Category Archive Home

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

Mathayo 26:39 “Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?

41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU”.

Sentensi hiyo … ‘Roho ipo tayari lakini Mwili ni dhaifu’… inamaanisha kuwa Tunapotaka kufanya kitu chochote cha KiMungu…roho zetu zipo tayari kufanya jambo hilo, lakini miili yetu haipo tayari…

Katika habari hiyo hapo juu tunasoma, Baada ya Bwana Yesu kuzunguka mchana kutwa pamoja na wanafunzi wake kuifanya kazi, jioni ilipofika hawakupata muda wa kupumzika badala yake walikwenda moja kwa moja kwenye nyumba moja ambayo waliandaliwa wakae, wakiwa humo Bwana aliendelea kuzungumza na wanafunzi wake mambo mengi, pamoja na kuwaaga, maana huo ndio ulikuwa usiku wa mwisho kukaa nao, hivyo walikaa masaa mengi kwenye hiyo nyumba, wakiwa wanaimba, na kuonywa katika safari yao, na kutiwa moyo na Bwana..zaidi ya hayo katika usiku huo huo ndio Bwana aliwaosha miguu wanafunzi wake kuwapa kielelezo, pamoja na kushiriki meza ya Bwana…hivyo walichelewa sana muda wa kulala…Ukifuatilia kwa makini utakuja kugundua kuwa sio chini ya saa nane usiku ndio waliacha kuzungumza…Kwahiyo ni wazi kuwa walikuwa wamechoka mno.. Lakini cha kipekee ni kwamba, baada ya mazungumzo hayo ya muda mrefu hivyo, bado Bwana aliwaambia wakasali pamoja naye wasilale…

Hebu tafakari mchana kutwa mmetembea huku na huko, na bado mpaka muda wa usiku mmechelewa kulala, badala mpumzike ndio kwanza mnaambiwa mkasali, kwa hali ya kawaida ni ngumu kidogo lakini Bwana alijua hilo linawezekana…Na ndio maana akawaambia ya kuwa ‘siku zote roho ipo radhi, lakini mwili ndio dhaifu’…Hivyo hapo ni vita vya kupambana na mwili..Ikiwa na maana kuwa tukiweza kuushinda mwili basi tutafaidika sana katika roho.

Sasa ni namna gani ya kuushinda mwili?

Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa, sisi kuwa na mwili sio dhambi! Kusudi la Mungu kututengenezea mwili pamoja na tamaa zake halikuwa baya tangu mwanzo, wala halikuwa mtego! Bwana alitutengenezea hii miili, pamoja na tamaa zake ili tuweze kuishi katika hii dunia kwa raha na furaha pasipo kuboreka, ndio kusudi la mwili, kwamba ili tusikwazike kipindi mwili unataka kupumzika, akauumbia kitu kinaitwa usingizi, hivyo wakati mwili ukitaka kupumzika, unazama kwenye usingizi mzito, ambao unampa mtu raha sana anapolala…hebu tafakari kusingekuwa na usingizi, na miili yetu inajizima ghafla tu inapochoka halafu tunaisubiria masaa labda 7 au 8 ndio ijiwashe tena, tuweze kuendelea na shughuli zetu, tungeichoka hii miili kiasi gani??

kadhalika ili mtu asiboreke katika kula, Mungu akauwekea mwili hamu ya kula kiasi kwamba mtu atatamani kula hata kama wakati mwingine hana njaa…lakini kusudi kuu la kula si kutupa sisi raha, bali kuupa mwili nguvu…tafakari endapo kungekuwa hakuna raha yoyote katika kula, lakini tunalazimika kula hivyo hivyo tungeichoka hii miili kiasi gani?..na tungeilisha hata vitu visivyofaa..n.k

Vivyo hivyo ili tuufurahie ulimwengu huu, tusije tukajihisi tumewekwa sehemu isiyo na maana Mungu katuumbia tamaa nyingi tofauti tofauti, ambazo hizo ni kama zinaongeza ladha za kuishi katika huu ulimwengu, tamaa ya kukusanyika pamoja, kucheza pamoja, kufurahi pamoja, na nyingine nyingi….Ndilo lilikuwa ni kusudi la Mungu tuishi katika ulimwengu huu pasipo kuboreka wala kuona ni mahali pabaya….

Lakini baada ya Adamu na Hawa kuasi, dunia yote ikaingiliwa na uovu, hivyo sio kila kitu kikawa kinafaa tena kutamani katika ulimwengu…Adamu akampa shetani milki ya ulimwengu huu, shetani akavumbua na kuwekeza mambo yapotezayo mengi, hivyo kwa yeyote atakayeangukia kwa tamaa moja wapo ya mambo yake aliyoyavumbua yeye, atakuwa amepotea, hivyo ndio maana biblia inatuambia tutoke katika ulimwengu, wala tusiutamani ulimwengu, kwasababu ulimwengu umeshaharibika.

Sasa tukirudi kutafakari ni namna gani tutaushinda mwili.

Mwili hatutaushinda kwa kuukemea, kwasababu tamaa hizi ziliumbwa na Mungu mwenyewe,wala hazikuwekwa na shetani…. huwezi kukemea njaa, wala usingizi, wala huwezi kukemea pua zako zisisikie harufu nzuri, wala huwezi kukemea mwili wako usisimke unapopitia hali Fulani ya kuusisimua.

Njia pekee ya kuushinda mwili, ni kujitenga mbali na vishawishi vinavyosababisha tamaa, kwamfano ukitaka mate yasikutoke, dawa ni moja tu! Kukaa mbali na sehemu wanazotengeneza vyakula unavyovipenda, huwezi kujizuia usitamani chakula mbele ya chakula, ni vita ngumu ambayo hutaiweza, kadhalika unapotaka kujizuia usiwake tamaa za mwili, dawa ni kukaa mbali na vichochezi vyote kama utazamaji wa picha chafu( pornography) pamoja na kampani za kidunia, ambazo kutwa kuchwa ni kuzungumzia hayo mambo, miziki ya kidunia, na pia kutakaa kuwa katika mahusiano na mtu yeyote kabla ya ndoa,Hilo tu! Utasikia mtu anakumbia niombee nishinde tamaa, tamaa zinanisumbua!!! Hakuna maombi yoyote ya kushinda hayo mambo ndugu yangu! Usidanganyike!! Dawa ni kukaa mbali na hivyo vitu.

Kadhalika ukitaka kushinda usingizi dawa ni kukaa mbali na kitanda na kuwa bize!..Unatoa mawazo yako katika kulala na kuyapeleka katika kitu kilichopo mbele yako.. Hakuna maombi yoyote ya kuuzuia usingizi…Bwana Yesu hakuwaambia wakina Petro waamke waanze kukemea pepo la usingizi!! Hapana…aliwaambia waamke wasali!…ikiwa na maana kuwa hakuna cha pepo hapo..Ni jambo la kuamua tu!.

Nimekutana na mtu akiniambia kila nikiingia kwenye ibada, au nikiwa katika kusali au kusoma Neno usingizi unanijia? Lakini nikitazama movie Fulani usingizi haunijii…kwahiyo hilo litakuwa ni Pepo Fulani linalonizuia kusoma Neno!…Ndugu hilo sio pepo! Ni wewe mwili wako umeupa nafasi ya kulala unapotaka kusoma Neno..Utauliza kivipi?…Hebu tafakari kama ni shetani ndiye anayekupa usingizi wakati wa kusoma biblia, jiulize ni movie ngapi za kidunia ambazo pia ulipozifungua kuziangalia tu haijapita dakika tano umelala?..utagundua kuwa hata hizo za kidunia kama umeboreka nazo unalala pia! Sasa kama ni shetani ndiye anayekuletea usingizi unaposoma Neno, vipi unaposinzia wakati unaangalia hizo za kidunia zinazokuboa?..je! na hapo ni shetani? Kwamba anakuletea usingizi usiangalie movie za kidunia?…Hivyo utaona usingizi unakuja wenyewe popote pale unapofanya jambo lisilokunufaisha au lisilokusisimua sana…

Kwahiyo dawa ya kushinda usingizi unaposali ni kwenda kujifunza kwa kina umuhimu wa maombi, ukishajua umuhimu wa maombi, na ukijifunza kutotoa udhuru kuwa ni shetani kakupitia kamwe hutalala!..usingizi utakapokuja utauzima tu!..Wengine wasiolala wala hakuna chochote cha kipekee ndani yao kinachowafanya wasilale wala wasikudanganye kuwa ni pepo lipo juu yako! Hakuna pepo hapo ni wewe mwenyewe hujaamua kuwa makini tu!…Mimi sijawahi kulala ibadani, na wala hakuna chochote cha kipekee kinachoendelea ndani yangu, wala hakuna pepo lolote ninaloshindana nalo ndani, wala hakuna maono ninayoona kujizuia kufanya jambo hilo…Nikujizuia tu! Na kuelewa umuhimu wa hicho kitu! Basi!..Na wote wasiolala wasikudanganye kuwa wao ni wa kiroho sana!…hapana! ni wameelewa tu umuhimu wa kinachoendelea pale na wamejifunza kuuzuia usingizi! Wengine wametambua kuwa kila wakiingia kwenye ibada wakiwa wamekula ni rahisi kulala, hivyo wanajifunza kula baada ya kutoka kwenye ibada n.k….ndicho kinachowafanya wao wasilale, hakuna cha ziada!, wala wasikudanganye kuwa unahitaji kufanyiwa maombi ya deliverance!..hakuna !Ni wewe kubadilika tabia tu!.

Biblia inasema Roho I radhi lakini Mwili ni dhaifu….Roho zetu zipo tayari kutenda mapenzi ya Mungu, vita kubwa ni sisi kuishinda kwa kuelewa ufunuo wa maombi, na kusoma Neno..Kadhalika, tutaishinda kwa kukaa mbali na vitu vinavyonyanyua tamaa ya mambo hayo. Pia nenda kasali mbali na kitanda chako, kama upo mwenyewe, lakini ni vizuri zaidi ukisali na mwenzako au wenzako, kwasababu mtatiana nguvu.

Kwa kumalizia Kumbuka kuwa! Ulimwengu huu, sio ule Bwana alioukusudia tuuishi kwa tamaa za miili yetu, ulimwengu huu shetani amekabidhiwa hivyo, matendo yote ya mwili na tamaa zake zote mwisho wake ni ziwa la moto..Biblia inasema…

Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.


Rudi Nyumbani

Print this post

TOA HUDUMA ILIYO BORA.

Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu ambalo ni mwanga wa njia yetu, na taa iongozayo miguu yetu..

Biblia inatuambia katikaAyubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia”….Ikiwa na maana kuwa Mema hayawezi kuja wala Amani tusipomjua Mungu vizuri, hivyo moja ya tatizo kubwa linalotukabili sisi wanadamu hususani wakristo ni kutokumjua Mungu vizuri, Hatumjui Mungu anafanyaje kazi, na anawapatiaje watu mema.

