Kuota unavua samaki, kunamaanisha nini?

Kuota unavua samaki, kunamaanisha nini?

Jiunge  >>>  WHATSAPP  <<< kwa mafundisho.

Ikiwa ndoto hii inakujia mara kwa mara, Au imekujia kwa uzito fulani, basi hwenda Mungu anasema na wewe rohoni. Ndoto hii inaweza kuja katika maumbile mengi. Wengine wanaota wakivua samaki kwa mikono, wengine kwa ndoano, wengine kwa wavu, wengine wakivua samaki wadogo/wakubwa. n.k. Kwa vyovyote vile maadamu ni kuvua basi maudhui yake ni moja.

Kiroho, uvuvi humaanisha kuwavuta watu kwa Kristo kwa kazi ya injili.

Yesu alipokutana na wale thenashara, wengi wa hao walikuwa wakifanya kazi ya uvuvi. Hivyo hiyo ilikuwa ni njia rahisi ya Yesu kuwaeleza kusudi lake timilifu juu ya hicho wanachokifanya.

Ndio maana siku ile alipomfanyia Petro muujiza ule wa kupata samaki wengi, baada ya kutaabika usiku kucha bila kupata chochote, Yesu alimwambia usiogope tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.

Luka 5:10

[10]na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni.Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.

Kuonyesha kuwa uvuvi wa nje, ni ufunuo wa uvuvi wa rohoni.

Utaona hata huduma ya malaika siku ile  ya mwisho ya kuwatenga watu waovu na wema inafananishwa na huduma ya uvuvi wa samaki.

Mathayo 13:47-50

[47]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;

[48]hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.

[49]Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

[50]na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Hivyo kwa namna moja au nyingine ikiwa umeokoka  basi Bwana anakutaka uhihubiri injili, kwa wengine kwasababu wakati huo umefika kufanya hivyo. Usiangalie uzoefu wako, kwasababu kumshuhudia Kristo hakutegemei uzoefu bali nia ya upendo. Na Mungu mwenyewe ameahidi kukusaidia kunena uwashuhudiapo watu.

Lakini kama hujaokoka, basi Yesu anakuita na anaona wito wako kutokea mbali, kwamba ukawahubirie wengine. Hivyo ni wajibu wako kumtii na kuupokea wokovu ili kusudi hilo alilolipanga ndani yako alifanikishe juu yako, haijalishi ndoto hii umeota mtu wa dini gani au imani gani, iwe mwislamu, mhindu, mshirikina. Maana umeota msalaba. Ujue Kristo anakuita akuokoe.

Ikiwa upo tayari sasa kumpokea Yesu basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo.

>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UVUVI BORA HAUCHAGUI, CHA KUVUA.

TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

CHAMBO ILIYO BORA.

Kuota unakimbizwa.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kuota msalaba maana yake ni nini?

Jiunge  >>>  WHATSAPP  <<< kwa mafundisho.

Ikiwa wewe bado hujamjua Kristo kabisa/ hujaokoka. Fahamu kuwa ndoto hii inakujuza kuwa Kristo anakuita akuokoe.

Msalaba hufunua wokovu wa Yesu Kristo, tulioupata kwa kifo chake juu ya mti huo.

Waefeso 2:16

[16]Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.

Hivyo fungua moyo wako upokee wokovu huu bure, Kumbuka hakuna uzima wala tumaini, wala, amani,wala raha, wala faraja nje ya Kristo. Ndio maana umeota msalaba kwasababu Kristo anakupenda, hataki uangamie. Ikiwa upo tayari kumpokea leo basi fungua hapa kwa msaada…

>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Lakini ikiwa tayari umeokoka. Kristo anakutaka kumuangalia yeye zaidi… Kuongeza kiu yako, kwake, na mawazo yako kwake, na hiyo inaambatana na kujikana nafsi.

Luka 9:23-24

[23]Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.

[24]Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

Hivyo kwa ujumla wake ndoto ya msalaba, aidha umeushika au umeubeba, au umeuona, ni ishara ya kumtazama Kristo.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.

KUOTA UPO MAKABURINI.

KUOTA UMEACHWA NA GARI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kuota unapewa biblia kuna maanisha nini?

Jiunge  >>>  WHATSAPP  <<< kwa mafundisho.

Biblia ni kitabu pekee chenye ukweli wote, umuhusuo Mungu, na mwanadamu, ni kitabu kinachoifunua njia ya uzima. Hivyo kuota unapewa biblia fahamu kuwa ndoto hiyo ni ya ki-Mungu, kwasababu kamwe shetani hawezi kukuongoza mahali ambapo utapata nuru ya maisha yako.

Zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Hivyo ikiwa wewe bado hujamjua Kristo, basi fahamu Mungu anakupenda na hivyo anataka kukuongoza katika ukweli wote, Ndio maana umeota unapewa biblia haijalishi utakuwa mwislamu, mhindu, mpagani n.k Fahamu kuwa Yesu anakupenda, na anataka kukuokoa. Hivyo unachopaswa kufanya ni kumkubali tu maishani mwako, ili aweze kukufikisha katika ukweli wote, na majibu yote ya maisha yako.

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya imani >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Baada ya hapo, tafuta kitabu hichi (BIBLIA), Haraka iwezekanavyo uanze kusoma. Huku ukisaidiwa na waalimu sahihi wa Neno la Mungu. Kumbuka Wewe kufika hapa sio bahati mbaya, tovuti hii uliyopo sasa, Bwana ameiweka kwa ajili yako ina mafundisho mengi yatakayoweza kukusaidia kuielewa biblia vizuri. (www.wingulamashahidi.org). Itembelee mara kwa mara. Yapo mafundisho mengi sana, pamoja na majibu ya maswali mengi ya biblia. Lakini pia kama unatumia mtandao wa Whatsapp basi bofya hapa >>> WHATSAPP

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUOTA UNAPEWA PESA| MAANA NA TAFSIRI YA KIROHO

Je! Kuota unakabwa, mara kwa mara ni ishara ya nini?

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya jivikeni silaha ya nia ile ile? (1Petro 4:1)

SWALI: Biblia inamaana gani kusema jivikeni silaha ya nia ile ile? (1Petro 4:1)

1 Petro 4:1-3

[1]Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 

[2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 

[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;


JIBU: Tukiangalia undani wa hilo neno hapo anaposema silaha ya nia. Ni kutuonyesha kuwa kumbe  “Nia ”, inaweza kuwa silaha.

Mara nyingi tunapofikiria silaha kibiblia mawazo yetu moja kwa moja yanakimbilia zile za  Waefeso 6:10-18, silaha za haki, kama vile upanga wa Roho ambalo ni Neno la Mungu, chapeo ya wokovu, ngao ya imani, dirii ya haki n.k. 

Lakini hapa tunaonyeshwa kuwa ipo pia silaha ndani ya Nia, ambayo nayo tunashauriwa tuwe nayo, kwasababu ilikuwa kwanza ndani ya Kristo.

Na silaha  yenyewe ilikuwa ni kukubali kuteswa katika mwili ili kuiua dhambi. 

Bwana wetu Yesu Kristo alijua dhambi ina nguvu sana pale mwili unapopewa raha zake. Hivyo aliikubali Nia ya kuteswa, ili dhambi ife.

Kumbuka sababu ya yeye kuchukiwa na watu, kuudhiwa, kuwindwa auawe, kuteswa mpaka kusulubiwa ni kwasababu alitangaza uadui na dhambi, Vinginevyo asingepitia maudhi yale katika mwili. Na tunaona mwisho wake ulikuwa ni ushindi. Kwani kwa kifo chake dhambi ilihukumiwa kabisa kabisa.

Alisema..

Yohana 7:7

[7]Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 

Hivyo maandiko yanatuambia na sisi pia, tujivike nia ile ile ya kukubali pia mateso kwa ajili ya Kristo. Kwasababu tukifanya hivyo tunaonyesha kuwa tumeachana na dhambi(tumeihukumu dhambi).

