SWALI: Nini maana ya mstari huu Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana”
JIBU: Rafiki anayezungumziwa hapo ni rafiki wa kweli ambaye humwazia mema mwenzake, Hivyo inapotokea umeumizwa kwa maneno ya Ukweli aliyokuambia, ni bora kuliko kusifiwa na watu ambao nyuma yake ni maadui zako.
Ukweli unaoumiza, ni kimelea cha upendo sahihi wa ki-Mungu. Bwana Yesu alikuwa ni mtu anayewaeleza ukweli watu wote, hususani wale mafarisayo kwa mambo ya kinafiki waliyokuwa wanayafanya kinyume na Neno la Mungu,(Mathayo 23) jambo ambalo makutano walishindwa kufanya kinyume chake walikuwa wanawasifia tu masokoni kila walipowaona, lakini matokeo yake ikawa ni wao kumchukia Yesu badala ya kumpenda.
Mtume Paulo alilikemea kanisa la Galatia, kwa tabia yao ya kurudia mafundisho manyonge kiwepesi, ambayo walikuwa wameshayaacha huko nyuma mpaka akawakemea na kusema hamna akili, ni nani aliyewaloga?. Wao walitegemea kuambiwa mambo ya faraja wakati wote, lakini haikuwa hivyo wakati huu, bali lilikemewa sana na Paulo, na ndio maana akasema maneno haya;
Wagalatia 4:16 Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?
Lakini alikuwepo Yuda ambaye alimsaliti Bwana wake kwa kumbusu, akijifanya kama anampenda kumbe, anamundia njia ya kumsaliti.
Maana yake ni kuwa, ukikaa na ndugu, ambaye anakueleza ukweli unaokupasa hata kama ni kwa kukukemea au kukukaripia, na unakuumiza mpende huyo kuliko makundi ya watu wanaokusifia wakati wote hata pale unapokosea. Ukikaa katika fundisho ambalo unakemewa dhambi na mambo yako mabaya na mwenendo usiostahili, ni heri hapo kuliko kubaki katika mafundisho ambayo yanakusifia na kukufariji wakati wote.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?
VITA DHIDI YA MAADUI
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
USIWE ADUI WA BWANA
Haini ni mtu gani? Mithali 13:2
Rudi nyumbani
Print this post
JIBU: Jibu ni ndio.
Kosa alilolifanya Sulemani la kushawishiwa na wake zake kuwajengea madhabahu miungu, (1Wafalme 11:3:13) maandiko hayatuthibitishii kuwa lilikuwa ni endelevu, kana kwamba alimwacha Mungu moja kwa moja, hapana, au alitenda dhambi isiyosameheka kabisa hapana. Ni wazi kuwa Sulemani alitubu, kwa kosa lile, tunaposoma kitabu cha Mhubiri ambacho alikiandika katika uzee wake, kinatupa picha ya mambo mengi ambayo aliyatenda au aliyadhania kuwa ni sawa lakini mwisho wake akagundua ni ubatili ni sawa na kuufuata upepo. Na ndio maana mwisho kabisa akahitimisha, kuwa jumla ya yote yampasayo mtu ni kumcha Bwana na kuepukana na uovu. Kuonyesha kuwa Sulemani aligundua usahihi upo wapi, kabla hajafa.
Lakini pia asingetajwa katika vizazi vya ukoo wa Bwana Yesu kama angekuwa ni mmojawapo wa waliopotea. Hivyo hatuwezi kusema kuwa Sulemani alikwenda kuzimu, hata kama hakuna maandiko ya moja kwa moja yanayoonyesha mahali alipotubu.
