Ni kwa namna gani baraka ya Bwana haichanganyi na huzuni, nyuma yake?
Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”
JIBU: Kwanza ni vema kufahamu hapo anaposema ‘Baraka ya Bwana hutajirisha’ hamaanishi kuwa kipimo cha kuwa umebarikiwa na Bwana ni utajiri unaofuata baada ya hapo, hapana, Kwasababu wapo watu ambao si wakristo na hawamchi Mungu lakini ni matajiri, na wapo ambao si matajiri na wengine ni maskini kabisa lakini ni matajiri kwa Bwana.
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani”.
Baraka ya Bwana haipimwi kwa mali, bali kwa mwitikio wa wokovu ndani ya mtu.
Lakini katika mstari huo, anaeleza tofauti iliyopo kati ya utajiri unaopatikana kwa Mungu na ule unaopatikana penginepo. Kwamba ule wa ki-Mungu Hauchanganyi huzuni ndani yake. Lakini ule wa kwingine unafuatana na huzuni nyingi nyuma yake.
Kwamfano mtu amepata mali kwa njia ya biashara ya madawa ya kulevya. Ni wazi mtu kama huyu hawezi kuwa na raha, kwasababu wakati wote atakuwa katika kujilinda, na mashaka ya kukamatwa na vyombo vya dola. Au mwingine kapata utajiri kwa njia ya rushwa, atakuwa na hofu sikumoja kukamatwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuhujumu uchumi. Au mwingine kwa njia ya uganga, atapewa masharti, atoe wengine kafara, au alale chooni sikuzote za maisha yake, ili utajiri wake uendelee.
Hivyo utajiri wowote nje ya ule unaopatikana na Mungu, unavimelea vingi vya mateso. Visasi, vinyongo, wivu, hofu, mashindano n.k. Kwa kifupi ni kuwa hauna raha, Hivyo Bwana anatushauri kama kufanikiwa tufanikiwe kwake ambapo kunaendana na kanuni ya kumcha yeye kwa bidii (Kumbukumbu 28), kufanya kazi halali, na kuwa mtoaji. Na utakapobarikiwa basi Bwana atakupa raha katika vitu hivyo.
Bwana awe nawe.
Je! Upo ndani ya Kristo? Kama ni la! Wakati ndio sasa, geuka upokee ondoleo la dhambi zako kwasababu muda ni mchache tuliobakiwa nao, tubu pokea wokovu sasa Parapanda inakaribia kulia. Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA
Ni sahihi kwa mkristo kupokea fedha kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu?
Rudi nyumbani
Print this post
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Swali: Maandiko yanasema “Haki huinua Taifa”.. Je hii imekaaje kiundani zaidi?
Jibu: Tusome,
Mithali 14:34 “HAKI HUINUA TAIFA; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote”.
Kwa tafsiri ya kawaida mtu mwenye haki ni yoyote yule anayefanya matendo ya haki bila kujali kile anachokiamini, lakini kibiblia ni tofauti kidogo…Kibiblia mtu “mwenye haki” ni yule anayemcha Mungu na “asiye haki” ni yule asiyemcha Mungu.
Kwahiyo hata kama mtu atajitahidi kufanya matendo mazuri na yenye kukubalika katika jamii yake yote, lakini kama moyoni mwake hamwamini Mungu, huyo kibiblia ni mtu asiye haki hata kama ana sifa njema.
Kwahiyo wanapoongezeka watu wanaomcha Mungu wengi katika Taifa maana yake “Haki na yenyewe inazidi kuongezeka”. Na matokeo ya kuwepo Wenye haki wengi juu ya nchi kuliko wasio haki ni kunyanyuka kwa Taifa, na kinyume chake wanapokuwepo wasio haki wengi katika nchi kuliko wenye haki basi Taifa linakuwa hatiani kuanguka. Sasa utauliza ni kwa namna gani?.. Hebu tujikumbushe kidogo ile habari ya Ibrahimu na Elohimu wakati ule wa Maangamizi ya Sodoma na Gomora
Mwanzo 18:22 “Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. 23 Ibrahimu akakaribia, akasema, JE! UTAHARIBU MWENYE HAKI PAMOJA NA MWOVU? 24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, WALA HUTAUACHA MJI KWA AJILI YA HAO HAMSINI WENYE HAKI WALIOMO? 25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? 26 BWANA AKASEMA, NIKIONA KATIKA SODOMA WENYE HAKI HAMSINI MJINI, NITAPAACHA MAHALI POTE KWA AJILI YAO. 27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. 28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. 29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. 30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. 31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. 32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake”.
