Category Archive maswali na majibu

Tafsiri ya Wakolosai 2:18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu,

SWALI: Nini maana ya vifungu tunavyovisoma katika Wakolosai 2:18,

 ‘Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;


JIBU: Tukianzia mistari ya juu anasema..

16  Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

17  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;

Katika vifungu hivyo, Mtume Paulo anaanza kwa kuwaambia ‘mtu asiwanyang’anye thawabu yenu’. Akiwafananisha na wana-michezo ambao wanashiriki katika mashindano Fulani, ambao hujitahidi kwa kila namna kujizuia, na kujichunga ili wafanye vema katika mashindano hayo wachukue tuzo.

Sasa Paulo, anatoa angalizo, akirejea mfano wa washindani hao, yawezekana mwingine akamfanyia hila mwenzake, ili asiwe na ufanisi, kwenye michezo hiyo akashindwa kushiriki vema na kuchukua tuzo, kwamfano anaweza kumpa kinywaji Fulani ambacho kitadhoofisha uchezaji wake, au atamdanganya afanya zoezi Fulani,  ambalo anajua kabisa halina manufaa kwake, kwamfano labda mchezaji ni mwana-riadha, utaona Yule mwingine anamwambia akanyanyue vyuma vizito atakuwa mwepesi kukimbia. Kumbe kukimbia hakuhusiani na misuli mikubwa bali pumzi.

Vivyo hivyo Paulo aliona kuwa kuna waalimu wa uongo, viongozi wa uongo,watakaozuka, kuwadanganya watu waiache njia sahihi, ya kukubaliwa na Mungu. Na ndio hapo anataja  mambo matatu ambayo watakuwa nayo;

Jambo la kwanza,

Watachukua thawabu yao kwa kunyenyekea kwa mapenzi yao wenyewe tu,

Kunyenyekea sio kubaya, ni tunda la Roho Mtakatifu ndani ya mtu, na wakristo wote, tunasukumwa katika unyenyekevu. Lakini angalia hapo anasema kunyenyekea KWA MAPENZI YAKE MWENYEWE. Maana yake, ni kuwa hanyenyekei kwa mapenzi ya Mungu, bali yake. Na hiyo ni mbaya, kwasababu watu wa kidini leo hii ndio kanuni yao, hubuni njia zao za kumwabudu Mungu, na hiyo huwavutia watu wengi, waone kama ni Mungu kweli anaabudiwa, kwa unyenyekevu na heshima, nao wanaingia kwenye mkondo huo. Wanasahau kuwa ibada lazima ifanyike kwanza katika Roho na Kweli.

Mambo kama kusujudia, kuvaa mavazi Fulani meupe, kutawadha mwili, kuvua viatu katika nyumba za ibada, kuomba kwa sauti ya kuvuta sana, ya upole, huku umeinamisha kichwa chini, unaibusu biblia. Hudhanikuwa kuwa ndio hicho Mungu anakitaka,  Lakini ndani, kinywa chake kina matusi, akitoka hapo anakwenda kuishi maisha kishirikina, na ulevi.  Huo ni udanganyifu mkubwa sana.

Ndicho Paulo alichokiona kwa kanisa la Kolosai, kulitokea watu wanawaambia usile kambale ni chukizo kwa Mungu, shika siku  ya sabato, inatosha.. Yote hayo yakifanyika kimwili. Lakini wasifundishe kwamba unyenyekevu wa ki-Mungu hutoka rohoni, ukisukumwa na neema katika  Roho Mtakatifu, Ambapo mtu kupaswa kukubali wokovu kwanza, na kutii kwa kumfuata Kristo anayeweza kumfanya mtu kiumbe kipya, na sio jambo la kufanya kimwili tu, akidhani atampendeza Mungu.

Jambo la pili

 wanaweza kuwanyang’anya thawabu yao kwa mafundisho ya kuabudu malaika.

