Biblia ina maanisha nini iliposema “Asiyefanya kazi na asile”?
Maandiko hayo yanapatikana kutoka katika kitabu cha 2 Wathesalonike 3:10 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”.
Mstari huo unatafsiriwa isivyopaswa na wengi wanaousoma..
Lakini mstari huo, unawahusu Wakristo! yaani watu wanaokusanyika pamoja kanisani.
Katika Kanisa la Kwanza ulikuwepo utaratibu wa Waumini wote kufanya vitu kwa shirika, ikiwemo kila mmoja kutoa sehemu ya mali zake na kuzileta kanisani ili zitumike katika kusaidiana pamoja na kunyanyuana..hususani kwa wale wenye mahitaji…. Hilo tunalisoma katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2
Matendo 2:44 “Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa”.
Matendo 2:44 “Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,
45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa”.
Sasa kilichokuwa kinatokea ni kwamba, kulikuwepo na watu wachache ambao, walikuwa na uwezo wa kwenda kufanya kazi, lakini kwasababu wanaona kuna ofa hiyo ya kugawiwa baadhi ya vitu bure ikiwemo chakula kanisani, wakawa hawaendi kufanya kazi, na kukaa kusubiria hilo fungu la kanisa lifike wapewe, hivyo hiyo ikawa inasababisha kanisa kulemewa, kwa kuongezeka kwa watu wasio na shughuli zao na huku bado wanataka kupewa fungu kutoka kanisani.
Sasa kulitatua tatizo hilo, Ndipo Mtume Paulo kwa Uwezo wa Roho akaagiza katika makanisa yote kwamba watu wakafanye kazi, wale chakula chao wenyewe ili kanisa lisilemewe…Wabakie tu wale wanaostahili kweli kweli kupata fungu kutoka kanisani…Na wengi wa hao wanaostahili walikuwa ni wajane wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, tena wasio na ndugu wa kuwasaidia, wameachwa wenyewe, na pia wana rekodi nzuri ya kuifanya kazi ya Mungu kanisani…hao ndio waliostahili kupokea sehemu ya fungu… na watu wasio na uwezo kabisa..Lakini wengine waliosalia wasipewe kitu chochote hata chakula kutoka kanisani, wakafanye kazi ili kanisa lisilemewe.
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
JE! KUBET NI DHAMBI?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Wengi wa wanaompa Yesu Kristo maisha yao kwa mara ya kwanza, ndio maswali ya kwanza kwanza kujiuliza…nitaombaje! namna gani ya kuomba ili Mungu anisikie!
Kiuhalisia hakuna fomula fulani maalumu ya kuomba wala chuo fulani maalumu cha kujifunzia kuomba, Kwasababu Mungu wetu si mwanadamu wala hana udhaifu wa kutuelewa…Sehemu nyingine katika maandiko inasema “Baba yetu wa mbinguni anajua tujayohitaji hata kabla sisi hatujamwomba”
Unaona? kwa sentensi tu hiyo inaonesha kuwa Mungu si dhaifu wa kutuelewa sisi, kiasi kwamba tunahitaji course fulani tukasome ndipo atuelewe au kutusikia. Kitendo cha Kuwa mwanadamu tu! tayari Mungu anakuelewa kuliko unavyojielewa.
Hivyo mbele za Mungu, hatuendi na mpangilio mzuri wa Maneno kama tunavyoandaa hotuba kwenda kuisoma mbele za Mkuu wa Nchi…Isipokuwa tunakwenda na hoja zenye nguvu...Na hoja hizo ndio zile Bwana alizotufundisha wakati wa kuomba..katika Mathayo 6
“9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina”.
“9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina”.
Kwamba tuombapo tuhakikishe tunaomba toba, na pia tuhakikishe tunawasamehe wengine ili na sisi pia tusamehewe…Kadhalika tunapoomba tuhakikishe tunalitukuza jina la Yesu, na pia tunaomba ufalme wake uje…Na pia tusisahau kusema mapenzi yake yatimizwe…kwasababu sio kila kitu tunachokiomba ni mapenzi ya Mungu…Pia tunapaswa tumwombe Mungu atupe riziki zetu za kila siku, kama chakula, mavazi, malazi pamoja na fursa.
