Ni muungamaniko wa maneno makuu mawili. (Yaani Christian na Islamic). Likachukuliwa Neno la kwanza Chris katika Christian, likaunganishwa na Neno la katikati “slam” kutoka katika Islamic. Kuunda Christlam
Hii ni imani iliyozuka, katika taifa la Nigeria miaka ya 1970. Kufuatana ni migongano ya kiimani baina ya makundi haya mawili ya dini, ikizingatiwa kuwa Taifa La Nigeria ndio lenye watu wengi barani Africa, na takribani Nusu kwa Nusu, dini hizi mbili ndio zimechukua jamii kubwa ya watu.
Hivyo waasisi ya umoja huu walikuwa na madhumuni ya kuondoa tofauti za kidini, husani zilizo katika mataifa ya magharibu na ya mashariki ya kati, Lakini pia kwasababu hizi ndio dini kubwa duniani, basi pia zikiungana zinaweza kusaidia kuushinda upagani kwa sehemu kubwa.Na ukweli ni kwamba imani hii imepata umaarufu mkubwa duniani, hususani kwa kipindi cha sasa.
Waanzilishi walisukumwa kuunda umoja huu, wakiamini kuwa, sehemu kubwa ya dini ya kikristo inatajwa katika Quran, wakimrejea Yesu mwenyewe pamoja na manabii wa kale, kama Ibrahimu na wengineo. Lakini pia uislamu unamwingiliano mkubwa wa kitamaduni ambao hata katika ukristo upo. Hivyo kwa mujibu wa hoja zao hakuna sababu ya kuwa na utofauti wowote katika mashindano ya kidini.
Imani ya Kikristo na dini ya kiislamu haviwezi kuchangamana, ni sawa na chuma na udongo. Kwasababu kiini cha imani ya ukristo ni KRISTO mwenyewe, na kwamba mtu hawezi kwenda mbinguni pasipo kumwamini YESU kama mwokozi PEKEE anayewaokoa wanadamu. Jambo ambalo linakinzana na dini ya Kiislam, katika imani ya kufika mbinguni, ambapo kwa waislam Kristo ni kama mmojawapo wa manabii tu wengine. Na hivyo mbingu si kupitia Kristo, bali ni kupitia matendo mazuri kama vile kukaa mbali na uovu n.k.
Uislamu haumtambui Kristo kama Mungu, huamini kuwa yoyote anaye amini kuwa Yesu ni Mungu, ni makufuru, kwasababu Mungu hajazaa, wala hana mshirika. Hivyo aaminiye uungu wa Yesu, pepo haimuhusu.
Kwa vigezo hivyo, uislamu na ukristo ni imani mbili tofauti kabisa, ijapokuwa zitaonekana kushea baadhi ya desturi, lakini bado haziwezi kuletwa pamoja kuwa kitu kimoja.
Je! Hatupaswi kuwa waamini wa Chrislam
Ndio wewe kama Mkristo,, imani yako haipaswi kuchanganywa na nyingine yoyote, ukifanya hivyo ni Kosa kiimani. Sisi tunaamini, wokovu ni kwa kupitia Yesu Kristo anaotupa BURE kwa neema katika kumwamini Yeye, kwa kifo chake pale msalabani.
Tunamtegemea Kristo kutuokoa, kutupa nguvu ya kuishi maisha makamilifu, kutuongoza, kwa asilimia zote. Hivyo hatuna msingi au tegemeo lingine nje yake yeye. Na hata hivyo kibiblia, yoyote asiyekubaliana na Kristo Yesu, kama ndiye mwokozi pekee. Huyo ni mpinga-Kristo.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa wewe kama mwana wa Mungu, usijihusishe ni imani yoyote nje ya Kristo Yesu mwokozi wako.
Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
Praitorio ni nini? Na Kwanini ilikuwa ni najisi kwa wayahudi kuingia humo? (Yohana 18:28)
Uadilifu ni nini kibiblia?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Je kulikuwa na umuhimu wowote wa ile merikebu ya Iskanderia walioipanda Paulo na wafungwa wengine kutajwa jina lake ‘ndugu Pacha’,?
Matendo 28:11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha. 12 Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu. 13 Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. 14 Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.
JIBU: Safari ya mtume Paulo kama mfungwa, kutoka Kaisaria kwenda Rumi kuhukumiwa, haikuwa rahisi, iligubikwa na misuko suko mikubwa ambayo ilihatarisha maisha yao ukisoma Matendo 27, utaona mtume Paulo alionywa na Roho Mtakatifu kuhusu hatari hiyo lakini alipomwambia akida na manahodha, walipuuzia agizo lake, kwasababu watu wale hawakuamini habari za “miungu kabisa”. Maandiko yanasema walipoona upepo wa kusi umevuma kidogo tu, unaoruhusu kusafiri, wakadhani itakuwa hivyo mbeleni.
Lakini tunaona walipofika katikati, ghafla ile bahari iliwachafukia sana, upepo wa nguvu ukavuma merikebu yao ikawa karibu na kuzama, baadaye ilivunjika kabisa, na wakaokoka kwa shida kwasababu Mungu alimuhakikishia Mtume Paulo kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeangamia.
Walipookoka na kufika kisiwa kile kilichoitwa Melita, walikaa miezi mitatu pale, kuruhusu hali ya hewa kutulia, kabla ya kuondoka. Lakini tunaona walipotaka kuondoka, safari hii wale mabaharia pamoja na maakida, hawakuichukulia safari yao kirahisi rahisi, yaani hivi hivi tu bila uongozo wowote. Ndipo walipojifunza kuchagua merikebu yenye “ulinzi wa kiroho”. Wakaipata hiyo ya Iskanderia iliyokuwa na nembo ya “Ndugu Pacha” kwa mbele.
Ndugu Pacha ni miungu ya kipagani ya kiyunani, ukisoma tafsiri nyingine za biblia imewataja moja kwa moja miungu hiyo kama Castor na Pollux. Ni miungu ambayo waliamini inahusika na ulinzi wa safari za majini. Hivyo kwa imani yao ya kipagani, wakachukua nembo yao kuonyesha tunaiabudu na kuiheshimu hii miungu, na kutaka iwaongoze salama katika safari yao, hawategemei tena elimu zao na nadharia zao.
Sasa tukirudi kwenye swali, linalouliza, kulikuwa ni umuhimu gani, hiyo merikebu ya Iskanderia kutajwa hadi nembo yake ya ndugu Pacha. Sababu ndio hiyo, Sio kwamba biblia inatufundisha, na sisi tukaweke miungu ya kipagani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri kutuhakikishia ulinzi, hapana!
Bali inatufundisha Safari ya maisha hapa duniani. Kila mwanadamu anasafiri, lakini Je! Katika safari yako ni kitu gani kinakuongoza na kukulinda ili kukufikia ng’ambo yako salama?
Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kujiongoza mwenyewe. Na ndio maana utaona hawa kwasababu hawakumjua Mungu wa kweli iliwabidi wakatafuta vinyago visivyoweza kuwasaidia kitu viwaongoze, na kama sio mtume Paulo kuwepo ndani ya Merikebu ile, safari yao ndio ingekuwa mbaya mara mbili zaidi. Hawakujua tu waliongozwa na Kristo Yesu pasipo wao kujua kwa neema tu!. Kwasababu watumishi wa Mungu walikuwa ndani.
Na sisi, hapa tulipo, fahamu kuwa maisha yako, bila KRISTO ni mauti mbele. Shetani hakuwazii mema, wala akili zako mwenyewe hazikusaidii ndugu, hiyo elimu ni kazi bure, huo uzoefu na ujuzi ulionao ni bure rafiki. Unamuhitaji Kristo, yeye ndio awe nembo ya maisha yako. Mwamini leo akupe msamaha wa dhambi, mwamini leo akuokoe, safari yako iwe salama hapa duniani. Ukifa leo katika hali hiyo, fahamu ni jehanamu moja kwa moja. Umesikia injili ikihubiriwa mara ngapi, kwamba Yesu ni mwokozi lakini unapuuzia? Walio kuzimu wanatamani hata dakika moja, watubu hawawezi kwasababu kule hakuna maisha ya kuishi. Lakini wewe unaishi.
Usikiapo maneno haya, ugeuze moyo wako, umruhusu Kristo leo akuokoe, ikiwa upo tayari kumgeukia Bwana Yesu , na unatamani upate mwongozo wa kimaombi kwa ajili ya wokovu wako. Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii, bure.
Bwana akubariki.
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
Jibu: Turejee.
Mithali 20:1 “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima”.
Hili ni andiko linaloelezea mambo makuu mawili yanayowakosesha watu waliopungukiwa na Hekima.. na Mambo hayo ni “Mvinyo” pamoja na “Kileo”. Na vitu vyote hivi viwili vina madhara kwa mtu anayevitumia..
Sasa ni ipi tofauti kati ya Mvinyo na Kileo? Na madhara yake ni yapi kwa mtumiaji?.