Ni Dhahiri kuwa mema mengi tunayoyatafuta ni mema ya hapa duniani, kama vile kuwa na mali, kufanikiwa katika kazi, kupata mume mzuri au mke mzuri wa Maisha, kupata kibali na vingine vingi..Lakini Mema ya ufalme wa Mbinguni ni bora Zaidi na yenye faida mara dufu!

Kwa ufupi leo tujifunze ni kwa namna gani Mungu anawapatia mema watu wake (mema ya hapa duniani).

Biblia inasema Mungu ni Mungu mwenye haki (Zaburi 7:9-11, Zab.11:7, Isaya 45:21), ikiwa na maana kuwa huwapa haki wale wanaostahili haki. Mungu kamwe hawezi kumpa mtu kitu asichokistahili.

Hebu tujifunze kwa mifano kidogo. Inatokea mtu ana biashara yake ya kawaida tu!, na ni Mkristo ambaye ni mwombaji mzuri, na kila siku anaiombea kazi yake, na anatumia mpaka Mafuta, na maji kuiweka wakfu, na pia anayo mpaka picha ya Bwana Yesu nyuma ya ukuta WA jengo la biashara yake, na kila siku kabla ya kuanza kazi anaiombea hata lisaa limoja, lakini bado unakuta pamoja na jitihada zote hizo mambo bado hayaendi vizuri anapata hasara au anaishia kupata mapato kidogo…Sasa yapo mambo mengi yanaweza kusababisha hilo lakini leo tutaangalia jambo kubwa sana linalosababisha matokeo hayo!… Na hilo si lingine Zaidi ya KUTOKUTOA HUDUMA INAVYOSTAHILI.

Unaweza kuwa mkristo mwombaji kweli na mwaminifu katika kuisogeza kazi yako mbele za Mungu, lakini kama hutajifunza kutenda mapenzi ya Mungu katika kazi yako, maombi yako au ya mwingine juu yako hayatasaidia kitu, yatakuwa ni kazi bure, kama ndani ya kazi yako hutatoa huduma nzuri inayovutia, inayostahili wewe kupata faida, kama hutatoa huduma itakayomvutia yule anayetaka kununua kutoka kwako aweze kurudi tena, kama hutakuwa mnyenyekevu, na mtu wa kujishusha katika kazi hiyo, kama hutakuwa mtu wa kupokea ushauri na kuuchuja katika Neno na kuufanyia kazi, kamwe maombi hayatakusaidia chochote, kadhalika kama hutakuwa msafi katika kazi yako, kama hutakuwa ni mpole kwa wateja wako hata ukibandika picha 20 zenye sura zinazofanana na Bwana Yesu nyuma ya ukuta wa jengo hilo, na kuweka stika za Mistari ya biblia 100, hazitasaidia chochote..

Sasa kwanini Vitu hivyo havisaidii chochote katika kukuletea faida?

Ni kwasababu hujajua kuwa Mungu ni Mungu mwenye haki. Na Watumishi wa Mungu wote wanatumika katika kuwapelekea watu huduma njema sharti walifahamu hilo, Mungu hawezi kumtumia mtu kuwapikia uchafu au sumu watu wake!..hivyo kama wewe ni mchafu katika mahali ulipo kwenye kazi yako labda ya Mgahawa, hiyo ndio sababu Mungu hawezi kuinyanyua izidi kusitawi, hapo ili utumike na Mungu kuwalisha watu wake chakula bora ni sharti uwe msafi sana, kwasababu kuna watu wameamka asubuhi kutoka majumbani mwao na huku wamemwomba Mungu awaepushe na hatari zote ikiwemo sumu na uchafu kuingia katika miili yao, sasa Mungu hawezi kuwajibu hao maombi yao kwa kuwaleta kwenye mgahawa wako ambao unapika uchafu na vyakula visivyo na ubora! Kwa kujidanganya kuwa Mungu ameifunika biashara yako..hapana Mungu ni Mungu mwenye haki! Hawezi mtu kumwomba Mkate akampa jiwe!..Mungu hayupo duniani kuwapatia watu mabaya bali mema…

Hivyo ukitaka kazi yako ya mgahawa isitawi usitegemee maombi tu peke yake…Kuwa Msafi wa viwango vya juu sana,kupita wengine..pika chakula freshi na chenye viwango… ndipo Mungu atakufanya kuwa mtumishi wake kuwapatia chakula safi wanadamu wake na utaona wateja ambao hujawahi kuwaona wakimiminika kwenye hiyo kazi yako.

Na kitu kimoja kisichojulikana na wengi, ni kwamba Mungu hatendi kazi kama shetani atendavyo, shetani ndio ana kitu kinaitwa chuma ulete, au mazingaumbwe anatumia kiini macho,kwamba mtu anaweza kupata chochote katika hali hiyo hiyo aliyopo, hata akiwa mchafu, anaweza kutumia nguvu za giza, kuleta wateja..Mungu hana hicho kitu chuma ulete, wala hatumii kiini macho kuwaletea watu wake fedha!..vinginevyo sifa yake ya kuwa Mungu mwenye haki haitakuwepo!.

Kadhalika kama ni duka, Mungu hawezi kukutumia wewe kuwalisha watu vitu vilivyoisha muda wake wa matumizi (vilivyo-expire), hata kama unakesha kwa wiki mara mbili kuiombea, hata kama unaitolea sadaka nyingi kiasi gani, haiwezekani Mungu kukunyanyua.…kwanini hawezi kufanya hivyo kwasababu, yeye sio Mungu wa kuwapa watu sumu..kama tu asivyokuwa Mungu wa watumishi wa uongo (manabii wa Uongo)..Na kadhalika wafanya biashara wa uongo Mungu hawezi kuwa nao, hata wawe waombaji kiasi gani…atawaepusha watu wake na duka lako….

Pia unapokuwa katika kazi yako unapaswa uwe mnyenyekevu, hupaswi kuwa mtu wa hasira na mtukanaji, au mkorofi. Mungu hawezi kukutumia kuwahudumia watu wake uende ukawatukane na kuwazalilisha..Pia unapaswa kuhakikisha unafanya juhudi kufikisha huduma yako mpaka mlangoni mwa wateja wako au wanaohitaji!..Kwasababu hata watumishi wa Mungu wa kweli anaowatumia hutuletea Neno la Mungu mpaka ndani ya mageti yetu kwa unyenyekevu wote, na ndivyo injili ilivyofanikiwa duniani kote…Kadhalika katika kazi yako, kama unauza mkate mfikishie mteja wako mpaka mlangoni, Mungu anapendezwa na watu wanaotua huduma njema, watu wake wahudumiwe mpaka mahali walipo, na mtu anapohudumiwa kwa njia hiyo, moyoni atafurahi na hivyo atamtukuza Mungu na kumshukuru, na akishafurahi na Mungu atafurahiwa na wewe na hivyo kuibarikia hiyo kazi yako izidi kusonga mbele Zaidi..Hapo ndipo atakapomshawishi Yule mtu kuja tena, na Yule mtu kumwambia mtu mwingine, hivyo hivyo mpaka wanakuwa wengi.

Kadhalika Kama ni mjenzi Mungu hawezi kukutumia wewe kuwajengea watu nyumba ambazo zipo chini ya viwango, kwasababu kuna watu wamemwomba Mungu awapatie nyumba zilizobora na fundi aliyemwaminifu na mwenye ujuzi wa kutosha, hivyo ili Ukidhi hiyo nafasi ya kuwa Mtumishi wa Mungu katika eneo hilo, ni sharti ujitahidi kuielewa vyema hiyo kazi kwa kwenda kutafiti mbinu mpya za ujenzi, kuongeza ujuzi wako na kuongeza ustadi…ili Mungu achague kukutumia wewe na si mwingine katika nafasi hiyo, hapo ndipo utakapoona mafanikio makubwa, usikimbilie kutafuta faida ya haraka haraka, …lakini kama hutataka kutafuta kutoa huduma bora yenye viwango, Bwana Mungu atatafuta mtu mwingine hata kama asiye mkristo aliyekidhi hivyo viwango, kuifanya kazi hiyo…..kwahiyo maombi peke yake hayatoshi!. Matendo ndio yenye nguvu zaidi..Inakupasa ujitahidi uwe bora Zaidi ya wengine ili ukawafanyie watu kilicho bora wamtukuze yeye…

Kadhalika na mambo mengine yote yaliyosalia…jambo ni lile lile…. “JITAHIDI KUTOA HUDUMA ILIYO YA VIWANGO VYA KIMBINGUNI ”

Hata unapotafuta kuoa au kuolewa!! Formula ni hiyo hiyo, NI lazima uwe mtakatifu, usipofanya hivyo na kutegemea maombi peke yake, nakuhakikishia hutaolewa wala hutaoa!…au kama utaoa au kuolewa basi utaoa mtu asiyesahihi au kuolewa na mtu asiyesahihi.

Kwanini?

Kwasababu wewe ni mwenye kiburi na mwasherati halafu unamwomba Mungu akupe mume mwenye hofu ya Mungu, mpole, mnyenyekevu, atakayekujali na kukupenda na kukuheshimu, na asiyekuwa mwasherati….Hujui kwamba huyo mume unayemwomba aliye na vigezo hivyo vya hofu ya Mungu, naye pia anamwomba Mungu ampe mke aliye kama yeye alivyo, mwenye hofu ya Mungu kama yeye, msikivu kama yeye alivyo, asiye mwasherati kama yeye, asiye mwenye kiburi na aliye mnyenyekevu…. Sasa Mungu hawezi kumpa mtoto wake nyoka aliyemwomba samaki!…Kwahiyo Mungu atahakikisha anamtafutia Mke mwema yule mwanamume mwenye hofu ya Mungu kama yeye…Na huyo mke atakuwa sio wewe kwasababu wewe huna vigezo hivyo…..Wewe utaishia kupata mwenye vigezo kama vya kwako vya uasherati, kiburi, na kahaba..Lakini ukiwa mtakatifu Mungu atakupatia Mtakatifu mwenzako na wala haitachukua Muda!…Na pia utakatifu ni wajibu!..hatuwi watakatifu tu kwasababu tunatafuta wachumba!..Ni wajibu wetu kuwa watakatifu maadamu tunaitwa wakristo!

Ndio maana Kuna umuhimu wa kumjua sana Mungu, ili mema yakujie…Mungu anataka tufanye kazi ya haki, tupate haki, anataka tuwe watakatifu tuwapate watakatifu, anataka tuwe wakujitoa ndipo na wengine wajitoe kwa ajili yetu…anataka tuwe watu wa kutoa huduma njema ndipo atubariki. Anataka tumjue kwa mapana hayo….Maombi yanafaa sana endapo tutaomba na kutenda!

