Tunasoma mara baada ya Bwana Yesu kuwatuma wanafunzi wake wengine 70 wawili wawili wamtangulie kila mahali alipotaka kwenda, na kuwapa amri ya kufanya ishara zote alizokuwa anafanya yeye, walipotii na kwenda kuhubiri kwa furaha na kurudi kumpa Bwana ripoti ya mambo yote yaliyotendeka huko…Wao Hawakujua ni kitu gani Bwana Yesu alikuwa anaona huku nyuma, pengine wao kwa nje walikuwa wanaona ni jambo la kawaida tu, wanatimiza wajibu wao uwapasao kufanya, lakini Bwana Yesu aliwafumbulia alichokuwa anakiona aliwaambia maneno haya:
Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”.
Unaona yaani kwa jinsi walivyokuwa wanalisambaza lile Neno la Mungu na kuiangaza nuru ya injili kila mahali, huku Nyuma shetani alikuwa anaanguka kwa kasi ya ajabu sana mfano wa Umeme/radi, hakuna kitu kinachosafiri kwa kasi zaidi ya umeme, hivyo hapo Bwana alipokuwa anasema nilimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme, alimaanisha ni anguko ambalo halikuwa na kipingamizi chochote kile (flawless). Leo hii shetani anaweza kuleta vipingamizi katika maombi, anaweza ukaomba lakini bado shetani akabakia pale pale ameshikilia..Lakini kwa pamoja tunapoamka na kwenda kuhubiri injili ya Kristo kila mahali, anajua hawezi kubaki pale pale, ni lazima aanguke tu, na ndio maana jambo kubwa ambalo shetani analipiga vita kuhubiri injili.
Kumbuka kibiblia mbinguni sio tu, kule Mungu alipo, mbinguni inaweza ikawa nafasi ya juu sana, ambayo kimsingi ndio inayompasa Mungu peke yake aikalie, lakini wanadamu au shetani wanaweza kutafuta nafasi hiyo kwa nguvu na kuketi hapo, na hivyo rohoni wakaonekana kama wamefika mbinguni. Soma Danieli 4:9-37, soma pia:
Isaya 14:13 “Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;”
Ikiwa wewe umeokoka na umekaa katika hali hiyo kwa miezi sasa, au miaka, na hutaki kuangaza nuru ya injili kwa wengine ili na wenyewe waokoke kama wewe, hutaki kuitumia karama Mungu aliyoiweka ndani yako kumtangaza yeye na huku unamwomba Mungu watu waokolewe nataka nikuambie shetani atendelea kuwatesa tu..Usitegemee kuwa shetani ataondoka kwenye jamii unayoishi, usitegemee huyo mkuu wa giza ataacha aliye katika eneo lako ataacha kuwapufusha watu macho wasiiamini Injili..Ataendelea sana kuziangusha roho za wengi…
Unadhani mapepo hayo yatadondoka kwa maombi tu?…Bwana Yesu hakuwaambia kauli ile walipotoka kusali, lakini aliwaambia kauli ile walipotoka kuhubiri..Vivyo hivyo na wewe, leo hii usipozaa matunda utafika wakati Bwana atakukata, unaposikia injili Mungu anatazamia na wengine waisikie hiyo hiyo uliyoisikia kwa kupitia wewe..Lakini kama wewe utakuwa ni kupokea tu hutaki kutoa ili na wengine waokolewe, wakati utafiki utakatwa.
Popote pale ulipo unaweza kuwahubiria wengine injili, iwe ni kazini, iwe ni shuleni, iwe ni mtaani, iwe ni nyumbani, iwe ni mitandaoni, iwe ni safarini, iwe barabarani..Kwa karama Mungu aliyokupa na mlango aliokufungulia itumie hiyo hiyo kumletea Kristo faida..Tukishirikiana kwa pamoja, hakuna nguvu yoyote ya shetani itakayoweza kuzuia watu wasimjue Mungu, yeye kazi yake itakuwa ni moja tu, kila sekunde ni kuanguka huko aliko kwa kasi ya umeme. Kuhubiri Injili ni moja ya zile silaha zilizotajwa katika..
Waefeso 6: 13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani”
Unapowahubiria wengine wokovu, unammaliza shetani na upande wa pili.
Ni maombi yangu utafanya hivyo kuanzia huu wakati. Bwana akubariki…
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
Luka 14: 25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33 Basi, KADHALIKA KILA MMOJA WENU ASIYEACHA VYOTE ALIVYO NAVYO, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”
Bwana Yesu alisema katika mstari wa 26 kuwa asiyemchukia Baba yake na Mama yake, mke wake, mwanawe, na ndugu zake wakiume na wake hawezi kuwa mwanafunzi wake..
Chuki inayozungumziwa hapo sio chuki ile ya dhambi, kwamba umchukie Baba yako au mama yako kwa nia ya kumdhuru, au kumdharau, au kumshushia heshima hapana! Bali chuki inayozungumziwa hapo ni “kuyachukia mapenzi yake ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu”…Baba anakuambia mwanangu tunapaswa tuende kwa waganga na wewe hali unajua kuwa hayo ni machukizo kwa Mungu, hapo unapaswa uyachukie hayo mapenzi ya Baba yako na kumwambia wazi kwa ujasiri kuwa “Baba mimi siwezi kwenda huko, kwasababu ni Mkristo, namwabudu Mungu aliye mbinguni”..
Mama yako anakwambia ukajiuze tupate pesa, wewe unatakiwa umwambie wazi kuwa “mimi siwezi kufanya hivyo kwasababu ni Mkristo”..Mume wako anakuambia ufanye mambo machafu ambayo ni machukizo kwa Mungu, na anakulazimisha, kutenda dhambi.. hapo unapaswa kumweleza wazi msimamo wako kwamba wewe ni Mkristo, na kama hataki kuishi na wewe, basi anayoruhusa ya kuondoka!…Biblia imeruhusu matengano Katika mazingira kama hayo (soma 1Wakorintho 7:15).
Kuna mtu mmoja alikuwa anazungumza na mimi anasema alikuwa ameokoka tu vizuri yeye na mchumba wake, tena walikuwa wamesimama ipasavyo katika imani, lakini siku ya kwenda kutambulishwa kwao, mama yake Yule mwanamume akamwambia kama hutaacha huo wokovu wako, mimi sio mama yako, na nitakuachia laana..Sasa Yule mwanamume kwa kuwa alikuwa anampenda mama yake zaidi ya Kristo, akaamua kuacha wokovu anakamshawishi na mke wake wote wakaucha wokovu, wakaanza kuwa watu wa ajabu, Yule mwanamume akawa mzinzi na mtu wa kidunia kishinda hata walipokuwa hapo mwanzo..Sasa watu wa namna hiyo Kristo anasema hawafai kwake, na aliposema hawafai alimaanisha kusema kweli hawafai..
Na jambo lingine Bwana alilolisema ni kwamba 33…KADHALIKA KILA MMOJA WENU ASIYEACHA VYOTE ALIVYO NAVYO, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”
Pia mtu asiyeacha vyote alivyonavyo…Maana ya kuacha vyote ulivyo navyo ni kuvitoa vile vitu ndani ya moyo wako…kila mtu anafahamu namna ya kukitoa kitu moyoni, hakuna haja ya kuelezea… “unapotoa kitu moyoni, unakuwa unakifuta ndani yako, kinakuwa sio kitu tena kinachokupa raha, kiwepo kisiwepo ni sawa tu” Wakati mwingine hiyo hali inaweza kuambatana na kuviacha vitu kwa nje kabisa wazi wazi…
Ulikuwa ni Tajiri unauacha utajiri wako unamfuata Yesu, maana yake…Hata mali zote zikipukutika katika safari yako ya kumfuata YESU hilo hujali, kwasababu hazipo tena moyoni mwako, Unamhisi Yesu moyoni kuliko utajiri ulionao…Na pia unakuwa humfuati Yesu ili akupe mali au azilinde mali zako, unamfuata kwasababu Moyoni mwako unaona una haja naye…Kuna upendo fulani ambao unamiminika ndani yako ambao hauwezi kuuelezea, Unajikuta tu unampenda tu Yesu bila sababu kama yeye anavyokupenda wewe bila sababu yoyote.
Kadhalika Ulikuwa ni MASKINI, unauacha Umaskini wako unamfuata YESU. Unauondoa umaskini moyoni mwako….Usimfuate Yesu kwasababu hauna gari! Au kwasababu umaskini unakutesa na kukuumiza… Hapo hujajikana nafsi ndugu! Usimfuate Yesu kwasababu unataka utajiri, au unataka heshima katika jamii, au kwasababu unataka kuwakomesha maadui..Unatakiwa Uuache umaskini wako ndipo unamfuata Yesu kiasi kwamba hata katika safari yako ya Imani, ukiongezekewa na kuwa Tajiri wa mambo ya kimwili, hilo kwako halina maana sana!…mali zikiongezeka ni kama vile moyoni mwako hakuna kilichoongezeka…lakini uhusiano wako na Yesu unapoimarika ndipo unajihisi uchangamfu wa Ajabu unakuvaa….Inafikia mahali umasikini na Utajiri kwako ni sawasawa tu! Kama Ayubu, ilifika wakati hata mali zilipoongezeka hakufurahia (Soma Ayubu 31:25)..
Wapo watu ni maskini lakini hata katika huo umaskini wao, hawajawahi kumwomba Mungu katika sala zao utajiri, wameridhika na wana amani ya Ajabu mioyoni mwao..wawe nacho wasiwe nacho, hilo kwao halijalishi maadamu wanaye Yesu, hilo kwao ndio linalojalisha, huo ndio utajiri mkubwa kwao. Hivyo ni lazima kabla ya kumfuata Yesu kuuacha umaskini! Na kumfuata yeye wewe kama wewe.