“Mvinyo” (kwa lugha ya kiingereza ni “wine”) ni kilevi kinachotengenezwa kwa “Matunda yaliyosagwa” kama Zabibu, mananasi, maembe n.k Mfano wa mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu ni “Divai”.
Wakati “Kileo” (Kwa lugha ya kiingereza Beer/Bia) ni kilevi kinachotengenezwa kwa nafaka kama Ngano, mahindi, ulezi, mtama, mchele n.k
Kikawaida Mvinyo ndio wenye kilevi kingi kuliko Kileo. Na matokeo ya mtu anayetumia mvinyo au kileo yanakaribiana. Hebu tuangalia madhara ya kimoja baada ya kingine kibiblia.
1. MVINYO
Biblia anasema “Mvinyo hudhihaki”.. maana yake ni kuwa mtu anayetumia mvivyo anakuwa ni mtu wa kudhihaki na kudhihakiwa!.. kwasababu ya wingi wa maneno yao yasiyo na maana yatokayo midomoni mwao.
Ndio maana utaona kile kipindi cha Pentekoste, walipowasikia wanafunzi wa Bwana YESU wakinena kwa lugha, walidhani wamelewa kwa mvinyo mpya na hivyo wakaanza kuwadhihaki..
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 WENGINE WALIDHIHAKI, WAKISEMA, WAMELEWA KWA MVINYO MPYA. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 WENGINE WALIDHIHAKI, WAKISEMA, WAMELEWA KWA MVINYO MPYA.
14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli”.
Umeona hapo?.. walianza kuwadhihaki wakidhani wamelewa kwa MVINYO MPYA, ikimaanisha kuwa Mvinyo huleta dhihaka kwa anayekunywa. Na mtu anayelewa kwa mvinyo atapokea dhihaka nyingi katika maisha yake..
2. KILEO
Biblia inaendelea kusema kileo huleta “UGOMVI”. Asilimia kubwa ya watu wanaogombana mpaka kufikia hatua ya kudhuriana ni walevi wa pombe, mafarakano mengi yanatoka kwa watu waliolewa..
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Ulevi wa aina yoyote ile uwe wa “Mvinyo” au wa “Kileo” matokeo yake ni mabaya katika maisha ya ulimwengu huu na ule ujao…. Kulingana na biblia walevi wote hawataurithi uzima wa milele (soma 1Wakorintho 6:9-10 na Wagalatia 5:19-20)..
Warumi 13:13 “Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ULAFI NA ULEVI, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Warumi 13:13 “Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ULAFI NA ULEVI, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Maran atha.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;
“Si watu wa kutumia mvinyo sana”, je tunaruhusiwa kutumia mvingo kidogo?(1Timotheo 3:8).
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
WhatsApp
Swali: Je lile shauri la kupeleka wapelelezi Kanaani lilitoka kwa nani?..Maana sehemu moja katika biblia inasema lilitoka kwa Bwana (Hesabu 13:1-3) na sehemu nyingine inasema lilitoka kwa wana wa Israeli (Kumbukumbu 1:22-23). Je! lipi ni sahihi, na je biblia inajichanganya?.
Jibu: Turejee mistari hiyo, mmoja baada ya mwingine.
Hesabu 13:1 “Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao. 3 Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli”.
Hesabu 13:1 “Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,
2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.
3 Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli”.
Hapa tunaona ni MUNGU ndiye anamwamuru Musa apeleke wapelelezi.
Kumbukumbu 1:22 “Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia. 23 Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila”
Kumbukumbu 1:22 “Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia.
23 Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila”
Na hapa tunasoma kuwa ni “Wana wa Israeli” ndio waliopendekeza kupeleka wapelelezi Kanaani. Sasa swali ni je!..biblia inajichanganga?.
Jibu ni La!.. Biblia haijichanganyi mahali popote, isipokuwa fahamu/pambanuzi zetu ndizo zinachojichanganya au kuchanganyikiwa.
Sasa ni kwanini hapo sehemu moja iseme ni Mungu na sehemu nyingine iseme wana wa Israeli? Ukweli ni upi?
Ukweli ni kwamba wazo la kupeleka wapelelezi wakaiepeleze Kanaani ni Wana wa Israeli ndio waliolitoa, kamwe Mungu asingeweza kuwaambia wana wa Israeli wapeleke wapelelezi kwasababu yeye ana nguvu nyingi na wala hahitaji utafiti wa wanadamu katika kuokoa au kuharibu!…Kama ndivyo angefanya kwanza kwa Farao, lakini tunasoma Farao alikuwa kama mnyoo tu mbele za Bwana, na Taifa la Misri kwa wakati huo lilikuwa na nguvu Zaidi hata ya Kanaani.