Mwanzo 18:22 “Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.
23 Ibrahimu akakaribia, akasema, JE! UTAHARIBU MWENYE HAKI PAMOJA NA MWOVU?
24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, WALA HUTAUACHA MJI KWA AJILI YA HAO HAMSINI WENYE HAKI WALIOMO?
25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
26 BWANA AKASEMA, NIKIONA KATIKA SODOMA WENYE HAKI HAMSINI MJINI, NITAPAACHA MAHALI POTE KWA AJILI YAO.
27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.
29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.
30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.
31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.
32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake”.
Umeona? Kumbe Miji ya Sodoma na Gomora iliteketea kwasababu ya kukosekana wenye haki ndani yake, kumbe wangeonekana tu wenye haki 10, basi miji ile yote ingepona!…lakini walipokosekana ndipo miji ile ikaanguka na kuangamia.
Ikiwa na maana kuwa Amani ya Miji na Mataifa ni kwasababu ya wenye haki ndani yake, ni kwasababu ya watu wa Mungu kuwepo ndani yake, hao wakiondolewa Taifa au mji unaanguka na kuangamia.
Ndio maana maandiko yanazidi kutufundisha kuwa dhiki kuu haitaanza mpaka Kanisa (wenye haki) watakapoondolewa, ikimaanisha kuwa uwepo wa watu wa Mungu katika dunia ndio unaozuia mambo kuharibika.. lakini hao watakapoondolewa ndipo Mataifa yataanguka, na ulimwengu mzima kwa ujumla.
2Wathesalonike 2:6 “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; LAKINI YUKO AZUIAYE SASA, HATA ATAKAPOONDOLEWA. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
2Wathesalonike 2:6 “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; LAKINI YUKO AZUIAYE SASA, HATA ATAKAPOONDOLEWA.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
Je na wewe ni miongoni mwa wenye haki?
Kumbuka katika zama hizi tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo… Na si kwa matendo yetu yasiyo na Imani yoyote…
Wagalatia 2:16 “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki”.
Maran atha!
Mataifa ni nini katika Biblia?
Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)
TUNA WAJIBU WA KUOMBEANA KWA KINA.
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 14:23 “Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu”
JIBU: Kitabu cha Mithali na Mhubiri ni vitabu vilivyobeba mafunzo mengi sio tu yale ya kiroho bali pia hata ya maisha ya kawaida. Mstari huo unaelezea uzito wa kitu kinachotendewa kazi zaidi ya kile kinachozungumzwa tu. Kwamfano hapo anaanza kwa kusema “katika KILA KAZI mna faida”.. Maana yake ni kuwa katika kazi yoyote (iliyonjema), inafaida nyuma yake,. Iwe ni ya kudharaulika au yenye heshima, iwe ni ngumu iwe ni rahisi, iwe ni ya kipato kikubwa au kidogo, maadamu kazi fulani inatendeka ni lazima faida tu itaonekana nyuma yake.
Lakini mtu akiwa ni wa mipango mikubwa, mikakati mingi, akili nyingi za kubuni namna ya kutenda kitu Fulani, vikao vingi, halafu hakitendei kazi, Bwana anasema, badala ya faida kinyume chake ni hasara tu atapata..
Vivyo hivyo na katika roho. Bwana anataka tuwe watendaji wa Neno lake, Sio kusikia tu au kuomba tu peke yake. Unaweza ukaomba usiku kucha lakini kama sio mtendaji wa Neno lake uliombalo, ni unapoteza nguvu tu.
Kwamfano unaomba Bwana akusaidie uushinde uasherati, lakini bado unashikamana na vichocheo vyake vyote, una picha chafu kwenye simu yako, kinywa chako kinazungumza mambo ya kizinzi na vijana wenzako, unachati na watu wa jinsia tofauti muda wote, unatazama tamthilia zenye maudhui hayo, unasikiliza miziki ya kidunia, unaishi na boyfriend/girlfriend. Unategemea vipi tamaa zisikutawale? Utaomba usiku kucha na hutaona matokeo yoyote, kwasababu hukitendei kazi kile unachokiomba.
