Title February 2024

Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; 

SWALI: Nini maana ya Mithali 25:13

Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao;  Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao. 


JIBU: Kwa wanaoishi maeneo ambayo kuna misimu ya theluji, wanafahamu kuwa vipindi hivyo vya baridi vinapofika, huwa kunakuwa na upepo-baridi unaovuma.

Sasa kwa mujibu wa vifungu hivyo, anasema, Kama upepo huo ukivuma kipindi cha mavuno, ambacho kimsingi ni wakati wa kiangazi,na sio baridi, kingekuwa ni shangwe kubwa sana kwa wavunaji.

Kwa namna gani?

Kazi ya uvunaji inafanyika wakati wa jua kali, kwasababu mazao pia wakati huo yanakuwa yamekauka. Lakini pia mfano jua lile likapoozwa na upepo wa baridi, huuburudisha sana moyo wa mvunaji.

Vivyo hivyo anafananisha na wajumbe waaminifu wanaotumwa kupeleka habari fulani anasema; 

“Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao”. 

Mjumbe wa kwanza mwaminifu aliyetumwa ni Bwana wetu Yesu Kristo. Alimburudisha Baba moyo wake, kwasababu yote, na kusudi alilopewa kulifanya la kutukomboa sisi alilitimiza lote.

Vivyo hivyo na sisi, tumewekwa kuwa wajumbe wa Bwana, wa kuenenda  kuihubiri injili ya Kristo kwa kila kiumbe, ulimwenguni kote. Yatupasa tuwe waaminifu, mfano wa Bwana na mitume wake, ili moyo wa Kristo wetu ufurahi.

Na thawabu ya kuuburudisha moyo wa Bwana ni sisi kupewa mamlaka kubwa kule ng’ambo tufikapo, kwa mfano ambao Bwana Yesu aliutoa katika vifungu hivi;

Luka 19:12-26

[12]Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 

[13]Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. 

[14]Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. 

[15]Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 

[16]Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

[17]Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 

[18]Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 

[19]Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

[20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. 

[21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 

[22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 

[23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 

[24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 

[25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 

[26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho. 

Je na sisi tunaweza kuwa mbele za Bwana Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; ?

Bwana atusaidie.

Je! Umeokoka?

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?

SWALI: Je! ni sahihi kwa mkristo kufanya biashara za kifedha mitandaoni kama vile Forex, na crypto-currency mfano wa bitcons?


JIBU: Ni vema kufahamu biashara za kifedha mitandaoni kama forex ni nini?

Ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni katika soko la dunia. Yaani ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, sawa tu ile tuliyowahi kuisikia, ijulikanayo kama Bureau de change, ambayo watu wanakwenda kununua/kuuza pesa za kigeni, isipokuwa hii hufanyika mitandaoni, tofauti na bureau ambayo hufanyika kwa makarati ndani ya ofisi Fulani maalumu. Biashara hii ya forex na nyinginezo Mara nyingi hufanywa na taasisi kubwa za kifedha kama mabenki na makampuni, lakini pia hata watu binafsi.

Ni biashara ya bahati nasibu, inayofanana na michezo ya kubahatisha kitabia.. Lakini ni tofauti kabisa kimaudhui.

Biashara  hii ni ya uwekezaji, ambayo imehalalishwa ki-ulimwengu, japokuwa hatusemi kuwa kila biashara iliyohalalishwa na taifa kuwa ni halali kwa mkristo kufanya, hapana mfano zipo pombe zimehalalishwa kitaifa lakini kwa mkristo sio sawa kufanya biashara kama hizo.

Lakini, biashara hii, haihusishi katika kumdhulumu mtu, au kumlaghai mtu kiakili, apoteze kitu Fulani ili wewe ujilimbikizie fedha zake ambazo hazina mzungumko wowote wa kimaendeleo. Mfano wa hizo ni kama vile “Betting na kamari”. Kwa mkristo kushiriki katika biashara hizo za betting na kamari sio sawa. Kwa urefu wa somo lake pitia link hii >>>JE! KUBET NI DHAMBI?

