Biblia inatufundisha kuwa Mazungumzo mabaya ndiyo yanayoharibu tabia njema ya mtu.
1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”.
Maandalizi ya dhambi karibia zote yanaanzia katika “mazungumzo”.. wanaopanga kuua wanaanzia na mazungumzo, wanaopanga kuiba wanaanzia katika mazungumzo, hali kadhalika wanaopanga kufanya zinaa na uasherati wanaanza na mazungumzo.
Kwahiyo kama mtu wa Mungu jiangalie sana aina ya mazungumzo yako hali kadhalika na mtu unayezungumza naye.
Yusufu alijua siri ya mazungumzo na hiyo ikamsaidia kushinda dhambi ya “zinaa”. Kwani maandiko yanasema Yusufu hakukubali kulala na mke wa Potifa na hata KUZUNGUMZA NAYE!
Mwanzo 39:7 “Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, WALA AONGEE NAYE”.
Wengi tunaishia hapo kuwa Yusufu alikataa kulala naye.. lakini biblia inatuonyesha kuwa alikataa pia KUONGEA NAYE..
Huu ni mtego ambao shetani anawanasa wengi katika siku hizi za mwisho, utakuta mtu anajisifia hawezi kuanguka, lakini ni mtu aliejaa mazungumzo na jinsia nyingine kwa kiwango kikubwa!, ni mtu wa mizaha na utani na wa maneno maneno…hawezi kukaa bila angalau kuanzisha mazungumzo yasiyo na maana na mwingine, hawezi kutulia asipochati na mtu mwingine..
Hapo ni ngumu kushinda dhambi ya zinaa, au dhambi nyingine yeyote… Kwasababu biblia imeshasema kuwa, mazungumzo mabaya ndiyo yanayoharibu tabia ya mtu! (1Wakorintho 15:33), haihitaji maelezo mengi!
Ni lazima tu utaharibikiwa tabia ukiwa ni mtu wa mazungumzo mazungumzo yasiyo na maana… hususani na watu ambao bado hawajamjua Mungu.. na watu wa jinsia nyingine.
Chunga mdomo wako, kama unaipenda tabia yako!
Maran atha
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
JIHUDHURISHE, ILI AANZISHE MAZUNGUMZO NA WEWE
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE
Amri za kwanza Mungu aliziandika juu ya mawe aliyoyachonga yeye mwenyewe, lakini mawe yale ambayo juu yake amri 10 yalivunjwa vunjwa na Musa wakati ule ule aliposhuka kutoka mlimani…
Kutoka 31: 18 “Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu”
Baadaye Mungu akamwambia Musa achonge, mbao nyingine mbili za mawe mfano wa zile za kwanza zilizochongwa na Mungu mwenyewe..Na Musa alipochonga aliwapa wana wa Israeli…
Kutoka 34:1 “Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, hizo ulizozivunja”.
Mbao hizi za pili nazo hazikudumu muda mrefu, kwamaana alipokuja Mfalme Nebukadreza alivunja sanduku na kuzipoteza kabisa,.na kukawa hakuna tena sanduku la ushuhuda ambalo ndani yake mna mbao hizo za mawe zilizobeba Amri za Mungu.
Lakini baada ya miaka Mingi kupita Bwana Mungu akarudia tena kuziandika amri hizo kwa mara nyingine ya mwisho, lakini safari hii si katika mwamba aliouchonga yeye kwa vidole vyake, wala si katika mwamba uliochongwa na Musa, BALI KATIKA MOYO WA MTU.
Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; NAMI NITAKUWA MUNGU WAO, NAO WATAKUWA WATU WANGU.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Umeona? Kumbe agano jipya linahusu Moyo!.. Maana yake hatuhitaji tena kwenda Yerusalemu kuzisikia amri, wala sharia wala maagizo ya Mungu, bali tunapomwamini Yesu zile sharia zinaandikwa ndani yetu na kidole cha Mungu mwenyewe.