Bwana alisema kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa ndani yake.(Yakobo 2:17). Kukitendea kazi kile kimoja ukiombacho, kina nguvu sana kuliko maneno elfu unayoweza kumwomba Mungu mwaka mzima.
Yakobo 1:22 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo”.
Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;
Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
Isaya 46:3 “Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani; 4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa”.
Isaya 46:3 “Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa”.
Mstari huu wa faraja unatuonyesha fadhili za Mungu jinsi zilivyo nyingi kwa watu wake, Anaonyesha jinsi asivyoweza kuwaacha watu wake, tangu wakiwa tumboni mwa mama zao hadi kufikia uzee wao. Kila hatua ya maisha yupo nao, kila pito liwe rahisi au liwe gumu yupo nao, wakiwa watoto, wakafikia ujana, kisha nguvu zikaisha wakiwa wazee, Mungu yupo nao. Haleluya.
Daudi alilitambua hilo pindi alipoishiwa nguvu zake, akaandika…
Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula”.
Hivyo huna haja ya kuhofu kesho yako itakuwaje au uzee wako utaishaje, maadamu upo na Bwana, maadamu unamtumikia, siku hizo zikifika, atakuhifadhi Mungu wako. Mwingine anasema mpaka sasa sina mfuko wa mafao, na nguvu zangu zinakaribia kuisha, ni nani atakayenisaidia, ni nani atakayekuwa karibu na mimi? Jibu ni kuwa Bwana ndiye atakayekuwa karibu na wewe. Kwasababu tangu zamani ulimtumainia. Lakini hata kama utakuwa na mali, huwezi kuwa na raha moyoni wakati huo endapo Kristo hayupo nafsini mwako sasa.
Hivyo wekeza maisha yako kwa Bwana sasa, ili kesho yako pia iwe na matumaini na raha tele. Ikiwa wewe ni kijana wakati huu uliopo, mtafute muumba wako, upokee WOKOVU kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu, mtumikie Mungu, kimbia kweli kweli tamaa za ujanani, kabla zile nyakati mbaya za hatari hazijafika, Kwasababu maandiko yanasema kuna siku-mbaya mbeleni zitawakumba watu ambao hawakumcha Mungu tangu zamani.
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.
Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako leo , na kumkaribisha Bwana Yesu maishani mwako, basi bofya hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU
UFANYE WEMA WAKO KATIKA MAARIFA.
ANGALIENI MWITO WENU.
Praitorio ni nini? Na Kwanini ilikuwa ni najisi kwa wayahudi kuingia humo? (Yohana 18:28)
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.
Ayubu 20:4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi, 5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu? 6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni; 7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
Ayubu 20:4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,
5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?
6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
Waovu wanayo ‘shangwe’ maandiko yanasema hivyo, lakini shangwe yao ni ya muda mfupi tu. Usishangae kuona mtu ni tapeli na muuaji lakini anaishi maisha ya raha, yenye afya, watoto wake wanafanikiwa sana, uso wake unang’aa kila wakati, na biashara zake zinachanua. Ndio! hilo jambo lisikushtushe, kwasababu maandiko hayatuahidi kuwa waovu watapitia shida wakati wote duniani. Hapana.
Tena anasema wataweza kufikia kuwa na ukuu usio wa kawaida mfano wa kuifikia mbingu, ikiwa na maana wanaweza kuonekana hata ni miungu duniani. Lakini hiyo yote ni kwa muda tu, siku watakapokufa habari yao itakuwa imeishia hapo, Biblia inatumia mfano wa ‘Mavi’ jinsi yapoteavyo, ndivyo watakavyopotea watu hao milele.
Hakuna mtu anaweza kukitafuta kinyesi chake alichojisaidia mwaka jana au mwezi uliopita,. Ni wazi kabisa alishakisahau, na tayari kilipofika chooni kiliyeyuka na kuingia katika mfumo wa chemba ya maji machafu, kikatowekea huko. Sasa ndivyo itakavyokuwa kwa mtu Yule ambaye anashindania raha ya dunia hii anaacha kutafuta raha ya kudumu inayotoka kwa Yesu Kristo peke yake.
