Je! ni kweli Bwana alimaanisha hatutaonja mauti kabisa tukimwamini?(Yohana 11:25)

Je! ni kweli Bwana alimaanisha hatutaonja mauti kabisa tukimwamini?(Yohana 11:25)

Naomba ufafanuzi wa huu mstari Yohana 11:25-26″  Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? “

hususani hapo anaposema (naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele.) ana maana gani?


JIBU: Tunajua Yesu Kristo ndio ule mti wa uzima uliozungumziwa katika bustani ya Edeni kule mwanzo kwamba ukila matunda yake utaishi milele, na matunda yake leo hii tunayajua ni NENO lake, na neno lake ndio UZIMA wenyewe na siku zote palipo na uzima hapana kifo. 

Tukichunguza katika mstari huo tunaona Bwana Yesu alizungumza kwa watu wa aina mbili tofauti,

Aina ya kwanza: ni “yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi”. Hili ni kundi ambalo linajumuisha watu wote waliomwamini Bwana watakaokufa watakuwa wanaendelea kuishi katika paradiso wakingojea ufufuo wa mwisho lakini kundi hili halikufanikiwa kufikia utimilifu wa imani ya kumwamini Mwana wa Mungu, hivyo basi itawapasa wafe lakini kwa kuwa walimwamini Mungu kwa sehemu ya imani watakuwa wanaendelea kuishi huko paradiso. Na ni watu wengi leo hii wanakufa katika hali hii.

Aina ya pili : “naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele”. Hili ni kundi lililofikia imani timilifu ya kumwamini na kumjua sana mwana wa Mungu inayozungumziwa katika kitabu cha…

 (waefeso 4:13”hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; )


hata kufikia hatua ya kushinda kifo na mauti. Mfano wa watu kama hawa tunawaona kama Henoko, Eliya, na kanisa ambalo litakuja kunyakuliwa siku ya mwisho. Hata leo hii inawezekana mtu kutokuonja mauti kabisa tukimwamini mwana wa Mungu (YESU KRISTO) katika utimilifu wote, tutachukuliwa juu hatutakufa kama  ilivyokuwa kwa Eliya na Henoko, maana biblia inasema Eliya alikuwa ni mtu mwenye tabia sawa na sisi lakini kwa bidiii na kwa imani akachukuliwa juu. Mahali pengine Bwana Yesu alisema katika…

 Yohana 8:51 “Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.

52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. ” mstari huu unaelezea jinsi Bwana alivyokuwa akijaribu kuwaeleza juu ya jambo hili lakini wayahudi hawakutaka kulipokea.

Sehemu nyingine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake,

Mathayo 16:28″Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. “

leo hii zipo shuhuda nyingi duniani za watu waliochukuliwa na Bwana pasipo kuonja mauti lakini shetani anataka kuwafanya watu waamini kuwa hilo jambo haliwezekani kwamba ni manabii tu wa zamani ndio walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo siku hizi hayo mambo hamna. usidanganyike katika kila kizazi Bwana ana watu wake wanaoshinda. Hivyo maneno haya yanatupa changamoto ya sisi kuongeza uhusiano wetu na Mungu kwasababu hata kanisa litakalokuja kunyakuliwa halitaonja mauti na ni lazima liwe na hiyo imani swali je! wewe unayo? kama hauna ndio wakati wa kuitafuta sasa maana Bwana Yesu mwenyewe alisema

Luka 18:8”……walakini atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?”

kwahiyo ni lazima aione imani kwanza ndipo aje hivyo tuitafute hii imani vinginevyo hatutakwenda kwenye unyakuo kumbuka ni Kristo anayetungojea sisi tuwe wakamilifu ndipo aje kutuchukua na sio sisi tunayemngojea yeye.

Mungu akubariki.


 

Mada Nyinginezo:

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

KUPAYUKA PAYUKA KUNAKOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NDIO KUPI?

MWANZI ULIOPONDEKA.

HADITHI ZA KIZEE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
10 months ago

Leave your message we uko sahihi
kufa ni kutomjua Mungu wala imani sahihi ya dini
kufufuka ni kumjua Mungu na kuachana na imani potofu ya awali

kila mtume alikuja kuwafufua watu wake na yule aliyekuwa akimwamini huyo mtume akamfata basi hakufa katika imani kamwe(milele) mpaka siku ya mauti yake

Meshack
Meshack
1 year ago

Sukuelewi maelezo ya Kwanza, ajapokufa atakuwa anaishi maanake mtu yeyote afaye katika dhambi huyu sawa na mfu kwa kule kutengana na mungu na mtu afaye katika bwana atakuwa anaishi kwa kuwa amekufa katika bwana na yupo pamoja na mungu mbinguni sio hayo unayoyasema unapotosha angalia usije hukumiwa