Zaburi 18:25 “Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;

26 Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.”

Bwana akubariki sana!. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

MJUE SANA YESU KRISTO.

ITAFAKARI VEMA KAZI YA MUNGU


Rudi Nyumbani

Print this post

KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.

Waebrania 6:11 “Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;

12 ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

13 Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,

14 akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.

15 Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi”.

Neno uvumilivu siku zote limekuwa sehemu ya Mungu, na sisi vivyo hivyo tunapaswa liwe sehemu ya maisha yetu, Kama Mungu asingekuwa mvumilivu ni wazi kuwa mimi na wewe tungekuwa tumeshapotea siku nyingi, kwani wakati tu tuliposikia injili kwa mara ya kwanza, siku hiyo hiyo Mungu alitazamia tubadilike lakini wengi wetu tulikuwa wakaidi, ndio tukazidi kuwa watenda dhambi hata zaidi ya hapo mwanzo miezi ikapita, miaka ikapita, japo tulikuwa tunasikia kila siku mahubiri yanahubiriwa lakini hatukuzingatia, Sasa kama ingekuwa Mungu ni mtu wa kukataa tamaa mapema, sio mvumilivu, sidhani kama mpaka leo hii tungekuwa tunaishi,.. 

Lakini uvumilivu wake, umekuwa neema kwetu na umemzalia matunda si yeye tu, bali sisi pia. Mimi binafsi ninayo kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwa mvumilivu kwangu, kwa maana maovu mengi niliyoyafanya huko nyuma nilidhani nilishamkufuru Mungu siku nyingi. Na ni kwanini Mungu anakuwa mvumilivu kwetu?..Jibu ni ili kutuvuta tufikie TOBA halisi.

Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?”

Zaburi 86: 15 “Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli”

Vivyo hivyo na sisi tulio katika imani, Uvumilivu ni moja ya nguzo muhimu sana. Katika mbio hizi zilizo mbele yetu, japo tumewekewa thawabu kubwa huko mwisho mwa safari lakini ukweli ni kwamba milima na mabonde ya ibilisi hayakwepeki, majaribu na masumbufu, na wakati mwingine dhiki tutakutana nazo hapa duniani, na Bwana Yesu alishatueleza kabisa kuwa mambo hayo tutakuwatana yao wala hakutuficha,(Yohana 16:33)..Hivyo ni safari inayohitaji uvumilivu.

Lakini Swali ni Je! uvumilivu wa aina gani huo unaohitajika kwetu?

Kuna mwingine anaweza akawa labda anapitia matatizo yake binafsi, labda uchumi wake umeyumba, au amekumbana na matatizo ya kifamilia, au magonjwa n.k..na huku nyuma hata hana habari na Mungu, sasa mtu wa namna hii, anaweza akatiwa moyo kibinadamu awe mvumilivu katika hali ngumu anayoipitia kwa huo muda..Lakini huo sio uvumilivu unaozungumziwa katika maandiko.

Uvumilivu unaozungumziwa ni uvumilivu unaolenga Imani. Yaani kutokukatishwa tamaa na hali unayopitia sasa hivi ambayo inaweza kukusababishia kupoteza thawabu yako uliyoandaliwa mwisho wa safari..kwamfano wakati mwingine unaweza ukaona unapitia katika hali Fulani ngumu ambayo sababu yake tu ni uliamua kutokukifanya hicho kitu ambacho ni kinyume na mapenzi ya Mungu, unaweza ukawa unatengwa au unachukiwa kwasababu tu umeacha kufanya dhambi, mwanzoni ulikuwa unakunywa pombe na marafiki zako lakini sasa hunywi tena, mwanzoni ulikuwa unakwenda disco lakini sasa huendi tena, mwanzoni ulikuwa msengenyaji lakini sasa husengenyi tena, na matokeo yake kumetokea kundi la watu wanakutengenezea visa tu, wanakuwekea vikwazo,wanakusema vibaya..wakati mwingine ndugu, hata kazini kwako n.k.

Hapo ndipo unapopaswa uvumilie, biblia inasema katika Mhubiri 7: 8 “Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi. 
9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu”…… 

Pasipo uvumilivu hatuwezi kumzaliwa Mungu matunda..Kama vile Bwana alivyotoa ule mfano wa mpanzi, akasema mbegu nyingine ziliangukia pembezoni mwa barabara nyingine zikaangukia kwenye miamba nyingine zikaangukia kwenye miiba,..nyingine kwenye udongo mzuri, hapo Bwana alikuwa anafunua aina tatu ya vipingamizi mtu atakavyokutana navyo kabla ya kuufikia mwisho mzuri wa safari yake, awali ya yote shetani atataka kumpokonya kile alichokisikia, itafika tena wakati ataudhiwa kwa ajili ya hilo Neno aliloendelea kulishika, baadaye tena baadhi ya mambo yatataka kumsonga asizae, na shughuli za ulimwengu huu na anasa, na tamaa ya mambo mengi …

Lakini Yule ambaye atazaa 30, mwingine 60 mwingine 100 Biblia inasema, hakuifikia hiyo hatua hivi hivi tu, bali aliifikia kwa KUVUMILIA vipingamizi vyote.

Luka 8:11 “Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.

12 Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.

13 Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.

14 Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.

15 Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda KWA KUVUMILIA.’’

Hivyo ndugu, tunapaswa tuilinde Imani Mungu aliyotupa mara moja tu, Na hiyo tutailinda kwa kuvumilia mabaya yote shetani atakayojaribu kutulea mbele yetu yatakayotufanya tuuache wokovu au turudi nyuma….Iwe ni magonjwa, iwe shida ya fedha, iwe ni kukosa mavazi, iwe ni kuwa yatima, iwe ni kuwa mjane, iwe ni kuwa tasa, iwe ni kupigwa au kutengwa au wakati mwingine kufungwa, vyovyote vile yasitufanye sisi kukosa uvumilivu wa kuyaongojea tuliyoandaliwa mbele. Tuige mfano wa Ibrahimu. 

Ufunuo 2:3 “tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.”

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MNGOJEE BWANA

SHUKURU KWA KILA JAMBO.

TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?


Rudi Nyumbani


Print this post

WALIOITWA NI WENGI, ILA WATEULE NI WACHACHE.

Kama Ukijifunza Biblia kwa undani utagundua kuwa Bwana Yesu hakuwa na wanafunzi 12 tu! Bali alikuwa na wanafunzi wengine wengi sana Zaidi ya 70 biblia inasema hivyo katika (Luka 10:1-2)…Lakini baadaye alikuja kuteua wanafunzi 12 tu miongoni mwao wakutembea naye kila mahali alikokwenda ambao aliwaita Mitume. 

Sasa kama ukizidi kufuatilia kwa makini, utagundua kuwa Bwana Yesu alianza kwanza kuchagua wanafunzi wake wengi katika hatua ya Kwanza, ikiwemo wale 12, kwahiyo tuseme lilikuwepo jopo la watu kama 80 hivi waliochaguliwa na Bwana, na ni wazi kuwa wote Bwana aliowaita aliwaambia kuwa watakuwa na shughuli ya uvuvi wa watu…alipita huko na huko kuwaita kutoka katika ulimwengu, katika njia ile alikutana na mvuvi Petro akamwita, katika njia nyingine akakutana pengine na fundi wa nyumba akamwita, sehemu nyingine akakutana na Mathayo mtoza ushuru akamwita…wengine pengine walikuwa hawana shughuli yoyote wapo mtaani akawaita, likawa kundi moja la watu kama 80 hivi walioitwa….Na wote walioitwa walikuwa sawa machoni pa Bwana Yesu, hakuna aliyekuwa mkubwa zaidi ya mwingine, na wote aliwaambia waache vyote wamfuate, na walimtii..Sasa hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya wito..kundi kubwa la wanafunzi liliitwa…. (Kwa somo refu jinsi gani Bwana aliwachagua wanafunzi wake na jinsi anavyowachagua sasa unaweza kututumia ujumbe inbox tutakutumia hilo somo).

Hatua ya pili ilifuata kipindi kifupi baadaye, pengine baada ya miezi kadhaa, ambapo Bwana akaanza tena kuwatenga wanafunzi 12, miongoni mwa lile kundi kubwa la wanafunzi wake…kumbuka hawa 12, hawakuteuliwa moja kwa moja kutoka kwenye ulimwengu, hapana! bali kutoka katika lile kundi la wanafunzi wengine aliokuwa nao…Huo ndio ulikuwa mchujo wa pili, Ndio siku ile Bwana Yesu alipokwenda kukesha kwenye maombi na Mungu akamfunulia mitume 12 miongoni mwa lile kundi…

Luka 6:12 “ Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 13 Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; AKACHAGUA KUMI NA WAWILI MIONGONI MWAO, ambao aliwaita Mitume; 14 Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, na Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartolomayo, 

15 na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote, 

16 na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti. 

17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Uyahudi wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao; 18 na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa”

Unaona?..Mitume 12 walichaguliwa miongoni mwa kundi la wanafunzi wengi…sasa hawa 12 hawakuchaguliwa kwasababu ya jitihada yao yoyote waliyokuwa nayo, au kwasababu ya utakatifu wao, au kwasababu walikuwa wanajuhudi kuliko wengine, au kwasababu mbele za Mungu wenyewe ndio walikuwa wanaonekana wanaunafuu…Hapana, walichaguliwa kwa Neema tu… Neno ‘neema’ linakaribiana sana kufanana na neno ‘bahati’….lakini sio bahati…Neema ni Zaidi ya bahati, bahati mara nyingine inamwangukia mtu ambaye amestahili, lakini Neema siku zote ni kwa mtu ambaye hajastahili…Hivyo hawa 12 waliochaguliwa katika mchujo wa Pili walipata NEEMA na sio BAHATI. Walikuwa hawastahili kuchaguliwa lakini walichaguliwa…Na hata hao wengine pia sio kwamba hawakuchaguliwa kwasababu walikuwa waovu au kwasababu walikuwa watakatifu sana, hapana! ni uchaguzi tu wa Mungu! Ndivyo ilivyompendeza awachague wale na hao wengine awaache, hatuwezi kuelezea kibinadamu, na wala hatuwezi kumwuliza Mungu kwanini kafanya hivyo! (soma Warumi 9:13-25).

Sasa katika hatua hii ya Pili ndipo linapotimia Neno hili “walioitwa ni wengi ila wateule ni wachache”…Hapo liliitwa kundi kubwa pengine la watu Zaidi ya 80, lakini walioteuliwa kwa Neema kuwa mitume ni 12 tu!.

Lakini bado mchujo unaendelea kwasababu hata miongoni mwa hao walioteuliwa 12, bado kuna uwezekano wa kupotea…Sio kwasababu tu! Umeitwa Mteule basi ndio tiketi ya kusema nimeokolewa…

Biblia inatuambia kuwa hata “wateule wanaweza kudanganyika”.