Kwa ufupi ni kuwa ukichukia maisha ya dhambi, tafsiri yake ni kukubali dhiki katika mwili kwa ajili ya Kristo. Hivyo zipende sasa dhiki hizo kama Kristo alivyozipenda, ili dhambi isikutawale. Hiyo ni Silaha kubwa sana.

2 Timotheo 3:12

[12]Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 

kubali shida, kwasababu umeamua kuacha ile biashara haramu, furahia kutengwa na kuonekana mshamba, kwasababu umeamua kuacha mienendo ya marafiki wabaya, penda kupigwa na kufungwa kwasababu unahubiri kweli. Hiyo ndio SILAHA YA NIA. iwezayo kuishinda dhambi.

Ndio maana vifungu vinavyofuata anasema..

“Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 

[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 

Daima tujivike silaha hii, tukikumbuka kuwa vita vyetu si vikali tena kama vile alivyovipiga Kristo.

Waebrania 12:4

[4]Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi; 

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?

NDUGU,TUOMBEENI.

DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)

KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.

Rudi Nyumbani

Print this post

Uchambuzi na Mwandishi wa kitabu cha Wagalatia

Kitabu cha Wagalatia ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika kwa makanisa aliyoyapanda. Tunaona mwanzoni kabisa mwa waraka huu Paulo mwenyewe anajitambulisha akionyesha kuwa yeye ndiye mwandishi.

Waraka huu unamwonyesha Paulo akiwastaajabia watakatifu wa kanisa la Galatia kwa kuacha Imani ambayo aliwaachia hapo mwanzo, alipokuwa analisimamisha kanisa hilo, jambo ambalo lilimfanya mpaka imani yake impelekee kufikiri kuwa wamelogwa(Wagalatia 3:1), kwa jinsi tu walivyoiacha imani kwa haraka.

Kwa mujibu wa waraka huu, tunaona Paulo alilijenga kanisa hilo katika msingi wa imani katika neema ya Yesu Kristo.Na si katika msingi wa matendo ya sheria kama kigezo cha kukubaliwa na Mungu.

Kutokana na kuwa kanisa hili lilikuwa na mchanganyiko wa wayahudi pamoja na watu wa mataifa waliomwamini Kristo.Hapo ndipo tatizo lilipoanzia baada ya baadhi ya wakristo wa kiyahudi kuanza kuwashurutisha watu wa mataifa kwa kuwaambia kwamba hawawezi kuokolewa kama hawataishika torati ya Musa, kama hawatatimiza maagizo kama tohara, kushika siku, miezi, na miaka.(Wagalatia 4:8-10)

Hivyo hiyo ikawafanya watu kuacha kuishi tena kwa Imani iliyo katika neema ya Kristo Yesu, na kuangalia matendo ya sheria kama ndio kigezo cha kukubaliwa na Mungu?

Hivyo Paulo alipojua mageuzi hayo, ndio akawaandikia waraka huo kwa ukali, akiwaambia wokovu wetu huja kwa imani iliyo katika Yesu Kristo itendayo kazi katika upendo. Na si katika matendo ya sheria. Kwasababu kama ingekuwa hivyo Kristo alikufa bure. Torati ingeendelea tu kutawala.

Wagalatia 5:6

[6]Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Akasema torati, haikuwahi kumkamilisha mtu, na mtu anayeishi kwa hiyo ametengwa na Kristo, bado yupo chini ya laana.

kuishi kwa sheria ni kurudia mafundisho manyonge.

Lakini Swali ambalo alitarajia lingeulizwa na wagalatia, ni hili;

Je sasa hatuna haja ya kuyatazama matendo mema, tuishi tu, kama tunavyotaka kwasababu tunahesabiwa haki kwa neema ya Kristo tu?

Mbeleni kabisa katika sura ya tano, Mtume Paulo alitolea ufafanuzi, na kuwaambia tukishaokolewa, Maana yake ni kuwa tumeusulubisha mwili pamoja na tamaa zake mbaya..Hivyo hakuna nafasi ya dhambi kupata nguvu ndani yetu.

