Ndio Maandiko yanatuonyesha kuwa tutatambuana tukifika mbinguni. Ifahamike kuwa fahamu zetu au kumbukumbu zetu za hapa ulimwenguni hazitaondolewa kabisa, tufikapo mbinguni, kila pito tulipitialo, na kila jambo lililowekwa na Mungu sasa hapa duniani, lina sehemu kubwa ya fundisho la maisha yajayo. Hivyo maisha ya duniani yana thamani kama yalivyo tu maisha yatakayokuja. Ndio maana kabla ya kuingia kule ilitupaswa kwanza tupitie hapa.
Zipo sehemu kadha wa kadha katika maandiko zinatuthibitishia kuwa tutatambuana kule mbinguni.
Tunaona Bwana wetu Yesu Kristo alipofufuka na mwili mpya wa utukufu, aliweza kutambuliwa . Kwamfano siku ile ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena, akiwa pale kaburini alimtambua Bwana Yesu alipozungumza naye.
Yohana 20: 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).
Halikadhalika wakati ule Bwana Yesu anawachukua mitume wake watatu Petro, Yohana na Yakobo na kuwapeleka juu ya mlima ule mrefu, na kuwabadilikia sura, kama tunavyosoma watu wawili walitokea ambao ni Musa na Eliya.
Mitume waliweza kuwatambua ijapokuwa hawakuwahi kuwaona uso kwa uso hapo kabla.
Mathayo 17:3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
1Wakorintho 15:42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko
Mstari huo unatuonyesha kuwa hatutaondolewa uhalisia wetu Tutabakia kuwa sisi sisi., isipokuwa tutavikwa utukufu wa juu zaidi. Maana yake ni kuwa tutatambuana.
1Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
1Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana
hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Tutarejeshwa, na kuonana. Hivyo kwa mujibu wa vifungu hivyo katika ulimwengu ujao sote tutajuana na kufahamiana.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Print this post
Sheria ni agizo la shuruti linalotolewa na mamlaka kuu…, na KANUNI ni mwongozo au utaratibu maalumu unaotolewa kuhusiana na utekelezaji wa sheria iliyowekwa au agizo lililotolewa..
Kwamfano katika biblia kulikuwa na Sheria ya “kuishika Pasaka” lakini ilikuwepo pia kanuni (ambayo ni mwongozo wa namna ya kuiadhimisha hiyo siku), kwamba ni lazima kwanza iwe siku ya 14 ya mwezi wa kwanza wa kalenda ya kiyahudi, na pia siku hiyo ni lazima achinjwe mwana kondoo na kumwoka motoni na aliwe pamoja na mboga zenye uchungu n.k (Soma Kutoka 12:1-12).
Sasa huo mwongozo wote wa jinsi ya kuiadhimisha hiyo siku ndio unaoitwa Kanuni, lakini sheria ni hiyo moja tu kwamba Waishike Pasaka..
Hesabu 9:14 “Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa Bwana; kama HIYO SHERIA YA PASAKA ILIVYO, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; MTAKUWA NA SHERIA MOJA, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi”.
Katika biblia kila Amri au sheria ilikuwa na Kanuni zake na hukumu zake.
Tunayo sheria na amri ya Kristo pia ambayo ni UPENDO, lakini huu upendo unao kanuni…ni lazima tuzitafute kanuni za upendo na tuzijue.
Isaya 28:13 “Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo”.
Maran atha!
Mafundisho mengine:
Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?
Nini tofauti kati ya kileo na divai?
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Je! kuna mwanamke mwingine aliyempaka Bwana marhamu (manukato) zaidi ya Mariamu ndugu yake Lazaro?
Jibu: Neno Utakatifu linatokana na Neno “utakaso”.. kitu lilichotakasika kinaitwa “kitakatifu”.. na kitu kilichotakasika/takata maana yake hakina uchafu.
Kwahiyo utakatifu kwa tafsiri rahisi maana yake ni “kuwa safi, (kutokuwa na uchafu)”.. Mtu anaweza kuwa msafi (mtakatifu) mwilini na rohoni.
