Category Archive Home

Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu?

Swali: Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu kwa mgonjwa aliye katika uhitaji huo, kwaajili ya kuokoa maisha yake?


Jibu: Biblia inasema maneno yafuatayo…

1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU.

17  Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”

Maadamu mtu akiondolewa damu kiasi kidogo mwilini mwake, Hafi!!.. na vile vile mtu anayepokea damu mwilini mwake pia Hafi!, kinyume chake ndio anapata UZIMA! (wa mwilini).. basi ni wazi kuwa si dhambi kuchangia damu kwa mtu mwingine…..Zaidi sana ni jambo la upendo, ikiwa hakuna njia nyingine ya kumsaidia mhitaji huyo zaidi ya hiyo ya kumchangia damu.

Kwanini si dhambi!.. ni kwasababu hata sehemu ya damu tulizonazo tumepokea kutoka kwa wazazi wetu!…HAKUNA MTU ANAYEZALIWA DUNIANI NA DAMU YAKE MAALUM (Special), wote tunazipokea kutoka kwa wazazi wetu ndio maana zinamfanano na hao!, na zinamfanano na ndugu zetu tuliozaliwa nao familia moja.

Kwahiyo kumchangia damu mgonjwa si dhambi!… Maana utamchangia atapona!, na kwa njia hiyo yaweza kuwa sababu ya kumvuta kwa KRISTO, (akiona upendo wako namna hiyo).. lakini kama ukimnyima na akifa katika hali yake ya kutokuamini hakuna faida yoyote wewe unayoipata…

Kwahiyo ni afadhali utafute namna ya kuokoa roho kwa njia hiyo, kwasababu hakuna hasara yoyote unayopata katika mwili wako utoapo kiasi kidogo hiko cha damu na kumpatia mwingine!.. ni lita ngapi za damu umepoteza wakati wa mzunguko wako (wewe mwanamke) na bado unaendelea kuishi.

Ni lita ngapi za damu umepoteza wewe mwanaume ulipopata majeraha au ulipofyozwa na hao mbu kutandani mwako siku zote za maisha yako?.. Kwa kutafakari hayo yote hakuna sababu ya kumnyima damu ndugu yako, ikiwa kuna ulazima huo, na wala hakuna sehemu yoyote kwenye biblia iliyokataza kuchangia damu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA? 

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini kuna mrudio wa uumbaji kwenye Mwanzo sura ya pili?

Swali: Tukisoma Mwanzo sura ya kwanza tunaona Mungu akimaliza kazi yote ya uumbaji kwa zile siku saba, lakini tukirudi kwenye Sura ya pili tuona ni kama tena Mungu anarudia uumbaji anamuumba mwanadamu,  na pia mimea, je kulikuwa na uumbaji wa aina mbili ulitokea pale. Na ni nini tunajifunza pale?


JIBU: Jibu ni hapana, uumbaji wa Mungu ulikuwa ni ule ule mmoja, tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani. isipokuwa Sura ya kwanza Mungu anaeleza ‘kwa taswira ya ujumla’, lakini katika sura ya pili anaeleza jinsi ‘utaratibu wa uumbaji wake ulivyokuja kutokea’, mpaka kuileta hiyo picha ya ujumla.

Kwamfano katika Sura ya kwanza anasema Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume..

Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Lakini katika sura ya pili anaonyesha jinsi alivyoanza kumuumba  kwa kumtoa ardhini mpaka alivyompulizia pumzi ya uhai, hadi utaratibu wake wa kutawala.

Mwanzo 2:4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.  7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

Umeona,? Vilevile ukisoma Mwanzo 1:11&12, utaona Mungu anaumba mimea yote . Lakini hapo kwenye sura ya pili anaonyesha  jinsi mime hiyo inavyokuja kutokea, anaeleza kwanza inaanza  katika mbegu, kisha inyeshewe mvua, ikue baadaye ndio iwe mche kamili wenye matunda.

Hivyo, Kulikuwa na umuhimu wa kuwekwa sura zote mbili, ili tuelewe  kanuni za Mungu za utekelezaji wa mipango yake. Maana kama tungeishia tu sura ya kwanza tusingeelewa ni kwa namna gani mambo yanaendelea kama yalivyo leo.