Mathayo 24:23 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 

24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; WAPATE KUWAPOTEZA, KAMA YAMKINI, HATA WALIO WATEULE.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.

 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”.

Yuda alikuwa miongoni mwa wateule 12, lakini alidanganyika na kupotea!…na hapo biblia inatuonya kuwa katika siku za mwisho watatokea makristo wa Uongo, watatoa ishara na maajabu wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule…

Wakati huo tunaoishi ni sasa, wateule wanaozungumziwa hapo ni wale wote ambao Bwana ameshawaita watoke katika ulimwengu, na kuwateua miongoni mwa watu wake, na kuwapa neema ya kuzijua siri za ufalme wa mbinguni kama wewe unayesoma hapa…Kumbuka sio mambo yote Bwana Yesu alikuwa anawaambia makutano, ni machache sana ndio alikuwa anawaambia makutano, siri zake nyingi alikuwa anawafunulia wale mitume 12 tu aliowachagua…wengine wote alikuwa anawafundisha kwa mifano…

Mathayo 13:10 “Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? 

11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa”.

Unapopata Neema ya kusikia injili popote pale, tena unapata kuzijua siri za ufalme wa mbinguni ambazo wengine hawazioni wala kuzipata, na kuna kitu ndani kinakushuhudia kuwa ni kweli… fahamu kuwa wewe ni mteule, lakini katika hizi siku za mwisho wateule wengi watadanganyika kama tu vile Yuda alivyodanganyika na kuishia kumsaliti Bwana Yesu… Yuda alishawishika kabisa ndani ya moyo wake kumwamini Bwana Yesu katika hatua za kwanza za wito wake, alipata ufunuo kabisa kuwa Yesu ndiye masihi aliyetabiriwa, na hivyo akaingia gharama ya kuacha kila kitu na kumfuata Yesu, kwasababu hakuna mtu yeyote ambaye angemfuata Yesu bila kuacha kila kitu na kujikana nafsi yake, Yuda alifanya vyote hivyo, aliitikia wito inavyopaswa….lakini ilifika wakati akaanza kulizoelea Neno, akaanza kuingiwa na tamaa ya vitu vya ulimwengu, akaanza wizi kidogo kidogo, akaanza kuipenda dunia kidogo kidogo, Bwana hakumfukuza asiambatane naye, alimwacha mpaka mwisho, wala upako wake haukukatika aliendelea nao alitoa pepo na kuombea watu kama kawaida na kupokea uponyaji, lakini mwisho wake ulikuwa mbaya, alipasuka matumbo (Matendo 1:16-20).

Na hata leo, ulianza vyema kusikia injili na kuamua kumfuata Yesu kwa moyo, hapo ni Bwana alikuita kweli na akakuteua kuwa karibu naye Zaidi ya wengine, uliacha vyote na kumfuata…lakini imefika kipindi sasa umelizoelea Neno, umeoza ndani, unamwibia Bwana, umekuwa ni mwana wa ulimwengu huku, huku bado unatembea na Yesu, kumbuka Bwana hatakufukuza wala hatakutenga, ataendelea kutembea nawe kama alivyotembea na Yuda, wala hataonesha dalili ya kukudharau wala kukuvunjia heshima, na wala nguvu ya kufanya miujiza hatakupokonya, lakini mwisho wako utakuwa kama wa Yuda!…ili maandiko yatimie , Yuda alikuwa ni mteule lakini Bwana alisema ni kheri asingezaliwa mtu kama huyo kuliko mambo mabaya ambayo yatakwenda kumpata!…Hebu fikiria Mtu aliyeteuliwa na Mungu mwenyewe anaambiwa maneno hayo?.

Ndugu hizi ni siku za mwisho sana, Hayo ya akina Yuda yalitokea ili kutufundisha sisi watu wa siku hizi za mwisho, kuwa tufanye IMARA WITO wetu na UTEULE WETU. Kama maandiko yanavyotuambia..

2 Petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi KUFANYA IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.


Imarisha wito wako ewe Mteule. Ni wakati wa kumrudia Bwana pasipo mguu mmoja nje wala mguu mmoja ndani, kabla wakati wa kupasuka matumbo haujafika, kabla wakati wa kujutia kama Yuda haujafika, kabla wakati wa kula tonge la mwisho la Bwana, na shetani kukuingia haujafika, siku hiyo mlango utakuwa umefungwa, Yuda baada ya kulila lile tonge shetani alimwingia, ikawa ndio mwisho wake pale. Tengeneza wakati wako, linda wito wako na utendee kazi uteule wako.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

JE! UMECHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU?

JE! KARAMA NI UTHIBITISHO WA KUWA NA MUNGU?


Rudi Nyumbani


Maran atha!

Print this post

TUKAZE MWENDO ILI TUUFIKILIE UTIMILIFU.

Mambo ya dunia hii yanatupa picha halisi ya mambo yanayoendelea rohoni, Kwamfano tukiangalia mataifa yaliyoendelea kama ya Ulaya, tukiyalinganisha na mataifa ambayo hayajaendelea kama vile ya Afrika, utagundua kitu kimoja cha tofauti, utaona watu wa huku wanapambana maisha yao yote ili kupata yale mahitaji ya msingi (Basic needs) kama vile Chakula, malazi na mavazi,.Na mtu aliyefanikiwa kuwa na hivyo vitu basi anaonekana tayari ametoka kimaisha ndio maana tunajulikana kama mataifa machanga..Lakini ukitazama yale mataifa yaliyoendelea utagundua kuwa vitu kama hivyo sio kipaumbele chao kwani karibu kila raia anao uhakika wa kupata mahitaji hayo ya msingi wengine tangu wanazaliwa tayari wanayo, kwani serikali tayari ilishaandaa mazingira mazuri kwa raia wao..

Wao kipaumbele chao kikubwa kipo katika mambo ya utafiti, utakuta jopo kubwa la watu limejikita katika mambo ya utafiti maisha yao yote, na matokeo yake ndio tunayoyaona sasa kwa teknolojia wanazozianzisha duniani, uwezo wa kusafiri katika anga za mbali na mambo ya mawasiliano n.k…Na hiyo ndio inayowafanya waonekane kuwa ni mataifa makubwa na watu wake waonekane kama ni watu bora kuliko wengine tukizungumza kibinadamu.

Vivyo hivyo katika mambo ya rohoni, Mtume Paulo aliona baadhi ya makanisa yapo katika hali ya Uchanga, kipindi kirefu kinapita hata wakati mwingine maisha yao yote lakini bado wanahangaika na mambo yale yale ya msingi ya awali, hawaonyeshi dalili ya kuendelea mbele, Watu wanataka kila siku wapigiwe kelele juu ya mafundisho yale yale ya awali,.wanyweshwe maziwa tu na sio vyakula vigumu vya rohoni, Sio kana kwamba Mtume Paulo alikuwa hawezi kuwafundisha mengine, hapana lakini alikuwa anaona kama tu yale ya msingi wanapata shida kuyatii haya mengi watawezaje?..

Na mafundisho yenyewe aliyoyoataja pale ni kama haya: Mafundisho ya TOBA, mafundisho ya kumwamini Mungu, Mafundisho ya Ubatizo, mafundisho ya ufufuo unaokuja, mafundisho ya Hukumu za Mungu zinazokuja, na mafundisho ya ukombozi(kuwekea watu mikono).

Ambayo kimsingi haya yote ni mafundisho ambayo kila siku tunajifunza na tunafundishwa, makanisani, mitandaoni, mikutanoni n.k..

Hapo Je! sisi si, watoto wachanga?, sisi si maskini wa kiroho?.

Waebrania 5:10 “kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

11 Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

12 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya”.

Waebrania 6 :1 “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu,

2 na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.

3 Na hayo tutafanya Mungu akitujalia”.

Hivyo kabla ya kumwomba Mungu atupeleke katika hatua nyingine ya kujifunza siri za ndani za Yesu Kristo, kama hizo ambazo mtume Paulo alizidokeza alipomfananisha na Melkizedeki, kwa jinsi Melkizedeki alivyokuwa hana baba, wala mama, wala mwanzo wa siku wala mwisho, na ndivyo Bwana wetu Yesu alivyokuwa, mfano wa Melkizedeki kuhani wa milele, kuna siri nyingine nyingi sana zimuhusuzo Bwana wetu Yesu Kristo hatuzijui bado , ambazo tukizijua hizo, hatutaishi kama tulivyo..

Kwasababu ni wazi kuwa bado Kristo anajifunua kwetu kila siku, mpaka Yule malaika wa 7 atakapokuwa tayari kupiga baragumu lake, hapo ndipo Siri yote ya Mungu itakapotimizwa.. Na itakapotilimilika SIRI hiyo (Ambayo inamuhusu Yesu Kristo mwenyewe), Mwisho wa kila kitu utakuwa umefika..

Ufunuo 10:5 “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,

6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;

7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii”.

Hivyo tumwombe Mungu atusaidie tuvute katika hii hatua ya uchanga tuliyopo sasa, Tusifurahie tu wakati wote kuhubiriwa habari za kutubu dhambi, na kubatizwa,..hayo ni maziwa ndugu, bado hatujaanza kula chakula, Tukiweza kuvuka hayo ndipo Mungu atakapotupeleka katika hatua nyingine..Toba na Ubatizo ni mafundisho ya awali ya msingi, lakini jengo lenyewe bado halijasimama…Lengo ni kupandisha jengo sio msingi, ndio maana tunahitaji kukua kila siku…

TUKAZE MWENDO ILI TUUFIKILIE UTIMILIFU.

Shalom. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

SAUTI AU NGURUMO?


Rudi Nyumbani

 

Print this post

YAKUMBUKE YA NYUMA.

Nguvu ya kuendelea mbele tunaipata kwa kutazama tulipotokea…Usipokuwa na jicho la kutazama ulipotokea, usipokuwa na jicho la kukumbuka ni wapi ulipitia, utaishia kuwa mtu wa kunung’unika na kulalamika …

Ili tuweze kuishi Maisha ya ushindi siku zote katika haya Maisha ya hapa duniani, ni lazima tuishi Maisha ya kutafakari ni mambo gani ya nyuma Mungu aliyotutendea….unatazama kama Mungu wakati fulani alikupigania kwa kile, wakati huu atanipigania pia kwa hichi, Imani ndio inapokuja hapo..Ukishindwa kukumbuka ya nyuma kamwe hutaweza kuyashinda yanayokuja.

Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana, wakati mwingine kuandika chini, mambo yote makubwa na madogo Mungu anayokutendea ili usisahau, hiyo itakusaidia pindi utakapokutana na tatizo kama hilo basi utakumbuka kirahisi uweza wa Mungu aliokupigania huko nyuma na utapata nguvu mpya.

