SWALI: Huyu “Yeye ashindaye” anayezungumziwa katika kila mwisho wa jumbe za makanisa saba. Ni mtu mmoja maalumu au wengi?
JIBU: Tunasoma Bwana Yesu alipotoa agizo au onyo kwa yale kanisa saba mwishoni alimalizia na kutoa thawabu. Lakini thawabu hiyo aliielekeza kwa yule ashindaye tu.
Kwa mfano ukisoma juu ya lile kanisa la Thiathira alisema..
Ufunuo wa Yohana 2:26
[26]Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
Sasa swali huulizwa je? kuna mtu mmoja maalumu ambaye anaonekana atashinda? na kupokea tuzo hiyo ya kuwa na mamlaka juu ya mataifa au ni mjumuiko wa watu.
Ni raisi kudhani tuzo hiyo imeelekezwa kwa mtu fulani mmoja lakini ukweli ni kwamba inamuhusu kila mtu…ni sawa na mwalimu awaambie wanafunzi wake atakayefaulu mtihani wangu..nitamlipia ada ya muhula mmoja.
Sasa yeye kutumia lugha ya umoja “atakaye” na sio “watakao”…hamaanishi kuwa amemlenga mtu fulani mmoja.
maana yake ni kuwa yeyote yule atakayefaulu, basi atalipiwa ada, iwe ni mmoja, au wawili au wote. watalipiwa. Kwasababu wamefaulu. Kigezo ni kufaulu sio atakayefaulu kuliko wote.
Vivyo hivyo na Bwana alichokimaanisha hapo kwenye hayo makanisa saba. Lengo lake ni wote washinde lakini inaonekana ni kama si wote watakaoshinda…bali wale watakaoshinda watazipokea hizo thawabu.
Hivyo ni kujitahidi…kwasababu kuna uwezekano wa wengi kukosa thawabu hizo.
Mtume Paulo alitumia mfano wa wachezaji ambao hushiriki katika mchezo, kwamba wachezao ni wengi lakini apokeaye tuzo ni mmoja..(1Wakor 9:24)
Lakini hakumaanishi kwetu sisi atakuwa mmoja, ni mfano tu alitumia kueleza uhalisia kwamba kuna kunga’ng’ana ,sio jambo rahisi rahisi…fahamu kuwa sisi wakristo hatuna mashindano ya ukubwa na nafasi mbinguni…tunashindana ili tuyatende yale tuliyoagizwa na Bwana kikamilifu na sio kuzidiana…
Ndio maana mahali pengine akasema watatoka wengi, kutoka mashariki, na magharibi kuja kuketi na Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote, (Luka 13:28-29) Umeona kumbe wazee wetu hao, ni kama vile wamewekwa sehemu moja na wengine watakuja kuungana nao. Na wote watakua kitu kimoja na wao, lakini pia angalizo ni kwamba watakaofikia hapo si wengi sana.
Mathayo 8:11
[11]Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
Kwahiyo ni kujitahidi hapo tusikose..Kwa kumaanisha kweli kweli kujitwika misalaba yetu na kumfuata Yesu. Na kujitenga na dhambi, na hakika thawabu hizo tutazifikia wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)
Rudi Nyumbani
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Zipo aina tatu za Utakatifu, na leo tutaangalia moja baada ya nyingine, na tutajua ni upi unaotufaa sisi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Danieli 2:2
[2]Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.
Wasihiri ni kundi la wachawi, lililojikita kwenye mazingaumbwe. Linatumia uchawi kubadili vitu kwa hila, mbele ya macho ya watu kuwafanya waone kama ni muujiza umetendeka, na wakati mwingine kutumia njia hiyo kuleta madhara kwa watu.
kwamfano wale yane na yambre kipindi cha Musa walikuwa ni wasihiri, walijaribu kubadili fimbo kuwa nyoka, na kuleta vyura.(Kutoka 8:7)
Mfano mwingine ni yule Simoni mchawi, tunayemsoma katika;
Matendo 8:9-11
[9]Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.