Ni fundisho gani lipo hapo?

Hata sasa Mungu anasema jambo. Lakini pia huna budi kuelewa mpango wake wa utekelezaji wa hilo jambo! Ili usiudhike, au usikate tamaa, au usijikwae, au usiwe na mashaka. Unatafakari ni kweli Mungu alimuumba mwanamke tangu awali, lakini kutokea kwake kulikuja baadaye sana, tena sio ardhini bali ubavuni mwa Adamu. Kama hilo tusingelifahamu, tusingeelewa kwanini tunaambiwa sisi wote ni mwili mmoja.

Kama tusingejua kuwa  ili mti ufikie matunda, kama Mungu alivyoukusudia, ni lazima uanze kwanza kama mbegu, ioze ardhini, kisha ipate mvua, imee, itoke katika jani, hadi shina, hadi mti. Tungesema hii si sawa, kuna shida, mbegu kuoza ardhini, hakuna mmea hapo?.

Halikadhalika hata sasa Mungu amekuahidi pengine, atakupa jambo Fulani. Sasa usitarajie lije ghafla tu, pengine litapitia hatua Fulani, huwenda likaonekana kama limetoweka kabisa,kama vile mbegu inayooza ardhini, lakini mwishowe itakuja kutokea tu, kama tu Yusufu alivyoonyeshwa kuwa ndugu zake watamwinamia, Au Ibrahimu kuonyeshwa atakuwa  baba wa mataifa mengi, lakini mapito yao unayajua, Yusufu kuuzwa utumwani, kutupwa gerezani, Ibrahimu kuwa tasa. Lakini mwisho utaona yale waliyoahidiwa yalikuja kutokea vilevile.

Tunapaswa tumwelewe sana Mungu ili tuwe na amani, Neno la Mungu linaposema, kwa kupigwa kwake sisi tumepona, amini kuwa umepona kwa kifo cha Yesu, hata kama utahisi maumivu mengi kiasi gani leo, daktari atakuambia huwezi kupona ugonjwa wako hautibiki. Wewe amini, tu hilo jambo litatokea, haijalishi litachukua wakati gani, utapitia mateso mengi kiasi gani leo, mwisho wa siku utakuwa tu mzima.

Usiishi tu na mwanzo sura ya kwanza, ishi pia na sura ya pili. Utamwelewa Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI

Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)

Ni maneno gani Bwana Yesu aliyokuwa anayaandika ardhini? (Yohana 8:7).

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini biblia ni neno la Mungu?

Swali: Je ni kweli biblia ni Neno la Mungu?


Kabla ya kujibu kwanini biblia ni Neno la Mungu, na si kitabu kingine chochote?… hebu tujiulize kwanza na tujadili kwanini

Biblia ni Neno la Mungu kwasababu lina maneno yaliyo hai..

Vivyo hivyo biblia ni kitabu cha Mungu, kwasababu kimebeba taarifa sahihi kumhusu Mungu.. Na taarifa KUU ndani ya kitabu hiko kitukufu, ni taarifa ya mwanadamu kuondolewa dhambi kupitia YESU KRISTO (Hiyo ndiyo taarifa kuu) ambayo inaleta “UZIMA WA MILELE KWA MTU”..Na ndio karama kuu ya MUNGU kwetu.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Vitabu vingine vyote vilivyosalia havijabeba suluhisho lolote la ondoleo la dhambi za Mtu, badala yake zimebeba tu taarifa za maadili, au staha, mambo ambayo yanapatikana hata katika vitabu vya sheria za nchi.

Lakini taarifa na njia ya ondoleo la dhambi zipo katika BIBLIA TU PEKE YAKE!!!..

Kwasababu “dhambi” ndio sumu pekee ya mwanadamu, na hiyo ndio kizuizi kikubwa cha mtu kumkaribia Mungu, hivyo mtu akiondolewa hiyo anakuwa ameokoka! Hata kama maisha yake hapa duniani bado yanaendelea.

Na ni kwa njia gani mtu anaondolewa dhambi zake moja kwa moja??

