Jibu: Turejee…
Matendo 7:58 “wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi WAKAWEKA NGUO ZAO MIGUUNI PA KIJANA MMOJA ALIYEITWA SAULI. 59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu”.
Matendo 7:58 “wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi WAKAWEKA NGUO ZAO MIGUUNI PA KIJANA MMOJA ALIYEITWA SAULI.
59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu”.
Zipo tafiti zinasema kuwa zamani za biblia, akipatikana mtu na kosa la kustahili kuuawa kwa kupigwa mawe, basi wale mashahidi waliolishuhudia kosa la huyo mtu, kabla ya kutekeleza mauaji walivua nguo zao kama ishara ya kiapo walichokitoa/ushahidi kuwa ni kweli.
Lakini dhana hiyo haina marejeo yoyote ya biblia, hivyo si ya kusadikika.
Lakini sababu pekee yenye kuleta maana ya mavazi ya mashahidi kuwekwa miguuni mwa Sauli ni ili wawe wepesi katika kutekeleza zoezi hilo la mauaji.
Ni kawaida wana michezo au wapiganaji kupunguza mavazi yao kabla ya mchezo kuanza ili wawe wepesi, ndicho walichokifanya hawa mashahidi, walipunguza mavazi yao ya nje, na kumpatia kijana Sauli awahifadhie kwa muda na baadae wazichukue baada ya kumuua Stefano.
Na tunasoma Sauli (ambaye baadaye ndiye aliyekuja kuwa Paulo), alikubali kuwatunzia..
Matendo 22:20 “Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua”.
Sasa ni kwanini Bwana MUNGU aruhusu mavazi ya wauaji yatunzwe na Sauli?.
Sababu kuu ni kwamba Bwana MUNGU alijua Sauli atakuja kugeuka baadaye na kuwa mtumishi wake kwa watu wa Mataifa.
Hivyo kitendo cha zile nguo kuwekwa miguuni mwa Sauli ni kuweka sababu baadae ya Wayahudi pamoja na wakristo waliopo Yerusalemu kumkataa, ili aende kwa watu wa mataifa…
Kwani watakapokumbuka lile tendo la kushiriki kwake kumuua Stefano, wamkatae na kumwona hafai..
Matendo22:17 “Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho, 18 nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, KWA SABABU HAWATAKUBALI USHUHUDA WAKO katika habari zangu. 19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi. 20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua. 21 Naye akaniambia, Enenda zako; KWA KUWA NITAKUTUMA UENDE MBALI KWA WATU WA MATAIFA”.
Matendo22:17 “Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho,
18 nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, KWA SABABU HAWATAKUBALI USHUHUDA WAKO katika habari zangu.
19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi.
20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua.
21 Naye akaniambia, Enenda zako; KWA KUWA NITAKUTUMA UENDE MBALI KWA WATU WA MATAIFA”.
Na utaona faida ya Paulo kuhubiri kwa watu wa Mataifa ndio mazao ya nyaraka zote za Paulo, ambazo mpaka leo zimekuwa msingi wa Neno la Mungu.
Tunachojifunza zaidi kuwa yapo makosa ambayo yalitokea zamani, na MUNGU aliyaruhusu yatokee kwasababu yamebeba kusudi kubwa mbeleni.
Makosa mengine yaliruhusiwa zamani ili yatuondolee viburi leo, mengine yaliruhusiwa ili tupate fursa njema leo, na mengine ni ushuhuda kwa wengine na maonyo kwa wengi e n.k
Hivyo kila jambo lina kusudi lake.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.
Rudi Nyumbani
Print this post
Swali: Je ni sahihi kusema waraka fulani wa Mtume Paulo ni kwaajili ya kanisa fulani tu?…Mfano waraka wa Wakorintho uliwahusu Wakorintho tu peke yao hivyo si vitu vyote vya kuchukua huko…
Vile vile waraka wa Waefeso uliwahusu waefeso peke yao? Na si makanisa yote ikiwemo sisi, hivyo kuna vitu si sahihi kuvibeba kutoka kwenye waraka huo?.
Jibu: Awali turejee salamu za kwanza za Paulo kwa baadhi ya makanisa…
Wakolosai 1:1 “Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, 2 kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, WALIOKO KOLOSAI. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu”.
Wakolosai 1:1 “Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu,
2 kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, WALIOKO KOLOSAI. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu”.
Ni kweli hapa anaonyesha kuwa waraka huu umekusudiwa kwa wakristo walioko KOLOSAI…
Lakini swali ni je?…ni wakristo walioko Kolosai tu ndio waliokusudiwa wasome huu waraka au hata makanisa mengine ya mahali pengine ikiwemo sisi tuishio wakati huu wa mwisho?.
Jibu la swali hili tutalipata katika waraka huu huu wa Wakolosai…
Wakolosai 4:16 “Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi”.
Kumbe ulikuwepo waraka mwingine ulioandikwa wa kanisa la Laodikia ambao ungepaswa usomwe kwa Wakolosai, na huu wa Wakolosai ulipaswa ukasomwe kwa kanisa la Laodikia.
Ikiwa na maana kuwa nyaraka za Paulo, ijapokuwa alizipeleka katika kanisa husika lakini hakuzizuia zisisomwe katika makanisa mengine, kwasababu mambo aliyokuwa anayahubiri kanisa moja na kuyakemea ndio hayo hayo atakayoyafundisha na kuyakemea katika makanisa mengine, na ndio hayo hayo pia yanatufaa katika makanisa ya siku za mwisho.
Utaona pia salamu ya kwanza ya Paulo kwa Wagalatia, ilihusu makanisa yote yaliyopo Galatia na si kanisa moja tu….
Wagalatia 1:1 “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), 2 na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia”.
Wagalatia 1:1 “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu),
2 na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia”.
Maana yake kama makanisa yaliyokuwepo Galatia yalikuwa mia (maana Galatia ilikuwa ni kubwa mno, tazama ramani)..basi makanisa yote yalisomewa huo waraka pasipo kujalisha tabia zao.
Pia utazidi kulithibitisha hilo katika kitabu cha waraka kwa Wakorintho, utaona Paulo anaelekeza kuwa si kwa Wakorintho peke yao bali na kwa watu wote wanaoliitia jina la Bwana kila mahali ikiwemo sisi..
1 Wakorintho 1:1 “Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu”
1 Wakorintho 1:1 “Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu”
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba nyaraka zote za Mtume Paulo na biblia yote kwa ujumla yafaa kwa mafundisho kwa makanisa yote na vizazi vyote..
2 Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki”
Hivyo si sahihi kusema waraka huu waliandikiwa Wakorintho tu peke yao au Wagalatia bali unatuhusu hata sisi..
Mafundisho yaliyohusu utakatifu ikiwemo kujisitiri na kuishi maisha ya kuepuka dhambi yaliwahusu watu wa kanisa la kwanza na yanatuhusu sisi pia..
Mafundisho yanayohusu nafasi za wanawake na wanaume katika kanisa sawasawa na 1Wakorintho 14:34 na 1Timotheo 2:8-12, yanatuhusu hata sisi.
Kupunguza Neno lolote katika biblia ni kosa, Bwana atusaidie.
Shalom
ISHARA YA KANISA LA LAODIKIA
Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wakorintho wa kwanza (1Wakorintho)
Uchambuzi na mwandishi wa kitabu cha Waefeso.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Biblia inasema nini kuhusu mtu ‘Mwenye kujipendekeza (Mithali 29:5)
WhatsApp
Arkipo ni mmoja wa wahudumu wa agano jipya. Ambaye alikuwa na ushirika wa karibu na mtume Paulo katika kazi ya kuieneza injili.
Paulo alipokuwa anamwandikia waraka Filemoni, anamtaja Arkipo kama ASKARI mwenzake.
Filemoni 1:1-2
[1]Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, [2]na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.
[1]Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi,
[2]na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.
Lakini pia katika waraka ambao Paulo aliundika kwa Wakolosai tunaona katika salamu zake za mwisho, anatoa agizo maalumu kwa mtu huyu kwa kumwambia, aiangalie sana huduma Ile aliyopewa na Bwana ili aitimize.
Wakolosai 4:17
[17]Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.
Kuonyesha kuwa alikuwa na sehemu ya huduma kwa hawa watakatifu wa Kolosai. Ijapokuwa biblia haijatueleza ni huduma ya namna gani.
Lakini ni kwanini amwambie vile?
Paulo anasisitiza kuwa huduma hiyo amepewa na Bwana, (ikiwa na maana si mwanadamu)..huwenda alidhani alichokirimiwa hakikuwa na msukumo kwa Bwana, ni yeye tu mwenyewe ameanza kukitenda..Au watu wamekipuuzia au kukiona cha kawaida, hivyo na yeye pia akakiona cha kikawaida, hakitakiwi kutiliwa mkazo sana.
Au Pengine Arkipo alipitia kuvunjwa moyo, au mashaka fulani, na hiyo ikampelekea kutowajibika vya kutosha katika nafasi yake.
Hivyo Paulo anamtia moyo kwa kumwambia huduma hiyo ni ya Mungu, hivyo hakikisha unaitimiza.
Ni lipi la kujifunza kwa Arkipo.
Hata sasa kila mtu aliyeokoka ni askari wa Bwana. Na hivyo amepewa huduma ndani yake, kufuatana na karama aliyokirimiwa ambayo anapaswa aiangalie na kuitimiza.
Kama askari wa Bwana ni lazima tufahamu kuwa tutakumbana na vita na kuvunjwa moyo, na kutaabishwa, na dhiki, na kupungukiwa, na taabu za namna mbalimbali lakini pia Raha katika huduma.
Kwa vyovyote vile Hatupaswi kupoa, au kulegea, au kuvinjika moyo. Bali tubakie tufahamu kuwa ipo siku tutatolea hesabu uwakili wetu.
Kama askari ya Kristo Timiza huduma yako
Shalom.
Mhunzi ni nani? (Isaya 54:16)
Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?
Kuwanda ni kufanya nini?
Aristarko ni mmoja wa wahudumu wa injili katika agano jipya. Paulo anamtaja kama mtenda kazi pamoja naye (Filemoni 1: 24), wengine wakiwa ni Luka, dema, na Marko.
> Aristarko ni mmoja wa watu walioamini injili mahali palipoitwa Thesalonike, Paulo alipokuwa anahubiri, ambao kwa mioyo yao wenyewe wakaamua kuambatana na Paulo katika ziara zake za kuhubiri injili kwenye mataifa mengine.
Matendo ya Mitume 20:4
[4]Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.
> Kati ya watendakazi wa Paulo waliovamiwa na kundi la mataifa ( Paulo aliwaita hayawani wakali) kule Efeso, mmojawapo alikuwa ni Aristarko. Ijapokuwa biblia haituambii kama walipigwa au kuwajibishwa vikali…Lakini ni wazi kuwa walipitia dhiki na hwenda ilikuwa ni kupigwa kwelikweli.
Matendo ya Mitume 19:29
[29]Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia mahali pa michezo kwa nia moja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.
> Aristarko anatajwa pia na Paulo kama mfungwa mwenza. Kuonyesha kuwa si tu alishiriki mapigo, bali pia na vifungo pamoja na Paulo, tangu kwenye safari yake akiwa kama mfungwa kuelekea Rumi, mpaka Rumi kwenyewe alipokuwa mfungwa kwenye nyumba yake mwenyewe.
Matendo ya Mitume 27:2
[2]Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi.
Wakolosai 4:10
[10]Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Kwa ufupi, tunaweza jifunza mengi kwa watendakazi kama hawa, ambao walikuwa washirika wenza wa Paulo. Kwanza kwa kujitoa kwao kwa hiari kuitumikia injili. Lakini kuzidi kuwa thabiti hata katika mapigo na vifungo bila kuikana imani. Kwamfano tunapoisoma ile safari ya Paulo kama mfungwa kuelekea Rumi jinsi walivyopitia majanga makubwa baharini, mpaka wakakata tamaa ya kuishi, huyu aristarko alikuwa pia katika dhoruba ile.
Kufanikiwa kwa huduma ya mtume Paulo ni kwasababu ya mashujaa kama hawa walioisimama pamoja naye katika nyakati zote.
Bwana awanyanyue wakina Aristarko wengi, kwenye makanisa yetu na huduma zetu. Ili injili ya Bwana ifike na kuenea kiwepesi ulimwenguni kote.
Ndugu Yule anayezungumziwa kwenye 2Wakorintho 8:18 ni nani?
Sosthene ni nani katika biblia? (Matendo 18:17)
Mchuuzi ni nani? (Hosea 12:7).
MIMI NA WEWE TU KAZI YA MUNGU.
Sosthene ni mmoja wa wahudumu wa injili Katika agano jipya. Mshirika mmojawapo wa mtume Paulo, katika kazi ya kuitetea injili.
Katika kitabu cha matendo anatajwa kama mkuu wa sinagogi, kule Korintho
Matendo ya Mitume 18:17
[17]Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.
[17]Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya
kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.
> Alikuwa ni mmoja wa wayahudi(washika-sheria), waliokutana na injili ya Paulo na kuamini.
Paulo alipofika Korintho Mungu alimtokea katika maono na kumwambia asiogope aendelee kuhubiri kwasababu katika Mji huo anao “watu wake wengi”
Hivyo aliendelea kuhubiri kwa ujasiri mwingi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu na watu wengi sana miongoni mwa wayahudi waliamini ikiwemo huyu Sosthene na Krispo.
Matendo 18:9-11
[9]Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, [10]kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. [11]Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu
[9]Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,
[10]kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.
[11]Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu
Baadaye wayahudi wenye wivu waliamka kinyume cha Paulo, na kumpeleka mbele ya Galio liwali ili ashitakiwe kwa kuleta machafuko ndani ya dini yao.
Lakini Galio akawatawanya kwasababu kesi yao haikuwa ya uhalifu au dhuluma bali ya mambo ya kiimani..Ambayo kwa mujibu wa sheria za kirumi hazisikilizwa kwenye mahakama zao.
Hivyo wayahudi kuona Paulo hajahukumiwa, wakamkata huyu Sosthene mkuu wa Sinagogi na kumpiga mbele ya kiti cha hukumu. Na hiyo yote ni kutokana na kwamba aliisapoti huduma ya Paulo, pengine aidha kwa kumruhusu ahubiri injili ndani ya masinagogi yao au kwa kutochukua hatua zozote stahiki dhiki ya injili ya mtume Paulo.
Lakini pia tunakuja kuona baadaye Paulo wakati anaandika waraka kwa Wakoritho anamtaja Sosthene kama mshirika mwenza wa utume wa Kristo.
1 Wakorintho 1:1
[1]Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
Hiyo ni kuonyesha kuwa alikuja kuwa nguzo hasaa kwa watakatifu wa Korintho. Mpaka Paulo anamtaja kama mshirika mwenza.
Ni Nini cha kujifunza katika habari ya Sosthene?
Ni kuonyesha uweza wa Mungu wa kugeuza watu wa aina zote. Kikawaida kwa taratibu za kiyahudi mpaka mtu ameaminiwa kuwa mkuu wa sinagogi, maana yake ni kuwa mtu huyo amethibitishwa kuijua na kuishiya torati kwelikweli na nidhani zote za kiyahudi na taratibu zao.
Kwahiyo kwa mtu kama Sosthene kubadilika ghafla na kuwa mfuasi wa injili, haikuwa rahisi, ilihitaji neema ya Mungu kubwa, ndio maana kwa wayahudi alionekana kwa mwasi wakampiga sana.
Bwana anataka tusibague wa kuwahubiri injili, kwasababu injili ni uweza wa Mungu(Warumi 1:16), Umwonapo imamu mhubirie, Shehe mhubirie, Buddha mhubirie, baniani mhubirie, padri, askofu, mganga wa kienyeji..wahubirie kwasababu hapo ulipo kuna “watu wa Mungu wengi sana” hujua ni yupi Bwana aliyemkusudia kuwa chombo chake kama Sosthene.We hubiri tu.
Bwana akubariki
MKUU WA GIZA.
Tikiko ni nani kwenye biblia?
Tikiko ni mmoja wa washirika waliohudumu na mtume Paulo katika kazi injili. Ijapokuwa si mtu anayejulikana sana..lakini ametajwa sehemu kadha wa kadha katika vitabu vya agano jipya.
> Anatajwa kama mmoja wa watu waliomua kufuatana na Paulo katika ziara za injili maeneo mbalimbali (Makedonia na Asia).
Matendo ya Mitume 20:3-4
[3]Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia. [4]Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.
[3]Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
> Paulo anamtaja pia kama Mhudumu mwaminifu katika Bwana. Maana yake aliupima uaminifu wake, akauthbitisha kuwa hauna unafiki, mpaka akamfanya kama mbeba taarifa zake za kihuduma kwa makanisa.
Waefeso 6:21
[21]
Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
Wakolosai 4:7-8
[7]Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; [8]ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu;
[7]Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;
[8]ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu;
> Lakini pia kwa jinsi Paulo alivyomtaja tunaweza kusema alisimama kama mwangalizi-mwenza wa viongozi wa makanisa.
2 Timotheo 4:12
[12]Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso.
Tito 3:12
[12]Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.
Hivyo ijapokuwa si mtu aliyemaarifu, lakini alifanyika nguzo si tu katika mafanikio ya huduma ya mtume Paulo lakini pia kwa makanisa ya Mungu.
Je! Makanisa yetu yaweza kuwa akina Tikiko, watu waaminifu kwa viongozi wao, na kwa kanisa la Kristo?
Bwana atusaidie.
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Silwano ni nani,kama tunavyomsoma kwenye biblia?(1Petro 5:12)
Epafra ni nani katika biblia? (Wakolosai 1:7)
Mathayo 6:28 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala HAYASOKOTI 29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo”
Mathayo 6:28 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala HAYASOKOTI
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo”
Maana ya kusokota kama inavyozungumziwa hapo ni “kitendo cha kusokota nyuzi na kuunda vazi”.
Zipo nguo/mavazi yaliyotengenezwa kwa kufuma na mengine kwa kusokota nyuzi aidha kwa mkono au mashine.
Kutoka 39:28 “na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa”
Walawi 13:52 “Naye atalichoma moto vazi hilo, kwamba ni lililofumwa au kwamba ni lililosokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu cho chote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaokula; vazi hilo litachomwa moto”.
Soma pia Walawi 13:58..
Sasa sisi wanadamu ili tuweze kuvaa vazi zuri lililofumwa au kusokotwa ni lazima tufanye kazi za kujiingizia kipato ili tukanunue mavazi hayo ya kusokota au sisi wenye tusokote kwa mikono yetu au mashine na kujivika…lakini kwa kawaida haiwezekani tule chakula halafu mavazi mazuri ya kusokotwa yatokee mwilini kama vile kucha inavyotokea mwilini…hilo jambo haliwezekani.
Lakini kwa upande wa MAUA ya kondeni hilo linawezekana.. yenyewe hayafanyi kazi yoyote ya kusokota lakini yanavikwa kwa rangi nzuri na za kupendeza ambazo hata Sulemani hakuwahi kuvikwa kama mojawapo ya hayo.
Kadhalika na hali yake mtu amwaminiye Bwana YESU, atakuwa hana haja ya kuhangaika sana kupata mavazi au chakula, kwasababu Bwana anajua anahitaji hayo yote.
Hata ikotokea anapitia vipindi vya kupungukiwa basi huenda ni darasa tu la muda anapitishwa lakini haitaliwa hivyo siku zote.
Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”
Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”
Kwa urefu kuhusiana na kuvikwa kwa maua ya kondeni na mfalme Sulemani fungua hapa》》》》Hii ni maana ya Mathayo 6:29 hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo
Kwanini pawekwe MITI pale bustanini na si kitu kingine?.
Kwanini MUNGU alimzuia Daudi asimjengee HEKALU? (1Nyakati 17:12)
Mwerezi ni nini?
UNAUELEWA, HISOPO UMEAO UKUTANI?
Si jambo la kawaida mwanadamu kula Udongo!.. Hivyo inapotokea mtu anakula udongo kupitiliza, basi hilo laweza kuwa tatizo la kiroho zaidi ya kuwa tatizo la kisayansi..
Ndio zipo tafiti chache zinazoonesha kuwa mwanamke anapokuwa mja mzito anaweza kuwa na hamu ya kula udongo, na pia mtu aliyepungukiwa na madini Fulani mwilini anaweza kula udongo..
Tafiti hizi zaweza kuwa kweli kwa sehemu, lakini inapotokea Mtu chakula chake kinageuka kuwa udongo, na wengine hata baada ya kumaliza kubeba ujauzito bado wanaendelea kula udongo, na hata kwenda kununua basi hilo ni tatizo la kiroho Zaidi.
Kwasababu maandiko yanasema anayekula mavumbi/udongo ni nyoka tu peke yake.
Mwanzo 3:14 “Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, NA MAVUMBI UTAKULA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO”
Hivyo kama unaona unalo tatizo la kula udongo kwa kiwango cha kushindwa kujizuia, basi ipo roho inayokutumikisha katika hilo, kama tu vile roho ya kujichua, hivyo suluhisho kwanza ni kumkaribisha BWANA YESU katika maisha yako, kwa kutubu na kumaanisha kuacha dhambi, kisha kutafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU, na baada ya hapo hiyo roho itaondoka yenyewe na utarudi kuwa mtu wa kawaida.
TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA
JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?
TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.
Kunyoa denge ni kufanyaje na je ni dhambi? (Walawi 19:27).
Jibu: Turejee.
Isaya 1:31 “Na mtu hodari atakuwa kama MAKUMBI, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima”.
“Makumbi” ni malighafi yoyote inayotumika katika kuanza au kuchochea moto, mfano; mbao, vijiti au nyasi kavu.
Katika kitabu hiko cha Isaya, biblia imemtaja mtu hodari kwamba siku hizo atakuwa si kitu bali kama tu vijiti vishikavyo moto na kuteketea.
Isaya 1:28 “Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa. 29 Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua. 30 Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji. 31 Na mtu hodari ATAKUWA KAMA MAKUMBI, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima”.
Isaya 1:28 “Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa.
29 Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
30 Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji.
31 Na mtu hodari ATAKUWA KAMA MAKUMBI, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima”.
Bwana hata sasa atusaidie tusimwache, bali tuzishike amri zake na maagizo yake ili tusiteketee kwa moto wake.
Yeremia 5:11 “Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema Bwana. 12 Wamemkataa Bwana, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa; 13 na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa. 14 Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika KINYWA CHAKO KUWA MOTO, NA WATU HAWA KUWA KUNI, NAO MOTO UTAWALA”
Yeremia 5:11 “Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema Bwana.
12 Wamemkataa Bwana, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa;
13 na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.
14 Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika KINYWA CHAKO KUWA MOTO, NA WATU HAWA KUWA KUNI, NAO MOTO UTAWALA”
Maran atha!
TUZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
Nimrodi ni nani?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Mhubiri 4:4 “Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.
Amali ni “kazi ya tabu/kuchosha”.. Mtu anayefanya kazi yenye kuchosha mwili na akili, kazi yake hiyo inaitwa “Amali”.
Hivyo mstari huo wa Mhubiri 4:4 unaweza kueleka hivi….
Mhubiri 4:4 “Tena nikafikiri KAZI ZOTE ZA TABU, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.
Maana yake kazi nyingi za kuchosha zinatokana zinahusisha mambo maovu ikiwemo Tamaa, Uchungu, Wivu, uchoyo, hasira na visasi.
(Ingawa pia si zote, yaani si wote wenye kufanya kazi za taabu/kuchosha wapo juu ya misingi hiyo, wapo wengine nia zao ni njema kabisa wana amani na Bwana anawatunza na kuwaonekania.. lakini wengi wao msingi wao ni uovu).
Mhubiri 4:8 “Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa”.
Lakini kama mtu atakuwa na Amali na akamcha Bwana ana heri, kwani tabu yake si bure kama maandiko yasemavyo, ila kwa mwenye kumweka Bwana pembeni, amali yake itakuwa bure.
Mistari mingine yenye kutaja Amali ni pamoja na Mhubiri 5:19, na Mhubiri 8:15.
Ikiwa kazi yako ya mikono, inakulemea akili na nguvu na huoni faida yake basi kimbilia kwa Bwana YESU naye atakutia mizigo sawasawa na ile Mathayo 11:28.
Zaburi 127:2 “Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi”.