Lakini Forex na nyinginezo zijulikanazo kama biashara za uwekezaji, zinahitajika sana, kwasababu kama zikikosekana, basi mzunguko wa fedha za kigeni, ungekuwa mgumu sana, na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji uchumi, katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia.

Hivyo tukirudi kwa mkristo, je kufanya biashara hii ni dhambi?

Kimsingi ikiwa anafanya kwa lengo la uwekezaji wake, huku akijua pia ni kwa faida ya uchumi, na hamdhulumu au kumlaghai mtu. Hafanyi kosa. Lakini akiwa na fikra za kikamari, kama vile afanyavyo kwenye betting, Kwake itakuwa ni kosa, kwasababu dhamiri yake inamshuhudia, ameigeuza kama kamari moyoni mwake.

Ndio hapo hili andiko linakuja.

Warumi 14:22  Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.

23  Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.

Maana yake ni kuwa ukiwa na mashaka moyoni mwako kuifanya kazi hii, basi ni heri usifanye kabisa, kwasababu mashaka yoyote ni dhambi. Lakini kimsingi biashara hii sio kosa kwa mkristo, ambaye ana maarifa/elimu ya kutosha juu ya biashara za kifedha katika ulimwengu wa sasa.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Rudi nyumbani

Print this post

Neno kupomoka linamaana gani kwenye biblia?(Hesabu 16:22)

Hesabu 16:20 Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,  21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.  22 Nao WAKAPOMOKA kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?

Soma pia

Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 

14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?

Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi baadhi; Hesabu  16:4, 16:45,

Ni Kiswahili cha zamani cha Neno kuporomoka.  Yaani kuanguka chini, kwamfano maji yanayoelekea chini kwa wingi tunasema maporomoko ya maji, au udongo unaoanguka kutoka milimani kwa wingi tunasema maporomoko ya udongo.

Hivyo, katika vifungu anaposema Musa na Haruni wakapomoka kifudifudi, anamaanisha wakaanguka chini kifudi fudi mbele za Mungu kumlilia Bwana rehema.

Je! Na sisi tuombapo rehema au  tumtakapo Bwana kwa jambo Fulani muhimu ni lazima tupomoke chini ili tusikiwe ?

Jibu lake ni kwamba sio takwa kufanya hivyo. Kwasababu Mungu anaangalia moyo, kupomoka kwetu kunapaswa kuwe moyoni. Lakini pia si vibaya kuomba kwa namna hiyo, na ni vema, kwasababu pia ni ishara moja wapo ya unyenyekevu wa moyo. Ni sawa tu na tunapopiga magoti, au kunyosha mikono juu wakati wa kumwomba Mungu, kama ishara ya unyenyekevu mbele zake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?

LAANA YA YERIKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

UJAZO WA BIBLIA KATIKA MGAWANYO WAKE.

> Kuna vitabu vingapi katika Agano Jipya na Agano la Kale?,

> Kuna sura/milango mingapi katika kila mgawanyo?

> Na watu gani waliotajwa sana katika biblia zaidi ya wengine wote?

KUJUA HAYO YOTE, TAZAMA MAJEDWALI YAFUATAYO 

(Slide kushoto kusoma zaidi taarifa katika jedwali).

N/AMGAWANYOIDADI YA VITABUIDADI YA SURA (MILANGO)IDADI YA MISTARI
1.AGANO LA KALE3926023,145
2.AGANO JIPYA279297,957
JUMLA661,18931,102

JINANAFASI (KATIKA BIBLIA)IDADI ALIZOTAJWA (Mara ngapi)NAFASI
YOABUJemedari wa Mfalme Daudi12916
ISAKAMwana wa Ibrahimu12915
SAMWELINabii (Mwana wa Elkana)14214
YEREMIANabii (Mwana wa Hilkia)14513
PETROMtume (Mwana wa Yona)19312
YOSHUAJemedari wa Israeli21911
PAULOMtume (Mwenyeji wa Tarso)22810
YUSUFUMwana wa Yakobo2469
SULEMANIMfalme (Mwana wa Daudi)2728
ABRAHAMUBaba wa Imani2947
HARUNIKuhani Mkuu3426
SAULIMfalme (Mwana wa Kishi)3625
YAKOBOIsraeli (Mwana wa Isaka)3634
MUSANabii (Mwana wa Amramu)8033
DAUDIMfalme (Mwana wa Yese)9712
YESU KRISTOMFALME wa Wafalme, Bwana wa mabwana, Mwana wa Mungu, Mwokozi, Simba wa kabila Yuda, Mesia, Mwokozi na Mchungaji Mkuu.1,2811