Kikubwa tujifunze katika kosa alilolifanya. Maandiko yanasema kutii ni bora kuliko dhabihu. Kama Sulemani angetii agizo la Bwana la kutokuoa wanawake wa-kimataifa, hayo yote yasingemkuta. Lakini alidhani kwa hekima zake kuwa nyingi asingeweza kudanganyika. Ndio alikuwa mjanja mwanzoni katika ujana wake, lakini sekunde za mwisho za uzee wake shetani alimpiga mweleka. Zipo dhambi ambazo shetani anakuandalia uzitende baadaye, lakini maandalizi yake anayatengeneza sasa. Tii kila agizo la Mungu, hata kama ni dogo kiasi gani, hata kama litaonekana ni jepesi kulishinda kiasi gani sasa, wewe tii, kwasababu Mungu anaona mbele wewe unaona hapa. Simama katika Neno, sio katika mitazamo yako, ndipo utakapoweza kumshinda shetani, ikiwa wenye hekima kama hawa walinaswa katika tundu bovu wewe ni nani usinasike pindi unapolipuuzia Neno la Mungu linalokusemesha moyoni mwako uache hiyo tabia au hiyo dhambi?.
Bwana atusaidie.
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?
Nchi ya Nodi ambayo Kaini alikimbilia ndio nchi gani kwasasa?(Mwanzo 4:16).
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’? Mhubiri 3:11
JIBU:
Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Mwanadamu alivyoumbwa ni tofauti na wanyama au viumbe hai vingine. Kwani vyenyewe tangu vilipoumbwa mpaka sasa havibadiliki, wala haviendelei, kimaarifa, kiuelewa, au kiujuzi.. Lakini sisi wanadamu kila siku ndani yetu kuna kiu ya kujua zaidi na zaidi, kufahamu zaidi na zaidi, kutafuta zaidi na zaidi, kutokuridhika hata kama tumepata.. Na hiyo ndiyo inayotupelekea kupiga hatua mpya kila leo. Sasa hiyo hali isiyokoma ndani yetu ndio inayoitwa UMILELE.
Na Mungu ameiruhusu iwepo ndani ya mwanadamu, kuvumbua, mambo mapya, tangu zamani hata sasa, na anafanya bidii kutafuta akidhani labda atafikia ukomo anaoutazamia, lakini kila kunapokucha ndipo anapogundua kuwa bado sana kuyaelewa mambo ya Mungu. Wanadhani pengine kwa kugundua ndege, ndio itawafikisha mbinguni, lakini kumbe, ndio wanaona anga halina mwisho.
Maana yake ni kuwa, hata milele yote ya maisha, au ya maarifa, au ya uvumbuzi kamwe hatutakaa tummalize Mungu. Yatosha sisi kukaa katika pendo lake, kuyatenda mapenzi yake katika Kristo Yesu,. Lakini tusipoteze nguvu zetu kumtafiti Mungu, ni heri tutumie hizo kuutafiti utukufu wake ili tumwabudu kuliko kuzitafiti njia zake, au kanuni zake alizojibunia, tutapoteza muda.
Sulemani alisema..
Mhubiri 8:17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Dumu katika mapenzi yake Mungu, tunayojifunza kupitia biblia, kwani hilo ndio FUNGU letu tulilowekewa.
Ndio maana ya hilo Neno; Mhubiri 3:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi? Umejiandaaje? Tubu mgeukie Bwana akuponye.
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
SWALI: Biblia ilimaanisha nini iliposema Kaini ‘Akatoka mbele ya uso wa Bwana’. Kutoka kule kulimaanisha nini?
JIBU: Tunaona baada ya Kaini kumuua ndugu yake Habili kwa wivu, ambao ulizuka baada ya sadaka yake kukataliwa na ya ndugu yake kukubaliwa. Mungu alimsemesha, na kumweleza laana yake itakayompata baada ya pale. Lakini mwisho wa maneno yale, Tunaona Kaini anaonekana akitoka mbele ya uso wa Bwana. Maana yake ni nini?
Tusome.
Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. 13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni”
Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni”
Kutoka mbele ya uso wa Bwana hapo, sio Kuahirisha mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea baina yake yeye na Mungu hapana. Bali ni kumwacha Mungu moja kwa moja. Yaani kwa ufupi mkataba wake na Mungu aliumalizia pale. Hakuna cha dhabihu tena wala sadaka, wala kumwomba Mungu, wala kujihusisha na tendo lolote la kiibada. Akaanza kujishughulisha na mambo ya kidunia tu, na sayansi, na utafiti na uvumbuzi, na akafanikiwa sana katika bidii yake hiyo, yeye na uzao wake wote, wakawa watu hodari duniani, lakini waovu sana (Soma Mwanzo 4:20-22). Na hawa ndio waliopelekea gharika kuletwa duniani.
Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, wao waliendelea kuwepo mbele ya uso wa Bwana, wakitaka fadhili na rehema kwa Mungu daima,wakiliitia jina lake.
Mwanzo 4:25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana”.
Mpaka sasa makundi haya mawili yapo duniani. Lipo ambalo halina habari na Mungu,(Ambao ndio uzao wa Kaini rohoni) bali mambo ya kidunia tu, na limefanikiwa sana katika hayo, ni jepesi katika uvumbuzi na utafiti, lakini Mungu kwao ni kama historia za mababu wa kale, ni kama vile mashariki na magharibi zilivyo mbali. Lakini sisi hatupaswi kufanana wa watu hao. Bali kama Watoto wa Adamu kwa Sethi. Furaha yetu ipo katika Bwana. Tegemeo letu ni yeye, na nguvu zetu ni yeye, haijalishi tutakosa vyote au tutapata vyote. Yeye ndiye atakayekuwa urithi wetu milele.
Je! Wewe upo kundi lipi? Uthibitisho ni maisha yako ulipoyaelekeza.
Hizi ni nyakati za mwisho. Kristo anarudi. Tubu mgeukie Bwana, mtafute yeye.
Maran Atha.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bustani ya Edeni ipo nchi gani?
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.
Wagalatia 6:1 ‘Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
JIBU: Hapa biblia inatupa mwongozo sahihi wa jinsi ya kuwavuta upya ndugu ambao walianguka katika dhambi.
Tunafundishwa tuwarejeshe katika Roho ya upole, maana yake sio ya kulaumu au ya ukali. Kwamfano utakuta mtu karudi nyuma katika ulevi wake aliokuwa nao mwanzoni. hapo yakupasa utumie busara kumrejesha upya ili iwe rahisi tena mtu huyo kugeuka na kutubu, kuliko kutumia ukali mfano kumkaripia au vinginevyo. Ukitumia kauli za lawama au mashtumu, si rahisi kumvuta, kinyume chake zitamfanya achukie zaidi au akasirike.
Lakini pia sehemu ya pili anasema..ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
. Maana yake ni kwamba hata wewe mwenyewe Unaweza ukajaribiwa na shetani uwapo katika kazi hii ya kuwavuta wengine waliokengeuka katika wokovu. Kwamfano huyo mlevi anaweza akakutukana, halafu wewe ukakasirika, ukaanza kurejesha lugha za matusi kwake kwasababu ya hasira, hapo tayari umeshaanguka katika dhambi.
Baadhi ya watu wa Mungu wamejaribiwa na kuanguka katika uzinzi walipokuwa wanafanya huduma Kwa watu walio wa jinsia tofauti na wao. Wengine katika anasa waliposhirikiana na watu wa kidunia waliowashuhudia habari za Yesu.
Hivyo tunapaswa tujichunge nafsi zetu sana tuwapo katika kuipeleka habari njema kwa makundi ya watu tofauti tofauti. Kwasababu na sisi pia shetani anatuwinda. Lakini Tukiwa watu wa maombi na kuliishi Neno tutajilinda sana nafsi zetu na mitego hiyo ya shetani. Ndio maana ya hilo Neno ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
Mada Nyinginezo
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.
NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU
Rudi Nyumbani
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu katika kuyatafakari maneno ya uzima.
Leo tutaona Tabia Moja ya ahadi za Mungu, na Kwa kuijua hiyo basi itakutia moyo wewe ambaye upo katika matarajio ya kuzipokea ahadi timilifu za Mungu.