Tangu zamani, kulikuwa na watu waliowaweka malaika katika nafasi ya Mungu. Na kuvuka ile mipaka ya kutuhudumia tu sisi  (Waebrania 1:14). Hivyo ikiwa mtu alikuwa na karama Fulani ya maono, ambapo mengine huletwa kwa mikono ya malaika, tunaliona hilo mara nyingi tangu Musa, na wana wa Israeli jangwani, pamoja na mitume mpaka Yohana kule Patmo. Mungu aliwatumia malaika kwa sehemu kubwa kutufikishia sisi jumbe zake, kwasababu waliwekwa kutuhudumia sisi.

Lakini dini na imani zikazuka kuanzia hapo, kwa baadhi ya watu wakaanza kuwafanyia ibada, jambo ambalo ni chukizo kwa Bwana. Hata leo utaona zipo sala za malaika na watakatifu kuwataka wawaombee. Au wawasaidie vitani. Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu umeokoka, kuwa makini na ibada hizo, taabu yako kwa Mungu yaweza kuwa bure, kwasababu unamudhi Mungu. Ibada za namna hiyo hazina tofauti na ibada za majini. Usiabudu mwanadamu, wala kiumbe chochote kilicho mbinguni wala duniani.

Jambo la tatu

Na mwisho anasema wakijivuna bure kwa akili zao za mwili.

Kujivuna, maana yake kusifia vitu vya mwilini mfano vipaji vyao, wengine ujuzi wa kuongea vizuri, na kupangalia maneno, werevu, elimu za falsafa, mambo ambayo Paulo aliyaona, yakiwavuta wengi, na kuacha njia kamilifu ya Kristo iliyo katika neema, upendo,  Imani na nguvu za Mungu. (2Wakorintho 11:18-20).

Injili inabadilishwa inakuwa vichekesho, na kanuni za ki-ujasiriamali,

Hata leo mimi na wewe ni kuwa makini, bidii yako katika Kristo isichukuliwe na udini, bali Neno, isichukuliwe na maono na karama, na ibada za malaika bali Mungu, isichukuliwe na falsafa za kibinadamu, na mwonekano, bali, Roho Mtakatifu na kweli, katika neema.

mtu asichukue taji lako

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Rudi Nyumbani

Print this post

Malimbuko ya Akaya maana yake nini? (1Wakorintho 16:15).

Swali: Haya malimbuko ya Akaya tunayoyasoma katika 1Wakorintho 16:15 yalikuwaje?

Jibu: Turejee..

1Wakorintho 16:15 “Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa STEFANA kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu)”.

“Akaya” inayotajwa hapo si mtu, bali ni eneo/mji uliopo maeneno ya Ugiriki kwa sasa. Mji huu umetajwa pia katika Matendo 18:12, Matendo 19:21, 2Wakorintho 1:1, 1Wathesalonike 1:7-8 na Yuda 1:6.

Mji huu wa Akaya, ulikuwa ni moja ya miji ambayo Mtume Paulo alipita kuhubiri injili ya BWANA YESU. Na mmoja wa watu wa kwanza kabisa kumpokea Bwana YESU na kuokoka katika Mji huo ni huyu mtu aliyeitwa STEFANA pamoja na nyumba yake yote.

Hawa ndio walikuwa watu wa kwanza kabisa kuipokea injili katika mji huo, na baadaye wakaongezeka wengine wengi. Hiyo ndio maana ya Malimbuko iliyotajwa hapo… Sio malimbuko ya mazao ile inayotajwa katika Kutoka 22:29, bali inayomaanisha “wa kwanza kupokea injili”.. kwamaana maana tu ya malimbuko ni “kuzaliwa kwa kwanza”, hivyo hawa watu walikuwa ni wa kwanza kuzaliwa katika injili katika mji huo wa Akaya.

Lakini sifa nyingine ya kipekee aliyokuwa nayo huyu Stefana pamoja na nyumba yake yote ni roho ya UKARIMU, ambayo waliionyesha sana kwa Paulo na watumishi wengine waliokwenda kuhubiri injili katika miji hiyo, walikuwa tayari kutoa vya kwao ili kuwatunza watumishi wa Mungu.

Na kwa tabia hiyo, ndiyo Mtume Paulo kwa kuongozwa na roho anawaagiza watu wa Korintho pamoja na sisi kwa ujumla tuige tabia kama hiyo na pia tuwatii sana watu wanaojitoa kwaajili ya kuishika mkono kazi ya Mungu, na pia tuwe tayari kushirikiana nao..