Sasa kikawaida kitu chochote kinapokuwa safi, huwa kinatoa Mng’ao unaopendeza.. sasa ule mng’ao unaotafsiri usafi wa kitu kile ndio unaoitwa UTUKUFU, kwamfano dhahabu inaposafishwa na kuwa safi huwa inatoa mng’ao mzuri wa kipekee, sasa ule mng’ao ndio utukufu wa ile dhahabu au kito, na vitu vingine vyote ni hivyo hivyo.
Hali kadhalika mtu aliyetakaswa dhambi zake kwa damu ya YESU, na yeye mwenyewe kujilinda na kujitenga na uchafu wote wa rohoni na mwilini, basi mtu huyo ni mtakatifu na anao utukufu, ambao ni NURU inayong’aa, ambayo shetani na mapepo yake hayawezi kustahimili mwako wake.
Lakini zaidi sana MUNGU wetu aliyetuumba ndiye mwenye utukufu MKUU, ambao huo unatokana UTAKATIFU alionao, uzidio viumbe vyake vyote.. Mng’ao wa utukufu wake hata malaika wanainama mbele zake na kujifunika kwa mbawa zao, na utukufu wake unang’aa mpaka duniani.
Isaya 6:1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. 2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. 3 WAKAITANA, KILA MMOJA NA MWENZAKE, WAKISEMA, MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU, NI BWANA WA MAJESHI; DUNIA YOTE IMEJAA UTUKUFU WAKE”.
Isaya 6:1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
3 WAKAITANA, KILA MMOJA NA MWENZAKE, WAKISEMA, MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU, NI BWANA WA MAJESHI; DUNIA YOTE IMEJAA UTUKUFU WAKE”.
Naam nasi tuliompokea YESU ni lazima tufanane naye, na hatuwezi kuwa na utukufu bila kuwa watakatifu, na hatuwezi kukosa utukufu tukiwa watakatifu, na kuwa mtakatifu duniani inawezekana..
Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.
Bwana atusaidie.
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
NYUMBANI MWA BABA YANGU MNA MAKAO MENGI.
YESU NI ALFA NA OMEGA .
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU
Katika agano la kale dhambi ilitokea na kuhesabiwa katika maeneo mbalimbali.
Kwamfano
> Kulikuwa na makosa ya jamii nzima. Yaani taifa zima kuasi. (Kutoka 32,)
> Makosa ya mtu binafsi. Mfano kutenda uzinzi, Wizi, uuaji n.k.
> Makosa ya kuwatendea vibaya wanyonge: Mfano maskini, wageni, mayatima na wajane (Amosi 5:11-12),
> Makosa ya kukaidi sherehe za kidini (Walawi 11-15),
> Makosa ya kuvunja maagano (Yeremia 17:21-23),
> Makosa ya kuabudu miungu mingine (sanamu).
Lakini pia kulikuwa na aina nyingine mbili za makosa..
> Aina ya kwanza ni makosa ya kukusudia
> Aina pili ni yale ya kutokusudia.
Ikiwa mtu alitenda dhambi kwa kutojua, alihesabika kuwa ni dhambi, hivyo alilazimika atoe sadaka ya dhambi. Lakini kama alitenda dhambi ya makusudi kinyume na mwenzake, ili kuondoa kosa Ilipasa atoe sadaka ya hatia.
Aina ya sadaka hizi zinaelezwa kwa urefu kwenye kitabu cha Walawi 4:1 – 5:13
Dhambi za kutokusudia Mfano wake ilikuwa ni kama kuvunja amri bila kujua au kutojua Sheria ya vitu safi au najisi ilivyo. Hivyo mtu alijikuta tu anatenda kwa kukosa ufahamu.
Walawi 4:1-3
[1]BWANA akanena na Musa, na kumwambia, [2]Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; [3]kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.
[1]BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
[2]Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo;
[3]kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.
Dhambi za kukusudia ni zote ambazo zilitendwa kinyume na mtu mwingine au mambo matukufu mfano wa hizi ni kama kuiba, kusema uongo, viapo Vya uongo, hivyo iliambatana pia na kutoa fidia ya vitu hivyo.
