Category Archive Home

Wale manabii 400 waliomtabiria mfalme Ahabu wakati wa Mikaya walikuwa ni manabii wa Mungu au?

JIBU: Ndio wale manabii 400 waliomtabiria Ahabu (tunaowasoma katika 1wafalme 22 ) walikuwa ni manabii wa Mungu, na hapo kabla walikuwa wanapokea unabii sahihi kutoka kwa Mungu kwasababu manabii zamani ilikuwa ni lazima wajaribiwe kwanza kabla ya kuitwa mbele za wafalme,. Ni lazima nabii huyo ashuhudiwe kutoa unabii na kutimia vinginevyo hawezi hata kumkaribia Mfalme. kwahiyo ni dhahiri walikuwa wanatoa unabii na unatimia kabisa, japo mioyo yao haikuwa mikamilifu mbele za Mungu kama ilivyokuwa kwa nabii Mikaya…

walikuwa wanapenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu na ndio maana walikuwa wanakaa katika majumba ya kifalme, wakipenda kuwatabiria watu mambo mazuri tu ya faraja hata kama wapo katika dhambi zao, Hivyo tabia hiyo ikawapelekea kupata sifa nyingi kutoka kwa wafalme, lakini hawakujua kuwa Mungu alikuwa amewaacha. Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake Luka 6: 26 ” Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.”

 Mfano mwingine wa manabii kama hawa tunamwona nabii Balaamu (hesabu 22), aliyetaka kwenda kuwalaani Israeli kwa ujira wa udhalimu ili amridhishe tu mfalme Balaki.. 

Huu ni mfano pia wa manabii wengi tulionao sasa wanapenda kusifia pesa,umaarufu,ukubwa, vyeo, wanawatolea watu unabii ili wapate pesa, na kupendwa, sasa manabii kama hao ni rahisi kuingiwa na roho zidanganyazo, hivyo kuwafanya leo wasikie kutoka kwa Mungu kesho wasikie kutoka kwa shetani..lakini manabii kama Mikaya ambao ni wachache sana wao husimama katika Neno, huishi maisha matakatifu na kusema kile Mungu anachotaka tu waseme pasipo kujali cheo cha mtu,utajiri wa mtu, au hali ya mtu, hivyo Mungu anawaepusha na roho zidanganyazo na unabii wao unakuwa thabiti na hakika siku zote, lakini kwa hao wengine wanafungua milango kwa roho zidanganyazo kama ilivyowatokea wale manabii 400.(Mapepo yalivyowaingia wote na kutabiri uongo mbele za Mfalme) 

Hivyo ndugu ni kuwa makini na aina ya manabii waliopo leo hii. Mtu yeyote anayejiita nabii akija na kukutolea unabii ni vizuri kabla ya kuupokea huo unabii, uupime kwanza kwenye NENO, kisha ukilandana nalo ndipo uuchukue, kama haulandani hata kama alishakutolea unabii hapo kabla na ukatimia, usipokee. Kwamfano mtu alikutabiria na kukwambia Bwana kamwonyesha baada ya mwezi mmoja utabeba mimba ya mapacha na wewe wakati huo ni mgumba, na kweli huo wakati ulipofika ukapata mimba na kujifungua mapacha kama alivyokutabiria, lakini leo hii anakuja tena na kukwambia Bwana kamuonyesha umuache huyo mume uliyefunga naye ndoa uliye naye leo ukaolewe na mwingine Bwana aliyekukusudia..Sasa kiharakaharaka ni rahisi kumwamini kwasababu alishakutabiria mara ya kwanza na ikatimia lakini wewe hujui mahusiano yake na Mungu wake yalishaharibika hivyo kumfanya apokee maono mengine kutoka kwa shetani akidhani ni ya Mungu, kwasababu ulinzi ndani yake haupo, dhambi imemtawala amekuwa lango la shetani …Ndivyo walivyofanya wale manabii 400 wa Ahabu. 

Sasa unapokutana na unabii kama huo unakumbuka lile neno linalosema “mtu atakayemwacha mume/mume wake isipokuwa kwa habari ya uasherati na kwenda kuolewa na mwingine azini na anamfanya yule aliyemwacha kuwa mzinzi”…Hivyo hapo unauacha huo unabii na kulishikilia Neno. Soma mstari huu. 

Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,

2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;

3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.

4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako”. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

MPINGA-KRISTO

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?

SEHEMU ISIYO NA MAJI.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

Marko2:18 “Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile.   

