Title October 2019

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Ikiwa imetokea umekufa ghafla, muda huo huo utawaona malaika wa Mungu wamesimama pembezoni mwako, ili kukuchukua na kukupeleka mahali panapokustahili, Sasa ikiwa wewe ni mtakatifu (Yaani ulipokuwa hapa duniani uliishi kwa KRISTO, na kujitenga na uovu) basi malaika hao wanakuchukua kwa furaha na kwa shangwe na kwa nyimbo na kukupeleka moja kwa moja sehemu inayotwa Peponi wengine wanaiita Paradiso (Luka 23:43)..

Bwana Yesu alitumia ule mfano wa Lazaro kueleza picha halisi ya kinachomtokea mtakatifu mara baada ya kufa..

Luka 16:22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa”.

Kifuani mwa Ibrahimu ndio peponi kwenyewe kwa lugha nyingine, ni mahali pazuri sana, ni sehemu ya mbingu japo sio kule mbinguni kabisa Mungu alipo, ni sehemu ya kitambo tu ambapo watakatifu wanahifadhiwa wakisubiria siku ile ya Unyakuo ifike warudi makaburini kuichukua miili yao, na kwa pamoja sasa waungane na wale watatakatifu ambao watakuwa hai wakati huo, kisha wote kwa pamoja wapewe miili ya utukufu waende kumlaki Bwana Yesu mawinguni, baada ya hapo safari ya mbinguni moja kwa moja inaanza, kwenda kula karamu ya mwana-kondoo kwa Baba mahali ambapo hakuna hata mmoja wetu amefika kwasasa, huko ndipo tutakapomwona Mungu wetu uso kwa uso..tutaona vitu ambavyo hatujawahi kuona, wala kusikia.

Lakini kinyume chake ni nini kinatokea baada ya kifo kwa mwenye dhambi? ikiwa amekufa akiwa mlevi, mzinzi, muuaji, mtukanaji, yaani kwa ufupi yupo nje ya Kristo, basi wale malaika ambao Mungu aliwaandaa kwa kazi ya kuyatenga magugu na ngano (waovu na wema) wanafanya kazi yao hapo,..

Mathayo 13:49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

50 na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Kumbuka biblia inaposema Mwisho wa dunia inamaanisha mwisho wa aina mbili, aina ya kwanza ni ule mtu anapokufa ndio unakuwa mwisho wake wa dunia, vilevile siku ile ya kiama ambapo dunia yote itahukumiwa nayo pia inaitwa mwisho wa dunia, vyote viwili malaika watafanya kazi hiyo..

Hivyo basi mtu kama ni mwovu, akifa bila kupoteza muda atachukuliwa na malaika hawa na kwenda kutupwa mahali panapoitwa JEHANAMU, huku Jehanamu ni mahali tofauti kabisa na ZIWA LA MOTO, Jehanamu ni kama mahabusu, watu waovu wanahifadhiwa kwa muda tu, wakisubiria hukumu ya mwisho, kisha ndio wakatupwe kwenye lile ziwa la moto siku ile ya mwisho, kama hujafahamu bado Jehanum ni mahali pa namna gani utanitumia ujumbe inbox nikutumie maelezo yake..

Sasa huko ni mahali pa mateso sana, sehemu mbaya, ndio kule Yule tajiri wa Lazaro alipopelekwa

Luka 16.22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.

Mtu huyu atakaa huko huko katika mateso hayo muda wote huo akisubiria ufufuo ambao utakuja mara baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha, ndipo atakaposimama sasa mbele ya kiti cha hukumu cha mwana-kondoo kisha atahukumiwa kutokana na maovu yake yote, na kisha kutupwa katika lile ziwa la moto mahali ambapo pana mateso makali sana ya moto usiozimika…Na Baada ya hapo habari yake itakuwa imeisha.(Ufunuo 20:11-15)

Hivyo usidanganyike kuwa baada ya kifo kutakuwa na nafasi ya pili, hapana biblia imeweka wazi kabisa katika..Waebrania 9:27 “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”;

Ukishakufa leo, shughuli zote za hukumu zinaendelea juu yako, hakuna maisha tena hapo..

Swali linakuja je! Na wewe umejiwekaje tayari ikiwa siku hiyo imekukuta kwa ghafla?, Je! Unao uhakika wa kusikia sauti nzuri za malaika wakikuimbia nyimbo za ushindi wakikunyanyua na kukupeleka kule peponi walipo watakatifu wengine au kuwaona wakija katika hasira kali kukukokota ili kwenda kukutupa Jehanum?. Jibu lipo moyoni mwako,

Na mara nyingine malaika hawa huwa wanawatokea watu hata kabla hawajakata roho vizuri, japo si mara zote, Na ndio maana utaona muda mfupi kabla hawajafa, wengine wakiwa na amani sana, wengine wakitabasamu, wengine wakisema wanaona malaika karibu yao wakizungumza nao, n.k. ukiona hivyo ujue hawa hatma yao ni njema, lakini wapo wengine pia utaona kabla hawajafa muda mchache wanahangaika sana, au wanateseka, wengine wanakufa wakiwa na mwonekano kama vile wamenyongwa, au wameuawa n.k. Ujue kuwa malaika hao wanawachukua kwa hasira na kuwapeleka kule Jehanamu.

Je! Wewe utakuwa upande gani,?Jibu unalo badilika, tengeneza maisha yako kwa Bwana YESU sasa, ikiwa bado unasua sua, kwasababu hiyo kesho unayoisumbukia pengine inaweza isiwe yako. Na baada ya kufa ni hukumu

Ubarikiwe.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

SIKU YA HUKUMU ITAKUWAJE?

UNYAKUO.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

Shalom! Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima!

Karibu tujifunze Biblia, kwa Neema Bwana aliyotupa.

Biblia inasema katika Wagalatia 1:7b

“…. lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.

8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe”.

Maneno hayo aliyazungumza Mtume Paulo kwa Uweza wa Roho, na Roho Mtakatifu mwenyewe akayatia Muhuri yafae kwaajili ya kutuonya na kututahadharisha sisi watu wa vizazi vyote. Ni maneno ambayo huwezi kuamini kama yapo kwenye Biblia Takatifu hususani katika agano jipya, lakini yapo!