Matendo 2:36 “ Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU”.

Kanuni ya kuondolewa dhambi, ni kutubu na kubatizwa (Marko 16:16). Na toba halisi ni ile inayotoka moyoni yenye madhamirio ya kugeuza mwelekeo moja kwa moja. Na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la BWANA YESU (Matendo 8:16, na Matendo 19:5).

BWANA YESU AKUBARIKI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JIPE NAFASI KATI YA TAARIFA UNAYOIPOKEA NA MAAMUZI UNAYOYATOA.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.

UWEZA WA MUNGU NJE YA WAKATI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Nyota ya bahati yangu ni ipi?

Je ni kweli kuna watu wenye nyota ya bahati? Na je nitaipate nyota hiyo maishani mwangu?


JIBU: Nyota ya bahati inasadikika ni pale mtu anapobahatika kupata kitu kwa haraka au kwa wepesi, au bila matarajio yake,au nguvu zake nyingi katika kukipata tofauti na wengine. Kwamfano labda mtu ni mchimba madini, mara ghafla anatapa dhahabu nyingi tofauti na wachimbaji wengine. Au mwingine amehitimu chuo, mara anapata kazi nzuri, yenye cheo, zaidi hata ya wengine wengi waliomtangulia. Au ni mfanya-biashara mara anapata tenda kubwa ambayo inainua biashara yake kwa kasi zaidi ya wengine. N.k.

Sasa mtu kama huyu wengi husema ana nyota ya bahati. Lakini je ni kweli?

Ukweli ni kwamba twaweza kusema ana-bahati –tu, lakini hana nyota-ya-bahati. Kwavipi.

Kwasababu mafanikio hayo, yanaweza kuondoka tena kwake, na kama yakibaki, bado bahati hiyo hainunui tunu za rohoni. Mfano amani, upendo, utu wema,  imani, adili, unyenyekevu, na uzima baada ya kifo. N.k., Ni mafanikio ambayo hata mashetani huyatoa.

Lakini ni lazima ujue nyota halisi ya bahati ni ipi? Ambayo katika hiyo unaweza kupata vyote, Kisha uifuate.

Hiyo si nyingine zaidi ya YESU KRISTO. Vitabu vitakatifu vinasema hivyo, Vilevile Watu wote wanalijua hilo, ikiwemo wachawi wote, wanajimu wote, malaika wote, na mashetani yote.

Soma hapa;

Mathayo 2:1  Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, MAMAJUSI WA MASHARIKI walifika Yerusalemu, wakisema,

2  Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana TULIIONA NYOTA YAKE MASHARIKI, nasi tumekuja kumsujudia.

3  Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4  Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

5  Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6  Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

7  Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.

8  Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.

9  Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.

10  NAO WALIPOIONA ILE NYOTA, WALIFURAHI FURAHA KUBWA MNO.

11  Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.

Ikiwa Yesu yupo moyoni mwako. Ikiwa umemwamini, kisha ukamfanya Bwana na kiongozi wa maisha yako. Jambo la kwanza analolifanya ndani yako ni kuondoa laana yote ya dhambi, ambayo humfanya mwanadamu aende kuzimu, ambayo kila mwanadamu anayo. Na wakati huo huo huyo mtu anaitwa mbarikiwa, anaitwa mtakatifu, makosa yake yote yanakuwa yamefutwa, hahesabiwi dhambi tena.

Na moja kwa moja anapewa, Roho Mtakatifu. Sasa Kazi ya huyu Roho Mtakatifu, ni kumtengeneza roho yake,kumsafisha kutoka katika ubaya kumweka katika wema, na kumfanya aweze kushinda dhambi na maovu yote.

Ndio hapo kama alikuwa mlevi, kiu hiyo inaondolewa, alikuwa mzinzi, hamu ya mambo hayo yanakufa ndani yake, alikuwa ana uchungu, furaha inaanza kujengeka, alikuwa ni mwenye hasira, upendo wa ki-Mungu unaumbika sana moyoni mwake, anaanza kupenda watu wote.

Na zaidi sana, anapokea uzima wa milele, hata akifa ghafla, haendi kuzimu, hapotei, bali anakuwa amelala tu, anasubiri siku ya ufufuo, aamshwe aende mbinguni.

