SWALI 1:Bwana Yesu aliposema huu mfano alikuwa anamaanisha nini?..
“Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na WATOTO wanaokaa SOKONI,WANAOWAITA wenzao,wasisema,Tuliwapigia FILIMBI,wala hamkucheza; TULIOMBOLEZA,wala hamkulia.MAANA YOHANA ALIKUJA,HALI WALA HANYWI,WAKASEMA,YUNA PEPO.MWANA WA ADAMU ALIKUJA,AKILA NA KUNYWA,WAKASEMA,MLAFI HUYU,NA MLEVI,RAFIKI YAO WATOZA USHURU NA WENYE DHAMBI!” NA HEKIMA IMEJULIKANA KUWA INA HAKI KWA KAZI ZAKE”.(Mathayo11:16-19).
JIBU: Mfano huo ni sawa ni kizazi cha sasa hivi tulichopo tuchukulie tu mfano, Mtu akitokea ni mtumishi wa Mungu kweli, maisha yake yote ameyachagua ni kukaa tu kanisani, au milimani kuomba, hafanyi kazi yoyote isipokuwa ni kuomba tu, na kuhudumu kanisani, hana pesa nyingi, nguo zake sio mpya sana, hana mke, wala marafiki, yeye kazi yake ni kumtumikia tu Mungu basi, kajikana maisha yake yote hataki chochote isipokuwa Mungu kajizuia kila kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni ..Unadhani watu huku nyuma watamchukuliaje mtu kama huyo??..Si ajabu watamwita mlokole masalia, au kalogwa, watasema Mungu hayupo hivyo, Mungu anataka watumishi wake wawe na maisha ya kujifurahisha, kama vile Sulemani, na sio kuwa kama vichaa wa barabarani wasiokuwa na malengo..watamwambia hakika wewe utakuwa umeingiliwa na roho nyingine ambayo si ya Mungu….hivyo hatutaweza kukusikiliza mtu kama wewe maskini wa roho na kimawazo…sisi tunawasikiliza wahubiri wenye malengo, na mafanikio.
Lakini watu hao hao, mfano wakimuona mtumishi wa Mungu kweli labda Mungu kampaka mafuta anahubiri Neno na Mungu katika kweli yote, kambariki na maisha mazuri ya duniani, labda kampa nyumba nzuri, nguo nzuri, kampa familia nzuri, kampa mali nyingi, analo kanisa kubwa, ..utashangaa watasema, watumishi wa Mungu huwa hawapo hivyo, watumishi wa Mungu hawawezi wakawa matajiri, huwa wanakaa tu milimani wanautafuta uso wa Mungu usiku na mchana, na sio kwenye majumba ya kifahari kama watu wa mataifa…..Kwahiyo kwao pia watasema hatuwezi kuwasikiliza nyie matapeli mnakula Fedha za waumini..
Na ndivyo ilivyokuwa katika mfano huo, Mungu alipojaribu kuwapeleka Israeli nabii aliyejikana kwa kila jambo, (Yohana mbatizaji) wakasema mtu wa kawaida hawezi kuishi maisha kama hayo ya kutokula wala kujichanganya na wengine, ni lazima atakuwa anao pepo, Lakini Bwana alipokuja anakula na kunywa pengine akidhani kuwa labda watamsikia na yeye wakamwambia ni mlafi na mlevi, manabii wa Mungu hawawi hivyo…….Ndio mithali hiyo inakuja, walipopigiwa filimbi ili wacheze wakakataa, pengine wanahitaji maombolezo, lakini pia walipoombolezewa hawakulia,..sasa waelewekeje! Kwenye raha hawapo kwenye huzuni hawapo..Na ndivyo ilivyo katika kizazi hiki..hata kipewe ishara gani ya nabii hakitaamini isipokuwa wale tu waliokusudiwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaoamini ..
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU?
WATU WASIOJIZUIA.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)
Rudi Nyumbani:
Print this post
SWALI: Yohana hapa anasema Bwana ametufanya kuwa Ufalme na Makuhani Ufunuo1:6 …(Sasa hapa anamaanisha sasa hivi sisi ni wafalme na makuhani au ni katika ule umilele ujao?) na je! ni sahihi kumuita mwanamke kuhani??