Hivyo kilichowasukuma wana wa Israeli kupeleka wapelelezi ni hali ya ugumu wa mioyo yao, ambayo baada ya kutoka Misri walianza kuusahau uweza wa Mungu na kumdharau Mungu, kiasi kwamba hawakuamini kwamba angeweza kuwashindania kama alivyowashindania walipotoka Misri, lakini kinyume chake wakaukataa uweza wa Mungu, mioyo yao ikawa migumu, wakajitwika silaha, na wakapanga mipango yao.
Hesabu 14:11 “Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao”.
Sasa kwakuwa wana wa Israeli tayari walikuwa wameshamdharau Mungu na uweza wake, hivyo Mungu aliruhusu baadhi ya Mambo wayafanye, katika kiwango cha uweza walichompimia. Na mojawapo ya jambo ambalo aliliruhusu ni hilo la kwenda kupeleleza.
Hivyo Musa aliposikia mpango wa wana wa Israeli kwenda kuipeleleza, alienda kuuliza kwa Bwana, na Bwana akawapa ruhusa sawasawa na hiyo Hesabu 13:1-6. Na sio jambo hilo tu ambalo Mungu alitoa ruhusa bali yapo na mengine mengi ambayo wana wa Israeli walijiamulia na Mungu akaruhusu yaendelee katikati yao, lakini hayakuwa mapenzi makamilifu ya Mungu, baadhi ya mambo hayo ni yale ya wana wa Israeli kujitakia mfalme katika (1Samweli 8:5) na yale ya talaka ambayo Bwana YESU aliyasema katika Mathayo 19:3-8.
Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. 7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, MUSA, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, ALIWAPA RUHUSA KUWAACHA WAKE ZENU; LAKINI TANGU MWANZO HAIKUWA HIVI. 9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini”
Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, MUSA, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, ALIWAPA RUHUSA KUWAACHA WAKE ZENU; LAKINI TANGU MWANZO HAIKUWA HIVI.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini”
Hii ikitufundisha kuwa, kuna mambo ambayo Mungu anaweza kuyaruhusu katika maisha yetu yatokee lakini yakawa si mapenzi makamilifu ya Mungu. Hivyo ni muhimu sana kutafuta kuyajua na kuyafanya mapenzi makamilifu ya MUNGU, na ndivyo tutakavyompendeza Mungu, na kuishi kama atakavyo yeye.
Kanaani ililaaniwa (Mwanzo 9:20-25,) kwanini Mungu awapeleke wana wa Israeli katika nchi iliyolaaniwa?
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
EPUKA KUPELELEZA KILA KITU MUNGU ANACHOKUAHIDIA.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.
Swali: Roho ya kukata tamaa ipoje na inatendaje kazi na inawezaje kumtoka mtu?
“Roho ya kukata tamaa” ni roho inayomwingia mtu na kumfanya asiweze kuendelea mbele Zaidi. Roho hii inapomwingia mtu inamfanya asiwe na nguvu ya kufanya au kutafuta jambo lolote lile lililo zuri. Ndio hapo utaona mtu anakata tamaa ya kuendelea kusubiri jambo Fulani au kuendelea kuomba au kuendelea kutafuta.
Roho hii inasababishwa na “shetani” kwasababu kamwe MUNGU hawezi kumkatisha mtu tamaa kwa jambo lolote jema mtu apangalo kulifanya au kulitafuta. Yeye (Mungu) anasema maneno yafuatayo..
Luka 18:1 “Akawaambia mfano, ya kwamba IMEWAPASA KUMWOMBA MUNGU SIKUZOTE, WALA WASIKATE TAMAA”.
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”
Lakini adui kazi yake ni kukatishata tamaa, aidha kwa njia ya mawazo, ndoto au maneno ya watu.
Zifuatazo ni njia za kushughulika na roho ya kukata tamaa.
1. MPOKEE YESU
Kama bado hujaokoka, fahamu kuwa wewe ni windo tosha la adui, na moyo wako ni malango ya maskani za roho zote chafu zikiwemo za kukatisha tamaa, hivyo maisha yako yatatawaliwa na kuvunjika moyo na kutokusonga mbele.
2. SOMA NENO.
Soma sana Neno la MUNGU (Biblia) kwasababu ndani yake limejaa maneno ya Faraja, ambayo yanaweza kukufaa na kukutia nguvu katika nyakati zote utakayopitia za kukatisha tamaa, Kama magonjwa ndiyo yaliyokukatisha tamaa ndani ya biblia ipo mistari mingi ya kutia moyo wa kuendelea mbele.