Kuna hatari kubwa sana ya kuigeuza Injili ya Yesu Kristo kwa makusudi..ili tu mtu upendwe, au upate wafuasi wengi, au ujulikane…Kufundisha Injili nyingine tofauti na hiyo iliyohubiriwa na Mitume ndio “kuongeza Neno la Mungu” kunakozungumziwa katika biblia….ambapo Biblia imesema mtu wa namna hiyo ataongezewa mapigo katika siku ile.

Ufunuo 22: 18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki”.

Biblia inaposema wazi kuwa waasherati na waabudu sanamu pamoja na walevi watakwenda kwenye ziwa la moto, na wewe unasema “si kweli acha kuhukumu”..unaposema biblia imeruhusu pombe!! hapo ni sawa na unahubiri Injili nyingine tofauti na ile Iliyohubiriwa na hivyo “Umelaaniwa”

1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”

Biblia inaposema wazi katika Agano jipya kwamba Wanawake wavae mavazi ya kujisitiri, si kwa kusuka nywele!..

1Timotheo 2: 9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.

Wewe unasema “Mungu haangalii mavazi anaangalia roho” sentensi ambayo haipo kwenye Biblia nzima…uliisikia kutoka kwa mtu fulani asiyefahamu maandiko nawe ukai-copy bila kuchunguza imetoka wapi!…..fahamu kuwa unahubiri Injili nyingine ambayo haipo kwenye Biblia…Na hakuna mtu yoyote anakuhukumu hapo..bali biblia yenyewe ndio inayokuhukumu kwamba UMELAANIWA!

Biblia inaposema katika Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”. Wewe unasema kuwa ubatizo haujalishi sana! Si lazima ubatizwe, Hapo unahubiri Injili ya Laana!

Pengine ulikuwa hujui kwamba hizo injili ni za laana! Na ulikuwa unazihubiri, Lakini leo umejua..Tubu mlipize shetani kwa uongo aliokudanganya kwa muda mrefu! Tubu nenda kachome vimini vyote ulivyokuwa unavaa,(na nguo zote zinazochora maungo yako) na kamwe usihubiri Injili hiyo uliyokuwa unaihubiri ya Laana kwamba Mungu haangalii mavazi…Ulikuwa unasuka nywele!, kafumue ziweke katika hali yake ya asilia Mungu alizokuumbia, ulikuwa unavaa mawigi, na kupaka lipstick pamoja na mapambopambo ya kidunia..jirudishe katika hali yako ya asili..Umesoma haya kwa macho yako! Hutasema siku ile hujaambiwa, wala hukusikia, au haujafafanuliwa vizuri!..

Ukikubali maonyo na kugeuka ni vizuri! Utakuwa umeisalimisha roho yako, lakini ukikataa pia ni vizuri, kwasababu Injili sio kitu cha kulazimishwa……isipokuwa hakikisha kama unajipamba jipambe kikweli kweli, Kama unavaa vimini tafuta vile vikali kabisa, kama unasuka, suka mitindo yote na ya kila namna…unapaka poda, uwanja, weka mwingi wa kutosha unavaa wigi tafuta za kila mtindo….usiwe nusu nusu, ili siku ile katika ziwa la moto usije ukajuta kwanini hukujipamba sana, utakapoona ulijipamba kidogo tu na bado umetupwa katika ziwa la moto!…usije ukajuta kwanini ulikuwa una nguo moja tu! Kimini ambacho ulikuwa unakivaa mara moja tu kwa mwezi katika tukio maalumu…na nguo nyingine ndefu za kujisitiri ulikuwa unazivaa kila siku na bado umetupwa kwenye ziwa la Moto!

Kama umechagua kwenda kuzimu usikubali kinguo kimoja tu kikupeleke kule! Tafuta madebe ya vimini na suruali zile zinazobana kabisa, pamoja na maboksi ya lipstick yatumie… kwasababu Bwana Yesu alisema mwenyewe katika Ufunuo.

Ufunuo 22:10 “ Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Maran atha!

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

NGUVU YA UPOTEVU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

LAANA YA YERIKO.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.

INJILI YA MILELE.

JE! KUBET NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

MAKERUBI NI NINI?

Kerubi au Makerubi ni Malaika wa Mungu,..Moja ya makundi ya malaika walioko mbinguni ambao kazi yao hasaa ni kuilinda enzi ya Mungu, na kumtukuza..Shetani naye alikuwa ni kerubi kabla hajaasi, lakini sasa sio kerubi tena,..

Ezekieli 28:14 “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.

16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto”.

Makerubi utaona wakitajwa katika kitabu cha Mwanzo mara baada ya Adamu na Hawa kufukuzwa katika bustani ya Edeni wakawekwa ili kuilinda njia ya mti wa Uzima wasiifikie (Mwanzo 3:24), Utaona pia Musa alipoagizwa atengeneze sanduku la Agano ndani ya Hema ya kukutania alipewa masharti afanye makerubi wawili juu ya sanduku lile ili kukifunika kiti cha rehema..(Kutoka 25:17-22), vile vile hata katika hekalu maagizo hayo yalitolewa.

2Nyakati 3:10 “Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akafanyiza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunikiza kwa dhahabu.

11 Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.

12 Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza.

13 Yakaenea mabawa ya makerubi hayo mikono ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba”.

Tunawasoma pia katika kitabu cha Ezekieli makerubi ni malaika wenye  sifa ya kuwa na mabawa manne, mawili walitumia kupaa, na mawili walitumia kufunika miili yao, na kila mmoja mwenye nyuso nne, (Ezekieli 10)..wanafananishwa na wale wenye uhai wanne tunaowasoma katika kitabu cha Ufunuo 4

Hivyo kwa ufupi makerubi na malaika wanaoonekana kuwa karibu sana na kiti cha enzi cha Mungu kuliko malaika wengine wote, wakimsifu na kuuhubiri ukuu wake usiku na mchana (Soma Ufunuo 4:6-9).

Nasi tunapokuwa katika hali ya kumsifu Mungu na kumwimbia kwa nguvu zetu zote, basi kundi hili la malaika linakuwa karibu sana na sisi, tufauti na tunaposali au kuhubiri.

Ubarikiwe.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

MALAIKA WA MAJI NI YUPI? NA JE KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

KAZI YA UZURURAJI WA SHETANI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

AMANI YA BWANA /AMANI YA MUNGU.