Kadhalika tunamwomba asitutie majaribuni hiyo inahusisha kumwomba Bwana atuepushe na yule mwovu katika maisha yetu, imani yetu, familia zetu, kazi zetu, huduma zetu za kila siku za kuwaleta watu kwa Kristo, tunazungukwa na nguvu za yule adui kila mahali, hivyo ni muhimu kumwomba Bwana atuepushe na mitego yake yote.
Na bila kusahau kurudisha utukufu, na kutambua kuwa uweza, nguvu na mamlaka vina yeye milele na milele…Hivyo hakuna kama yeye, na yeye ndiye mwanzo na mwisho.
Hizo ndio hoja zenye nguvu…usitazame ni maneno kiasi gani umekosea kuongea, wala ni lugha gani umezungumza wakati wa kuomba, hakikisha tu maombi yako yanahusisha hivyo vipengele.
Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye namba hizi: +255789001312/ +255693036618
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
FAIDA ZA MAOMBI.
SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)
TUMEAMBIWA TUNAPOSALI TUSIPAYUKE-PAYUKE, JE! HUKO KUPAYUKA PAYAUKA NDIO KUPI?
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.
Ni kwa namna gani malaika wa mbinguni wanaweza kutuhubiria sisi injili?
Maana ya kanisa ni “walioitwa” kwahiyo watu walioitwa watoke sehemu fulani wanaitwa kanisa…..Hivyo tafsiri ya kanisa sio jengo kama inavyodhaniwa na wengi…
Kwahiyo katika maandiko kanisa la kwanza lilianza siku ile ya PENTEKOSTE. Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya watu! Soma Matendo Mlango wa pili yote.
Wale waliomwamini Yesu, na kubatizwa walishukiwa na Roho Mtakatifu, na hivyo Roho huyo huyo aliwaongoza kukusanyika pamoja kwa lengo la kujifunza Neno ambalo Mitume ndio waliokuwa wanalifundisha, pia walidumu katika kushiriki meza ya Bwana, katika kufanya ushirika na katika Kusali. Hayo mambo manne ndiyo yaliyokuwa yanafanyika katika kanisa la kwanza.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”.
(Hilo ndilo kanisa la kwanza)
Kanisa katoliki llinalosemekana kama kanisa la kwanza, hilo ilikuja kuzaliwa mwaka wa 325 Baada ya Kristo. Ambalo hilo lilikuwa kinyume na kanisa la kweli la Kwanza la Pentekoste.
Kanisa katoliki, ni kanisa la uongo kwasababu halikudumu katika hayo mambo manne hapo juu… halidumu katika fundisho la Mitume kama kanisa la Kwanza, fundisho la Mitume linasema tusiabudu sanamu na pia linasema mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu Yesu Kristo, wakati kanisa katoliki linaamini Mariamu pia ni mpatanishi…..
Pia kanisa katoliki halidumu katika kumega mkate, kwani mwenye ruhusu ya kushiriki ni Padre tu! peke yake jambo ambalo ni kinyume na maandiko, pia halidumu katika kufanya ushirika wala kusali…Sala zinazofanywa ni za desturi za kipagani, kusalia rozari na sanamu jambo ambalo kanisa la kwanza halikufanya. Maombi ya moja kwa moja kwa Mungu hayatiliwi mkazo, na zaidi ya yote maombi ya masafa marefu hayapo kabisa ndani ya kanisa katoliki.
MARIAMU NI NANI?
UHURU WA ROHO.
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?