Kwanini YESU KRISTO ndiye anayeonekana kutajwa sana katika Biblia??.. Ni kwasababu yeye ndiye kitovu cha UZIMA, na Biblia yote inamhusu yeye, na kutuelekeza kwake.

YESU KRISTO, ndiye Njia, KWELI na UZIMA.. Mtu hawezi kumwona MUNGU nje ya YESU KRISTO (Yohana 1:18 na 14:6)

Tafadhali shea na wengine;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

TAKWIMU ZA KIBIBLIA

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Rudi nyumbani

Print this post

Mistari ya biblia kuhusu shukrani.

Ifutayo ni mistari kadhaa ya biblia ihusuyo shukrani/ kushukuru.


Zaburi 9:1 “Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu”.

Zaburi 18:49 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”

2Samweli 22:50 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”.

Zaburi 30:12 “Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele”

Zaburi 35:18 “Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi”

Zaburi 52: 9 “Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako”

Zaburi 118: 21 “Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu”.

Zaburi 71:22 “Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli”.

Zaburi 119: 7 “Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako”

Zaburi 106:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele”.

Zaburi 28:7 “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru”.

2Wakorintho 2:14  “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu”.

Ikiwa uko kwenye soko, https://www.swisswatch.is/product-category/rolex/explorer/ jukwaa letu ni chaguo lako bora! Duka kubwa zaidi la ununuzi!

Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”.

Zaburi 100:4 “Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake”

Zaburi 107:7 “Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa

8 Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu”.

1Wakorintho 15:57  “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”.

Zaburi 95: 2 “Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi”.

Wakolosai 3:15  “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani”.

Ufunuo 11:17 “wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki”

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

NENO LA FARAJA KWA WAFIWA.

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

Rudi nyumbani

Print this post

NENO LA FARAJA KWA WAFIWA.

Maandiko ya faraja kwa wafiwa/ Neno la kufariji wafiwa (waliopatwa na msiba).


Ikiwa Mtu kafariki katika Kristo, basi lipo tumaini la kumwona tena..lakini kwa namna moja au nyingine, wafiwa watakuwa katika huzuni kwasababu hawatamwona tena kwa kitambo…hivyo yafuatayo ni maneno machache yanayoweza kuwafaa waliofiwa.

Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”

Yoshua 1:9 “Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako”.

Yakobo 1:2  “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

3  mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”

Yohana 16:22  “Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye”.

Mathayo 5:4  “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”

Zaburi 34:18 “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa”.

Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”

Zaburi 73:26 “Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele”

Warumi 8:18 “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu”

Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”

Makala haya yanatoa usafirishaji wa bila malipo kwa bidhaa zinazostahiki, http://swisswatch.is au ununue mtandaoni na uchukue dukani leo katika Idara ya Matibabu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

Mistari ya biblia kuhusu maombi.

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).

MAOMBI YA YABESI.

JE! MUNGU NI NANI?

Rudi nyumbani

Print this post

WEKA ANWANI HII KATIKA MAHUBIRI YAKO!

(Masomo maamulu kwa watumishi wa Mungu).

Je wewe ni mtumishi wa MUNGU?..Basi fuatilia mfululizo wa masomo haya katika tovuti yetu hii (www.wingulamashahidi.org).

Kama mtumishi wa Mungu kuna  Anwani au nembo au Lebo ambayo inapaswa iambatane na kila fundisho unalolitoa kwa wahusika. Na Anwani/lebo hiyo/nembo hiyo si nyingine Zaidi ya “TOBA”. Hakikisha mahubiri yako yanalenga Toba, au kuwakumbusha watu umuhimu wa kujitakasa.