JIBU: Ndio sasahivi sisi ni ufalme na makuhani wa Bwana katika roho,..kama vile Bwana Yesu alivyokuwa duniani tangu siku za kuzaliwa kwake mpaka siku za kuondoka kwake,,…tayari yeye alishakuwa mfalme,..Kama unakumbuka wale Mamajusi walimuuliza Herode yuko wapi mfalme wa wayahudi tunataka kumsujudia (Mathayo 2:3)? unaona hapo tangu alipokuwa mdogo tayari ni mfalme, pia Pilato tunaona baadaye siku chache kabla ya kuondoka kwake duniani alikuja kumuuliza Bwana …
Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.
Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?
35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.
Kwahiyo hata sisi tuliookolewa, na kuoshwa kwa damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, ni makuhani na ufalme. Lakini mambo hayo yatakuja kudhihirika katika ulimwengu unaokuja kama Bwana alivyosema ufalme wake ni wa ulimwengu unaokuja!…Na ukuhani wenyewe hautakuwa wa kuvukiza uvumba tena, ule ulikuwa ni taswira ya mambo yatakayokuja yanayofunua kumkaribia Mungu..
Vivyo hivyo na katika huo ulimwengu unaokuja hatutakuwa tu wafalme bali tutakuwa na uwezo kumkaribia Mungu kwa namna ya kipekee mfano wa makuhani, ambao sio watu wote watapewa uwezo huo bali ni wale watakaoshinda tu!.. Na thawabu hiyo itakuwa ni kwa wote…wanawake na wanaume.
Hivyo ukuhani wako mbele za Mungu unautengeneza ukiwa hapa hapa duniani, kwahiyo tunapaswa tukaze mwendo ili tusikose thawabu hizo.
Ubarikiwe sana.
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?
NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO?
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
JIBU: SALA ni neno la ujumla linalojumuisha maombi yote, iwe ya shukrani, mahitaji, ibada, sifa, toba,ulinzi, Baraka n.k…Kwamfano yale maombi ya Baba yetu uliye mbinguni Yesu aliyowafundisha wanafunzi wake….Ni mfano wa SALA.
Kwahiyo unaposhukurau ni sala, unapoomba toba ni sala, unapomba hitaji lolote Kwa Mungu kama chakula, mavazi, nyumba n.k. hizo zote ni sala, unapomshukuru Mungu kwa maombi ni sala, na pia unapomwimbia Mungu sifa kama Daudi alivyokuwa anafanya kadhalika ni sala.
Lakini maombi ya Dua ni tofauti kidogo na sala, kwasababu sala ni Neno la ujumla kama tulivyosema lakini DUA imeegemea sana katika maombi ya MAHITAJI..
Kumbuka pia kuna maombi ya kawaida ya mahitaji haya ni yale ambayo unamwomba Mungu akufanyie jambo Fulani, kama tulivyosema hapo juu kuomba riziki, chakula, pesa, n.k. lakini Dua ni maombi ya hitaji isipokuwa haya yanakwenda ndani zaidi, (na ya masafa marefu) ndiyo yanayohusisha na kuomba rehema, kumsihi Mungu akutendee jambo Fulani ambalo pengine usingestahili kulipata, na dua huwa inaambatana na kujinyenyekeza kwa hali ya juu, na wakati mwingine inahusisha pia na kufunga kwa muda mrefu. Kwamfano unapoomba toba juu ya Kanisa, nchi au familia yako, au ndoa yako kwamba Mungu airehemu kwa makosa Fulani yaliyofanyika, huwezi kwenda kwa maombi ya kawaida tu kama unavyokwenda kumwomba akupe chakula, au pesa, au mavazi, au kazi, hapana hapo utamwendea kwa unyenyekevu, kwa kuomboleza, wakati mwingine kufunga kumsihi Mungu juu ya uovu wa kanisa, au nchi au familia yako ausamehe, sasa hiyo ndio inayoitwa Dua.
Mfano ulio hai tunaweza kuuona kwa Danieli, pale alipoomba DUA juu ya makosa na uovu wa watu wake uliowasababishia mpaka kupelekwa Babeli,
Danieli 9: 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa MAOMBI NA DUA, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. 4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako…………; )
Danieli 9: 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa MAOMBI NA DUA, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako…………; )
Maombi ya namna hii tunaona pia yalifanyika kwa Nehemia, pale alipopata taarifa juu ya uharibifu wa Yerusalemu na maovu ya watu wake yaliyokuwa yametendeka Yerusalemu, aliomba Dua kwa Mungu kwa kuomboleza na kufunga kama Danieli alivyofanya. Soma (Nehemia 1).