Nataka tujifunze Kwa Ibrahimu. Kama tunavyojua Mungu alimwahidia kuwa atakuwa na uzao mkubwa kama nyota za mbinguni kwa idadi yake jinsi zisivyoweza kuhesabika. (Mwanzo 15:5).
Lakini katika kuzipokea haikuwa sawa na matarajio yake, Bali zilikuwa za kukwama kwama sana. Utaona Sara alikuwa mgumba, mpaka Ibrahimu anakufa aliambulia mtoto mmoja tu kutoka Kwake mwanamke aliyeitwa mama wa mataifa mengi..Lakini heri ingekuwa Kwa Ibrahimu tu, lakini bado tunaona Kwa Isaka,. Rebeka naye alikuwa na shida katika uzazi, mpaka kuwazaa wale watoto wawili yaani Esau na Yakobo, lilikuwa ni jambo la kulisumbukia sana.. Vivyo hivyo hata Kwa Yakobo, mke wake kipenzi Raheli alikutwa na matatizo hayo hayo…
Hawa wote ndio watu ambao waliahidiwa na Mungu kuwa uzao wao utaongezeka Kwa wingi Kwa mfano wa nyota za mbinguni…lakini tunaona Kila wanapotaka kuongezeka walikwama kwama.
Utajiuliza ni kwanini?
Sio kwamba walikuwa na shida au laana za ki-ukoo kama wengi wanavyodhani..au kwasababu ya majina yao yamefungwa, Jibu ni hapana.. kwasababu Mungu tayari alishambariki Ibrahimu kwa kumwambia atakuwa baba wa mataifa mengi, alishabarikiwa, lakini Mungu anataka kutufundisha sisi Tabia za ahadi zake jinsi zilivyo katika baadhi ya majira.
Sasa tunaona wakati wa Mungu ilipofika jambo hili lilikuja kugeuka ghafla. Na watu Hawa ambao walionekana ni wenye wagumba wengi.. walianza kuzaliana Kwa wingi ambao uliushtusha ulimwengu. Pindi walipoenda Misri, walianza kuzaa, Kwa kasi hata ya kulipitia taifa la Misri ndani ya wakati mfupi sana .walienda watu sabini tu lakini Kwa muda mfupi walikaribia kulizidi taifa la mamilioni ya watu.
Ikawa tishio kubwa Kwa Wamisri, mpaka wakabuni mpango wa kuwauwa watoto wote wa kiume watakaozaliwa..lakini bado hilo halikuzuia kitu. Wakati familia Moja ya Wamisri inazaa watoto wawili, familia Moja ya kiisraeli inazaa watoto kumi na Tano. ..
Kutoka 1:8-22
[8]Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. [9]Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. [10]Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. [11]Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. [12]Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. [13]Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; [14]wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali. [15]Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; [16]akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. [17]Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. [18]Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? [19]Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. [20]Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. [21]Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. [22]Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
[8]Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
[9]Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.
[10]Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
[11]Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
[12]Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.
[13]Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;
[14]wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
[15]Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;
[16]akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
[17]Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.
[18]Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?
[19]Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.
[20]Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.
[21]Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.
[22]Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
Lakini ongezeko hilo.kubwa, halikuanza hivyo.. uhodari huo wa Waisraeli kuzaliana Kwa kasi vile haikuwa kipaji, au Hali waliyokuwa nayo tangu mwanzo, Bali walianza kama Kwa kusua-sua sana..Lakini mwisho wa siku ahadi ilipokomaa ule uwingi kama nyota za mbinguni waliuona, hakukuwa na mgumba.
Ni Nini nataka tuone?
