Category Archive Home

UFUNUO: Mlango wa 13

Tukisoma kitabu cha Ufunuo mlango wa 13 tunaona kuna wanyama wawili wanaozungumziwa pale; wa kwanza akiwa ni yule mwenye vichwa saba na pembe 10 aliyetoka baharini na wa pili ni yule aliyekuwa mfano wa mwanakondoo mwenye pembe 2 akitoka katika nchi.

Kwa ufupi tuwatazame hawa wanyama wanawakilisha nini na wanachukua nafasi gani katika siku hizi za mwisho:

MNYAMA WA KWANZA:

Ufunuo 13:1-5″ Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.

4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?

5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.

6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.

7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

9 Mtu akiwa na sikio na asikie.

10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu. “

Hapa tunamwona huyu mnyama akiwa na vichwa saba na pembe 10, na juu ya zile pembe zake ana vilemba 10, sasa hivi vichwa 7 inafahamika vinawakilisha ngome/mamlaka ambazo shetani alizikalia na kuzitumia kupambana na kuuharibu uzao wa Mungu hapa duniani tangu taifa la Israeli lilipoundwa. Na tawala hizi tunaweza tukaziona katika biblia nazo ni 1) MISRI   2) ASHURU, 3) BABELI 4) UMEDI & UAJEMI   5) UYUNANI   6) RUMI   7) RUMI -KIDINI.

Lakini Yohana alimwona yule mnyama akiwa na PEMBE 10 katika kichwa chake, kumbuka zile pembe 10 hazikuwa zimesambaa juu ya vichwa vyote saba kama inavyofikiriwa na watu wengi, bali zote 10 Yohana alizoziona zilikuwa juu ya kichwa KIMOJA TU! na sio kingine zaidi ya kile kichwa cha saba. Kwahiyo kile kichwa cha saba ndicho Yohana alichokikazia macho kwasababu kilikuwa ni tofauti na vingine vyote.

Hivyo zile pembe 10 kulingana na maono aliofunuliwa Danieli juu ya ile sanamu ya Nebukadneza alioiona yenye miguu ya chuma na nyayo zenye vidole 10 zilizochanganyikana nusu chuma, nusu udongo, kama inavyojulikana ile miguu ya chuma ni utawala wa RUMI na vile vidole ni utawala wa RUMI uliokuja kugawanyika na kuwa yale mataifa kumi ya ULAYA wakati ule ambayo yalikuwa bado hayana nguvu kwasababu yalikuwa bado hayajavikwa vilemba(CROWNS). Hivyo vile vidole 10 ndio zile pembe 10 zinazoonekana juu ya yule mnyama na ni mataifa 10 yaliyopo katika umoja wa ULAYA (EU), na kama tunavyoona sasa kwa huyu mnyama zile pembe 10 zimetiwa VILEMBA inaashiria kuwa utakuja wakati haya mataifa yanayounda umoja wa ulaya yatapewa nguvu ya utawala na yule mnyama kutenda kusudi la kuwaua watakatifu katika kipindi cha ile miaka mitatu na nusu ya mwisho ya dhiki kuu.

Leo hii tunaona umoja wa ulaya unaundwa na mataifa zaidi ya 10, lakini yatakuja kuishia kuwa 10 tu ili kutimiza unabii wa kwenye biblia na yapo mbioni kuvikwa vilemba( yaani kupewa utawala wa dunia) yakiwa chini ya yule mnyama ( RUMI) chini ya utawala wa PAPA ambaye ndiye mpinga-kristo biblia inayomwitwa “mtu wa kuasi”, mwana wa uharibifu ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.(2Thesalonike 2). Leo hii bado hayana nguvu kwasababu Danieli alionyeshwa kuwa vile vidole kumi nusu yake vitakuwa na nguvu na nusu yake vitakuwa vimevunjika ndivyo ilivyo sasa hivi Umoja wa ulaya hauna nguvu sana, lakini utakuja kupata nguvu duniani kote ili kutimiza kusudi la yule mnyama(mpinga-kristo)

Tukiendelea kusoma mstari wa tatu tunaona moja ya kichwa chake (ambacho ndio kile kichwa cha saba) kimetiwa jeraha la mauti nalo likapona. Kumbuka Rumi-ya kidini(UKATOLIKI) iliyokuwa chini ya UPAPA katika historia ilikuwa inatawala dunia nzima, na ilifanikiwa kupata nguvu dunani kote kiasi cha kwamba mtu yeyote aliyeonekana anakwenda kinyume na hiyo dini adhabu ilikuwa ni kifo tu, mamilioni ya wakristo waliouwa wote waliokataa kuisujudia miungu yao ya kipagani, jambo hili liliendelea na hii dini ilizidi kupata nguvu hadi kufikia karne ya 16 wakati wa matengenezo ya kanisa ambapo Mungu alianza kuwanyanyua watu wake kama Martin Luther ambaye alianza kufundisha watu “kuhesabiwa haki kwa imani” na kukosoa mafundisho potofu ya kanisa Katoliki lakini PAPA alipotaka kumuua mfalme wa Ujerumani alisimama kumuhifadhi Luther, ndipo watu wengi wakaanza kuacha hii dini ya uongo na kuligeukia NENO la Mungu hivyo Ukatoliki ukaanza kupungua nguvu, na wakati huo huo Mungu aliwanyanyua wengine kama Calvin, Zwingli, Knox n.k. ili kulitengeneza tena kanisa lililokuwa limeharibiwa na mafundisho ya uongo ya Kanisa katoliki.

Hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa lile jeraha la yule mnyama lakini pigo hasa lilikuja karne ya 18 mwaka 1798 katika mapinduzi huko Ufaransa Jenerali Berthier alipeleka vikosi vyake Roma na kumng’oa PAPA katika utawala wake, akamchukua mateka pamoja na mali zake zote za dini yake, Hivyo ikapelekea dini ya kikatoliki iliyokuwa inatiisha dunia kuwa karibuni na kutoweka kabisa, hilo lilikuwa pigo kubwa sana lilofananishwa na jeraha la mauti lakini tunaona Biblia inasema lile JERAHA LA MAUTI lilipona,

 Je! Jeraha hili liliponaje na lilipona lini?.

Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia, matatizo yalikuwa mengi duniani, uchumi ulishuka sana, mataifa ya ulaya yaliaanza kuanguka na kupoteza nguvu zao kutokana na athari ya vita, Hivyo kiu ya kutafuta amani duniani ikaongezeka kumbuka wakati huo huo Marekani ilianza kupata nguvu, na likiwa kama taifa la kikristo (protestant) lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi hivyo kwa kushirikiana na mataifa ya ulaya kwenye harakati za kutafuta amani, (isiyokuwa ya kivita) walianza kuutambua umuhimu wa PAPA Kwasababu alionekana kuwa ni mtu mwenye mvuto na anayekubalika na watu wengi duniani, hivyo mataifa mengi yakaanza kutuma mabalozi wake kwa papa ajihusishe na masuala ya AMANI YA DUNIA. Sasa kuanzia hapo jeraha lake la mauti likaanza kupona, wale ambao walikuwa wanafanya mageuzi kinyume chake(protestants) wakaanza kushirikiana nae tena, uprotestant ukabakia kuwa jina tu na ndio huko inapoundiwa ile sanamu ya mnyama nitakayoielezea zaidi mbeleni…

Tukiendelea mstari 4 & 5, Tunaona lile joka ambaye ni Shetani mwenyewe alimpa nguvu yule mnyama naye akaanza kunena maneno makuu ya makufuru. Tukisoma pia kitabu cha Danieli alizungumziwa kama ile PEMBE ndogo iliyozuka na kungo’a wale wafalme watatu na kunena maneno ya makufuru Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. “ Na huyu si mwingine zaidi ya mpinga-kristo ambaye ni PAPA,..Si ajabu PAPA leo anasimama “badala ya mwana wa Mungu duniani”..Vicarivs filii Dei, ..Papa leo amejivika uwezo wa kusaheme dhambi jambo ambalo BWANA YESU KRISTO mwenyewe ndiye anayeweza kulifanya ..haya yote ni maneno ya makufuru, na yapo mambo mengi zaidi ya hayo ambayo ni makufuru. Kumbuka ninaposema PAPA namaanisha kile “CHEO”..kwahiyo yeyote anayekikalia hicho cheo amejitwika cheo cha mpinga-kristo mwenyewe.

Na tunaona wakati wa mwisho atapewa uwezo wa kutenda kazi miezi 42, hii ni miaka mitatu na nusu, kati ya ile miaka saba ya mwisho ya lile juma la 70 la Danieli. Hichi kitakuwa kipindi cha DHIKI KUU, sasa hivi PAPA anaonekana kama mtu asiyekuwa na madhara yoyote, anakuja kwa njia ya kujipendekeza ili apate nguvu kiurahisi, kama kitabu cha Danieli kinavyomtabiri, leo hii duniani kote anajulikana kama “MTU WA AMANI”, Ni mtu mwenye wafuasi wengi duniani, na aneyekubalika kuliko mwanasiasi yoyote duniani, dini nyingi zimeanza kuvutiwa naye, hata waislamu sasa wanamwona kama ni mtetezo wao mtu anayejali watu wote, PAPA anasema wote tunamwabudu Mungu mmoja ila kwa njia tofauti tofauti (yaani wakristo, waislamu wahindu, wabudha tunamwabudu Mungu mmoja), angali biblia inasema YESU ndiye njia pekee ya kumfikia Mungu, na cha ajabu umaarufu wake unaongozeka na watu wanamfurahia ili kutimiza ule unabii kwamba “watu wote ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaomsujudia.” Na kumsujudia sio kumpigia magoti bali ni kukubaliana na mifumo yake na imani yake.

Ndugu yangu mpinga-kristo hatakuja na mapembe kichwani, akilazimisha watu wamwabudu, kumbuka biblia inasema shetani ana HEKIMA kuliko Danieli, na sehemu nyingine biblia inasema ile roho itataka kuwadanganya yamkini hata wateule. Siku zote anakuja kama malaika wa nuru, usitazamie kuwa mpinga-kristo atakuwa muislamu au muhindi au freemason, hapana ndugu yupo kanisani amebeba biblia na anafanya kampeni za amani duniani na watu wanamshangilia na kumbusu, biblia inasema hapo ndipo “PENYE HEKIMA ” .

Kwahiyo inahitajika Hekima kumjua vinginevyo utachukuliwa na mafuriko yake kama wengi walivyochukuliwa huu ni wakati wa kuwa macho sana, jali maisha yako ya umilele yanayokuja. Chunguza maandiko kama watu wa Beroya, sio kila roho inayoshabikiwa na wengi unaipokea moyoni mwako kwasababu biblia inasema IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NJEMA MACHONI PA WATU..LAKINI MWISHO WAKE NI UPOTEVU, na BWANA YESU alisema njia iendayo upotevuni ni PANA na wengi wanaiendea hiyo.

MNYAMA WA PILI:

Ufunuo 13:11-18″

11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.

12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.

13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.

14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.

15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.

16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. “

Tunaona huyu mnyama wa pili ana pembe kama mwanakondoo, lakini sio mwanakondoo, na huyu anaonakana ametoka katika nchi na sio katika bahari na yeye hana vichwa saba Kama yule mnyama wa kwanza, ikiwa na maana kuwa utawala wake haukuanzia mbali kama yule mnyama wa kwanza bali ulizuka mwishoni. Hivyo huyu mnyama si mwingine zaidi ya MAREKANI. Ukiangalia katika ile nembo ya Marekani katika ile dola yao utaona yule tai akiwa ameshika mishale 13, ile piramidi kuna ngazi 13, kuna nyota 13 juu ya yule tai, matawi 13 ya ule mzeituni ulioshikwa ..nk. kila mahali 13..13… na taifa la Marekani linaonekana katika UFUNUO 13.

Pia huyu mnyama alipewa uwezo wa kufanya watu wote wakaao duniani wamsujudie yule mnyama wa kwanza na kuunda ile SANAMU YA YULE MNYAMA.

Sasa Sanamu ya mnyama ni ipi?

Marekani kama taifa lilokuwa la kiprotestant ambalo hapo kwanza lilikuwa halishakamani wala halishirikiani na kanisa Katoliki kwa namna yoyote, lakini katika karne ya 20 baada ya vita ya pili Vya dunia liliacha njia ya kweli ya NENO LA MUNGU, na kurudi kuiga tabia za yule mnyama,kazi nzuri na juhudu zote zilizofanywa na wale wana-matengenezo zikawa ni bure, ni sawa na mbwa aliyerudia matapishi yake.

Baada ya kuibuka jopo kubwa la madhehebu ya kiprotestant duniani, viongozi wa madhehebu ya kimarekani walikutanika kwa agenda ya kutaka kuondoa tofauti katikati ya wakristo ili kufikia muafaka mmoja wa IMANI, ndipo walipounda BARAZA LA MAKANISA ULIMWENGUNI (World Council Of Churches), na NATIONAL COUNCIL OF CHURCHES , na ndio chimbuko la EKUMENE. (Ecumenical council)

Na Kanisa Katoliki likiwa kama washirika wao wa karibu wakiwasaadia.

Baraza hili la UMOJA WA MAKANISA liliazimu kuyarudia mambo yale yale ya ukahaba yaliyofanywa na kanisa Katoliki, Iimekuwa ni SHIRIKA LA KI-DINI, na Linasheria zake na itakadi zake ambazo zinaenda kinyume na mpango na NENO LA MUNGU. Kwahiyo UMOJA HUU ndio unaoitwa SANAMU YA MNYAMA..Kwasababu tabia zote zilizokuwa katika kanisa kahaba katoliki zipo nazo kule na hivi karibuni yule mnyama (America) ataenda kuipa PUMZI ILE SANAMU INENE, ili watu wote waiabudu, hii ikiwa na maana siku sio nyingi watu wote duniani watenda kulazimishwa kuwa washirika wa muunganiko wa hayo makanisa mtu yeyote atakayeonekana kwenda kinyume atauawa.

Na kama tunavyoona huyu mnyama wa pili (MAREKANI) anaweza kufanya ishara kubwa hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni, jambo hili linatupa picha nguvu za kijeshi walizonazo Marekani kama uwezo wa kushusha makombora makubwa ya vita kutoka angani mabomu ya atomic n.k.