Kwanini iko hivyo?

Hebu tujifunze kwa mmoja ambaye ni mjumbe wa Agano, tena ndiye Mwalimu wetu MKUU na Mwinjilisti MKUU YESU KRISTO.

Yeye katika mahubiri yake yote alihubiri “Toba”.. Huenda unaweza kusoma mahali akiwa anafundisha na  usione likitajwa neno Toba, lakini fahamu kuwa alikuwa anahubiri Toba kila siku katika mafundisho yake yote… Kwani biblia inasema kama yote aliyoyafanya BWANA YESU kama yangeandikwa basi dunia isingetosha kwa wingi wa vitabu.

Yohana 21:25 “Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa”

Kwahiyo Mahubiri ya BWANA WETU YESU yote Yalikuwa yamejaa toba.. sasa tunazidi kulithibitishaje hilo?.. hebu tusome maandiko yafuatayo..

Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”

Nataka tuutafakari kwa undani huu mstari… anasema “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”…. Zingatia hilo neno “TOKEA WAKATI HUO….TOKEA WAKATI HUO…TOKEA WAKATI HUO”.. Maana yake “kilikuwa ni kitu endelevu”, sio kitu cha kusema mara moja na kuacha, (hiyo ndiyo ilikuwa lebo ya mafundisho yake daima).. Kila alipohubiri lazima aliwahubiria pia watu watubu.

Umeona?. Je na wewe Mchungaji, na wewe Mwalimu wa injili, na Wewe nabii, na wewe Mtume, na wewe Mwimbaji wa injili.. LEBO YA MAHUBIRI YAKO NI IPI????.

Je! injili yako unayohubiri ni ya TOBA, au ya kuwafariji watu katika dhambi zao??.. Je unazunguka huku na kule kuhubiri injili ya namna gani?..Je ni injili ya Toba au ya Mali tu!.

Luka 24:45  “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

46  Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

47  na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

48  Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya”

Hakuna furaha, hakuna mafanikio, hakuna Amani ikiwa mtu yupo katika maisha ya dhambi.. utamhubiria afanikiwe lakini hata akiyapata hayo mafanikio basi dhambi itamuua tu na kumkosesha raha.. Raha pekee na Amani mtu ataipata baada ya kutubu, ndivyo maandiko yasemavyo..

Matendo 3:19 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Toba ni nini?

VYA MUNGU MPENI MUNGU.

NAYAJUA MATENDO YAKO.

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.

Rudi nyumbani

Print this post

Toba ni nini?

Swali: Toba maana yake nini?.. na je ina umuhimu gani kwetu?


Jibu: Neno “Toba” liinatokana na neno “kutubu”. Mtu anayetubu maana yake kafanya “TOBA”. Na kutubu maana yake ni “kugeuka, kutoka katika njia uliyokuwa unaiendea”.. Maana yake kama mtu ameshawishika kugeuka kutoka katika njia au mwenendo aliyokuwa anauendea kwa njia ya majuto na maombi ya kuomba msamaha kama njia hiyo ilikuwa ni kwanzo kwa mwingine, mtu huyo anakuwa ametubu, au amefanya TOBA.

Kibiblia mtu aliyegeuka na kuiacha njia ya dhambi aliyokuwa anaiende na kuomba msamaha kwa Mungu wake aliyemkosea, basi mtu huyo anakuwa amefanya TOBA, na ndio hatua ya kwanza kabisa ya Mtu kumsogelea MUNGU, hakuna njia nyingine tofauti na hiyo!.

Injili ya Yohana Mbatizaji na ya BWANA YESU (Mjumbe wa Agano jipya) ilianza na Toba.

Yohana 3:1  “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,

TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Maana yake watu waageuke na kuacha maisha ya kuabudu sanamu, waache maisha ya mauaji, waache maisha ya uzinzi na uasherati, waache maisha ya ulevi na utukanaji n.k.. kwasababu Ufalme wa mbinguni hautawapokea watu wa namna hiyo.