Pamoja na hilo, hata yale mengine ambayo alikuwa anayatafuta au anayapata kwa shida, Yesu anampa mafanikio pia  kiwepesi kwasababu aliahidi hivyo. Zile bahati ambazo anatamani azipate, Yesu anamletea mara mia (100), katika maisha yake.

Mathayo 19:28  Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

29  NA KILA MTU ALIYEACHA NYUMBA, AU NDUGU WA KIUME AU WA KIKE, AU BABA, AU MAMA, AU WATOTO, AU MASHAMBA, KWA AJILI YA JINA LANGU, ATAPOKEA MARA MIA, NA KUURITHI UZIMA WA MILELE.

Umeona, mwisho wa siku unakuwa umepata vyote, kwasababu kwa Yesu vipo vyote.

Huoni kuwa hiyo ni NYOTA nzuri sana ya bahati? Kwanini uende wa waganga wa kienyeji, kutafuta laana, huko? Kwasababu wale wanakurushia mapepo, ambayo mafanikio yao ni batili, ni kitanzi, mwisho wa siku ni kukuangamiza, sasa unakuwa umepata faida gani? Wakati mafanikio ya Yesu Kristo, hutajirisha wala hayana huzuni ndani yake, biblia inasema hivyo;

Mithali 10:22 Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo

Ungoja nini usimpokee Yesu leo? Ikiwa umedhamiria kwa dhati kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa namna ya kuokoka leo >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

NYOTA YA ASUBUHI.(Opens in a new browser tab)

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu.

Ni nini tunajifunza katika maisha ya Nuhu, ambaye Mungu alimshuhudia kuwa mwenye haki katika kizazi chake? Lakini baadaye akaja kunaswa katika ulevi uliomletea aibu kubwa nyumbani mwake?

Mwanzo 9:20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;  21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

Ulishawahi kujiuliza kama Nuhu asingekuwa mkulima wa mizabibu, angekuwa na wazo la kutengeneza divai? Na hatimaye kuanguka kwenye makosa?

Jibu ni la! Kwasababu bila shaka Nuhu alikuwa mkulima, ili ajipatie rizki, na sio ili atengeneze divai. Lakini hakujua kuwa nyuma ya kazi yake ya halali upo mtego wa dhambi. Na hivyo akauridhia na ndio ikamshawishi mpaka kutoa bidhaa isiyopasa katika maisha yake kwa kazi hiyo.

Hata sasa watoto wengi wa Mungu wanashindwa kujua kuwa “shughuli za ulimwenguni zilizo za halali kabisa” zina udanganyifu Fulani nyuma yake, unaolewesha ambao unaweza mpelekea mtu anguko kubwa sana, kama asipokuwa makini.

Bwana Yesu alisema..

Marko 4:18  Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, 19  na SHUGHULI ZA DUNIA, NA UDANGANYIFU WA MALI, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.

Kwamfano labda ni kijana, ameokoka, hapo mwanzo alikuwa amesimama vizuri tu, katika Bwana, anapata muda wa kuomba, kushuhudia, kujisomea Neno n.k. lakini akapata kazi nzuri, na ile kazi ikawa inamlazimu, awe bize wiki nzima, isipokuwa jumamosi na jumapili. Sasa katika miezi ya mwanzo, alikuwa anatimiza majukumu yake ya ushuhudiaji/ kuhudhuria mikusanyiko ya nyumbani na maombi, bila shida siku ya jumamosi, na jumapili anahudhuria ibadani , kama kawaida. Lakini baada ya miezi kadhaa, alivyozidi kufanikiwa, uvivu na udanganyifu wa mali ukaanza kumuingia, akasema, huu muda wangu wa jumamosi, nifanye kitu kingine cha kuniingizia kipato, (jambo  ambalo si baya), lakini hajui kuwa analisogeza mahali ambapo sio sahihi. Na kweli akajiongezea kitu cha kufanya, matokeo yake jumamosi yake yote ikawa ni kazi zake za miradi. Hakuna ushuhudiaji tena, hakuna ibada za jumuiya tena, hakuna maombi.

