Category Archive Home

Ni kweli mtu anaweza akafa lakini roho yake ikawa inatumika kama msukule (kumilikiwa na mtu fulani kwa wakati) mahali pengine?

JIBU: Biblia inasema mtu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu, (waebrania 9:27). Hivyo mtu akishakufa, amekufa hawezi kurudi tena. Lakini hiyo unayosemea kwamba mtu kafa halafu anatumika mahali fulani, kiuhalisia ni kwamba mtu huyo bado hajafa, Kwasababu mtu akishaenda kuzimu au peponi kurudi tena huku haiwezekani . bali mtu huyo anakuwa amehamishwa tu, roho yake bado ipo hapa hapa duniani pamoja na mwili wake sehemu fulani.. Huo ni uchawi tu wa shetani(watu wengine wanaita kiini macho) na mambo kama hayo yapo tu, Hivyo watu wa namna hiyo jinsi ya kuwatambua inahitaji macho ya rohoni, au kama sio hivyo basi ni kuomba kwa imani kwa jina la YESU KRISTO na mtu huyo atarudi (sasa hapo ni kulingana na imani yako mwenyewe).

Kwasababu biblia inasema yote yawezekana kwake yeye aaminiye. Kumbuka pia hayo mambo sio ya kuyahofia kana kwamba shetani anayomamlaka ya kujiamulia kumteka kila mtu kwa jinsi apendavyo. Hapana bali watu wanaokutwa na mambo kama hayo sehemu kubwa wanakuwa ni watu waliombali sana na Mungu, au walishajihusisha na uchawi hapo kabla katika maisha yao Ndiyo inapelekea wigo mwepesi zaidi kwa shetani kuwachezea jinsi apendavyo. Lakini sio kwa kila mtu anayemwona. Na pia kuna vifo vingine vinatokea, ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili baadaye Bwana aje kudhihirisha uweza wake, na mfano huo tunauona kwa Lazaro. Na watu kama hao nao hawawi wamekufa kabisa(yaani kwenda sehemu za wafu) hapana bali wanakuwa wamelala (japo hata hilo linawezekana kwa Mungu). Hivyo nao pia kwa jina la YESU wanaarudishwa na kuwa hai tena. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE!MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA ALIVYOFANYA KWA MFALME SAULI?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?

NGUVU YA UPOTEVU.

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.


Rudi Nyumbani:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Watakaodanganywa baada ya miaka 1000,watatoka wapi?

Swali linaendelea….Angali tunajua ndani ya ule utawala kutajawa na watakatifu tu? sasa hawa watu ambao shetani atawadanganya watatokea wapi kama tunavyosoma katika Ufunuo 20:7 “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.”

JIBU: Katika utawala wa miaka 1000 biblia inarekodi kuwa wenye dhambi watakuwepo, lakini dhambi haitatawala dunia kwasababu mkuu wa ulimwengu ule atakuwa ni MFALME WA AMANI yaani Yesu Kristo, tofauti na dunia ya sasa ambayo mkuu wa ulimwengu huu ni shetani. Hivyo Dhambi na wenye dhambi watakuja kuondolewa wote mara tu baada hukumu ya kile kiti cheupe cha Mungu ambayo itakuja mara baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha. Kwahiyo kama vile biblia inavyosema Kristo atatawala kwa fimbo ya chuma pamoja na sisi ukisoma..

Ufunuo 2:26 ″Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.”

(fimbo ya ni kwa ajili gani? na ni kwanini iwe ya chuma?. >> Ni dhahiri kuwa Ufalme wowote ni lazima uongozwe kwa mamlaka fulani, na utii chini ya kila kitakachoamriwa pasipo majadiliano wala mahojiano na ndivyo itakavyokuwa katika utawala wa Bwana wa miaka 1000, hivyo kwa yeyote atakayekaidi atalazimika kutumikia adhabu kali ). Hautakuwa utawala wa kimabavu bali ni wa amani na utaratibu lakini kwa watakaokuwa wanaenda kinyume na sheria ya MFALME (KRISTO) na watakatifu wake wataangukia laana. Kwa muda wako binafsi unaweza ukasoma Zekaria 14 yote, inaelezea adhabu zitakazowakuta mataifa yote wasiokwenda kumwabudu mfalme mwaka kwa mwaka Yerusalemu,

Ukisoma pia Isaya 65:17-20 Inasema..;

“17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.