Na pia baada ya kuacha vyote namna hiyo, kitakachofuatia ni kuchukiwa, kutengwa, kuonekana umerukwa na Akili, kuonekana mjinga katika jamii na kuonekana hufai…Na hivyo pia unapaswa uwe navyo tayari! Bwana Yesu hakutuficha kabisa alituambia ili tukikutana nayo tusiseme mbona hivi mbona vile..Upige gharama kabisa kabla ya kuanza kujenga Mnara! Usije ukafika katikati ukashindwa kumalizia…
Ndivyo ilivyo kwa Bwana Yesu kabla ya kumfuata, piga hesabu kuwa kuna kuchekwa huko mbele, kuna kudharaulika, kuna kupungukiwa wakati mwingine hata kwa kipindi kirefu sana, wakati mwingine hata miaka kadhaa, hata miaka 5, au 10, hata 15, lakini haitadumu hivyo hata milele, kuna kutengwa na kuonekana mjinga, hata kwa miaka kadhaa…piga gharama zote hizo..Kama haupo tayari! Kuonekana mshamba kwa muda mrefu hivyo, au kuonekana mjinga kwa miaka kadhaa, au kudharaulika kwa miaka kadhaa, au kama haupo tayari kukosana na mama yako kuhusiana na Imani yako, au kukosana na Baba yako, au Watoto wako, au mke wako..kama unajua yatakushinda huko mbeleni…Biblia inasema tafuta sharti ya Amani mapema!…Usijiingize mahali ambapo hujajua yatakayokupata mbeleni, ukaja ukakutana na ambayo hukutegemea ukaanza kujuta na kulalamika.
Kwasababu Bwana Yesu anasema:
Luka 12: 51 “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano.
52 Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu.
53 Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu”.
Je! Umejikana nafsi?..Umejitwika msalaba wako na kumfuata Yesu? Fahamu kubwa mtu yeyote anayeingia gharama kubwa kama hizo, Sio bure bure tu, Huyo anapelekwa katika viwango vya juu zaidi vya kuwa karibu na Kristo zaidi ya watu wengine wote, anafanyika kuwa mwanafunzi wake, na zaidi ya yote Bwana atakuja kumpa mara mia, na siku ile ataketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi akiwahukumu mataifa..(Mathayo 19:27-30)
Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?(MATHAYO 6:24)
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
JE? NI HATUA ZIPI MUHIMU ZA KUFUATA BAADA YA KUBATIZWA?
MTI WA MLOZI ALIOONYESHWA NABII YEREMIA 1:12 TAFSIRI YAKE NI NINI?
Hesabu 19:1 “Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2 Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake”;
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa VAZI LILILOCHOVYWA KATIKA DAMU, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.”
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
Sasa Roho Mtakatifu anajua kabisa hatuwezi kumtumikia Mungu katika hali hiyo ya utumwa wa Kesho itakuwaje! Kwasababu hiyo basi ni lazima ampitishe katika kipindi fulani cha madarasa, kuipunguza hiyo hofu ndani ya Mtu ili aweze kuishi kwa furaha akiwa ndani ya Yesu.
Hebu fikiria mwanao, anakaa nyumbani mwako, halafu anakwenda shule huku anamashaka kwamba Kesho anaweza asipate chakula nyumbani, au akiwa na mashaka kwamba atakosa ada! Je! Huyo mtoto atasoma kweli, au atafanya vizuri darasani? Ni wazi kuwa hatasoma bali atakuwa ni mtu tu wa mawazo siku zote! Na itamsababishia kufeli, na hivyo hivyo Mawazo ya Maisha haya na mawazo ya Kesho itakuwaje! Itatusababishia tusimwelewe Mungu na kutusababisha tufeli mitihani mingi ya Maisha yetu ya kikristo.
Kulitatua hilo Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake masomo kadhaa, ya kutohofia Kesho, na hivyo kwa masomo hayo pia anatufundisha na sisi…Embu tusome tukio hili moja..
Mathayo 16:5 “Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate.
6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.
7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.
8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate?
9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota?
10 Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota?
11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.
12 Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo”
Somo hilo Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi baada ya Wanafunzi wake kusahau kubeba mikate ya safari yao..Hivyo walipofika njiani, Bwana Yesu akawaambia wajihadhari na chachu ya mafarisayo, wenyewe wakadhani anawashutumu kwanini hawakubeba mikate katika safari yao..na hivyo hawana kitu cha kula, kwamba Bwana kawakataza wasile chachu ya mafarisayo…(kumbuka chachu ni hamira, na chachu ilikuwa inawekwa kwenye mikate, hivyo mtu akizungumzia chachu ilikuwa inajulikana kwamba anazungumzia mikate yenye Hamira)..
Hivyo wanafunzi wakahuzunika sana, kwasababu watakwenda kukaa na njaa bila chakula huko wanakokwenda…Lakini Bwana Yesu aliwakemea na kuwaambia wana Imani chache…kwasababu wameshasahau jinsi gani Bwana alifanya miujiza ya kutokeza maelfu ya mikate kutoka katika mitano tu na maelfu ya watu wakala na kusaza na kukusanya mabaki mengi tena mara mbili… kama Mungu aliweza kufanya hivyo huko nyuma kwanini asiwafanyie tena hivyo huko mnakokwenda?? Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Bwana! Wasianze kutafakari tafakari Kesho wakula nini? Kesho kutwa watavaa nini…wao kazi yao ni kuangalia mbele kuitenda kazi ya Mungu na hayo mengine watazidishiwa…
Tunaona tena mahali pengine Bwana Yesu alizidi kulitilia mkazo jambo hilo katika Mathayo Mlango wa 6
Mathayo 6: 24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”
Unaona! Bwana anatufundisha ni jinsi gani, Kesho yetu ipo mikononi mwake, kwamba haijalishi leo sina chochote lakini Kesho nitakuwa na kitu..Bwana hawezi kutupungukia kabisa ikiwa tu tupo katika kusudi lake, anasema hivyo katika Neno lake (Waebrania 13:5), anajua tuna haja ya chakula, mavazi, malazi, makazi n.k lakini anachotutaka ni sisi kumtafuta kwanza yeye..Tusiwe na hofu ya Kesho..Kwasababu Hofu ni utumwa, hakuna mtu yeyote mwenye hofu, akapiga hatua yoyote mbele, hakuna.
Tatizo lililopo tunataka pindi tu tunapomkaribisha Yesu Maishani mwetu, basi atupe ratiba ya leo, Kesho na miaka mitano au kumi mbele itakuwaje! Tunataka tuone Kesho tutakuwa na shilingi ngapi mifukoni mwetu, uhakika wa kila kitu…Mungu si wakati wote anatenda kazi hivyo, wakati mwingine unaweza kukupitisha katika ukame leo, na huku hujui Kesho utakuwaje na ghafla ukashangaa kafungua mlango Kesho ukapata unayohitaji tena na zaidi ya matarajio yako…
Hivyo yeye anataka tu tumwamini kwamba hatatuacha kabisa! Anafahamu tunayohitaji!
Kama unafanya shughuli yoyote ambayo inakupatia kipato, na ikatokea ukapungukiwa kabisa, anatakiwa umwamini kuwa hajakuacha, na wala hana mpango wa kukuacha!..kumbuka wakati fulani nyuma ambapo ulipitia kupungukiwa na akakufungulia mlango kimiujiza…ukumbuke huo muujiza, na usikie sauti yake leo moyoni mwako ikikuambia…HUJAFAHAMU TU?..Haujafahamu bado?..Siku ile ulipopungukiwa na akakufungulia mlango kimiujiza?..Yatafakari matendo yake ya nyuma kisha Uinyanyue Imani yako kwake..na siku zote utaishi Maisha ya furaha na yasiyo na hofu, ukijua kuwa Baba yako wa Mbinguni, sio Baba wa kambo, ni Baba wa damu kabisa ambaye hapendi kuona utakufa njaa wala kuteseka.
Maombolezo 3:36 “Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa”.
Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada nyinginezo:
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
SI SHETANI BALI NI WEWE. (CHAGUA MEMA)
Hii ni moja ya ndoto inayootwa na watu wengi, ikiwa na wewe ni mmojawapo na inajirudia rudia mara kwa mara basi fahamu kuwa lipo jambo ambalo Mungu anataka kukukumbusha, Sikuzote meno yanafanya kazi mbili kuu, ya kwanza ni kumeng’enya na ya pili ni kung’ata,..asilimia kubwa ya viumbe vyote vinatumia meno kwa kazi mojawapo ya hizo, isipokuwa tu mwanadamu inaongezeka nyingine hapo, ambayo ni kuzungumza, mtu usipokuwa na meno huwezi kuzungumza, atatoa sauti tu zisizoeleweka…
Vilevile Mtu Ukipoteza meno huwezi kula vitu vigumu, wala huwezi kung’ata kitu chochote Na ndio maana mtu unapoota meno yake aidha ya juu au ya chini au magego yanang’oka halafu ghafla ukashtuka saa hiyo hiyo na kujiona yupo salama huwa anashukuru kweli, anasema afadhali imekuwa ndoto, ni kwasababu unajua thamani iliyo katika meno yake.
Sasa ukiota meno yanatoka Hapo ni Mungu anakukumbusha, kuwa unakaribia kupoteza Meno yako ya rohoni, yenye thamani kubwa zaidi ya haya ya mwilini, ikiwa hujaokoka basi nakushauri utubu haraka sana, umegukie Mungu wako, kwasababu mara kikipotea hicho basi fahamu kuwa kitapotea milele…Ukishaondolewa uwezo wako wa kupambanua na kuyaelewa mambo ya rohoni basi hutakaa uwe nao tena, ukishaondolewa uwezo wako wa kung’ata maadui zako wa rohoni kwa meno makali Mungu aliyokupa basi fahamu utabakia hivyo milele, Vilevile Ukishaondolewa uwezo wa kuzungumza na Mungu wako rohoni basi ndio utabakia hivyo milele na milele hatakaa akuelewe wewe, hiyo inamaanisha hata ukiomba dua yao hawezi kukusikia…Na hiyo yote ni kwasababu ya dhambi zako unazozitenda sasa hivi.
Zaburi 58:3 “Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka; Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.
5 Asiyeisikiliza sauti ya waganga, Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
6 Ee Mungu, UYAVUNJE MENO YAO VINYWANI MWAO; Ee Bwana, uyavunje magego ya wana-simba.
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu”.
Ndugu Usiipuuzie Injili ya msalaba hata kidogo, inapohubiriwa mbele zako, Mungu ameona jambo hilo kwako na hivyo anakuonya kwasababu anakupenda, mgeukie muumba wako, anza kuzingatia Neno lake kile anachokuambia tii na yeye mwenyewe atakuokoa na kukulinda na kukuongoza hadi unyakuo.