WhatsApp
Yesu ni nani? Hili ni swali ambalo sio tu linawachanganya watu wengi wa leo, lakini pia limekuwa ni swali lililowasumbua watu wengi tangu enzi na enzi vizazi na vizazi huko nyuma, hata tangu wakati Bwana Yesu mwenyewe akiwa hapa duniani utaona siku moja aliwauliza wanafunzi wake nao swali kama hilo,
Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Unaona, hata leo hii tu angekuwepo duniani angetuuliza na sisi swali hilo hilo, tunamnena yeye kama nani, ni wazi utasikia kila mtu anatoa jibu lake wengine utawasikia watasema, ni mjumbe wa Mungu, wengine watasema ni mmojawapo wa mitume wa Mungu, wangine watasema alikuwa ni nabii wa Mungu, wengine watasema ni mkombozi, wengine watasema ni Mungu…nk. N.k
Lakini Je hiyo inamaanisha mitazamo yao wote haipo sawa?, jibu ni hapana, wanaweza wakawa sawa mahali fulani lakini si sawa kulingana na Mungu anavyotaka watu wamjue Yesu kama nani..Ni sawa tu na leo usimame na boss labda tuseme mbele ya watu 1000 tofauti tofauti, na ukasema kila mmoja aanze kumzungumzia , hutashangaa katikati ya huo mkutano wengine wakimwita, mjomba, wengine wakimwita rafiki, wengine wakimwita baba, wengine wakimwita binamu, wengine wakimwita jirani, wengine wakimwita mwenyekiti, wengine wakimwita shemeji, wengine wakimwita mwenetu n.k…
Hapo utaona akiitwa kila aina ya cheo ambacho hujawahi kutazamia kwamba anaweza akawa nacho boss wako, sasa hapo huwezi kusema hawapo sawa kisa tu kwasababu hukumsikia hata mmoja wao akimwita boss, wao kila mmoja alimwita kulingana na mahusiano aliyonayo naye..ikiwa ni mtoto wake alisimama mbele yake hawezi kumwita shemeji au boss ni lazima atamwita Baba tu..
Lakini hata kama wapo sawa kiasi gani, Bado hawapo sawa kulingana na wewe unavyotaka watu wale wamjue kama boss.
Na vivyo hivyo kwa Bwana Yesu, wengi wanamjua kama mtume wa Mungu, na kweli ndivyo alivyo yeye ndiye mtume mkuu, wengi wanamjua kama nabii, na ni kweli ndivyo ilivyo yeye alikuwa ni nabii mkuu, wengine wanamjua kama kiongozi na kweli ndivyo alivyo, vile vile wengine wanamjua kama Mungu mwenyewe aliyeuchua mwili na kuishi na sisi duniani, na kweli ndivyo ilivyo maandiko mengi yanathibitisha hilo kuwa YESU ndiye Mungu mwenyewe katika mwili wa kibinadamu..lakini swali linakuja pale pale Je! Mungu anataka sisi tumjue YESU kama nani?.
Sasa tukiendelea kusoma pale chini tunaona Petro anamjibu Bwana maneno haya:
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”Unaona Ufunuo aliopata Petro juu ya YESU kama KRISTO, aliyekuja kama mwana wa Mungu, ndio aliokuwa anauhitaji na ndio kwa kupitia huo huo YESU amelijengea kanisa lake na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda.
16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”Unaona Ufunuo aliopata Petro juu ya YESU kama KRISTO, aliyekuja kama mwana wa Mungu, ndio aliokuwa anauhitaji na ndio kwa kupitia huo huo YESU amelijengea kanisa lake na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda.
Hivyo hatupaswi kuhangaika sana, kutafuta kumjua YESU ni nani? Tukianza kumchambua hatutammaliza, lakini biblia imetupa mwongozo mwepesi uliomwelezea yeye kwamba tumjue yeye kama KRISTO, maana ya neno Kristo ni mtiwa mafuta, yaani mtu aliyetiwa mafuta kuwakomboa wanadamu,..hivyo tukishamjua YESU kama mkombozi huo ni ufunguo mkubwa sana uliobeba vyeo vyake vingine vyote vilivyobakia.. Kwamba yeye ndio njia ya kwenda mbinguni, na mtu hawezi kufika kwa Mungu pasipo kupitia yeye.