Amani ya Bwana Ni nguzo ya Muhimu sana katika kumwongoza Mkristo.

Moja ya njia Mungu anazotumia kuzungumza na Mtu ni kwa kupitia amani…

  • AMANI INA SAUTI: Inazungumza, Ni kama mtu wa pili ndani ya Mtu..Hata katika mambo ya kawaida Mtu akikosa amani ya moyo ya kufanya jambo fulani, basi jambo hilo halifanyi tena…au hata akilifanya hatalifanya vizuri litamweka katika mashaka makubwa…Hiyo yote ni kwasababu Amani iliyopo ndani yake haijamruhusu kufanya hivyo.

Vivyo hivyo na Mungu wetu anazungumza na sisi mara nyingi kwa kupitia  AMANI.

Akitaka kukuzuilia jambo fulani lililo nje ya mapenzi yake, utaona umekosa amani ghafla ya kufanya jambo hilo.

Hata katika maombi..moja ya uthibitisho kama maombi yako yamejibiwa ni AMANI UTAKAYOIPATA; Kama moyo wako umekuwa mzito, pengine una majonzi, huzuni, umekosa furaha na unatamani Mungu azungumze na wewe, ingia kwenye magoti omba mpaka uone amani fulani imeingia ndani yako..Ukiona kuna amani imekuja ndani yako ya kipeee Hapo jua Roho Mtakatifu katenda jambo.

Na amani hii inapokuja juu yako utaona inakufanya unazidi kumpenda Mungu zaidi, na utaona inakusukuma kutenda wema zaidi kuliko ubaya…utajikuta kama kuna mtu au kitu kilikuwa kimekuudhi ghafla unaona unahaja ya kusamehe, ghafla unasikia kama vifungo fulani vimeachia…ulikuwa unampango wa kulipiza unajikuta unasamehe, ulikuwa na hasira ghafla unajikuta furaha fulani imekuvaa..kadhalika uchangamfu fulani unakuingia..n.k hiyo ndiyo amani ya Kristo..Amani ya ulimwengu huu, matunda yake ni kutenda dhambi…ulikuwa na hasira na ulipofikiria kwenda kulipiza kisasi amani fulani ikakuingia kwenda kufanya hicho kitendo hiyo ni amani ya ulimwengu huu..

Bwana Yesu alisema katika kitabu cha Yohana..

Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.

Ni muhimu kuitafuta sana Amani ya Kristo.

Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

Wakolosai 3:14 “Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani”.

Hii Amani ya Mungu chanzo chake ni KUOKOKA! na mtu unaokoka kwa kutubu kwanza na kudhamiria kuacha dhambi zako na kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.

Itafute Amani ya Mungu, ambayo ndio amani ya moyo inayolenga mapenzi ya Mungu. kwasababu inapatikana…kumbuka alisema mwenyewe kuwa “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo.”

Ubarikiwe.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

NYOTA ZIPOTEAZO.

KUONGEZEKA KWA MAARIFA.

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.

MAFUMBO YA MUNGU.

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA


Rudi Nyumbani:

Print this post

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

Waefeso 5.12 “kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena”.

Zamani ilikuwa ni rahisi kumtambua mtu mwenye dhambi kwa kumtazama tu au kumwangalia mienendo yake kwasababu karibu kila ouvu uliokuwa unafanyika chanzo chake kilikuwa ni cha nje kabisa kinachoonekana, kwa mfano zamani ilikuwa ili kuwapata watu wanaotembea tupu au makahaba ilikuwa ni lazima uende mahali kama kasino, au disco za usiku, au kwenye madanguro lakini sasa hivi mambo hayo yote unayapata mitandaoni na kwenye simu za mikononi bure, maovu yanayotendeka sasa hivi kwa siri ni mabaya zaidi kuliko hata yale ya kipindi kile,..mtu anaweza akatembelea madanguro hata 30 katika simu yake katika siku moja.

Unaweza ukajifanya mwema kwa nje, haunywi pombe, hauendi disco, hauzini na wanawake, au wanaume, tena umebatizwa, na unasema wewe ni mkristo, lakini ndani ya simu yako kwa siri ume download video za pornography unatazama na hakuna mtu anayejua, nataka nikuambie biblia inasema hilo nalo litafika hukumuni siku ile..

Mhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja NA KILA NENO LA SIRI, likiwa jema au likiwa baya

Wala usijidanganye, kusema mengine yote nimeyashinda ni hili tu ndio linalonisumbua siku ile Mungu atanihurumia, ndugu kuzimu utakwenda, biblia inasema

Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote”.

Kila unapoingia mtandaoni kazi yako ni kutafuta picha na video za watu wa kidunia wanaozini, kila update ya video za ngono wewe unayo, Kumbuka Moja ya vitu sita ambavyo Mungu anavichukia ni pamoja na mtu aliye na miguu miyepesi kukimbilia maovu..(Mithali 6:18)

Wewe hujui ni kwa namna gani unamkasirisha Mungu, Badala uwe mwepesi kutafuta maneno yake mitandaoni wewe unatumia wepesi huo kwenda kutafuta miziki ya kidunia ambayo maudhui yake ni uasherati tu, na matusi, ni kibaya zaidi unajiita mkristo.

Hujui kuwa unatimiza maandiko ya wale wakristo baridi wanaozungumziwa kuwepo katika siku za mwisho, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu.(2Timotheo 3:4 )

Ni heri ukatupilia mbali hiyo simu kama inakukosesha kuliko kuwa mtumwa wa ibilisi na ukaenda kuzimu, biblia inasema kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate….wapo watu wengi kuzimu leo hii, wanatamani wakuhubirie wewe injili, uache kutazama hayo mambo machafu unayoyatazama huko mitandaoni, lakini hawawezi kutoka huko, laiti ungewaona, wanavyohangaika na ule moto kwa kosa moja kama unalolifanya wewe leo hii, usingetamani hata kutazama pornography, fahamu kuwa asilimia 99 kama sio 100, ya watu wote wanaoigiza mikanda hiyo ni mawakala wa kuzimu, tena wale wa hali ya juu sana, wanapokea maagizo hayo kutoka kwa ibilisi baba yao, na wanaelekezwa namna ya kufanya mambo hayo, sasa wewe usiyejua unavutiwa kwenda kutazama, hujui kuwa kuna roho mbaya zenye nguvu mara 7 zaidi ya zile zilizokuwepo Sodoma na Gomora, zimetegeshwa pale, unapotazama kidogo tu, moja kwa moja, zinakuvaa na ndio hapo tamaa zisizo za kawaida zinakuvaa, zinakufanya uwe kama mnyama aliyerukwa na akili asiyeona aibu kufanya jambo lolote lile, na hizo hazitoki leo wala kesho, ndio hao wengine wanaishia kuwa mashoga na wasagaji, wengine wanazini na wanyama, wengine na wazazi wao, wengine na watoto wao, wengine ndugu zao, wengine na majirani zao, wengine wanafanya mustarbation… sasa hizo zote ni roho za mauti, ambazo mwisho wake ni kuzimu na hizo roho huwezi kuzishinda kama utaendelea kuwa mbali na Kristo..

Lakini ukidhamiria kuacha Kabisa na kutubu dhambi zako, Kristo atakuvika uwezo wa kushinda hivyo vyote, Wengi hawawezi na wamekuwa watumwa wa hayo mambo ni kwasababu hawajadhamiria kwa miguu yao yote kumfuata Kristo, moyoni mwao anasema nikimfuata YESU inamaanisha sitakunywa pombe tena, sitatukana tena, sitakwenda disco tena, sasa watu wa namna hiyo hata kama leo hii wakitubu na kusema wamemkabidhi YESU maisha yao, na huku wanavitamani bado vitu hivyo, hawawezi kuvikwa huo uwezo utokao juu wa kuyashinda hayo yote, hata wafanye nini lakini ukidhamiria kwa dhati na kusema, kuanzia leo dunia bye! Bye!

Mimi kwa miguu yote naenda kwa Kristo bila kugeuka nyuma, kwasababu nataka niende mbinguni, nakuambia wewe mwenyewe utaona jinsi itakavyokuwa rahisi kuishinda dhambi, hata sisi tulikuwa huko, tukatolewa ile kiu ya pombe Yesu ataimaliza yote, ile kiu ya sigara itamalizwa yote, ile tamaa ya uzinzi Mungu ataiua, ile tamaa ya kufanya punyeto, itakufa yote, ile tamaa ya ushoga na usagaji itakufa yenyewe..Lakini sharti kwanza useme nimeamua kwa moyo wangu wote, na akili zangu zote, na nguvu zangu zote kuanzia leo kumfuata Kristo. Ukafuta video zote ulizozidownload, ukaacha kutembelea website zote ngono unazotembelea, ukafuta miziki yote ya kidunia, na ukakaa mbali na wazinzi wote, basi Mungu atakubadilisha haraka sana.

Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba.. “Mungu hawezi kutupa maagizo ambayo anajua sisi hatuwezi kuyafanya”…

Hawezi kutuambia tusizini na huku anajua hatuwezi kuishi bila kufanya uzinzi, kwahiyo anajua kabisa kuna namna mwanadamu anaweza kuishi bila kuzini kabisa! Ipo namna! Na ni rahisi sana…anajua hilo, hivyo ni jukumu letu kuivumbua hiyo, na Hiyo namna ipo kwa Yesu tu mwanawe mpendwa basi!! Ukivifuta hivyo vitu na kuviacha yeye si mwongo kutupa mzigo tusioweza kuubeba…utashangaa tu! Uwezo wa ajabu umekuja juu yako unaokufanya usitamani tena huo uchafu milele!

Kama ni hivyo, na unataka kumkabidhi Bwana YESU maisha yako tena, basi sali sala hii ya toba : hapo ulipo Piga magoti, kisha chukua muda mchache mweleze Mungu kuwa ulimkosea, kwa kuwa vuguvugu, na kutenda dhambi nyingi kwa siri, mwelezo bila kumficha chochote kwasababu mambo yote uliyokuwa unayafanya kwa siri yote anayajua, hivyo mweleze kuwa hutaki kufanya hivyo tena, na kwamba umedhamiria kuacha maisha ya kidunia na sasa unamfuata Kristo..

Ukishasema hivyo kwa kumaanisha kabisa..Ujue kuwa Bwana YESU amekusikia,..baada ya sala hiyo, ni kufuta sasa hivi bila kuangalia kushoto wala kulia kila picha, mziki, video chafu yoyote uliyonayo kwenye simu, flash, laptop au popote pale na Hatua inayofuata ni kutafuta kanisa la kiroho wanalobatiza ubatizo sahihi wa maji mengi kwa jina la YESU KRISTO nenda ukabatizwe kwa ajili ya kukamilisha wokovu wako, kulingana na Matendo 2:38, Kisha Mungu atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu bure atakayekuwa msaidizi wako, kukufundisha na kukuongoza kulielewa Neno na kuishi Maisha ya utakatifu…Vile vile usiache kwenda kanisani kuanzia leo ili Mungu ayakamilishe maisha yako mpaka siku ile ya wokovu.

Bwana akubariki sana. Ikiwa utapenda kuendelea kujifunza Neno la Mungu pamoja na sisi jinsi ya kukua kiroho, basi usiache kutembelea website yetu hii (www wingulamashahidi org).

Maran Atha!

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KWANINI MAHUSIANO YA JINSIA MOJA NI DHAMBI?

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA.

EPUKA MUHURI WA SHETANI.

KUZIMU NI WAPI.

MLIMA WA BWANA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake”

Haijalishi tuna ujuzi wa kuongea kiasi gani?, haijalishi tuna vipaji vya kuongea na vya kupangilia maneno kiasi gani, haijalishi tunayajua maandiko kiasi gani…Mbele za Mungu watu wote ulimwenguni hatujui kuomba jinsi ipasavyo! Hata kama tunaweza kujiona tumeomba vizuri kiasi gani au tumebobea kiasi gani…bado hatujui kuomba jinsi ipasavyo…

Utauliza hata mchungaji, au Nabii, au Mwalimu, au Askofu aliyekaa kwenye wokovu miaka mingi, bado atakuwa hajui kuomba jinsi ipasavyo?..Jibu ni ndio! Hata kama atakuwa amekaa miaka mia katika wokovu, na kila siku anasali, na anajua maandiko yote na kuyanukuu kisahihi wakati wa kuomba…Bado pasipo Roho Mtakatifu atakuwa hajui kuomba jinsi ipasavyo, na hivyo maombi yake huwa hewa mbele za Mungu.