Hili baraza la makanisa duniani sasa linafanikiwa kuzivuta dini zote ulimwenguni pamoja, ikiasisiwa na PAPA kiongozi wa kanisa katoliki duniani, itafika wakati kama hautakuwa mshirika wa dini au kanisa ambalo halijaunganishwa katika huu UMOJA WA MAKANISA NA DINI hutaweza kuuza wala kununua wala kuabudu, wala kuishi katika jamii,

Leo hii tunaona vitendo vya kigaidi na vya mauaji vikiongezeka, wanasiasa wameshindwa kuirejesha amani ya dunia, na matatizo yote yahusuyo amani yanatokana na mizozo ya kidini tunaweza kuona mambo yanayoendelea mashariki ya kati mfano Israeli, syria-kuna ISIS,Iraq, Lebanoni-kuna hezbolah, myanmar huko Asia kuna warohighya, sehemu za Afrika nchi kama Nigeria kuna Boko kuna haramu, Somalia-alshabaab, central Africa- antibalaka ..na makundi mengine mengi sana,. tunaona mizizi yote ya migogoro inaanzia katika DINI. Hivyo atahitajika mtu wa KIDINI mashuhuri kutatua migogoro ya kidini na sio wanasiasa au watu wa kijamii – Na huyu atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA kwasababu yeye ndiye anayekubaliwa na dini zote pamoja na wafalme wote wa dunia.

Hivyo atapokwisha kupata nguvu, ataibua mfumo mmoja wa kutambua watu wote duniani kwa imani zao, kwa kivuli cha kuleta amani na kukomesha vitendo vya uvunjifu amani duniani kumbe nia yake itakuwa ni kuwateka watu wote duniani na kuwatia ile CHAPA YA MNYAMA. Wakati huo watu wengi duniani wataufurahia huo mfumo pasipo kujua ndio wanaipokea chapa hivyo. Wengi watasajiliwa katika madhehebu na dini zao zilizokuwa na ushirika huo wa UMOJA WA MAKANISA ULIMWENGU , Vitatumika vitu kama CHIPS, IDS, na utambulisho mwingine utakotengenezwa ili kuyafikia makundi yote, sasa wale watakaokaidi ndio watakaopitia dhiki kuu, hao ndio watakaoonekana magaidi na wavunjifu amani, kama sivyo kwanini wasikubali utambulisho huo mpya? na kumbuka watakuwa ni wachache sana watakaogundua kuwa ndio CHAPA YENYEWE ,

Hivyo ndugu injili tuliyonayo sasa hivi inasema ..UFUNUO 18:4-5″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU,MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Ndugu toka katika mifumo ya madhehebu kwasababu yameshirikiana na yule mnyama(kanisa katoliki) kufanya ukahaba, na kuua watakatifu wa Mungu wengi, yeye anaitwa BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA ikiwa na maana kama yeye ni mama wa makahaba ni dhahiri kuwa anao mabinti na wao pia ni makahaba kama mama yao alivyo na hao mabinti sio wengine zaidi ya madhehebu yote yaliacha uongozo wa Roho mtakatifu na kuandamana na desturi za kanisa kahaba Katoliki, hivi karibuni tumesikia WALETHERANI wameungana rasmi wakatoliki.!! Biblia inasema TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU, kama ukishirikiana naye inamaanisha kwamba na wewe pia utashiriki mapigo yake ndivyo Mungu anavyokuchukulia.

Ufunuo 14:9 ” Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. “

Bwana ametuita kuwa BIKIRA SAFI, na bikira tu ndiye atakayeingia katika karamu ya mwanakondoo, toka kwenye mifumo ya madhehebu umwabudu Mungu katika ROHO NA KWELI.

Mungu akubariki, na Mungu atusaidie katika safari yetu tuumalize mwendo salama

Amen.

Kwa Mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 14

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana…


CHAPA YA MNYAMA

DANIELI: Mlango wa 2

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

UFUNUO: Mlango wa 21


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 12

MAELEZO JUU YA “UFUNUO 12”

Ufunuo 12

1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.

2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.

3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.

5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.

6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.

7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.

15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

Ukisoma Ufunuo mlango wa 11, utaona habari ya wale MASHAHIDI WAWILI wakifanya kazi ya kuwahubiria injili wale Wayahudi 144,000 na kutiwa muhuri (Ufunuo 7). Na tunaona walifanya kazi yao miezi 42, (yaani miaka mitatu na nusu) na baada ya kumaliza ushuhuda wao yule mnyama atokaye kuzimu atawaua lakini baada ya siku tatu na nusu tunaona Mungu atawafufua.

Kumbuka baada ya kanisa kunyakuliwa, injili itahamia Israeli na itakuwa imebakia miaka 7 tu mpaka mwisho wa dunia utakapofika kulingana na unabii wa Danieli 9:27, kwenye lile juma moja la mwisho kati ya yale majuma 70 aliyoonyeshwa.

Hivyo ndani ya hii miaka 7, nusu yake yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza, hawa manabii wawili watafanya kazi ya kuwahubiria wayahudi, na nusu ya pili iliyobaki itakuwa ni kipindi cha ile DHIKI KUU (yaani miaka 3.5 ya mwisho).

Sasa tukiendelea kusoma kitabu cha Ufunuo 12 tunaona Yohana akiona ishara kuu mbinguni, yule mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12.

Ukiangalia huyu mwanamke anawakilisha taifa la Israeli, ukisoma mwanzo 37:9 utaona ile ndoto aliyoota Yusufu aliona jua na mwezi na zile nyota 11 zikimwinamia ambayo tafsiri yake tunafahamu ilikuwa ni Yakobo kama jua, mwezi kama mama zake, na wale wana 11 wa Israeli kama zile nyota. Hivyo yule mwanamke ni taifa la Israeli.

Ukiendelea kusoma mstari wa pili utaona yule mwanamke alikuwa na mimba, na katika hali utungu wa kutaka kuzaa, na akamzaa mtoto mwanamume ambaye atawachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Maana ya ule utungu ni unabii au matarajio ya kuzaliwa masiya katika Israeli ambaye alikuwa akisubiwa kwa muda mrefu, Na huyu mtoto mwanamume si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO yeye ndiye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma katika ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 2:27).

Ukizidi kusoma utaona pia katika mstari wa 3-6, utaona ishara nyingine ilionekana lile joka kubwa jekundu (ambalo ni shetani) likiwa limejiandaa pale atakapozaliwa yule mtoto limmeze, lakini halikufanikiwa, jambo hili tunaliona lilitimia wakati Bwana YESU anazaliwa Mfalme Herode, alipopata habari kuwa mfalme aliyetabiriwa kazaliwa katika Israeli alifadhaika na kutaka kumwangamiza mtoto YESU, Lakini hakufanikiwa mpaka Mungu alipomchukua juu mbinguni katika kiti chake cha enzi.