Hivyo ukiulizwa leo YESU ni nani, jibu tayari lipo yeye ni KRISTO, yaani mkombozi wa ulimwengu, hilo linatosha kumwelezea yeye..Na mtu yeyote akimwelewa kwa namna hiyo hivyo akamruhusu ayakomboe maisha yake basi ajue kuwa shetani atagonga mwamba, tiketi ya kwenda mbinguni ipo mikononi mwake.
Ubarikiwe.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
UBATILI.
RACA
KWANINI AWE NI PUNDA NA MWANA-PUNDA?
MUNGU MWENYE HAKI.
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Biblia inasema “Heri” heri maana yake “amebarikiwa yeye”…na inasema pia heri wafu wafao katika Bwana, ikiwa na maana kuwa sio kufa tu! bali kufa katika Bwana.. Wafu ambao hawajafa katika Bwana ni kinyume chake, kwamba Ole wao…
Sentensi hizo zinamaanisha kuwa kuna kitu kitafuata baada ya kifo, nacho si kingine zaidi ya hukumu! Na watakaokufa katika Kristo wanatumaini la kufufuliwa tena na kupewa uzima wa milele, na kupata raha isiyoisha..ndio maana wanaambiwa wana heri…. ingekuwa hakuna kitu kinachofuata, isingesema heri wafu! bali ingesema heri walio hai!
Je! maisha yako umeyatengeneza kiasi kwamba, una uhakika, hata leo hii ukiondoka ulimwenguni! utakuwa na heri? Utayatengenezaje?..kwa matendo yako! kwasababu Matendo ya kila mtu yanamfuata popote aendapo! Majumba tukifa tutayaacha, magari tutayaacha, mali tutaziacha lakini matendo tunakwenda nayo huko ng’ambo ya pili. Hivyo sio kitu cha kukichukulia kiwepesi!
kumbuka hakutakuwa na nafasi ya pili baada ya kifo.
Waebrania 9:27 “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”;
Mgeukie Bwana Yesu kikamilifu. Kimbilio letu na Tumaini letu
Maran atha!
SIKU YA HUKUMU ITAKUWAJE?
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?
Chanzo cha Baraka zote ni Mungu..Na Mungu anaweza kumbariki mtu moja kwa moja kupitia yeye mwenyewe…na anaweza pia kumbariki mtu kupitia mtu mwingine.
Kwamfano kwenye Biblia Mungu alimbariki Ibrahimu moja kwa moja…akamwambia
Mwanzo 22:15 “Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni 16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; 18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”.
Mwanzo 22:15 “Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”.
Na pia Mungu anaweza kumbariki mtu kwa kupitia Mtu mwingine, kwa mfano “Mzazi ana uwezo wa kumbariki mwanawe” na baraka hizo zikamfikia vile vile kama alivyombariki. Mfano katika Biblia tunamwona Yakobo Mwana wa Isaka, aliwabariki wanawe 12, na kila mmoja baraka aliyombarikia ilimfikia.
Hivyo Ili tufanikiwe katika maisha yetu, hatuna budi kutafuta Baraka, na Baraka hizo zinakuja kwa kumpendeza Mungu, pamoja na wanadamu…Kuyashika maagizo ya Mungu, na Kuwaheshimu wazazi pamoja na watu wote. Kinyume na hapo ni kujitafutia Laana.
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
KWANINI MUNGU HAKUMUUA NYOKA MPAKA AKARUHUSU AJARIBIWE PALE BUSTANI NA EDENI?
JE! MTU ALIYEOKOKA ANARUHUSIWA KUMILIKI GUEST HOUSE AU LODGE AMBAYO INA BAR NDANI YAKE NA KUTOA FUNGU LA KUMI KWA KUPITIA HIYO KAZI?
JIBU: Ili tusichanganyikiwe jambo la muhimu tulinalopaswa kujua ni kuwa Katika biblia Neno “mbinguni” limetumika kuwakilisha sehemu tofauti tofauti tatu.
Sehemu ya kwanza ni anga hili ambalo lipo juu yetu: Ambalo ndilo hili tunaloliona lenye nyota, mawingu, mwezi jua na sayari, ambalo ndege wote wa angani wanaruka na kufurahia, biblia imelitaja kama mbingu..Tunasoma..