Sio tu kusamehewa bali pia kuweka mambo sawasawa kwa kulipia fidia.
Mfano wa tendo hili, tunaona kwa Zakayo, alipofikiwa na wokovu, alitubu kwa kurejesha mara nne ya vyote alivyodhulumu. (Luka 19:8) huo ni mfano wa sadaka ya hatia.
Katika agano jipya dhambi Zote Za kukusudia na kutokusudia na nyingine zote zinaondolewa na sadaka moja tu ya daima nayo ni DAMU YA YESU (Waebr 9:26, Isaya 53:10, 1Petro 2:24). Hiyo tu ndio inafuta hatia zote.
Lakini pamoja na hayo, sadaka hizi hutukumbusha pia kila tuombapo rehema, (kwa unajisi tunaojitia kila siku), hatuna budi kuomba sio tu kwa dhambi tuzijuazo bali pia kwa zile tusizozijua.
Kwasasa dhambi tusizokusudia ni kama vile kumkwaza mwenzako bila kufahamu, Kutowaombea wengine(2Samweli 12:23), kuwaza vibaya, kutotumiza nadhiri zetu, au wajibu wetu N.k.
Je umesamehewa na kuondolewa dhambi zako? Kama ni la! basi wakati ndio sasa, unapomgeukia Bwana Yesu, anakuondolea kumbukumbu lote la makosa. Hivyo fungua hapa kwa msaada huo wa kumpokea yeye >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Nini maana ya dhabihu na matoleo hukutaka? (Waebrania 10:5).
Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?
Jibu: Kulingana na biblia UBATIZO unapaswa ufanyike mara moja tu katika kipindi chote cha maisha ya mtu, ikiwa mtu huyo atakuwa ametimiza vigezo hivi viwili.
1. KABLA YA KUBATIZWA AWE AMEELEWA MAANA YA UBATIZO NA KUTUBU:
Maana ya Ubatizo ni kuzika utu wa kale na kufufuka katika utu upya, hivyo ikiwa mtu ameelewa kuwa lengo la ubatizo ni kuacha maisha ya kale na kuanza maisha mapya katika KRISTO, basi hiko ni kigezo cha kwanza cha Uthabiti wa Ubatizo wake,
Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu TULIBATIZWA KATIKA MAUTI YAKE? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 MKIJUA NENO HILI, YA KUWA UTU WETU WA KALE ULISULIBISHWA PAMOJA NAYE, ILI MWILI WA DHAMBI UBATILIKE, TUSITUMIKIE DHAMBI TENA”.
Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu TULIBATIZWA KATIKA MAUTI YAKE?
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
6 MKIJUA NENO HILI, YA KUWA UTU WETU WA KALE ULISULIBISHWA PAMOJA NAYE, ILI MWILI WA DHAMBI UBATILIKE, TUSITUMIKIE DHAMBI TENA”.
Na kwa kigezo hiki, watoto hawabatizwi kwani wanakuwa bado hawajatambua maana ya maisha mapya katika KRISTO ni nini?, watoto wanawekewa mikono tu na sio kubatizwa….Kwahiyo kama mtu alibatizwa utotoni hana budi kubatizwa tena upya.
2. NI AINA GANI YA UBATIZO ALIOBATIZWA.
Hiki ni kigezo cha Pili, kama mtu alibatizwa sawasawa na maandiko kwa maji mengi na kwa jina la Mwokozi YESU sawasawa na Mathayo 28:19 na Matendo 2:38 na si kwa maji machache na kwa majina ya watu wengine, basi huyo mtu hahitaji kubatizwa tena.
Lakini kama alibatizwa kwa ubatizo wa maji machache hata kama alishatubu dhambi zake, ni lazima abatizwe upya mara nyingine, kwasababu katika biblia hakuna mahali popote panaonyesha mtu yeyote amebatizwa kwa kunyunyiziwa, kwasababu maana tu yenyewe ya ubatizo ni kuzamisha/kuzika
Vile vile kama mtu alibatizwa kwa ubatizo wa Yohana, au wa mtu Fulani tofauti na YESU hana budi kubatizwa upya.. Biblia inatuonyesha watu waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana kurudia ubatizo wao baada ya kukutana na injili ya ubatizo wa jina la YESU.