Lakini pia si kutubu tu, bali ni pamoja na “KUZAA MATUNDA YAPATANAYO NA HIYO TOBA”.. Maana yake baada ya kugeuka na kuacha dhambi, basi mwongofu huyo anapaswa ajifunze kuishi maisha yanayoendana na toba yake hiyo, maana yake asirudie tena machafu ya nyuma yatawale maisha yake.

Luka 3:8 “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto”.

Je na wewe umetubia dhambi zako na kumkaribisha YESU maishani mwako? Kama bado basi fungua hapa ufuatilize sala hii ya TOBA na KRISTO YESU ataingia maishani mwako kwa Imani >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.

ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Rudi nyumbani

Print this post

Je watu waliookoka wanaruhusiwa kukopa?

Swali: Je wakristo tunaruhusiwa kukopa benki au kutoka kwa watu?..kama ni ndio, kwanini maandiko yaseme mtakopesha wala hamtakopa? (Kumbukumbu 15:6).


Jibu: Turejee..

Kumbukumbu 15:6 “Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao”

Kuna kukupa kwa aina mbili; 1) KWA AJILI YA KUTATUA TATIZO/JANGA…. 2) KWAAJILI YA KUJITANUA.

    1. KUKOPA KWAJILI YA KUTATUA MATATIZO.

Kukopa kwa namna hii ni ile hali ambayo, mtu anapatwa na baa Fulani au janga, hivyo ili kujikimu au kujikidhi anakwenda kutafuta msaada kwa njia ya kukopa!.. Sasa kukopa kwa namna hii ndiko kunakozungumziwa hapo katika Kumbukumbu 15:6 (kwamba tutakopesha wala hatutakopa).

Na kwanini tutakuwa watu wa namna hiyo (ya kutokukopa)?.. ni kwasababu Mungu ni msaada wetu ambaye hataruhusu tupate matatizo hayo pasipo kuwa na sababu yoyote. Hivyo tutabaki katika usalama wake ambao utatuhifadhi dhidi ya madhara yote ya yule adui.

Hivyo kama mkristo ukiona unapitia vipindi vya mfululizo vya kukopa ili kukidhi mahitaji yako ikiwemo chakula, basi jaribu kulitazama jambo hilo kiroho Zaidi, na Bwana atakusaidia kukutoa hapo!.

       2. KUKOPA KWAAJILI YA KUJITANUA.

Hii ni aina ya pili ya UKOPAJI, ambayo biblia haijaikataza!.. Inapotokea huna janga lolote, huna baa lolote, na unaishi vizuri kwa katika neema ya Mungu, kiasi kwamba ukipatacho kinakidhi hali ya kutokuwa na haja ya kukopa!.. Lakini ukapenda kujitanua Zaidi ya hapo kifedha au kibiashara au kimiradi kama mtu wa Mungu, na ukaamua kwenda kukopa ili kuongeza labda ule mtaji ulio nao ili kutanua kazi au biashara..

Kukopa kwa namna hii “hakujakatazwa kwa mkristo” na wala hakumaanishi kuwa wewe ni maskini, kwasababu hata watu wengi walio matajiri sana pia wanakopa!!.. lengo lao la kukopa si kukidhi mahitaji (kwamba wana janga fulani au baa fulani, hivyo wasipopata huo mkopo wanaweza kudhurika) bali mara nyingi ni kwa lengo la kutanua biashara zao wazifanyazo au miradi yao.

Na Mkristo anapofikia mahali anahitaji kutanuka Zaidi anaweza kuchukua mkopo, na isiwe na tafsiri yoyote kwamba ni maskini au muhitaji, na kwamba pasipo huo hawezi kuishi.

Kanuni ya KUKOPA ni sawa na ile ya KUUZA tu!… Mtu anayeuza shamba kwaajili ya matatizo, ni tofauti na yule anayeuza shamba kama biashara!..kadhalika mtu anayekopa kwaajili ya kutatua matatizo/au janga Fulani ni tofauti na yule anayekopa kwaajili ya kujitanua.

Bwana atusaidie katika yote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.

Rehani ni nini katika biblia?

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.