Wagalatia 5:24

[24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Je hilo inawezekanaje? kama hatuna sheria?

Linawezekana kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Ambaye tumepewa na Mungu.

Wagalatia 4:6

[6]Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.

Hivyo Paulo anaendelea kueleza ni wajibu wa kila mwamini kutembea katika Roho. Ili awasaidie Roho kuzishinda tamaa zote za mwili, na mambo maovu.

Wagalatia 5:16-21

[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

[18]Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

,[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Je waraka huu ulilenga hasa nini?

Kwamba kwa nguvu zetu, au dini zetu au torati kamwe hatuwezi kumpendeza Mungu bali tuitegemee neema ya Kristo ambayo kwa hiyo tumepokea Roho awezaye kutufanya wakamilifu.

Hivyo ni wajibu wako kama mkristo. Kila wakati wote kujawa Roho (Waefeso 5:18). Ambayo hiyo huja kwa kuwa waombaji, wasomaji Neno, na kufanya ibada mioyoni mwetu wakati wote..

Tukiwa watu wa namna hiyo sheria wala dhambi inakuwa haina nguvu ndani yetu. Kwasababu tunakuwa chini ya neema ya Yesu Kristo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni uchafu gani unaozungumziwa katika Wagalatia 5:19?

je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?

Rudi Nyumbani

Print this post

Msingi wa imani ya kikristo ni upi?

Msingi ni chimbuko, au mwanzo au kiini cha kitu fulani.

Ni wazi kuwa kila jambo lina msingi wake. taifa lina msingi wake, taasisi ina msingi wake, kabila lina msingi wake vilevile pia imani ina msingi wake.

Hivyo tukirudi katika ukristo. Msingi wa imani yake ni upi?

Msingi wa ukristo ni YESU KRISTO mwenyewe, na kazi yake aliyoikamilisha ya kufa na kufufuka kwake. Na sio kanisa, au dhehebu, au mapokeo fulani, au kikundi fulani cha wanaharakati.

Pasipo Yesu hakuna ukristo.

Yeye anafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni, ambalo hakuna mjenzi aliyeweza kusimamisha jengo bila kuliweka hilo.

1 Petro 2:6

[6]Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. 

Habari kamili za Yesu, na kazi yake aliyokuja kuifanya duniani unaipata katika kitabu kimoja tu kiitwacho BIBLIA. Hivyo huwezi kutenganisha biblia na Yesu Kristo.

Ili mtu ashawishwe kuipokea imani, ni sharti, aisikie kwanza injili yake ambayo hiyo utaipata katika Neno la Mungu yaani biblia..(Warumi 10:17)

Mpaka mtu aitwe mkristo ni lazima amtambue kwanza Kristo ni nani, na nini amekileta duniani, vinginevyo hawezi kuwa mkristo, hata kama atajiunga na kanisa, au dhehebu na kuyashika mapokeo yote aliyoyakuta huko, au kuisoma biblia yote, huyo bado hajawa mkristo.

Ni muhimu sana kumtambua Yesu ni nani kwetu. Kumtambua Yesu kama mwana wa Mungu bado inaweza isikupe wokovu, hata kumtambua Yesu kama Mungu bado inaweza isikupe wokovu (ijapokuwa vyote hivyo ni vyeo vyake). Lakini vyeo hivyo sio kiini cha ukristo.

 Yesu ni nani na ni nini alikileta duniani?

Yesu ni MKOMBOZI, kama tafsiri ya jina lake linavyojieleza( Mathayo 1:21)

mkombozi wa nini?

Alikuja kutukomboa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu, Na kama ilivyo kanuni ya kiroho ili jambo hilo liweze kukamilika ilipasa itolewe kafara isiyo na kasoro yoyote(yaani dhambi). Na aliyeweza kukidhi vigezo hivyo ni Yesu pekee.

