicho maadui zao walichokuwa wanakisubiria kwao, aidha watoke wawaue, au wafe na njaa ndani. Hivyo hali ilikuwa ni ya kutisha sana. Lakini tunaona siku moja Nabii Elisha, akapewa unabii na Mungu, na kuambiwa kuwa chakula kitapatikana na kuuzwa kwa bei ya chini kiasi ambacho hakijawahi kuuzwa hapo kabla siku ya kesho yake, ni sawa na uambiwe siku ya kesho, gunia la mahindi, linauzwa kwa  Tsh1, wakati unatambua kuwa halipungui wastani wa bei ya Tsh,70,000. Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli, Mungu alipompa Elisha unabii huo akaambiwa siku ya kesho yake, chakula kitauzwa kwa bei ile.

Sasa kulikuwa na wakoma wanne(4), waliokuwa nje ya mji, wakoma hawa walitengwa na taifa, kwasababu ilikuwa ni kuwa watu walioathirika na ugonjwa huu watengwe mbali na makazi ya watu  wao wasije kuleta maafa hayo ndani ya jamii, ni sawa na ugonjwa wa Ebola tunavyouona sasa, ndivyo ilivyokuwa ukoma kwa wakati ule.

Tengeneza picha watu hawa walikuwa ni wagonjwa, hawana wa kuwatazama, na zaidi sana wamekuwa dhaifu kwa njaa kali. Lakini tunaona walishauriana jambo kisha wakafanya maamuzi, ambao ndio ulikuwa ukombozi wa taifa la Israeli; Tusome hapo;

2Wafalme 7:1 Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 

2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula

3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 

4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 

5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 

6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 

7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 

8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 

9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 

10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 

11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.

Ni nini kimejificha hapa?

Siri nayotaka uone ambayo imejificha nyuma ya hawa wakoma wanne, ni kwamba, pindi tu walipoamua kufanya uamuzi, wa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha yao, na kuanza mwendo, kuelekea kambi ya maadui, kumbe kule kwenye kambi ya washami, wanasikia kama JESHI kubwa sana la maaskari linawafuata. Hivyo wakakimbia kwa kasi sana, na kuacha kila kitu nyuma. Lakini wale maaskari wa kiisraeli waliokuwa wazoefu wakati huo wamejifungia ndani ya mji hawadhubutu kuchukua hatua..

Watu waliokuwa dhaifu na wagonjwa, ndio waliowafukuza washami na kuleta ukombozi Israeli. Watu wanne tu, waligeuka kuwa jeshi la maaskari elfu rohoni.

Hiyo ni kutufundisha nini?

Na sisi pia pale tunapoamua kufanya jambo kwa ajili ya Mungu, bila kujali hali zetu au udhaifu wetu, tufahamu kuwa jeshi la shetani linaogopa na kutetemeka kushinda hata sisi tunavyoweza kudhani. Daudi alijijua kuwa yeye si mtu wa vita, hajazoea vita, hawezi kutumia upanga wala mkuki, lakini yeye ndiye aliyesimama, kinyume na Goliathi, na kulifukuza jeshi lake lote.

Hivyo, hupaswi kujidharau, ikiwa umeokoka leo, au jana, usiseme mimi sina uzoefu, au sijui biblia vizuri, kama kushuhudia watu wenye dhambi ambao wengine wameshindwa, wewe nenda, usisubiri mpaka mchungaji wako afanye hivyo, hujui kuwa wakati huo ndio Mungu kakuchagua kuwa sababu ya ukombozi kwa wengine.

Hivyo, popote unapojiona hukidhi vigezo, fahamu kuwa rohoni ndio unakidhi. Unajiona hustahili, jua tu kwa Mungu unastahili, kuwa na imani, chukua hatua, usingoje ngoje. Tumia karama uliyopewa ndani yako kuujenga ufalme wa Mungu. Popote pale unapojiona unafaa, basi tumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa wengine. Na hakika rohoni shetani atatoweka kama jeshi la washami.

Bwana akubariki.

Shalom.

Je, umeokoka? Kama bado basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo huo wa kumwalika Yesu maishani mwako.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).

MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!

Yerusalemu ni nini?

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.

Rudi nyumbani

Print this post