1Wakorintho 16:14 “Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

15  Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);

16  WATIINI WATU KAMA HAWA, NA KILA MTU AFANYAYE KAZI PAMOJA NAO, NA KUJITAABISHA.

17  Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu”

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SADAKA YA MALIMBUKO.

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

Yerusalemu ni nini?

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Ijapokuwa amekufa, angali akinena(Waebrania 11:4)

SWALI: Maandiko yanaposema Habili ijapokuwa amekufa angali akinena, je! Ananenaje, wakati yeye ni marehemu. Je! Hiyo inamaana wazee wetu wa zamani wanaweza kunena na sisi?

Waebrani 11:4  Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena


JIBU: Kibiblia ni kweli kabisa watakatifu waliokufa kale hunena nasi. Lakini kunena kwao ni tofauti na huku kunakodhaniwa, kwamba mzimu unakutokea kwenye ndoto, au unasikia sauti ya petro makaburini ikizungumza na wewe,  Hapana, ukiona hivyo ujue huzungumzi na huyo mtu, bali ni pepo.

Sasa watakatifu waliokufa wanazungumzaje na sisi?

Ni kwa ushuhuda waliouacha. Maisha yao na maagizo yao, ndio huzungumza nasi, sikuzote, kana kwamba tupo nao sasa, kwa mafundisho yao yaliyopo  mpaka sasa kana kwamba tunawaona wenyewe kumbe wamekufa.

Ndio maana ile habari ya Yule tajiri wa Lazaro, tunaambiwa alipofika kule kuzimu akaomba mtu atolewe kwa wafu awahubirie injili, akakataliwa, kuonyesha kuwa hakuna mtu aliyekufa mwenye uwezo wa  kuja tena kuzungumza na sisi, nafasi hiyo haipo kwao. Lakini waliambiwa WANAO MUSA NA MANABII, WAWASIKILIZE.

Luka 16:29  Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

Maana yake ni kuwa sio kwamba Musa kweli alikuwepo duniani, au manabii wa kale kama Isaya walikuwa duniani kwa wakati huo, anaambiwa hayo maneno. Lakini shuhuda zao na mahubiri yao, huwawakilisha wao. Tunaweza kusema “ijapokuwa wamekufa wangali wakinena”

Ndivyo ilivyo kwa Habili, ijapokuwa aliuliwa na ndugu yake, lakini IMANI yake inasema nasi mpaka leo. Mitume wa Kristo ijapokuwa hawapo duniani lakini sauti zao tunazisikia hadi sasa.

Lakini pia kuna mahali pengine biblia inasema damu ya Yesu hunena mema kuliko ya Habili (Waebrania 12:24). Kufahamu kwa kina damu ya mtakatifu  hunenaje? Pitia somo hili. >>> DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.

ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Yakobo alimaanisha nini kusema ‘ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’ Mwanzo 28:21

Mwanzo 28:21

[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.


JIBU:

Sura hiyo inaeleza ugumu wa safari ya Yakobo alipokuwa anamkimbia ndugu Yake Esau kuelekea nchi ya ugenini ya baba zake. 

Hivyo akiwa huko jangwani peke yake, haoni mbele wala nyuma, haoni msaada kwa mtu wala kitu, ndipo akamwekea Mungu nadhiri, na kumwambia maneno hayo. 

‘nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’. 

Lakini swali linakuja je hakumwamini Mungu, au kumfanya Mungu wake mpaka hapo ambapo angetimiziwa nadhiri zake? Kwamaana baada ya miaka 20, ndio tunaona yakitimia hayo yote? je hiyo miaka yote ya hapo katikati YEHOVA hakuwa Mungu wake, mpaka wakati ambapo angetimiziwa nadhiri yake?

Jibu: mstari huo haumaanishi kwamba Yakobo alikuwa anamweka kwanza Mungu kwenye majaribio halafu akishamfanikisha ndipo amfanye rasmi kuwa Mungu wake.