Zaburi 92:7 Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;
Yesu alisema itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako, au utatoa nini badala ya nafsi yako? Ujue kuwa kusudi la wewe kuwepo duniani sio kula na kunywa, au kupanda na kujenga au kuwa milionea au kuwa maarufu. Bali ni kuyatenda mapenzi ya Mungu kwanza kisha hayo mengine yafuate baadaye.
Kubali kubadilika leo Yesu ayaponye maisha yako. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa mwongozo wa kumpokea Yesu maishani mwako >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?
Beelzebuli ni nani? (Mathayo 12:24).
SHUGHULIKA SANA NA DHAMBI YA KUSAHAU.
Je! tunaweza kuwaamuru Malaika kama tunavyoyaamuru mapepo?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)
Kumwambia mtu mwenye dhambi kuwa atakwenda kuzimu asipotubu Je! ni kuhukumu?
Ayubu 5:6 “Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi;”
Watu wengi tumekuwa tukilaumu mazingira, tukilaumu wanyama, tukilaumu ardhi, na vitu vingine vya asili kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu, chanzo ya shida zetu na mashaka yetu rohoni. Lakini maandiko yanatupa uhalisia kwamba taabu na mashaka havichupuki ardhini, kama vile mchicha umeavyo, bali vinatoka ndani yetu wenyewe.
Makosa yetu ndio zao la kila aina ya matatizo yetu. Asili ya migogoro katika ndoa, sio ule m-buyu uliokaribu na nyumba zetu. Unaweza kuhama hata nchi ukakaa chini ya mizeituni na mizabibu mizuri, na maua, lakini bado ndoa yako ikaendelea kuwa na matatizo tena makubwa zaidi hata yale ya mwanzo.
Sababu ya kuteswa na mapepo, sio Yule paka mweusi wa jirani anayekuja kulala batini kwako kila siku usiku. Bali ni kwasababu Kristo hayupo ndani yako.
Sababu ya kutokupiga hatua kiroho, sio hiyo ardhi unayoishi, au unayoimiliki, usihangaike na maombi ya kufungua/ kukomboa ardhi, hangaika na vifungo vilivyomo ndani yako. Ambavyo vinatokana na aidha kutolielewa Neno la Mungu, au kuwa nje ya wokovu.
Biblia inasema..
Yohana 8:36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
Na tena inasema…
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Rekebisha mwenendo wako, pokea wokovu wa kweli, kisha liishi Neno la Kristo kila siku. Hakika utaona jinsi tatizo lako linavyotalika kirahisi, ndipo utaacha kuyalaumu mazingira ya nje.
Je! Umeokoka? Kama bado unasubiri nini? Je! Unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi, tunaishi katika muda wa nyongeza tu, siku yoyote unyakuo wa kanisa unapita, watakatifu kuchukuliwa mbinguni na wenye dhambi kwenda motoni?. Fanya uamuzi sahihi sasa, ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.
LAKINI WAKATI WA TAABU WATASEMA, SIMAMA UKATUOKOE.
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
SWALI: Mhubiri anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona, anamaana gani,?
JIBU: Tusome,
Mhubiri 7:27 Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla; 28 ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona.
Ukichunguza hapo utaona Sulemani hajaenda moja kwa moja kutaja mtu aliyemwona Kwamba ni mtu ‘mkalimifu’ au ‘ mtu anayeelekea ukamilifu’.
Katika maisha yake ya kuchunguza na kulinganisha mambo kwa hekima ya ki-Mungu, aliona kuna vitu Fulani vipo katika jinsia fulani na kuna vitu Fulani havipo katika jinsia husika,. Kumbuka Sulemani alikuwa na uzoefu wa kuishi na wanawake wengi, alikuwa na wake mia saba na masuria mia tatu, bado na wakwe zake kama angependa kuwahesabu, jumla yao ingekuwa ni kubwa sana. Hivyo alipokuwa anayasema maneno hayo, hakuwa anabahatisha mawazo yake, au anaonyesha udhaifu kwa wanawake hapana..