[10]Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
[11]Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.
Tofauti na waganga ambao, wenyewe wanajifanya kama matabibu, na wachawi na wale wakaldayo ambao ni wanajibu(wasoma nyota)…hawa wasihiri kazi yao hasaa ni ile ya kiini macho.
Lakini Mungu anathibitisha kwamba makundi yote haya, hakuna hata moja lenye uwezo wa kufikia hekima ya Mungu ipitayo vyote Hayana nguvu ya kupambanua mambo. au kufanya miujiza. Hakuna mganga wala wachawi, mwenye uwezo wa kufanya muujiza.
Sasa utauliza ni nini kile wanachokifanya kama sio miujiza?
Awezaye kutenda miujiza ni Mungu tu. wasihiri na waganga wanafanya kazi ya kulaghai fikra za watu kwa elimu ambayo ni ya siri (ya mashetani), ndio maana wanaofanya hizo kazi huenda kujifunza kufanya hivyo, namna ya kuchezea fikra za watu, na si kingine.
Sasa wewe kwasababu hujaijua hiyo elimu unaweza ukasema umeona muujuza kumbe ni uongo tu..wamekudanganya.
ni sawa na leo unapoona mtu akiwasiliana na mtu mwingine akiwa mbali na kuiona sura yake kwenye kioo, kama huijui elimu ya darasani, utasema ni muujiza lakini kumbe ni maarifa tu ya kibinadamu.
vivyo hivyo na hawa wachawi na wasihiri, hawana jipya kusema wanafanya muujiza fulani, ni elimu zao tu za kipepo
Hawawezi kuumba chochote. wale vyura waliofanya kutokea kipindi cha Farao, hawakuumba vyura wao wapya kimiujiza..Vinginevyo mpaka leo shetani angekuwa na uwezo wa kuumba na angeumba vyura wake wengi tu na viumbe vyake vimwabudu. Alichokifanya pale ni kuchukua vyura walioumbwa na Mungu, na kuwapumbaza watu macho, waone ni mawe yamegeuzwa vyura kumbe hakuna kitu. Ndio maana ujinga wao ulikuwa wazi baadaye…walipodhani kila eneo ni kiini macho, walipojaribu kwa chawa wakashindwa, kibao kikawageukia, wakakiri ni Mungu tu awezaye.
Kwahiyo wewe uliye na Yesu, shetani anakuona kama mungu duniani, mwenye nguvu nyingi sana, hekima mamlaka zaidi ya yeye. Wewe unaweza kutenda muujiza kabisa kwa jina la Yesu. yeye hawezi
mwamini Yesu mtegemee yeye tu, kwanini kutafuta msaada kwa vitu dhaifu, ukamtia Mungu wivu?. Kwenda kwa waganga ni kupungukiwa akili, ni kujitenga na fadhili zako, mwenyewe, ni kumdharau muumba wa mbingu na nchi, Yehova, atupaye vyote.
Okoka sasa, mpokee Yesu, upate uzima wa milele. Wachawi waliokutana na Yesu walisalimu amri na kuchoma mikoba yao. sasa wewe unaenda kufanya nini huko?
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
JIHADHARI NA ROHO YA YEZEBELI.
Rudi Nyumbani
Huu ni mwongozo maalumu ya njia bora ya kuiomba sala ya Bwana. Wengi wetu tunaiomba aidha kwa kukariri au kwa kukosa ufahamu wa jinsi ipasavyo kuombwa, kulingana na majira ya nyakati za agano jipya. Lakini kama tukijua namna ya kuiomba ipasavyo basi tutaweza fungua milango mingi sana rohoni, ukizingatia kuwa ni sala ambayo Bwana wetu mwenyewe alitufundisha kwasababu ndio hiyo hiyo hata yeye alikuwa anaiomba.
fungua chapisho hili lililo katika pdf kwa kubofya download uweze kusoma;
Kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mafundisho mengine:
MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?
https://wingulamashahidi.org/2023/04/01/jinsi-ya-kupigana-maombi-ya-vita/.