Tukiendelea kusoma kuanzia ule mstari wa 7-12, Tunaona habari nyingine inayohusu vita vinavyoendelea mbinguni, kati ya Malaika watakatifu na shetani pamoja na malaika zake, kwa maelezo marefu juu ya vita hivyo unaweza kufungua hapa >> Vita vinavyoendelea mbinguni

Lakini tukiendelea mstari wa 13 tunaona baada ya yule mtoto kunyakuliwa juu (yaani Yesu kupaa AD 30) yule joka aliendelea kumuudhi yule mwanamke,tunaona katika historia alizidi kumuudhi kwa takribani muda wa miaka 2000 mpaka sasa, aliwatesa na kuwaua wayahudi katika nyakati tofauti tofauti, mfano wakati wa utawala wa Adolf Hitler aliwaua wayahudi zaidi ya milioni 6, katika historia tunaona wayahudi ni watu wamekuwa wakichukiwa na mataifa mengi n.k.

Mstari wa 14, tunasoma mwanamke yule baada ya kuudhiwa muda mrefu akapewa MABAWA MAWILI YA TAI yule mkubwa ili aruke aende mbali na yule Joka aliyetupwa chini ili kufanya vita na watakatifu kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Yale mabawa ya Tai ni injili ya wale manabii wawili wa ufunuo 11, watakaowahubiria wayahudi ili kuwafanya wamjue yule joka kubwa jekundu ni nani (MPINGA-KRISTO), na utendaji kazi wake na namna ya kumuepuka, na ndiye anayetaka kukaa katika Hekalu la Mungu kuabudiwa kama Mungu.

Kumbuka wale manabii wawili katika injili yao ndio watakaomfunua yule mpinga-kristo kwa wayahudi kuwa si mwingine zaidi ya kiongozi maarufu anayetoka katika utawala wa RUMI, mwenye kivuli cha Amani kumbe ndani yake ni joka linalotaka kuabudiwa, Kama tu vile lile joka lilivyokuwa ndani ya HERODE-Mrumi kutaka kumwangamiza YESU vivyo hivyo hilo joka litakuwa ndani ya mpinga-kristo atakayetoka katika utawala ule ule wa Rumi kutaka kuwaangamiza wayahudi.

Hivyo wale wayahudi 144,000 (ufunuo 7), watakapoamini ile injili ya wale manabii wawili watakayoihubiri ile miaka mitatu na nusu ya kwanza, pamoja na zile ishara na yale mapigo yatakayofuatana nao, Hawa wayahudi wachache 144,000 watafahamu kuwa yule joka anawawinda, na kwamba DHIKI KUU itaanza hivi karibuni, hivyo Mungu atawafungulia mlango wa kuwaficha mbali na yule JOKA pale dhiki itakapoanza,

Kwahiyo hili kundi dogo litaondoka ISRAELI, Mungu atawapeleka mahali alipowaandalia mahali ambapo yule mpinga-kristo hataweza kuwafikia (hii ndio maana ya kupewa mabawa ya Tai), lakini kumbuka sio wayahudi wote wataikubali ile injili ya wale manabii wawili bali ni wale tu 144,000 tu.

Watakaosalia ile miaka mitatu na nusu ya mwisho itakapoanza (ambacho ndio kipindi cha dhiki kuu), watapata mateso mengi yasiyokuwa na mfano tangu ulimwengu kuumbwa na hayatakuwepo hata baada ya hapo, kumbuka dhiki hii itajumuisha pia watu wote wa mataifa watakaokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita.

Kama tu vile kipindi cha kuzaliwa kwa YESU wale mamajusi walipomletea Herode habari ya kuzaliwa mfalme Israeli, malaika walimwonya Mariamu na mwanawe waondoke Israeli kwasababu mpinga-kristo(Herode) anakwenda kuleta dhiki, walikimbilia Misri kabla ya ile dhiki kuanza, lakini yule Herode alipoona kuwa wale mamajusi wamemlaghai, alikasirika akaenda kufanya vita na uzao wote uliobakia wa watoto wa Israeli,

Tunaona kulikuwa na maombolezo makuu Yerusalemu watoto wote walichinjwa. Vivyo wale manabii wawili (Ufunuo 11) wanafananishwa na wale MAMAJUSI ambao walimtangazia Herode habari mbaya za kuzaliwa mfalme, na wakati wa mwisho wale MANABII WAWILI pia watamtangazia mpinga-kristo kwamba mfalme kazaliwa tena mioyoni mwa WAISRAELI na kwamba anayepaswa kuabudiwa ni yule mtoto na sio yeye, na kama vile Herode alivyowakasirika mamajusi pamoja na Mariamu na mtoto vivyo hivyo mpinga-kristo wakati wa mwisho atawakasirikia wale MASHAHIDI WAWILI na kuwaua, lakini baadaye hakufanikiwa kuwaangamiza kabisa kwani walifufuka kama vile wale mamajusi walivyopewa njia ya kumtoroka Herode,

Na kama vile ni mwanamke mmoja tu (Mariamu) kati ya wanawake wote wa Israeli ndiye aliyekuwa na mimba ya mwokozi ndani, vivyo hivyo ni lile kundi dogo tu (144000) ndio litakalokuwa na ufunuo wa YESU mioyoni mwao utakaoletwa na wale manabii wawili wanaofananishwa na mamajusi.

Na pia kama tunavyoona Mariamu alipelekwa peke yake Misri mbali na Herode vivyo hivyo na wale 144,000 ndio tu watakaopelekwa mbali na mpinga-kristo wakati wa dhiki itakapoanza walioabakia wote yaani mamilioni ya waisraeli itawapasa wapitie DHIKI KUU kama tu wale wanawake wengine wa Israeli walivyouliwa wana wao.

Kwahiyo hawa 144,000 hawataguswa na yule joka kubwa jekundu na ndio maana tunawaona katika Ufunuo 14 wakiwa wamesimama na mwanakondoo juu ya mlima Sayuni, bikira safi wa Mungu, hawa wataingia katika ule utawala wa miaka 1000, pasipo kupitia madhara yoyote.

Kwa ujumla Ufunuo sura ya 12, inaelezea ISRAELI na jinsi yule mwanamke alivyofananishwa na taifa la Israeli.

Kwahiyo ndugu tazama ni wakati gani tunaishi, je! umepokea kweli Roho Mtakatifu? umebatizwa katika ubatizo sahihi? Maisha yako yanastahili unyakuo?. Kumbuka sasa Taifa la Israeli linanyanyuka, dalili zote zinaonyesha kuwa unyakuo upo mlangoni na injili inakaribia kurudi Israeli, Maombi yangu utubu,

Fahamu tu yule JOKA kubwa jekundu alishatupwa chini akiwa na ghadhabu nyingi akijua muda wake umebaki mchache, Hivyo utendaji wake wa kazi wa sasa sio kama ule wa zamani anatafuta kukupeleka kuzimu kwa gharama zozote, hivyo ni wakati wako wewe kusimama imara na kuuthibitisha wokovu wako.

Mungu akubariki.

Kwa mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 13

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana..


MARIAMU

UZAO WA NYOKA.

MPINGA-KRISTO

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.


Rudi Nyumbani

Print this post

BWANA YESU ALIKUWA ANAONYESHA KUWA MUNGU NI MUNGU MWENYE AKILI TIMAMU.

