Danieli 12:3 “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.”
Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;
13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; NI NYOTA ZIPOTEAZO, AMBAO WEUSI WA GIZA NDIO AKIBA YAO WALIOWEKEWA MILELE”.
Amosi 5: 8 “mtafuteni YEYE AFANYAYE KILIMIA NA ORIONI, NA KUKIGEUZA KIVULI CHA MAUTI KUWA ASUBUHI, NA KUUFANYA MCHANA KUWA giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana, ndilo jina lake;”
Ayubu 9:7 “Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri.
8 Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9 Yeye afanyaye hizo NYOTA ZA DUBU, na ORIONI, na hicho KILIMIA, Na makundi ya nyota ya kusini”.
Ayubu 38: 31 “Je! Waweza kuufunga mnyororo wa KILIMIA, Au kuvilegeza vifungo vya ORIONI?
32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake?….”
Mada Nyinginezo:
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
UTEKA ULIOGEUZWA.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Kwanini maombi ya Usiku yana nguvu kuliko ya mchana?
Kadhalika usiku wakati watu wamelala ndio wakati Adui anaiba vipawa vya watu..Kwahiyo unapokwenda kusali usiku, maana yake, unaingia kwenye uwanja wa mapambano uso kwa uso na Adui yako na ni rahisi kumwangusha..Kwahiyo yanakuwa ni maombi ya shabaha..Na yana madhara makubwa kwa shetani na ufalme wake.
Shetani hapendi watu wasali usiku kwasababu anajua madhara yatakayomfikia.
Bwana akubariki. Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
FAIDA ZA MAOMBI.
MAOMBI YA YABESI.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
UPUMBAVU WA MUNGU.
Mbinguni ni mahali mbali sana na upeo wetu wa kufikiri, na umbali huo haupo katika mfumo wa kilometa, au maili hapana! bali kiufahamu…Katika miili hii ya damu na Nyama hatuwezi kufika mbinguni. Ni sawa uwaambie paka wote duniani au mbwa wote duniani, wajikusanye wafanye bidii wafike kwenye wafike kwenye kifaa kilichotengenezwa na wanadamu kinachoitwa satelite kilichopo kule juu sana mawinguni..
Unaona? jambo hilo haliwezekani..kwanini? kwasababu wao upeo wao upo mbali sana na upeo wa wanadamu…Ili wafike kwenye satelite kule mbinguni ni sharti kwanza wawe wanadamu, wawe na ufahamu kama wa wanadamu ndipo waweze kufika kule.
Kadhalika na sisi tunahitaji kubadilishwa miili yetu, ifanane na malaika ndipo tuweze kufika mbinguni. Kwa jitihada zetu sisi kamwe hatuwezi kufika mbinguni, Malaika watakatifu walipo
Ubarikiwe!
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?
Mpaka umefikia kuuliza hili swali, naimani ni mtu unayependa kuabudu kitu unachokifahamu..Na pia naamini unapouliza dini ya kweli ni ipi unamaanisha kuwa ni Imani ipi ya kweli..Leo duniani zipo dini zaidi ya 4300 zinazofuatwa na wengi, hiyo ni mbali na madhehebu na vikundi vidogo vidogo, vikihesabiwa na hivyo hata laki vinafika..Na kila moja inadai kuwa Mungu wake ni sahihi..Mpaka unashindwa kujua Mungu wa kweli yupo wapi,
Upo katika tovuti hii, ambayo ni ya kikristo, mfano nikikupa jibu la haraka kuwa ukristo ndio Imani sahihi, bila shaka unaweza ukaamini kuwa huyu mtu anataka kunivuta kwake. Vivyo hivyo ukienda na kwingine, Hivyo maneno matupi hata yakijaza dunia, hayawezi kubatilisha ukweli wa maneno matano tu.
Hivyo ikiwa kweli umekusudia kufahamu Dini ya kweli, na Mungu wa kweli, jambo ni rahisi, Mungu aliye Mungu wa kweli sikuzote huwa anajitetea mwenyewe na wala hajitetei…Hivyo kama umemaanisha kweli kumtafuta Mungu huyo tenga muda wako mwenyewe binafsi kisha piga magoti, halafu omba kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni, usipomaanisha hakuna kitu kinachoweza kukutokea mwambie Ee Mungu wa kweli jidhihirishe kwangu na nionyeshe njia ya kweli na dini ya kweli ya kukufikia wewe..
Ukishamaliza kuomba basi wewe tulia, njia atakayoileta mbele yako ifuate, mimi siwezi kukuelezea atakujibuje jibuje lakini akikujibu utafahamu kuwa amekujibu kwa mambo yatakayofuatana na wewe baada ya hapo.
Fanya hivyo na Mungu wa kweli bila shaka atajidhihirisha kwako, na huyo ndiye umfuate kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote na kwa roho yako yote.
Ubarikiwe.
DINI NI NINI?.
JE! KUBET NI DHAMBI?
EPUKA MUHURI WA SHETANI.
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
Dini ni nini? Dini ya kweli ni ipi? na Imani ya kweli ni ipi?
Dini ni tendo linalotokana na Imani fulani (mambo ya rohoni), pale tu mtu anapoamini uwepo wa Mungu au hata uwepo wa shetani au hata kitu chochote kisichoonekana cha kuabudiwa basi hapo hapo dini inazaliwa, ndipo hapo utaona mtu anajiwekea miiko Fulani ya kufuata au utaratibu Fulani au ustaarabu Fulani kwamfano wanaoamwamini Buddha utaona wanao taratibu zao za kufuata ili kumwabudu mungu wao ipasavyo ndipo hapo utakuta ni lazima wote wavae mavazi Fulani, au wapitie madarasa Fulani, au waishi maisha Fulani ya kujinyima au kutokushirikiana na jamii Fulani ya watu au kufunga, au kutokula aina Fulani ya vyakula n.k sasa hiyo ndiyo inayoitwa dini..
Vivyo hivyo na katika ukristo, mtu yeyote mwenye imani ya kweli ya YESU Kristo ni lazima atakuwa na kiwango Fulani cha dini ndani yake, kwamfano ukiwa mkristo ni lazima utajikuta wewe mwenyewe unajijengea utaratibu wa kuomba kila siku, utajikuta unajijengea utaratibu wa kufunga mara kwa mara, licha tu ya biblia kuagiza lakini utajikuta unahudhuria ibada kanisani kila wakati, utajikuta unajijengea utaratibu wa kutoa sadaka na kuwasaidia na wengine n.k.…Na ndio maana biblia inasema..
Yakobo 1:26 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. 27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”
Yakobo 1:26 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”
Hivyo dini ya kweli ni ipi? Ni hiyo hapo juu kwenye mstari wa 27..Lakini sasa hiyo haimpi tiketi ya moja kwa moja kwenda mbinguni , bali inamrahishia tu njia ya kwenda mbinguni..tofauti na Imani nyingine kwao kushika dini ndio kuokoka, lakini katika ukristo usipomwamini YESU KRISTO na kuoshwa dhambi zako katika damu yake hata kama unashika dini vipi mbinguni huwezi kwenda…
Unaweza ukawa unafunga lakini kama maisha yako yapo mbali na Kristo kuzimu utakwenda, unaweza ukawa unahudhuria ibada kila siku na kushika mambo yote unayoambiwa kanisani kwako kufanya lakini kama hauna Roho Mtakatifu ni bure…Tofauti na dini nyingine ambao kwao dini ni kitu cha kujivunia..
Hivyo kwa ufupi Dini ni njema kama itakuwa imeambata na imani ya kweli ipasavyo, ni sawa na shule yenye maabara na walimu wazuri, inamjengea mwanafunzi mazingira mazuri ya kufaulu siku za mwisho lakini shule pekee haimfanyi mwanafunzi afaulu mitihani kama hatakuwa na bidii yake binafsi..
Baada ya kujua dini ni nini na dini ya ukweli ni ipi…Ni vizuri kujua Imani ya kweli ni ipi?..Imani ya kweli ni ile iliyopo katika kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu na aliyetumwa kuja kuwaokoa wanadamu. Hiyo ndiyo imani ya kweli..Imani nyingine tofauti na hiyo ni imani ya uongo na unayopotosha na kupeleka watu mautini.
