Biblia inasema lipo WINGU kubwa la MASHAHIDI linalotuzunguka katika mashindano yaliyopo mbele yetu ukipata nafasi lisome hili wingu lote katika Waebrania sura ya 11, utaona ni jinsi gani walishinda mbio kwa saburi, na kama sisi tusipokuwa na juhudi katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu, basi zile tuzo nono kule zitachukuliwa na wengine waliostahili, ukisoma biblia inatuambia watu wale(wingu kubwa la mashahidi) ulimwengu haukustahili kuwa nao,
Walikuwa ni wasafiri duniani, watu ambao mawazo yao waliyaelekeza katika ulimwengu ujao mpaka kuhesabu maisha ya hapa duniani kuwa si kitu (mfano Ibrahimu), mpaka kufikia hatua Mungu mwenyewe anajivunia kuitwa Mungu wao kwa vile walivyoyaelekeza mawazo yao mbinguni, walikatwa na misumeno, walipigwa, walisulibiwa lakini hawakuikana imani yao,na sisi je! Tutapate kuwa kama hao kama tusipojikana na tusipojitesa na kuitumikisha miili yetu sasa hivi?..(soma waebrani 11 yote utaona jambo hilo)