Sulemani aliona katika jambo la juhudi ya kuulekea ukamilifu wote aliouhitaji Mungu, halikuwa kwa jinsia zote, bali kwa jinsia ya kiume tu, na tena kati ya hao ni wachache sana aliowaona, yaani mmoja kati ya elfu, lakini kwa wanawake hakuwahi kuona hata kwa mmoja,. Lakini hakumaanisha kwamba mtu huyo aliyemwona tayari alikuwa ni “Mkamilifu”..Kwasababu kipindi chote kile alichokuwepo, hakukuwahi kutokea mwanamume aliyempendeza Mungu kwa utimilifu wake wote, isipokuwa wapo waliojitahidi kusogelea hatua hizo lakini hawakufikia, mfano wa hao ni kama Ayubu, na Henoko. N.k. Lakini hao wote bado hawakuwa wakamilifu kwa viwango Mungu alivyovitaka, japo kulikuwa na vimelea hivyo, tofauti na katika ile jinsia nyingine.
Lakini maono yake yalikuja kutimia kwa mwokozi wetu YESU KRISTO, yeye ndiye aliyeishi asilimia mia maisha ya ukamilifu ya kumpendeza Mungu bila kutenda dhambi yoyote,ambaye alijaribiwa kama sisi tulivyojaribiwa bila kumkosea Mungu. Na ndio maana kwanini Masihi hakuja katika jinsia ya kike, kuukomboa ulimwengu bali jinsia ya kiume.
Hivyo huyo mwanaume pekee aliyefikia ukamilifu ni Yesu tu, Sisi wengine wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, iwe ni wa jinsia ya kike au ya kiume. Na wote tunaokolewa kwa neema yake tu pindi tunapomwamini yeye. Hiyo ikiwa wewe bado hujaupokea wokovu, na unatamani kufanya hivyo sasa, basi bofya hapa ili uweze kupata mwongozo huo wa kumruhusu Kristo aingie maishani mwako akuokoe.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?
MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.
Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?
Biblia inasemaje kuhusu Nywele?
Shalom, nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mwokozi wetu. Karibu tujifunze maneno ya uzima maadamu siku ile inakaribia.
Katika siku hizi za mwisho ni lazima uwe makini sana na mahali ulipo, kwasababu zama zimebadilika, si kila jambo la kuliamini, vilevile si kila jambo la kutoliamini. Unamuhitaji Roho Mtakatifu sana kukusaidia kuchagua kilicho sahihi.
Bwana anatufananisha sisi na kama kondoo, na yeye kama mchungaji. Na sikuzote, mchungaji mwema, huwa anawapeleka kondoo wake katika maji ya mito-salama. Na si kila mto ilimradi mto tu anawapeleka kondoo zake kunywea maji hapana, bali pale tu palipo na maji ya utulivu ndipo anapowapeleka kondoo zake.
Ndio maana katika Zaburi ya 23 Inasema;
Zaburi 23:1 ‘Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. 2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza’.
Ni kwanini maji ya utulivu, kwasababu maji yenye mvurugano, au yaliyotibuliwa yana hatari nyingi, huwenda ni makao ya viboko na mamba na hivyo kutembea kwao huko ndio kunafanya maji Yale yawe na mvuragano, kwahiyo kondoo akinywa maji pale yupo hatarini kuvutwa na mamba, akafanyika kitoweo.
Au huwenda maji hayo ni mkondo wa mafuriko, hivyo kitu chochote kitakachotelezea kule mtoni, si rahisi kupona kinyume chake ni kitasombwa na kupotelea mbali.
Hivyo maji yasiyotulia, si salama kwa mifugo. Na mchungaji apendaye kondoo huwa hawapeleki mifugo yake hapo.
Ndivyo ilivyo kwa Kristo, anapotuokoa, anatuongoza kwa Roho wake palipo na maji ya utulivu tukae hapo tunywe. Lakini tatizo linakuja ni sisi kuyakataa maji ya utulivu, tunayatafuta maji ya mivurugano.