Na inapofika jumapili, anaamka amechoka, anasema, aa wiki hii napumzika, wiki ijayo nitaenda..anaanza kuwa mdokoaji-dokoaji wa ibada,  hivyo baada ya miezi miwili, anapokea mialiko ya marafiki zake, kwenda kwenye party, picnic, vikao vya kirafiki, sinema, n.k. vyote hivyo vinapaswa vifanyike siku ya jumapili ambayo yupo free. Matokeo yake anahudhuria kanisani mara moja kwa mwezi au miezi miwili. Hilo linaendelea mwaka mzima. Hajui kuwa mwili unafurahia kweli, lakini roho yake inadhoofika siku baada ya siku. Sasa baada ya kipindi kirefu hapo ndipo anashangaa haoni tofauti yake ni watu wa kidunia, kila jambo la ki-Mungu anaona ni mzigo kulifanya, yeye ambaye alikuwa anawaombea wengine anakuwa wa kuombewa, yeye ambaye alikuwa anawaokoa wengine, anafikiwa kuokolewa tena.Hana nguvu tena, ameshaleweshwa, shetani kamweka chini.

Sasa huyu ndio mfano wa Nuhu, Amelewesha na kazi yake. Na utumishi wake. Kwasababu hakujiwekea mipaka,.

Ndio maana maandiko yanatutaka tuwe na kiasi, katika huu ulimwengu.

1Wakorintho 7:31  Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.

Kuwa buzy kupita kiasi, si afya ya kiroho au kimaisha. Ni lazima upate nafasi ya kutosha kujijenga nafsi yako kwa Mungu. Ni vema utumie siku za tano, usiku na mchana kama ni hivyo kuwekeza na kupangilia ratiba yako, lakini upate pia nafasi nyingi ya kumwabudu na kumkaribia Mungu bila masumbufu. Umeajiriwa katika kazi ambayo siku zote saba za wiki, upo kazini, hupewi muda wa kupata ibada yako na Mungu, fahamu hiyo si kazi itokayo kwa Mungu. Fikiria kutafuta kazi nyingine.

Kama ubize, basi Mungu angekuwa buzy zaidi yetu sisi, kwasababu yeye ndio aliyeumba ulimwengu mzima, lakini alijipa pumziko Siku ya saba, akaiweka wakfu, akatuambia na sisi. Tufanye hivyo. Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na wengi wataikosa mbingu kwa ubize usiokuwa na tija wa mambo ya ulimwengu huu, yanayopita.

Ni heri ukose vya dunia, lakini nafsi yako itajirike, kuliko kutajirika duniani na huku nafsi yako unaangamia. Uzima wako upo katika mambo ya rohoni, Jinsi unavyojitenga na Mungu ndivyo unavyojiua mwenyewe.

Kamwe usiyaige ya Nuhu mabaya ya ajira yake, bali yale mema aliyoyafanya kabla ya Gharika.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

UMUHIMU WA KUBATIZWA.(Opens in a new browser tab)

NUHU WA SASA.(Opens in a new browser tab)

(Opens in a new browser tab)KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Mlango la kondoo ulikuwaje?(Yohana 5:2)

Swali: Ule mlango wa kondoo unaotajwa katika Yohana 5:2, ulikuwa ni mlango wa namna gani?, na umebeba ujumbe au ufunuo gani sasa?


Jibu: Turejee.

Yohana 5:2 “Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano”.

Mlango wa kondoo unaozungumziwa hapo ulikuwa ni mlango mdogo katika hekalu la Mungu, uliokuwa unatumika kupitishia kondoo kwaajili ya sadaka ya kuteketezwa (dhabihu).  Ulikuwepo mlango wa kuingilia watu na wa kuingizia wanyama ndani ya hekalu (katika Ua wa ndani).

Utaona lango hili linatajwa pia katika Nehemia 3:1, Nehemia 3:32 na Nehemia 12:39.

Nehemia 3:1 “Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga LANGO LA KONDOO; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli”

Lango hili la kondoo lilikuwa linamfunua BWANA YESU, kwani yeye mwenyewe katika Yohana 10:7 ametajwa kama LANGO LA KONDOO..