Matendo 19:3 “Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu 5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”
Matendo 19:3 “Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu
5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”
Hapa tunaona hawa watu walibatizwa upya baada ya kusikia kuwa ubatizo sahihi ni wa Bwana YESU sio tena wa Yohana..
Kwahiyo na sisi hatuna budi kujihakika kama kweli tumebatizwa ubatizo sahihi, kama tumebatizwa ubatizo sahihi kulingana na vigezo hivyo hapo juu basi hatuna haja ya kubatizwa upya, Huo ubatizo unatosha, kinachobakia ni kuendelea kuishindania Imani kwa kujilinda na ulimwengu na kutimiza wito ulioitiwa..
Lakini kama ubatizo wetu haujakamilishwa na Neno la MUNGU, hatuna budi kurudia ubatizo kwani si dhambi.
Na kumbuka matokeo ya ubatizo sahihi ni kumfanya mtu asimame imara katika IMANI, wengi waliobatizwa ubatizo sahihi baada ya toba kamili na uelewa kamili juu ya ubatizo ni ngumu kuishi tena maisha ya dhambi baada ya hapo, bali wanakuwa wanasimama maisha yao yote, kwani ubatizo unawaongezea Neema ya ziada ya kuweza kuishi bila kurudi rudi nyuma.
Mtu aliyebatizwa kwa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU, halafu akarudi tena kwenye maisha ya dhambi kama mwanzo, basi kuna shida katika KUAMINI KWAKE tangu mwanzo, huenda hakuelewa maana ya ubatizo kabla ya kubatizwa, na hivyo hakutubu kisawasawa, lakini kama angetubu kisawasawa na akabatizwa asingeweza kurudi tena alikotoka, hiyo ndio nguvu ya ubatizo.
Ikiwa bado hujabatizwa na unahitaji kubatizwa basi wasiliana nasi kwa namba hizi, 0789001312, tutakupa mwongozo sahihi wa kujua maana ya ubatizo na hatimaye kukubatiza ikiwa utakuwa maeneo karibu na tulipo, na ubatizo ni bure.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.
Ubatizo wa moto ni upi?
Je ni lazima kupitia mafundisho ya muda mrefu kabla ya kubatizwa?
Jibu: Hakuna kosa lolote Raheli alilolifanya, lililomfanya afungwe tumbo asizae.. Lakini tukisoma maandiko twaweza kuona sababu kama mbili zilizopelekea yeye kufungwa tumbo na MUNGU mwenyewe.
1. KUMNYENYEKEZA RAHELI na KUMTIA NGUVU LEA.
Tunasoma kuwa Lea ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzaliwa, na Yakobo alimpenda zaidi Raheli kuliko Lea, (na jambo hilo lilikuwa wazi linaonekana) kwahiyo labda ingetokea Yakobo aliyebeba ahadi za MUNGU kumuoa Raheli, na tena akazaa naye mtoto wa ahadi, huenda jambo hilo lingemfanya Raheli kujivuna/kujigamba mbele ya Lea dada yake, na hivyo Lea angekuwa duni/mnyonge mbele ya mdogo wake, kwahiyo MUNGU akamfunga tumbo.
Mwanzo 29:28 “Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe. 29 Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. 30 Akaingia kwa Raheli naye, AKAMPENDA RAHELI KULIKO LEA, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine 31 Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai. 32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. 33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. 34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. 35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa”.
Mwanzo 29:28 “Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe.
29 Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake.
30 Akaingia kwa Raheli naye, AKAMPENDA RAHELI KULIKO LEA, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine
31 Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.
32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.
33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa”.
2. KUKITHAMINISHA KITAKACHOZALIWA BAADAYE.
Hii ni sababu ya pili ya Raheli kufungwa tumbo: Tunasoma ijapokuwa Raheli alifungwa tumbo muda mrefu, lakini ulifika wakati akazaa, na mwana aliyemzaa alikuwa wa tofauti na wale wengine 10 waliotangulia, kwani ndiye aliyekuwa YUSUFU, ambaye alikuja kuwa Mkuu zaidi ya ndugu zake wote, na tena Mkuu juu ya nchi yote ya Misri, baada ya Farao.