Aidha kama wewe tayari upo ndani ya Kristo, na unaota ndoto za namna hiyo hapo Mungu anakuonyesha pia ni jinsi gani unaelekea kupoteza ule uwezo wako wa thamani uliokuwa nao wa kupambanua mambo ya rohoni na ukali wako, hivyo simama imara kama ulikuwa umeshaanza kuyumba yumba, au kupoa simama imara ili usije ukabakia kuwa mbwa bubu tu asiyeweza hata kubweka rohoni (kukemea dhambi )kwa kukosa meno.
Isaya 56:10 “Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
12 Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi”.
Zingatia hayo na Bwana hakika atakuwa na wewe katika kila hatua moja unayopiga kwake…Hizi ni siku za mwisho na Unyakuo wa kanisa upo karibuni, tengeneza mambo yako.
Ubarikiwe.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?
Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa asilimia kubwa ya ndoto tunazoota kila siku au mara kwa mara huwa zinatokana na mawazo yetu wenyewe, naweza kusema hata asilimia 95 ya ndoto zote tuziotazo usiku hutokana na sisi wenyewe, na hizo zinakuja aidha kwa shughuli tunazozifanya kila siku au mazingira yanayotuzunguka au kitu tunachokiwaza sana…
Hivyo ndoto kama hizi, huwa hazibebi ujumbe wowote wa rohoni, ikitokea umeota wewe zipuuzie tu vinginevyo utajikuta unachanganyikiwa ukidhani kuwa kila ndoto unayoota ina maana, ikiwa bado hujaweza kuzitofautisha aina za ndoto katika makundi yake basi pitia kwanza somo hili ili upate msingi kisha tuendelee. >>>NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?
Lakini kama ndoto unayoota haihusiani na mazingira uliyopo, na huwa inajirudia mara kwa mara, basi lipo jambo ambalo Mungu anataka kukuonyesha hapo.
Sasa Kuota unaendesha gari na wakati mwingine umewapakiza watu nyuma, ni ishara kwamba wewe mwenyewe unayaongoza maisha yako au maisha ya wengine, kukufikisha mahali Fulani au kuwafikisha mahali fulani..Kama wewe umeokoka na unalifanya kusudi la Mungu au unaifanya kazi ya Mungu basi zidisha mwendo katika safari yako kwasababu lengo lako utalifikia, kama hutapunguza mwendo kama alivyofanya Yehu, pale alipokuwa anakwenda kumuua Yule mfalme muasi Yoramu na mama yake Yezebeli waliowakosesha Israeli mpaka kupelekea wakaingia kwenye uchawi na ibada za sanamu, na Kumkasirisha Mungu kwa viwango vya juu sana.
2Wafalme 9:20 Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Amewafikilia wala harudi tena; na mwendo huu ni kama mwendo wa Yehu mwana wa Nimshi; MAANA ANALIENDESHA GARI KWA KASI.
Hivyo kama unalo kusudi la Mungu mkononi mwako,litimize bila kuogopa kipingamizi au mitazamo ya watu..
Lakini pia,
unapaswa uwe makini ni gari la aina gani unatumia kuliendesha kusudi la Mungu wakati Fulani mfalme Daudi alikuwa analitoa sanduku la Mungu kutoka kwa Abinadabu kwenda Yerusalemu, lakini alifanya makosa kuwatumia ng’ombe kama usafiri wa kulisafirisha kusudi la Mungu badala ya kutumia watu tena makuhani ambao ndio Mungu aliowaagiza walibebe wakati wote, wao wakawaweka ng’ombe kama magudurumu ya gari lao na ikapelekea kifo cha mtu mmoja..soma 1Nyakati 13:7
1Nyakati 13:7 “Hivyo Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio WAKALIENDESHA LILE GARI.
8 Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.
9 Hata walipofika penye uga wa Nakoni, Uza akaunyosha mkono wake alishike sanduku; kwa maana wale ng’ombe walikunguwaa.
10 Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu.
Hivyo uwe makini unapolifanya kusudi la Mungu na wale unaowaongoza, zingatia vigezo cha maandiko . Na ndio maana wengine wanaota wanaendesha vyombo tofauti tofauti , wengine wanaota wanaendesha malori, wengine wanaota wanaendesha baiskeli, wengine wanaota wanaendesha pikipiki n.k. Vyovyote vile, kuendesha ni kuendesha tu, hiyo ni kulingana na kusudi Mungu alilokupa cha msingi hapo ni kutimiza kusudi hilo kwa ukamilifu wote, ili uepuke kulaumiwa huko mbeleni.
Lakini kama unajijua wewe bado ni mwovu na hadi sasa upo katika dhambi, Hiyo ni Ishara mbaya sana kwako, Aidha Unajiongoza mwenyewe katika mauti au unawaongoza wengine katika mauti, au vyote viwili kwa pamoja..
2Nyakati 21:12 “Likamjia andiko kutoka kwa Eliya nabii, kusema, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa sababu hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda;
13 lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, UKAWAENDESHA KATIKA UASHERATI Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe;
14 tazama, Bwana atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote;
15 nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku.
Unaona hapo huyu mfalme Yehoramu, alikuwa mtu mwovu, alikuwa ni muuaji, na mwabudu sanamu, akawafanya na Israeli wote wote wawe kama yeye, au kwa lugha nyingine akawaendesha waisraeli mpaka kwenye uasherati wa kiroho, kwa sababu hiyo basi Mungu akampiga kwa mapigo yale..
Hata na wewe, unayaongoza maisha yako sasa ukidhani kuwa upo salama, lakini mwisho wake utakuwa ni mauti kama hutatubu, unawasababishia wengine mauti wale walio chini yako, au wanaokutegemea, au wanaokutazama kwa mwenendo wako na maisha yako..
Hivyo Bwana anakupenda na ndio maana anakuonya Leo hii, Utubu umgeukie yeye, ili uliendeshe gari la maisha yako katika njia sahihi ya kutimiza makusudi ya Mungu na sio makusudio ya Shetani.
Ubarikiwe.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.
Kila mwanadamu atafikia ukomo wa siku zake, (yaani siku ya Mauti yake)..Lakini kabla ya siku yenyewe ya kuondoka ulimwenguni haijafika…Kinakuwepo kipindi fulani kifupi ambacho kinaweza kuwa ni miaka 10, au 5 kabla ya kuondoka kwako, au kinaweza kuwa mwaka mmoja au mwezi mmoja au wiki moja….Kipindi hicho kifupi ndicho kinachojilikana kama SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WA MTU.
Katika kipindi hicho, Kuna hali fulani mtu anakuwa anaanza kuipitia, mara nyingi inakuwa ni kumbukumbu ya mambo yaliyopita nyuma, ndio utakuta mtu anaanza kukumbuka mambo yake yote ya nyuma aliyoyapitia na jinsi alivyoyaishi, kipindi hichi sio kipindi kizuri kwa Mtu ambaye hakuwa ndani ya Kristo, kwasababu ni kipindi cha mashaka mazito, mara nyingi kwa mtu ambaye hajampa Kristo maisha yake huko nyuma, ni ngumu sana kushinda hali atakayopitia wakati wa hiki kipindi. Wengi wanaishia kujiua.
Ndio maana Biblia ikasema katika Mhubiri.
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”
Umeona hapo? biblia haisemi mkumbuke muumba wako wakati wa siku zilizo mbaya..Hapana! bali inasema mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijakaribia siku zilizo mbaya…Siku zilizo mbaya zinazozungumziwa hapo ndio hizi SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WAKO.
Siku hizo ni ngumu kumrudia Muumba wako, kama katika siku za ujana wako ulikuwa unaichezea Neema, na kumbuka pia siku za ujana sio tu siku za miaka ya ujana kama vile miaka 15-45 hapana..bali siku za ujana ni siku ambazo ulikuwa unauwezo wa kumgeukia Mungu, na mazingira yote yalikuwa yanakuhimiza kufanya hivyo lakini hukutaka!
Hivyo huu sio wakati wa kuzunguka huko na huko mitandaoni na mitaani kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayopita, huu ni wakati wa kutafuta wokovu kwa nguvu zote. Biblia inasema Ufalme wa Mbinguni unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu ndio wauteka..Je! wewe nguvu zako unazipeleka wapi sasa katika ujana wako? katika ulimwengu au kwa Yesu?..Kama ni katika ulimwengu basi tambua kuwa SIKU ZA KUFA KWAKO ZINAKARIBIA na katika siku hizo, hazitakuwa siku za furaha bali huzuni.
Daudi aliziona siku zake na alikuwa na furaha..akafurahi akamwusia mwanawe kuzifuata njia za Bwana.
1Wafalme 2:1 “Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,
2 Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume;
3 uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;”
Yakobo naye aliziona siku za kufariki kwake akafurahi, akawabariki wanawe…
Na siku hizo zinakuja kwako mimi na wewe! Umejiandaaje?..je zitakuja na huzuni au furaha kwako?
Tubu mgeukie Kristo sasa, angali mlango wa Neema bado upo..Angali u kijana.Na Kristo atakupa tumaini la maisha ya sasa, na yale yajayo!
Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?
Hakukuwa na mtu mmoja maalumu aliyefika mwezini, kulingana na Sayansi…Waliofika mwezini ilikuwa ni TEAM ya watu watatu (Neil A. Armstrong, Michael Collins na Edwin E. Aldrin Jr.) Hao ndio waliokuwa ndani ya chombo cha Kwanza kulichotua mwezini, na wote watatu walikuwa ni wa-Marekani na safari yao iliyojulikana kama Apollo 11. Safari yao ilichukua siku 8 na masaa 3..Kwenda na kurudi, Na hiyo ilikuwa ni Mwaka 1969.
Sasa kumbuka tukio lolote linaloendelea duniani, linafunua tukio fulani linaloendelea katika roho.
Kama wanadamu wamefikia hatua ya kutengeneza chombo ambacho kimewafanya wafike juu zaidi ya mawingu, na kutua Mwezini. Kadhalika kuna kitu pia kinaendelea kutengenezeka sasa katika roho, ambapo itafikia kipindi kitakamilika, na hicho kitalifanya kanisa kupaa juu sana zaidi ya mawingu na zaidi ya mwezi na kulifanya lifike mahali panapoitwa Mbinguni.
Na kama tunavyoona hiyo safari ya kwenda mwezini ilihusisha watu wachache sana, kadhalika, safari ya kwenda mbinguni itahusisha watu wachache sana, kwasababu biblia inasema mlango ni mwembamba na njia imesonga ielekeayo uzimani..