Sikuzote jambo lolote ambalo Mungu anatuahidia, ni kawaida katika hatua za mwanzo kuenda kama Kwa kusua sua hivi, SI vyepesi kuona vikitirika Moja Kwa Moja kama wengi tunavyotarajia..Kitaanza kidogo kama unaona mwanga Fulani hivi, halafu kitasimama, baadaye Kitaanza Tena, Kisha kitasimama, kitaonyesha dalili zote za kuongezeka, Kisha hakitaendelea Tena..hivyo hivyo kinaweza pita kipindi Fulani. Sasa ukijikuta katika Mazingira kama hayo hupaswi kuvunjika Moja na kujiona kama utakuwa na makosa Fulani, au Mungu ameghahiri ahadi zake..Jibu ni hapana. Hupaswi kukata tamaa, shikilia ahadi ya Mungu, ukiamini kuwa yeye ni mwaminifu lazima atimize ahadi zake kwako, kukuongeza.
Moja siku isiyokuwa na jina. Utaona mtiririko ambao haujautarajia, itakuwa siku baada ya siku ni kuongezeka tu, Wala hakuna kupungua. Wala kukwama-kwama kama mwanzo. Lakini hiyo yote hutegemea kung’ang’ana kwako na ahadi za Mungu sasa.
Jambo hili linasimama Mahali popote pale Mungu alipoweka maono yake moyoni mwako. Iwe ni katika huduma, kazi, uzao.n.k. Usiache tu kushikilia ahadi za Mungu, Tena ufurahi kwasababu maandiko yanasema hivyo, kwani uwingi wako upo karibuni.
Isaya 54:1
[1]Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Je umeokoka? Je unamtambua kuwa Yesu yupo mlangoni kurudi? Ikiwa bado unasubiri nini? Tubu dhambi zako ukabatizwe katika jina la Bwana Yesu Kristo upokee ondoleo la dhambi zako.
Kumbuka: UNYAKUO UPO KARIBU.
NINI NI KILICHOMFANYA IBRAHIMU AKUBALI KUMTOA MWANAWE SADAKA?
PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.
Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.
WEWE U MUNGU UONAYE.
Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
SWALI: Katika ule mlima mrefu, aliopanda Yesu na wanafunzi wake kuomba, kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine? Mfano wa Isaya au Samweli?
JIBU: Awali ya yote yeye kutokewa na wale watu halikuwa Kwa lengo lake. Bali Kwa lengo la wale wanafunzi aliokuwa nao, Ili kutimizi mambo yafuatayo.
a) Unabii wa kwanza ni ule alioutoa Musa kuwa atakuja Nabii mwingine kama yeye na kwamba watu wamsikilize..
Kumbukumbu la Torati 18:15
[15]BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.
Soma pia Matendo 3:22-25,. Hivyo wayahudi walikuwa na matarajio ya kuona mtu anayefanana na Musa atakayeleta Sheria mpya akija duniani, lakini akiwa na nguvu na uweza mwingi mfano wa Musa..
Ndio sababu ya Musa kutokea mbele ya wanafunzi wake, ili Mungu awathibitishie huyu ndio yule Musa aliyemnenea habari zake.
b) Lakini pia unabii uliohusu kutangulia Kwa Eliya kabla ya Kuja kwake duniani.
Wanafunzi walikuwa na dukuduku kama huyu, ndiye Kristo aliyetabiriwa au sio, na kama ndio mbona Eliya hajatangulia mbele yake tukamwona? Kwasababu waliambiwa hivyo na waandishi. Lakini sasa walipomwona Eliya mwenyewe amesimama mbele ya Yesu wakaamini lakini bado hawakuelewa..Sasa walipokuwa wanashuka ndio wakapata nguvu ya kumuulizia hilo swali.. Na hili ndio likawa jibu lake.
Mathayo 17:9-13
[9]Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. [10]Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? [11]Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, [12]ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. [13]Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
[9]Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
[10]Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
[11]Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
[12]ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
[13]Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Utakumbuka kabla ya kupanda mlimani aliwaliza watu kuwa wanamzungumzia kuwa yeye ni nani? Wanafunzi wakamjibu kuwa wanasema yeye ni Eliya, wengine mmojawapo wa manabii wa Kale.n.k. Hivyo kulikuwa na utata mwingi. Lakini siku hiyo alitoa utata huo Soma.Mathayo 16:13-18.