Isaya 55:10 “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Luka 17:24 “kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake”.
Isaya 55:10 “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”
Luka 17:24 “kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake”.
Sehemu ya Pili ya mbingu ni makao ya Mungu yalipo: Na hii ipo katika Roho, sehemu ambayo Mungu na malaika zake wanaishi, hatuwezi kuiona kwa jicho la kibinadamu wala hatuwezi kufika huko kwa kifaa chochote cha kibinadamu, lakini ni mahali halisi kabisa. Tiketi ya pekee ya kufika huko biblia inatuambia ni Yesu Kristo tu, Na hii mbingu ni pana sana ndio imejumuisha ile mbingu mpya na nchi mpya ambayo itakuja kuwa ni makao ya watakatifu baadaye, pamoja na ile paradiso (peponi) kule ambapo wale wote waliokufa zamani na wanaokufa sasa hivi katika Kristo wanahifadhiwa kwa muda wakisubiria ufufuo siku ile ya Unyakuo ili kwa pamoja waingie katika makao ya Mungu mwenyewe yaliyo juu sana na ndio maana utaona mtume Paulo alinyakuliwa mpaka mbingu ya Tatu, mbingu hii ya tatu ni hiyo ya makao ya Mungu mwenyewe, akaonyeshwa sehemu ya maono ya huko, na kusema mambo yaliyo huko hayajuzu hata mwanadamu kuyatamka,(2Wakorintho 12:2-4). na ndiko watakatifu waliokombolewa watakapokwenda siku ile ya Unyakuo itakapofika, ni mahali patakatifu na pasafi ambapo mtu yeyote mchafu hataingia..
1Wafalme 8:27 “Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!”
1Timotheo 6:16 “ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.”
Na sehemu ya tatu biblia inapataja kama mbinguni ni mahali pa juu sana, makao ya juu sana: Mahali ambapo Mungu pekee ndiye anayestahili kuwepo, jambo ambalo hata hapa duniani linaweza kufikiwa,
Watu walio ndani ya Yesu, ambao wameokoka kikamilifu kwa kumwamini Yesu na kubatizwa, katika ulimwengu wa roho, ni sawa na wameketi pamoja na Kristo mbinguni..
Waefeso 2:5 “hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. 6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”
Waefeso 2:5 “hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”
Kadhalika pia, Ufalme wowote au mtu yeyote anayetafuta kuinuliwa ziadi ya vitu vingine vyote huyo katika roho anaonekana anakipandia cheo cha Mungu kilipo, na Mungu yupo mbinguni, hivyo anaonekana kama amefika mbinguni.
Danieli 4:19 “Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako. 20 Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote; 21 ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake; 22 ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
Danieli 4:19 “Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.
20 Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote;
21 ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake;
22 ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
Mathayo 11:23 “Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.”
Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo”.
Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo”.
Hivyo kwa vyovyote vile, tunapaswa tujitahidi ili tufike huko, si kwa kujiinua tukiyatumainia haya Maisha, bali kwa kupitia Yesu Kristo, kwasababu biblia inasema mambo tuliyoandaliwa huko, jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
JE! NI KWELI DUNIA ILIUMBWA TAKRIBANI MIAKA 6000 ILIYOPITA? NA JE! SHETANI ALIKUWEPO DUNIANI WAKATI DUNIA INAUMBWA?
JE! KUNA DHAMBI KUBWA NA NDOGO?
NI NANI ANAYETAWALA DUNIA KATI YA MUNGU NA SHETANI?.
Biblia imeweka wazi kuwa Mariamu, mama yake Yesu alikuwa na watoto wengine..
Mathayo 13:53 “Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake. 54 Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? 55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? 56 Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote? 57 Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe”.
Mathayo 13:53 “Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake.
54 Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
56 Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?
57 Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe”.
Maumbu kama inavyosomeka kwenye mstari wa 56, maana yake ni ndugu wa ‘KIKE’ (madada)..Kwahiyo Mariamu alikuwa ana watoto wengine wakiume na wakike.