Leo tutajifunza Umuhimu wa Kuwa na Roho Mtakatifu katika kuomba! Kwa maana yeye ndiye atusaidiaye kuomba!…Sasa Utauliza Roho Mtakatifu anatuombeaje? Je yupo huko mbinguni amekaa akituombea kwa Baba muda wote akipeleka mahitaji yetu hata kama wakati tukiwa tumelala au vipi?..Na swali lingine ni kwamba je! Kama anatuombea sisi tuna haja gani tena ya kuomba..maana yeye ndiye anayetuombea vizuri Zaidi.

Ili kupata majibu ya maswali hayo, tujifunze kwanza kidogo jinsi Roho Mtakatifu anavyotenda kazi katika kuwavuta watu kwake..

Mtu aliyejaa Roho Mtakatifu, anapokwenda kuhubiri kwa watu walio nje ya Kristo, yule Roho aliyeko ndani yake, anaingia ndani ya wale watu ambao wapo nje ya Kristo, na kumsaidia kuhubiri ndani ya mioyo yao…Kwahiyo huyu mhubiri mwenye kigugumizi na asiyejua kuongea vizuri, labda pengine atazungumza maneno machache tu lakini kwasababu anaye Roho Mtakatifu anayemsaidia kuhubiri katika mioyo ya wale wenye dhambi upande wa pili…unakuta wale wenye dhambi kuna nguvu ndani yao inayowashawishi mara mbili zaidi watubu waache dhambi, watajikuta hata hawategemei tena maneno ya yule mhubiri, lakini ile nguvu ndani yao inaanza kuwahubiria dhambi na kuhukumu maisha yao ya dhambi……

Sasa hicho kitendo cha wenye dhambi kusikia kama wanahubiriwa kwa nguvu mara mbili Zaidi katika mioyo yao zaidi ya wanavyosikia katika masikio ya nje…Huo ndio unaoitwa Msaada wa Roho Mtakatifu kwa yule Mhubiri..Hivyo kitendo hicho tunaweza kukiweka katika sentensi hii..

“Roho Mtakatifu amemsaidia yule Mhubiri, kuwahubiria wale wenye dhambi mioyoni mwao kwa kuugua kusikoweza kutamkika” Matokeo yake wale wenye dhambi wakawahi kukubali kumpa Yesu Maisha yao kuliko yule Mhubiri angekosa huo msaada.

Yohana 16:7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.

Sasa endapo huyo Mhubiri angekuwa hana Roho Mtakatifu ndani yake, wale watu mioyoni mwao wasingesikia chochote kinachowahubiria hivyo wangemsikiliza yule mhubiri na kigugumizi chake, na mwisho wa siku wangeishia kumcheka na kumwona anapoteza muda..na wangemwona hajui kuongea wala kujieleza na wasingetubu!..Au hata kama ungekuwa unajua kuongea vizuri na kupangilia maneno na kunukuuu, wangekusifia tu kwamba unajua kuongea vizuri na kwamba ni mhubiri mzuri lakini ndani ya mioyo yao wasingesikia chochote kinachowasukuma wao kutubu dhambi, na hivyo kuishia kupata hasara badala ya faida.

Sasa kwa formula hiyo hiyo, ndiyo Roho Mtakatifu anayotusaidia kuomba mbele za Mungu…Unapoingia magotini kumwomba Mungu, hoja zako wewe zina madhaifu mengi, na wala hazieleweki mbele za Mungu, hata kama umejiona umezipangilia kiasi gani, hata kama umejiona umenukuu maandiko kiasi gani…Lakini kwasababu tu hunaye Roho Mtakatifu, Unakuwa una msaada wa anayekusaidia kuomba upande wa pili, katika moyo wa Mungu.

Sasa Roho Mtakatifu anakusaidia kuzipeleka zile hoja zako mbele za Moyo wa Mungu, kiasi kwamba unanena maneno machache, lakini huku nyuma Roho anayahubiri yale maneno uliyoyanena moyoni mwa Baba mbinguni kwa ufasaha Zaidi, na hivyo kuuchoma na kuugusa moyo wa Mungu kwa namna isiyoweza kutamkika mpaka kufikia kuleta majibu yanayotakiwa. Haleluya!

Huo ndio umuhimu wa Roho Mtakatifu kwa mwaminio yeyote! Tunamhitaji sana Roho Mtakatifu katika mambo yote maana pasipo yeye sisi hatuwezi, ndio maana biblia imemwita “MSAIDIZI” Msaidizi maana yake anatusaidia pale tunapokwama..

Tunaposali tunamhitaji huyu msaidizi, hakuna chuo chochote cha kwenda kusomea jinsi ya kuomba! Roho Mtakatifu pekee yake ndiye anayeweza kutuombea jinsi ipasavyo…Na anatuombea pale tunapoomba! Sio wakati tumelala…hapana! Hata mhubiri anamsaidia kuhubiri pale anapohubiri, sio wakati ambao hahubiri.

Hivyo kama mtu hana Roho Mtakatifu basi umekosa kitu kikubwa sana na cha maana sana, ni heri angekosa utajiri wote wa ulimwengu huu au kukosa kila kitu kuliko kumkosa Roho Mtakatifu..kwasababu Biblia imesema katika Warumi 8:9 kuwa “Mtu yeyote asiye na Roho huyo sio wa Mungu”

Je! Umepokea Roho Mtakatifu?…Au bado unaomba tu bila msaada wake?..Lakini Utauliza nitampokeaje? Jibu lipo ndani ya Biblia Takatifu katika Mstari ufuatao…

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”

Fomula ya kumpokea ndiyo hiyo, kutubu kwanza kwa kumaanisha kuacha Maisha ya dhambi kama ulevi, anasa, uasherati, uvutaji sigara, chuki, visasi, utazamaji picha chafu, utukanaji, ulawiti, usagaji, ushoga, ushirikina, uchawi, n.k Kisha ukishatubu kutoka moyoni kabisa na Bwana akiiona Toba yako na Imani yako kuwa ni ya dhati kabisa…ATAKUSAMEHE KABISA! Na baada ya msamaha huo wa Bure utakaoupata hatua inayofuata ni kwenda kutafuta ubatizo sahihi, ambao huo ni wa kuzamishwa mwili wote kwenye maji na kwa JINA LA YESU KRISTO, Kisha baada ya huo Roho Ataingia ndani yako, Msaidizi wetu ambaye ni Zawadi kutoka kwa Baba, ambayo tumepewa sisi na Watoto wetu na wote tutakaowahubiria kumjua yeye.