Hivyo huu Si wakati wa kijivunia dini tena…bali kujivunia wokovu katika Yesu Kristo…Hivyo kama hujaokoka na kuingia katika Imani ya kumwamini Yesu Kristo..Bado hujachelewa ingawa mlango wa Neema upo karibuni kufungwa hivyo mgeukie Kristo leo kwa kutubu dhambi zako zote na kuoshwa kwa damu yake, naye atakusamehe na kukurehemu.
Bwana akubariki sana.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
HADITHI ZA KIZEE.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
SWALI LA KUJIULIZA!
NI NINI KINAKUPATA UNAPOIPUUZIA INJILI?
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;tukiomba kwa Babaye, maombi asikiyaLakini twajikosesha, twajitweka vibaya; kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia.Haifai kufa moyo, dua atasikia.Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia;atujua tu dhaifu; maombi asikia. Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.Watu wangekudharau, wapendao dunia,hukwambata mikononi, dua atasikia.
Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;tukiomba kwa Babaye, maombi asikiyaLakini twajikosesha, twajitweka vibaya; kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.
Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia.Haifai kufa moyo, dua atasikia.Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia;atujua tu dhaifu; maombi asikia.
Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.Watu wangekudharau, wapendao dunia,hukwambata mikononi, dua atasikia.
Joseph Scriven alizaliwa mnamo 1819 katika familia ya kitajiri huko Banbridge, County Down, Ireland. Alihitimu digrii yake kutoka Chuo cha Trinity, huko Dublin mnamo 1842. Mpenzi wake alizama kwenye maji na kufa kwa bahati mbaya mnamo 1843, usiku kabla ya kuolewa.
Mnamo 1845, akiwa na umri wa miaka 25, aliondoka nchi yake ya asili na kuhamia Canada, na kukaa Woodwood, Ontario. Alibaki Canada kwa muda mfupi tu baada ya kuugua, lakini akarudi mnamo 1847
Mnamo 1855, alipokaa na James Sackville huko Bewdley, Ontario, kaskazini mwa Port Hope, alipokea habari kutoka kwa Ireland ya mama yake kuwa mgonjwa sana. Aliandika shairi la kumfariji mama yake inayoitwa “Omba bila Kukata tamaa”. Baadaye iliwekwa kwa muziki na ikabadilishwa jina na Charles Crozat Converse, ikawa wimbo wa “Yesu kwetu ni Rafiki”. Scriven hakuwa na dhamira yoyote wala ndoto kwamba shairi lake litakuja kuchapishwa kwenye gazeti na baadaye kuwa wimbo unaopendwa kati ya mamilioni ya Wakristo ulimwenguni.
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
WhatsApp
SWALI: Mwanzo 29:16 “Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. 17 Naye Lea macho yake yalikuwa DHAIFU, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. 18 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.”
Hapo Anaposema macho ya Lea yalikuwa dhaifu:Ni Udhaifu wakutokuona mbali au ni udhaifu wa namna gani huo??
JIBU: Biblia haituambii macho yake yalikuwa ni dhaifu kwa namna gani, kwamba ni makengeza, au yaliyolegea, au yenye kasoro ya kimaumbile kwamba ni makubwa sana au madogo sana au yanayoona karibu au mbali, hatujui lakini tunachojua ni kuwa alipofananishwa na mwenzake, Raheli alionekana ni mzuri kuliko yeye,…
Lakini Mungu hakuangalia hilo kama kigezo cha kuliunda taifa la Israeli, kwamba ampendelee Raheli zaidi ya Lea katika wana, kisa tu yeye ni mzuri wa sura na kwamba Yakobo kampenda zaidi…hapana kwanza utaona Lea ndiye aliyepewa uzao mkubwa zaidi, karibu nusu ya makabila yote ya Israeli yalitoka kwake isitoshe lile kabila la Bwana wetu Yesu Kristo kabila la YUDA lililoshinda makabila yote lilitoka kwa Lea…Hivyo hiyo inatufundisha pia kutokukubaliwa na watu haimaanishi kuwa hatujakubaliwa na Mungu, Yabesi alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika huzuni mpaka mama yake akamwita jina hilo ambalo lilimaanisha huzuni, Lakini Yabesi alijitahidi kuishi katika amani kwa heshima, kuliko ndugu zake wote, mpaka ikafikia wakati akamuomba Mungu dua amfanikishe katika mambo yake na Mungu akaisikia dua yake, mpaka habari yake leo hii tunaisoma katika biblia (1Nyakati 4:9-10,) …Hivyo ulemavu wowote mtu alionao haimaanishi kuwa hawezi kuwa jemadari katika ufalme wa mbinguni.
YESU MPONYAJI.
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
JIPE MOYO.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
UNYAKUO.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Kama mkristo ili uweze kuenenda kikamilifu katika safari yako ya wokovu hapa duniani bila dosari zozote zisizokuwa na sababu, ipo mistari miwili ya kuzingatia..
Wa kwanza ni huu:
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.
Na wa pili ni huu
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate KUISHI KWA KIASI, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate KUISHI KWA KIASI, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Tukiweza kutembea na kanuni hizo mbili yaani kuishi kwa Kiasi na kufanya jambo lolote kwa kumshirikisha Mungu, basi tuwe na uhakika kuwa njema zetu zitanyooka, Sasa tukirudi kwenye swali lililoulizwa kuhusu picha za video (movies), hatuwezi kusema moja kwa moja usiangalie kabisa, ni kweli hakuna asiyejua movie nyingi hazina maudhui yoyote ya kumfaa au kumjenga mkristo lakini bado hatuwezi kusema ni zote, ni kama tu vipindi vya TV vipo vilivyo vizuri na vipo vilivyo vibaya, hivyo hatuwezi kumwambia mtu asiangalie TV kabisa kwasababu kuna vipindi vibaya vingi, hapo tutakuwa tumepoteza shabaha ya kulitibu tatizo..kwasababu kwenye TV pia kuna vipindi vya mahubiri na taarifa ya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaweza kumjenga mtu kiroho au kumfunza au kumjuza.
Lakini tukiwa na kiasi, inamaana kuwa hata tukitazama movie tutazama kwa kiasi tena zile tu ambazo zinaonekana kuwa na manufaa kwa mkristo, lakini leo hii utaona mtu anatazama series, kuanzia asubuhi mpaka jioni, hana muda wa kusali, hana muda wa kujisoma biblia, hana muda wa kwenda kanisani, hana muda wa kwenda fellowship, sasa hapo hata kama movie hiyo inayo maadili kiasi gani, lakini kwa kukosa tu kile kitu kinachoitwa kiasi tayari imekuwa ni kikwazo kwake na dhambi..
Vilevile utamwona mwingine anatazama tamthilia za mapenzi, au movie zilizojaa mambo maovu maovu tu, hajui kuwa moyo wa mwanadamu unatabia ya kujazwa na kile kinachofanywa, au kinachozungumzwa au kinachowazwa muda mrefu, kwa mfano ukiwa mtu wa kutafakari Neno la Mungu kila saa na kila wakati basi lile Neno linakuwa sehemu ya maisha yako..Vivyo hivyo ukiwa ni mtazamaji wa movie ambazo hazina vimelea vyovyote vya ki-Mungu ndani yake basi utakuwa mtu wa kufuatana na hivyo unavyovitazama,..Huko huko ndipo roho za uzinzi zinapozaliwa, na uuaji, na ulevi na matusi n.k…Na hiyo yote ni kwasababu hujazingatia lile Neno linalosema lolote mfanyalo kwa Neno au Kwa tendo fanyeni yote kwa jina la Yesu Kristo…Yaani kwa lugha nyepesi kufanya kwa jina la Yesu Kristo ni kabla hujafanya unaangalia je! Hichi ninachokitazama kina umuhimu gani katika maisha yangu ya rohoni…kama hakina unakiacha, kama kinayo unakitazama, huko ndio kufanya kwa jina la YESU.
Ukiweza kutembea na mistari hiyo miwili basi hakuna jambo lolote litakalokuwa dhambi kwako, sio movie, sio radio, sio tv, sio simu, sio computa n.k.
Bwana akubariki.
JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?
JE NI SAWA KWA MKRISTO KUUZA MAZAO YA KUTENGENEZEA POMBE KAMA VILE MTAMA?
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?
JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?
NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU?
MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE”?
NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO?.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
Naomba ufafanuzi wa huu mstari Yohana 11:25-26″ Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? “
hususani hapo anaposema (naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele.) ana maana gani?
JIBU: Tunajua Yesu Kristo ndio ule mti wa uzima uliozungumziwa katika bustani ya Edeni kule mwanzo kwamba ukila matunda yake utaishi milele, na matunda yake leo hii tunayajua ni NENO lake, na neno lake ndio UZIMA wenyewe na siku zote palipo na uzima hapana kifo. Tukichunguza katika mstari huo tunaona Bwana Yesu alizungumza kwa watu wa aina mbili tofauti,Aina ya kwanza: ni “yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi”. Hili ni kundi ambalo linajumuisha watu wote waliomwamini Bwana watakaokufa watakuwa wanaendelea kuishi katika paradiso wakingojea ufufuo wa mwisho lakini kundi hili halikufanikiwa kufikia utimilifu wa imani ya kumwamini Mwana wa Mungu, hivyo basi itawapasa wafe lakini kwa kuwa walimwamini Mungu kwa sehemu ya imani watakuwa wanaendelea kuishi huko paradiso. Na ni watu wengi leo hii wanakufa katika hali hii.Aina ya pili : “naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele”. Hili ni kundi lililofikia imani timilifu ya kumwamini na kumjua sana mwana wa Mungu inayozungumziwa katika kitabu cha…
(waefeso 4:13”hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; )
hata kufikia hatua ya kushinda kifo na mauti. Mfano wa watu kama hawa tunawaona kama Henoko, Eliya, na kanisa ambalo litakuja kunyakuliwa siku ya mwisho. Hata leo hii inawezekana mtu kutokuonja mauti kabisa tukimwamini mwana wa Mungu (YESU KRISTO) katika utimilifu wote, tutachukuliwa juu hatutakufa kama ilivyokuwa kwa Eliya na Henoko, maana biblia inasema Eliya alikuwa ni mtu mwenye tabia sawa na sisi lakini kwa bidiii na kwa imani akachukuliwa juu. Mahali pengine Bwana Yesu alisema katika…
Yohana 8:51 “Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.
52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. ” mstari huu unaelezea jinsi Bwana alivyokuwa akijaribu kuwaeleza juu ya jambo hili lakini wayahudi hawakutaka kulipokea.
Sehemu nyingine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake,
Mathayo 16:28″Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. “
leo hii zipo shuhuda nyingi duniani za watu waliochukuliwa na Bwana pasipo kuonja mauti lakini shetani anataka kuwafanya watu waamini kuwa hilo jambo haliwezekani kwamba ni manabii tu wa zamani ndio walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo siku hizi hayo mambo hamna. usidanganyike katika kila kizazi Bwana ana watu wake wanaoshinda. Hivyo maneno haya yanatupa changamoto ya sisi kuongeza uhusiano wetu na Mungu kwasababu hata kanisa litakalokuja kunyakuliwa halitaonja mauti na ni lazima liwe na hiyo imani swali je! wewe unayo? kama hauna ndio wakati wa kuitafuta sasa maana Bwana Yesu mwenyewe alisema
Luka 18:8”……walakini atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?”
kwahiyo ni lazima aione imani kwanza ndipo aje hivyo tuitafute hii imani vinginevyo hatutakwenda kwenye unyakuo kumbuka ni Kristo anayetungojea sisi tuwe wakamilifu ndipo aje kutuchukua na sio sisi tunayemngojea yeye.Mungu akubariki.
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?
KUPAYUKA PAYUKA KUNAKOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NDIO KUPI?
MWANZI ULIOPONDEKA.