Na matokeo ya sharia, na amri za Mungu kuandikwa ndani ya mioyo yetu, maana yake muda wote zitakuwa zinabubujika na hivyo hakuna haja ya mtu kukufundisha kuzishika amri, zenyewe tu zitakuwa zinabubujika ndani yako.. kama maandiko yanavyosema hapo katika mstari wa 34…. “Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana”.
Hiyo ndio sababu kwanini watu waliompokea Yesu kikweli kweli na kujazwa na Roho wake Mtakatifu, haihitaji kuwaambia wala kuwakazania kuwa ulevi ni dhambi, au uvaaji mbaya ni dhambi.. Tayari sheria ipo ndani yao, hata pasipo kuambiwa na mchungaji,… ndani ya mioyo tayari kuna mahubiri yaliyoandikwa na kidole cha Mungu mwenyewe yanayowaambia kuwa si sawa kufanya baadhi ya mambo. Hayo mahubiri haihitaji wasafiri mbali kwenda kuyatafuta, tayari yanakuwa yameandikwa ndani yao, haihitaji kuwakumbusha kusali, tayari hayo mahubiri yapo ndani yao, haihitaji kuwakumbusha kwenda ibadani, tayari hayo maagizo Bwana kayaandika ndani yao, hivyo daima yanabubujika.
Kumbukumbu 30:11 “Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali.
12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya?
13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?
14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na MOYO WAKO, upate kulifanya”
Lakini maandiko hayo hayawezi kuandikwa ndani ya moyo wa mtu, kama mtu huyo hajafungua moyo wake kwa kumwamini Yesu na kumkiri kwa kinywa, vile vile kwa kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, pamoja na kubatizwa, kwa maana maandiko yanasema hivyo..
Warumi 10:6 “Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini),
7 au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)
8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.
Je sheria za Mungu zimeandikwa ndani yako??
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Mawaa ni nini? Mawaa ni dosari au kasoro iliyo katika kitu, ambayo inapelekea kukifanya kitu hicho kisifae tena, au kikose vigezo.
Kwamfano mtu ambaye ana sifa ya kuwa na uso mzuri halafu, kukatokea jipu shavuni. hapo ni sawa na kusema ana-mawaa. Jipu lile limeuharibu uzuri wake.
Au ukinunua bati la kuwekeza kwenye nyumba yako, halafu ukaona tobo katikati ya bati hilo, tayari lina mawaa, halifai kwa ujenzi. Au shati jeupe halafu likawa na doa dogo jeusi, huo ni mfano wa mawaa, halifai kwa kuvalika.
Vilevile rohoni na sisi pia hatupaswi kuonekana na mawaa ya aina yoyote, Kwamfano katika vifungu hivi; Mungu anatarajia kanisa lake alilolikomboa kutoka katika dhambi lisionekane na mawaa (dosari yoyote) ndani yake
Wakolosai 1:21 “Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama”
Hivyo wewe kama mkristo uliyeokoka, ni lazima ujue kuwa una wajibu wa kuishi maisha ya utakatifu na ukamilifu, usiseme nimeokolewa kwa neema Yesu alishayamaliza yote, Hivyo unaenda kama utakakavyo, anaitenda kazi ya Mungu huku unaishi na mke/mume ambaye si wako. Wewe una mawaa, na hivyo mbingu huwezi kuiona.
Au unatoa zaka, unaimba kwaya, ni kiongozi wa vijana, na huku unatazama picha za ngono mtandaoni, hapo una-mawaa, Unafunga na kusali, unadumu hekaluni usiku na mchana na huku unakula rushwa kazini kwako. Hapo ndugu una-mawaa.
Hivyo hatuna budi kuwa kanisa la Kristo kwelikweli Bwana analolitazamia lisilo na mawaa wala lawama, wala kunyanzi. Ndivyo tutakavyopokewa kuingia katika uzima wa milele.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi
1Timotheo 6:13 “Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Yohana 1:27 “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”.
Soma pia
Waebrania 9:14, 2Petro 2:13
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka, kama la! Ni nini unachosubiria mpaka sasa, una habari kuwa parapanda inakaribia kulia, Yesu anarudi? Dalili zote zimeshatimia? Fikiri akikukuta katika hali hiyo utamweleza nini? Angali ukweli umeshaujua? Embu tubu leo dhambi zako, mgeukie Kristo, azioshe, akupe uzima wa milele bure.
Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo akupe uzima wa milele bure, basi fungua hapa ili uweze kupata mwongozo wa sala hiyo. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.
Katika maandiko hakuna vifungu vya Moja Kwa Moja vinavyorekodi tukio la Bwana Yesu kunena Kwa lugha.
Lakini Kwa ufahamu wa Rohoni tuliopewa twajua kuwa ni wazi Yesu alinena Kwa lugha. Kutokurekodiwa Kwa tukio hilo hakumaanishi kuwa hakuwahi kunena Kwa lugha, kwasababu maandiko yanasema yapo mambo mengi aliyoyafanya Yesu kama yangeandikwa hata vitabu vyote duniani visingeweza kutosha, Kwa wingi wa habari zake.(Yohana 21:25)
Hivyo si Kila tukio la Bwana Yesu limeandikwa kwenye biblia.
Halikadhalika Ifahamike kuwa taaarifa za kunena Kwa lugha aliyezieleza kwa mara ya kwanza Kwa mitume ni Bwana Yesu.(Hawakufunuliwa baadaye) Hivyo hawezi kuwaambia watu jambo ambalo yeye mwenyewe halipo ndani yake, au hajawahi kulifanya.
Marko 16:17-18
[17]Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
[18]watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Vilevile Yesu ndiye mwanadamu pekee aliyetiwa mafuta mengi na Roho kuliko mtu yeyote aliyewahi kutokea duniani, (Waebrania 1:9). Zile karama zote za Roho zilikuwepo ndani yake, alikuwa ni nabii, mwalimu, mwinjilisti, mchungaji, mtume, n.k. na karama za uponyaji, miujiza, upambanuzi alikuwa nazo, hivyo hatuwezi kushangaa pia na hii kunena Kwa lugha kuwemo ndani yake.
Kwa kuhitimisha ni wazi kuwa Bwana Yesu alinena Kwa lugha. Hivyo akampendeza kukimwaga kipawa hicho na kwetu pia.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
IJUE FAIDA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA!
YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.
Masomo maalumu kwa wanawake.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Je wewe ni mwanamke? Na unapenda upate kibali mbele za watu?..au je wewe ni binti na unatamani upate ndoa, tena iliyo bora na ya Baraka?, au je wewe ni mwanamke uliyeolewa na unatamani ndoa yako Bwana aibariki na pia upate kibali na heshima Zaidi katika ndoa yako?. Kama ndio basi hakikisha unazingatia mapambo!!..
Katika biblia kuna wanawake waliofanya utafiti wa mapambo yaliyo bora na mazuri na yenye mvuto mkubwa, ili kwamba wawe na mvuto wa heshima mbele za watu, wengine ili wapate ndoa nzuri na kibali kwa wenzi wao..na walipoyatumia hayo mapambo wakafanyika kuwa wanawake bora kuliko wote, na wenye kukubalika kuliko wote.
Wanawake hawa hawakutumia mapambo ya kiulimwengu kama kupaka wanja machoni au kupaka rangi mdomoni ili waolewe au waheshimiwe na waume zao, vile vile hawakuvaa nusu uchi ili wavutie mbele ya wanaowatafuta kuoa, wala hawakusuka nywele ili waonekane warembo, wala hawakupaka rangi katika kucha zao, ili wavutie mbele za watu na kupata ndoa, lakini walitumia mapambo ya aina nyingine na hayo hakawapa ndoa wanazozitafuta, yakawapa heshima wanayoitafuta, yakawapa kibali wanachokitaka n.k.
Na mapambo hayo ni yapi…..?
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, ILIYO YA THAMANI KUU MBELE ZA MUNGU.
5 MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote”.
Nataka tuuangalie huo mstari wa 5 unaosema “MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI”..
Kwahiyo kumbe zamani kulikuwa na wanawake “watakatifu” na “wasio watakatifu”. Na kila kundi lilikuwa na aina yake ya mapambo ili lipate kibali na kuvutia.