Swali: Simo ni nini, au ni nani kama tunavyosoma katika Ayubu 17:6.
Jibu: Tusome mistari hiyo mpaka ule wa saba (7).
Ayubu 17:6 “Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli”
Neno hili “Simo” linasomeka tena katika Ayubu 30:9.
Ayubu 30:9 “Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao, Naam, nimekuwa simo kwao.
10 Wao hunichukia, na kujitenga nami, Hawaachi kunitemea mate usoni”.
Na maana ya neno hilo (simo) ni “MTU ANAYEDHARAULIKA”
Wakati Ayubu mtumishi wa MUNGU anapitia yale majaribu ya kufiwa na wanawe na kupoteza mali zake zote, na zaidi ya yote kupitia matatizo ya kiafya, ile fahari yake yote iliisha na kusababisha watu wengi kumdharau ikiwemo mke wake, mpaka hatimaye naye kuliona hilo na kusema hayo maneno.
Lakini pamoja na kuwa SIMO mbele ya watu, kwa MUNGU alikuwa LULU kubwa sana, kwani majaribu yale hayakuwa kwasababu ya yeye kumwacha MUNGU bali ni kwasababu ya yeye kumkaribia Mungu zaidi, na wakati ulipofika alipata mara mbili, ya alivyovipoteza na miaka mingi zaidi ya kuishi (Ayubu 42:12-16).
Na sisi tunajifunza mambo hayo hayo, kuwa tujaribiwapo kwaajili ya haki tuna heri…
Lakini tupitiapo majaribu mfano wa yale ya Ayubu tukiwa katika dhambi, tunapaswa tujifikiri mara mbili, kwani huenda ni mapigo na laana kutoka kwa Mungu ili tutubu na si kwa lengo la kuzijaribu imani zetu kama Ayubu.
Ndivyo Neno linavyoma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28.
Kumbukumbu la Torati 28:15-16,37-39 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)
Huwezi kufanya kazi zote peke yako..
Aliyeunda injini ya gari, alihitaji mwingine mwenye ubobezi katika utengenezaji wa matairi, lakini pia alimhitaji mbobezi wa umeme wa magari, hivyo ili gari lisimame na kuanza kutembea limegharimu mikono na ujuzi wa wataalamu wengi.
Vile vile, mtumishi wa Mungu mmoja hawezi kufanya mambo yote peke yake, kuna wakati wengine watahusika tu.
Katika biblia kuna mahali Filipo alihubiri na kubatiza, lakini lakini Petro na Yohana waliwaombea hao waliobatizwa ili wajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo 8:12 ”Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu”
Umeona? mmoja Anabatiza wengine wanaombea ujazo wa Roho Mtakatifu..
Mambo yote yanakamilika namna hiyo katika ushirikiano na umoja wa Roho, na ndivyo kanisa la kwanza lilivyoenenda, hakukuwa na mashindano wala wivu katikati yao, tofauti na leo ambapo kila mtu anajiona bora kuliko mwingine.
Maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa hata Paulo, hakupanda na kuwagia yeye, bali matunda yake yalipaliliwa na wengine.
1 Wakorintho 3:6-7 “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye”.
Kama mtumishi wa Mungu, Je unaweza kuruhusu watumishi wengine wawajenge wale uliowatafuta wewe?…
Kumbuka si kila mtumishi ni wa kweli!…wengi ni wa uongo, lakini je inapotokea umehakiki kuwa kweli yule ni mtumishi wa Mungu, je waweza kuruhusu yule uliyemvua wewe ajengwe na mtumishi mwingine kama wewe?.