18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.

19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.

20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; BALI MTENDA DHAMBI MWENYE UMRI WA MIAKA MIA ATALAANIWA.”

Hivyo tunaona atakayetawaliwa hapo kwa fimbo ya chuma sio mkristo bali watakuwa ni watu wengine watakaokuja kuzaliwa ndani ya huo utawala wa miaka 1000. Na ndio maana huo mstari unasema “mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa” ikimaanisha kuwa ndani ya huo utawala kutakuwa na makundi mchanganyiko. Kwasababu kumbuka ile siku ya mwisho ya Bwana inayowaka kama Tanuru, atakayokuja pamoja na sisi(Bibi-arusi) kuuharibu ulimwengu wa sasa haitamaliza watu wote bali kuna watu wachache sana watakaosalia,soma Isaya 13:9-13

Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;

12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.

13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.”

Umeona hapo watu wataadimika kuliko dhahabu,ni jinsi gani watakavyobaki wachache sana na hao ndio watakaopata neema ya kuingia katika utawala wa miaka 1000 katika miili yao ya asili( Na hawa ndio watakaokuwa wakizaa na kuzaliana) lakini sisi tutakao kuja na Kristo kutakuwa hakuna kuzaa wala kuzaliana kwa sababu tutakuwa na ile miili ya utukufu iliyotoka mbinguni. Na pia wale waliouawa na mpinga-kristo (wanawali wapumbavu) nao watafufuliwa na kuhukumiwa kisha wataingia katika utawala wa miaka 1000. Ufunuo 20:4.

Sasa baadhi ya hawa watu (watakaozaliwa kwenye huu utawala) baadaye Shetani atakapokuja kufunguliwa kuwajaribu, shetani atawadanganya ndio watakaotaka kufanya vita dhidi ya watakatifu, kama biblia inavyosema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote. ndipo hukumu ya kiti cheupe itafuata kwenye ufufuo wa pili. ambapo waovu wote watahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto pamoja na shetani na kisha tutaingia katika umilele ambapo dhambi haitakuwepo tena wala waovu.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

Wale Watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu WALIKUWA WAPI KABLA YA KUFUFUKA kwao je! walikuwa Peponi au ni wapi?.

Je! ni kweli dunia iliumbwa takribani miaka 6000 iliyopita? na je! Shetani alikuwepo duniani wakati dunia inaumbwa?

JINA LA MUNGU NI LIPI?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

JIBU: Hili ni swali watu wengi wanajiuliza ni Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, badala yake akamwacha Hawa ajaribiwe na yeye?.

Tunapaswa tufahamu wakati mwingine Mungu anaruhusu sisi wanadamu tujaribiwe kwa makusudi maalumu ili tuujue uweza wake na asili yake kwetu sisi na pia tumjue yeye zaidi, kwamfano jaribu kufikiria tungemjuaje kama yeye ni mwokozi kama tusingepotea katika dhambi?, tungejuaje yeye ni mponyaji kama tusingeumwa, tungejuaje yeye ni wa rehema kama tusingeanguka, tungejuaje yeye ni wa neema kama tusingekuwa hatuna haki, tungejuaje yeye ni mwenye msamaha kama tusingekuwa na makosa n.k…

Kumbuka pia sikuzote dhahabu ili ing’ae lazima ipitishwe kwenye moto mkali ijaribiwe na sisi kama watoto wa Mungu ni lazima tujaribiwe na ndio maana Mungu hakumuua shetani. Hata tulipokuwa shuleni, lengo la mwalimu kututungia mitihani migumu sio kutufanya sisi tufeli, hapana bali ni kutuimarisha zaidi ili tuweze kukabiliana na changamoto za mbeleni. Na ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni.   Mungu ana makusudi makubwa sana na sisi chini ya jua na ndio maana anatupitisha katika njia hiyo. Tunachopaswa kufahamu ni kuwa siku zote Mungu anatuwazia mawazo yaliyo mema  

Yeremia 29:11 ” Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”  

Yote haya Mungu kayaruhusu ili kutuwekea msingi mzuri wa maisha yajayo matamu ya umilele yasiyokuwa na mwisho.   Hiyo ndio sababu kwanini Mungu hakumuua nyoka mwanzoni kabisa pale Edeni kabla hajaasi.