Hivyo ndugu, huu ni wakati wa kuingia ndani ya Kristo, kwani injili sasa inahubiriwa na teknolojia tunazoziona, Hizi ni zile siku za mwisho ambazo biblia imesema maarifa yataongezeka…Na tunaona jinsi yanavyoongezeka kwa Kasi, na katika roho pia yanaongezeka, watu wa Mungu hivi karibuni watafikia Imani ya kunyakuliwa na hivyo kuondoka kwenda mbinguni kwa Bwana..Je! na wewe utakuwa miongoni mwao?
Jibu unalo, tubu mpe Kristo maisha yako na uishi maisha yanayopatana na Toba yako.
Bwana akuabariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?
Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha pengine umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye n.k.
Kibiblia kuna upendo wa aina tatu:
UPENDO WA KWANZA NI UPENDO UNAOTOKANA NA HISIA:
Upendo huu unajulikana kama “EROS” Ni upendo unaozaliwa na hisia, Upendo huu ni maarufu sana kwa mke na mume, katika biblia Sulemani alijaribu kuuleza upendo ya namna hii:
Wimbo 1:13 “Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi”.
Huu ni Upendo ambao hauwezi kufananishwa na upendo kama wa mtu na ndugu yake au Rafiki yake.
AINA YA PILI YA UPENDO NI UPENDO UNAOZALIWA KWA VITU VINAVYOENDANA:
Unajulikana kama “PHILEO”. Upendo huu unazuka kutokana na mahusiano Fulani mtu mmoja alionao na mwenzake, anaweza akawa ni ndugu, au rafiki, au mchezaji mwenzake, au mfanyakazi mwenzake. Ni upendo ambao kusipokuwa na mahusiano Fulani ya karibu au faida Fulani ambayo mtu anaweza kuipata kwa mwenzake, hauwezi kuzaliwa.
Tunapaswa tupendane sisi kwa sisi, biblia inatuambia hivyo katika (1Yohana 2:9-10), vilevile inatuambia tupendane sisi tulio ndugu katika Bwana, lakini upendo wa namna hii haupo tu kwa waaminio bali hata kwa watu waovu pia wanao..Bwana Yesu alisema:
Mathayo 5:46 “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo”?
Unaona kwahiyo upendo huu bado hujafikia vile viwango vyenyewe.
AINA YA TATU YA UPENDO NI UPENDO USIO NA MASHARTI. UNAOJULIKANA KAMA “AGAPE” (UPENDO WA KI-MUNGU).
Huu ndio upendo Yesu Kristo aliokuwa anauzungumzia, ni upendo unaompenda mtu bila ya sababu yoyote, Ni upendo wa kiwango cha juu sana, unampenda mtu kwa kutokujali kama na yeye anakupenda au hakupendi, kama anakuchukia au hakuchukii, kama anakusema vibaya au hakusemi vibaya, kama anafaida yoyote kwako au hana faida yoyote kwako.
Upendo huu ndio YESU alikuwa nao kwetu, biblia pale inaposema “alitupenda Upeo”(Yohana 13:1), ilimaanisha kusema hivyo Alitupenda upeo kweli kweli, sio kwasababu tulikuwa ni watakatifu, au kwasababu tulikuwa waovu…au kwasababu alikuwa anatafuta ukubwa kwetu hapana, alitupenda tu, tena ile wa kutoka moyoni hadi kufikia hatua ya kuutoa uhai wake kwa ajili yetu.
Kama ilivyoelezwa katika makala haya, https://www.swisswatch.is/product-category/tag-heuer/grand-carrera/ unaweza kuvinjari chaguo lako la ofa zinazopatikana kwenye simu mahiri na chapa maarufu na uchunguze mipango ya huduma inayokidhi mahitaji yako.Na upendo wa aina hii ndio Bwana anataka kila mmoja wetu awe nao, Ni ngumu kuufikia, hususani pale tunapoona mtu Fulani anayetuchukia au anatuzungumzia vibaya halafu huyo huyo ndio tunapaswa tumpende, kuna kama ugumu fulani..Lakini Huo ndio Mungu anataka kuuona kwetu haijalishi tutawapenda wake zetu na waume zetu kiasi gani, au ndugu zetu wengi kiasi gani au rafiki zetu wengi kiasi gani kama hatujaweza bado kuufikia huu upendo wa AGAPE, mbele za Mungu bado hatuna upendo..
Hizi ndizo tabia za upendo wa AGAPE.
1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
Hivyo ili mimi na wewe tuweze kuufikia Upendo wa namna hii hatupaswi kuungojea kama hizo aina mbili juu, bali tunapaswa tuupapalilie kwa kuvumilia, kwa kutokurudisha baya kwa baya, kwa kutokusengenya, kwa kutokuhesabu mabaya ya mtu tu sikuzote, kuwaelewa watu ..n.k.
Tuombe Mungu atusaidie sote tufike hapo, kwasababu hapo ndipo Mungu mwenyewe alipo, na hiyo ndio inayojulikana kama karama iliyo kuu kuliko zote. Ukiwa nayo hiyo wewe ni zaidi ya nabii yoyote, au mwalimu yoyote, au mwinjilisti yoyote, au mtume yoyote duniani. Mungu anakuwa karibu sana na wewe.