Mitume walipoona sura za manabii wao wa kale wamesimama mbele ya Yesu, mwenye utukufu mwingi sana kupitia wao. Wakaamini yeye ni zaidi ya manabii wote wakubwa Kwa wadogo waliowahi kutokea katika historia.
Musa alikufa, lakini Eliya alipaa.
Yesu ndio mtu pekee miongoni mwa wanadamu, aliyekufa, Kisha akazikwa, kisha akafufuka.na mwisho akapaa. Kwa hiyo Ile ilikuwa ni lugha ya kinabii, kueleza hatma yake na ndio maana hata manabii Hao walikuwa wakizungumza mambo yahusuyo kufa kwake na kufufuka.(Luka 9:31).
Hizo ndio zilikuwa sababu kuu za Bwana kutokewa na manabii wale wawili na sio wengine. Na walipokuwa wanashuka Akawaambia wanafunzi wake wasimwambie mtu mpaka atakapofufuka katika wafu.
Kufunua nini?
SI wote watamwona Yesu katika kilele Cha utukufu wake, isipokuwa wale tu walio na kiu na yeye. Ambao watakuwa tayari kuwa karibu naye wakati wote mfano wa Hawa wanafunzi watatu yaani Yohana, Petro na Yakobo.
Ukimpenda Yesu tumia muda mwingi kuwepo uweponi mwake. Utamjua sana Kwa mapana na marefu yake.
Je! Umeokoka? Je unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi? Dalili zote zimeshatimia, unasubiri nini usimpe Bwana maisha yako, embu fanya uamuzi leo. Tubu dhambi zako, mgeukie Yesu, Unyakuo usikupite. Ikiwa utapenda upate mwongozo huo, wasiliana nasi kwa namba zetu hizi bure +255693036618 /+255789001312
Shalom
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
LAKINI MAKINDA WAWEZA KUYATWAA UWE NAYO.
Jina la Bwana Yesu litukuzwe Daima. Nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Mungu.
Lipo andiko ambalo tunaweza kuona ni la kinyonge lakini linatiba kubwa sana kama tukilitumia. Embu tuone ni nini mwandishi huyu mwenye hekima aliomba Kwa Bwana
Mithali 30:7-9
[7]Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. [8]Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. [9]Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Nataka uone hapo aliposema..
“Usinipe umaskini wala utajiri;”
Katika maombi yetu ni rahisi sana kumwomba Mungu asitupe Umaskini, lakini ni ngumu sana kumwomba Mungu asitupe “UTAJIRI”.. Nadhani huo ndio ukweli..
Utajiri ni Ile Hali ya kuwa na uwezo wa kumiliki au kuwa na vitu vingi.
Lakini huyu mtu hapa anamwekea Mungu mipaka katika maeneo hayo mawili, yaani Utajiri na Umaskini, Kwa lugha nyingine anamwambia Mungu sitaki UTAJIRI.. na sababu anaitoa pale “Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani?”
Alijua Kuna madhara ya kuwa na tamaa ya kutaka vitu vingi, mfano kuwa na mabilioni ya pesa kwenye akaunti, kuwa na mahekari ya mashamba mengi, kuwa na nyumba nyingi za kuishi na za kupanga, kuwa na magari mengi n.k. Alijua hayo ni matamanio ya Kila mwanadamu lakini alikataa kuyaomba kabisa.
Lakini Watu wengi tunaposoma huu mstari tunaelekeza mawazo yetu kwenye mambo ya Mali tu. Lakini Bwana anamaanisha pia utajiri wa kiroho.
Uchu huu wa kupata Kila kitu, kuwa na Kila kitu, umewavaa watu wengi hata watumishi wa Mungu. Labda utaona anakwenda mbele za Mungu, maombi yake na matazamio yake ni kuwa na upako kuliko watu wote, anachotaka ni Mungu ampe karama zote za Roho. Yeye naye awe Nabii, awe Mchungaji, awe mwinjilisti, awe mwalimu, awe mtume, awe na karama zote 9 za Roho. Yaani atakaposimama mimbarani watu wamwone yeye ni kama Yesu. Awe mhubiri wa Dunia nzima wa kimataifa, mwenye mafunuo mengi kuliko wote duniani, mwenye kanisa kubwa kuliko yote duniani.