Kama hilo jambo gumu basi msaada wa haraka kutoka kwa Bwana unahitajika kwasababu ndivyo Mitume walivyofanya na sisi tunapaswa tufuate hivyo vielelezo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya vifungu hivi;
Mathayo 6:29
[29]nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
JIBU: Katika habari hiyo Mungu anaeleza jinsi anavyoweza kutujali na kututunza sisi kipekee kwa uweza wake wa ki-Mungu, akifananisha na jinsi anavyoyatunza maua yake ya kondeni ambayo leo yapo kesho yananyauka na kutupa tanuruni.
ndio hapo anasema tusiwe na shaka ya leo tuvae nini, kama Mungu anayavika vizuri maua hayo ambayo ni kwa muda mfupi tu huchanua baadaye hunyauka, si zaidi sisi tulio na thamani nyingi zaidi ya hivyo vyote?
Tena anasisitizia hata Sulemani katika fahari yake yote, hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya maua hayo.
Kumbuka Sulemani alikuwa ni mtu tajiri sana, mavazi yake yalikuwa ni ya thamani sana, lakini yalitegemea kuchovywa na kurembwa kwa rangi mbalimbali, ambazo hizo baada ya kipindi fulani hupauka au kuchuja.
Lakini maua hayapakwi rangi bali uzuri ule ni rangi yao kwa asili itokayo ndani. hayafifi rangi. Sulemani hakuwahi kuwa na vazi la namna hiyo.
Isitoshe maua nayo licha ya kuwa na mwonekano mzuri lakini pia hutoa harufu yao nzuri ya asili, kitu ambacho hawezi kukiona kwenye vazi la aina yoyote zuri duniani kutoa harufu yake yenyewe, yanategemea kupuliziwa marashi.
Hivyo hiyo ni kutufundisha kuwa Mungu anaweza kutunawirisha na kutupendezesha zaidi ya matarajio yetu, lakini hiyo hutimia kwanza pale tunapojishughulisha na mambo ya ufalme wake, ndio hayo mengine sasa ya chakula na mavazi atuzidishie.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
ONA FAHARI JUU YA BWANA.
Nyinyoro ni nini?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Rudi Nyumbani
(Masomo maalumu yahusuyo faida za matoleo).
Jifunze kutoa sadaka!!, jizoeze kutoa sadaka, jitaabishe kutoa sadaka!!.
Utoaji si agizo la washirika bali hata viongozi (wachungaji, waalimu, wainjilisti na watu wote wanaoujenga mwili wa Kristo), pasipo kujali Umri wala kipato. Hili ni agizo la Bwana YESU lenye baraka na laana nyuma yake (soma Mathayo 25:31-46).
Sadaka inayotolewa katika misingi ya Neno la Mungu, inafanya mambo makubwa zaidi ya yale tuyajuayo.
Sadaka inayotolewa katika msingi wa Neno la Mungu, inameza sadaka nyingine zilizotolewa na upande wa ibilisi.
Ile fimbo ya Musa ilibidi aitoe na kuitupa, ndipo ilipoweza kumeza zile fimbo nyingine za wachawi wa Farao.
Sasa zile fimbo zilizomezwa, laiti zingeendelea kuwepo zingeleta madhara mengine kwani zilikuwa ni za kichawi, na zilitumika na wachawi kwa shughuli za kichawi.
Sasa ilimgharimu Musa kuitoa fimbo yake kwanza ili imeze zile nyingine. Vile vile iliwagharimu wachawi kutoa fimbo zao za gharama ili wahindane na Musa.
Vile vile kuna mambo mengine yanahitaji tu matoleo yatatuke..(Kasome Waamuzi 20:20-40).
Sasa wale waganga wa Misri walizigharimia zile fimbo zao, hazikutokea tu… huenda walizinunua kwa fedha na kuzifanyia matambiko mengi.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatuonyesha jinsi waganga wanavyougharimia uganga wao.