JIBU: shalom! Mfano huo sawa tu, na mwanafunzi aliye na mwalimu wake, pindi anapokuwa naye anao uwezo wa kumuuliza swali lolote na likajibiwa, au akampelekea mwalimu wake maswali yote magumu yanayomsumbua na yakatatuliwa pindi wakati yupo naye, lakini kikifika kipindi cha mitihani, labda mtihani wa NECTA, pale ambapo anawajibika kuketi mwenyewe kwenye chumba cha mtihani mahali ambapo mwalimu wake hawezi kuwepo tena hapo ndipo itampasa atumie nguvu na jitihada ya ziada kutatua maswali yote peke yake anayokutana nayo kwa maarifa aliyopewa na mwalimu wake, lakini hapo mwanzo angeweza kumpelekea tu kila swali linalokuja mbele yake na akasaidiwa pasipo hata kujishughulisha…  

Na ndivyo ilivyokuwa kwa mitume wa BWANA wetu YESU KRISTO wao walipewa neema ya kipekee kutembea na Mungu( BWANA YESU) duniani tofauti na wanafunzi wa Yohana au masadukayo, sasa unategemea vipi watu kama hao wafunge, au kujisumbua kwa lolote, wakati wanayemwomba wapo naye hapo hapo…wakiwa wanahitaji ufunuo wa jambo fulani si wanamkimbilia BWANA na kumuuliza kwasababu yupo nao hapo?!!!…

Na ndio maana akasema wakati utafika Bwana arusi atakapoondolewa…hapo ndipo watalazimika kufunga kama wenzao. Wakitaka ufunuo wa jambo fulani sasa itawapasa wafunge, wakitaka kutatua au kujua jambo fulani itawapasa wafunge kwanza na kuomba,Kwahiyo kile kitendo cha wao kutembea, kula, kuishi na kufundishwa na BWANA ndio kualikwa kwenyewe Harusini.   Kuna kipindi Bwana alimwamsha Petro na wenzake wasali, lakini walilemewa na usingizi wakalala, lakini baada ya Bwana kuondoka unamwona Petro anakuwa wa kwanza kusali na kufunga mpaka anazimia kwa njaa (Matendo 10:9).  

Kadhalika na sisi tunapompokea Kristo kwa mara ya kwanza kunakuwa na neema fulani ya kipekee inakuwa juu yetu, kila tuombalo tunalipokea haraka sana, kwasababu bado hatujajua umuhimu wa kuomba, hatujajua umuhimu wa kufunga, hivyo neema ya Mungu inakuwa juu yetu kubwa kama watoto wachanga, lakini unafika wakati Bwana anaipunguza ile neema, (Bwana arusi anaondolewa )unakuwa ili upate jambo fulani inakupasa uombe kwa bidii, wakati mwingine kwa kufunga, ili upate ufunuo wa Roho inakupasa kujifunza sana maandiko kwa muda mrefu n.k, kwasababu unakuwa sio mtoto tena, Bwana anakutoa hatua moja kwenda nyingine.  

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:


Rudi Nyumbani:

Print this post

Paulo alimwambia Timotheo atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake, Je! tunaruhusiwa na sisi pia kutumia pombe?

Tukisoma hilo andiko Biblia inatuambia

1Timotheo5:23″ TOKEA SASA USINYWE MAJI TU LAKINI TUMIA MVINYO KIDOGO,KWA AJILI YA TUMBO LAKO,NA MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.  

JIBU: Mtume Paulo alivyosema hivyo hakuwa na maana ya kuhalalisha pombe hapana!! kumbuka divai nyakati za zamani ilikuwa na matumizi mengi, ilikuwa inatumika kama dawa kutibia vidonda,n.k. Kwamfano unamwona yule Msamaria ambaye tunasoma habari zake

Luka 10: 33 “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.

Unaona hapo?   Na ilikuwa pia ina matumizi mengine mengi, sasa zamani za kanisa la kwanza wakristo wengi walikuwa wanafunga muda mrefu, na kusafiri umbali mrefu kwenda kuhubiri injili, kwasababu kulikuwa hakuna magari wakati ule, au ndege kama tulizonazo sasa , kwahiyo kutokana na hari za jua na majangwa, na kufunga juu yake, wakati mwingine utumbo unakuwa unajisokota, au kunakuwa na udhaifu fulani katika mwili,   Sasa Mtume Paulo kwa kulijua hilo kutokana na uzoefu wa muda mrefu aliokuwa nao wa kusafiri masafa marefu kuhubiri injili, alimshauri Timotheo asitumie maji tu bali na mvinyo(divai) kidogo kwa ajili ya tumbo, na sio kwaajili ya kujifurahisha au kujiburudisha wanavyofanya watu sasahivi,