Yohana 10:7 “Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, MIMI NDIMI MLANGO WA KONDOO.

8  Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.

9  Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”

Kama vile ule mlango wa kwanza wa kondoo ulivyokuwa lango la yule aliyekuwa hawezi kwa miaka 38 kuponywa na Bwana YESU katika birika lile la Bethzatha vile vile  BWANA YESU ambaye ndiye LANGO halisi amebeba uponyaji wote wa roho zetu na miili yetu.

Je umempokea?

Kama bado fahamu kuwa upo katika hatari kubwa sana ya kuharibiwa na adui, kwani unakuwa upo nje ya zizi, ambapo yupo adui ambaye kazi yake ni kuchinja, kuharibu na kuua.

Yohana10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIMZIMISHE ROHO.

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

JE! UNAMPENDA BWANA?

WALIKUWA WAMECHOKA NA KUTAWANYIKA KAMA KONDOO WASIO NA MCHUNGAJI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kuota unakemea mapepo/ unashindana na nguvu za giza.

Kunaweza maanisha namna tatu, ya kwanza, ni kwamba unapitia kweli vita vya kiroho, lakini ya pili ni unaonyeshwa na Mungu uhalisia wa vita vya kiroho, na tatu unaonyeshwa uwezo wa hali yako ya  kiroho.

Maandiko yanasema

Waefeso 6:12  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama

Tukianza na maana ya kwanza,

Mara nyingine adui huanzisha mashambulizi kuanzia ndotoni, wakati mwingine utakuta mtu anaota ameumwa labda na nyoka kidoleni halafu  anapoamka, anashangaa kinauma kweli, na kama haiishii hapo, anaanza kuona kidole kinazidi kutengeneza kidonda, mpaka kuleta madhara mwili mzima, sasa hayo ni mashambulizi ya kipepo. Na hivyo ikiwa ndoto yoyote umeiota ambayo unaona uhalisia wake mpaka nje, unashindana na mapepo halafu linakukaba, unahangaika kitandani. Ujue ni mashambulizi ya adui, hapo unayo mamlaka ya kubatilisha, kwa jina la Yesu.

Lakini mara nyingine, utajikuta unaota tu unakemea mapepo, unashindana nayo. Si kwamba utakuwa unamashambulizi ya adui, lakini unaonyeshwa tu uhalisia wa vita vya kiroho, na hivyo vipo halisi, au vitakuja mbeleni katika safari yako ya maisha, na unapaswa uvishinde, kwa jina la YESU, kwa simama imara ndani yake..

Na mwisho ni Mungu anakuonyesha kiwango cha kiroho, ulichopo au unachopaswa uwe nacho. Mwingine atakuwa ameokoka, lakini anahofu ya kutoa pepo au kuombea watu, Mungu anakuonyesha uwezo wa kushindana na nguvu za giza unao, au unapaswa uanze kazi ya kuwaombea wengine wanaosumbuliwa na nguvu za giza. Lakini pia pale unapojiona umezidiwa nguvu zao, ni kuonyesha uongeze kiwango chako cha kiroho, kwa maombi, utakatifu, na Neno, ili uwe thabiti rohoni kuzipinga hila za adui.

Kwahiyo kwa vyoyote vile kuona unakemea mapepo, au unashindana na wachawi kwa jina la Yesu. Ni kuonyesha kuwa ni wakati wa kusimama  imara na Bwana. Kwasababu shetani ni adui wako, na adui za ndugu zako, na hivyo unapaswa umpinge sikuzote kwa kuwa thabiti rohoni kwa wewe ambaye umeokoka.

Lakini Ikiwa hujaokoka, basi ni vema ukafanya hivyo leo kwa kumkaribisha Yesu moyoni mwako, ukifahamu kuwa kamwe huwezi kumshinda adui kwa nguvu zako unamwita Kristo.

Ikiwa upo tayari  waweza kufungua hapa kwa mwongozo wa sala ya kuupokea wokovu. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?(Opens in a new browser tab)

Je Mungu anaketi katika giza? (1Wafalme 8:12)

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?