Ndio maana ilimgharimu afe, kama fidia ili sisi tupokee ondoleo la dhambi na msamaha wa dhambi kwa kifo chake. Hivyo yoyote anayeamini(yaani anayeupokea wokovu huo aliouleta).

kwa toba ya kweli na ubatizo, Basi anakuwa ameokoka, hivyo ile ghadhabu ya Mungu kwa wenye dhambi wote haiwi tena juu yake, tangu huo wakati anaitwa mbarikiwa, au mkristo, kwasababu dhambi zake zinakuwa zimefutwa kabisa.

Na zaidi ya hayo mtu huyu moja kwa moja anapewa zawadi ya Roho Mtakatifu, ambaye tangu huo wakati na kuendelea anakuwa ndani yake kama msaidizi, kumsaidia madhaifu yake, katika kuomba, kuijua kweli, kumkumbusha aliyoyasema Yesu, kumpasha habari ya mambo yajayo, na kumtia nguvu ya kumtumikia Mungu, pamoja na kumpa nguvu ya kushinda dhambi.

Huyu ndiye mkristo.

Swali ni je! umemwamini ipasavyo? au umempokea kwa namna ile ya kidini?

Usifikiri kuhama dini, wewe ni Kristo, au kuzaliwa kwenye familia ya kikristo wewe ndio mkristo, au kusomea theolojia, hapana hizo ni kampeni tu, ukristo halisi huja kwa kumwelewa Kristo ni nani na ni nini amekifanya kwako.

Ikiwa bado hujaokoka na unataka kumpokea leo ili upate ondoleo la dhambi zako. Basi uamuzi huo ni bora sana kwako. Wasiliana nasi namba uzionazo chini  kwa mwongozo wa sala ya toba.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

 +255693036618/ +255789001312

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

YESU NI NANI?

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?

Rudi Nyumbani

Print this post

ORODHA YA WAANDISHI WA BIBLIA.

Biblia kitabu kikamilifu, na kitakatifu kimeandikwa na waandishi Zaidi ya 40 kwa Uvuvio wa Roho Mtakatifu. Ndani ya biblia kuna taarifa zinazohusu maisha ya watu zilizobeba sauti ya Mungu nyuma yake, pia kuna taarifa za Mataifa mbalimbali pia zenye kubeba sauti ya Mungu nyuma yake, lakini Zaidi sana kuna Nabii za wakati ujao.

Ifuatayo ni orodha ya waandishi 40 wa Biblia kuanzia Agano la kale hadi Agano jipya.

Agano la kale.

  1. Amosi – Mwandishi wa kitabu cha Amosi
  2. Danieli – Mwandishi wa kitabu cha Danieli.
  3. Daudi- Mwandishi wa kitabu cha Zaburi, kwa baadhi ya Zaburi.
  4. Ezekieli- Mwandishi wa kitabu cha Ezekieli.
  5. Ezra- Mwandishi wa kitabu cha Ezra.
  6. Habakuki – Mwandishi wa kitabu cha Habakuki.
  7. Hagai – Mwandishi wa kitabu cha Hagai.
  8. Hosea- Mwandishi wa kitabu cha Hosea.
  9. Isaya- Mwandishi wa kitabu cha Isaya.
  10. Yeremia – Mwandishi wa kitabu cha Yeremia
  11. Yoeli – Mwandishi wa kitabu cha Yoeli
  12. Yona- Mwandishi wa kitabu cha Yona.
  13. Yoshua- Mwandishi wa kitabu cha Yoshua.
  14. Malaki- Mwandishi wa kitabu cha Malaki.
  15. Mika- Mwandishi wa kitabu cha Mika.
  16. – Mwandishi wa kitabu cha Esta.
  17. Musa – Mwandishi wa kitabu cha Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Kumbukumbu la Torati, Hesabu, Ayubu na Zaburi 90.
  18. Nathani (Nabii) – Mwandishi wa kitabu cha 1Samweli na 2Samweli (sehemu baadhi)
  19. Nabii Gadi- – Mwandishi wa kitabu cha 1Samweli na 2Samweli (sehemu baadhi)
  20. Nahumu- Mwandishi wa kitabu cha Nahumu.
  21. Nehemia- Mwandishi wa kitabu cha Nehemia.
  22. Obadia- Mwandishi wa kitabu cha Obadia.
  23. Samweli- Mwandishi wa kitabu cha Samweli (Sehemu baadhi)
  24. Sulemani- Mwandishi wa kitabu cha Mithali, Mhubiri na Wimbo ulio bora.
  25. Sefania -Mwandishi wa kitabu cha Sefania.
  26. Zekaria-Mwandishi wa kitabu cha Zekaria.
  27. Wana wa Kora-Mwandishi wa kitabu cha Zaburi 42, Zaburi 44-49, Zaburi 84-85, na Zaburi 87-88.
  28. Asafu- Mwandishi wa kitabu cha Zaburi 50, na Zaburi 73-83.
  29. Ethani – Mwandishi wa kitabu cha Zaburi 89 (sehemu).
  30. Heman – Mwandishi wa kitabu cha Zaburi 89 (sehemu).
  31. Aguri – Mwandishi wa kitabu cha Mithali 30.
  32. Lemueli – Mwandishi wa kitabu cha Mithali 31.