kwahiyo unaona hapo? anamshauri atumie kama DAWA, ni sio kama kiburudisho, ni sawa na mimi nikushauri wewe unaposafiri mahali palipo na ukame kidogo wa chakula kwa ajili ya injili usinywe maji matupu peke yake, bali unywe kinywaji chenye nguvu kidogo (mfano Energy drink),ili mwili usipungukiwe nguvu njiani. unaona hapo nia yangu sio kukwambia unywe energy drink kila wakati, kujiburudisha hapana bali nia yangu ni kukuzuilia mwili usidhoofike njiani kwa muda ule utakapokuwepo safarini, kutokana na uzoefu nilio nao kusafiri mda mrefu.  

Hivyo mtu yoyote anayeshikilia hilo andiko kiuhalalisha atajua kabisa pombe ni makosa, kwasababu hakuna mtu yoyote anayekunywa pombe kama dawa katika mwili wake,.wote wanakunywa kwa ajili ya tamaa za mwili na ulevi, ambayo ni dhambi na hata hivyo ukiangalia kwa makini utaona pombe zote tulizonazo sasahivi hazina matumizi mengine zaidi ya ULEVI tu, basi zimetengenezwa mahususi kwa ajili ya kazi hiyo na si vinginevyo…Hivyo mkristo yoyote anayekunywa pombe anafanya makosa mbele za Mungu kwa kisingizio cha huo mstari.  

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MATUMIZI YA DIVAI.

JE! MABALASI BWANA YESU ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?

JE NI SAWA KWA MKRISTO KUUZA MAZAO YA KUTENGENEZEA POMBE KAMA VILE MTAMA?

RABONI!

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Musa aliua lakini bado Mungu alimchangua kuwaongoza wana wa Israeli, je! Mungu anaruhusu mauaji?

JIBU: Kumbuka Musa alipokuwa Misri alikuwa bado hajamjua Mungu wa Yakobo, alikuwa ni mpagani tu akiabudu miungu ya kimisri kama wamisri wengine, hajasafishwa bado matendo yake ya kipagani,.Na siku alipojigundua kuwa yeye ni mwebrania, ndipo akajaribu kutaka kuwaokoa ndugu zake (wana wa israeli) kwa njia zake za kisiasa na kiburi cha ujuzi wa kimisri aliokuwa ameupata katika jumba la Farao, lakini Mungu hatendi kazi hivyo ndio maana tunaona Mungu alimpeleka kwanza jangwani kumnyenyekeza kwa muda wa miaka 40, Na aliporudi tunaona hakuua tena alikuwa mtu mwingine, biblia inasema Musa alikuja kuwa mtu MPOLE kuliko watu wote DUNIANI

Hesabu 13:3″ Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”.

 Unaona Mungu hafanyi kazi na watu wenye kiburi na WAUAJI,Kwahiyo Mungu alianza kutembea na Musa baada ya ile miaka 40 lakini kabla ya hapo Musa alikuwa anajiamulia mambo yake mwenyewe alikuwa ni hodari katika maneno biblia inasema (matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo”), lakini baada ya kunyenyekezwa tunaona akimwambia Mungu yeye sio mnenaji

Kutoka 4:10 ″Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.”

 Kadhalika na sisi pia Mungu hafanyi kazi na watu wenye kiburi tunaweza tukawa tumeitwa vizuri tu!, lakini ujuzi wetu, elimu zetu, uhodari wetu ukawa kikwazo kikubwa mbele za Mungu…Tunapaswa tutupe vyote tuende mbele zake sisi kama sisi, ndipo atutumie. 

Yakobo 4: 6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?

TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO IPO WAPI?

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

RACA


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?

SWALI: Ule msalaba unaowekwa kwenye kaburi, na ile ibada inayofanywa vina umuhimu wowote kwa mkristo?

JIBU: Inategemea hiyo ibada inayofanywa ina maudhui gani, kama ibada imelenga kumwombea huyo mfu hayo ni makosa mbele za Mungu, lakini kama imelenga kushukuru au kuwafundisha na kuwaonya watu waliosalia ambao bado wanaishi, kuhusu mwanzo wa safari yetu hapa duniani hadi mwisho wake, na kwamba kila mtu aweke mambo yake sawa na Mungu wake, ibada hiyo ni njema na inakubalika mbele za Mungu, 

Mhubiri 7: 2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake”. 