Zaburi 103:12 “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. 13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. 14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. 15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo”.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

UZAO WA NYOKA.

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?

CHANZO CHA MAMBO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! mtu aliyeokoka anaruhusiwa kumiliki Lodge ambayo ina Bar ndani yake?

Swali linaendelea….na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo?,kwa mfano mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kampuni ya TBL kazi ya kampuni hii ni kutengeneza na kuuza bia kama yalivyo makampuni mengine kama Serengeti nk. Huyu ndugu ni mkristo aliyeokoka na jumapili bila shaka hutoa fungu la kumi na sadaka zingine pia ana cheo kanisani ..je! ni kuna makosa yoyote kufanya hivyo?


 

JIBU: Kumiliki bar ni dhambi, vilevile kumiliki lodge lenye bar ni dhambi..biblia inasema wazi katika

Kumbukumbu 23:18 “usilete ujira wa kahaba wala mshahara wa mbwa katika nyumba ya Bwana, ni machukizo”

Kumbuka na sio tu kazi ya bar tu, bali hata na kazi nyingine yoyote isiyokuwa halali mfano biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi, ulanguzi,uuzaji pombe,wizi, kamari, uuzaji sigara n.k kamwe usijaribu kufanya hivyo ukadhani kuwa Mungu ataziridhia sadaka zako, hata kama unatoa nyingi kiasi gani au kwa moyo kiasi gani, kwa kufanya hivyo utakuwa unajichukulia laana badala ya baraka, ni machukizo mbele za BWANA, kutii ni bora kuliko dhabihu(1 Samweli 15:22) Mungu ni mtakatifu na sio mtaka-vitu.

Kwahiyo unapokwenda mbele zake ni vema kufahamu kuwa yeye ni Mtakatifu na anahitaji roho yako sana zaidi ya vitu vyako. Kwahiyo kuhusu hiyo kazi anapaswa aache, kwasababu biblia imeturuhusu kiungo chetu kimoja kikitukosesha tuking’oe. kumiliki bar ni dhambi..Hivyo amwombe tu Mungu awe mwaminifu atampa kazi nyingine tena nzuri zaidi ya hiyo.. Mungu Alisema kuwa anajua tunayahitaji hayo yote

Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”

Kwahiyo asiwe na wasiwasi hilo suala la baada ya kuiacha hiyo kazi atakula nini? hilo amwachie Mungu.Hivyo mshauri atafute kazi nyingine inayompa Mungu utukufu.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

SADAKA ILIYOKUBALIKA.

TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.

IMANI YENYE MATENDO;


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?

JIBU: Kuzimu ipo, na ni sehemu iliyo halisi kabisa biblia inaelezea katika (Luka 16:19-31)… Mtu anapokufa katika dhambi (yaani hajaoshwa dhambi zake kwa damu ya YESU KRISTO)..mtu huyo anaenda moja kwa moja kuzimu/jehanum, huko kuna mateso mengi sana, mtu huyo atakaa huko akingojea ufufuo wa wafu, ambao utakuja baada ya ule utawala wa YESU KRISTO wa miaka 1000 kuisha ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu..  

Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.  

Ukisoma pia Yohana 5:28 BWANA YESU aliyasema maneno hayo..