Kama ni Ndoa ndio iliyokukatisha tamaa, yapo maneno ya faraha na kutia nguvu yahusuyo ndoa ndani ya biblia, kama ni anguko Fulani limetokea na likakukatisha tamaa, ndani ya biblia ipo mistari ya kutia nguvu ya kukunyanyua tena katika hali unayopitia. N.k
3. MAOMBI
Fanya maombi kila siku, hii utakusaidia kukuweka katika lile joto la kiroho, na hivyo kufunga milango yote ya roho za adui za vitisho na kukatisha tamaa. Ukiwa mwombaji utakuwa katika usalama wa Roho daima.
Kwa njia hizo tatu basi waweza kujifungua na kila kifungo cha kukata tamaa, au kukatishwa tamaa.
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
KWANINI UKATE TAMAA?
Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.
Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)
USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.
Swali: Roho ya umasikini ipoje na inatenda kazi kwa namna gani, na inawezaje kumtoka mtu?
“Roho ya umasikini” ni roho inayomshusha mtu kiuchumi, hata kumfanya asifike kule anakotaka kufika kimaendeleo.
Roho hii inapomvaa mtu inamfanya wakati mwingine awe katika hali ya mahitaji kupindukia na hata kuwa katika hali ya madeni mazito.
Kibiblia watu wa Mungu umasikini si sehemu yao.. Ingawa kuna vipindi ambavyo Mungu anaweza kumpitisha mtoto wake kuonja umasikini kwa muda ili kumfundisha baadhi ya mambo, ambayo yatamfaa baadaye atakapobarikiwa.
Na urefu wa kipindi hicho cha madarasa ya Mungu kinategemea mtu na mtu. Wapo ambao watadumu katika hiko kipindi kwa muda mrefu kidogo lakini baadaye watatoka huko, na wapo ambao watadumu katika kipindi kifupi na baadaye watatoka huko na kupewa pumziko la faraja ya Bwana.
Lakini kwa ujumla Mkristo hajapewa umasikini wa kudumu kama sehemu maisha yake…au labda mtu huyo atake mwenyewe kujifanya maskini kwa nafsi yake au kwaajili ya Bwana.
Mtu anayejifanya maskini kwa ajili ya Bwana ni yule ambaye Mungu anamfungulia milango ya kupata vingi lakini kila anachokipata anakitoa na hivyo muda wote anakuwa katika hali ya kutokuwa na vingi…(Mtu wa namna hii ni maskini ingawa ni tajiri).
Mtu huyu anakuwa hawezi kuona furaha au Amani akiwa na viwili wakati mwingine hana hata kimoja. Mtu wa namna hii anakuwa anajifanya mwenyewe maskini kwaajili ya Bwana na kwa taji yake mbinguni, ikiwa anafanya hivyo kwa dhamiri njema na si kama sheria.
Mfano wa watu waliojifanya wenyewe kuwa maskini ingawa wangeweza kuwa matajiri ni Yohana Mbatizaji na BWANA WETU YESU KRISTO.
2Wakorintho 8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Na pia wapo ambao walikuwa matajiri na wakadumu na utajiri wao, mfano wa hao ni Ibrahimu na Ayubu..
Sasa hakuna agizo lolote maalumu katika biblia kuwa ni sheria tujifanye kuwa maskini, kama alivyokuwa Bwana au Yohana Mbatizaji, mtu akijifanya hivyo basi iwe kwa nafsi yake na Mungu wake, na si amri wala agizo.
Lakini pamoja na hayo, upo umaskini mwingine ambao hauletwi na Mungu bali unaletwa na adui shetani. Mara nyingi umasikini huu ni ule unaompata mtu anapokuwa nje ya KRISTO (Maana yake hajaokoka).. au aliyeokoka lakini amepungukiwa na baadhi ya Maarifa ambayo yangemsaidia kusogea kimaisha.
Sasa ni njia gani za kushughulika na roho ya umaskini unaoletwa na adui shetani?
1. KUOKOKA
Unapookoka kikweli kweli kwa kumaanisha, basi roho zote za adui zinazochochoe na kutengeneza umaskini maishani mwako zinaondoka, na hivyo maisha yako kutengenezeka upya kama yalikuwa yameshaharibiwa na pepo la umasikini.
2. KUOMBA
Maombi ni silaha tosha kwa kila mwamini, na maombi ni ULINZI, Kama umeshuhudiwa kuwa hali unayopitia sio ya kawaida na wala haitokani na MUNGU, basi ni wakati wa kuingia vitani katika maombi, kuvunja na kukemea kila roho yote inayotaka kujiinua kinyume na maendeleo yako.
3. PATA MAARIFA.
Kama umeshaokoka na tena ni mwombaji sana lakini bado unaona hali hiyo ya umasikini inadumu muda mrefu, basi huenda Mungu kashakufungulia milango mbele yako ili upige hatua, lakini milango hiyo huioni aidha kutokana na kupungukiwa na MAARIFA, sawasawa na Hosea 4:6.
Hivyo tia bidii katika kutafuta maarifa ya jinsi ya kujiendeleza mbele kupitia kanuni za kibiblia. (Soma sana biblia, na pia sikiliza mafundisho mbalimbali kutoka kwa watumishi wa kweli wa Mungu yahusuyo namna ya kujiendeleza, vile vile ongeza ujuzi katika kile ukifanyacho).
Kupitia njia hizo tatu basi utaweza kujifungua kutoka katika kifungo cha umasikini.
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
UKITAKA KUMFUATA YESU NI SHARTI UACHE VYOTE!
Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Swali: Kwanini tutoe sadaka? Na Je ni lazima kutoa sadaka?..Na mtu asipotoa sadaka ni dhambi?
Jibu: “Utoaji” (uwe wa sadaka au wa kitu kingine chochote) ni wajibu wa kila “Mwamini”.. Mtu ambaye si mtoaji bado hana badiliko la kweli ndani yake!…na wala Mungu hayupo ndani yake.
Sasa kwanini tunatoa sadaka? Na kwanini mtu ambaye si mtoaji hana Mungu ndani yake?
Jibu, Tunatoa sadaka kwasababu Mungu naye ni Mtoaji (vyote tunavyonufaika navyo ni yeye katupa bure bila gharama). Na kwanini Mungu awe mtoaji na sisi tuwe watoaji?.. Ni kwasababu tumeumbwa kwa sura na Mfano wake! (Mwanzo 1:26).
Kama mtu hatoi maana yake ule mfano wa Uungu ndani yake haupo kwasababu Mungu sifa yake kuu ni utoaji!.. Ametoa uzima bure, ametoa maisha bure Zaidi sana ametupa uzima wa milele bure kupitia kumtoa mwanawe wa pekee (Yohana 3:16) na mambo mengine mengi.. Hivyo na sisi ni lazima tuwe kama yeye…ndivyo maandiko yanavyotuambia.
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Na kutoa ni “Wajibu” Zaidi ya “Agizo”.. Mtu anayejua wajibu wake, hakumbushwi kumbushwi, halazimishwi lazimishwi wala hasukumwi sukumwi.. Anatimiza wajibu wake kwasababu anajua pia ni kwa faida yake.
Ukiona utoaji ni sheria ngumu kwako, kwamba unaona uchungu kumtolea Mungu.. au unaona kama unafilisika, au unaonewa au unadhulumiwa wahi kutafuta msaada kutoka kwa BWANA, Mlile mwambie aiondoe hiyo roho ndani yako kwasababu ndio roho ile ile iliyokuwa ndani ya Kaini alipoona kumtolea Mungu sehemu ya kwanza ya vitu vyake ni hasara kubwa!.. na kwasababu anasukumwa sukumwa na sheria ya utoaji, akalazimika kumtolea Mungu sehemu hafifu na sadaka zake na hivyo zikakataliwa.
Mungu anayekupa pumzi na maisha bure unaonaje uchungu kumtolea sehemu ya kumi tu! Na sehemu 9 zilizosalia zibaki kwako?.. Huoni kuna shida kama unaona uchungu kwa hicho kidogo?..
Mungu unayekanyaga ardhi yake bure, unayevuta hewa yake bure tangu umezaliwa, unayefurahia jua lake bure bila kulipia hata mia, na wakati huo huo unawalipa tanesco fedha nyingi kwa kukupatia tu kanuru kadogo wakati wa usiku.. Huyo Mungu akupaye hayo yote, unamwonea uchungu na hata kumwibia, na ukiambiwa kuhusu kumtolea unaona unafilisiwa na kudhulumiwa, utaachaje kuwa kama KAINI WEWE!!. Moyo wako hauwezi kuwa kwa MUNGU Kamwe!, haijalishi utakuwa unaomba sana wewe bado utakuwa mnafiki.
Usikwepe kumtolea Mungu na tena ifanye kuwa ni wajibu, na si Agizo wala Amri!. Na madhara ya kutomtolea Mungu (kukwepa wajibu) yanapatikana katika Mathayo 25:41-46
+255789001312 au +255693036618
Kwanini Sadaka ya Kaini ilikataliwa? (Mwanzo 4:5).
SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.
Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?.