Maombi ya namna hii ni maombi ya utajiri. Na mara nyingi tunapoomba hivi Bwana Huwa hatupi, kwasababu si mapenzi ya Mungu kuomba vitu vilivyo zaidi ya uwezo wetu alivyotukirimia. Kila mmoja kawekewa kipimo chake na Mungu. Na katika hicho ndio tunaomba Mungu akibariki. Lakini si kila huduma Kila karama itakuwa ni yako.
1 Wakorintho 12:28-30
[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. [29]Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? [30]Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?
[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
[29]Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?
[30]Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?
Hivyo pale tunapokuwa na Nia ya kiasi, ndipo Mungu anapotuongezea neema, na ndio tutakapomtumikia Mungu vizuri. Hekima inatufundisha tubadilishe matamanio. Yetu kutoka katika UCHU, mpaka “kutosheka na mishahara yetu”. Na hivyo tutafanya vizuri zaidi katika huduma, karama, na utumishi wetu Kwa ujumla. Watu watasaidika na kile ulichonacho sasa, kuliko kile usichokuwa nacho unakingoja.
Nabii Eliya ambaye alikuwa ni mkuu Kwa nguvu za Mungu, lakini pamoja na hayo hata katika maombi yake alisema “Mimi SI mwema kuliko Baba zangu (1Wafalme 19:4)”akataka Bwana asitishe huduma yake. Kwasababu aliona kama kipimo kile hakustahili kupimiwa.. Hakuwa na uchu wa kiroho. Si ajabu Kwanini Mungu akamtumia Kwa viwango vikubwa namna Ile.
Bwana atusaidie tuonyeshe sasa bidii katika nafasi zetu alizotukirimia leo, zaidi vile ambavyo tunavitazamia kesho. Tutumike Kwa kadiri ya alivyotujalia.
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.
Biblia inasema askofu anapaswa awe mume wa mke mmoja! Je! Wale wasiooa kwa ajili ya injili hawawezi kuwa maaskofu?
SWALI: Mstari huu unamaana gani? Mithali 19:21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.
JIBU: Kila moyo wa mwanadamu, unamatamainio mengi, lakini uhalisia ni kwamba sio matamanio yote ni ya ukweli au yanania nzuri baadaye, kwamfano mtu atataka mali nyingi, lakini moyo wake unasema atakapopata nyumba kubwa na gari atawakomoa waliomdharau, atalipiza kisasi, atafanya anasa ,atatembea kwa majigambo, ataongeza Masuria.
Na ndio maana mengi ya malengo kama haya yawezi kusimama kwa watoto wa Mungu, kwasababu yana hila nyingi nyuma yake. Mtume Yakobo aliliweka wazi jambo hili, ni kwanini wakati mwingine hatupokei majibu ya maombi yetu alisema..
Yakobo 4:2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”
Lakini kinyume chake anasema Shauri la Bwana ndilo litakalosimama. Maana yake ni kuwa Hekima ya Bwana inayopima haya yote imaamua cha kutoa na kutokutoa. Hivyo si matamainio yako yote unayoyaona ni mema, basi yatakuwa mema pia mbele za Mungu, mengine yana udaganyifu mwingi. Ndio maana Yeremia 17: 9 inasema “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua”?
Hivyo tuombapo jambo ni busara kumalizia na kusema “Bwana mapenzi yako yatimizwe”.
Amen.
Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala Mwangalie sana
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
JIFUNZE KUDUMU UWEPONI MWA MUNGU.
Je ni kweli Yuda hakuwa na dhambi kwa kumsaliti Bwana, kwasababu tayari ilikuwa imeshatabiriwa?
Mhubiri 10:16 “Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!”