“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”  

Unaona wale wanaotenda mabaya wote watafufuliwa kwa ufufuo wa hukumu, hivyo baada ya kuhukumiwa kulingana na matendo yao ndipo watakapotupwa kwenye lile ZIWA LA MOTO atakapokuwepo shetani na malaika zake, lenye mateso mengi kuliko jehanum. ni kama tu vile mtu anapokamatwa na hatia anawekwa kwanza mahabusu kwa muda fulani akisubiria kupandishwa mahakamani, sasa akishahukumiwa mahakamani kulingana na makosa yake ndipo anapopelekwa magereza kutumikia makosa yake. na ndivyo itakavyokuwa kwa waovu wote walioikataa neema ya msalaba wa Bwana YESU KRISTO watakapokufa sasa hivi wataenda kuzimu kwenye vifungo na mateso, wakingojea hukumu ya mwanakondoo kisha baadaye watatupwa kwenye lile ziwa la moto.

Lakini wanaokufa sasa katika haki, wanapelekwa mahali panapoitwa “Paradiso” . Paradiso ni mahali panapofanana na mbinguni, lakini sio mbinguni, ni mahali pa raha, wanawekwa humo kwa muda fulani wakingojea ufufuo wa wenye haki, atakapokuja Bwana mawinguni, watafufuliwa na kuvaa miili ya utukufu na kuungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja kwenda na Bwana mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo.   Paradiso kwa jina lingine ni Peponi.

1 Wathesalonike 4: 15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”  

Hivyo ndugu fahamu kuwa kuzimu ipo. Ni sehemu halisi kabisa.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

SWALI:Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?


JIBU

HATUA YA UNYAKUO.

Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema  

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

  Hivyo anazidi kusema…  

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.

Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani, na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye baada ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.  

HATUA YA DHIKI KUU.

Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote (wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.

Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo.   Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikira wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.  

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote wasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16).   Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga (Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.

(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani.   Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).  

HATUA YA UTAWALA WA MIAKA 1000. 

Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),

VITA YA GOGU NA MAGOGU

japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),

Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.  

HUKUMU YA KITI CHEUPE CHA ENZI.

Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.  

HATUA YA ZIWA LA MOTO.

Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…

Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9).   Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

DANIELI: Mlango wa 1

UFUNUO: Mlango wa 16.

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

UDHAIFU WA SADAKA!


Rudi Nyumbani:

 

 

Print this post

Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?

JIBU: Tukisoma Kumbukumbu 10:17 inasema…

“Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa”.  

Hapa tunaona Mungu anajitambulisha yeye kama “Mungu wa miungu” sasa swali hawa miungu ni wakina nani?.   Bwana Yesu alisema mahali fulani katika kitabu cha Yohana,..  

Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?”  

Kwahiyo unaona hapo miungu inayozungumziwa hapo ni WATOTO WA MUNGU, (yaani sisi tuliomwamini yeye na kuoshwa kwa damu yake) inadhaniwa na wengi kuwa miungu iliyozungumziwa pale ni “SANAMU” LA! sivyo. Mungu hawezi akawa ni Mungu wa sanamu. Sanamu hata siku moja haziwezi zikampa Mungu utukufu, Na tunajua tabia za miungu ni lazima zifanane na Mungu, Hivyo basi kazi zile zile Mungu anazozifanya lazima na miungu izifanye, kwa mfano Mungu alitumia NENO lake kuumba na kufanya kila kitu na sisi vivyo hivyo kwa NENO lake tunaweza tukafanya kazi za Mungu vile vile kama yeye. Lakini tusipoweza kufanya hivyo inamaana sisi sio miungu kwasababu hatufanani na yeye. ni sawasawa tu na alivyojiita yeye ni MFALME wa wafalme, au BWANA wa mabwana.  

Kwahiyo ili sisi tuwe miungu lazima tuwe ni WATOTO WA MUNGU wenye tabia kama za kwake nazo ni: Upendo, Imani, Haki, Utakatifu, utu wema, kiasi n.k Wagalatia 5:22 hivyo tuzidi kutia bidii katika kumjua yeye ili tustahili kuitwa miungu.  

Maelezo haya unaweza kuyapata kwa njia ya video mwisho wa somo hili

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=Jqkm6O2IdUQ[/embedyt]


Mada zinazoendana:

BWANA YESU ALIKUWA ANAONYESHA KUWA MUNGU NI MUNGU MWENYE AKILI TIMAMU.

JE! MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA ALIVYOFANYA KWA MFALME SAULI?