Tunaona pia kwa malkia Esta na wayahudi wote walipotangaziwa kuuawa, walijinyenyekeza mbele za Mungu kwa kufunga na kuomboleza kwa ajili ya maangamizi yao, Mungu akasikia dua zako, akawaokoa na maangamizi.
Kadhalika na Daudi mara nyingi alipokuwa akipitia shida, aliingia katika maombi ya Dua kwa ajili yake mwenyewe na Mungu amwepushe na adui zake.(Zaburi 28:2, zaburi 30:8).
Bwana wetu Yesu Kristo pia alikuwa anaomba Dua. Waebrania 5: 7 “Yeye [YESU], siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, MAOMBI NA DUA pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;” Unaona hapo?
Hata sisi pia tunapaswa tuwe watu wa SALA na DUA kwa ajili yetu wenyewe kuomba rehema mbele za Mungu, na kwa ajili ya Kanisa, na kwa ajili ya Nchi ili Mungu aweze kufungua mambo mengine yaliyofungwa mbele yetu. Kwasababu biblia pia imetukumbusha hilo katika:
1Timotheo 2: 1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka DUA, na SALA, na MAOMBEZI, na SHUKRANI, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;”
1Timotheo 2: 1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka DUA, na SALA, na MAOMBEZI, na SHUKRANI, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;”
FAIDA ZA MAOMBI.
MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.
MAOMBI YA YABESI.
ELIYA ALIOMBA KWA BIDII, JE! KUOMBA KWA BIDII KUKOJE?
OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!
MKUU WA GIZA.
MJI WENYE MISINGI.
JIBU: Kuongoka maana yake ni kugeuka au kutubu..Katika habari hiyo tunasoma..
Luka 22: 31 “Akasema [YESU], Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe UTAKAPOONGOKA waimarishe ndugu zako.33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Luka 22: 31 “Akasema [YESU], Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe UTAKAPOONGOKA waimarishe ndugu zako.
33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.
34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Tunaona hapo Bwana alishafahamu kuwa wakati wa mamlaka ya giza umefika, kwa Bwana pamoja na wanafuzi wake katika muda mchache mbeleni watatiwa chini ya yule mwovu, na ndio maana kwa kulijua hilo kuwa wanafunzi wake watashindwa kustahimili majaribu pasipo msaada wake, alimwambia Petro maneno yale, “Nimekuombea wewe ili imani yako isitindike”, kwasababu shetani atakwenda kuwapepeta kama ngano, hivyo inaweza ikawapelekea kuikana Imani mara moja, na kurudi nyuma kuacha kabisa kuambatana na Bwana…
Tena Bwana akamwambia nimekuombea ili Imani yako isitindike pale utakapojaribiwa, na utaona jaribu lile lilikuwa ni kumkana Yesu mara tatu muda mchache baadaye, hivyo kama Bwana asingemuombea angeweza kujinyonga kabisa kama Yuda au kuacha kabisa kuambatana na njia ya Kristo badala ya Kuongoka(kutubu). Utakuja kuona Wale wanafunzi wengine walikuwa tayari katika mashaka ya kuiacha imani..Hivyo Bwana alimchagua Petro ili baada ya yeye kutubu (kuongoka) kwa machozi pale alipata nguvu ya kwenda kuwaimarisha na wale wanafunzi wengine waliokuwa wametawanyika.
Na ndio maana baada ya Bwana kufa Petro ndiye alikuwa anashughulika kuwakusanya wanafunzi wote, hata wakati wa kwenda kuvua samaki wanafunzi wengine walitaka kwenda nae, utaona pia yeye ndiye aliyetoa pendekezo la kuteuliwa mwanafunzi mwingine mahali pa Yuda kadhalika hata katika siku ile ya Pentekoste Petro ndiye alikuwa wa kwanza kufungua kinywa na kuwaeleza watu upya habari ya maneno ya wokovu kwa nguvu nyingi…Kwahiyo Petro alishughulika sana kuwaimarisha ndugu zake (mitume) waliokuwa naye.
Kadhalika hili neno KUONGOKA, limeonekana katika
1Timotheo 3: 2 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)6 WALA ASIWE MTU ALIYEONGOKA KARIBUNI, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.”