Mstari huu umegawanyika katika sehemu mbili;
Hapo mhubiri anajaribu kueleza uhusiano uliopo kati ya uongozi na ukomavu wa mtu. Akatumia mfano wa kijana, kwasababu mara nyingi ni ngumu sana kuipata busara kwa vijana, kutokana na kuwa hawana uzoefu mwingi wa maisha na pia hawajaandaliwa vya kutosha, kumudu nafasi za uongozi, kinyume chake kitakachowaongoza ni hisia tu za ujana na si vinginevyo. Na ndio maana mtu kama Sulemani alilitambua hilo alipotawadhwa tu mfalme akiwa bado kijana mdogo, alimwomba Mungu ampe hekima ya namna ya kuwaongoza watu wake. Na Bwana akamjalia.
1Wafalme 3:7 “Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili”
1Wafalme 3:7 “Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.
9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili”
Walikuwepo pia wafalme wengine waliotawadhwa wakiwa wadogo kama Yoashi, lakini akasaidiwa na kuhani Yehoyada katika ufalme wake, na ukawa bora (2Wafalme 11-12)
Lakini tunakuja kuona kwa mwanawe Sulemani aliyeitwa Rehoboamu. Yeye naye alikuwa ni kijana lakini hakutaka mashauri kwa wazee waliomtangulia, kinyume chake, akasikiliza mashauri ya vijana wenzake Hivyo ikapelekea ufalme wake kugawanyika, na kupoteza makabila kumi kati ya kumi na mbili ya Israeli.(Soma 1Wafalme 12:1-16)
Maana yake kwamba kuwa na viongozi ambao wanatanguliza maslahi yao kabla ya kazi, nchi hiyo sikuzote huishia pabaya. Sikuzote watu wanakwenda kufanya kazi asubuhi, wakitarajia kile walichokihangaikia kutwa nzima ndio wakifaidi jioni, lakini hapa tunaona ni kinyume chake. Na jambo hili ni kweli, Tunaona katika baadhi ya mataifa yanayoendelea, wananchi wao wanapitia katika taabu, na umaskini wa hali ya juu, kutokana na kuwa viongozi wao, wanatazama maslahi yao binafsi wanapoingia madarakani na sio maslahi ya taifa.. Uchu wa madaraka na ukuu, ndio wanachokitazama lakini sio kujenga mataifa yao.
Hii inafunua nini rohoni?
Neno hili linawahusu, watumishi wote wa Mungu wanaosimama katika ngazi za uongozi. Ikiwa wewe bado ni kijana au mchanga katika huduma(hata kama una-mvi) na umepewa kundi ulichunge, Omba sana hekima kwa Mungu, pia kuwa tayari kujifunza kwa waliokutangulia, Sikuzote viongozi-wachanga, katika hatua za awali wanajiamini kuwa wanajua kila kitu, lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanavyotambua kasoro zao nyingi. Hivyo ili kuepuka, kufanya makosa ya kiutumishi, tafuta sana msaada kwa Mungu katika hekima na mashauri.
Lakini pia, ikiwa wewe ni mchungaji, askofu, mtume, mwalimu, au unatumika katika huduma yoyote, epuka tamaa hususani ya mali. Si kila shilingi unayoipata uipeleke tumboni, au kujijengea majumba na biashara. Ni heri ukatazama kwanza hali ya kanisa la Kristo. Kama mchungaji mwema yakupasa kuipendezesha kwanza nyumba ya Bwana, kisha Baadaye Bwana mwenyewe ndio akupendezeshe wewe. Unatembelea gari ya Tsh milioni 40, halafu kanisa ni la makuti, Hapo ni nini unategemea kama sio ufukara wa kiroho hadi kimwili baadaye.
Kwahiyo hekima hizi zinatuonya, ili uongozi wetu usianguke mbeleni, hivyo tuzingatie sana maneno haya ya hekima. Bwana akubariki.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
VIJANA NA MAHUSIANO.
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?