Mungu aliupenda ulimwengu kwasababu asili yake upendo, Maandiko yanasema yeye ni UPENDO.

1Yohana 4:16  Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

Lakini ifahamike kuwa aliposema ameupenda ulimwengu haimaanishi kuwa amependa kila kitu ulimwenguni, ikiwemo mifumo ya ulimwengu huu, hapana, kazi nyingi za ulimwengu ni mbovu, na hivyo hawezi kuzipenda, tena alizikemea (Yohana 7:7), bali aliwapenda walio-ulimwenguni (yaani sisi wanadamu). Bila kujali jinsia zetu, rangi zetu, jamii zetu, mataifa yetu, waovu, na wema, wote alitupenda sawa.

Ni upendo uliodhihirika katika hali yetu ya kupotea. Mahali ambapo tulikuwa hatuna tumaini lolote, hatuna uzima wowote wa milele ndani yetu, tumeteswa na ibilisi, yeye mwenyewe kwa mapenzi yake akatuhurumia, ndipo akatujia tena ili kutuokoa katika hali ya kifo na mauti tuliyokuwa nayo bure.

Na hivyo hakutupenda kwa mdogo tu, bali aliingia gharama. Na gharama yenyewe ni kumtoa mwanawe wa pekee Yesu Kristo, kuja katika mwili wa kibinadamu ili afe kama fidia ya dhambi zetu, ili sisi tupone kwa kifo chake yeye. Tupokee uzima wa milele.

Maana yake mtu yeyote ambaye ataukubali wokovu huo, ulioletwa kwa kufa na kufufuka kwake, basi uzima wa milele unaingia ndani yake. Ndio maana ya hilo andiko;

Yohana 3:16  Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Lakini ijapokuwa uzima umeletwa kwetu bure kwa gharama kubwa, wapo wengine hawaukubali, wakidhani kuwa wataweza kuushinda huu ulimwengu kwa nguvu zao, au kwa dini zao, au kwa matendo yao wenyewe.

Yohana 3:19  Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Je! Umeupokea uzima huu wa milele?. Ikiwa bado basi fungua moyo wako sasa, mwamini Yesu, mpokee kama ‘Bwana’ kwako, umfuate kwa moyo wako wote, uokoke, dunia hii ni ya kitambo tu, vilevile kesho yako huijui kama utakuwa hai au maiti. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi fungua hapa kwa msaada wa mwongozo wa sala ya wokovu >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini tunakwenda kanisani?

Maisha ya wokovu, hayatoshi tu kusema nimeokoka, halafu basi, nitamwabudu Mungu kivyangu. Hapana, Mungu hajaagiza hivyo, na kuna hatari kubwa ya kuenenda kwa namna hiyo, tutaona ni kwanini?

Ni sawa na mwanafunzi anayesema mimi sihitaji shule, nitajisomea tu nyumbani peke yangu, nitapata elimu yote, na maarifa yote kupitia vitabu na tafiti zangu. Ukweli ni kwamba si rahisi akipate anachokitafuta, kwasababu shuleni wapo waalimu atawahitaji wamfundishe vitu asivyovijua, atauliza maswali pale ambapo hajaelewa, wapo wanafunzi wenzake atajadiliana nao, zipo nidhamu atajifunza, ipo hamasa ataipata, tofauti na akiwa peke yake, na mambo mengine kadha wa kadha, .

Vivyo hivyo na maisha ya rohoni. Wokovu ni mtu binafsi, lakini kusimama katika wokovu na kuendelea mbele na kukua kunahitaji kanisa. Mungu aliagiza hivyo akasema, tusiache kukusanyika pamoja.

Waebrania 10:25  wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia

Akasema pia, heri walio wawili kuliko mmoja, kwasababu katika wingi, kuna kutiana nguvu ya kuendelea mbele.

Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Mkusanyikapo pamoja mtatiana moyo, mtaomba pamoja n.k.

Vilevile Kanisa la kwanza lilikuwa na desturi ya kukusanyika pamoja, kusikiliza fundisho la mitume, kumsifu Mungu na kumega mkate,  nyumba-nyumba kwa nyuma pamoja na Kutambuana.