1Timotheo 3: 2 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
6 WALA ASIWE MTU ALIYEONGOKA KARIBUNI, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.”
Sasa hapo neno hilo limetumika kwa mtu aliyetubu hivi karibuni (yaani kumpa Bwana maisha yake hivi karibuni)..Mtume Paulo alitoa maagizo kwamba kazi ya uaskofu inahitaji mtu aliyedumu kwa muda fulani mrefu katika Imani, ili isiwe rahisi kwa mtu huyo kunaswa na mitego ya ibilisi kiwepesi.
Tunajifunza nini?..Kama tu vile shetani alivyowataka mitume kuwapepeta kama ngano, na sisi vivyo hivyo anatutaka leo kutupepeta, na nia yake ni tuikane imani, hivyo wewe kama mkristo ni jukumu lako kudumu katika fundisho la mitume(biblia), na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali, kama maandiko yanavyotuagiza katika (Matendo 2:42 ). Ili uwe na nguvu ya kushinda mawimbi ya shetani.
NINI TOFAUTI YA HAYA MANENO. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
NOTI YA UFALME WA MBINGUNI.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
JIWE LA KUKWAZA
JIBU: Kwanza, ni vizuri kufahamu kubatizwa, ni tendo la rohoni, na linapaswa litoke rohoni, kitendo cha mtu kwenda kubatizwa kwanza anapaswa awe tayari kugeuka [kutubu], kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake, kuacha maisha ya dhambi, na kuanza maisha mapya katika Kristo…
Sasa mtu wa namna hiyo BWANA YESU KRISTO akishaona moyo wake kweli umedhamiria kugeuka, na hajafanya hivyo kama ni desturi za kidini tu ili kutimiza wajibu, sasa moja kwa moja mtu wa namna hiyo anapewa UWEZO WA KUSHINDA dhambi, kwasababu yeye mwenyewe hawezi. soma
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”
Sasa Uwezo huo hauji juu ya mtu kama hajadhamiria kabisa kuacha dhambi zake, ikiwa na maana kudhamiria kuacha ulevi, anasa, uasherati, utukanaji, uongo, wizi na mambo yote yanayofanana na hayo..
Hivyo kitendo cha Kubatizwa kama mtu akizingatia vigezo hivyo, ubatizo ule unakuwa na maana kubwa sana katika maisha yake kuanzia huo wakati na kuendelea, yeye anakuwa ni milki halali ya Kristo YESU. Ile hatia ya dhambi Bwana anaifuta juu yake, na UWEZO wa kushinda dhambi unaachiliwa juu yake..Kwahiyo, kitu anachopaswa kufanya sasa kuanzia huo wakati wa kubatizwa na kuendelea, ni KUTOKUMZIMISHA ROHO WA MUNGU NDANI YAKE….Na hii inakuja kwa kudumu katika usafi wa roho, na kujifunza Neno la Mungu, na kukaa karibu na ndugu wa kikristo wenye Imani moja na wewe.
Ubarikiwe.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?
CHANZO CHA MAMBO.
SWALI: Naomba kufahamu kwanini Bwana wetu Yesu Kristo kwanini amesema “Waandishi na MAFARISAYO wameketi katika KITI CHA MUSA;” basi YEYOTE watakayo watakayowaambia,MYASHIKE na KUYATENDA;LAKINI KWA MFANO WA MATENDO YAO MSITENDE;maana wao hunena lakini hawatendi.Wao hufunga MIZIGO MIZITO na kuwatwika watu mabegani mwao;WASITAKE WENYEWE KUGUSA KWA KIDOLE CHAO.Kwakuwa hupanua HIRIZI ZAO,huongeza MATAMVUA yao”.(Mathayo23:1-5).?
JIBU: Kwanini alisema hivyo sababu ameshaitoa hapo…“hunena lakini hawatendi” hiyo ndiyo sababu akawaambia wanafunzi wake wasitende matendo kama yao.Na aliposema mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa anamaana mafarisayo na masadukayo, wameisoma sana torati ya Musa na ni wepesi kuhukumu kwa kupitia hiyo torati, hivyo wanakuwa kama wawakilishi wa Musa, jambo lolote likitokea mfano mwanamke kafumaniwa kwenye uzinzi ni rahisi kutumia torati ya Musa kuhukumu,.na hali wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanafanya hayo hayo.