Hakuna mfariji wa kweli kama ROHO MTAKATIFU.

Bwana akubariki.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU.

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.

JE! KARAMA NI UTHIBITISHO WA KUWA NA MUNGU?

NGURUMO SABA

UNYAKUO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

Jinsi Mungu anavyotuhudumia sisi ni tofauti na sisi tunavyoweza kufikiri, Sisi tunatazamia Mungu atatuhudumia kutoka mbinguni, lakini yeye yupo tofauti, msaada wake ameuweka sehemu ya chini sana, ambayo imedharauliwa na wengi, Leo hii ukimwomba Mungu jambo basi toa yale mawazo kwamba atakupa majibu kutoka katika mambo makubwa….Ni kweli matokeo ya majibu yatakuwa makubwa, lakini chanzo cha majibu yako kinaweza kisiwe huko unapokitazamia. Naamani alikuwa mkuu wa majeshi wa Taifa la Shamu, ambalo lilikuwa ni moja ya mataifa makubwa sana enzi zile za wafalme, lakini alisumbuliwa na ukoma kwa muda mrefu sana mpaka siku moja aliposikia kuna nabii wa Mungu Israeli, ambaye ni Elisha, tunaona lakini alipomfuata ili aponywe majibu yake yalikuwa ni tofauti na alivyotazamia. Tusome:

2Wafalme 5:9 “Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha.

10 Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.

11 Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.

12 Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.

13 Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?

14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.”

Unaona, hata leo watu wengi wamemwomba Mungu awafanyie mambo Fulani Fulani katika maisha yao, wengine wanayo magonjwa yanawasumbua wengine ni matatizo, lakini walipofika kwa Mungu waliposikia kuna maagizo Fulani ya kuzingatia, kwamba wanapaswa waokoke kwanza wao wanapuuzia, kwamfano biblia inaagiza kila mmoja anapaswa abatizwe kwa kuzamishwa katika maji mengi ili apate ondoleo la dhambi zake…

Lakini mtu akisikia hivyo utaona anaanza kutoa udhuru, wakitoa tafsiri zao, aah! Ubatizo haumpeleki mtu mbinguni!, Ubatizo hauondoi dhambi kinachoondoa dhambi ni damu ya YESU, wengine watasema, dini yetu haituagizi hivyo, wengine watasema batizo zote ni sawa za kunyunyiziwa na za kuzamwishwa ni sawa, wengine watasema nenda mto Yordani na wewe ukabatizwe kama Bwana Yesu ndio tujue kuwa kweli umebatizwa ipasavyo n.k Mtu huyo huyo pia atakuwa tayari kwenda kila mwisho wa wiki kuogelea baharini au kwenye mabwawa ya starehe kwa masaa mengi bila hata kukinai wala kuchoka, lakini kuingia katika yale maji kubatizwa mara moja tu katika jina la Bwana Yesu, ni vita! Ujue ni roho ya namna gani ipo ndani ya mtu wa namna hiyo!

Na mtu huyu huyu bado anasema ameokoka, na amekaa katika wokovu kwa miaka mingi..Nataka nikuambie kitendo cha kubatizwa kinaweza kisiwe na maana sana kwako, lakini kina maana kubwa sana kwa YESU aliyetoa maagizo hayo..

Unatazamia uwekewe mikono lakini Bwana anakwambia kashuke kwenye yale maji nawe utapona!….Unatazamia Bwana akwambie funga masaa mengi na uombe watu wakuombee au utoe sadaka nyingi….lakini Bwana anakupa maagizo marahisi tu, jishushe kafanye ibada ya kuwaosha miguu watakatifu nawe utaona matokeo makubwa tu!….wapo wengine wanasema kushiriki meza ya Bwana au kutawadhana miguu watakatifu havina maana yoyote, lakini Bwana Yesu alisema Heri ninyi mkiyafanya hayo.

Yohana 13:14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”.

Wewe utajiona na hadhi yako, huwezi kushika miguu ya mwingine na kuiosha, Bwana Yesu aliyekuwa ni Mungu katika mwili lakini alifanya hivyo, mimi na wewe ni nani tusifanye?..yeye aliiosha miguu ya wavuvi, sisi ni nani tusioshane miguu?..

Sasa Maagizo ya msingi kama hayo mtu hataki kuzingatia anategemea vipi Mungu atampatia haja yake kwa haraka, kama anavyotaka yeye?..anatazamia aambiwe njoo nunua maji ya upako, au awekewe mikono na watumishi, au afunge na kuomba,..akidhani hayo ndio maagizo sahihi ya Mungu kama Naamani alivyofikiri kumbe sio. Wayahudi walimtazamia MASIHI wao atakuja kama mfalme mkuu sana, ambaye ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi pale Israeli na kuwapigania dhidi ya maadui zao Warumi, lakini alipokuja katika familia ya kimaskini walipoteza shabaha, alipokuja hashiki silaha bali anahubiri upendo walimkosa, walipomuona amesulibiwa msalabani ndipo wakasema kabisa huyu amelaaniwa, lakini hawakujua kuwa Yule ndio Mungu mwenyewe aliyeuvaa mwili anaishi na sisi.

Vivyo hivyo na sisi tukitaka Mungu atuhudimie tunapaswa tujishushe, na kujishusha kwenyewe ni kuyatii maagizo yake mepesi aliyotupa, tusijione sisi ni wa rohoni sana, au tunajua zaidi yake mpaka tukadharau anachotuelekeza kufanya..Soma biblia ili ufahamu ukweli, na ukisha ujua ukweli basi uwe tayari kubadilika bila kujali dini yako au dhehebu lako linaamini vipi, na hiyo ndio dalili kubwa itakayokutambulisha kuwa ROHO WA MUNGU hajazimika bado ndani yako, ikiwa upo tayari kuyatii maagizo yake yote sawasawa na maandiko yanavyotulekeza.

Biblia inasema: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”. (Ufunuo 2:7)

Maran Atha.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

SIRI YA MUNGU.

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!