Hapana, ingekuwa hivyo tusingeona  katika kipindi hicho chote Yakobo akimtumainia Mungu wa baba zake, angeendelea tu na mambo yake mpaka huo wakati ufike.Lakini tunaona Yakobo hakucha kumwamini Mungu mahali popote.

Katika kauli hiyo hapo Yakobo alikuwa anaongezea tu, kujitoa kwakwe zaidi kwa Mungu, endapo  atarudishwa salama, na ndio maana maana ukiendelea vifungu vinavyofuata..

anasema atamtolea Mungu wake Fungu la kumi kwa kila atakachokipata..

jambo ambalo hapo mwanzo asingeweza kwasababu alikuwa hana chochote.

Mwanzo 28:21-22

[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.

[22]Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi. 

Kwa namna nyingine..anamwambia Mungu nitafanya vizuri zaidi kwako, endapo nitarudi salama, kutoka katika nchi ya ugenini.

Au ni sawa na leo mtu aseme Bwana nitakutumikia endapo utaniondolea huu ugonjwa wangu wa kupooza. 

Hiyo haimaanishi kuwa amemwekea Mungu masharti, kwamba sasahivi hataki mtumikia mpaka aponywe hapana, lakini anaeleza kikwazo chake. Na kwamba kikiondolewa ataweza timiza vizuri matakwa yake ya kiutumishi. Ndicho alichokimaanisha Yakobo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

USIMPE NGUVU SHETANI.

Kutoka 21:10 ina maana gani?.

Print this post

Epafrodito ni nani kwenye biblia?

Epafrodito alikuwa ni mmoja wa watendakazi wa makanisa yaliyokuwa Filipi. Anajulikana kama mhudumu wa mahitaji ya mtume Paulo. Tunaona upendo wa Kanisa la Filipi jinsi lilivyomkumbuka Mtume Paulo alipokuwa kifungoni Rumi. Hivyo likaazimu kumtumia mahitaji yake ya kifedha. Ndipo likamchagua huyu Epafrodito. Kusafiri umbali wote huo mrefu na kiasi hicho kingi cha fedha mpaka Rumi.

Wafilipi 4:18  Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

Na jambo hili lilikuwa ni desturi yao, kumtimizia Paulo mahitaji yake mara kwa mara (Wafilipi 4:16)

Lakini tunaona mbeleni katika waraka wa Paulo, anaeleza hali ya ndugu huyu ambaye Paulo  alimwita pia mtume,jinsi ilivyobadilika kwa kuugua sana karibu na kufa, akiwa katika kazi hiyo hiyo ya kumuhudumia Paulo. Lakini  Ijapokuwa alikuwa katika hali mbaya bado hakuacha kumuhudumia Paulo,

Tunasoma katika hali yake ngumu ya kuumwa, Mungu alimhurumia akamponya. Hatujui aliugua ugonjwa gani, lakini ni ugonjwa uliomdhoofisha kwelikweli, kiasi cha kudhaniwa ‘huyu ni wa kufa tu’, na bila shaka ulikaa ndani yake muda mrefu.

Lakini alipomaliza huduma yake, Ndio tunaona Paulo anawaandikia wafilipi waraka huo, na kuurejesha kwao kwa mkono wa huyo huyo Epafrodito,na ndani yake akielezea pia, shida zilizomkuta.

Wafilipi 2:25  Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.

26  Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.

27  Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni.

28  Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu.

29  Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.

30  Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu.

Ni nini tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu huyu?

Upendo wa kujali hali za wengine. 

Biblia inasema upendo hautafuti mambo yake wenyewe (1Wakorintho 13). Alikuwa tayari kufa, ili askari mwenzake asikose mahitaji yake. Si ajabu Paulo alimwita mtume. Mungu anathamini sana, utume wa namna hii.

Lakini Tunajifunza huruma ya Mungu ijapokuwa alikuwa karibu na kufa, bado Mungu aliweza kumponya akawa mzima kabisa. Hata mimi na wewe, je tunaweza kufikia hatua mbaya ambayo hata madaktari wanasema haiwezekani kupona? Kama ndio mkumbuke Epafrodito, una hali ngumu unayoweza kusema hapa sivuki, mwisho umefika? Mkumbuke Epafrodito. Yote yanawezekana kwa Mungu.