Matendo 2:46  Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,

Lakini pia kusaidiana kimahitaji, Kutiana moyo  (Warumi 1:12), Kuonyana  (Wagalatia 5:13)

Lakini pia kufaidiana kwa karama za Roho Mtakatifu. Yaana kuruhusu uweza wa Mungu kutenda kazi katikati ya waamini.(Waefeso 4:11, 1Wakorintho 12) Mambo ambayo huwezi kuyapata ukiwa peke yako.

Hivyo huwezi kutenganisha maisha ya wokovu na kanisa. Kila mwamini ni lazima awe na mkusanyiko, kwa uthabiti wa maisha yake ya rohoni. Usiabudu kivyako vyako.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA

FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.

(Opens in a new browser tab)WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZE

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?(Opens in a new browser tab(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Huyu Mkeni shemeji yake Musa alikuwa ni mtu wa namna gani? (Waamuzi 1:16)

Jibu: Turejee…

Waamuzi 1:16 “Hao wana wa Mkeni, HUYO SHEMEJI YAKE MUSA, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao”.

Wakeni walikuwa ni jamii ya watu waliokuwa wanaishi katika nchi ya “Midiani” (karibu na jangwa la Sinai).. Kwa urefu kuhusiana na waMidiani fungua hapa >>Midiani ni nchi gani kwasasa?.

Miongoni mwa hawa waMidiani ndiko alikotokea Babamkwe wake Musa aliyeitwa Yethro au jina lingine Rueli.. Huyu Yethro/Reueli ndiye aliyemzaa  Sipora aliyekuwa mkewe Musa.

Na huyu Yethro alikuwa na watoto wengine wa kiume mbali na wale mabinti wake saba tunaowasoma katika Kutoka 2:16, na mmoja wa mtoto wake wa kiume aliitwa “Hobabu” ambaye sasa “ndiye shemeji yake Musa (maana yake kaka yake Sipora, mke wa Musa)”.

Huyu Hobabu shemeji yake Musa alikataa kusafiri na wana wa Israeli, kwani wana wa Israeli walimtumaini yeye awatangulie njia kwani aliifahamu Zaidi, lakini alikataa kama maandiko yanavyosema..

Lakini maandiko mbeleni yanaonyesha alikubali, kwani uzao wake ulionekana ndani ya nchi ya Ahadi

Hesabu 10: 28 “Ndivyo zilivyokuwa safari zao wana wa Israeli kwa majeshi: yao; nao wakasafiri kwenda mbele.

29 Kisha Musa akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli Mmidiani, mkwewe Musa, Sisi twasafiri kwenenda mahali ambapo Bwana amenena habari zake hivi, Nitawapa ninyi mahali hapo; uje pamoja nasi, nasi tutakufanyia mema; kwa kuwa Bwana ametamka mema juu ya Israeli.

30 Naye akamwambia, Siendi mimi; ila nitairudia nchi yangu mwenyewe, na kwa jamaa zangu mwenyewe.

31 Naye akamwambia, Usituache, tafadhali; kwa kuwa wewe wajua jinsi tutakavyopanga nyikani, nawe utakuwa kwetu badala ya macho.

32 Itakuwa, ukienda pamoja nasi, naam, itakuwa mema yo yote Bwana atakayotutendea sisi, tutakutendea wewe vivyo

34 Na wingu la Bwana lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.

35 Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee Bwana, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao”.

Kwa funzo refu kuhusiana na habari hii ya Hobabu na Musa fungua hapa >>>>Kwanini Musa amtake Hobabu na tayari kulikuwa na Wingu linalowaongoza?

Kwahiyo huyu Hobabu ndiye aliyekuwa shemeji yake Musa na wanawe (yaani watoto wake) ndio hao wanaotajwa hapo katika Waamuzi 1:6 na Waamuzi 4:11 na pia wanatajwa katika sehemu mbali mbali za biblia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kuiaua Nchi ni kufanya nini? (Waamuzi 18:2).

BWANA NITIE NGUVU TENA. (Waamuzi 16:28)

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Rudi Nyumbani

Print this post