Ubarikiwe sana.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.
Shalom, mtu wa Mungu karibu tujifunze Biblia pamoja..
Wapo wanaodhani kuwa hakuna kuokoka duniani! lakini nataka nikuambie wokovu ni hapa hapa duniani..Mbinguni ni matokeo ya wokovu wetu.
Biblia inasema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu, Na kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu..Hivyo tukijifunza ni vitu gani vilikuwa vinaendelea muda mchache kabla ya Matukio hayo mawili ya kuangamizwa dunia, tunaweza kuelewa ni mambo gani yatatokea katika siku za kuja kwa Kristo mara ya pili.
Tukio la kipekee tunaloweza kuliona kabla ya Moto kushuka sodoma na gomora ni namna watu walivyookoka…Yapo matukio mengi lakini leo tutalizungumzia hili moja.
Biblia inasema.
Mwanzo 19: 12 “Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;
13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu.
14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. LAKINI AKAWA KAMA ACHEZAYE MACHONI PA WAKWEZE.
15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu”.
Tunasoma hapo, kabla ya gharika, kuna injili ya haraka haraka ilipita…Lutu aliambiwa akawaambie ndugu zake watoke mjini kwasababu mji unakwenda kuangamizwa, na laiti kama hao ndugu zake wangesikia, kila mmoja angeogopa na kwenda mbio kuwaambia ndugu zao wengine wa mahali pengine…na hao ndugu wengine wangewaambia wengine…Hivyo kwa kipindi kifupi watu wengi sana wangeokoka…laiti watu wangekuwa na masikio ya kusikia maonyo na kuwa hofu ya Mungu, hata baada ya hukumu ile kutamkwa bado kungekuwepo na nafasi ya KUOKOKA!..Lakini hata huo mlango mdogo wa Neema watu waliupuuzia na hivyo kusababisha kuangamizwa wote.
Na kama pia ukichunguza wakati wa Gharika, Nuhu hakuokoka peke yake, bali aliambiwa akawakusanye watu wa jamaa yake yote…Ni wazi kuwa naye pia alikwenda kuwaambia mambo yale yale…lakini inawezekana naye pia alionekana kama anacheza! Ndio maana akaishia kuingia safinani yeye na wanawe tu, kama Lutu alivyookoka yeye na wanawe!
Mwanzo 7:1 “Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki”.
Mwanzo 7: 5 “Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.
6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.
7 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”
Ndugu nafasi hii ndogo Mungu anayoitoa baada ya hukumu kutamkwa sio ya kwenda kutenda mema, hapana! ni nafasi ya kuokoka!! Hukumu imeshatamkwa..haiwezi kugeuzwa ni lazima ije tu kama ilivyotamkwa! Ni nafasi ya kuukimbia ulimwengu na kuingia safinani, hivyo hivyo kama ulivyo….Ni wakati wa kuikimbia sodoma na gomora ukiwa hivyo hivyo ulivyo…Usiende kumuaga mtu! Wala usiende kumwuliza baba yako au mama yako je! Natakiwa kuokoka? Ondoka sodoma kama ulivyo! Wewe kama wewe…wokovu unaanzia hapo hapo sodoma ulipo! kwasababu hukumu imeshatamkwa…Watoto wa Nuhu haikuhitaji utakatifu mwingi kupata nafasi ya kuingia safinani?..hawakuwa wakamilifu na ndio maana unaona baada ya kutoka safinani, Hamu aliuona uchi wa Baba yake…Lakini walitii injili ndio maana wakaokoka! tu Injili ya Nuhu ya mwisho ya kuokoka! Basi! Kulikuwa hakuna muda tena wa Mungu kusikiliza maombi ya watu…kulikuwa na mambo mawili tu! Aidha kuingia safinani uokoke au kubaki duniani uangamie.
Ukishaingia safinani tayari umeokoka! Hata kama mafuriko hayajaja!
Na siku za mwisho karibia na kuja kwa Yesu ndio injili ndio hiyo inahubiriwa na Roho Mtakatifu, hatuwezi kukaa na kumwomba Mungu kwamba asiiangamize dunia! Alishasema siku ya maangamizi itakuja ni kweli itakuja! Hakuna atakayeweza kubadilisha hilo… Na hivyo zipo chaguzi mbili tu mbele yetu! Kubaki ulimwenguni kuangamia au kuingia safinani kupona! Safina ni Bwana Yesu.
Kama unataka kuokoka na maangamizi..unamfuata Bwana Yesu ukiwa mwenye dhambi kama ulivyo wokovu ni hapa hapa duniani…haihitaji utakatifu kumwamini Yesu…Kwasababu kilichopo mbele ni kifo..Ukimwamini Yesu na kutubu moja kwa moja unapata nafasi ya kuingia safinani..na utakuwa umeokoka na maangamizi, kwasababu huwezi kuokoka mahali ambapo hakuna maangamizi!..Kisha baada ya hapo wewe mwenyewe atakuongoza katika utakatifu na ukamilifu wote,..wewe unachopaswa kufanya ni kuanzia huo wakati kutokuangalia nyuma tu,
Je! Upo safinani?…Umeitii Injili ya Roho Mtakatifu inayotuonya tujiepushe na ulimwengu?
Bwana akubariki
Mada Nyinginezo:
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?