Ikiwa ni mtumishi wa Mungu, usiohofu uteterekapo kiafya au kihali, Mungu anakuona, atakutia nguvu, usiache kumwamini.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

USIFE NA DHAMBI ZAKO!

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Rudi Nyumbani

Print this post

Epafra ni nani katika biblia? (Wakolosai 1:7)

Epafra ndiye alikuwa mwangalizi wa kanisa la Kolosai, Paulo alimtambua  kama mhuhudumu mwaminifu wa Kristo. Kiasili naye pia alikuwa mwenyeji wa mji huo huo wa kolosai kufuatana na kauli Paulo aliyoisema katika Wakolosai 4:12, “aliye mtu wa kwenu”

Waraka huu unaonyesha Epafra kama  mhudumu ‘mwaminifu’ wa Kristo. Ikiwa na maana alijitoa kikamilifu kwenye kazi ya Mungu bila kupunguza chochote, mtumwa aliyegawa posho kwa wakati.

Aliyeitwa pia mjoli wa Paulo. Ikimaanisha mtendakazi pamoja na Paulo katika shamba la Bwana.

Lakini pia Paulo alikuwa ni kiongozi na mshauri wake. Tunaona aliwasilisha ripoti zake kwake, za maendeleo ya kanisa. Jinsi upendo wao ulivyokuwa mwingi.

Wakolosai 1:7  kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu

8  naye alitueleza upendo wenu katika Roho.

Epafra alikuwa na juhudi sio tu kwa kanisa la Kolosai, bali pia na makanisani mengine ambayo ni  Laodikia na Hierapoli (Wakolosai 4:13).

Tunasoma pia Epafra alikuwa mtu wa bidii  ki-maombi kwa ajili ya kanisa la Kolosai

Wakolosai 4:12  Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.

13  Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli.

Lakini mbeleni katika waraka wa Paulo kwa Filemoni tunaona alikuja pia kufungwa, pamoja na Paulo kule Rumi.

Filemoni 1:23  Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu;

Ni nini tunajifunza katika maisha ya Epafra?

Kujitoa kwake kimaombi, kwa kanisa ili lisimame kamilifu na kuthibitika katika mapenzi ya Mungu. Epafra alikuwa na juhudi isiyo ya kawaida katika kuliombea kanisa. Alijua kanisa lisipoombewa haliwezi kusimama vema. Hivyo aliwekeza sana katika maombi na kuwa pia na bidii katika uaminifu kwenye  huduma.

Bidii yake hakika ilizaa matunda, na ndio maana Bwana akaruhusu habari zake ziandikwe, na kusomwa hadi leo.

Je! Na sisi tunathamini maombi katika kuliombea kanisa? Unapoona watu wamepoa kiroho, watu wanaishi kimwili kanisani, wanafanya mambo ya aibu, sio kumnyooshea kidole mchungaji, au shemasi au mzee wa kanisa na kumlaumu. Hapo huwezi tatua tatizo. Shida ipo kwenye kupungukiwa kwa maombi. Chukua muda mwingi kuliombea kanisa kuliko kuzungumza. Bwana atayatenda yote uliyoyatamani.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; (Luka 17:10) 

SWALI: Naomba kufahamu maudhui iliyo nyuma ya  Luka 17:10 inayosema..

[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.


JIBU: Kufahamu kwanini Yesu  aliwaambia wanafunzi wake maneno hayo. Ukianzia juu utaona ni kufuatana na swali walilomuuliza kuhusiana na IMANI. Walimfuata na kumwomba awaongezee Imani.

Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali mngeuambia mkuyu huu ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii.

Luka 17:6

[6]Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

Akimaanisha kuwa  sio suala la kuongezewa Imani, ili mweze kufanya makubwa, bali kile kidogo sana kinaweza tenda yote. Na kidogo hicho mitume walikuwa nacho ndani yao, ambacho hata mimi na wewe tunacho. Isipokuwa hawakujua namna ya kukitoa.

Ndipo Yesu akaendelea kuwaambia kwa mifano sasa, ili jambo hilo litokee, kanuni yake ni kuwa wanapaswa wawe kama watumwa wasiokuwa na faida kwa Bwana wao. Sasa kwa namna gani? fuatilia mfano wenyewe…

Luka 17:7-10

[7]Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?