Matendo 19:17 “Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu”
Hapo anasema gharama ya vile vitabu vya uganga vilivyochomwa ilikuwa ni elfu 50.
Sasa tukisema elfu 50, kwenye vichwa vya wengi inadhaniwa ni shilingi za kitanzania, zinazotosha tu gharama ya nauli kutola mkoa mmoja hadi mwingine..La!.
Kujua thamani halisi ya vipande vya fedha elfu 50…rejea kile kiasi Yuda alichoongwa ili amsaliti Bwana YESU, maandiko yanasema alipewa kiasi cha vipande 30 tu vya fedha na vipande hivyo vilitosha kununulia shamba (ambalo hatujui ni hekari ngapi) lakini tunajua ni hekari nyingi maana zilitumika kama eneo la makaburi..soma Mathayo 27: 3-7.
Sasa piga hesabu kama vipande 30 vya fedha ya Yuda vimenunua shamba, na hapo vitabu vya waganga gharama yake ni vipande vya fedha elfu 50..gawanya hapo uone waganga waliugharimia uganga wao kiasi gani…
Utaona hapo ni zaidi ya mashamba 1,600 na kama shamba moja litauzwa tu kwa gharama ya shilingi za kitanzania milioni moja…basi jumla yake vile vitabu vyote ni zaidi ya BILIONI MOJA.
Kwahiyo wale waganga waligharimia mabilioni kuusimamisha uganga wao!!!…..
Halafu wewe na mimi kuigharimia injili kidogo tu tunaona tabu!!!!…..Fikiri mara mbili…fikiri mara mbili!!!.
Jenga ufalme wa Mungu, kwani shetani anajenga ufalme wake kwa kasi na gharama.
Bwana atusaidie.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe.
Upo umuhimu wa kuhubiri injili mahali popote na katika mazingira yoyote kwasababu ni agizo la Bwana mwenyewe. Wapo wanaoamini kuwa injili ya mitaani na masokoni hazina faida yoyote kwasababu watu wanakuwa hawapo katika utulivu. Na pia wapo wanaoamini kuwa injili za kwenye mikutano au makanisani ndizo zilizo bora.
Lakini nataka nikuambie: Injili zote zina umuhimu. Za watu walio katika utulivu na utayari wa kusikiliza, na hata za wale ambao hawako tayari kabisa.
“Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku.”
(Matendo 17:17)
“Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu…”
(Luka 8:1)
Kikawaida ni ngumu kumsimamisha mtu barabarani na kumwambia asikilize. Lakini unapohubiri bila hata ridhaa yake, Neno linaweza kuingia ndani yake hata kama hataki. Lile Neno linaweza kuwa mbegu njema itakayochipuka kwa wakati wake.
Kwahiyo ni heri asikie moja kuliko kutokusikia kabisa. Wengine hawaendi kanisani, wengine ni wa imani tofauti, wengine wamejitosheleza – lakini kwa kuhubiri, unawafikia.
“Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana”
(Ezekieli 2:7)
Hata kama ni mara ya mia, huenda Neno moja tu likamgusa. Au wewe ndiye umeanza safari ya wokovu ndani yake ambayo itakamilika baadaye.
Wapo wanaohitaji kusikia mara nyingi. Ndio maana Bwana alituma manabii kupiga kelele:
“Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta…”
(Isaya 58:1)
Kazi ya kuhubiri si nyepesi. Lakini matokeo yake ni makubwa sana:
“Kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”
(Luka 15:10)
Pengine umesikia injili mara nyingi lakini bado hutaki kubadilika. Injili ya kurudia rudia si tangazo, ni ushuhuda dhidi yako.
“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”
(Mathayo 24:14)
“Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu”
(Warumi 2:16)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, basi wasiliana nasi:
📞 +255789001312
📞 +255693036618
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya hapa:
👉 https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mafundisho mengine:
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?