Rudi Nyumbani:

Print this post

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

Katika biblia nzima hakuna mahali utaona pametabiriwa kwa wazi kuwa Kristo atakaa kaburini siku tatu, na baada ya siku ya tatu atafufuka. Hakuna mahali popote kwenye Biblia palipoandikwa ufunuo huo…Tunaona unabii wa Kristo kuzaliwa na Bikira uliandikwa wazi katika Isaya 7:14 kwamba atazaliwa na Bikira, kadhalika unabii wa Kristo kuzaliwa Bethlehemu ya Uyahudi ulitabiriwa wazi katika kitabu cha Mika.

Mika 5: 2 “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”…

Kadhalika unabii wa Bwana Yesu kuteswa kwa ajili ya dhambi zetu uliandikwa wazi katika Isaya

Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Na Nabii nyingine Nyingi zimuhusuzo Yesu ziliandikwa wazi hata za kuja kwake mara ya pili…Lakini katika unabii wa kukaa kaburini siku tatu, huo haukuandikwa wazi..Uliihitaji Ufunuo wa kipekee wa Roho ili kuujua…Kwasababu Yesu mwenyewe alisema ilipaswa yote yatimie yaliyoandikwa na Manabii, Torati na Zaburi. Na pia ulipaswa utimie unabii alioandikiwa yeye kuhusu kukaa kaburini siku tatu.

Luka 24:44 “ Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika TORATI YA MUSA, NA KATIKA MANABII NA ZABURI.

45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

46 Akawaambia, NDIVYO ILIVYOANDIKWA, KWAMBA KRISTO ATATESWA NA KUFUFUKA SIKU YA TATU;”

Sasa ni wapi palipotabiriwa kuwa Kristo atakaa kaburini siku tatu?

Pasipo ufunuo wa Roho hakuna mtu angejua kuwa Yesu Kristo alitabiriwa hayo, hata Wanafunzi wa Yesu walikuwa hawajui, si Zaidi Mafarisayo..Lakini tunaona Roho Mtakatifu mwenyewe alifichua fumbo hilo na kutuonesha sisi katika maandiko kuwa ni wapi Kristo alitabiriwa kukaa siku tatu kaburini…tunasoma katika..

Mathayo 12:39 “Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi”

Unaona? Kumbe Maisha ya Yona yalikuwa ni UFUNUO WA YESU KRISTO kukaa kaburini siku tatu?? Nani alikuwa analijua hilo?? Hata Yona mwenyewe alikuwa halijui.

Sasa kama Maisha ya Yona yalikuwa yamebeba siri nzito namna ile, inayomhusu Yesu….ya Yusufu yatakuaje? Ya Musa yatakuaje?, ya Ayubu na Danieli yatakuwaje?..Tunamhitaji Roho Mtakatifu atufunulie maandiko tuweze kumwelewa. Hakika pasipo yeye hatutaelewa chochote katika maandiko.

Yohana 14:26 “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia”.

Ukisoma tena katika maandiko utaona Bwana YESU alikuwa yupo tayari kutueleza pia mambo ya mbinguni, lakini kwa kutokuamini kwetu, hakutueleza(Yohana 3:12),.. Lakini Kristo mwenyewe aliahidi kuwa huyo Roho Mtakatifu atakapokuja atayatwaa yaliyo yake na kutupasha sisi habari,(Yohana 16:14).

Umeona umuhimu wa kuwa na Roho Mtakatifu sasa?, Swali ni Je! Umempata?..Na hata kama unaye je! amejaa kwa wingi ndani yako? Bwana atusaidie!

Kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako, mlango wa Neema bado upo wazi, lakini hautakuwa hivyo siku zote.Tubu kwa kumaanisha kuacha dhambi kama hujatubu, na zingatia kutafuta ubatizo sahihi, wa kuzama mwili wote majini na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38. Na yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu bure kama alivyoahidi katika Neno lake kwa wale wote waaminio.

Maran atha!

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU NI IPI?

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

NIKUPE WEWE URITHI WA BABA ZANGU?

1Wafalme 21:1 “Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria.

2 Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake.

3 Nabothi akamwambia Ahabu, BWANA APISHE MBALI NIKUPE WEWE URITHI WA BABA ZANGU.

4 Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula”.

Katika agano la kale ilikuwa ni sheria hakuna mtu yeyote kuuza shamba la familia au ukoo, vitu vingine vyote viliweza kuuzwa lakini linapokuja suala la shamba la urithi ni utaratibu uliokuwepo hakuna mtu yeyote kuuza shamba hilo haijalishi kafilisika au halitumii, hata sasa kwenye jamii zetu nyingi mambo kama hayo tunayaona, mtu ukiuza shamba la ukoo, anaweza akatengwa kama sio kufukuzwa kabisa na ndivyo ilivyokuwa hata katika desturi za wayahudi..

Hapa tunaona mtu mmoja wa kawaida tu aliyeitwa Nabothi alikuwa na shamba lake lililokuwa karibu sana na hekalu la Raisi wake, Ahabu..Hiyo inatupa picha kamili kuwa shamba hilo lilikuwa ni lenye thamani nyingi sana, kama angekuwa ni mtu mwenye tamaa basi angeliuza kwa gharama kubwa sana, kiasi kwamba angepata pesa ya kununua mashamba mengine kama yale hata zaidi ya 10 mahali pengine na bado angebakiwa na pesa na kujenga na kula katika maisha yake yote na familia yake…

Shamba hilo ni wazi kuwa lilikuwa zuri sana, kiasi cha kwamba lilimfanya hata mfalme Ahabu akose usingizi kwa kunyimwa kuuziwa shamba lile na mmiliki mwenyewe Nabothi, Sio kwamba Nabothi alipenda kumdharau mfalme, au hakuwa na shida na mali hapana, lakini alijua kuwa shamba la urithi haliuuzwi, haijalishi ni nani amesimama mbele yake, ni mkuu,au sio mkuu, ni tajiri au sio tajiri, kanuni ni ile ile shamba la urithi haliuzwi… Nabothi alikuwa tayari kufa lakini sio kuachia shamba lile liende nje ya ukoo wake. Ukiendelea kusoma pale utaona mpaka Yezebeli anamuundia visa auawe ili alichukue shamba lile.