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?
Swali: Kwanini sadaka ya Kaini ya Mazao ilikataliwa na ile ya Habili ya wanyama ilikubaliwa? Je ni kwamba “wanyama” ni bora kuliko “mazao” mbele za Mungu?
Jibu: Turejee,
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.
Sababu ya sadaka ya Kaini kukataliwa si kwasababu Mungu anapendezwa sana na wanyama kuliko mazao.. LA! Zaidi sana Mazao yanaweza kuwa bora kuliko wanyama kwasababu hayahusishi umwagaji wa damu.
Lakini sababu kuu ya Sadaka ya Kaini kukataliwa ni hiyo tunayoisoma katika mstari wa 3 na wa 4..
“Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta WAZAO WA KWANZA wa wanyama wake na SEHEMU ZILIZONONA za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;”
Habili alileta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona… Lakini Kaini hakupeleka sehemu za kwanza za mazao yake!..bali alipeleka sehemu dhaifu, kama ni mahindi pengine alipeleka yale yaliyoharibika haribika, kama ni matikiti alipeleka yale yaliokaribia kuoza! N.k..na zile njema na nzuri aliona zinamfaa yeye na si Mungu anayempa pumzi, na uhai na maisha.
Hivyo alimfanya Mungu wapili katika mali zake, na Mungu naye akamfanya wa pili mbele ya ndugu yake Habili.
Lakini Mungu ni wa upendo, huwenda alifanya vile kwa kukosa maarifa.. hivyo alimwonya na kumfundisha njia iliyobora ya kutoa sadaka ili sadaka yake ikubaliwe kama ya nduguye, lakini kwa kiburi alishupaza shingo, na akaenda kumwua ndugu yake, ikawa dhambi kubwa sana kwake.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. 8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “
Ni jambo gani tunajifunza hapo?
Jambo kuu tunalojifunza ni kuwa Mungu anaziangalia sadaka zetu, na kupitia hizo anatuhukumu nazo!.. Maandiko yanasema “hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakapokuwepo (Mathayo 6:21)”.. Kama hazina yako ya kwanza haipo kwa Mungu, na Moyo wako hauwezi kuwa kwa Mungu, na ndicho kilichokuwa kwa Kaini.. Hazina yake kamilifu haikuwa kwa Mungu ndio maana hata Moyo wake haukumwelekea Mungu baada ya pale.
Lakini kama sehemu ya kwanza ya Hazina yako (sadaka) ipo kwa Mungu hata moyo wako utakuwa kwa Mungu..
Na kama unataka kujipima kama moyo wako kweli upo kwa Mungu “jiangalie utoaji wako”..(Hicho ndio kipimo kirahisi sana cha kujitambua wewe ni mtu wa namna gani).. Kwasababu hiyo basi ni dhambi kubwa sana kukwepa matoleo, haihitaji elimu kubwa kufahamu hilo….mtolee Bwana Zaka, mtolee Bwana sehemu zilizonona wala usimwibie, na moyo wako utakuwa kwake na utabarikiwa pia.
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?
SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
Swali: Kwanini Mungu alimkataa Mfalme Sauli na tunapata funzo gani?
Jibu: Sauli alikataliwa na Mungu kwasababu ya mambo makuu mawili, 1) UASI na 2) UKAIDI WA MOYO.
Hayo ndio mambo mawili yaliyomkosesha Sauli, na biblia imeweka wazi..
1Samweli 15:22 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. 23 Kwani KUASI ni kama dhambi ya uchawi, Na UKAIDI ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.
1Samweli 15:22 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
23 Kwani KUASI ni kama dhambi ya uchawi, Na UKAIDI ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.
1. KUASI
Kuasi maana yake ni kuondoka katika njia sahihi na kuwa adui wa hiyo njia. Ndicho kilichomtokea Sauli, Moyo wake ulianza kuondoka kwa MUNGU kidogo kidogo, na akaanza KWENDA KINYUME na sheria ya MUNGU huku akijua kabisa kuwa anachokifanya si sawa.
2. UKAIDI
Dhambi ya pili ya Sauli ni “Ukaidi”. Mkaidi ni mtu asiyeshaurika wala hakubali kubadili mawazo yake…anachokiamini amekiamini!!,…anachokishikilia amekishikilia!..
Na Mfalme Sauli alikuwa mkaidi kwa BWANA!, Kwani utaona alipofanya kosa la kwanza la kutoa dhabihu kinyume na sheria ya Mungu katika 1Samweli 13:18 na kukemewa na Bwana, lakini utaona anakuja kurudia kosa linalofanana na hilo katika 1Samweli 15:14 pale alipoleta dhabihu haramu kutoka kwa waamaleki na kutaka kuzitoa kwa Bwana.