Bwana Yesu mara nyingi alikuwa akiwaaminisha watu kwa mifano, yaani ni jinsi gani Mungu alivyo na akili timamu na alivyo na kumbukumbu nzuri sana katika mambo yake yote, alijaribu kila namna kuwatolea watu ile dhana ya kuwa Mungu ni kiumbe cha ajabu kilicho mbinguni kinahitaji kuabudiwa tu wakati wote, na hakina muda wa kutazama mambo mengine manyonge yawahusuyo wanadamu, nikisema mambo manyonge ninamaanisha mambo yanayozunguka maisha ya mwanadamu ya kila siku, kama vile majukumu, afya, chakula, malazi, matamanio ya maisha bora, raha, sherehe n.k..

Yesu alituhakikishia kuwa Mungu anatuzingatia sana, kwa kutumia mifano mirahisi kabisa iliyo hai ili kutuonyesha sisi ni jinsi gani Mungu alivyo na kumbukumbu ya haraka sana juu ya watu wake na viumbe vyake vyote..Embu chukua muda tafakari huu mfano kama ulivyo, najua unaweza kuwa na tafsiri nyingi unazozifahamu lakini naomba kwa sasa usiongeze chochote utafakari tu kama ulivyo, naamini utajifunza kitu kikubwa sana ndani yake…

Mathayo 6:26 “Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. NINYI JE! SI BORA KUPITA HAO?”.

Nataka nikuambie Mungu hategemei msaada wako wewe ili akutimize mahitaji yako ya riziki, yeye anaweza kufanya hayo yote bila msaada wako na ukaishi vizuri tu,,..Huoni kama hilo linaweza kuwa ni faraja kwako katika kile UNACHOKIFANYA sasahivi, kiwe ni kinakidhi au hakikidhi?, pengine umekata tamaa ya maisha kwa namna moja au nyingine na kuona kama vile Mungu haoni unayopitia, lakini nataka nikumbie kama ndege hawamwongezei chochote na analo jukumu la kuwalisha, wewe hupaswi kuwa na hofu hata kidogo..Kwasababu wewe ni mara nyingi sana zaidi ya wao.

Mfano mwingine ni huu..

Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?”.

Nilipokuwa ninautafakari sana huu mstari na kujiuliza ni wapi maua yanamzidi Sulemani kwa kuvikwa vizuri, nikagundua japo kuwa hayajisumbukii kwa chochote yapo pale pale, lakini kumbe rangi za maua huwa hazifubai, lakini mavazi ya Sulemani yalikuwa yanachakaa na kila siku anahitaji yabadilishwe apewe mapya.

Japo Sulemani alikuwa anaoga kila siku lakini aliishia kutoa jasho lakini maua hayana historia ya kuoga lakini yanatoa harufu nzuri miilini mwao, ambazo ndio hizo wanadamu hutumia kujinakshi miili yao na majumba yao na kutengenezea marhamu mbali mbali…Kwa Hapo Sulemani ameachwa mbali sana na maua ya kondeni.

Lakini nataka nikuambie, hata wewe utajiri wako, au mali zako, au UMASKINI wako hauwezi kumsaidia Mungu, kukupendezesha au kukufanya mpya zaidi na kuvutia.. Fahamu tu ukipenda kudumu katika kuutafuta ufalme wake basi, lile Neno “Je! hatazidi sana kuwavika ninyi enyi wa imani haba” litakuwa ni la kwako, iwe ni katika uchache au katika wingi..

Mfano mwingine tena ni huu…

Mathayo 7:11 “Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?”.

Watoto wetu wakituomba, tuchukulie mfano baiskeli tutafanya juu chini kwenda kuwanunulia…hata kama hakitakuja kwa wakati husika lakini kwa jinsi wanavyoendelea kusumbua tutafanya juu chini tuwanunulie tu hata kwa kukopa au kujichanga…

Sasa kama wewe unaelewa hali ya mwanao, kwanini yeye Mungu wetu wa mbinguni asielewe yako?, mpaka unapaniki na kuogopa na kukosa raha ya maisha kama vile yeye sikio lake ni zito, yupo mbali hakuoni wala hakusikii.. Nataka nikuambie huna haja ya kufunga na kuomba juu ya hilo, Mungu yupo “very sensitive, more than any living creature on Earth or Heaven”..Anao upeo mpana wa kufikiri na kuhisi mambo kuliko wewe unavyodhani, anaweza kuhisi tatizo lako ni lipi kabla hata halijaingia akilini mwako. Biblia inalithibitisha hilo.

Mathayo 6: 7 “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

8 Basi msifanane na hao; MAANA BABA YENU ANAJUA MNAYOHITAJI KABLA NINYI HAMJAMWOMBA”.

Unaona?, Anajua hata unalokwenda kumwomba wiki ijayo,,, ashindweje kujua taabu au shida unayopitia sasa hivi, anajua unaumwa na unateseka katika magonjwa na unahitaji kupona, analijua hilo, anafahamu una haja na kuwa na maisha mazuri anajua, anajua unahitaji kuolewa na umri umeshakwenda, anajua unahitaji pesa uvae nguo nzuri upendeze, anajua unahitaji uishi katika nyumba yako mwenyewe uwe na uhuru wako binafsi, anajua kwasasa ungependa uwe na usafiri wako,,..anafahamu hayo yote…Lakini unajiuliza inakuwaje sasa?

Sasa sikiliza hekima zake zinavyomalizia na kusema..

Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33 BALI UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE, NA HAKI YAKE; NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA.

34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.

Anasema Utafute kwanza ufalme wake…rafiki, tamani kumjua kwanza Mungu maishani mwako, tamani kufahamu hukumu zake na mapenzi yake kwako,..Weka mambo yako ya wokovu wako sawa sasa, uwe unahukika kwamba hata leo ukifa Mbingu ni yako, uwe na uhakika kwanza hata unyakuo ukipita leo usiku wewe utakuwa wa kwanza kuisikia sauti ya Bwana Yesu ikikuita mawinguni…Na kisha hayo mengine mwachie yeye atamalizana nayo.. NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA.

Fahamu kuwa Mungu anazo akili timamu zaidi ya unavyofikiri.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

JE! UMEFUNDISHWA?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.

TOA HUDUMA ILIYO BORA.

WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA


Rudi Nyumbani

Print this post

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

Musa alipewa maagizo na Mungu atengeneze nyoka wa shaba, amning’inize ili wale wote waliomuasi Bwana watakapomtazama nyoka Yule wapone saa ile ile.

Hesabu 21: 8 ‘’Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.

Lakini Mungu hakuwahi kuwaagiza Wana wa Israeli kuwa wakati wowote watakapokutana na madhara au matatizo basi wamsimamishe nyoka wa shaba wamtazame ili wapone, hakuwahi kufanya hivyo, lakini wana wa Israeli walitazama wakagandua SIRI ndani yake, wakasema ni lazima kutakuwa na uponyaji Fulani kwenye nyoka wa shaba kama sivyo Mungu asingemwagiza Musa kuiunda, hivyo ngoja tujijengee utaratibu wetu, wa kuifanyia ibada, na kumwomba Mungu kupitia ile naye Mungu atatusikia dua zetu..

Hivyo hilo jambo lilikuja kuendelea hivyo kwa mamia ya miaka mbeleni, mpaka likajengewa madhabahu kubwa na kuwa jambo maarufu sana Israeli, watu wakawa wanakwenda kuiinamia ile sanamu ya nyoka na kumwomba Mungu wa Israeli kupitia ile awaponye matatizo yao, wakaifukizia uvumba..

Hawakujua hilo lilikuwa ni chukizo kubwa sana kwa Mungu ndilo lililowapelekea hata kukumbana na matatizo yote yale ikiwemo kuchukuliwa utumwani tena.. Ndipo sasa baada ya miaka mingi sana kupita akatokea mfalme mmoja anayeitwa Hezekia yeye ndiye aliyefanikiwa kuliona hilo chukizo mara moja, Tusome:

2 WAFALME: 18:1 ‘’Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.

2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.

3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake.

4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ILE NYOKA YA SHABA ALIYOIFANYA MUSA; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake NEHUSHTANI

5 Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia’’.

Embu jaribu kutafakari kwa utulivu uone kitu hapo! AGIZO lilikuwa ni la Mungu mwenyewe lakini sasa linageuka kuwa kitanzi na kikwazo kikubwa sana kwa watu…Tunaweza kuwalaumu wale tukasema walipungukiwa na akili lakini nataka nikuambie sisi wa kizazi hiki ndio tuliopungukiwa akili zaidi ya wale..Tutaona ni kwa namna gani tunafanya makubwa zaidi ya wao.

Mungu alimwagiza Musa achonge nyoka wa shaba kama ISHARA tu! ya kitu Fulani tu rohoni, nacho ndicho tunakuja kukiona sisi watu wa agano jipya, kuwa tendo lile Mungu aliliruhusu lifanyike vile kumfunua Bwana wetu Yesu Kristo atakapotundikwa msalabani kwamba kila mtu atakayemwamini aokolewe, hilo tunalithibitisha kwa maneno yake mwenyewe..

Yohana 3:14 ‘’Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye’’.

… lakini hakukuwa na kitu chochote cha maana ndani ya ile SHABA, uponyaji halisi haukuwa ndani ya shaba ile bali ulitoka kwa Mungu mwenyewe..matokeo yake watu wakaacha kumtazama Mungu ambaye ni mponyaji wao wakaigeukia shaba isiyoweza kusema, wala kunena, wala kuzungumza..

Leo hii tunajua ni kweli Mungu alimwagiza Elisha achukue CHUMVI na kuitia katika chemchemi ya maji iliyokuwa inazaa mapooza..Na baadaye maji yale yakawa matamu,.Lakini kumbuka sio chumvi iliyotibu maji bali ni Mungu ndiye aliyefanya vile, lakini ni kwanini leo hii tunaihusisha chumvi na mambo ya ibada ikiwa hatujaongozwa kuitumia?.Nasi tunasema vile vile kama wana wa Israeli, Mungu kaweka uponyaji wa kiungu ndani ya chumvi,..tunasema kuna nguvu fulani ndani ya chumvi kama sivyo kwanini Mungu alimwagiza Elisha aiweke katika maji?…Tunamtia Mungu wivu pasipo sisi kujijua..

Halikadhalika tunayapa MAJI heshima, na kusema maji yana nguvu ya kusafisha mtu ndani yake, na kumtakasa, Tunamweka nyuma Mungu tunayapa maji heshima, ndugu Huko ni sawa kuiabudu sanamu ya Shaba.

Vivyo hivyo na vitu vingine vyote, tunasema UDONGO unabeba uhai, kwahiyo tukiumwaga kwenye biashara zetu, utazifufua, huku tukishikilia kile Bwana Yesu alichokifanya alipotengeneza TOPE ardhini na kumpaka Yule kipofu machoni, na macho yake kufumbuka, tunasema kama udongo usingekuwa na uponyaji Fulani Yesu asingeagizwa kutengeneza tope na kumpa kipofu..na kibaya zaidi mpaka tumeshavipa majina kama VITENDEA KAZI VYA KIROHO.

Tunahusisha MISALABA katika Ibada zetu. Kama unapenda msalaba wako kwanini usiunig’inize nyumbani kwako kama kumbukumbu lako la Bwana kukufia msalabani, lakini ni kwanini unakwenda kuuinamia, kuomba kupitia huo, unadhani unampa Mungu heshima hujui kuwa ni ASHERA hilo umeiweka moyoni mwako.

Na mambo mengine mengi, tunayafanya hatujui kuwa ndivyo tunavyomtia Mungu wivu. Fumbua macho yako, utoke kwenye uchanga wa kiroho, ikiwa Mungu amekuongoza kutumia mojawapo ya vitu hivyo kama ishara ya kitu Mungu anachokifanya rohoni ni sawa, kama amekuongoza kutumia maji tumia, amekuongoza kutumia mafuta tumia, na uthibitisho wa kuwa umeongozwa na Mungu kufanya hivyo, ni kwamba hakitakuwa unakirudia rudia,….Elisha halikuwa hatumii chumvi kila tatizo linalokuja mbele yake…Wala sio kila mgonjwa aliyekuja mbele yake alikuwa anamwambia akaoge mto Yordani mara saba. Alikuwa anafanya vile pale alipokuwa anaongozwa tu! Na sisi tunapaswa tuwe hivyo hivyo.

lakini kama tunageuza Imani yetu kutoka katika nguvu ya uweza wa DAMU YA YESU inayoweza kufuta na kuondoa kila kitu na kuvipa vitu hivyo visivyo na uhai heshima Fulani ya kiroho kwamba vina nguvu Fulani au uwezo Fulani wa wa kusababisha mambo, basi tujue moja kwa moja tunamfanyia ibada shetani. Na Mungu anachukizwa nazo kupindukia kwa namna ile ile anavyochukizwa na waabudu baali na Jua.

Na madhara yake ni kwamba, Mungu atatupiga kwa kukosa kwetu maarifa, wakati mwingine badala ya tatizo kuisha ndivyo litakavyoongezeka, kwasababu biblia inasema ni heri ungekutana na ghadhabu ya Mungu kuliko WIVU wake, na ibada zote za sanamu zinaleta wivu mbele za Mungu.

Mithali 27:4 ‘Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya WIVU’.

Wimbo uliobora 8: 6“………….wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.”

Huu ni wakati wa kutubu (yaani kugeuka), na kumwabudu yeye katika Roho na Kweli.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele. Amin.

 Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa  Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312



Mada Zinazoendana:

FIMBO YA HARUNI!

HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.

 Shalom. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Neno la Kristo linasema:

1 Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume, KAENI NA WAKE ZENU KWA AKILI; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”

Agizo hilo biblia iliyotoa linawahusu wanaume waliooa , na si kila mwanamume tu!..kwasababu utasikia mtu ambaye anaishi na mwanamke ambaye hawajaoana, au anaishi na mwanamke ambaye si mke wake, bali ni mke wa mtu mwingine…. anakwambia… “Biblia imetuambia tuishi na wake zetu kwa akili”… nataka nikuambia ndugu hapo utakuwa huishi kwa akili, bali kwa kukosa akili…kwasababu mtakuwa mnafanya uzinzi na uasherati! Utasema hilo lipo wapi katika maandiko

Mithali 6: 32 “Mtu aziniye na MWANAMKE HANA AKILI KABISA; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika”.

Umeona? Akili inayozungumziwa hapo?..sio akili ya kuwa beberu ndani ya nyumba, au kuchepuka.. Ikiwa na maana kuwa moja wapo ya akili anazotakiwa mwanamume awe nazo anapoishi na mke wake ndio hiyo… “ KUWA MWAMINIFU KATIKA NDOA YAKE KWA KUJIEPUSHA NA ZINAA NJE YA NDOA YAKE”.

Kwasababu biblia inasema mtu aziniye na mwanamke atapata jeraha na kujivunjiwa heshima yake..itakufaidia nini unafanya zinaa nje ya ndoa yako halafu siku moja unafumaniwa na watu wanaanza kukunyooshea kidole?..hapo utakuwa umefanya jambo la kipumbavu, na biblia inasema fedheha yako haitafutika..Ni doa la daima.

Na hiyo AKILI ya kushinda, uasherati inakuja kwa kumwamini Yesu Kristo tu!, na kuoshwa dhambi zako kwa damu yake na kufanyika kiumbe kipya…haiji kwa kuongeza mke wa pili au watatu…Yesu pekee ndiye atakayeweza kukuondolea kiu ya mambo yote machafu ya ulimwengu huu.

⏩Maana nyingine ya kuishi na mke kwa akili, ni kumpenda na kumjali, upendo husitiri mambo mengi sana..Na hakuna mtu anayechukia kupendwa, kwahiyo upendo wa kweli na wa dhati ukiwepo hakuna matatizo yoyote yatakayojitokeza katika maisha ya ndoa..kutakuwa siku zote ni furaha, hiyo nayo ni akili.

⏩Maana nyingine ya kuishi na mke kwa akili, ni kugundua kasoro zake, na mapungufu yake, na kujua namna ya kuyatatua hayo ki BIBLIA!..Zingatia hilo neno KI BIBLIA! Sio kwa kutumia hekima za waswahili, au wasanii, au mila, au marafiki hapana! Bali biblia…epuka sana kutafuta suluhisho la “wahenga walisema”..au “wazee wazamani walisema” au “watu wanasemaga”…badala yake ni lazima UJIFUNZE kutafuta suluhisho kutoka kwenye Biblia(Maandiko matakatifu). Hekima za watu wa ulimwengu huu, zinafaa kwa baadhi ya mambo lakini si yote! Asilimia kubwa ya hekima za dunia hii zinazoshauri kuhusu masuala ya ndoa zinapotosha nyingi ni za Yule adui.

Kwahiyo hapo, ni lazima MWANAMUME ulijue NENO LA MUNGU kwa wingi ndani yako, hiyo ndio AKILI ya kuishi na mke wako?.

⏩Na maana ya mwisho ya kuishi kwa akili ni kuishi kwa Malengo Fulani ya kimaisha, ambayo hayakinzani na Neno la Mungu, hapa ndio linakuja suala la kupanga maisha na namna ya kujiongezea kipato kwa kazi zinazompa Mungu utukufu na mambo yote yanayofanana na hayo kwa ajili ya maisha mazuri ya familia.

⏩Lakini pia kumbuka Neno la Mungu halijamzuia pia mwanamke kuishi na mwanamume kwa akili, kwasababu na yeye kapewa akili vile vile, nanapaswa na yeye pia aishi na mume wake kwa akili, Kwa kujiepusha na zinaa na mambo yote tuliyojifunza hapo juu.

Pia wewe kama mwanamke soma vifungu hivi vitakusaidi kujua mwanamke mwenye akili kibiblia ni yupi..si yule wa kukaa vibarazani na kuwasema watu.

Mithali 31: 10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.

11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.

15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.

16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.

18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.

19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.

20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.

21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.

22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.

23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.

26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.

27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,

29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.

30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa. 31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225683036618/ +225789001312



Mada Zinazoendana:

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

NINI TOFAUTI KATI YA UZINZI NA UASHERATI ?


Rudi Nyumbani

Print this post

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

Ukisoma vitabu vya Injili utaona mfano wa kwanza kabisa BWANA YESU alioutoa ni ule mfano wa Mpanzi, utaona jinsi mpanzi alivyotoka na kwenda kupanda mbegu zake, ukiendelea kusoma pale utagundua kuwa ule mfano haukueleweka kwa wengi, sio tu kwa makutano bali pia kwa wanafunzi wake..Lakini walipomfuata na kumwomba awafafanulie kuna kauli Bwana Yesu aliitoa pale nataka tuione; nayo ni hii:

Marko 4.13 ‘Akawaambia, Hamjui mfano huu? BASI MIFANO YOTE MTAITAMBUAJE?’.

Tafakari hilo Neno, BASI MIFANO YOTE MTAITAMBUAJE?..Kumbe Mfano huo ni msingi wa kuielewa na mifano mingine yote iliyobakia, kwa watu wanaofahamu somo la Hisabati vizuri wanaelewa kuwa kanuni ya PAI π..Ni kiungo kikuu cha Hisabati, ukitaka kutafuata Eneo la kitu chochote kile iwe ni duara au tufe, pipa, n.k. basi PAI ni lazima itumike.

Vivyo hivyo tukirudi kwenye maandiko ili kuielewa mifano yote Yesu aliyokuwa anaifundisha kuhusiana na ufalme wa mbinguni basi tafsiri ya mfano ule wa Mpanzi ni lazima kuulewa vinginevyo hutaambulia chochote.

Sasa tukirudi katika huo mfano kwa kuwa unajulikana hatutaweza kuuleza wote hapa, lakini mpanzi Yule alipotoka kwenda shambani malengo yake yalikuwa ni mbegu zake zote zimee vizuri na kuzaa nyingine 30, nyingine 60, nyingine 100. Lakini tunasoma zilikumbana na changamoto kadhaa kabla ya kufikia hatua ya kuzaa matunda.

Sasa kabla hatujafika mbali nataka tuone mifano miwili iliyofuata mbele yake baada ya huo..Ili itusaidie kuunga kiini cha somo letu la leo vizuri ..

Tusome..

Marko 4:26 ‘Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;

27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye.

28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.

29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.

30 Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani?

31 Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi,

32 lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.

33 Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia’.

AMEN.

Sasa Nataka tuichukue kwa pamoja mifano hii mitatu, tuunde kitu ambacho kitatusaidia wote,..Mifano hii, yote inaonyesha historia ya mbegu, jinsi zilipotoka na jinsi zilivyoishia isipokuwa katika TABIA tofauti tofauti na mapito tofauti tofauti.

Kumbuka kule nyumba kabisa kwenye mfano wa mpanzi Bwana Yesu alitoa tafsiri ya Ile mbegu kuwa lile ni NENO LA Mungu (Luka 8:11) lililopandwa ndani ya moyo wa mtu. Hivyo Neno la Mungu linapopandwa katika moyo wa mtu katika hatua za awali penda lisipende litapita katika nyakati TATU kulingana na mifano hiyo mitatu.