Biblia inatuambia mambo hayo yaliandikwa kwa mifano ili kutufundisha sisi, ambao sisi tutakuja kuishi katika agano lililo bora zaidi (1Wakorintho 10:11).. Na sisi pia tunao urithi tulioachiwa na mababa zetu wa Imani (Mitume), na urithi huo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO,

1Petro 1:3 “Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;

4 TUPATE NA URITHI USIOHARIBIKA, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.

5 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho”.

Unaona mtu yeyote aliyempokea Kristo moja kwa moja tayari, ameupokea Urithi usioharibika ambao ulianza tangu enzi na enzi za mitume Baba zetu ambao hao walikuwa watangulizi wetu waliokuwa tayari hata kufa lakini wasiuuze urithi waliopewa na Mungu mbinguni yaani Kristo maishani mwao, na walipoondoka wakaturithisha na sisi urithi huo huo ambao ni YESU KRISTO Bwana wetu, ili na sisi pia wakati ukifika tuwarithishe Watoto wetu, sasa cha kushangaza leo hii utaona watu wengi wanasema wao ni wakristo, wameokoka, lakini wapo tayari kuuza urithi huu kirahisi rahisi tu, mtu yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya mali, yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya wazazi, au ndugu, yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya mwanamke au mwanaume…Yupo tayari kurudi nyuma ki-wokovu kwa ajili ya rafiki zake, kwa ajili ya wafanyakazi wenzake, kwa ajili ya boss wake, kwaajili ya ujana wake, kwaajili ya umaarufu wake…Kirahisi rahisi tu, jambo lolote likijitokeza ambalo anaona kabisa ni kinyume na imani yake yupo tayari kuacha mara moja, akidhani kuwa Imani hiyo akishaichia ipo siku ataipata tena,,Ndugu yangu usidanganyike biblia inatumbia IMANI hii tuliyonayo tunakabidhiwa mara moja tu, hakuna cha mara mbili wala mara tatu..soma…

Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.

Na hiyo ndio inatufanya tuwe makini sana kuilinda kwasababu tukishaipoteza kuipata tena ni ngumu..

Ni sawa na mtu anayeliuza shamba, akishaliuza mara moja, basi hatakaa alipate tena milele, linakuwa ni milki halali ya mtu mwingine..Vivyo hivyo na leo hii wewe unayeuuza wokovu wako kirahisi rahisi tu, unarudi nyuma kirahisi rahisi tu, siku Roho Mtakatifu akiondoka kwako basi ndio moja kwa moja hivyo , hakuna toba hapo.. Umesikia injili mara ngapi lakini bado wiki hii unaompango wa kwenda kuzini, unamfanyia jeuri Roho wa Mungu, unadhani kuna siku itafika utubu…tambua hakuna jambo kama hilo saa ya wokovu ni sasa, jitwike msalaba wako mfuate YESU.

Marko 8:35 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?

38 Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu”.

Ifikie wakati uwe na ujasiri wa kumwambia ibilisi ki-vitendo “Nikupe wewe urithi wa Baba zangu?”..weka mbali mambo ya ulimwengu huu uanze kuulinda urithi wako.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

EDENI YA SHETANI:

CHUKIZO LA UHARIBIFU

YEZEBELI ALIKUWA NANI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

DUNIANI MNAYO DHIKI.

Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Bwana wetu YESU KRISTO mwenyewe ambaye yeye hakuwa na dhambi hata moja. Ni mtu aliyependwa na Baba kuliko mtu mwingine yeyote ambaye alishawahi kutokea hapa duniani kwa jinsi tu ule mwenendo wake ulivyokuwa mkamilifu..Mtu ambaye alikuwa  akimwomba Mungu jambo lolote anafanyiwa haraka sana, angetaka utajiri wote duniani angepewa, angetaka kuabudiwa angeabudiwa, alikuwa hana shida ya jambo lolote, lakini bado hapa tunaona anawaambia wanafunzi wake “Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”…

Hivyo dhiki haijalishi wewe ni mtakatifu kiasi gani, maadamu upo tu duniani utakumbana nazo kwa namna moja au nyingine, dhiki zinazokuja kutokana na Imani yako, kuchukiwa kutengwa, kudharauliwa, kupigwa, kufungwa, kuwindwa, kupungukiwa, kufiwa na ndugu wa karibu, magonjwa n.k.

Lakini pamoja na hayo alituahidi kuwa atakuwa nasi sikuzote hadi ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:20)na kwamba hatutajikwaa hata tukitembea katika majaribu mazito namna gani atatembea na sisi kuhakikisha hatuanguki, kama tu bado tutakuwa katika wokovu.

Zaburi 34:7 “Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa”.

Zaburi 91:11 “Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe”.

Na ndio maana akatuambia hapo TUJIPE MOYO. Kama yeye ameyashinda, basi tuwe na uhakika kuwa na sisi tutayashinda kwasababu yeye yupo pamoja na sisi kutusaidia..Kwahiyo ndugu yangu mkristo, uliyeokoka ambaye upo katika tumaini la kumngojea Bwana, nataka nikuambie usifadhaishwe na dhiki ya aina yoyote mbele yako wewe JIPE MOYO, aliye ndani yako hawezi kukuacha. Hakumwacha Danieli katika tundu la Simba, hawezi kukuacha na wewe, kukutana na simba haikumaanisha ndio mwisho wa kila kitu, wewe kukutana na dhiki haimaanishi ndio mwisho wako umefika, jipe moyo tu, hakuwaacha akina Shedraka, Meshaki na Abadnego katika tanuru la moto mkali namna ile hatoweza kukuacha na wewe..Hakumwacha Yusufu katika dhiki zile kule gerezani milele ulifika wakati akamfariji hatakuacha na wewe. Ikiwa bado unaishikilia imani yako, na kudhamiria kweli kweli kumfuata Kristo bila kigugumizi.

Wakati wako utafika mawimbi yote yatakwisha, lakini maadamu upo sasahivi katika hali hiyo liweke hili Neno moyoni, JIPE MOYO, JIPE MOYO, JIPE MOYO…Bwana yu pamoja nawe..USHINDI NI LAZIMA. Kama yeye alivyoshinda hivyo SONGA MBELE..

Maran Atha!

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JIPE MOYO.

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA.

WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.

VITA BADO VINAENDELEA.

TUKAZE MWENDO ILI TUUFIKILIE UTIMILIFU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post