[8]Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?

[9]Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Mfano huo unajieleza, zamani mtumwa aliponunuliwa hakuwa anafanya kazi kama mwajiriwa, bali kama mnyama tu mfano wa punda ambapo kazi yake ilikuwa ni moja tu kumuhudumia Bwana wake, na sio kujitafutia maisha.

Sasa hapo Yesu anatumia mfano wa huyo Bwana mwenye mtumwa wake ambaye amemweka kuwa mkulima wa shamba lake, ambaye asubuhi huondoka jioni hurudi kwa Bwana wake.

Anasema, je atakaporudi atamwambia kaa hapo upumzike? wakati mimi bado sijala? Ni wazi kuwa ataongezewa majukumu, mpaka ahakikishe Bwana wake ameshiba, hana mahitaji tena ndipo sasa na yeye apewe nafasi ya kupumzika na kula.

Hivyo Yesu alitumia mfano huo, kuwaambia wanafunzi wake, jinsi na wenyewe wanavyopaswa kuwa kwa Mungu.

“[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.”

Akiwa na maana, mkihitaji hilo jambo la IMANI mjaliwe, yawapaswa muwe kama watumwa wasiokuwa na faida. Mtumikieni kwanza Bwana wenu sana, kama watu wasiotazamia malipo yoyote.

Ukihubiri sana miaka ishirini, unatanga na jua huoni faida yoyote iliyoongezeka kwenye maisha yako, huoni maendeleo yoyote. Usimuulize Bwana mbona hujanipa chochote mpaka leo. kuwa kama mtumwa asiye na faida.

Huu ndio utumishi Bwana anaoutaka kwetu, leo hii wahubiri wengi, watumishi wengi, wachungaji wengi wamepoa, wamerudi nyuma kwasababu walitazamia malipo kutoka kwa Bwana katika kwa kile walichokuwa wanakifanya, na waliopoona hawapati, kinyume chake maisha yao ndio yanakuwa magumu, wakaacha utumishi wakaenda kutafuta mambo yao.

Ndugu ni lazima tuelewe kanuni za Mungu wetu. Ikiwa unaenda kuifanya kazi ya Bwana ili ukusanye sadaka, upate unafuu kimaisha..Ni heri ukaacha ukatafute biashara nzuri uwekeze nguvu zako huko. Mungu anaweza asikupe chochote kwa miaka mingi, unataabika tu,  je utaendelea kumtumikia?

tukubali kuwa watumwa wasio na faida. Akitupa sawa, asipotupa sawa. Lakini tujue kuwa sikuzote anatuwazia yaliyo mema.

Ujumbe wa Bwana hapo ni kwamba tukitaka imani itoke tuwe watumwa wa namna hii.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.

Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.

Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani.

Rudi Nyumbani

Print this post

Fahamu mana ya Zaburi 48:14 Yeye ndiye atakayetuongoza

SWALI: Ipi tafsiri ya Zaburi 48:14 ?

[14]Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele  Yeye ndiye atakayetuongoza.


JIBU: Mwandishi anajivunia sifa ya Mungu wao wa milele. kwamba ndiye atakayewaongoza.

Akiwa na maana atayewaongoza katika mambo yao yote, kwamba kamwe hawezi kuwaacha, atakayewaongoza njia sahihi ya uzima, njia sahihi ya kupigana vita, ya kujenga na kupanda.

Ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli. Mungu alikuwa nao jangwani kwa nguzo ya moto na wingu kuwaongoza, aliwapelekea malaika wake kuwalinda, aliwafundisha namna ya kupata faida katika shughuli zao, akawainulia na waamuzi, pamoja na wafalme na manabii kuwachunga na mwisho akawaletea mkombozi, ambaye ndio ukamilifu wa yote. Kuonyesha wema wake na kiu yake ya kuwaongoza  watu wake.

Hata sasa, sifa yake ndio hiyo hiyo, ndio maana na sisi tuna ujasiri wa kusema…

‘Yeye ndiye atakayetuongoza’.Sio tu kwa wakati huo, bali mpaka siku ya kufa kwetu.