Agano Jipya.

  1. Mathayo – Mwandishi wa kitabu cha Mathayo.
  2. Marko – Mwandishi wa kitabu cha Marko.
  3. Luka – Mwandishi wa kitabu cha Luka na Matendo ya Mitume.
  4. Yohana – Mwandishi wa kitabu cha Yohana Mtakatifu na 1 na 2Yohana pamoja na Ufunuo.
  5. Yakobo – Mwandishi wa kitabu cha Yakobo.
  6. Yuda – Mwandishi wa kitabu cha Yuda.
  7. Paulo- Mwandishi wa kitabu cha Warumi, 1 na 2Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wakolosai, Wafilipi, 1 na 2Wathesalonike, 1na 2Timotheo, Tito na Filemoni.
  8. Petro – Mwandishi wa kitabu cha 1 na 2Petro.

Kwanini waandishi wapo Zaidi ya 40 na si 40 kamili?.. Ni kwasababu biblia pia imewataja wana wa Kora, ambao hatujui walikuwa ni wangapi, zaidi sana yupo mwandishi wa kitabu cha Waebrania, ambaye hajatajwa ni nani, huenda akawa ni Mtume Paulo, lakini kama si yeye bali ni mwingine, basi ataongezeka katika idadi ya walioiandika biblia.

Kumbuka tena, biblia ni kitabu cha Mungu kilichoandikwa na WATU, kwa uvuvio wa ROHO MTAKATIFU, Hivyo maneno yaliyoandikwa ndani ya Biblia, yana uzima.

2Timotheo 3:16  “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.

Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume.

Je ni Mungu au Malaika?

Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Je kweli Abramu alikuwa hajui aendako kulingana na Waebrania 11:8?.

Swali: Je kipindi Ibrahimu anatoka Uru ya Ukaldayo, hakuwa anajua anakokwenda kwamba ni Kaanani? au alikuwa anaongozwa na Roho Mtakatifu mpaka pale alipofika, ndipo Bwana akamwambia hapo hapo atulie?…na mbona tukisoma Mwanzo 12:5 tunaona kama Abramu alikuwa anajua kabisa anakoelekea, au je biblia inajichanganya?


Jibu: Biblia, Neno la Mungu halijichanganyi kamwe..

Turejee …

Waebrania 11:8 “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka ASIJUE AENDAKO”.

Hapa ni kweli panaonesha kuwa Ibrahimu alikuwa hajui aendako, lakini hebu tusome maandiko mengine ndipo tutapata kuelewa zaidi..

Mwanzo 12:1 “BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka………………

5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani”

Hapa panaonyesha kuwa Abramu alikuwa anajua anakokwenda, kuwa ni Kaanani, Je lipi ni sahihi?

Jibu ni kwamba Abrahamu alikuwa anajua anakokwenda isipokuwa alikuwa hajui kama nchi hiyo aiendeayo (yaani ya Kaanani) kama ndio itakuwa ya ahadi..