Na pia sio vibaya kuweka msalaba juu ya kaburi la marehemu, kwasababu ile ni ishara ya mauti ya mkristo na tumaini la ufufuo wa wafu, lakini ni makosa kuweka msalaba na kuuangalia kama ndio utimilifu wote, ule uwe ishara tu, usihusishwe na masuala yoyote ya ibada, kuepuka ibada za sanamu. Na vivyo hivyo kanisani sio vibaya kuweka msalaba kama ishara ya imani ila usitumiwe tu kusujudiwa kama baadhi ya madhehebu yanavyofanya. Utakuta hata kukemea pepo kiongozi anatumia msalaba badala ya jina la Yesu, sasa hayo yote ni makosa mbele za Mungu. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE! KIONGOZI WA DINI ANAOUWEZO WA KUSAMEHE DHAMBI ZA MTU, MFANO PADRE?

JE! NI SAHIHI MTU KUNING’INIZA PICHA NYUMBANI MWAKO KAMA YA YESU?

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?

NJIA YA MSALABA

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?

Tukisoma pale mpaka mwisho inasema;

Marko 2:21 Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; 22 ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kukuu,na pale palipotatuka huzidi. ″Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikukuu;ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. BALI HUTIA DIVAI MPYA KATIKA VIRIBA VIPYA. ??

 JIBU: Mfano huo unawalenga watu wote wanaojiona kuwa ni wakristo..Viriba ni vyombo maalumu vilivyokuwa vinatumika zamani kuwekea divai, vilikuwa ninatengenezwa kwa ngozi, sasa nadhani utakuwa unafahamu pombe huwa inafura wakati inapoanza kuchachuka, na pombe zote ndivyo zilivyo, sasa, kwa wayahudi walikuwa wanatumia viriba vya ngozi ambayo bado ni mbichi, hivyo wakiweka divai ambayo bado inaendelea kuchachuka wakati ikiendelea kuvimba basi ile ngozi kwasababu bado ni laini, na mbichi, hutanuka pamoja na divai, kama vile kiatu cha ngozi, unaweza ukanunua mwanzoni kikakubana lakini baadaye utakavyozidi kuendelea kukivaa kinakuenea vizuri kwasababu ni ngozi ambayo haijakakamaa haijawa ngumu bado…  

Vivyo hivyo na kwa divai pia,..kwahiyo mfano ile pombe ikiwekwa kwenye kiriba ambacho kimeshakauka au kukaa sana inamaanisha kuwa ile ngozi itakuwa ishakuwa ngumu, kwahiyo ukiweka pombe changa mule ndani ni lazima kipasuke kwasababu ile pombe itavimba na kwa vile hakiwezi kutanuka zaidi mwisho wa siku kitapasuka tu…kwahiyo kiriba kipya, ni kwa divai mpya, huwezi kuweka divai mpya kwenye kiriba cha kale.   Hiyo inafunua tabia za wakristo wa leo, ambao roho zao zimegandishwa na mafundisho ya kale, wasiotaka kubadilika kwa kumruhusu Roho wa Mungu kutenda kazi ndani yao, hao ni sawa ni viriba vya kale visivyoweza kutanuka tena, Hivyo mfano ukija ufunuo wa kweli wa Roho Mtakatifu, ufunuo mpya mbele yao ambao hawajawahi kuusikia katika dini zao, au maisha yao, kwasababu ni viriba vya kale visivyotaka kutanuka basi vinapasuka..

Na ndio maana watu kama hao hawawezi kuupokea Ufunuo wa Roho wa Mungu hata kama ni kweli vipi au upo dhahiri kiasi gani, wanaishia kupinga tu kama mafarisayo kwasababu hawana uwezo wa kuchukuliana na ufunuo mpya wa Roho wa Mungu wao wataaishia kupinga tu, na kibakia katika dini zao, na ndivyo walivyokuwa mafarisayo na masadukayo wakati wa Bwana, Yeye alipowaletea kitu kipya hawakuweza kukipokea kwasababu roho zao zilikuwa zimegandishwa na mafundisho yao ya kale. Lakini wale wote waliokubali na kuilainisha mioyo yao kwa Bwana. Basi waliweza kuupokea ndio wale waliokuwa Mitume wa Bwana baadaye. Na ndio maana Bwana akawapa mifano hiyo….  

Hivyo ni vizuri kila siku kumruhusu Roho wa Mungu kututengeza kwa jinsi apendavyo ili kuutambua ujumbe wa wakati wako unaoishi…tusije tukawa tunaishi wakati wa ujumbe wa kanisa la kwanza wakati tupo katika ujumbe wa kanisa la mwisho la Laodikia. Kadhalika na mfano wa Kiraka kipya na kikuu kuu maana yake ndiyo hiyo hiyo.   Huu ni wakati wa kijiachia mbele za Mungu, mruhusu akufundishe unaposikia jambo jipya ambalo hujawahi kulisikia hapo kabla usikimbilie kupinga tu! Fanya kama watu wa Beroya, lichunguze kwanza kwa maandiko uone kama ni sawa au sio sawa, vinginevyo utakuwa kiriba cha kale, kisichoweza kupokea divai mpya kama wale mafarisayo na Masadukayo.    

Ubarikiwe sana.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

MJUE SANA YESU KRISTO.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Malaika wa maji ni yupi na Je kuna aina ngapi za malaika?

SWALI:Katika kitabu cha Ufunuo 16:5, Tunaona akitajwa malaika wa maji ” Swali Huyu malaika wa maji ni nani? Naje! Kuna malaika wa aina ngapi?

JIBU: Ulimwengu wa malaika ni mkubwa/Mpana sana kama vile ulivyo ulimwengu wa wanadamu, Kama vile Mungu alivyotoa vipawa tofauti tofauti kwa wanadamu, vivyo hivyo alitoa vipawa tofauti tofauti kwa malaika zake,..wapo malaika wa maji,(hawa wanashughulika na mambo yote yanayohusiana na maji,mfano kuleta gharika kama wakati wa Nuhu,kutenganisha bahari kama wakati wa Musa,kusababisha au kuzuia mvua kama wakati wa Eliya , kutokeza maji mwambani kama wakati wa Wana wa Israeli jangwani, kutokeza chemichemi, kugeuza maji kuwa kitu chochote kama damu n.k.)..Na watakuja kufanya hizo kazi tena katika siku ile kuu ya Bwana baada ya kanisa kunyakuliwa..Wapo pia malaika wa moto (utawaona katika..

Ufunuo 14: 18 “Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana”

 Wapo pia Malaika wa vita, mfano Mikaeli na wenzake,kazi yao ni kudhibiti nguvu za yule adui kwa watakatifu wa Mungu, wapo malaika wajumbe kama Gabrieli na wenzake (Danieli 9:21) ambao kazi zao ni kuwasilisha ujumbe fulani kutoka kwa Bwana kwa watakatifu, na wapo pia wa sifa (makerubi na maserafi) na shetani naye alikuwa kwenye hili kundi kabla ya kuasi, n.k.Hawa wapo mbele ya kiti cha Enzi cha Mungu milele,

Isaya 6: 1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”. 

kwahiyo wapo wengi hata wengine hatuwajui, na wala hatujawahi kuwaona, wapo wanaoshughulika na ULINZI tu,soma Zaburi 91: 11 “Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote”.

Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.”

Wapo malaika wa kila nchi, wapo wa kila mkristo mmoja mmoja, na wapo wanaosimama kwa kila huduma, n.k kila mmoja anatenda kazi kulingana na alivyopangiwa na Mungu mwenyewe…Wapo pia malaika wa Uponyaji, (Yohana 5:15). 

Na karama nyingi za rohoni zinachochewa na hawa malaika wanaotembea na watakatifu. Kwamfano karama za upambanuzi wa roho,miujiza n.k.(Waefeso 4:8) Lakini hawa wote hawaonekani kwa macho, ni viumbe wa rohoni,(japo wakati mwingine wanaweza wakaonekana kwa macho) ndio maana MUNGU WETU ANAITWA BWANA WA MAJESHI! unaweza ukajiuliza hayo majeshi ni akina nani??? sio wanadamu kwasababu wanadamu sisi tunaitwa WANA WA MUNGU (Waebrania 1:5).. Bali ni malaika ndio wanaoitwa MAJESHI ya BWANA…yapo MAELFU kwa MAELFU ya malaika wanazunguka kila siku duniani kuwahudumia watu wa Mungu (Waebrania 1:13-14).Inasema..

“ 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”.

 Kwahiyo uwezekano wa mtu kuzungukwa na wingu kubwa la malaika kama ilivyokuwa kwa Nabii Elisha inategemea na kiwango cha utakatifu wake na kiwango chake cha kulitii Neno la Mungu. Kwasababu hawa wanafanya kazi katika kanuni za Neno la Mungu tu! Nje ya hapo! Wanakuwa Hawana msaada wowote kwako..Kwamfano Neno la Mungu linaposema waheshimu Baba yako na mama yako upate siku nyingi za kuishi duniani..

Sasa mtu anapolishika hilo NENO kwa bidii , wale malaika wanaohusika na ulinzi, wanatumwa kuhakikisha kwamba maisha yako hayaathiriwi ni kitu chochote kile mpaka ule umri utakapotimia ndio hapo utakuta hata ikitokea ajali ya namna gani wanaweza wakafa watu wote yeye ukapona, au labda magonjwa Fulani yanaowapata wazee kama upofu,n.k., utashangaa wengine wanayapata lakini yeye hayakupati, ni kwasababu umelishika lile Neno hivyo siku zote anakuwa anazungukwa na jopo kubwa la malaika..

Kadhalika na ahadi zote za Mungu vivyo hivyo zinaambatana na Malaika wa Bwana. Lakini kama hutaishi kulingana na Neno la Mungu, ina maana kuwa hao malaika watakuwa hawapo, kinyume chake mapepo ndio yatachukua nafasi zao, ndio unaweza kushangaa, mtu anakufa kabla ya wakati wake, wachawi wanamloga, wengine magonjwa yasiyoeleweka, wengine mikosi n.k. Kwahiyo jambo kubwa linalofukuza uwepo wa malaika ni dhambi katika maisha ya mtu.

 Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

JE SISI TUTAWAHUKUMUJE MALAIKA?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

NINI MAANA YA ELOHIMU?

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

JIBU: DHAMBI: Kibiblia yale mambo yote yaliyokuwa yanafanyika kinyume na TORATI/SHERIA ya Mungu, yalikuwa yanajulikana kama DHAMBI. Ikiwa na maana kuwa mtu yeyote atakayeonekana ameivunja hiyo sheria ni sawa na amefanya dhambi au ameiasi sheria. Ilijulikana kuwa mtu huyo kabla ya kuiasi sheria yenyewe alijua kabisa jambo hilo analolifanya lilishahakikiwa na kutolewa rasmi kuwa ni makosa na kwamba mtu yeyote anayefanya hivyo hana udhuru, atastahili adhabu fulani, lakini yeye kwa makusudi anakwenda kufanya..Hiyo kwake inakuwa ni dhambi na haina huruma ni lazima atumize deni lake la kuadhibiwa. Kwamfano tunaona biblia ilikataza na hata sasa imekataza kuzini, au kuua, au kuabudu sanamu hivyo basi angali mtu akijua kabisa Mungu kakataza kufanya mambo hayo mapaka akaamua kuyaandika katika mawe, na nyingine katika kitabu halafu mtu huyo anaenda kuzini, au kuiba, au kuabudu sanamu kwa makusudi kabisa..Mtu huyo ndio tunasema kafanya dhambi/ kaiasi sheria.  

MAOVU: Kadhalika, na mambo mengine yote ambayo kwa namna moja au nyingine “hujayaonekana” au “hajaandikwa” katika Torati/Biblia lakini yanafanyika na inajulikana kabisa kwamba hayo mambo hayastahili kufanywa huku dhamira ya mtu mwenyewe ikimshuhudia ndani yake, na mtu akaenda kuyafanya hayo..Sasa hayo ndio yanajulikana kama MAOVU/MACHUKIZO. Mfano wa maovu tunaweza kuyaona yalitendeka katika kipindi cha Nuhu, na kipindi cha Sodoma na Gomora, kumbuka watu wa wakati ule walikuwa bado hawajapewa Torati/sheria kutoka kwa Mungu, kama tulionayo sisi. Tunasoma  

Mwanzo 6: 5 “Bwana akaona ya kuwa MAOVU ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.”

Unaona hapo?. Kwahiyo mfano wa mambo yaliyokuwa yanatendeka kipindi kile mpaka yakapelekea dunia kuteketezwa ndiyo yaliyotabiriwa kutokea katika siku za mwisho kwamba maovu mengi yataongezeka.. Leo hii tunaweza kuona mambo mabaya hata yamezidi yale yaliyoandikwa kwenye biblia, yameijaza dunia, vitu kama uvutaji sigara, utoaji mimba, biashara haramu kama za watu, madawa ya kulevya,uchunaji ngozi, n.k. mambo ambayo hata kwenye biblia huwezi kuona yakitajwa moja kwa moja, lakini yanajulikana kuwa ni makosa, sasa haya yote ndiyo yanayoitwa MAOVU.  

KOSA: Na kosa, ni sawa na kutofanya kitu kisivyostahili. Kwa lugha rahisi mtu anaposema “Nimekosea” ni sawa na kusema amefanya kitu hicho isivyostahili. Mfano biblia inaposema.

Matendo 2:38 ” ….Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”  

Halafu mtu anakwenda kumnyunyizia maji kichwani kama ishara ya ubatizo na kuepuka ubatizo wa maji ya kuzamishwa.kisha akatumie Jina lingine ambalo sio la YESU KRISTO kubatizia, sasa huyo mtu ni sawa na kafanya KOSA. Ametenda isivyostahili, (yaani kapindisha kile kilichoamriwa).   Hivyo ili mkristo uwe mtu asiwe na HILA, wala WAA, lolote mbele za Mungu, unapaswa uepuke yote matatu (yaani DHAMBI, MAOVU, MAKOSA)..Na haya yote unaweza ukayakwepa tu! endapo utafanya NENO LA MUNGU kuwa msingi pekee wa kuyaendesha maisha yako. Lakini kama utapenda kushikilia itikadi za dini fulani au dhehebu fulani, kumkosea Mungu, au kufanya dhambi au kutenda maovu huwezi kuepuka kwa namna yoyote ile.

DUMU katika maneno matakatifu ya Mungu, huku ukimwomba Mungu akufunulie njia sahihi ya kuiendea, na ukitia nia hiyo kwa kumaanisha, Roho Mtakatifu mwenyewe atakuongoza, na mwisho wa siku utajikuta unakuwa yule mwanawali mwerevu ambaye siku Bwana wake alipokuja alimkuta na mafuta ya ziada ndani yake(sasa yale mafuta ya ziada ni Ufunuo wa Roho mtakatifu), lakini wale wapumbavu hawakuwa na mafuta ya kutosha katika chupa zao, na pale Bwana wao alipokuja walikutwa hawana kitu, hivyo wakatupwa nje, ambapo kuna kuliko na vilio na kusaga meno. (Mathayo 25)  

Dunia ya leo imejaa maovu ya kila namna, usiruhusu uchukuliwe na namna ya dunia hii (Warumi 12:2). Hivyo ili mkristo uwe mtu asiwe na HILA, wala WAA, lolote mbele za Mungu, unapaswa uepuke yote matatu (yaani DHAMBI, MAOVU, MAKOSA)..Na haya yote unaweza ukayakwepa tu! endapo utafanya NENO LA MUNGU kuwa msingi pekee wa kuyaendesha maisha yako. Lakini kama utapenda kushikilia itikadi za dini fulani au dhehebu fulani, kumkosea Mungu, au kufanya dhambi au kutenda maovu huwezi kuepuka kwa namna yoyote ile.

Mungu akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

Mfano wa wanawali kumi(Mathayo 25), unaelewekaje?

SWALI: Ule mfano wa wanawali 10 (Mathayo 25), wale watano hawakuwa na mafuta ya ziada katika chupa zao je yale mafuta ya ziada yanawakilisha nini?

Mathayo 25 : 1-11

“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

JIBU: Kama hiyo mistari ya Mathayo 25 inavyoelezea, kwamba wote walikuwa ni wanawali ikiwa na maana kuwa wote ni wakristo wanaomngojea Bwana. Na yale mafuta waliokuwa nayo wote ni “Roho Mtakatifu”. Lakini wengine walionekana kuwa na mafuta ya ziada, na wengine hawana.Hii inafunua aina mbili za wakristo watakaokuwepo siku za mwisho, 

AINA YA KWANZA: Hawa ni wale wakristo werevu waliopokea Roho Mtakatifu na kuruhusu Roho wa Mungu kufanya kazi ndani yao kwa kutaka kujifunza na kuendelea kupokea mafunuo zaidi ya Roho wa Mungu mpaka kufikia cheo cha utimilifu Kristo (Waefeso 4:13), mtu wa dizaini hii kila siku anakuwa tayari kujifunza jambo jipya, hivyo anahama kutoka utukufu hadi utukufu kila siku kiu na bidii ya kuendelea kumjua Mungu inaongezeka,ndani yake, anakuwa hafungwi na mifumo fulani ya dini au dhehebu, bali Neno la Mungu ndio taa yake, mtu kama huyu anakuwa haridhiki kukaa katika hali moja ya kiroho kwa muda mrefu. 

Hivyo basi Mungu anamfungulia mlango wa kufahamu mafunuo ya ziada (hiyo ndiyo ile mana iliyofichwa, ambayo si kila mtu ataipata ufunuo 2:17) kutokana na jitihada yake ya kumtafuta Mungu hivyo basi inamfanya yeye kuwa watofauti na wakristo wengine. Kwahiyo hata Bwana atakapokuja atakuwa na NURU ya kwenda kumlaki hatakuwa gizani. Na siku hiyo haitamjilia kama mwivi kwasababu taa yake inawaka siku zote.

 AINA YA PILI: Hawa ni wale wakristo wapumbavu ambao walishapokea Roho Mtakatifu (ambayo ndio yale mafuta kwenye taa zao) lakini sasa baada ya kupokea Roho wa Mungu WANAMZIMISHA ndani kwa kutomruhusu tena aendelee kuwafundisha mambo mapya, na kuwatoa hatua moja ya kiroho hadi nyingine. Kwasababu kumbuka kazi ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza katika kuijua kweli yote, soma Yohana 16:13″ Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”.

Kwahiyo aina hii ya wakristo wanakuwa wameridhika na hali walionayo na mafundisho ya dini zao au madhehebu yao tu, hawataki kujifunza jambo jipya na wakiambiwa hata kama linatoka kwa Mungu hawatataka kusikia,kwasababu dini yao haiwaambii hivyo, kiu na bidii ya kuendelea kumjua Mungu hawana ndani yao, mwanzoni walianza na moto, lakini ikafika wakati fulani ule moto ukazimika, huko ndio kumzimisha ROHO.

Hivyo basi wakati Bwana atakapokuja hawatakuwa na NURU ya kumtambua na kwenda kumlaki, Kwao siku ile itakuwa kama mwivi ajavyo usiku. wataingia katika ile dhiki kuu ya mpinga-Kristo. Kwahiyo kama wewe ni mkristo fahamu jambo moja Mungu mpaka leo anatenda kazi anaongea, anatoa mafunuo mapya, anaonya, anawapasha watu habari ya mambo yajayo, na anawapa wale tu wanaompenda na kumtafuta kwa bidii na kutaka kuufahamu ukweli hao ndio atakaowafunulia, Ndugu fahamu tu UNYAKUO hautakuwa SIRI kwa watu wote, wale wapumbavu ndio hawatajua siku ya kuondoka, lakini wenye mafuta ya ziada watajua. 

Kwahiyo ukiwa kama mkristo kwa ulimwengu tunaoishi leo mtafute Bwana kwa moyo wako wote mwombe Bwana aendelee kujifunua kwako ili siku ile isikujie kama mwivi. hivyo usiwatazame hao wakristo wapumbavu wewe kuwa mwerevu kwa kumruhusu Roho Mtakatifu kuendelea kufanya kazi ndani yako siku baada ya siku.

 Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

UNYAKUO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

KIFAA BORA CHA MATUMIZI.

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni halali kubatiza watoto wadogo?

JIBU: Si halali kuwabatiza watoto wadogo, kwasababu, ubatizo huwa unafuata baada ya TOBA ya dhati kutoka ndani ya moyo, kwamba mtu anatubu kwanza kwa kumaanisha kuziacha kabisa dhambi zake na maisha yake ya dhambi ya zamani aliyokua anaishi na kumpa Bwana maisha yake ayaongoze kuanzia huo wakati, sasa baada ya toba kinachofuata ndio Ubatizo, kwahiyo kinachotangulia ni Toba kwanza halafu ufuate ubatizo. Na sio ubatizo kisha Toba.

Hivyo kwanini watoto wachanga hawabatizwi? ni kwasababu hiyo hiyo, bado hawajajua jema na baya, bado hawajajitambua kwamba wao ni wenye dhambi, bado hawajaujua msalaba na umuhimu wake, bado hawajaona umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili, kwa ufupi bado hawajajitambua kwa namna yoyote, hata akilini tu ya mambo kawaida hawana, wataelewaje mambo ya rohoni?, hivyo hawawezi kubatizwa. Wao wanawekewa mikono tu ili kubarikiwa sawasawa na BWANA YESU alivyofanya kwa wale watoto waliomwendea wakati akiwa katika huduma yake.(Marko 10:16).

 Kwahiyo kufanya hivyo au ni sawa na umemchukua mtu asiyeamini na kwenda kumbatiza kwa nguvu na kusema tayari ameshabatizwa, unaona hapo utakuwa hujambatiza kwasababu ubatizo halisi unatokana na maamuzi kwanza ya mtu binafsi kwamba ametubu na kuamua kubatizwa na sio kumbatiza kwa niaba ya mwingine au kubatizwa kwa kuepuka matatizo, au kitimiza makusudi ya dhehebu lako..hapana Kufanya hivyo sio sawa kulingana na maandiko.

 Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

MWANA WA MUNGU.

MELKIZEDEKI NI NANI?


Rudi Nyumbani:

Print this post