Alipokuja mwokozi hakutuacha hivi hivi kama mayatima, bali alituachia msaidizi ambaye anatuongoza na kututia katika kweli yote, ndiye Roho Mtakatifu.

Yohana 16:13

[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Bwana akubariki.

Je umempokea Yesu?  Kama bado ni nini unasubiri ? Fungua hapa kwa mwongozo wa sala  ya toba ya imani. >>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

Rudi Nyumbani

Print this post

‘Waibao watu ‘ sawasawa na 1Timotheo 1:10 humaanisha nini?

SWALI: Biblia inapowataja ‘waibao watu ‘ sawasawa na 1Timotheo 1:10 humaanisha nini?


JIBU: Tusome;

1 Timotheo 1:8-10

[8]Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

[9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

[10]na wazinifu, na wafiraji, na WAIBAO WATU, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

Tangu zamani dhambi ya wizi, haikuwa tu katika vitu na mali, bali ilikuwa hata katika watu. Ndio kilele cha juu kabisa cha wizi.

Wizi huu ulikuwa na  malengo mbalimbali mojawapo ilikuwa ni kuwapeleka vitani, lakini pia kuwauza kama watumwa mfano katika biblia utamwona Yusufu (Soma Mwanzo 40:14-15). Na kama tunavyofahamu pia katika historia bara la Afrika lilikumbwa na tatizo hili, katika karne ya 17, waafrika wengi waliibiwa, na kuuza katika mabara ya ulaya.

Lakini kwa nyakati hizi wizi huu, umekuwa mbaya zaidi, kwasababu watu hawaibi tena watu kwa lengo la kuwatumikisha, bali kwa lengo la kuwafanyisha biashara ya kikahaba, wengine kuwaua ili wachukue viungo vyao kwa kazi za kishirikina, wengine wauze viungo vyao vya ndani kama vile figo, ili wapate fedha.

Jambo ambalo ni baya sana, ndio maana kwenye maandiko katika enzi za agano la kale adhabu ya wizi wa watu  haikuwa ndogo bali kifo.

Kumbukumbu la Torati 24:7

[7]Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Lakini sisi katika agano jipya, hatuna ruhusa ya kuua watu wa namna hiyo, isipokuwa tuonapo vitendo kama hivyo vikitokea ni ripoti katika vyombo vya dola, hapo utaisaidia jamii, kudhibiti uovu kama huo Lakini pia kumwomba Mungu, aiondoe roho hii chafu isiwepo katikati ya  jamii zetu, ili kuiponya kuiponya jamii.

Na Mungu atakubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea. Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.

Je! Malaika wanazaliana?

USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).

Rudi Nyumbani

Print this post

Marimari ni nini? (Luka 7:37)

Jibu: Tureje..

Luka 7:37  “Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya MARIMARI yenye marhamu”.

 “Marimari” ni jina lingine la “Marumaru”, kwahiyo popote katika biblia palipotajwa Marimari ni sawasawa na Marumaru. Na marimari ni mawe ya kaboni, ambayo yanatumika katika urembo wa ujenzi, mawe haya ni maarufu sana kwa kutengenezea Tiles za ukutani au chini.

Vile vile yanatumika kutengenezea baadhi ya vyombo vya kinakshi mfano wa cha hicho cha mwanamke katika Luka 7:37 n.k

Maandiko mengine yanayotaja Marimari ni pamoja na 1Nyakati 29:2, Wimbo ulio bora 5:15 na Ufunuo 18:12… lakini andiko lililotaja Marimari kama Marumaru ni Esta 1:6.

Je umempokea BWANA YESU, na kubatizwa katika ubatizo sahihi?.. Je unatambua kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU mara ya pili, na wakati wowote parapanda ya mwisho inalia?

Je macho yako yanaona hayo yote?.. kama huyaoni hayo basi fahamu kuwa upo gizani na yule mkuu wa giza (shetani) amekupofusha macho ili usione, Leo harakisha kupokea msaada kutoka kwa YESU.

Ikiwa utahitaji kumpokea YESU leo, basi fuatiliza sala hii hapa >>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

Rudi Nyumbani

Print this post