Na aliposema wao WANAPANUA HIRIZI ZAO hakumaanisha wao wana hirizi, kama hizi wanazotumia wachawi, hapana! Neno hirizi zamani lilitumika kuwakilisha “kiboksi” kidogo kilichobeba maandishi Fulani madogo ambacho watu walikuwa wanatembea navyo, kama kumbukumbu kila waendapo wasisahau yale aliyoyakusudia kuyafanya au kuyatunza katika maisha yake. Mfano katika dunia ya sasa wanandoa wanavaa pete na kutembea nazo kila mahali,..zile ni hirizi za wakati huu wa sasa, kwamba mtu akiitazama inamkumbusha agano aliloingia yeye na mke wake mbele za Mungu siku ile walipofunga ndoa.
kwahiyo, wana wa Israeli waliamuriwa na Mungu waandike baadhi ya vifungu vya maneno ya torati katika viboksi Fulani vidogo kisha wawe wanatembea navyo popote waendapo, wavivae kama utepe katikati ya macho yao, au mkononi. sasa huo utepe waliokuwa wanauvaa katikati ya kipaji cha uso ndio unaoitwa hirizi.
Tukisoma
(kumbu 6:4-9) “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
Kwasasa jambo hili limezoeleka kuonekana likifanywa na wachawi, lakini asili ya neno hirizi sio uchawi. Kama vile neno kafara lisivyokuwa la wachawi, shetani anatabia ya kugeuza mambo na kuyafanya yawe yake. Isipokuwa sisi wakristo hatufungi hirizi mwilini bali hirizi zetu [sheria za Mungu] tunazifunga rohoni.
Sasa hawa mafarisayo, wenyewe badala ya kuweka utepe mdogo tu(mfano wa kiboksi kidogo cha nchi 2) katikati ya macho yao, wao waliongeza ukubwa wa utepe likawa ni li-boksi likubwa ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu sana,
kadhalika na MATAMVUA yao waliyaongeza, matamvua ni sehemu ya mwisho wa kanzu za wayahudi katika sehemu za mikono, hizo waliamuriwa wazishone wakichanganya na michirizi ya rangi ya samawi(yaani blue), lakini wao wakawa wanashona makubwa kupita kiasi ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu zaidi.
Hivyo badala ya hizo hirizi zao kuwa ni za kiasi tu, wao wakaziongeza na kuwa kubwa ili waonekane na watu ni watakatifu zaidi na wanashika sheria zaidi, kadhalika na matamvua yao badala yawe ya madogo kiasi wao wakayafuma na kuwa mafundo makubwa kupita kiasi ili kila mtu atakapowaona waonekane kuwa wanaijua sheria zaidi, ili kuelewa vizuri tazama picha chini…
Huu ni mfano dhahiri, wa viongozi wa kidini na madhehebu na baadhi ya wakristo wa sasa, wanavaa majoho marefu, na misalaba mikubwa, na kubeba biblia kubwa na kujionyesha mbele za watu, nia yao hasaa sio kumtangaza Kristo, hapana bali waonekana na watu kuwa ni watu wa kuheshimiwa zaidi na kuogopwa katika kanisa, nia yao ni kuonyesha vyeo vyao, lakini ndani yao hawayashiki yale wanayoyaonyesha kwa nje.
Hivyo tunafundishwa na sisi pia tusiwe wanafki, kuigiza mambo ambayo sisi wenyewe hatuyatendi ni unafki mbele za Mungu..na itageuka kuwa OLE!! Katika siku ile.
CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!.
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
MELKIZEDEKI NI NANI?
Kadhalika naomba kufahamu.. (b)Mashahidi watatu washuhudiao mbinguni wanatajwa, Neno ambaye ndiye Yesu bado ana nafasi ya mwana hata baada ya kutoka duniani? (c)mashahidi wa duniani (roho,maji na damu) wanaotajwa ni kwa namna gani wanashuhudia? BARIKIWA SANA !
