Title September 2019

Usiku huu wa leo wanataka roho yako!” Ni wakina nani hawa?

SWALI: Luka 12:20 inasema “USIKU HUU WA LEO WANATAKA roho yako!” Ni wakina nani hawa wanaoitaka roho yake?

Luka 12:13 Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

JIBU: Tunaona huyu mtu mawazo yake yote yalikuwa kwenye Mali tu, akijitumainisha katika mali za dunia hii, asijitajirishe kwa MUNGU, alifahamu kwa wingi wa mali zake hata akiumwa anao madaktari wataalamu wa kumuhudumia. Lakini biblia inasema “Usiku wa leo WANAITAKA roho yako!”…Kumbuka haijasema ANAITAKA roho yako, hapana bali WANAITAKA, ikiwa na maana kuwa ni Zaidi ya mmoja.

Pengine wakati amestarehe usiku na familia yake, kulikuwa na majambazi mahali Fulani, tayari wamejiandaa kuja kumvamia na kumuua ili wachukue mali zake, na yeye hapo hajui chochote, au pengine wachawi walimwonea wivu kwa mafanikio yake, sasa wakati huo huo usiku walikuwa vilingeni wakimpangia mikakati ya kumuua kichawi .Au Pengine maadui zake, walimpangia tukio baya usiku huo huo la kumwangamiza, n.k. Sasa hawa wote kwa ujumla ndo hao WANAOITAKA roho yake kama biblia inavyosema. Laiti mtu huyo angekuwa amejitajirisha kwa Mungu, Mungu angemwepusha na hizo hatari zote,lakini yeye aliona Mungu sio kitu cha maana sana kwake kulinganisha na Mali, aliona mali kwake ni ulinzi Zaidi ya Mungu.

Vivyo hivyo na sisi tunazungukwa na hatari nyingi sana pasipo kujua. Tunapotumainia mali au wanadamu kama kinga zetu,badala ya YESU KRISTO na kuudharau WOKOVU unaopatikana kwa njia ya msalaba, na kuona ni kitu kisichokuwa na maana, kama huyu tajiri na ulinzi wake wote, hakupona mikononi mwa shetani..biblia inasema Waebrania 2: 3 “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”

Na pia inasema.

Zaburi 127: 1 “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure”.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

UNYAKUO.

NGURUMO SABA

MIHURI SABA

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno;” maana yake nini?

SWALI: Nini maana ya huu mstari? “Mathayo 13:30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. ”


JIBU: Mfano huu Bwana alioutoa unahusu siku za mwisho, na kumbuka siku za mwisho ndio hizi tunazoishi sasa mimi na wewe, kwamba Bwana atatuma wavunaji watakaovuna watu, sasa ili kuelewa hawa wavunaji ni wakina nani hebu tusome mstari ufuatao..

Mathayo 9:37 “ Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”

Unaona hapo, siku hizi za mwisho, wahubiri ndio wavunaji, na siku hizi za mwisho Bwana amesema atawatuma wengi,wa ukweli na wauongo, ambao watawavuna watu wote walioko ulimwenguni (waovu na wema), wale walio waovu (wanaofananishwa na magugu) watafungwa matita matita (yaani watafungwa katika madhehebu mbali mbali) na watasubiria kutupwa katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, kwasababu ni magugu.

Kama unapenda uasherati, utapata muhubiri atakayekufariji katika uasherati wako, vivyo hivyo na mambo mengine maovu, utapata wahubiri na waalimu na makanisa yanayochukuliana na hayo mambo.

Lakini wale walio wema(yaani zile ngano njema) zitakusanywa pamoja na kuhifadhiwa ghalani (na ghalani ni mbinguni), wale walio tayari kufumbua macho yao waone, kufumbua masikio yao wasikie, Bwana anawakusanya katika siku hizi za mwisho kupitia wahubiri wake waaminifu na wa kweli na kuwaweka tayari kwa ajili ya unyakuo.

Je! Na wewe umejiandaaje? Huu ni wakati wa kukusanywa,Unakusanywa wapi leo? Kwenye dhehebu lako? au katika Neno la Mungu?.