SAYUNI NI NINI?
NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?
KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?
SABATO HALISI NI LINI, JE! NI JUMAPILI AU JUMAMOSI?, NI SIKU GANI ITUPASAYO KUABUDU?
MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?
Hakuna mahali popote Biblia imerekodi kifo cha Mariamu, wala hakuna mahali popote Biblia imerekodi kifo cha Mtume Petro, wala Yusufu mume wake Mariamu, wala Mtume Paulo, wala Mtume Adrea wala Tomaso, Nathanieli, n.k…manabii wengi sana na mitume vifo vyao havijarekodiwa kwenye Biblia takatifu..
Na ni kwanini biblia havijarekodi vifo vya hawa watu, ni kwasababu sio vitu vya muhimu sana kuvijua kwetu sisi…Inatusaidia nini sisi kujua Petro alikufa mwaka gani? au mwezi gani?.. unaona haitusaidii chochote! Lakini tunajua kuwa Petro alikufa, Paulo alikufa, Yusufu alikufa…kadhalika na Bikira Mariamu alikufa vile vile.
Mariamu hakuwa mtu wa tofauti sana na watu wengine…Eliya ambaye hakufa bali alipaa, Biblia inamtaja kuwa mtu wa mwenye tabia sawa na sisi, (soma Yakobo 5:17) itakuwaje Mariamu ambaye hakupaa?..Ni mmoja tu ndiye aliyekuwa wa kipekee ambaye biblia inasema alikufa na kufufuka na akapaa mbinguni, na huyo ni Yesu Pekee yake, ndio maana wokovu upo kwake. Kulikuwa hakuna haja ya kuja Bwana Yesu kama Mariamu alikuwa na wokovu .
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Mariamu alikufa kama watu wengine.
JE MARIAMU NI NANI?
KWANINI MUNGU AWACHOME WATU KWENYE ZIWA LA MOTO NA HALI YEYE NDIYE ALIYEWAUMBA?
Jambo moja linalowachanga watu wengi wa Mungu, ni kutokujua Ujio wa Yesu utakuwaje.
Ujio wa Bwana Yesu umegawanyika katika sehemu kuu 3. nazo ni UJIO WA KWANZA, UJIO WA PILI na UJIO WA TATU.
UJIO WA KWANZA: Ni wakati Bwana Yesu alipozaliwa na Bikira Mariamu, na kuifanya kazi yake kwa miaka mitatu na nusu, na kufa, na kufufuka, kisha kurudi mbinguni alikotoka. Huo ulikuwa ni ujio wa kwanza.
UJIO WA PILI: Utakuwa ni wakati wa unyakuo…Ujio huu hautahusisha Bwana kushuka kabisa duniani, bali Bwana atakuja na ataishia mawinguni, sisi tulio hai tutaungana pamoja na wale waliokufa katika Kristo, kwa pamoja tutanyakuliwa kwenda kumlaki mawinguni, na kwenda mbinguni kwenye karamu yake aliyotuandalia, (1 Wathesalonike 4) ambapo huko tutakaa kwa muda wa miaka 7…
UJIO WA TATU: Utahusisha Bwana kurudi tena na watakatifu wake duniani walionyakuliwa, atakuja duniani kwa ajili ya Hukumu ya Mataifa, Vita ya Harmagedon, pamoja na kuanzisha utawala mpya duniani wa Amani utakaodumu kwa miaka 1000. Ujio huu ndio kila jicho litamwona akija wa majeshi ya mbinguni..Na atashukia Israeli. Hapo ndio yatakuwa makao yake makuu kipindi cha utawala wake duniani.
Kwa urefu wa ujio huo pitia somo hapa chini linalosema UTAWALA WA MIAKA 1000.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
KATI YA UNYAKUO WA KANISA, DHIKI KUU, VITA VYA HAR-MAGEDONI, UTAWALA WA MIAKA 1000, VITA YA GOGU NA MAGOGU, HUKUMU YA KITI CHA ENZI CHEUPE. JE, NI KIPI KINAANZA NA KINGINE KUFUATA?
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE