Usiku huu wa leo wanataka roho yako!” Ni wakina nani hawa?

Usiku huu wa leo wanataka roho yako!” Ni wakina nani hawa?

SWALI: Luka 12:20 inasema “USIKU HUU WA LEO WANATAKA roho yako!” Ni wakina nani hawa wanaoitaka roho yake?

Luka 12:13 Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

JIBU: Tunaona huyu mtu mawazo yake yote yalikuwa kwenye Mali tu, akijitumainisha katika mali za dunia hii, asijitajirishe kwa MUNGU, alifahamu kwa wingi wa mali zake hata akiumwa anao madaktari wataalamu wa kumuhudumia. Lakini biblia inasema “Usiku wa leo WANAITAKA roho yako!”…Kumbuka haijasema ANAITAKA roho yako, hapana bali WANAITAKA, ikiwa na maana kuwa ni Zaidi ya mmoja.

Pengine wakati amestarehe usiku na familia yake, kulikuwa na majambazi mahali Fulani, tayari wamejiandaa kuja kumvamia na kumuua ili wachukue mali zake, na yeye hapo hajui chochote, au pengine wachawi walimwonea wivu kwa mafanikio yake, sasa wakati huo huo usiku walikuwa vilingeni wakimpangia mikakati ya kumuua kichawi .Au Pengine maadui zake, walimpangia tukio baya usiku huo huo la kumwangamiza, n.k. Sasa hawa wote kwa ujumla ndo hao WANAOITAKA roho yake kama biblia inavyosema. Laiti mtu huyo angekuwa amejitajirisha kwa Mungu, Mungu angemwepusha na hizo hatari zote,lakini yeye aliona Mungu sio kitu cha maana sana kwake kulinganisha na Mali, aliona mali kwake ni ulinzi Zaidi ya Mungu.

Vivyo hivyo na sisi tunazungukwa na hatari nyingi sana pasipo kujua. Tunapotumainia mali au wanadamu kama kinga zetu,badala ya YESU KRISTO na kuudharau WOKOVU unaopatikana kwa njia ya msalaba, na kuona ni kitu kisichokuwa na maana, kama huyu tajiri na ulinzi wake wote, hakupona mikononi mwa shetani..biblia inasema Waebrania 2: 3 “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”

Na pia inasema.

Zaburi 127: 1 “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure”.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

UNYAKUO.

NGURUMO SABA

MIHURI SABA

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply