Ikiwa Mtu kafariki katika Kristo, basi lipo tumaini la kumwona tena..lakini kwa namna moja au nyingine, wafiwa watakuwa katika huzuni kwasababu hawatamwona tena kwa kitambo…hivyo yafuatayo ni maneno machache yanayoweza kuwafaa waliofiwa.
Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”
Yoshua 1:9 “Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako”.
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”
Yohana 16:22 “Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye”.
Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”
Zaburi 34:18 “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa”.
Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”
Zaburi 73:26 “Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele”
Warumi 8:18 “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu”
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” Makala haya yanatoa usafirishaji wa bila malipo kwa bidhaa zinazostahiki, http://swisswatch.is au ununue mtandaoni na uchukue dukani leo katika Idara ya Matibabu.
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”
2Wakorintho 1:3 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
1 Wathesalonike 4:13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Zaburi 147:3 Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.
Mistari ya biblia kuhusu maombi.
Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).
MAOMBI YA YABESI.
JE! MUNGU NI NANI?
Rudi nyumbani
Print this post
(Masomo maamulu kwa watumishi wa Mungu).
Je wewe ni mtumishi wa MUNGU?..Basi fuatilia mfululizo wa masomo haya katika tovuti yetu hii (www.wingulamashahidi.org).
Kama mtumishi wa Mungu kuna Anwani au nembo au Lebo ambayo inapaswa iambatane na kila fundisho unalolitoa kwa wahusika. Na Anwani/lebo hiyo/nembo hiyo si nyingine Zaidi ya “TOBA”. Hakikisha mahubiri yako yanalenga Toba, au kuwakumbusha watu umuhimu wa kujitakasa.
Kwanini iko hivyo?
Hebu tujifunze kwa mmoja ambaye ni mjumbe wa Agano, tena ndiye Mwalimu wetu MKUU na Mwinjilisti MKUU YESU KRISTO.
Yeye katika mahubiri yake yote alihubiri “Toba”.. Huenda unaweza kusoma mahali akiwa anafundisha na usione likitajwa neno Toba, lakini fahamu kuwa alikuwa anahubiri Toba kila siku katika mafundisho yake yote… Kwani biblia inasema kama yote aliyoyafanya BWANA YESU kama yangeandikwa basi dunia isingetosha kwa wingi wa vitabu.
Yohana 21:25 “Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa”
Kwahiyo Mahubiri ya BWANA WETU YESU yote Yalikuwa yamejaa toba.. sasa tunazidi kulithibitishaje hilo?.. hebu tusome maandiko yafuatayo..
Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”
Nataka tuutafakari kwa undani huu mstari… anasema “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”…. Zingatia hilo neno “TOKEA WAKATI HUO….TOKEA WAKATI HUO…TOKEA WAKATI HUO”.. Maana yake “kilikuwa ni kitu endelevu”, sio kitu cha kusema mara moja na kuacha, (hiyo ndiyo ilikuwa lebo ya mafundisho yake daima).. Kila alipohubiri lazima aliwahubiria pia watu watubu.
Umeona?. Je na wewe Mchungaji, na wewe Mwalimu wa injili, na Wewe nabii, na wewe Mtume, na wewe Mwimbaji wa injili.. LEBO YA MAHUBIRI YAKO NI IPI????.
Je! injili yako unayohubiri ni ya TOBA, au ya kuwafariji watu katika dhambi zao??.. Je unazunguka huku na kule kuhubiri injili ya namna gani?..Je ni injili ya Toba au ya Mali tu!.
Luka 24:45 “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. 46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. 48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya”
Luka 24:45 “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya”
Hakuna furaha, hakuna mafanikio, hakuna Amani ikiwa mtu yupo katika maisha ya dhambi.. utamhubiria afanikiwe lakini hata akiyapata hayo mafanikio basi dhambi itamuua tu na kumkosesha raha.. Raha pekee na Amani mtu ataipata baada ya kutubu, ndivyo maandiko yasemavyo..
Matendo 3:19 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana”
Toba ni nini?
VYA MUNGU MPENI MUNGU.
NAYAJUA MATENDO YAKO.
Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?
WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.
Swali: Toba maana yake nini?.. na je ina umuhimu gani kwetu?
Jibu: Neno “Toba” liinatokana na neno “kutubu”. Mtu anayetubu maana yake kafanya “TOBA”. Na kutubu maana yake ni “kugeuka, kutoka katika njia uliyokuwa unaiendea”.. Maana yake kama mtu ameshawishika kugeuka kutoka katika njia au mwenendo aliyokuwa anauendea kwa njia ya majuto na maombi ya kuomba msamaha kama njia hiyo ilikuwa ni kwanzo kwa mwingine, mtu huyo anakuwa ametubu, au amefanya TOBA.
Kibiblia mtu aliyegeuka na kuiacha njia ya dhambi aliyokuwa anaiende na kuomba msamaha kwa Mungu wake aliyemkosea, basi mtu huyo anakuwa amefanya TOBA, na ndio hatua ya kwanza kabisa ya Mtu kumsogelea MUNGU, hakuna njia nyingine tofauti na hiyo!.
Injili ya Yohana Mbatizaji na ya BWANA YESU (Mjumbe wa Agano jipya) ilianza na Toba.
Yohana 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, 2 TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Yohana 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2 TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Maana yake watu waageuke na kuacha maisha ya kuabudu sanamu, waache maisha ya mauaji, waache maisha ya uzinzi na uasherati, waache maisha ya ulevi na utukanaji n.k.. kwasababu Ufalme wa mbinguni hautawapokea watu wa namna hiyo.
Lakini pia si kutubu tu, bali ni pamoja na “KUZAA MATUNDA YAPATANAYO NA HIYO TOBA”.. Maana yake baada ya kugeuka na kuacha dhambi, basi mwongofu huyo anapaswa ajifunze kuishi maisha yanayoendana na toba yake hiyo, maana yake asirudie tena machafu ya nyuma yatawale maisha yake.
Luka 3:8 “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto”.
Je na wewe umetubia dhambi zako na kumkaribisha YESU maishani mwako? Kama bado basi fungua hapa ufuatilize sala hii ya TOBA na KRISTO YESU ataingia maishani mwako kwa Imani >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Maran atha!
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
Swali: Je wakristo tunaruhusiwa kukopa benki au kutoka kwa watu?..kama ni ndio, kwanini maandiko yaseme mtakopesha wala hamtakopa? (Kumbukumbu 15:6).
Jibu: Turejee..
Kumbukumbu 15:6 “Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao”
Kuna kukupa kwa aina mbili; 1) KWA AJILI YA KUTATUA TATIZO/JANGA…. 2) KWAAJILI YA KUJITANUA.
1. KUKOPA KWAJILI YA KUTATUA MATATIZO.
Kukopa kwa namna hii ni ile hali ambayo, mtu anapatwa na baa Fulani au janga, hivyo ili kujikimu au kujikidhi anakwenda kutafuta msaada kwa njia ya kukopa!.. Sasa kukopa kwa namna hii ndiko kunakozungumziwa hapo katika Kumbukumbu 15:6 (kwamba tutakopesha wala hatutakopa).
Na kwanini tutakuwa watu wa namna hiyo (ya kutokukopa)?.. ni kwasababu Mungu ni msaada wetu ambaye hataruhusu tupate matatizo hayo pasipo kuwa na sababu yoyote. Hivyo tutabaki katika usalama wake ambao utatuhifadhi dhidi ya madhara yote ya yule adui.
Hivyo kama mkristo ukiona unapitia vipindi vya mfululizo vya kukopa ili kukidhi mahitaji yako ikiwemo chakula, basi jaribu kulitazama jambo hilo kiroho Zaidi, na Bwana atakusaidia kukutoa hapo!.
2. KUKOPA KWAAJILI YA KUJITANUA.
Hii ni aina ya pili ya UKOPAJI, ambayo biblia haijaikataza!.. Inapotokea huna janga lolote, huna baa lolote, na unaishi vizuri kwa katika neema ya Mungu, kiasi kwamba ukipatacho kinakidhi hali ya kutokuwa na haja ya kukopa!.. Lakini ukapenda kujitanua Zaidi ya hapo kifedha au kibiashara au kimiradi kama mtu wa Mungu, na ukaamua kwenda kukopa ili kuongeza labda ule mtaji ulio nao ili kutanua kazi au biashara..
Kukopa kwa namna hii “hakujakatazwa kwa mkristo” na wala hakumaanishi kuwa wewe ni maskini, kwasababu hata watu wengi walio matajiri sana pia wanakopa!!.. lengo lao la kukopa si kukidhi mahitaji (kwamba wana janga fulani au baa fulani, hivyo wasipopata huo mkopo wanaweza kudhurika) bali mara nyingi ni kwa lengo la kutanua biashara zao wazifanyazo au miradi yao.
Na Mkristo anapofikia mahali anahitaji kutanuka Zaidi anaweza kuchukua mkopo, na isiwe na tafsiri yoyote kwamba ni maskini au muhitaji, na kwamba pasipo huo hawezi kuishi.
Kanuni ya KUKOPA ni sawa na ile ya KUUZA tu!… Mtu anayeuza shamba kwaajili ya matatizo, ni tofauti na yule anayeuza shamba kama biashara!..kadhalika mtu anayekopa kwaajili ya kutatua matatizo/au janga Fulani ni tofauti na yule anayekopa kwaajili ya kujitanua.
Bwana atusaidie katika yote.
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
Rehani ni nini katika biblia?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.
Tunapokisoma kisa cha Daudi, cha kumwiba mke wa shujaa wake (Uria), na kumlazimisha kuzini naye kwa siri, na baadaye kumuua mumewe , (2Samweli 11) tunaishia kuona picha mbaya sana ya Daudi. Na kumshutumu, na wengi wetu kusema Daudi ni mzinzi sana, iweje apendwe na Mungu namna ile, tena awe kipenzi cha Mungu?
Ni kweli kabisa alichokifanya Daudi hakistahili kufanywa na mtu yeyote, ambaye anamjua Mungu, mfano wa Daudi. Lakini kuna funzo kubwa sana ambalo wengi wetu hatulioni nyuma ya maisha ya Daudi baada ya pale.
Daudi alipozama katika dhambi ile, na kugundua makosa yake. Alikuwa na badiliko lisilo kuwa la kawaida. Sio kule alikokuwa anaomboleza usiku kucha, Hapana, lile lingekuwa la “kufoji” tu, ambalo yoyote anaweza kulifanya hata leo. Kinyume chake Daudi alikuwa na badiliko la kimatendo. Na hilo ndilo lililomfanya apendwe sana na Mungu.
Kwa namna gani?
Sasa angalia Daudi Yule Yule ambaye alikuwa ni mzinzi, mwenye tamaa ya hali ya juu,akiona tu mwanamke mzuri hajali, huyu ni mke wa mtu au la yeye alimwiba na kuzini naye. Lakini Dakika zake za mwisho hazikuwa hivyo. Alibadilika kwelikweli baada ya dhambi ile.
Utakumbuka hata alipokuwa mzee, Wakuu wa Israeli walikwenda kumtafutia Binti mzuri bikira katika taifa lote la Israeli, ili amlalie Daudi ampe joto kwasababu nguo za joto hazikutosha. Lakini biblia inasema Daudi alipolala naye ‘hakumjua’.
Kwa jinsi ya kibinadamu, binti alale, na mtu mwenye sifa ya tamaa kama Daudi, halafu asimwingilie. Lazima kutakuwa kuna jambo lingine limetendeka ndani ya maisha ya huyo mtu.
Tusome;
1 Mfalme 1:1
“Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto. 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto. 3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme. 4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
“Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.
4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
Ni wazi kuwa habari hiyo ilijulikana Israeli nzima, Daudi amelala na binti bikira mrembo miaka kadhaa lakini hajamwingilia. Ni shujaa kiasi gani. Hawakujua kuwa anawathibitishia Israeli kuwa yeye sio Yule wa zamani, sio Yule mzinzi mliyemzoea, ameshabadilika. Si mtu wa kulipuka lipuka tamaa ovyo kama alivyokuwa hapo mwanzo.
Hiyo ndio sababu Mungu alimpenda Daudi. Kwasababu alikuwa na badiliko la dhati Kwa Mungu wake. Je! Na sisi, tunaweza kusema tumeuacha ulimwengu kweli kweli pale tunapomgeukia Mungu, au tutakuwa na vimelea vya kidunia ndani yetu, pale tunapokutana na majaribu kama yale yale ya mwanzo. Tulipokuwa wazinzi na sasa tumeokoka, Je! Tuna ujasiri wa kuishi maisha ya mbali zinaa, au bado tupo nusu nusu.
Tuwe na badiliko la dhati, leo tumeanguka katika dhambi Fulani mbaya, sasa tumetubu, tusiwe tena walewale wa kuanza kuangalia angalia nyuma kama mke wa Lutu. Mungu atakuchukizwa na sisi na mwisho wa siku tutakuwa jiwe la chumvi kama sio kutapikwa mfano wa kanisa la Laodikia.
Tumaanishe kwelikweli kuacha mambo maovu tuliyoyazoelea. Jifunze kwa Daudi. Yule sio mzinzi kama wewe unayejitumaisha kwa visa vyake vya zamani, ukadhani kuwa utanusurika hukumu ikiendelea na tabia hiyo.
Shalom.
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?(Opens in a new browser tab)
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 4
Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?
(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
Rehani ni nini kibiblia?, na je sisi wakristo tunaruhusiwa kuweka kitu rehani?
Rehani ni mali iliyowekwa kama dhamana kwa mkopo uliochukuliwa, maana yake mkopo usipolipwa basi mali ile inachukuliwa ili kufidia ule mkopo.
Katika biblia (Agano la kale), Rehani iliruhusiwa lakini kwa kuiangalia hali ya mtu. Kama mtu alikuwa ni tajiri mwenye uwezo basi alipokopa alipaswa aweke rehani mali itakayosimama badala ya ule mkopo endapo atashindwa kuulipa.
Lakini kama mtu alikuwa ni maskini sana, na hana kitu isipokuwa jiwe la kusagia tu na mavazi, basi hakupaswa kutozwa rehani katika hivyo alivyo navyo, ilikuwa ni dhambi kubwa kutwaa jiwe la kusagia la maskini au mavazi yake kama Rehani.
Kumbukumbu 28: 6 “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani”.
Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani; 18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”.
Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”.
Kwa urefu kwanini si sawa kutwaa jiwe la kusagia la maskini kama rehani waweza kufungua hapa >>>Kwanini jiwe la kusagia Mungu alikataza lisiwekwe rehani? (Kumbukumbu 24:6).
Sasa swali je na sisi wakristo ni sahihi kuweka kitu rehani au kupokea rehani kutoka kwa mtu tuliyemkopesha?
Jibu: Rehani haijakatazwa katika biblia, kama umemkopesha mtu kitu cha thamani, na mtu huyo si ndugu yako katika Imani (yaani mpendwa mwenzako) au si ndugu yako katika mwili (yaani mwanafamilia) waweza kupokea Rehani, ili kumhamasisha kurejesha lile deni, (ikiwa lengo lako si kumkandamiza bali kumhamasisha na kama mtu huyo uwezo huo anao).
Lakini kama ni maskini na kaja kukopa kwako, si vizuri kuchukua rehani. Waweza kumkopa bila rehani yoyote, ni itakuwa baraka kwako.
Lakini kama ni ndugu yako katika Imani na katika damu, si vyema kumtoza rehani, wala riba, katika mazingira yoyote yale, awe tajiri au maskini, waweza kumkopa ukitumai kuwa atakulipa tu pasipo kutaka dhamana.
Lakini pia kama wewe ni mkopaji, (maana yake unakopa kutoka kwa mtu/taasisi kwaajili ya shughuli fulani) si dhambi kusimamisha kitu kama rehani itakayosimama kwaajili ya mkopo wako (kama mtu huyo au taasisi hiyo inahitaji hayo yote).
“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
LIONDOE JIWE.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Rahabu ni nani?
Jina “Rahabu” limeonekana mara kadhaa katika biblia likiwa na maana Zaidi ya moja. Maana ya kwanza ni linamwakilisha Mwanamke wa kikanaani aliyekuwa kahaba, aliyewahifadhi wapelelezi wa kiisraeli walioingia kuipeleleza Yeriko, na maana ya pili Taifa la Misri.
Kama tu vile neno “Mharabu” katika biblia linamaanisha Jamii ya watu wa Arabia, lakini pia linamaanisha “Mtu au Malaika anayeharibu Vivyo hivyo na jina Rahabu lina maana Zaidi ya moja.
1.RAHABU (Kahaba).
Habari ya Rahabu aliywakuwa kahaba tunaipata katika kitabu cha Yoshua mlango wa 2 na wa 6. Mwanamke huyu aliwahifadhi wapelelezi wa kiisraeli walioingia Yeriko kuipeleleza nchi ile.
Yoshua 2:1 “Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. 2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi. 3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. 4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka”
Yoshua 2:1 “Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi.
3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.
4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka”
2.TAIFA LA MISRI.
Jina Rahabu pia katika biblia limetumika kuwakilisha Joka kubwa la baharini ambalo ufunuo wake ni Taifa la Misri.
Isaya 30:7 “Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida; Kwa hiyo nimemwita, Rahabu aketiye kimya” Isaya 51:10 “Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?”
Isaya 30:7 “Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida; Kwa hiyo nimemwita, Rahabu aketiye kimya”
Isaya 51:10 “Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?”
Zaburi 87: 4 “Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo”
Soma pia Ayubu 26:12, na Zaburi 89:10..
Jambo kubwa na kuu tunaloweza kujifunza kwa RAHABU (Aliyekuwa Kahaba) ni IMANI.
Alikuwa na Imani juu ya mambo yatarajiwayo sawasawa na Waebrani 11:1. Aliziamini nguvu za MUNGU wa Israeli, hivyo akajua yatakayofuata baadaye kuwa ni anguko la Yeriko, hivyo akatafuta njia ya kujinusuru yeye na familia yake kwa kujiungamanisha na jamii ya Israeli.
Waebrania 11:31 “Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani”.
Yakobo 2:25 “Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa”.
Yakobo 2:25 “Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa”.
Maran atha.
RAHABU.
LAANA YA YERIKO.
Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.
Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Machukizo au Chukizo ni nini? kama tunavyosoma katika biblia?
Machukizo linatokana na neno “chukizo” na chukizo ni kitu kinachosababisha chuki/hasira. Kwa Mungu kitu chochote kinachoipandisha ghadhabu yake kinaitwa “chukizo”.
Na vitu vifuatavyo ndivyo vilivyokuwa machukizo kwa MUNGU.
1. Ibada ya Sanamu.
Sanamu ya aina yoyote ile ilikuwa ni machukizo kwa Mungu na hicho ndicho kitu cha kwanza kilichokuwa kinaletea wivu kwa Mungu.
Kumbukumbu 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina”.
Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo. 17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa”.
Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.
17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa”.
Soma pia Kumbukumbu 27:15, na 2Wafalme 23:24
2. Uasherati na ulawiti.
Walawi 18: 22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.
Soma tena Mambo ya Walawi 20:13
3. Mavazi yasiyopasa.
Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”
Mfano wa mavazi yasiyopasa, ni suruali kwa mwanamke, na nguo mfano wa magauni kwa wanaume.
4. Sadaka yenye kasoro.
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.
Kumbukumbu 17:1 “Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.
Na yapo machukizo mengine mengi!.
Lakini pia lipo chukizo moja KUU na KUBWA ambalo litatokea kule YERUSALEMU, ambalo ni CHUKIZO LA UHARIBIFU, linalomhusu Mpinga-kristo.
Kwa upana juu ya CHUKIZO LA UHARIBIFU, basi fungua hapa >>CHUKIZO LA UHARIBIFU
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.
Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Swali: Huyu Kemoshi alikuwa nani, na nini tunajifunza kutoka kwake?
Jibu: Turejee,
Yeremia 48:46 “Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani”.
“kemoshi” hakuwa mtu bali alikuwa ni “mungu” wa watu wa Moabu. Kumbuka kila taifa lilikuwa na mungu wake; Israeli walikuwa na MUNGU wao ambaye ni YEHOVA, Muumba wa mbingu na nchi, Tiro walikuwa na mungu wao anayeitwa “baali”, Sidoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “ashtoreti”, wana wa Amoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “milkomu”. N.k na hawa wana wa Moabu mungu wao ndio anayekuwa anaitwa “kemoshi” ambaye kiuhalisia ni “pepo”.
Sasa utaona Mungu aliwakataza wana wa Israeli wasiabudu miungu mingine tofauti na yeye…lakini wapo waliotii na wapo waliokaidi na kuamua kuifuata miungu hiyo ya mataifa mengine na kuiabudu na kuisujudia. Na Mfalme Sulemani alikuwa miongoni mwa waliokengeuka dakika za mwisho kwa kuifuata miungu hiyo ya mataifa, ingawa baadaye alikuja kutubu.
2Wafalme 23:13 “Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, MFALME WA ISRAELI, KWA ASHTORETHI, CHUKIZO LA WASIDONI, NA KEMOSHI, CHUKIZO LA MOABU, NA MILKOMU, CHUKIZO LA WANA WA AMONI, mfalme akapanajisi”.
Hii miungu hata leo inaabudiwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Africa, isipokuwa katika majina mengine tofauti na hayo.
Mila nyingi za kiafrica asili yake ni miungu hii, kwamfano mungu wa wasidoni aliyeitwa Ashtorethi alikuwa ni mtu wenye kuchongwa maumbile ya mtu, na kusujudiwa, na kufanyiwa matambiko..na sasa jamii nyingi na makabila mengi (ikiwemo na wakristo) wanafanya hayo hayo wanapokutanika katika vijiji vyao, pasipo kujua kuwa ni ibada za sanamu kama zile zile tu ambazo mataifa wasiomjua Mungu walikuwa wanazifanya.
Bwana atusaidie tuepukane na ibada hizo za sanamu.
Mistari mingine inayomtaja huyo mungu “kemoshi” ni pamoja na Hesabu 21:9, Waamuzi 11:24, 1Wafalme 11:7, 1Wafalme 11:33, Yeremia 48:7, na Yeremia 48:13.
Moabu ni nchi gani kwasasa?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?
MNGOJEE BWANA
USIJITUMAINISHE JUU YA SIRA YAKO ANGALI UPO KATIKA DHAMBI.
Antiokia ipo nchi gani kwa sasa? Na nini tunaweza kujifunza kupitia mji huo?
Jibu: Antiokia ni mji uliopo kusini mwa Taifa la UTURUKI na Kaskazini mwa Taifa la SIRIA.
Mji huu una historia kubwa sana ya kanisa, kwani ndicho kitovu cha jina “Ukristo”. Maandiko yanasema Wanafunzi (yaani watu waliomwamini YESU na kumfuata) waliitwa “wakristo” kwanza hapo Antiokia na si Yerusalemu kanisa lilipoanzia.
Matendo 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA. 27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia”.
Matendo 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA.
27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia”.
Antiokia ni mji uliomiminiwa uliokuwa na Neema ya Ukristo kuliko miji mingi, lililojaa Mitume, manabii na waalimu.. kwani hata Mtume Paulo safari yake ya kuanza kuhubiri injili ilianzia pale.
Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao. 4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro”.
Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.
2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro”.
Matendo 14:26 “Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza”.
Mji wa Antiokia kwasasa umejaa wa Islamu kutokana na Taifa hilo la Uturuki kuwa la kiislamu, ingawa kuna asilimia ndogo ya wakristo wanaoishi humo. Mahali ambapo uamsho mkubwa wa injili ulianzia sasa adui kapateka na kupafanya kuwa mji wa kipagani… Na miji mingine imenyanyuka yenye uamsho kuliko huo, sawasawa na Neno lile..
Marko 10:31 “Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”
Hivyo hiyo ni tahadhari hata kwetu, “Tushike tulicho nacho, mpaka mwisho adui asije akatupokonya taji yetu”.
Mji wa Antiokia mwaka 2023, Februari 6 kulitokea tetemeko kubwa sana lililoua watu elfu 55, na kuharibu makazi mengi sana.
Bwana atusaidie tuwe na mwisho mwema.
Yerusalemu ni nini?
Ninawi ni nchi gani kwasasa?
MJI WENYE MISINGI.
Babeli ni nchi gani kwasasa?
DANIELI: Mlango wa 8