Rudi nyumbani

Print this post

JE! UNAWEZA KUWA NA GEUKO KAMA LA DAUDI?

Tunapokisoma kisa cha Daudi, cha kumwiba mke wa shujaa wake (Uria), na kumlazimisha kuzini naye kwa siri, na baadaye kumuua mumewe , (2Samweli 11) tunaishia kuona picha mbaya sana ya Daudi. Na kumshutumu, na wengi wetu kusema Daudi ni mzinzi sana, iweje apendwe na Mungu namna ile, tena awe kipenzi cha Mungu?

Ni kweli kabisa alichokifanya Daudi hakistahili kufanywa na mtu yeyote, ambaye anamjua Mungu, mfano wa Daudi. Lakini kuna funzo kubwa sana ambalo wengi wetu hatulioni nyuma ya maisha ya Daudi baada ya pale.

Daudi alipozama katika dhambi ile, na kugundua makosa yake. Alikuwa na badiliko lisilo kuwa la kawaida. Sio kule alikokuwa anaomboleza usiku kucha, Hapana, lile lingekuwa la “kufoji” tu, ambalo yoyote anaweza kulifanya hata leo. Kinyume chake Daudi alikuwa na badiliko la kimatendo. Na hilo ndilo lililomfanya apendwe sana na Mungu.

Kwa namna gani?

Sasa angalia Daudi Yule Yule ambaye alikuwa ni mzinzi, mwenye tamaa ya hali ya juu,akiona tu mwanamke mzuri hajali, huyu ni mke wa mtu au la yeye alimwiba na kuzini naye. Lakini Dakika zake za mwisho hazikuwa hivyo. Alibadilika kwelikweli baada ya dhambi ile.

Utakumbuka hata alipokuwa mzee, Wakuu wa Israeli walikwenda kumtafutia Binti mzuri bikira katika taifa lote la Israeli, ili amlalie Daudi ampe joto kwasababu nguo za joto hazikutosha. Lakini biblia inasema Daudi alipolala naye ‘hakumjua’.

Kwa jinsi ya kibinadamu, binti alale, na mtu mwenye sifa ya tamaa kama Daudi, halafu asimwingilie. Lazima kutakuwa kuna jambo lingine limetendeka ndani ya maisha ya huyo mtu.

Tusome;

1 Mfalme 1:1

 “Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.

2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.

3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua

Ni wazi kuwa habari hiyo ilijulikana Israeli nzima, Daudi amelala na binti bikira mrembo miaka kadhaa lakini hajamwingilia. Ni shujaa kiasi gani. Hawakujua kuwa anawathibitishia Israeli kuwa yeye sio Yule wa zamani, sio Yule mzinzi mliyemzoea, ameshabadilika. Si mtu wa kulipuka lipuka tamaa ovyo kama alivyokuwa hapo mwanzo.

Hiyo ndio sababu Mungu alimpenda Daudi. Kwasababu alikuwa na badiliko la dhati Kwa Mungu wake. Je! Na sisi, tunaweza kusema tumeuacha ulimwengu kweli kweli pale tunapomgeukia Mungu, au tutakuwa na vimelea vya kidunia ndani yetu, pale tunapokutana na majaribu kama yale yale ya mwanzo. Tulipokuwa wazinzi na sasa tumeokoka, Je! Tuna ujasiri wa kuishi  maisha ya mbali zinaa, au bado tupo nusu nusu.

Tuwe na badiliko la dhati, leo tumeanguka katika dhambi Fulani mbaya, sasa tumetubu, tusiwe tena walewale wa kuanza kuangalia angalia nyuma kama mke wa Lutu. Mungu atakuchukizwa na sisi na mwisho wa siku tutakuwa jiwe la chumvi kama sio kutapikwa mfano wa kanisa la Laodikia.

Tumaanishe kwelikweli kuacha mambo maovu tuliyoyazoelea. Jifunze kwa Daudi. Yule sio mzinzi kama wewe unayejitumaisha kwa visa vyake vya zamani, ukadhani kuwa utanusurika hukumu ikiendelea na tabia hiyo.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?(Opens in a new browser tab)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 4

Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post