Na hapa biblia inatufundisha wanawake wa zamani waliokuwa watakatifu ijapokuwa katika masomo yao kulikuwa na vipodozi vingi, kulikuwa na rangi nyingi za kucha, na za uso na za mdomoni, lakini wao kwa ufunuo waliokuwa nao hawakuchagua mojawapo wa hayo mapambo, badala yake waliona yana kasoro, hivyo wakachagua mapambo ya ndani ambayo ni UPOLE, HESHIMA, UTII NA UTULIVU.
Wakaona hayo ndio yatakayowafanya waolewe, ndio yatakayowafanya wapendwe na waume zao, ndio yatakayowafanya wapate kibali katika ndoa zao na jamii zao, ndiyo yatakayowafanya waonekane wa thamani, na si kupaka wanja, au kupaka rangi mdomoni, au kujichubua, au kuvaa nusu tupu.
Ndio maana sasa utaona biblia inasema kama vile Sara alivyokuwa mtii kwa Ibrahimu mumewe hata kufikia hatua ya kumwita Ibrahimu “bwana”, Roho hiyo ya unyenyekevu na utii, na utulivu, ndio iliyomfanya Sara awe “mama wa mataifa” na si “wigi kichwani” wala rangi mdomoni, wala hereni sikioni. Kulikuwa na wanawake wengi katika ile nchi, ambao walikuwa wanajiremba na pengine hata kukaribia kufanana na malaika, lakini Ibrahimu hakuwachagua hata mmoja wao!.
Ibrahimu alimchagua Sara kwasababu alikuwa ni mtii, na mtulivu..(alikuwa na mapambo ya ndani)
“5 MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana…”
Vile vile roho ya upole na ya kujisitiri iliyokuwa juu ya Rebeka, ndio iliyomfanya apate kibali kwa Isaka, kiasi kwamba alipofikishwa kwa Isaka, alifunika kichwa chake kwa shela (Mwanzo 24:62-67), ndio iliyomfanya awe mama wa Taifa kuu la Israeli (Yakobo), na si mavazi ya vimini, au ya mgongo wazi,…Na vivyo hivyo wanawake wengine wote watakatifu walitumia mapambo hayo ili kujipatia kibali.
Lakini wale wengine wa kidunia, walitumia mapambo ya nje, yaani.. vipodozi vyote walivyovitaka, waliweka pini katika pua zao, waliweka rangi kwenye kucha na kwenye kope, na midomoni, walipaka wanja machoni, na kupaka hina mwilini na kuweka nywele bandia n.k lakini wengi wa hao waliishia kutamaniwa tu na si kupendwa kama walivyotafuta,
Na wengine waliishia kuonekana kama makahaba, kama Yezebeli, (maana biblia inaonyesha Yezebeli alikuwa ni mwanamke mwenye kupaka uwanja machoni na kupamba kichwa, maana yake kusokota rasta, na kuweka nywele bandia, na ndio maana biblia ikamtaja kama mwanamke kahaba na mchawi soma 2Wafalme 9:22,30, Ufunuo 2:20-22).
Na siku zote mapambo haya mawili hayawezi kwenda pamoja!, ukitumia moja lazima lingine utalikosa…
Ukiwa unapaka uso rangi, unajichubua, unatoboa pua huwezi kuwa na unyenyekevu, utii, utulivu, au mapambo mengine yote ya ndani huwezi kuwa nayo… ni lazima tu utakuwa na kiburi, tamaa, wivu,.
Na vile vile huwezi kuwa mtii, mnyenyekevu, mpole (mapambo yote ya ndani) halafu ukavaa nusu uchi, vimini au nguo za kubana…
Ingekuwa mapambo haya mawili yanaweza kwenda pamoja (yaani ya ndani na ya nje) basi biblia isingesema wanawake wasijipambe kwa “mapambo ya nje”, badala yake ingesema “wasijipambe kwa mavazi ya nje tu pake yake bali pia wajipambe kwa mapambo ya ndani”. Lakini utaona imekosoa moja na kulihakiki lingine, ikiwa na maana kuwa mapambo haya hayawezi kwenda pamoja.