Uweza wa Mungu unadhihirika mahali palipo na Imani, na Imani haiwezi kuja kama utayasahau matendo makuu ya Mungu aliyokutendea nyuma…Ndicho kilichowatokea wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, ilikuwa kila mara wanasahau mambo makuu Mungu aliyowatendea nyuma na hivyo kuishia kumdharau Mungu kwa mambo madogo yanayotokea mbele yao, Walipotuma wapelelezi kuipeleleza nchi ya Kaanani na kukuta wenyeji wa kule ni majitu makubwa, badala wakumbuke kuwa Mungu alishawapigania huko nyuma kumwangusha Farao ambaye alikuwa na nguvu kuliko hayo majitu, wao wakasahau na kuanza kujiona nafsi zao kama mapanzi, hivyo ikawa dhambi kubwa mbele za Mungu,

Hayo yamewapata ili kutuonya sisi watu wa zamani hizi, tunapaswa tukumbuke uweza wa Mungu..aliotutendea huko nyuma pindi tunapokutana na jaribu fulani mbele yetu..Hata mwanafunzi ili aweze kulipata swali kisahihi, ni lazima awe na uwezo wa kukumbuka ni wapi alishafanya swali kama hilo, na wapi mtego wa swali hilo upo..asipokuwa na uwezo huo kila kitu kwake kitakuwa ni kipya.

Na ndio maana katika agano la kale Wanyama ambao walikuwa hawacheui walijulikana kama najisi, Mnyama anayecheua ni ambaye anao uwezo wa kula chakula na kukihifadhi tumboni baadaye anakirudisha na kikitafuna tena na kukimeza kama vile ng’ombe,..Inafunua kuwa sisi kama wanyama wa Kristo tusio najisi, tunapaswa tuwe na uwezo wa kukumbuka mambo yote makuu Mungu aliyotutendea nyuma, huko ndio kutafuna tena kile tulichokula, lakini tukiwa wasahauji, ndio yatatukuta kama yale ya wana wa Israeli.

1 Wakorintho 10:9 “Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.

11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke

Unapopitia kupungukiwa kidogo, kumbuka kuna kipindi ulipitia hali ngumu kuliko hiyo na Mungu alikufungulia mlango, hivyo tumia huo ushuhuda kukabili tatizo lililopo sasa, useme kama Mungu alinipigania kipindi kile cha taabu atanipigania na sasahivi, kwasababu Mungu ni yule yule habadiliki!…Kama unapitia ugonjwa fulani sasa, kumbuka kipindi fulani nyuma ulipitia ugonjwa wa hatari na Bwana akafungua mlango wa wewe kupona…tumia huo ushuhuda kukataa mawazo ya kukata tamaa sasa..

Kama umezungukwa na hatari, au unakabiliana na hatari, au tatizo mbele yako, sio wakati wa kupaniki, ni wakati wa kurudisha kumbukumbu zako nyuma na kukumbuka Bwana alivyokuokoa kwenye mikono ya waovu, na alivyokuepusha na hatari kimiujiza miujiza.n.k n.k, na kusema kama alifanyia vile, atanifanyia na hata sasa vile vile kama aliwafanyia wale, atakufanyia na wewe,…Mungu aliwaambia wana wa Israeli maneno haya wakati wanakwenda kukabiliana na maadui zao katika nchi ya Kaanani..

Kumbukumbu 7:17 “Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kunipita mimi; nitawatoaje katika milki yao?

18 Usiwaogope; KUMBUKA SANA Bwana, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote;

19 uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje Bwana, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya Bwana, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.

20 Tena Bwana, Mungu wako, atampeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako.

21 Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho.”

Bwana akubariki!, kama utapenda kujifunza Zaidi na kwa urefu juu ya “kukumbuka wema wa Mungu, aliokufanyia nyuma” unaweza kufungua ujumbe huu >>> MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

Maran atha! . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

Katika agano la kale, wayahudi walivyochanganyikiwa sana juu ujio wa masihi mpaka kupelekea kugawanyika makundi mengi, ndivyo ilivyo hata katika agano jipya watu wengi wanavyochanganyikiwa katika habari ya Roho Mtakatifu jinsi anavyokuja juu ya mtu, hadi sasa imepelekea kutokea makundi mengi tofauti tofauti ambalo kila moja linaamini katika uthibitisho wake.

Kama tunavyofahamu katika agano la kale biblia ilishatabiri kuwa Masihi (YESU KRISTO) atakuja, lakini kwa bahati nzuri au mbaya haikueleza katika mtitiriko unaoeleweka sana, bali sisi wa agano jipya kwa Kutazama maisha ya Kristo ndio tunaoelewa jinsi maandiko yalivyotimia ,..Lakini katika agano la kale ilikuwa ni ngumu sana kuelewa, na saa nyingine maandiko yaliyonekana kama yanajichanganya..Kwamfano unabii alioutoa Isaya kuhusu Kristo katika (Isaya 53), inaonyesha kuwa Masihi atakuja kuteswa na kuuliwa kwa ajili ya dhambi za watu wengi..Lakini sehemu nyingine katika kitabu hicho hicho cha Isaya inasema Masihi atakuwa mfalme, naye ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, naye atadumu milele.

Unaona sehemu moja inasema atakufa lakini sehemu nyingine inasema atadumu milele,..Lakini je! Wale walioshikilia tu unabii mmoja labda tuseme wale walioamini kuwa Masihi atasulibiwa, au wale walioamini tu Masihi ataishi milele, je! wote Hawapo sawa? Jibu ni La!..Sisi tunaoishi katika agano jipya ndio tunaojua kuwa Wote wapo sawa kabisa, lakini wote walioweza kuamini nabii zote mbili ndio wapo sawa zaidi kuliko wale wengine, kwani ni Kweli kuna wakati Kristo atasulibiwa atakufa lakini atafufuka na atarudi tena, na atakaporudi atakuja kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho kama nabii zote mbili zilivyotabiri.

Yohana 2:33 “Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.

34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

35 Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako”.

Sasa tukirudi katika habari za Roho Mtakatifu, kama tusipoweza kuyavunja maandiko na kufahamu utendaji kazi wake, tutaishia kuchanganyikiwa sana, na mwisho wa siku kila mmoja ataamini anachokiamini…

Leo hii kuna watu wanaomini kuwa uthibitisho pekee wa mtu kuwa na Roho Mtakatifu ni kudhihirisha karama Fulani ndani yake, kama vile kunena kwa lugha, kutoa unabii, kufundisha, kuhubiri n.k…na mtu yeyote asipodhihirisha mojawapo ya karama yoyote basi huyo bado hajapokea Roho Mtakatifu na maandiko wanayoyasimamia ni haya …

Matendo 2:17 “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri”

Na ….

1Wakoritho 12:4 “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule”:

Vile vile wapo wengine wanaoamini kuwa uthibitisho wa Roho Mtakatifu, ni kuwa atakuongoza na kukutia katika kweli yote sawasawa na Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” ….

na hivyo uthibitisho mwingine wowote mbali na huo ni uongo..

Halikadhalika wapo wanaoamini kuwa uthibitisho pekee wa Roho Mtakatifu ni pale anapokushuhudia ndani yako kuwa wewe ni mwana wa Mungu, …sawasawa na Warumi 8:16 “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;”

Wapo wengine wanaoamini uthitisho wa Roho Mtakatifu peke yake ni kukufanya uwe mtakatifu kama vile jina lake lilivyo.…

Na makundi mengine mengi…

Lakini swali ni kama lile lile tu la watu wa agano la kale, je! Wote hawa ni waongo?…Jibu ni hapana wote wapo sawa kabisa!!, isipokuwa tu wanashindwa kutofuatisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu juu ya mtu kulingana na wakati na majira. Kama tu vile wale wa agano la kale walivyoshindwa kufahamu kuwa kuna kuja kwa kwanza kwa Kristo na kuja kwa pili.

Ifahamike kuwa Bwana Yesu aliposema hakuna mtu anaweza kuja kwake kama hakuvutwa na Baba yake aliyempeleka, alimaanisha kusema vile, Leo hii “huwezi hata kuchomwa moyo na maneno ya Mungu kama siyo matunda ya Roho Mtakatifu yanayofanya kazi ndani yako”, ukiona tu unaamini kuna Mungu, ukiona unatamani kumfahamu Mungu hata kama hujaokoka, ukiona unahukumiwa ndani yako kwa ajili ya dhambi zako, ukiona una hofu ya Mungu, basi ufahamu kuwa huyo ni Roho Mtakatifu anatenda kazi ya kukuvuta kwake,..Jambo ambalo si watu wote wanalo, usidhani kuwa injili unayoisikia na kukuchoma moyo inamchoma kila mtu duniani, dhambi uzifanyazo na kusikia kuhukumiwa zinamuhukumu kila mtu duniani, kama ingekuwa hivyo kusingekuwa na vitendo vya kinyama unavyoviona kila mahali..Si wote wapo hivyo, na ndio maana hupaswi kuichezea hiyo neema kwasababu kuna wakati utafika Roho Mtakatifu hatakuvuta tena kwa Mungu, ukishafika huo wakati ndugu, hata Bwana Yesu mwenyewe akutokee hapo, na malaika wote mbinguni, hutakaa ugeuke, kwasababu Roho wa kukuvuta hayupo.

Sasa, ikitokea mfano Yule mtu akautii ule wito na kuamua kutubu dhambi zake, na kufuata vigezo vyote alivyoambiwa na Bwana Yesu vya kwenda kubatizwa, katika maji mengi na kwa Jina la BWANA YESU, hapo ndipo Yule Roho aliyekuwa anamvuta anapata kibali cha kuingia ndani yake, na kufanya maskani humo, na akishaingia anakuwepo huko milele, mtu huyo ndio anakuwa amezaliwa mara ya pili..Sasa kwa kuwa Yule mtu bado ni mchanga kiroho, Roho Mtakatifu anaanza kazi kadha wa kadha ndani yake..mojawapo ni kumsafisha na kuua baadhi ya vitu ambavyo alikuwa hawezi kuviacha, Roho Mtakatifu anamfanya upya tena..

Tito 3:5 “si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;’’

Anaanza kumfanya aupende utakatifu kuliko kitu kingine chochote, hapo ndipo hamu ya baadhi ya mambo ya kidunia inakufa kabisa…hizo ni dalili za awali kuwa Roho Mtakatifu yupo ndani yako..Kwa nje unaweza usione chochote, wala usisikie msisimko wowote lakini ndani kunawaka moto wa kutaka kuwa kama Mungu..

Pili anatenda kazi ya kumwongoza na kumtia katika kweli yote: Hapa Anaanza kumwongoza katika vyanzo sahihi vya Neno lake, anaanza kumpa kiu ya kujifunza Neno la Mungu, faraja yake mtu huyo inakuwa kwenye Neno la Mungu tu, na si mahali pengine, anaanza kuona Mungu kwake ndio kila kitu..Uthibitisho ni kuwa hapo kabla hayo mambo alikuwa hayaoni…Ile kiu inaongezeka siku baada ya siku.