Ikifunua kuwa si kila kinachochelewa kina laana!.. Vingi vinavyochelewa ni kwasababu ya Utukufu wake, hivyo usimwone mtu kachelewa kupata mimba ukamdharau!.. Hujui atakayekuja kumzaa ni nani!.. Vile vile usihuzunike unapoona unachelewa kupata mtoto, kwani vizuri na vya thamani, vina gharama, na gharama yenyewe yaweza kuwa fedheha, matusi, kejeli na masimango.. Lakini vinavyokuja baada ya gharama hizo vinakuwa ni vizuri, endapo tu utazidi kusimama katika imani, haijalishi muda, vitatokea tu!.
Wagalatia 4:27 “Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume”. Bwana akubariki.
Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.
Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)
Raheli aliwalilia vipi watoto wake?
Zeri ya Gileadi ni nini?
Tunguja ni nini katika biblia? (Mwanzo 30:14).
WhatsApp
Swali: Bwana YESU alisema pepo anapomtoka mtu na baadaye akirudi na kukuta nyumba yake imefagiliwa na kupambwa huenda kuchukua pepo wengine saba,.. maaa yake nini kusafishwa na kupambwa?.. je mapepo wanapenda sehemu safi?
Jibu: Awali ya yote tuisome mistari hiyo.
Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, 25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka. 26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
Sasa kabla ya kujua nini maana ya “kufagia na kupambwa” hebu tuelewe kwanza maana ya nyumba kiroho..
Maandiko yanasema Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu..
1 Wakorintho 6.19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
1 Wakorintho 6.19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
Soma pia 1Wakorintho 3:16 utaona jambo hilo hilo..
Sasa kama miili yetu imekusudiwa iwe Hekalu/nyumba ya Roho Mtakatifu, maana yake ni kwamba isipokaliwa na Roho Mtakatifu basi itakaliwa na roho chafu za mapepo, maana yake badala ya mwili kuwa Nyumba ya Roho Mtakatifu, sasa inakuwa ni nyumba ya mapepo.
Hivyo mpaka hapo tumeshaelewa kuwa Nyumba inayozungumziwa hapo katika Luka 11:25-26, si nyingine zaidi ya miili yetu.
Sasa swali la pili: Nini maana ya kupambwa na kufagiliwa.
Hebu tena tutumie maandiko tujue mapambo ya nyumba ya Mungu (yaani miili yetu) ni yapi, na mapambo ya mapepo ni yapi.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
Angalia mstari wa tatu (3) anasema.. Kujipamba kwenu KUSIWE!, Zingatia hilo neno KUSIWE!!.. Maana yake ni kwamba mapambo yake ni kwamba mapambo yafuatayo si ya ki Mungu bali ni ya Ibilisi, ndio maana anasema hapo KUSIWE!.. Sasa hebu tuendelee tuangalie hayo mapambo..
…”Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI..”
Oo kumbe! kuweka wigi, kuvalia mavazi (ya kikahaba), na kuvaa dhahabu masikioni na shingoni na vikuku miguuni na mikononi ni mapambo ya mapepo, na tena tumeshaona kuwa “nyumba” tafsiri yake kiroho ni “miili yetu”, hivyo tunapoweka hereni masikioni, wigi kichwani, cheni shingoni na vikuku miguuni, tafsiri yake ni kwamba nyumba zetu (yaani miili yetu) tumeipamba kwa mapambo ya kipepo, ambayo yale mapepo yakiona yanafurahi na kwenda kutafuta pepo wengine saba, na kurudi kumwingia mtu.. Hii ni ajabu sana!.
Na ndio maana wengi (wanaume na wanawake) wanaopamba miili yao na kuvaa kikahaba wanakuwa wanasumbuliwa na mapepo na ndoto mbaya!, kwanini?..kwasababu miili yao ni nyumba iliyofagiliwa na kupambwa..
Sasa utauliza kufagiliwa ni kufanya nini?…Kufagiliwa ni maandalizi ya mapambo!..Maandalizi yote ya kiroho na kimwili kabla ya mtu kujitia mapambo ya nje ni “kufagia”..