Kanisa/muhubiri asiyekuhubiria kwamba Ibada za sanamu,ulevi,ulavi,ulawiti,uongo,rushwa,wizi,masturbation, chuki,usengenyaji,uvaaji vibaya, ni tiketi ya kwenda motoni, basi huyo ni mvunaji ametumwa kukufunga katika tita lake, na kukupeleka motoni, Biblia inasema mtu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni na pasipo huo UTAKATIFU hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Ubarikiwe!

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

HUIJUI KAZI YA MUNGU, AFANYAYE MAMBO YOTE.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.

LULU YA THAMANI.

MSHIKE SANA ELIMU.

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

TUZIJARIBU HIZI ROHO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

YESU alimaanisha nini aliposema “mkono wako ukikukosesha ukate?

Mathayo 5:29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.


JIBU: Hapo ni kama inavyojieleza, kiungo kinaweza kikawa kiungo kama kiungo cha mwilini, hususani viungo vya uzazi hivyo ndivyo vinavyowakosesha wengi,…lakini pia kinaweza kikawa kiungo cha nafsi yako, mfano ndugu, marafiki, jamii, kazi, fani, n.k….Yaani kwa ujumla chochote kile kinachoweza kukufanya usiwe na uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa ukiweke kando, mana ni heri kufanya hivyo uokoke kuliko kuwa nacho kisha ukaishia kuzimu.

Kwasababu Bwana Yesu alishasema katika,

Mathayo 16: 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?.

Ubarikiwe!

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

LULU YA THAMANI.

KWANINI USIICHAGUE TUZO ISIYOHARIBIKA?

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;

SWALI: Nini maana ya huu mstari? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.


JIBU: Hiyo ni hekima ya kidunia Sulemani aliiona ambayo pia inafananishwa na mambo ya rohoni. Ni wazi kuwa zizi lisilokuwa na ng’ombe au mfugo wowote, huwa ni safi ikiwa na maana kuwa hakuna mnyama atakayeweza kulichafua kwa kinyesi, au mikojo, au majani, hivyo kama ni mtu analimiliki hatateseka kwa namna yoyote ile kuligharamia, hatapoteza muda wake mwingi kulitunza, yeye atalifunga tu kwasababu litaendelea kuwa safi daima na kukaa pasipo na taabu yoyote, lakini mtu kama huyo kipo kitu atakikosa..

Lakini zizi ambalo lina mifugo, kama ng’ombe n.k. tunafahamu zizi kama hilo haliwezi kuwa safi kwasababu ng’ombe watakuwa wanajisaidia huko kila saa, mikojo itakuwa inafagiliwa mara kwa mara, kadhalika zizi nalo litapaswa liwe linapigwa dawa za kuuwa wadudu kila wakati vinginevyo mifugo haitaweza kukaa, zizi pia ni lazima liwe na majani ya kutosha, kama tunavyofahamu Ng’ombe ni mnyama anayekula sana hivyo mmiliki itampasa awe maporini muda mwingi kutafuta majani ya mifugo…Hivyo mmliki wa zizi hilo atapata dhiki na taabu nyingi zaidi ya yule ambaye zizi lake halina mfugo wowote isipokuwa huyu taabu yake haitakuwa ya bure, kuna wakati ataona taabu ya kuhangaika kwake.

Na ndio hapo tukirudi kwenye mithali anatumbia “bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi”…Hii Inamaana gani?.


Inamaana kuwa yule ng’ombe atakwenda KUMLIMISHA katika shamba lake, na kumletea faida nyingi kwa nguvu zake, tofuati na yule aliyeona ni taabu kumlea ng’ombe, siku ya ukulima wake itampasa sasa yeye mwenyewe akalime au aajiri kibarua.