Jambo lingine analolifanya Roho Mtakatifu ni kumshuhudia huyo mtu kuwa yeye ni mwana wa Mungu, kushuhudiwa huku sio kusikia sauti inakuambia wewe ni mwana wa Mungu, hapana, bali ni kuona maisha yako unayopitia yanafanana na wana wote wa Mungu waliopita huko nyuma,…..yaliyowapata watakatifu wa nyuma na wewe yanakupata yawe ni mema yawe ni mabaya..Biblia ndio itakuwa uthibitisho wako..Mungu kwako anajidhihirisha kama Baba.

1Petro 5:9 “….mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.”

Jambo lingine ni anakuwa kwako kama mfariji, na mshauri(1Thesalonike 1:16, 2Wakoritho 13:14)): Utaona tu, jinsi atakavyokuwa anakutia nguvu wakati baada ya wakati, unapoishiwa nguvu, utashangaa anaachilia jambo Fulani kubwa ambalo linakupa nguvu ya kuendelea mbele kwa muda mrefu sana…Na ndio maana tunasema mtu yeyote aliye na Roho Mtakatifu kweli hawezi kuishia njiani katika safari yake ya wokovu..(Isaya 40:27-31)

Na ndio maana katika hicho kipindi chote Roho wa Mungu anachokutengeneza, hupaswi kumzimisha,..Wengi wanamzimisha kwa kuanza kuyarudia yale machafu waliyoyaacha huko nyuma, tayari Mungu alishawafanya kuwa huru, lakini bado wanaurudia utumwa..Hapo ndipo mtu hakui wala hasongi mbele kiroho, anabakia kuwa katika hali ile ile, miaka nenda miaka rudi..yeye ni mchanga tu.

Lakini ikiwa mtu huyu atatembea na Roho Mtakatifu kwa uaminifu wote, Roho anakuwa anajaa ndani yake kidogo kidogo, mpaka anafikia ujazo kamili wa Roho Mtakatifu, na ujazo huo ni uhitimu. Hapo ndipo Roho Mtakatifu anakuvika nguvu za kuweza kuwa shahidi wake, kama vile Bwana Yesu alivyoaambia mitume wake..

Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi”.

Hichi ndio kile kilichomkuta Bwana Yesu wakati ule anakwenda kubatizwa, sio kana kwamba ile ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kumpokea Roho hapana bali Roho alikuwa naye tangu kuzaliwa kwake, lakini kwasababu ya kazi ilimpasa Mungu amwongezee nguvu kwa Roho Yule aliyekuwa ndani yake ili kushuhudia habari za ufalme wa mbinguni. Na ndicho kilichokuwa juu ya Mitume sio kwamba kipindi walichokuwa wanatembea na Bwana walikuwa hawana Roho Mtakatifu, walikuwa naye, ndio yule aliyemfunulia Petro kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu n.k isipokuwa walikuwa naye si katika kile kiwango kile Mungu alichokikusudia kwa kazi yake waliyokuwa wanakwenda kuifanya hapo mbele.

Ndivyo ilivyo hata sasa, wengi tunatamani tupokee Roho Mtakatifu katika hatua ya mwisho, lakini sio kuanzia katika hatua ya kwanza.. siku hiyo hiyo tumempa Kristo maisha yake, bado siku hiyo hiyo wanataka Roho Mtakatifu atupe nguvu ya kuwa mashahidi wake kwa mfano wa mitume,..Ni kweli Roho anaweza kufanya yote kwa pamoja, lakini fahamu kuwa ndani yake, bado utakaa chini tu akufundishe,atembee na wewe, akuandae na akuthibitishe.

Hivyo kaka/dada, fahamu kuwa Roho Mtakatifu ni zaidi ya kunena kwa lugha, au kuona maono..Usifurahie kusema tu nilipokea Roho Mtakatifu siku ile nilipoamini,,jiulize je! Hadi sasa Roho Mtakatifu anatembea na wewe, au ulishamzimisha siku nyingi..Je! anakurudisha katika utakatifu?, Je! Anakushuhudia kuwa wewe ni mwana wa Mungu. Je! Anakuongoza katika kweli yote..Je! anakupasha bahari ya mambo yanayokuja?..Ikiwa hivi vitu vimekufa ndani yako, tubu upesi umgeukie Mungu, mwambie Bwana nataka nianze na wewe upya.

Na ikiwa bado Roho Mtakatifu yupo mbali na wewe nikimaanisha kuwa hujamkabidhi bado Bwana maisha yako, fahamu kuwa biblia ipo wazi inasema, Warumi 8:9… “Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Pasipo huyo, usidhani kuwa utaiona mbingu, au utamfahamu Mungu..Tubu leo kwa kumaanisha kumfuata Kristo itii injili, kisha nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la Bwana Yesu Kristo, Roho Mtakatifu aingie ndani yako na aanze kufanya kazi kwako.

Bwana akubariki sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazondana:

Je! Umepokea kweli Roho Mtakatifu?

Hatua za Roho Mtakatifu katika kutuongoza.

Je! karama ni uthibitisho pekee wa kuwa na Mungu?

HOME

Print this post

UDHAIFU WA SADAKA!

Moja ya nguzo muhimu sana katika Imani ya Kikristo ni SADAKA, Sadaka ni nguzo muhimu sana, kwasababu hata Kristo mwenyewe alifanyika sadaka kwa ajili yetu ili sisi tuokolewe…Kama Kristo asingejitoa nafsi yake kwa ajili yetu sisi tusingekuwa popote, tungekuwa ni wana wa Jehanamu wote, hakuna hata mmoja ambaye angepona.

Kwahiyo kama Kristo alivyojitoa kwetu na sisi pia lazima tujitoe kwa wengine…Ndio maana sadaka ni Muhimu, Roho iliyokuwa ndani ya Kristo ilimpeleka kujitoa nafsi yake kuwa fidia kwa roho nyingi, halikadhalika na sisi kama tumeipokea Roho ile ile ambayo ilikuwa ndani yake, ni lazima itatusukuma na sisi kujitoa kwa ajili ya wengine, kulingana na karama tulizopewa…

Sadaka sio lazima kutoa mali, bali hata kujitoa Maisha ili kwamba wengine wapate uzima, kama Bwana Yesu hakutoa fedha ili sisi tuokolewe bali aliitoa damu yake na Maisha yake kwa kuishi na kufundisha watu njia ya wokovu ili waokolewe. Hiyo ni sadaka kubwa sana na kuu kuliko zote, kutoa Maisha kwaajili ya mwingine ili aokoke. Kama Biblia inavyotuambia katika..

1 Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu”.

Na sadaka sio mchango. Mchango ni kitu unachotoa kuchangia jambo Fulani liendelee mbele lakini sadaka, ni kitu kinachohusisha wewe kupungukiwa ili mwingine aongezewe, au wewe kupoteza ili mwingine apate, hiyo ndiyo maana ya sadaka…haina tofauti sana na neno MUHANGA..Kwahiyo sadaka ni KITU kikubwa Zaidi ya Mchango…Hivyo unapomtolea Mungu sadaka kwaajili ya kazi yake, zingatia kutoa kitu kikubwa Zaidi ya mchango, toa kitu ambacho kimekugharimu sana….ukitoa mchango utapata thawabu lakini sadaka ina thawabu kubwa Zaidi.

Sasa leo hatutaingia sana kuzungumzia Umuhimu wa Sadaka au nguvu ya sadaka, lakini tutazungumzia UDHAIFU WA SADAKA.

Utauliza, sadaka ina madhaifu?..Jibu ni ndio, sadaka ina madhaifu na mipaka..Inayo nguvu ya kubadilisha mambo lakini pia inayo mipaka ambayo haiwezi kupita..kuna mambo ambayo haiwezi kubadilisha…Hebu tusome mistari michache ifuatayo kisha tuendelee…

1 Samweli 15:20 “Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.

21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali.

22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.

Habari hiyo inamzungumzia Mfalme wa kwanza wa Israeli aliyeitwa Sauli, ambaye alilikaidi Neno la Mungu, aliambiwa akaangamize vitu vyote na watu wote (Waamaleki) asiache chochote, hata ng’ombe na mbuzi na kondoo wote auwe, lakini yeye akaangamiza vyote lakini akawaacha wafalme wa ile nchi hai pamoja na ng’ombe walionona na kondoo na kuvileta Israeli kwaajili ya kumtolea Mungu dhahibu, (dhabihu ni sadaka ya kuteketezwa). Kwa moyo wake alijua Mungu anapendezwa Zaidi na Sadaka kuliko kuyashika maagizo yake.. Hakujua kuwa nguvu ya sadaka sio kubwa kuliko nguvu ya kushika maagizo yake. Hivyo akajitumainisha kwa sadaka zile na Mungu akamkataa..

Huo ndio udhaifu wa Sadaka!..Ni kweli Mungu aliagiza watu wamtolee sadaka zilizonona, tena wasimtolee vilema, kwasababu ukimtolea sadaka kilema ilikuwa ni kujitafutia kulaaniwa badala ya kubarikiwa.(soma Malaki 1:13-14). Lakini sadaka hiyo hiyo, ina mipaka. Haiwezi kubadilisha mambo yote, haiwezi ikalivuka Neno la Mungu. Hatuwezi kumuonga Mungu kwa sadaka zetu, ili abadilishe Neno lake..Hapana! tutaongeza baraka tu kwa sadaka lakini si kulibadilisha Neno lake, akisema kuwa roho ya mwenye dhambi itakufa, hata tutoe fedha kiasi gani kama hatutalitii hilo neno na kuacha dhambi! Hizo sadaka hazina msaada wowote, kufa tutakufa tu!…Akisema waasherati na walawiti na waabudu sanamu sehemu yao ni katika lile ziwa la moto! Hata tutoe hazina zote za ulimwengu na kujitoa hata miili yetu, kama hatutatii na kuacha hivyo vitu…Jehanamu haiepukiki.

Sasa habu tuangalie mfano wa Mwisho ambao ni Bwana Yesu mwenyewe aliuota kuonesha udhaifu wa Sadaka!..Tusome.

Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.

26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho”

Mfano huo Bwana Yesu alioutoa kutufundisha kuwa tusiitegemee sadaka, kubadilisha Neno la Mungu..Katika habari hiyo anasema “kabla ya kuitoa sadaka yako, patana kwanza na mshtaki wako”…Ikiwa na maana kwamba kama kuna mtu anakudai, au kuna mtu umemdhulumu, au kuna mtu umegombana naye, na wewe ndiye mwenye makosa na hivyo bado kidogo atakwenda kukushitaki… usikimbilie kwenda kutoa sadaka! Kana kwamba hiyo sadaka uliyoitoa itakukuokoa….Kitu cha kwanza Kimbilia kwanza kwenda kupatana naye, kwasababu usipopatana naye ukachelewa kidogo tu! na yeye akaenda kuripoti polisi, na polisi wakaja kukuchukua na kukuweka ndani! Biblia inasema hutatoka huko…Na hiyo sadaka uliyoitoa ambayo ulitegemea kukusaidia, wakati huo haitakusaidia chochote kukutoa huko gerezani…Mungu hatakuwa upande wako hata kidogo…Hivyo Bwana anasema…Nenda kwanza kapatane naye kabla hajakwenda kukuripoti…sadaka utatoa tu! Nenda kwanza kapatane naye! kwasababu Neno lake linasema…

Warumi 12:18 “Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote”.