Hivyo alienda mpaka alipofika na alipofika ndipo Mungu akamtokea na kumwambia kuwa nchi hiyo aliyopo ndiyo itakuwa milki yake (ya ahadi).

Mwanzo 12:5 “Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.

6 Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.

7 BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea”

Sasa swali linakuja, je ni kitu gani kilichomwelekeza Abramu aende nchi ya Kanaani na si nchi nyingine?

Tulirejea ule mlango wa 11 wa kitabu cha Mwanzo, tunasoma kuwa wazo la kuhama Uru wa Wakaldayo na kuelekea Kanaani halikuanzia kwa Abramu, bali lilianzia kwa baba yake aliyeitwa Tera, huyo ndiye aliyefikiri kuhama Ukadayo na hata kuchukua hatua ya kuhama pamoja na watoto wake wote ikiwemo Abramu.

Mwanzo 11:31 “Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko”.

Umeona hapo?..sio Abramu aliyekuwa na wazo la kuondoka Ukaldayo bali ni Tera, na sababu za kuwaondoa kule hazijulikani, kwani biblia haijaweka wazi, labda huenda ni maasi ya nchi hiyo, au sababu nyingine za kijamii au kibiashara.

Lakini katika wazo hilo la kuhama, lilikuwepo pia kusudi la Mungu ndani yake, kwamba Abramu afike Kanaani.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Abramu alijua anakoenda, lakini hakujua nchi atakayopewa mpaka alipofika.

Nini tunajifunza hapo?

Wakati mwingine Bwana anaweza kutumia wazo la mtu mwingine kukupeleka wewe mahali Mungu anapotaka uwe.

Hivyo wakati mwingine usinung’unike unapoona unahamishwa mahali ulipo, kwani pengine Mungu anakupeleka mahali anapotaka wewe uwe, na ukishafika ndipo atakuonyesha.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya dhabihu na matoleo hukutaka? (Waebrania 10:5).

Swali: Je Mungu hapendezwi na dhabihu na matoleo, kulingana na mstari huo?


Jibu: Turejee..

Waebrania 10:5 “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari”.

Andiko hili limerejewa kutoka katika Zaburi 40:6, tusome ili tupate maana kamili.

Zaburi 40:6 “Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,

Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka”.

Hapo imewekwa vizuri kuwa ni kafara na sadaka zinazotolewa kwaajili ya DHAMBI!! ndizo asizozitaka…

Sasa Dhabihu ni sadaka za kuteketezwa (ambazo ni kafara za wanyama) zilizokuwa zinatolewa kipindi cha agano la kale kwaajili ya kufunika dhambi..

Na kasoro ya dhabihu za wanyama ndio hiyo, ilikuwa haiondoi dhambi bali inafunika tu..

Kwahiyo hapo anaposema “Dhabihu na matoleo hukutaka”.. alimaanisha kuwa hizo dhabihu za wanyama hazifai katika kumwondolea mtu makosa yake na kumtakasa bali mwili wa Yesu na damu yake ndio iwezayo kumtakasa mtu na kumwondolea kabisa dhambi zake.

Ndivyo maandiko yasemavyo kuwa damu za mbuzi na mafahali haziwezi kuondoa dhambi na kumtakasa mtu bali zilikuwa zinafunika tu.

Waebrania 10:3 “Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.

4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi”

Lakini dhabihu ya mwili wa YESU, kupitia kumwagika kwa damu yake, unaondoa kabisa dhambi… Na hiyo ndio sadaka Mungu aliyoihitaji na sio dhabihu za kondoo na mbuzi na mafahali.

Waebrania 10:10 “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu”.

Lakini kuhusiana na utoaji wa sadaka ni kwaajili ya shukrani, au kwaajili ya kazi ya ufalme wa mbinguni ni jambo linalompendeza Mungu na lenye baraka.

Lakini kama ni kwaajili ya dhambi (hakuna sadaka inayoweza kuondoa dhambi)..isipokuwa damu ya YESU ambayo tayari tumeshalipiwa bureee… tunachopaswa kufanya ili sadaka hiyo ifanye kazi juu yetu ni KUTUBU TU kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi!.

Tukiweza kutubu kwa kumaanisha basi tunapata msamaha na ondoleo la dhambi bure.

Je unaye YESU maishani?.

Kumbuka daima kuwa mwisho wa dunia upo, kama tu vile mwisho wa maisha ulivyo, ikiwa leo hii damu ya YESU si kitu cha thamani kwako, utasimamaje siku ile ya mwisho mbele zake?..Tafakari mara mbili.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Je maji na giza viliumbwa siku ya ngapi?

Swali: Je vitu kama giza, na maji viliumbwa siku ya ngapi, maana tunaona wakitajwa tu wanyama na mimea, je hivi vingine viliumbwa lini?


Jibu: Ni kweli katika kitabu cha Mwanzo tunaona uumbaji unaanza kwa kusema “giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji”, lakini haitaji ni lini giza liliumbwa wala ni lini maji yaliumbwa, badala yake tunaona uumbaji unaendelea na vitu vingine kama mimea pamoja na wanyama na wanadamu?..

Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji”.

Jibu la swali hili lipo katika mstari huo wa kwanza..

Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”.

Neno “hapo mwanzo”… halimaanishi kile kipindi cha siku saba (7) bali linamaanisha mwanzo kabisa wa uumbaji kabla ya kitu kingine chochote, Mungu aliumba mbingu (hii yenye mawingu na sayari) pamoja na mbingu ile yenye Malaika watakatifu.

Na vile vile aliumba “NCHI” Au kwa lugha nyingine ARDHI/DUNIA. Na ili ardhi iweze kukamilika ni lazima iwe na malighafi zake zote kama udongo, mchanga, mawe, milima, mabonde, chuma, madini, moto na maji na mengineyo.

Vile vile ili mbingu ikamilike lazima iwe na nyota na mwanga uwepo na giza liwepo, kwahiyo vitu hivi vyote viliumbwa Hapo Mwanzo, kabla ya zile siku sita za uumbaji.

Na baada ya Mungu kuumba Mbingu na nchi, hatujui ni kitu gani kilitokea kikaifanya nchi/dunia yenye milima na mawe na madini na mabonde na maji kuwa UKIWA! Au kwamba Mungu ndio aliiumba ikae hivyo ukiwa kwa kipindi Fulani cha muda..hatujui!, labda tutakuja kujua tutakapomaliza maisha haya na kufika huko kwake, tutamwuliza, lakini tunajua kuwa alisema hakuiumba ukiwa, bali ikaliwe na watu.

Isaya 45:18 “Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine”

Hivyo kama hakuiumba ikae ukiwa bali ili ikaliwe na watu, basi hana budi kuiikarabati na kumweka mwanadamu humo, na ndipo hapo siku sita za uumbaji wa wanyama na wanadamu na miti zilipoanza..

Lakini kiuhalisia tayari mbingu na nchi zilikuwa zimeshaumbwa hapo kabla, na malighafi zake zote (kama maji, udongo, mawe, madini, giza, hewa n.k)..na ndio maana hatuoni vikitajwa katika uumbaji.

Lakini pamoja na hayo, upo unabii unaoonyesha kuwa dunia itakuja kuwa tena ukiwa siku za mwisho, kipindi ambacho ghadhabu ya Bwana MUNGU itakapokuja kumwagwa juu wa wanadamu wote wakosaji, ambayo hata mmoja wetu hapaswi kuwepo..

Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze”.

Isaya 24:1 “Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake”.

Jambo litakalotokea siku hiyo ni lile tunalolisoma katika kitabu cha 2Petro 3:10-12 na Isaya 34:4.

Lakini wateule, waliomwamini Bwana na kuoshwa kwa damu yake, hawatakuwepo katika siku hiyo ya ghadhabu yake, kwani watakuwa mbinguni pamoja na Bwana.

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post