Mama, dada, binti unayetaka kwenda mbinguni?, na unayetaka kupendeza na kupata kibali.. basi zingatia kujipamba kwa mapambo ya ndani na nje jiweke katika hali yako ya asili, uone kama hutapata kazi unayoitafuta, au ndoa, au kibali popote pale uendapo kama ilivyokuwa kwa akina Sara, na wanawake wengine wa kwenye biblia, na Zaidi ya yote pia utaenda mbinguni kwasababu miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na si midoli ya matangazo ya nguo masokoni.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)
SWALI: Maandiko yanasema tusilaani, je! Paulo aliwalaani wagalatia na wakorintho?
Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
1Wakorintho 16:22 Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.
Mtume Paulo alipokwenda katika Galatia na kuwakuta baadhi ya watakatifu wa pale wamegeukia injili nyingine, iliyoletwa na wayahudi, inayosema ili mtu ahesabiwe haki ni lazima amwamini Kristo pamoja na sheria ya Musa, zaidi ya vile mtume alivyofundisha kwamba kinachoweza kumwokoa mtu ni Imani tu katika Kristo!. Sasa alipoona wamefikia hatua hiyo mbaya ndipo aliposukumwa kusema maneno hayo makali kwa wagalatia , kwamba “mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo waliyoipokea kwake, na alaaniwe”.
Lakini ni vema kufahamu kuwa kauli hii na ile ya 1Wakorintho 16:22 imetumiwa vibaya na baadhi ya wakristo kwa vizazi vingi, kwamba kwa ajili ya injili tunaruhusiwa kuweka laana kwa watu. Lakini je! Paulo aliwaalaani watu wale?
Jibu la! Kwasababu kama angekuwa ameruhusiwa kuwalaani maadui na wanaokwenda kinyume na , yeye basi asingesema tena maneno haya ya kubariki katika Warumi 12:14
Warumi 12:14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
Na isitoshe mtume Paulo alikuwa anawaombea sana rehema ndugu zake Wayahudi waliopotoka, mbali na neema (Warumi 10:1)
Kama hakuwalaana Je! Katika vifungu hivyo alimaanisha nini?
Hilo Neno kulaani, tukisoma katika tafsiri ya awali ya biblia ya kigiriki linasomeka kama “Anathema”
Ambalo linamaanisha “mtu aliye chini ya laana/Hukumu ya Mungu”
Hivyo katika vifungu hivyo, Mtume Paulo aliposema “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe” Alimaanisha Hivi;
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na awe kama mtu aliye chini ya laana ya Mungu”
Na ndio maana mtume Paulo katika hiyo nyaraka yake mbeleni alieleza kwa mapana zaidi, jinsi gani watu waliokuwa wanategemea sheria ili kuwaokoa walivyokuwa chini ya laana ya hukumu. Soma;
Wagalatia 3:10 Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
Kwa hitimisho ni kuwa, mtume Paulo hakuwalaani wakorintho au wagalatia. Bali aliwaeleza uhalisi, madhara ya kuipotosha injili ya Kristo. sisi kama wakristo hatupaswi kuwalaani watu ambao wanatupinga/ au wanahubiri injili inayopotosha, bali ni kuwaombea rehema, wageuzwe, lakini bila kuwaficha matokea ya kutenda kwao huko, Kwamba wapo chini ya laana ya Mungu na hivyo waogope! Kwasababu hukumu ipo.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).
Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?
Jibu: Jina la Bwana Yesu Kristo lisifiwe daima.
Matoleo ni Neno la ujumla linalomaanisha aidha sadaka, au michango.
Neno Matoleo linatokana na neno “Kutoa” Hivyo chochote kile mtu anachokitoa kwa Mungu wake kinaitwa Matoleo.
Lakini sadaka ni toleo rasmi ambalo linalenga moja kwa moja madhabahu, na matoleo ya sadaka tofauti na matoleo mengine kama michango ni kwamba sadaka inakuwa ni siri lakini michango mengine inaweza isiwe Siri,
Kwamfano yale matoleo Anania na Safira mkewe waliyoyatoa ya kuuza viwanja na kuleta thamani yake chini ya miguu ya mitume, hayakuwa siri, bali lilikuwa ni jambo linalowekwa wazi kwa wote.