JIBU: A) Kwanza ni muhimu kufahamu wakati, Bwana Yesu alipokuwa pale Kalvari, baada ya kuchomwa mkuki ubavuni na yule Askari wa Kirumi, kulitoka MAJI NA DAMU, ikiashiria kuwa dhambi zetu, zinaoshwa kwa damu na kwa njia ya maji. Ikiwa na maana kuwa mtu ili apate ondoleo la dhambi zake ni lazima akabatizwe kwanza kwa kuzamishwa katika MAJI mengi kama ishara, na ndipo dhambi zake ziweze kusafishika kwa DAMU ya Yesu Kristo. Na ndio maana Bwana alisema aaminiye na kubatizwa ataokoka…
B) Na aliposema wapo watatu washuhudiao mbinguni na wapo watatu washuhudiao duniani, haikumaanisha kuwa kuna nafsi tatu za watu duniani na kuna nafsi tatu nyingine mbinguni. Hapana haimaanishi hivyo kwasababu maji yatashuhudiaje? Hayawezi kuongea wala kuhubiri injili, hivyo anaposema wapo watatu duniani yaani maji, damu na Roho anamaanisha zipo hatua tatu “mwanadamu kuzifuata ili kukamilika duniani” yaani mtu anapaswa aoshwe dhambi zake kwa kubatizwa katika MAJI, ili apate ondoleo la dhambi zake kwa DAMU ya Yesu na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye ndiye muhuri wa Mungu.Hatua hizi tatu ndizo zinazoshuhudia kwamba mwanadamu akizifuata hizo amekombolewa na kukamilishwa.
Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
C) Na aliposema wapo watatu mbinguni hakumaanisha tena kuna nafsi tatu mbinguni kila moja inajitegemea, hapana! Biblia ilimaanisha kuwa zipo hatua tatu mbinguni MUNGU MMOJA alizozitumia “kumpatanisha mwanadamu na nafsi yake ”, hatua ya kwanza alizungumza na wanadamu kama Baba(yaani MUNGU JUU YETU), hatua ya Pili alizungumza nasi kama NENO(MUNGU PAMOJA NASI,EMANUELI,)
Waebr 1:1“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika MWANA, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.”
Hatua ya tatu kazungumza nasi kama ROHO MTAKATIFU(MUNGU NDANI YETU), katika Roho Mtakatifu ndio utimilifu wa Mungu kuzungumza katika ukaribu zaidi, yeye ndiye atufundishaye mioyoni mwetu na kututia katika kweli yote,
Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 WALA HAWATAMFUNDISHA KILA MTU JIRANI YAKE, NA KILA MTU NDUGU YAKE, WAKISEMA, MJUE BWANA; KWA MAANA WATANIJUA WOTE, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 WALA HAWATAMFUNDISHA KILA MTU JIRANI YAKE, NA KILA MTU NDUGU YAKE, WAKISEMA, MJUE BWANA; KWA MAANA WATANIJUA WOTE, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Kwahiyo kwa hatua hizi tatu mwanadamu amepatanishwa na kusogezwa karibu zaidi na Mungu….Tofauti na zile za kwanza(maji,damu, na Roho) ambazo ni mwanadamu anapaswa azifuate kukamilika mbele za Mungu, lakini hizi za mwisho(Baba, Neno na Roho) ni Mungu anazitumia kutupatanisha sisi na nafsi yake (au kutusogeza karibu zaidi na yeye)..
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??
JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
BIDII YA MFALME YOSIA.
MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.
SWALI: Bwana alikuwa na maana gani kusema mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili?(Mathayo 5:39)
JIBU: Bwana Yesu aliposema mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili na sawasawa na pale aliposema pia “mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.”
Kama tunavyofahamu ukiwa kama mkristo ni lazima ukutane na vikwazo vingi kutoka kwa wasioamini, Hii ikiwa na maana kuwa kwa kufanya hivyo utakuwa umeushinda uovu na utafanikiwa kuiokoa roho ya mtu huyo badala ya kuingamiza. kwasababu kwa kufanya vile Biblia inasema utakuwa umempalia makaa ya moto kichwani pake,atakuwa akijiuliza kila siku ni kwanini sikutendewa kama mimi nilivyomtendea yeye?. hivyo baadaye atajiona yeye ndiye mwenye makosa na kugeuka na kutubu kwasababu yale makaa ya moto yatakuwa yanachoma ndani yake. Biblia inasema katika..
Mithali 25: 21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”.
Mithali 25: 21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;
22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”.
Lakini sasa mfano atakapokupiga na wewe ukamrudishia, au atakapochukua mali yako nawe ukaenda kuchukua ya kwake, atakapokuabisha na wewe ukamwaibisha, atachomwaje dhamira na kujiona kama yeye ni mwenye dhambi?, hivyo atabakia kuwa vilevile tu na kukuona wewe ni mtu wa kawaida tu kama watu wengine walivyo. Na ndio maana Bwana Yesu alisema tuushinde ubaya kwa wema, ili tuwe wakamilifu kama Baba yetu alivyo mkamilifu. Aliendelea kusema..
Mathayo 5:41 “Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”
Mathayo 5:41 “Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”
KISASI NI JUU YA BWANA.
NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.
SHUKURU KWA KILA JAMBO.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.
KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?
JIBU:Tukisoma
Marko 2:2 “Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, 7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? 8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? 9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? 10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), 11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. 12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe..”
Marko 2:2 “Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),
11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe..”
Ukichunguza hapo utaona kuwa jambo la kwanza; Bwana aliona Imani yao kwake, aliona ndani yao walikuwa na kitu cha ziada zaidi ya imani ya kuponywa, nayo ni Imani kwa Yesu Kristo…..Na tunajua kitu cha kwanza kilichomleta Bwana Yesu duniani ni kuokoa dhambi za watu, na vitu vingine baadaye… Ukisoma
Yohana 8:24 Bwana aliwaambia makutano ..
“Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”
Unaona hapo? Ni lazima uwe na imani ya kumwamini mwana wa Mungu kwanza ndipo upate uzima… Inakupasa uamini kwanza. Na ndio maana jambo la kwanza alilolitamka yeye kama mkuu wa uzima wa roho za watu mara baada ya kuona Imani yao kwake, akamwambia sasa yule aliyekuwa amepooza..UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO…..Ni Neno zuri na la neema kiasi gani!!! Lakini wale wengine waliokuwa pale mawazo yao yalikuwa tofauti, wao walitazamia tu, Bwana amponye yule mtu kisha amwambie nenda zako, halafu yule mtu akaendelee kuishi maisha ya dhambi kisha mwisho wa siku afe aende kuzimu!..na uponyaji wake wa mwili usimfaidie kitu baada ya maisha ya hapa duniani. Sasa Ukiendelea kusoma pale utaona Bwana anawauliza tena wale watu,
Marko 2:9 “VYEPESI NI VIPI, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Unaona hapo, …Kwa mtu mwenye akili na anayethamini maisha yake ya rohoni atagundua kuwa ni afadhali usipone ugonjwa wako, lakini usamehewe dhambi zako…kuliko kuponywa halafu dhambi zako ziendeleee kubaki! Na ndio maana Bwana alimchagulia fungu lililo jema la kusamehewa dhambi zake kwanza, kisha baadaye aje amponye… Na ndivyo tunavyopaswa na sisi kama wakristo kufanya hivyo sasahivi kama Bwana Yesu alivyofanya, tunakimbilia kuwaombea watu magonjwa ,kupokea miujiza, na mafanikio tunasahamu kuwafundisha watu habari za msamaha wa dhambi ambao ndio msingi wa Imani ya kikristo..
VYEPESI NI VIPI??? Ni heri tukamuhubirie mtu habari za msamaha na toba, aokolewe roho yake hata kama hatapokea uponyaji, kuliko kuhubiri kila siku mimbarani pokea miujiza huku bado watu wanakufa katika dhambi zao. Ni vema tufanye vyote ikiwezekana kuliko kusahau habari za uponyaji wa roho za watu na kuegemea sehemu moja tu ya miujiza….VYEPESI NI VIPI? .
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.
JIBU:
Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; DHAHABU na UVUMBA, na MANEMANE.
Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.
11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; DHAHABU na UVUMBA, na MANEMANE.
Ukisoma hapo utaona zile zawadi wale mamajusi walizozipeleka ni tatu tu. Ndio tunu zenyewe nazo : (dhahabu, uvumba na manemane)…
Sasa hizi zawadi tatu kila moja ilikuwa na maana yake kubwa, Tukianza na dhahabu, wale mamajusi walifahamu kuwa aliyezaliwa ni mfalme na anastahili heshima ya kifalme na kitu chenye thamani kubwa kuliko vyote ambacho angestahili kupewa mfalme ni dhahabu, kwasababu dhahabu inaweza kubadilishwa na kuwa hata fedha na kutumiwa kwa matumizi mengine yeyote..kwahiyo hii zawadi ya dhahabu ilikuwa ni zawadi yenye manufaa kimaisha, tofauti na hizo zawadi mbili nyingine zilizobakia zenyewe zilikuwa na manufaa ya kiujumbe zaidi kuliko kimatumizi.. Kwa mfano zawadi ya UVUMBA.