Alileta kondoo na Ng’ombe (walionona) kutoka Taifa la Amaleki, ili amtolee Mungu dhabihu… Kwa jicho la Haraka inaweza kuonekana kuwa alifanya jambo la busara…lakini kwa jicho la ndani SAULI alifanya machukizo makubwa sana.
Kwani kitendo cha kutwaa Ng’ombe za watu wanaoabudu miungu, ambao wanaitolea miungu yao, na tena hajui hizo ng’ombe zina historia gani..na kuzichukua hizo kisa tu zimenona kisha kumtolea Mungu, ilikuwa ni kitendo cha dharau kubwa sana (1Samweli 15:14-15)!!.. Ni sawa tu na kutwaa msharaha wa kahaba na kumletea Bwana ule alioukataza katika Kumbukumbu 23:18..
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.
Hivyo Sauli alikuwa mkaidi kwa Mungu.. kwani sheria inasema Usimchinjie Bwana Ng’ombe wala kondoo aliye na kilema au MWENYE NENO OVU! (Kumbukumbu 17:1)..Na hapa Sauli analeta Ng’ombe walionona lakini waliojaa maovu ya Waamaleki kama sadaka kwa Bwana. (1Samweli 15:14-15)!!.. Huo ni UKAIDI MKUU..
Na hata leo, Mambo haya mawili (UASI na UKAIDI) yanamchukiza Mungu.
Yeremia 5:22 “Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita. 23 Lakini watu hawa wana moyo wa KUASI NA UKAIDI; wameasi, wamekwenda zao. 24 Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa. 25 Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate”.
Yeremia 5:22 “Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
23 Lakini watu hawa wana moyo wa KUASI NA UKAIDI; wameasi, wamekwenda zao.
24 Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa.
25 Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate”.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.
DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)
Dhabihu ni nini?
Gudulia ni nini? (1Samweli 26:11).
Habari ile ya Pilato kuchanganya zile damu za wayahudi na pamoja na dhabihu zao,(Luka 13) ilihusu nini?
Swali: Kwanini Mungu ametuumba? Na Sababu ya sisi kuwepo ni ipi?.. Na kwanini mmoja aumbwe hivi mwingine vile? kwa ujumla kwanini Mungu aliiumba dunia?
Jibu: Mungu katuumba sisi kwa “Kupenda kwake yeye (Mapenzi yake)”… Ili yeye afurahi kuwa pamoja nasi na sisi tufurahi kuwa pamoja naye!.
Ufunuo 4:11 “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na KWA SABABU YA MAPENZI YAKO VILIKUWAKO, navyo vikaumbwa”.
Kwetu kuumbwa ni “faida kubwa”…kwasababu hakuna faida yoyote ya “kutokuwepo”.. tengeneza picha haupo au hatupo!..je ni faida gani unapata au tunapata?..Lakini kama tukiwepo na tukaishi maisha ya milele na furaha basi ni heri sana!.
Na Mungu mwenyewe ametuahidia uzima wa milele kupitia mwanae YESU KRISTO.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”
Lakini kama mtu hatapenda kuishi, na wala hataki maisha basi njia ya kupoteza maisha ni kumkataa YESU.
1Yohana 5:12 “Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima”
swali la pili; kwanini mmoja aumbwe hivi mwingine vile?
Jibu rahisi ni kwasababu ndivyo ilivyompendeza yeye ili kututofautisha sisi kwa sisi (hajapenda wote tufanane kama sisimizi)…na hatuwezi kuhoji Zaidi!.
Warumi 9:20 “La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? 21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”
Warumi 9:20 “La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”
Lakini kwa vyovyote vile tulivyoumbwa tunapaswa tuutafute uzima wa milele na pia ni muhimu kufahamu kuwa kwa Mungu hakuna upendeleo wa mmoja Zaidi ya mwingine, wote tupo sawa mbele zake, pasipo kuangalia mwonekano, wala kimo, wala umri, wala jinsia.. Wote tunapendwa sawa, na tunapimwa sawa mbele zake .
Je unao uzima wa milele ndani yako?..Kumbuka uzima wa Milele upo kwa mmoja tu! YESU KRISTO!, Ikiwa bado hujampokea na unahitaji msaada katika kumpokea basi waweza wasiliana nasi kwa namba zetu..
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
NUNUA MAJI YA UZIMA.
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
FAHAMU VIASHIRIA VYA MTU ALIYESAMEHEWA DHAMBI ZAKE.
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?