Lakini hebu tuangalie mapambo ya ki MUNGU ni yapi!.. Tuendelee na mistari ile..
“Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu”.
“Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu”.
Bali anasema mapambo yetu yawe Utu wa moyoni, yaani Roho ya Upole, na utulivu (kwa ufupi utakatifu).Je! mama, dada, au kaka ni mapambo gani unayo?..ya nje au ya ndani??.. ni kweli utaonekana wa kisasa, unayekwenda na wakati, lakini fahamu kuwa mapambo hayo ndio mapepo wanayoyaangalia.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10 atusaidie.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Jibu: Turejee mistari hiyo..
Kutoka 15:24 “Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema,Tunywe nini? 25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO”
Kutoka 15:24 “Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema,Tunywe nini?
25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO”
Kuonja kunakozungumziwa hapo ni kuonja kiroho na si kimwili, siku zote mtu anayeonja kitu, lengo lake ni kukipima ubora wake, kilingana na vigezo anavyovitaka.
Na kiroho MUNGU anatuonja sisi mara kwa mara kwa kuangalia matendo yetu kama tupo sawa mbele zake…
Kwamfano utaona Bwana YESU anatumia lugha hiyo ya kiroho katika kitabu cha Ufunuo kuyapima matendo yetu..
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”
Umeona hapa?…matendo yetu yanapimwa kwa kinywa cha Bwana..kama tu Moto mbele zake basi tuna heri, lakini kama tu baridi au vuguvugu ni Ole!.
Kwahiyo hata kipindi wana wa Israeli wakiwa wanatoka Misri kuelekea nchi ya ahadi.. Mungu alikuwa anawaonja matendo yao…
Na kuna kipindi aliwatapika walipomjaribu na kumnun’unikia.
Lakini si tu Bwana akiyekuwa anawaonja, bali pia aliwaambia kuwa hiyo nchi wanayoiendea itawaonja matendo yao, na kama yakiwa mabaya itawatapika, kwa kuwa pia iliwatapika wenyeji waliokuwa wanaiishi kutokana na mateendo yao maovu.
Walawi 18:25 “na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi YATAPIKA wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Walawi 18:25 “na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi YATAPIKA wenyeji wake na kuwatoa.
26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ili kwamba hiyo nchi ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.
Je umempokea YESU?.
Je wewe ni moto?, au baridi au una uvuguvugu?…Uvuguvugu maana yake ni kuwa upo mguu mmoja nje!…mguu mmoja ndani!, leo unaenda kanisani kesho unaenda Bar, leo unatoa sadaka kesho unabeti, leo unavaa nguo ya sitara kesho nguo ya aibu..hapo Bwana amesema atatapika mtu wa namna hiyo.
Bwana atusaidie tumtii ili tusiwe miongoni mwa watakaotapikwa.
Maran atha!.
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
JIBU: Katika vifungu hivyo biblia inaeleza kwa ukubwa sifa zetu sisi tuliomwamini Yesu Kristo, jinsi zilivyo kuu, anasema sisi ni mzao mteule, na pia watu wa milki ya Mungu. Lakini sifa nyingine ndio hiyo ya ukuhani wa kifalme.
Angeweza kusema sisi ni ukuhani wa kisomi, au ukuhani wa kiroho, au ukuhani ki-mbingu, au ukuhani wa kitajiri. Lakini anatumia Neno ukuhani wa kifalme. Ikiwa na maana kuwa tunao ukuhani lakini si ukuhani tu bali wenye asili ya kifalme.
Sifa kuu ya kuhani, ni kuweza kumkaribia Mungu kusema naye, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wengi. Mfano wa Haruni na uzao wake. Tunaona hawa tu ndio waliopewa neema ya kuweza kumkaribia Mungu katika kiti chake che rehema, kuzungumza naye na kuomba rehemu kwa taifa zima. Wengine wote walikaa nje ya hema.
Lakini pia sifa ya mfalme ni uweza, mamlaka, nguvu, na utajiri. Mfalme anatawala, mfalme ana nguvu ya kijeshi, mfalme ni lazima awe tajiri na mwenye utiisho.
Sasa tukirudi kibiblia, Haruni na walawi wote ambao waliopewa sifa ya kikuhani, hawakuwa na ukuhani wa kifalme ndani yao. Waliishia tu kukaa hemani, na sio ni makuhani na wakati huo huo ni wafalme, lakini pia wafalme wengi (Mfano wa Daudi, Sulemani n.k.)hawakuwa na ukuhani pia ndani yao.. Hivyo waliishia tu kutawala lakini sio kuingia hekaluni kuvukiza uvumba. Alitokea mfalme mmoja kujaribu kufanya kazi hizo mbili kwa wakati mmoja, aliishia kupata ukoma kwasababu hakukuwahi kutokea mtu mwenye uwezo huo wa kutembea katika vyeo vyote viwili kwa wakati mmoja (2Nyakati 26:16-21).
Lakini yupo aliyetabiriwa na manabii kuwa atakuwa kuhani mkuu lakini pia mfalme. Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo. (Waebrania 7:11-17), Yeye alikuwa kuhani lakini pia alitokea katika kabila la kifalme la Yuda, kwa jinsi ya mwili.
Na mpaka sasa anatawala kama kuhani mkuu wetu, lakini pia mfalme wetu. Amewazidi makuhani wote, amewazidi wafalme wote.
Hivyo na sisi tuliozaliwa na yeye, tunarithi vyote alivyonavyo, maandiko yanasema hivyo (1Petro 1:3-4), Tunafanyika sio tu makuhani, ambao tunamkaribia Mungu kusema naye ana kwa ana, na kuwapatanisha wengine na yeye, lakini pia tunafanyika wafalme wenye mamlaka yote, na nguvu, na utajiri.
Sisi tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka, na nguvu zote za Yule mwovu, mamlaka ya kupooza kila aina ya magonjwa na madhaifu, mamlaka ya kufungua na kufunga jambo lolote. Vilevile tumepewa na utajiri wote wa hekima na maarifa ndani ya Yesu Kristo (Waefeso 1:3).
Na zaidi mamlaka ya ufalme tuliyonayo itakuja kudhihirika vema mbeleni kwenye utawala wa miaka 1000 wa amani wa Yesu Kristo duniani. Jinsi tutakavyo milika na kutawala na yeye kama wafalme, na yeye akiwa kama mfalme wa wafalme. (Ufunuo 19:16)
Ufunuo 5:10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Je!, umeipokea neema hii?
Ni nini unachosubiri usimpe Kristo maisha yako? Tafakari ahadi kubwa namna hii unapewa bure, ni nani anayeweza kufanya hivyo? Saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa na Mungu ndio huu, okoka leo, usamehewe dhambi zako, jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima.
ikiwa upo tayari kumpokea Yesu, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.
HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.
Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?
JIBU: Swali la kwanza la kujiuliza, je! mkristo ni mtu gani?..Mkristo ni mtu aliyemwamini,Yesu Kristo, kisha akapokea msamaha wa dhambi,kwa toba ya kweli, ubatizo na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu.
Mtu wa namna hiyo anakuwa na Kristo ndani yake. Na mtu mwenye Kristo Hawezi kuwa na mapepo, kwasababu Yesu hana pepo.
Vifungu hivi vinatuthibitishia kuwa hilo jambo haliwezekani;
1 Yohana 4:4
[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
2 Wakorintho 6:14
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Kuonyesha kuwa giza na nuru haviwezi kuwepo sehemu moja, wakati mmoja.
Lakini swali linakuja inakuwaje kuna baadhi ya watu waliokoka wanaonekana kuwa na mapepo ndani yao?
Kama tulivyoona mkristo hawezi kuwa na mapepo, lakini ni vema kufahamu kuwa kuna tofauti kati ya kukaliwa na mapepo, na kushambuliwa na kipepo.
Mtu aliyeokoka hawezi kukaliwa na mapepo, lakini anaweza akashambuliwa au kusumbuliwa na uwepo wa mapepo, hicho ndicho kinachoweza kumtokea, lakini sio kwamba ana mapepo ndani yake.
Sababu zinazoweza mpelekea asumbuliwe nayo, ni hizi kuu tatu;
Tukianza na sababu ya kwanza.
Kukosa kujua nafasi na mamlaka uliyo nayo ndani ya Kristo, shetani anaweza kukusumbua kwelikweli. Na wakati mwingine kukutesa. mapepo yanaweza kuwasumbua watu kifikra na kwa kuwawekea mawazo machafu akilini mwao, kuwashitaki, kwa kuwatupia ndoto mbaya, au kuwakaba usiku, au kuwaletea majaribu mbalimbali, lakini huyu mtu akijua kuwa ameshakabidhiwa mamlaka yote ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule mwovu,(Luka 9:1), akaitumia vema, shetani atamwogopa kumsogelea kwasababu anajua nguvu ya kimamlaka iliyo ndani yake ni thabiti haitoki mdomoni bali inasukumwa na ufalme wa Mungu ulio nyuma yake.. Ni sawa na mtu anayetoa amri kwa kinywa chake mwenyewe na yule anayetoa kwa agizo la raisi watu watamwogopa yule anayetoa kwa mamlaka aliyopewa na raisi. Hivyo ni muhimu sana kuitafakari na kuiamini mamlaka uliyopewa na Kristo ndani yako ili hayo maroho unapoona dalili ya kutaka kukusumbua unatamka jina la Yesu mara moja tu yanatetemeka na kukimbia. Mamlaka hiyo amepewa mkristo yoyote aliyeokoka, haijaishi ni mchanga au mkomavu.
Ukiokolewa, kwasababu ya kutoondoka mara moja kwa baadhi ya tabia, au msingi au mienendo ya kale, hivyo tabia hizo mara nyingine zinakuwa ni upenyo wa uwepo wa kipepo kuzunguka zunguka karibu yako. Vitu vichanga sikuzote hushambulika kirahisi, unyasi ukiwa mdogo hutikiswa sana na upepo, Ndio maana ni lazima uanze kuukulia wokovu, kwa kujifunza Neno, kujizoesha utakatifu, maombi, ibada, mambo ambayo adui hapendi kwasababu ni kama moto kwao. Mtu asipokuwa mkristo wa vitendo, sikuzote atasumbuliwa na roho za kidunia, na hatimaye atajiona kama ni ana mapepo kabisa, na akiendelea kuishi hivyo, mpaka kurudi nyuma atakufa kiroho, na Roho Mtakatifu kuondoka ndani yake, na mapepo ndio yatapata nafasi ya kumtawala kabisa. (2Petro 1:5-10)
Mtu aliyeokoka, akaanza kutenda dhambi za makusudi, anarudia yale yale kila siku, jambo hilo ni upenyo mwingine wa mapepo kumsumbua, kwasababu anakuwa ameyapa nafasi, na maandiko yanasema tumsimpe ibilisi nafasi. (Waefeso 4:27).
Kwamfano umeacha ulevi, baada ya kuokoka, na umekuwa hivyo kwa muda mrefu sasa, halafu ghafla unaanza tena kuwa mlevi, Mungu anakuonya uache hutaki, unaendelea kunywa pombe..kitendo hicho kinaweza kukupelekea kusumbuliwa sana na mapepo. Mfano tu wa Yule ambaye anatawaliwa nayo.
Mathayo 12:43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika,asipate. 44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Mathayo 12:43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika,asipate.
44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na
kupambwa.
45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye
mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Hivyo kwa hitimisho, ni kuwa mtu aliyeokoka, hawezi kukaliwa na mapepo, yaani kutawaliwa au kupagawishwa, au kuendeshwa nayo.. Isipokuwa anaweza kushambuliwa, kusababishiwa madhara, lakini kuvamiwa na uwepo wao. Ndio maana tumeambiwa tuvae silaha zote za haki, ili tuweze kumpinga shetani (Waefeso 6:10). Kwa kulijua Neno, utakatifu, maombi, na ibada.
Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.
Je mtu anaweza akawa hajaokoka akaombea mtu na Pepo likamtoka,