Kwa kawaida uvumba sio zawadi tunaweza tukasema uzito wa kumfaa mtu kwa wakati wote, ni zawadi isiyokuwa na thamani kubwa sana,hivyo hatuwezi kivile kuiweka katika makundi ya zawadi kama zawadi , tuchukulie kwamfano Mtu kasafiri kutoka mbali tuseme Marekani halafu anakuletea zawadi ya msalaba au ufunguo..Kwa namna ya kawaida wewe unayoipokea huwezi kwenda kuiuza au kuitumia kwa matumizi yako yoyote, zaidi sana utafahamu moja kwa moja kuwa ni zawadi iliyobeba ujumbe Fulani wa ndani zaidi ya kinachoonekana, Mfano mwingine tunafahamu pale binti anapoagwa baada ya kuposwa na kwenda kuolewa huwa kuna baadhi ya zawadi zinaambatanishwa naye kutoka kwa watu wa nyumbani kwake, licha ya kupewa vitu vya ndani na mali..lakini kuna mambo madogo madogo utakuta anakabidhiwa pia na hayo ndio yana ujumbe mzito kuliko hata vile vitu vya thamani alivyopewa, kwamfano utakuta anapewa ufagio, au ungo,..Ikiwa na maana kuwa mwanamke anapaswa awe Msafi na awe anazingatia Mapishi n.k…
Hivyo hivyo na wale mamajusi walipata ufunuo wa wanayemfauata ni nani, na ndio maana walikwenda na dhahabau lakini wakaongezea kubeba na Uvumba juu yake?..
Sasa Kumbuka katika hekalu la Mungu, uvumba ulikuwa unavukizwa tu na makuhani baada ya sadaka kutolewa sasa ile damu ilichukuliwa na kupelekwa katika madhabahu ya dhahabu iliyokuwa kule patakatifu, na hapo ndipo uvumba ulikochomwa kujaza ile nyumba ya Mungu harufu nzuri ya manukato na utukufu, na kumbuka kazi hiyo aliifanya kuhani mkuu peke yake. Hii ikifunua kuwa Huyu aliyezaliwa Yesu Kristo, licha tu ya kuwa mfalme atakuja kuwa KUHANI pia, kwasababu kila kuhani lazima awe na uvumba mkononi mwake wa kuvukiza mbele za Mungu…Na Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu wetu. Haleluya.
Waebrania 4: 14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”.
Waebrania 4: 14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”.
Kwahiyo wale Mamajusi walipata ufunuo huo kuwa Yule atakuja kuwa kuhani mkuu pia..Jambo ambalo wengi wa waliokuwa pale hawakulifahamu hilo, mpaka alipokuja kupaa mbinguni, mitume ndio wakamwandikia habari zake. Kadhalika MANEMANE, ni zao lililotoka katika miti likiwa na maana ya “Uchungu”, manemane ilitumika kutengenezea dawa, Hivyo zawadi kama ile isingeweza kuonekana inafaa sana kwa mazingira kama yale ya furaha ya kuzaliwa Mfalme duniani, lakini walifanya vile kwasababu ilikuwa inabeba ujumbe mwingine wa ndani zaidi..
Kama tafsiri ya jina lake lilivyo ilifunulia kuwa mtoto aliyezaliwa licha ya kuwa mfalme atapitia mateso na uchungu mwingi, na hilo lilikuja kujidhirisha alipoteswa na kusulibiwa kwa ajili yetu… Wakati akiwa katika safari yake ya kwenda msalabani wale askari walimchanganyia mvinyo na manemane na kumnyeshwa, lakini Bwana aliitema kwa jinsi ilivyokuwa chungu,(Soma Marko 15:23)..Gharama Bwana aliyoilipa kwa ajili ya dhambi zetu ni kubwa sana, mfalme kufa na kuteswa msalabani kwa ajili ya mtu mwenye dhambi asiyestahili kwa chochote, hakika ni jambo la neema sana.
Hivyo wale mamajusi Mungu aliwapa kuona mbali zaidi ya zile hazina walizozipeleka. Kama mamajusi ambao hawakuwa wayahudi walisafiri kutoka nchi za mbali kwa muda wa miaka miwili, ili tu kumwona mfalme YESU akiwa mchanga, tutapataje kupona sisi tulioshuhudia matendo yake makuu ya neema kuu namna hii ambayo kila siku yanatuita tutubu dhambi?. Tutapate kupona tukidharau leo!
NYOTA YA ASUBUHI.
WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.
UFUNUO: MLANGO WA 12
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?
KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?