Ndugu usiangalie ukubwa wa mto, au ukubwa wa Bwawa, haikuhitaji wewe kunywa mto mzima ndio ukate kiu yako. Namaanisha usiangalie wingi wa watu, au ukubwa wa jengo na madhabahu iliyopambwa, au utajiri wa kanisa ndio ufikiri kuwa hapo ni salama kwa roho yako. Bali tazama palipo na utulivu wa kiroho. Hapo ndipo utulize nafsi yako. Kwasababu unaweza kwenda mahali kwa lengo la kuikata kweli kiu yako kwa Bwana lakini kinyume chake ukakutana na mamba wakali wakakumaliza kabisa.
Palipo na maji salama ni wapi?
Kwanza ni pale Palipo na fundisho la Yesu: Yesu ndio maji yenyewe tulivu ya uzima, na sio nabii au mtume au askofu, au kanisa, au pesa, au umaarufu.. Hivyo angalia kiini cha fundisho unalofundishwa mahali ulipo, je yote yanalenga kukukuza kumjua Yesu au linakupeleka katika mambo mengine? Fikiri Tangu umekaa hapo, ni nini umeongeza katika kulijua Neno la Kristo katika kweli yote. Lakini Kama umejazwa maarifa ya ki-mwili tu zaidi yale ya Kristo, yaani ya ki-ndoa, ki-uchumi, uchawi, biashara, pesa, hiyo ni injili nyingine, ni mafuriko ya adui, hakuna maji tulivu hapo, utazombwa na kuangamia kabisa.
Yohana 4:13 “Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele”
Palipo na Upendo: Hicho ni kigezo cha pili.
Yakobo 3:16 “Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya”.
Katika mkusanyiko wowote, fundisho la tendo la upendo wa ki-ndugu linapuuziwa, au halihimizwi, ndani kuna vita visivyokoma kati ya washirika, pengine huwenda na viongozi kwa viongozi, hiyo ni ishara kuwa utulivu wa Roho haupo hapo, hivyo ni hatari pia kwa maisha yako ya kiroho.
Tujitahidi sana kuwa na vipimo hivi vya kiroho katika kuchagua mahali tukusanyikapo kupata maji ya uzima, vitakusaidia sana, kwasababu hizi ni siku za mwisho, na manabii wengi na makristo wa uongo na madhehebu na dini za uongo zimezuka kila pembe ili kuwatoa watu kwenye mstari.
Yajali maisha yako ya kiroho. Mpende Kristo na Agizo lake.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
WALIKUWA WAMECHOKA NA KUTAWANYIKA KAMA KONDOO WASIO NA MCHUNGAJI.
JE! UNAMPENDA BWANA?
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’ (Mithali 24:16)
JIBU: Ili kuielewa vema mstari huo tuanzie vifungu vya juu yake kidogo.
Mithali 24:15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; 16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
Mithali 24:15 Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
Hapo anazungumzia tabia za mtu mbaya anayejaribu kuharibu kazi za mtu mwema (mtakatifu). Kwamba anaweza kudhani kuwa kufanikiwa kwa mipango yake, kutamfanya Yule mtu akate tamaa ya kuendelea mbele, lakini kinyume chake, ni kuwa bado atanyanyuka tena na kuendelea mbele.
Kwamfano, watu Fulani wanaweza kuharibu umoja wa kanisa, kwa kupachika fitna na masengenyo ndani yake, na matokeo yake ikawa ni kanisa kuvunjika au kugawanyika, lakini kiuhalisia watoto wa Mungu wa kweli, wenye mbegu ya Mungu ndani yao, watasimama tena na kuujenga ule umoja walioupoteza. Lakini wengine wasio wa Mungu, watakimbia, au watakata tamaa na kurudi nyuma, na kufurahia kuanguka kule.
Au jengo la kanisa linaweza likaharibiwa na wapagani au mazingira ya asili, lakini watu wenye mbegu ya Mungu hawakati tamaa watanyanyuka na kulijenga tena upya.
Ndivyo ilivyokuwa kipindi cha wafalme wakati ambapo hekalu la kwanza linabomolewa na Nebukadreza mfalme wa Babeli, Baadhi ya wayahudi hawakumwacha Mungu wao moja kwa moja, bali waliendelea kumtafuta na kumwomba sana (Akiwemo Danieli) hatimaye baada ya miaka 70 wakarudi kulijenga upya tena. Hata baadhi ya wafalme walipotoa tamko la kusitishwa kujengwa kwa hekalu hilo bado walisimamia kusudi lao lilelile mpaka kulimaliza ijapokuwa waliwekewa vikwazo vingi sana.