Lakini sadaka haipaswi kuwa kitu cha kuonyesha mbele za watu, bali kinapaswa kiwe siri ya mtu na Mungu wake…kama Bwana wetu Yesu alivyotufundisha.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Na Matoleo yote (iwe changizo au sadaka). Yana thawabu kubwa mbele za Mungu kama yakitolewa kwa nia njema na dhamiri njema na kulingana na Neno la Mungu,na Mungu anayaangalia sana.
Ukiahidi au ukipanga kumtolea Mungu kitu, basi hakiksha unatimiza kama ulivyoahidi au ulivyopanga pasipo kupunguza hata kidogo, ili isiwe kwako dhambi kama ilivyokuwa kwa Anania na Safira mkewe, ambao waimdanganya Roho Mtakatifu kwa matoleo yao.(Matendo 5:1-11).
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +25569303661
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
2 Petro 1:3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe
4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Uungu ni Ile Hali ya kuwa kama Mungu.
Kwamfano mtu anayefanya vitendo viovu kama vya uuaji, utoaji mimba, uchawi, ushoga tunasema anafanya “Ushetani”.. Kwasababu anatenda kazi za shetani.
Vivyo hivyo tunaposema “Uungu”. Tunamaanisha kuwa kama Mungu, au kufanya kazi kama za Mungu, au kuwa na sifa za Mungu ndani yako.
Na Tabia ya Mungu ndani ya Mtu. Si Kila mtu anazo. Bali ni wale tu waliozaliwa na yeye. Yaani waliokoka
Hizi ni baadhi ya Tabia za kiungu.
Kitu ambacho Mungu anawakiria watu wake waliompokea ni uzima wa milele. Ambao upo ndani yake. Mwanadamu wa Tabia ya asili Hana uzima wa milele ndani yake. Akifa Hana Tumaini la kuishi. Lakini aliyezaliwa mara ya pili. Huishi milele. Kwasababu uungu upo ndani yake.
Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?”
Ukiwa kama mwana wa Mungu sifa hii ni lazima itaonekana ndani yako. Hakikisho la uzima wa milele, mwovu hana uzima wa milele.
Pili mtu mwenye uungu ndani yake, anatoa tabia za Mungu ndani yake, ndio zile tabia za Roho tunazozisoma katika Wagalatia 5:22, kama vile Upendo, , fadhili, uaminifu, utakatifu n.k.
Wagalatia 5:22-25
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. [24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. [25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Mambo ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwenye tabia ya asili. Yeye huwa kinyume chake, au akijaribu kufanya basi ni kwa unafki, kwasababu havipo moyoni mwake.
Na pia mtu mwenye tabia ya uungu unakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu(yaani dhambi) kama vile Kristo alivyoushinda ulimwengu..
1 Yohana 3:9
[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Maana yake,dhambi inakuwa haina nguvu ndani yake. Maandiko yanasema hata wao wenyewe wakishangaa tunawezaje kuishi maisha ya mbali na dhambi (1Petro 4:4). Hawajui Ni kwasababu sisi tuna tabia za uungu ndani yetu.
Maandiko mengine yanayoeleza Neno uungu. Ni haya (Matendo 17:29, Warumi 1:20).
Bwana akubariki.
Je! Na wewe utatamani uwe na tabia za Ki-Mungu ndani yako?. Ni wazi kuwa hii ni kiu ya kila mmoja wetu. Kama ni hivyo basi, hauwezi kwa akili yako au nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Kwasababu biblia inasema wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika wana wa Mungu (Yohana 1:12). Hivyo huu ni uwezo utokao kwa Mungu mwenyewe, na sio kwa mwanadamu. Na tunaupata kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kwa kumkiri Yesu, na kumfanya kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu. kisha kumpa nafasi ya kuyatawala maisha yetu.
Hivyo basi ikiwa upo tayari siku ya leo kutubu dhambi zako, ili Bwana akufanye kiumbe kipya. Basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?