Sasa ukikaa kwa vurugu na watu wote, hata utoe fedha kiasi gani kwa Mungu! Haitaruka Neno lake hilo kwamba “mkae na amani na watu wote”…Huo ndio udhaifu wa sadaka, haipiti Neno la Mungu….. “kutii ni bora kuliko dhabihu na kusikia kuliko Mafuta ya Beberu”.

Hivyo ndugu, inawezekana unatoa sadaka nyingi nzuri sana, hilo ni Jema Mungu atakulipa kwa ukarimu wako, lakini sadaka hiyo haiwezi kulipita Neno la Mungu linalosema…

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Wala kulipita Neno hili..

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Sadaka nzuri ni ile inayoambata na kulitii Neno la Mungu.

Uchaguzi unao wewe ambaye hujampa Kristo Maisha yako!..Kumwamini Yesu, na kutubu na kuamua kumgeukia huku ukidhamiria kuacha dhambi kabisa, utakapoamua kugeuka na kusema Kuanzia leo hii mimi na ulimwengu basii!! Kristo akiiona nia yako ndani yako kwamba kweli umedhamiria kuacha kwa vitendo, basi atakupa nguvu ya Roho wake Mtakatifu ambaye atakusadia kuweza kuzishinda dhambi kama ulivyosema kutoka katika kinywa chako mwenyewe. Mlango wa Neema bado upo wazi, lakini tunaishi kipindi cha kumalizia, ambapo parapanda siku yoyote inalia na watakatifu wataondolewa ulimwenguni, na ulimwengu kuharibiwa. Hivyo usikiapo maneno haya usifanye moyo wako mgumu, kama ulishampa Kristo Maisha yako, lakini umekuwa vuguvugu ni wakati wakuwa moto, kwasababu walio vuguvugu wote, Kristo alisema atawatapika. 

Bwana akubariki.

Maran atha! .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?

SADAKA ILIYOKUBALIKA NI IPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.

1 Wakorintho 10:23 “Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo

24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.

25 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;

26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.”

Hapo biblia inasema “vitu vyote ni halali” na inasema pia kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza uliza…

Sasa tunajua sokoni kuna vitu vingi vinauzwa, sio tu chakula, bali hata nguo, viatu, vyombo, vifaa mbali mbali, simu,tv n.k..Hivyo aliposema kila kitu kinachouzwa sokoni tule pasipo kuuliza uliza, tunapaswa tutumie hekima na sio kutafsiri tu mstari kama tunavyousoma…hivyo pale hakumaanisha kuwa kila kitu kinachouzwa sokoni kama kiatu, pombe,mabegi, nguo, sumu za panya, majembe, na mashoka tuyale! Tuyale kwasababu tu yanauzwa masokoni na maandiko yamesema kila kitu kinachouzwa tule bila kuuliza uliza.. Tukitafsiri maandiko kwa namna hiyo, hatutapata chochote!..Ndio maana pia inachanganya wengi sana, pale Mtume Paulo aliposema “nataka ninyi nyote mnene kwa lugha 1 Wakoritho 14:5” na kuutafsiri mstari kama unavyosomeka pale..bila kuelewa kwanini Mtume Paulo alisema vile…

Tunapaswa tuingie ndani ya mstari huo na kujua Maandiko yalikuwa yanamaanisha nini kuwa ‘kila kitu kinachouzwa sokoni tule bila kuuliza uliza’..

Aliposema kila kitu kuizwacho tule, alikuwa anazungumzia katika engo ya vyakula! Sio bidhaa nyingine tofauti na chakula ambazo zinauzwa masokoni, alikuwa anazungumzia tofauti ya aina ya vyakula, kwamfano umeenda China leo kuhubiri wenyeji wakakukaribisha na kukupeleka kwenye masokoni yao ya umma wanaponunuaga vyakula…na huko ukakuta kuna aina ya vyakula tofauti na vile ulivyovizoea kuviona vinauzwa katika jamii yako ya kiafrika..ukakuta pengine samaki wamechanganywa na majani ya mimea Fulani ambayo hujaijua bado, au nyama ya kuku imepikwa na kuchanganywa na vitu usivyovijua bado.. na wakaenda kukuandalia,Hapo ndio unaambiwa usiulize ulize wewe kula! Bila kuuliza uliza kwamba ni nyama ya kiumbe gani imetengenezewa. Wala usiwe na hofu moyoni mwako kwamba unamkosea Mungu wewe kula hivyo vyakula.. kwaajili ya dhamira zao.

Kwasababu wakikuona wewe unakataa kula aina Fulani ya chakula ambacho hata sio kilevi, bali pengine ni mchanganyiko tu wa vitu usivyovifahamu, wataanza moyoni kushtuka na kujiuliza kwanini huyu mtu hali chakula chetu! Ambacho sisi tunaona ni cha heshima, Kwahiyo watakuwa na maswali mengi ambayo hayana msingi wowote wa kuwavuta wao kwa Kristo, kwasababu hata hicho unachokataa wewe kukila Mungu hajasema usikile! Lakini endapo wamekwambia kwamba hichi ni chakula cha miungu yetu! Hapo utakataa ili wao wasije wakaona kwamba na wewe unakubaliana na wanachokifanya, lakini si kwasababu chakula kile ni najisi.

Au fikiria Mchina anakuja huku kwetu unamkaribisha kwako na unampikia mtori asubuhi, unamtengea ghafla! Anakwambia subiri kwanza! Huu mtori umetengenezwa na nini? Anataka umwelezee kila kitu kabla yeye hajaanza kula!!..kwa mtu mwenye roho nyepesi anaweza akakwazika kwa kitendo hicho tu!..Na kuanza kusema moyoni kwani huyu mtu ananifikiriaje?, anadhani mimi ninaweza kumwekea sumu? Au naweza kumwekea kilevi,? Au anakidharau chakula chetu! Au anatuonaje labda! Na mambo kama hayo!..Lakini utakapoona umemwandalia na yeye akakipokea vizuri hata kama hakula kingi, ni wazi kuwa moyoni mwako utafurahi na ni rahisi Zaidi kukipokea kile alichokileta kuliko endapo angekataa au kuanza kukitolea kasoro chakula chako…

Sasa mambo kama hayo ndio Biblia inasema tuyaepuke! Unapofika ugenini ni Dhahiri kuwa wanajua wewe ni mhubiri au mkristo, hivyo hawawezi kukuwekea sumu mezani, wala kilevi kwasababu ulishawahubiria, hivyo ukitengewa kula bila kuuliza uliza. Ili ndani ya dhamiri zao wasije wakajikwaa, na kukikosa hata kile kizuri ulichowapelekea. Hivyo wakati mwingine hata kama umefika mahali wamekutengea vyakula ambavyo huvipendi, kula tu hata kidogo ili mioyoni mwao wasije wakakwazika na kukikataa hata kile kizuri cha rohoni ulichowapelekea. Na sio tu unapokwenda kuhubiri hata unapoalikwa na rafiki yako au mtu yeyote usiwe mtu wa kuuliza uliza.

Sasa endapo ukiwa sokoni peke yako una uhuru wa kuchagua upendacho, , lakini kwa watu wenye Imani changa, epuka uchaguzi uchaguzi mbele yao, ni rahisi kuwapoteza…

Fanya vitu kwa faida ya wengine na sio faida yako wewe.

Kadhalika, unapokwenda kumhubiria kahaba, usifike tu na kumhukumu kwa mwonekano wake kwa mara ya kwanza, wala usikatae kumkaribisha kwako akiwa na mavazi yake ya kikahaba, ukimshutumu kwa mara ya kwanza tu kwa mwonekano wake pasipo hata kumhubiria chochote ni rahisi kumpoteza moja kwa moja, ataishia kukuchukia tu! Ndani ya dhamiri yake na kujiepusha na wewe.

Lakini ukaanza kumweleza kwanza mambo ya msingi, habari za Yesu Kristo na tumaini analotoa na hatima ya mambo yote ya ulimwengu huu, ataguswa moyo hata kama sio siku hiyo hiyo lakini baada ya muda Fulani atakwambia nifanyaje au yeye mwenyewe utaona anaanza kubadilika…Bwana Yesu alipokutana na yule mwanamke Msamaria kisimani habari ya kwanza hakuanza na kumwambia wewe ni kahaba, unawaume watano…

hakumwambia hayo mambo, alianza kuzungumza naye habari za ufalme wa mbinguni kwanza, baadaye sana ndipo alipoanza kumwambia habari za Maisha yake kuwa ana waume watano, na huyu aliyenaye sio wake..lakini angeanza tu kwa kumwambia wewe ni kahaba utakwenda motoni! Unadhani ni nini kingetokea? Hapo hakufanya jambo kwa faida yake binafsi, bali kwa faida ya ufalme wa Mbinguni.

Kadhalika unapomhubiria mtu asiye wa Imani yako labda muislamu, asiyejua chochote kuhusu Imani ya kikristo usianze kwa kumwambia unajua kula nguruwe ni ruksa!..sio najisi?..Hivyo kula nguruwe! Huku unamwonyeshea mistari….Ukifanya hivyo ataishia kukuchukia tu na pengine kuanzisha malumbano…Anza kwa kumweleza Habari za Yesu Kristo, na nguvu ya msalaba…hayo mambo mengine yatakuja baadaye sana…kwani asipokula nguruwe Maisha yake yote, siku ile ya hukuma Bwana atamwuliza kwanini ulikuwa huli nguruwe duniani?..unaona! hataulizwa hayo mambo…kwahiyo mambo mengine hayana maana sana kuyakazania kwa watu wachanga!. Hatupaswi kuhubiri ili kutimiza wajibu Fulani au kujionesha tunajua maandiko, bali tunapaswa tuhubiri kwa NIA thabiti kabisa ya kutafuta roho zilizopotea.

1 Wakoritho 8:1“…. Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga”

Kadhalika ukikutana na Muislamu na kuanza kumwambia YESU NI MUNGU! Hatakuelewa hata kidogo, mambo hayo yanahitaji ufunuo wa Roho, ambao huo ni Mungu mwenyewe anamfunulia mtu taratibu taratibu, sasa kwa mara ya kwanza mtu asiyemjua Mungu jambo hilo haliwezi kumwingia akilini, anahitaji kukaa chini ya madarasa ya Roho kwanza, taratibu taratibu Roho Mtakatifu baadaye sana ataanza kumfunulia SIRI YA YESU KRISTO kuwa ni Mungu sawasawa (1Timotheo 3:16)..