Halikadhalika Injili ya mitume ilizuiliwa mara nyingi, Kwamfano Paulo anasema shetani alimzuia mara tatu ili asiipeleke injili (1Wathesalonike 2:18). Wakati mwingine alifungwa Lakini hayo hayakumkwaza na kumfanya aache kuihubiri injili, kisa amezuiliwa, bali kila siku maisha yake yalikuwa ni ya utumishi kana kwamba hakuna kikwazo chochote mbele yake, hata alipokuwa gerezani alihubiri kwa nyaraka, ambazo baadhi ya hizo ndio hizi zinazofanyika Baraka kwetu hadi sasa.
Kama mitume wangehesabu vikwazo, vitisho, vifungo, kamwe wasingeweza kuieneza injili ile ulimwenguni kote kwa kasi ile. Hivyo na sisi, tufilisikapo, tupatapo hasara, tufiwapo, tusalitiwapo na baadhi ya ndugu, ikapelekea mpaka huduma kuvurugika, au maisha ya kiroho kudorora, tusife moyo wa kumtumikia Bwana au kuendelea mbele, bali tunaanza tena upya, kana kwamba ndio tumezaliwa tena mara ya pili leo.
Lakini mstari huo haumaanishi, kuanguka katika “dhambi”, kama wengi wanavyodhani. Mtakatifu hana tabia ya kuanguka anguka ovyo kwenye dhambi..Yaana leo adondoke kwenye uzinzi, halafu kesho tena aanguke kwenye uzinzi, kesho kutwa hivyo hivyo, halafu awe bado na nguvu ya kusimama kwa Bwana. Hilo jambo haliwezi kutokea kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili.
Kuanguka kwetu ni kuwekewa vikwazo na adui, vilivyo nje ya uwezo wetu, lakini sio vile vilivyo ndani ya uwezo wetu.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako (Mithali 27:23)
Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;
Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)
Kwanini samaki wasio na mapezi na magamba hawakuruhusiwa kuliwa?
Mierebi ni aina ya miti inayostawi Mahali palipo na maji maji, Mahali pengine popote haistawi. Tazama mwonekano wake kwenye picha juu.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja Neno hili;
Mambo ya Walawi 23:40
[40]Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.
Isaya 44:2-5
[2]BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua. [3]Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; [4]nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji. [5]Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.
[2]BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
[3]Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;
[4]nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.
[5]Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.
Soma pia Ayubu 40:22, na Isaya 15:7
Kama tunavyosoma hapo Bwana aliwaagiza Wana wa Israeli watumie matawi yake kama kitu Cha shangwe katika sikukuu ya vibanda..Pindi wanapokusanyika wayanyanyue juu wamwimbie Bwana nyimbo za furaha. Lakini bado tunaona sifa ya mti huu ni kuwa karibu na vijito vya maji.
Vivyo hivyo na watu wa Mungu Rohoni, Bwana anawaona kama mierebi yake, miti inayostahili kumsifu Bwana..Kwasababu ndani yao mito ya maji ya uzima inatiririka.. lakini wengine ambao hawana Kristo ni sawa na miti mikavu tu.
Na matokeo ya kukosa mito ya uzima ndani yako ni wewe kufanyika makao ya mapepo kwasababu mapepo ndio Yanakaa sehemu isiyo na maji.
Soma
Mathayo 12:43-45
[43]Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. [44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. [45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Umeona? Unasubiri nini usimpe Bwana Yesu maisha Yako? Huna Raha, Wala Tumaini, Wala faraja unapokuwa nje ya Kristo. Okoka Leo Bwana ayaponye maisha Yako.
Ikiwa upo tayari kuchukua uamuzi huo wa kuokoka na kufanyika Mwerebi mzuri wa Bwana basi fungua hapa Kwa ajili ya mwongozo huo>>
Mretemu ni mti gani?
Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?
Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?
Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?
NUNUA MAJI YA UZIMA.
Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).