Kadhalika katika roho, wengi wanapenda kuwa na mavuno mengi kwa Bwana, lakini hawapendi kuingia gharama za kuyafikia. Bwana Yesu aliwaambia makutano waliokuwa wanamfuata, wale waliopendezwa na njia ya Bwana lakini hawakuwa tayari kuingia gharama..soma

Luka 14: 25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Hivyo na sisi pia tunapashwa ili tuwe na mavuno mengi Bwana anatuagiza tuwe tayari kuingia gharama za kuyapata mavuno hayo..Na gharama zenyewe ndio hizo Bwana alizozitoa hapo juu.


Amen.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

TWEKA MPAKA VILINDINI.

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?

NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?

KITENDAWILI CHA SAMSONI

JINA LAKO NI LA NANI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

JIBU: ZAKA/FUNGU LA KUMI Ni moja ya kumi au sehemu ya kumi ya mapato yako yote, hicho huwa kinakwenda kwa Bwana na ni wajibu kwa kila mkristo mwenye shughuli ya kujipatia kipato kumtolea MUNGU sehemu hiyo ya mapato yake..

Walawi 27: 30 “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.”

Malaki 3: 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

Sasa fungu la kumi au zaka ni tofauti na ‘sadaka/matoleo’. SADAKA yenyewe ni kile ulichonacho juu ya fungu la kumi, kile ulichokirimiwa pasipo sharti lolote la utoaji unampelekea Mungu, sasa zipo sadaka za aina tofauti tofauti kulingana na mahali au mtu mwenyewe, kwa mfano zipo.

1) sadaka za shukrani, hizi huwa mtu anatoa baada ya Mungu kumtendea au kumfanikisha katika jambo Fulani, aidha, afya, ulinzi, masomo, biashara, kazi, familia, n.k. Huwa anaambatanisha sadaka yake ya shukrani mahali Bwana anapolia kiroho ni tofauti na fungu la kumi.

2) Zipo sadaka nyingine za michango: Hizo zipo nyingi kulingana na uhitaji wa kanisa, mfano jengo, uenezaji injili, vyombo vya nyumba ya MUNGU, mahitaji n.k. Hivyo sadaka/matoleo yapo ya aina nyingi, na pia Mungu hajaweka sharti lolote la utoaji ni jinsi mtu atakavyoguswa moyo na Mungu wake, ndicho atakachotoa.

Kutoka 35:5 Katwaeni kati yenu matoleo kwa Bwana; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;

Kwahiyo jambo la kukumbuka pia katika agano jipya, ni kwamba Mungu hajamwekea mtu sheria au tanzi yoyote katika kutoa ZAKA hata kama hajisikii tu atoe , hapana hiyo haipo katika Ukristo kwasababu Mungu hapendezwi na mtu atoaye kwa moyo wa huzuni au wa kulazimishwa. Lakini ni vizuri pia ikumbukwe kuwa ni wajibu wa kila mkristo yoyote kumtolea MUNGU wake aliyemuokoa. Ni ngumu kwa mtu yeyote kusema amejazwa Roho halafu suala la utoaji kwake ni mzigo.

2Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.”

Ubarikiwe ndugu.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

UDHAIFU WA SADAKA!

CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!

NUHU WA SASA.

UTIMILIFU WA TORATI.

UPEPO WA ROHO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Pentekoste ni nini?

SWALI: Matendo ya mitume 2:1 ″Hata ilipotimia “SIKU YA PENTEKOSTE” walikuwako wote mahali pamoja.Ndugu zangu hiyo Siku ya Pentekoste ilikuwa ni siku gani? Pentekoste ilimaanisha nini ndugu.?


JIBU: Pentekoste ni neno la kigiriki lenye maana “YA HAMSINI” . Hivyo kwa wayahudi walikuwa wanasherekea siku ya hamsini baada ya sikukuu ya pasaka (waliagizwa na Bwana wafanye hivyo) lakini wenyewe walikuwa hawaiiti kwa jina hilo la pentekoste, walikuwa wanaiita hiyo sikukuu kama “SIKU KUU YA MAJUMA”.

Bwana Mungu aliwaambia wahesabu majuma 7 yaani sabato 7 baada ya pasaka, yaani siku 49, na siku ya hamsini ( ndiyo pentekoste) wafanye sikukuu…Soma (Kumbu. 16:9 na Walawi 23:15).

Kwahiyo sasa kwasababu mambo yaliyokuwa yanafanyika agano la kale yalikuwa ni kivuli cha agano jipya, ilikuwa ni lazima sikukuu hizo ziwe na uhusiano mkubwa na mambo ya agano jipya,. Kwahiyo wayahudi pasipo kujua lolote walishangaa Roho Mtakatifu anashuka juu yao siku ile ile ya Pentekoste ambayo walikuwa wanasheherekea hiyo siku kuu yao ya Majuma, kama tu kusulibiwa kwa Bwana kulivyoangukia katika siku kuu yao ya pasaka kadhalika kumwagwa kwa Roho kuliangukia katika siku kuu yao ya majuma (yaani pentekoste). Na ilikuwa ni siku ya HAMSINI baada ya sikukuu ya Pasaka.

Ubarikiwe sana.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada Nyinginezo:

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.

NINI MAANA YA KIPAIMARA?.NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

ITAFAKARI VEMA KAZI YA MUNGU

MAFUNUO YA ROHO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

SWALI:Kama kijana mmoja yeye alimtuhumu muhubiri mmoja kuwa yeye ana KOSA HAWAONGOZI WATU SALA YA TOBA..Hilo ni kweli unaweza kumhesabia mhubiri kosa kwasababu hawaongozi watu sala ya toba ndugu zangu??Hiyo sala ya toba ikoje ndugu zangu?.


JIBU: Wokovu sio suala la kumsaidia mtu kufanya, wokovu ni jambo linalotoka katika moyo wa mtu…Kwasababu neno TOBA lenyewe linamaana ya KUGEUKA na sio KUZUNGUMZA…wapo watu wanasema hiyo sala usiku kucha lakini maisha yao hayageuki, kwasababu haitoki moyoni…na pia yupo asiyeisema hiyo sala lakini moyoni mwake akadhamiria kweli kugeuka na kuacha mienendo yake mibaya kuanzia huo wakati, Sasa mtu kama huyo mbele za Mungu ndiye aliyetubu.

Kumbuka ule mfano Bwana Yesu alioutoa juu ya wale wana wawili tukisoma katika

Mathayo 21: 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.

30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.

31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.”

Unaona hapo?, mimi binafsi kabla sijatubu nilishaongozwa sala ya TOBA mara nyingi, lakini muda mfupi baada ya pale nilirudi katika maisha yangu ya kale ya dhambi…lakini siku moja nilipoona mwenyewe ubaya wa dhambi na kuona umuhimu wa mbingu na YESU KRISTO maishani mwangu, sikuongozwa sala ya toba na mtu yeyote, lakini yale ya nyuma yote nilidhamiria kuyaacha kwa kumaanisha kuyaacha na kuanza kumtazama Mungu, na tangu huo wakati na kuendelea Mungu akawa upande wangu kunishikilia mpaka hivi sasa nimesimama kwa neema zake.

Hivyo kazi ya muhubiri sio kumwongoza mtu sala ya TOBA, hapana bali kumjengea mtu mazingira ya yeye mwenyewe kuchukua uamuzi wa kutubia dhambi zake…kwasababu TOBA halisi inatoka moyoni.

Japo upo wakati mtu atakuuliza nifanye nini ili niokoke? Na hapo unaona kabisa mtu kama huyo amedhamiria kweli KUGEUKA kwa wakati huo, na hafahamu lolote kuhusu mambo ya wokovu, hapo unaweza kumwongoza Sala, na sala hiyo kiuhalisia ni kama tu kumwongezea IMANI, ya kile alichokiamua rohoni mwake..lakini sio tiketi kwamba kwa kupitia hiyo amesamehewa. Hapana alishasamehewa pale tu alipodhamiria kugeuka kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake. Hivyo kama ulihubiri na hukuongoza mtu yeyote sala ya Toba, maadamu umehubiri Neno lililohai la Mungu, haupaswi kuhukumiwa na mtu yeyote, kwasababu huwezi jua tangu huo wakai ni wangapi waliotoka hapo wamegeuka kwa Neno lile au la! hata kama hakukuwa na hata mmoja aliyejionyesha katubu mbele za watu.

AMEN.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

KISASI NI JUU YA BWANA.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

JAWABU LA MAISHA YA MTU.

FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Matowashi ni wakina nani?

SWALI: Maana yake ni nini Bwana anaposema (Mathayo 19) “Maana wako 1.MATOWASHI-waliozaliwa hali hiyo toka MATUMBONI MWA MAMA ZAO; Tena wako

2.MATOWASHI-waliofanywa na WATU kuwa matowashi; tena wako 3.MATOWASHI-WALIOJIFANYA KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI.Awezaye kulipokea neno hili,na alipokee”.


 

JIBU: Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa Mungu, wasiojihusisha na mambo ya wanawake,(yaani kuwa na mke au watoto), mfano wa matowashi katika biblia ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo,Barnaba, n huwenda pia Yohana mbatizaji, Danieli na Eliya Mtishbi.

Sasa wapo wa aina tatu, wapo ambao tangu kuzaliwa tumboni mwa mama zao Mungu aliwaumba hivyo, hawana uwezo wa kuzalisha, wengi miongoni mwa hao Mungu amewachagua wawe wakfu kwake…kwa ajili ya utumishi wake.

Kadhalika wapo wengine wamehasiwa, hao ndio waliofanywa na watu kuwa hivyo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni…

Na pia wapo ambao wameamua kujifanya wenyewe kuwa matowashi..hawa hawajahasiwa wala hawana shida yoyote isipokuwa wao wenyewe wameamua kubaki hivyo hivyo wasioe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni yaani wajishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni kwa uhuru zaidi..mfano wa hao ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo, Barnaba.

Na kama Bwana Yesu alivyosema mtu yoyote awezaye kulipokea neno hilo na alipokee alikuwa anamaanisha kwamba “mtu akitaka kuwa hivyo na awe” ila sio lazima kama kama Mtume Paulo pia alivyosema kwa uweza wa Roho katika 1 Wakorintho 7:26-40.

Na pia kumbuka hiyo ni KARAMA watu wa namna hiyo huwa wanaona mke/mume kwao si kitu cha thamani kubwa sana kama kuwa tu karibu na Mungu. Hawajilazimishi wala kutumia nguvu nyingi kufanya hivyo, tofuati na wengi wanavyodhani. Mwanamke aliyejitoa kwa Mungu, kaamua kutojishughulisha na mambo ya mume, huyo naye anatafsirika kama towashi.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinaendana:

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

BIBLIA INASEMA ASKOFU ANAPASWA AWE MUME WA MKE MMOJA! JE! WALE WASIOOA KWA AJILI YA INJILI HAWAWEZI KUWA MAASKOFU?

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mtu ambaye amemwamini Yesu lakini akafa bila kubatizwa je! atenda mbinguni?

JIBU: Inategemea kama hapo kabla alishausikia ukweli au la, kwa mfano kama mtu alishaufahamu ukweli tangu zamani, na hataki kufanya hivyo au anapinga, huyo mtu atahukumiwa…Lakini kama huyo mtu ndio mara yake ya kwanza kuamini na kwa bahati mbaya akafa kabla ya kubatizwa, ataokolewa atafananishwa na yule mhalifu pale msalabani aliyekufa na Bwana.

Lakini Wapo watu baada ya kuujua ukweli, hawataki kuufanya uteule wao na wito wao imara kulingana na 2Petro 1: 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

Kadhalika biblia inasema pia katika

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. “

Soma tena hapa..

Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”.

Hivyo masuala ya rohoni ni ya kuyatimiza kwa kuogopa na kutetemeka, na sio ya kuyachukulia tu kijuu juu.. Tunapoujua ukweli na mapenzi ya Mungu tunapaswa kuyafanya.

Wafilipi 2:12”…. utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka”.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

UCHUNGU WA KUIBIWA.

UAMSHO WA ROHO.

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

nini maana ya haya maneno aliyosema Bwana ; Tuliwapiga filimbi wala hamkucheza; Tuliomboleza wala hamkulia?

SWALI 1:Bwana Yesu aliposema huu mfano alikuwa anamaanisha nini?..

“Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na WATOTO wanaokaa SOKONI,WANAOWAITA wenzao,wasisema,Tuliwapigia FILIMBI,wala hamkucheza; TULIOMBOLEZA,wala hamkulia.MAANA YOHANA ALIKUJA,HALI WALA HANYWI,WAKASEMA,YUNA PEPO.MWANA WA ADAMU ALIKUJA,AKILA NA KUNYWA,WAKASEMA,MLAFI HUYU,NA MLEVI,RAFIKI YAO WATOZA USHURU NA WENYE DHAMBI!” NA HEKIMA IMEJULIKANA KUWA INA HAKI KWA KAZI ZAKE”.(Mathayo11:16-19).


 JIBU: Mfano huo ni sawa ni kizazi cha sasa hivi tulichopo tuchukulie tu mfano, Mtu akitokea ni mtumishi wa Mungu kweli, maisha yake yote ameyachagua ni kukaa tu kanisani, au milimani kuomba, hafanyi kazi yoyote isipokuwa ni kuomba tu, na kuhudumu kanisani, hana pesa nyingi, nguo zake sio mpya sana, hana mke, wala marafiki, yeye kazi yake ni kumtumikia tu Mungu basi, kajikana maisha yake yote hataki chochote isipokuwa Mungu kajizuia kila kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni ..Unadhani watu huku nyuma watamchukuliaje mtu kama huyo??..Si ajabu watamwita mlokole masalia, au kalogwa, watasema Mungu hayupo hivyo, Mungu anataka watumishi wake wawe na maisha ya kujifurahisha, kama vile Sulemani, na sio kuwa kama vichaa wa barabarani wasiokuwa na malengo..watamwambia hakika wewe utakuwa umeingiliwa na roho nyingine ambayo si ya Mungu….hivyo hatutaweza kukusikiliza mtu kama wewe maskini wa roho na kimawazo…sisi tunawasikiliza wahubiri wenye malengo, na mafanikio.

 Lakini watu hao hao, mfano wakimuona mtumishi wa Mungu kweli labda Mungu kampaka mafuta anahubiri Neno na Mungu katika kweli yote, kambariki na maisha mazuri ya duniani, labda kampa nyumba nzuri, nguo nzuri, kampa familia nzuri, kampa mali nyingi, analo kanisa kubwa, ..utashangaa watasema, watumishi wa Mungu huwa hawapo hivyo, watumishi wa Mungu hawawezi wakawa matajiri, huwa wanakaa tu milimani wanautafuta uso wa Mungu usiku na mchana, na sio kwenye majumba ya kifahari kama watu wa mataifa…..Kwahiyo kwao pia watasema hatuwezi kuwasikiliza nyie matapeli mnakula Fedha za waumini..

 Na ndivyo ilivyokuwa katika mfano huo, Mungu alipojaribu kuwapeleka Israeli nabii aliyejikana kwa kila jambo, (Yohana mbatizaji) wakasema mtu wa kawaida hawezi kuishi maisha kama hayo ya kutokula wala kujichanganya na wengine, ni lazima atakuwa anao pepo, Lakini Bwana alipokuja anakula na kunywa pengine akidhani kuwa labda watamsikia na yeye wakamwambia ni mlafi na mlevi, manabii wa Mungu hawawi hivyo…….Ndio mithali hiyo inakuja, walipopigiwa filimbi ili wacheze wakakataa, pengine wanahitaji maombolezo, lakini pia walipoombolezewa hawakulia,..sasa waelewekeje! Kwenye raha hawapo kwenye huzuni hawapo..Na ndivyo ilivyo katika kizazi hiki..hata kipewe ishara gani ya nabii hakitaamini isipokuwa wale tu waliokusudiwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaoamini ..

Ubarikiwe!


Mada zinazoendana:

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU?

WATU WASIOJIZUIA.

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)


 

Rudi Nyumbani:

Print this post