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

JIBU: watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?..Ni swali ambalo halikuulizwa tu na watu wa kipindi cha Bwana Yesu pekee lakini hadi sasa swali hilo linaulizwa na wengi..

Tukisoma

Luka 13:23 ″Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache?   Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. ”

  Ukisoma tena..Mathayo 7:13 -14 Inasema..

13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwasababu njia imesongwa sana! lakini swali linakuja je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi ya ulimwengu huu ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki,tamaa, uasherati uliokithiri ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo, mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia,ufisadi n.k. na zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wengi wa uongo na hivyo kuifanya ile njia ya kweli isitambulike kirahisi, kwasababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi, imefikia hatua ya kwamba ukristo wa leo unapimwa na kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu na sio mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu), Neno la kweli limetupwa nje!.  

Bwana Yesu Kristo aliweka wazi pale aliposema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu? je! katika siku za Nuhu waliokoka watu wangapi? tunaona waliokoka watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani wakati ule..na tena alisema kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adama..je! wakati wa Lutu walipona watu wangapi?..Jibu ni dhahiri kuwa ni walipona watu 3 tu kati ya mamilioni waliokuwa wanaishi Sodoma na Gomora wakati ule. Na kumbuka Bwana Yesu hawezi kusema uongo,kizazi cha Nuhu na Lutu kimefananishwa na kizazi chetu.  

NA NI KWELI KABISA! watakaookolewa katika kizazi hiki cha mwisho tunachoishi ni WACHACHE MNO!!! Hivyo ndugu tujitahidi tuwe kati ya hao wachache watakaokolewa kwa kupita hiyo njia nyembamba iliyodharauliwa na kuchekwa na ulimwengu wote nayo ni UKRISTO ULE WA MTINDO WA KALE WA MITUME..ikiwa wewe ni mwanamke tupa nguo za kizinzi uvae kama mwanamke wa kikristo mwanamke wa kikristo havai vimini, suruali wala kaptula, hapaki wanja wala lipsticks, mwanamume wa kikristo hanywi pombe, sio mtukanaji, mkristo yoyote hapaswi kupenda mambo ya ulimwengu? Bwana Yesu alisema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako.? Ni wakati wa kutafuta vitu vya kimbinguni ili siku ile isitujie kama mwivi. Muda umeenda sana tunaishi katika kizazi kibaya kushinda vyote, tuwe macho Bwana yu mlangoni kuja. Amen.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UNYAKUO.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

1).Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli? 2).Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara? 3).Ubatizo Wa Mkristo Wa Kweli Ni Wa Namna Gani?

JIBU: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu anaweza kukipokea kwa shukrani mbele za Mungu…biblia inasema viumbe vyote vimetakaswa na Mungu, Tukisoma

1Timotheo 4:1-5 inasema..

“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”

Hivyo vyakula vyote ni halali lakini biblia inasema tule tu kwa IMANI, ila tukila kwa mashaka ni dhambi, na pia biblia inasema anayekula asimuhukumu yeye asiyekula, wala asiyekula asimuhukumu anayekula, kwasababu tumetofautiana ujuzi, haupaswi kumkwaza mwenzako(Ndugu yako) kwa ujuzi ulionao, ukimkosea mwenzako kisa hali nguruwe ni sawa na kumkosea Kristo mwenyewe

1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”…..

8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.    

Hivyo tunafundishwa tuwe na hekima tunapokuwa katikati ya jamii fulani ya watu, iwe ni wakristo au isiwe wakristo, sio tunapofika mahali na kukuta jamii fulani hawali chakula fulani (nguruwe), na sisi tunaanza kula mbele yao na kuwaudhi. Hivyo ni sawa na kumkosea Kristo, ndio maana Paulo anasema ni “heri nisile nyama kabisa kama itakuwa ni kikwazo kwa ndugu yangu.”  

Na pia tukisoma.

Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.

15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.

16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.

17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ” 

Hivyo katika agano la kale Mungu kukataza vyakula fulani visiliwe ni kwa ajili ya kutufundisha sisi wa agano jipya mambo kadha wa kadha, kwamfano, kama vile Bwana alivyotenga vyakula najisi na visafi, ilifunua rohoni kuwa kuna vyakula vilivyo visafi na najisi (mafundisho) hivyo wajitenge na vile vichafu, na kudumu katika vile vilivyo safi, kadhalika pia, ilifunua aina mbili za watu yaani waliowasafi (wayahudi), na walionajisi kwa wakati ule (mataifa) lakini Bwana alipokuja aliwatakasa wanadamu wote,(soma Matendo 10:9) kama aliwatakasa wanadamu je! si zaidi viumbe vyake vyote?..nk.

2) Mkristo wa kweli haruhusiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara wala kuuharibu mwili wake kwa namna yoyote ikiwemo kuchora alama kwenye miili (Tatoo),uzinzi, mustarbation n.k. kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hekalu la Mungu lazima liwe ni safi.

 1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

  3) Kuhusu ubatizo, ubatizo sahihi kulingana na maandiko ni wa kuzamishwa katika maji mengi, na inapaswa iwe ni katika JINA LA YESU KRISTO, kulingana na maandiko na sio kwa jina la BABA na Mwana na Roho Mtakatifu, kama inavyofanyika kimakosa na makanisa mengi, kwa ufafanuzi mrefu kuhusu UBATIZO SAHIHI fuata link hii  >> https://wingulamashahidi.org/2018/07/19/ubatizo-sahihi/

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.

BWANA YESU ANAMAANISHA NINI KUSEMA MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?

SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti kumweleza dhambi zako?.kwasababu imeandikwa “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;(Yohana 20:23)”

JIBU: Kwa kuongezea hapo Bwana Yesu pia alisema..

Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”

Hapo tunaona Petro alipewa funguo za ufalme wa mbinguni za kufunga na kufungua,(ambazo ni sawasawa tu na kumwondolea na kumfungia mtu dhambi) na vivyo hivyo na mitume wengine wote waliosalia walipewa funguo hizo hizo, lakini haikuwa na maana kuwa “wanao uwezo wa kumwondolea mtu dhambi kwa kumtamkia tu basi” hapana! bali walipewa “FUNGUO” za kumfanya mtu kuondolewa dhambi zake (UELEWA),, na ndio maana Petro na mitume wengine walipowahubiria watu na kuamini moja kwa moja waliwaambia WATUBU na WAKABATIZWE KILA MMOJA WAO KWA JINA LA YESU KRISTO ili dhambi zao ziondolewe (Matendo 2:38) lakini hawakuwaambia..”Njooni sisi tumepewa uwezo wa kuwaondolea dhambi zenu hivyo pokeeni msamaha”….

Unaona hapo huo ufunguo ni UFUNUO/UELEWA wa jinsi ya kufanya dhambi za mtu ziondolewe, Na ndio huo wa kumuhubiria mtu atubu, kisha akishatubu akabatizwe, hapo ndipo dhambi zake zitakuwa zimeondolewa.

Lakini Papa na Mapadre, na baadhi ya viongozi wengine wa kidini hawafanyi kama mitume walivyofanya bali wao wanawatamkia tu watu kwamba wamesamehewa dhambi zao basi, bila kufuata mwongozo sahihi kwa kisingizio cha hayo maandiko ya kwamba wao wamepewa hayo mamlaka….(kutokana na kukosa UFUNUO wa Roho Mtakatifu ndani yao wanayatafsiri maandiko kwa akili zao ili kutimiza matakwa yao wenyewe.) Mungu atusaidie. Kwahiyo kiongozi yeyote wa kidini akikwambia umesamehewa dhambi zako, pasipo toba binafsi na ubatizo sahihi matamshi yake ni batili yakatae.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE KUNA ANDIKO LINALOMRUHUSU MWANAMKE KUWA SISTER?

KATIKA MARKO 2:2-12, KWANINI BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE KIWETE?

KWANINI MTUME PAULO HAKUMSAMEHE MARKO, PINDI WALIPOTAKA KWENDA WOTE KAZINI?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

 


Rudi Nyumbani:

Print this post