Hadaa ni nini kibiblia? (2Petro 2:14)

Hadaa ni nini kibiblia? (2Petro 2:14)

Kuhadaa ni kudanganya, au kulaghai, kutumia njia isiyosahihi/ ya mkato kufanikisha au kupata jambo.

Neno hilo utalipata katika vifungu hivi baadhi;

Mwanzo 31:20 “Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia”

Mithali 12:5 “Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa”

Warumi 1:28  Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 1.29  Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na HADAA; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya

2Petro 2:14  wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;

2Petro 2:18  Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;

Mifano halisi ya kuhadaa ni hii;

> Kama mume, unapotoka na kwenda kwenye kumbi za starehe kucheza miziki na kuzini na kulala huko na makahaba, kisha unamwambia mke wako umesafiri, huko ni kuhadaa.

>Kama mfanyabiashara, unapopunguza uzito jiwe la mizani, ili umpimie mteja kipimo kidogo kwa bei ileile, au unapozidisha bei ya bidhaa juu zaidi ya ile iliyo elekezi, huko ni kuhadaa.

> Kutumia ujuzi wako, au utumishi wako, kusema uongo, ili kupata maslahi Fulani kutoka kwa huyo mtu. Kwamfano wewe ni mchungaji, halafu unasema Bwana ameniagiza mtoe kiwango Fulani cha fedha kila mmoja ili kupokea uponyaji kutoka kwangu, . Hapo umewahadaa watu wa Mungu, kwasababu unajua kabisa tumeambiwa tutoe bure, kwasababu tulipokea bure.

Tabia ya kuhadaa ni tabia ya shetani, kwani ndio silaha ya kwanza aliyoitumia kumwangusha mwanadamu pale Edeni, alipokwenda kumuhadaa Hawa, kwa kumwaminisha kuwa akila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hatokufa. Lakini ilikuwa kinyume chake.

Bwana Yesu anasema, shetani ni baba wa uongo. Hivyo na sisi tunapodhihirisha tabia hii ya kutumia udanganyifu na hila, ni wazi kuwa tunadhihirisha tabia za wazi na za asili za shetani.  Kumbuka Hadaa ni zao la wivu na kutokupenda maendeleo kwa wengine.

Tukiwa na upendo. Tabia hii itakufa ndani yetu. Tuutafute upendo wa Mungu

Je! Unasumbuliwa na dhambi hii au dhambi nyingine yoyote? Yesu pekee ndio tiba, atakusaidia kuishinda. Ikiwa upo tayari leo kumfanya kuwa Bwana na kuupokea msamaha wake bure. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA.

Sukothi ni nini? (Mwanzo 33:17).

Kuba ni nini (Ayubu 22:14)?

Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?

Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;

Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments