Chanzo cha Baraka zote ni Mungu..Na Mungu anaweza kumbariki mtu moja kwa moja kupitia yeye mwenyewe…na anaweza pia kumbariki mtu kupitia mtu mwingine.
Kwamfano kwenye Biblia Mungu alimbariki Ibrahimu moja kwa moja…akamwambia
Mwanzo 22:15 “Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”.
Na pia Mungu anaweza kumbariki mtu kwa kupitia Mtu mwingine, kwa mfano “Mzazi ana uwezo wa kumbariki mwanawe” na baraka hizo zikamfikia vile vile kama alivyombariki. Mfano katika Biblia tunamwona Yakobo Mwana wa Isaka, aliwabariki wanawe 12, na kila mmoja baraka aliyombarikia ilimfikia.
Hivyo Ili tufanikiwe katika maisha yetu, hatuna budi kutafuta Baraka, na Baraka hizo zinakuja kwa kumpendeza Mungu, pamoja na wanadamu…Kuyashika maagizo ya Mungu, na Kuwaheshimu wazazi pamoja na watu wote. Kinyume na hapo ni kujitafutia Laana.
Mada Nyinginezo:
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
KWANINI MUNGU HAKUMUUA NYOKA MPAKA AKARUHUSU AJARIBIWE PALE BUSTANI NA EDENI?
About the author