Wanafunzi wa Bwana Yesu wenyewe iliwachukua muda kuelewa jambo hilo, sembuse mtu anayemsikia Kristo leo kwa mara ya kwanza??..Hivyo unapaswa umhubirie kwanza nguvu za msalaba..Nini kilitokea Edeni na ni kwanini kwa kupitia mtu mmoja dhambi iliingia…na ni kwanini kwa kupita mtu mmoja dhambi isifutike!…hapo kidogo kidogo unaanza kumleta kwa YESU, acha amwelewe kuwa Yesu ni nabii tu, kwa kipindi cha mwanzo mwanzo, akishamwelewa kuwa ni nabii, na kumwamini baadaye Roho atampandisha hatua moja Zaidi na kumfunulia kuwa ni mwana wa Mungu, baadaye yeye mwenyewe ndiye atakayekuja kukuthibitishia kwa maandiko kuwa YESU NI MUNGU! Kwahiyo kila kitu ni hatua!

Hata sisi tulipokuwa wadogo hatukuambiwa Watoto wanapatikana wapi, badala yake tulidanganywa tu wanakwenda kununuliwa, lakini tulipokuwa kiufahamu ndipo tulielewa mambo yote kuwa wanazaliwa, na Watoto wa Kiroho ndio hivyo hivyo, hawawezi kujua au kuelewa mambo yote kwa mara ya kwanza.

Ndio maana kwenye huo mstari wa 24 Mtume Paulo anasema “mtu asitafuta faida yake mwenyewe bali ya wengine”

Bwana akubariki sana.

Kama hujaokoka! Kumbuka wokovu unaanzia hapa hapa duniani!…kama vile hukumu inavyoanza hapa hapa duniani, hivyo kama hujampa Bwana maisha yako kwa kutubu na kudhamiria kabisa kuacha dhambi bado unayo nafasi hiyo sasa kabla mlango wa Neema haujafungwa, tubu sasa na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa Jina la YESU kwa ajili ya ondoleo la dhambi na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, kumbuka biblia inasema wote wasio na Roho wa Yesu hao sio wake (Warumi 8:9) Hivyo tafuta Roho Mtakatifu..Huo ndio muhuri wa Mungu.

Maran atha!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

JE! MKRISTO ANARUHUSIWA KULA NGURUWE?

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

KARAMA ILIYO KUU NI IPI?.

KALAMU YA CHUMA.


Rudi Nyumbani

Print this post

UDHAIFU WA SADAKA!


Moja ya nguzo muhimu sana katika Imani ya Kikristo ni SADAKA, Sadaka ni nguzo muhimu sana, kwasababu hata Kristo mwenyewe alifanyika sadaka kwa ajili yetu ili sisi tuokolewe…Kama Kristo asingejitoa nafsi yake kwa ajili yetu sisi tusingekuwa popote, tungekuwa ni wana wa Jehanamu wote, hakuna hata mmoja ambaye angepona.

Kwahiyo kama Kristo alivyojitoa kwetu na sisi pia lazima tujitoe kwa wengine…Ndio maana sadaka ni Muhimu, Roho iliyokuwa ndani ya Kristo ilimpeleka kujitoa nafsi yake kuwa fidia kwa roho nyingi, halikadhalika na sisi kama tumeipokea Roho ile ile ambayo ilikuwa ndani yake, ni lazima itatusukuma na sisi kujitoa kwa ajili ya wengine, kulingana na karama tulizopewa…

Sadaka sio lazima kutoa mali, bali hata kujitoa Maisha ili kwamba wengine wapate uzima, kama Bwana Yesu hakutoa fedha ili sisi tuokolewe bali aliitoa damu yake na Maisha yake kwa kuishi na kufundisha watu njia ya wokovu ili waokolewe. Hiyo ni sadaka kubwa sana na kuu kuliko zote, kutoa Maisha kwaajili ya mwingine ili aokoke. Kama Biblia inavyotuambia katika..

1 Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu”.

Na sadaka sio mchango. Mchango ni kitu unachotoa kuchangia jambo Fulani liendelee mbele lakini sadaka, ni kitu kinachohusisha wewe kupungukiwa ili mwingine aongezewe, au wewe kupoteza ili mwingine apate, hiyo ndiyo maana ya sadaka…haina tofauti sana na neno MUHANGA..Kwahiyo sadaka ni KITU kikubwa Zaidi ya Mchango…Hivyo unapomtolea Mungu sadaka kwaajili ya kazi yake, zingatia kutoa kitu kikubwa Zaidi ya mchango, toa kitu ambacho kimekugharimu sana….ukitoa mchango utapata thawabu lakini sadaka ina thawabu kubwa Zaidi.

Sasa leo hatutaingia sana kuzungumzia Umuhimu wa Sadaka au nguvu ya sadaka, lakini tutazungumzia UDHAIFU WA SADAKA.

Utauliza, sadaka ina madhaifu?..Jibu ni ndio, sadaka ina madhaifu na mipaka..Inayo nguvu ya kubadilisha mambo lakini pia inayo mipaka ambayo haiwezi kupita..kuna mambo ambayo haiwezi kubadilisha…Hebu tusome mistari michache ifuatayo kisha tuendelee…

1 Samweli 15:20 “Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.

21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali.

22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”

Habari hiyo inamzungumzia Mfalme wa kwanza wa Israeli aliyeitwa Sauli, ambaye alilikaidi Neno la Mungu, aliambiwa akaangamize vitu vyote na watu wote (Waamaleki) asiache chochote, hata ng’ombe na mbuzi na kondoo wote auwe, lakini yeye akaangamiza vyote lakini akawaacha wafalme wa ile nchi hai pamoja na ng’ombe walionona na kondoo na kuvileta Israeli kwaajili ya kumtolea Mungu dhahibu, (dhabihu ni sadaka ya kuteketezwa). Kwa moyo wake alijua Mungu anapendezwa Zaidi na Sadaka kuliko kuyashika maagizo yake.. Hakujua kuwa nguvu ya sadaka sio kubwa kuliko nguvu ya kushika maagizo yake. Hivyo akajitumainisha kwa sadaka zile na Mungu akamkataa..

Huo ndio udhaifu wa Sadaka!..Ni kweli Mungu aliagiza watu wamtolee sadaka zilizonona, tena wasimtolee vilema, kwasababu ukimtolea sadaka kilema ilikuwa ni kujitafutia kulaaniwa badala ya kubarikiwa.(soma Malaki 1:13-14). Lakini sadaka hiyo hiyo, ina mipaka. Haiwezi kubadilisha mambo yote, haiwezi ikalivuka Neno la Mungu. Hatuwezi kumuonga Mungu kwa sadaka zetu, ili abadilishe Neno lake..Hapana! tutaongeza baraka tu kwa sadaka lakini si kulibadilisha Neno lake, akisema kuwa roho ya mwenye dhambi itakufa, hata tutoe fedha kiasi gani kama hatutalitii hilo neno na kuacha dhambi! Hizo sadaka hazina msaada wowote, kufa tutakufa tu!…Akisema waasherati na walawiti na waabudu sanamu sehemu yao ni katika lile ziwa la moto! Hata tutoe hazina zote za ulimwengu na kujitoa hata miili yetu, kama hatutatii na kuacha hivyo vitu…Jehanamu haiepukiki.

Sasa habu tuangalie mfano wa Mwisho ambao ni Bwana Yesu mwenyewe aliuota kuonesha udhaifu wa Sadaka!..Tusome.

Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.

26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho”

Mfano huo Bwana Yesu alioutoa kutufundisha kuwa tusiitegemee sadaka, kubadilisha Neno la Mungu..Katika habari hiyo anasema “kabla ya kuitoa sadaka yako, patana kwanza na mshtaki wako”…Ikiwa na maana kwamba kama kuna mtu anakudai, au kuna mtu umemdhulumu, au kuna mtu umegombana naye, na wewe ndiye mwenye makosa na hivyo bado kidogo atakwenda kukushitaki… usikimbilie kwenda kutoa sadaka! Kana kwamba hiyo sadaka uliyoitoa itakukuokoa….Kitu cha kwanza Kimbilia kwanza kwenda kupatana naye, kwasababu usipopatana naye ukachelewa kidogo tu! na yeye akaenda kuripoti polisi, na polisi wakaja kukuchukua na kukuweka ndani! Biblia inasema hutatoka huko…Na hiyo sadaka uliyoitoa ambayo ulitegemea kukusaidia, wakati huo haitakusaidia chochote kukutoa huko gerezani…Mungu hatakuwa upande wako hata kidogo…Hivyo Bwana anasema…Nenda kwanza kapatane naye kabla hajakwenda kukuripoti…sadaka utatoa tu! Nenda kwanza kapatane naye! kwasababu Neno lake linasema…

Warumi 12:18 “Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote”.

Sasa ukikaa kwa vurugu na watu wote, hata utoe fedha kiasi gani kwa Mungu! Haitaruka Neno lake hilo kwamba “mkae na amani na watu wote”…Huo ndio udhaifu wa sadaka, haipiti Neno la Mungu….. “kutii ni bora kuliko dhabihu na kusikia kuliko Mafuta ya Beberu”.

Hivyo ndugu, inawezekana unatoa sadaka nyingi nzuri sana, hilo ni Jema Mungu atakulipa kwa ukarimu wako, lakini sadaka hiyo haiwezi kulipita Neno la Mungu linalosema…

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Wala kulipita Neno hili..

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Sadaka nzuri ni ile inayoambata na kulitii Neno la Mungu.

Uchaguzi unao wewe ambaye hujampa Kristo Maisha yako!..Kumwamini Yesu, na kutubu na kuamua kumgeukia huku ukidhamiria kuacha dhambi kabisa, utakapoamua kugeuka na kusema Kuanzia leo hii mimi na ulimwengu basii!! Kristo akiiona nia yako ndani yako kwamba kweli umedhamiria kuacha kwa vitendo, basi atakupa nguvu ya Roho wake Mtakatifu ambaye atakusadia kuweza kuzishinda dhambi kama ulivyosema kutoka katika kinywa chako mwenyewe. Mlango wa Neema bado upo wazi, lakini tunaishi kipindi cha kumalizia, ambapo parapanda siku yoyote inalia na watakatifu wataondolewa ulimwenguni, na ulimwengu kuharibiwa. Hivyo usikiapo maneno haya usifanye moyo wako mgumu, kama ulishampa Kristo Maisha yako, lakini umekuwa vuguvugu ni wakati wakuwa moto, kwasababu walio vuguvugu wote, Kristo alisema atawatapika. 

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post