1) ⏩Kwanza ni lazima lipitie changamoto: Mtu aliyepandwa atakumbana na udhia, na misongo ya hapa na pale, kulingana na ule mfano wa mpanzi, Hili ni jukumu la mhusika mwenyewe kuhakikisha kuwa haling’olewi na Yule adui, wala halisongwi.

2)⏩ Pili Litakuwa linamea lenyewe: Hili sio jukumu tena la mtu, bali ni jukumu la Mungu mwenyewe, wakati linavumilia vipindi vigumu vya hatihati ya kung’olewa au kusongwa, huku kwa nyuma siku baada ya siku linakuwa lenyewe taratibu.

3) ⏩Na Tatu japo litaanzia katika udogo sana, likishafikia ukomavu litakuwa kubwa kuliko miti mingine yote. Hivyo mwisho wa safari ya utunzaji wa mbegu ile. Basi litakuwa baraka kubwa sana kuliko chochote kile duniani.

Hivyo ndugu, ndio maana sasa baada ya mifano ya namna hiyo kuisha YESU akaanza kuwafundisha watu mifano inayoelezea thamani ya mbegu hiyo akiifananisha na Hazina kubwa sana na lulu za thamani ..utaona anasema, ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara aliyekuwa anatafuta Lulu ya thamani kubwa, na alipoina akaenda kuuza vyote alivyonavyo na kwenda kuinunua lulu ile, anasema tena ni sawa na mtu aliyeona hazina iliyositirika katika shamba, alipoiona akaificha na kwa furaha akaenda kuuza vyote alivyonavyo na kwenda kulinunua shamba lile.

Hiyo yote ni kuonyesha kuwa ana AKILI sana mtu yule anayelisikia Neno la Mungu na kuzingatia kuliweka moyoni mwake, na kwenda kufanyia kazi kile anachofundishwa, anafanya bidii kulifakari Neno la Mungu, analiona kama almasi, anatafuta huku na kule huku akilinganisha na maandiko, akivulimilia dhiki zote zinazokuja kutokana na ukristo wake na itikadi zake kali za kuliishi Neno, na shutuma na kuchekwa, na kudharauliwa, na kutengwa, na kuchukiwa, akivumilia yote bila kuliacha hilo Neno lililopandwa moyoni mwake kudondoka, akihakikisha shughuli za ulimwengu huu hazimsongi mpaka anakosa muda wa kuwa karibu na Mungu wake, akihakikisha anapata muda mrefu wa kulitafakari Neno la Mungu kuliko kuchati..

Sasa Biblia inaeleza mtu huyo kuna faida kubwa inamngoja mbeleni yake.. Yeye kwa wakati huo hatajua chochote, wala hatafahamu kama kuna kitu kinakuwa ndani yake, anaweza kuona kama anafanya kitu ambacho hakimletei faida yoyote katika mwili, hakimwingizii pesa, hakimpi umaarufu, lakini kumbe kidogo kidogo, ile mbegu inamea, kutoka KUWA MBEGU MPAKA JANI MPAKA SUKE.. Na japo ilianza ndogo sana kama chembe ya haradali itakuwa yenyewe, kumbuka haihitaji msaada wowote kukuzwa na mtu, itakuwa na kuwa kubwa kuliko miti yote, na ndipo hapo watu watakuja kushangaa, kumetokea nini kwa mtu huyu tusiyemtazamia amekuwa hivi ghafla…Ndipo kama mfano unavyosema ndege watakuja kukaa chini ya huo mti, ndivyo itakavyokuwa kwa mtu huyo, atakuja kuwa msaada mkubwa kwa watu wengi kwa kila kitu. Kwa vitu vya rohoni na mwilini.

Hiyo ilimtokea kiongozi wetu mkuu YESU KRISTO, Biblia inasema alikuwa ni mtu wa kudharauliwa, wa kutokuaminiwa siku zote, lakini yeye alilitunza Neno la Mungu tangu utoto wake, mpaka utu uzima, mpaka alipofikia kilele sasa cha Neno lenyewe kutaka kuanza kuzaa matunda, ndipo walipomtambua kuwa Yule hakuwa mwanadamu wa kawaida..Utasoma pale walianza kujiuliza huyu sio Yule seremala, na ndugu zake tunao wote hapa? Sasa katolea wapi hekima yote hii ambayo hajasoma, na miujiza yote hii, ulimwengu mzima ulimfuata kumsikiliza, yeye ni nani hasa? Ukisoma biblia utaona kuna watu walitoka mpaka Uyunani huko kuja kutaka kumwona Bwana Yesu…Hayo ndio maajabu ya Neno la Mungu likitunzwa vizuri ndani ya mtu…Linafanya mambo makubwa, na ndio maana shetani katika hatua za kwanza atahakikisha kwa bidii zote analiondoa ndani yako.

Hizi ni siri kutoka kwa MKUU wetu YESU KRISTO, Kwamba kama na sisi tukizitumia, tutafika pale alipo yeye. Leo hii, mbegu nyingi zinatupwa ndani yako, unazidharau, kwasababu labda mtu huyo anayekuhubiria hajulikani, ni mtu tu wa mtaani unayemfahamu, lakini kumbuka ufalme wa Mungu ndani ya mtu unaanza kama chembe ya haradali, ndogo sana, maneno ambayo mtumishi yoyote yule wa kawaida anaweza akayabeba ndani yake, inaanza kwa maneno machache sana ya wokovu, ambayo baadaye yakiisha kukua ndani ya mtu yanaweza kuupindia ulimwengu mzima.. Usipuuzie Neno la Mungu leo unapolisikia, embu chukua hatua ya kuanza kulitunza, anza kulifanyia kazi, hakikisha shetani hakichukui hichi ulichokisia moyoni mwako, na dalili zitakazoonyesha hiyo mbegu inakuwa ni maadui kutokea, shetani atafanya juu chini kuing’oa lakini wewe zingatia kanuni hizo, UVUMILIE yote, iwe ni dhiki, iwe ni misongo ya mambo ya ulimwengu huu..Fanya bidii kulitunza Neno la Mungu, faida yake utaiona baada ya muda Fulani.

Ni matumaini yangu, utatubu leo na kumkabidhi Bwana maisha yako. Huo ndio mwanzo wa kuitunza mbegu yao.

Ubarikiwe sana.

Amen.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312


Mada Zinazoendana:

JE! WEWE NI MBEGU HALISI?

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.

TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

Shalom, Mwana wa Mungu karibu tujifunze maandiko…Leo tutajifunza kwa Neema za Bwana namna ya kuokoa roho.

Bwana Yesu alisema “sikuja kuziangamiza roho bali kuziokoa (Luka 9:56)” sentensi hiyo aliisema baada ya wanafunzi wake kumwomba ashushe moto uwaangamiza wale watu wa Samaria waliokataa kumpokea…Lakini kwanini alisema vile kuwa hakuja kuziangamiza bali kuziokoa?…ni kwasababu alikuwa na uwezo wa kuziangamiza lakini hakutaka kufanya vile..kinyume chake alitafuta namna ya kuwafikishia wokovu na sio kuwaua.

Wakati mwingine tunaweza tukawa na silaha mikononi mwetu au midomoni mwetu tulizopewa na Mungu kihalali kabisa za kujeruhi na kuangusha watu wote wanaokwenda kinyume na sisi..lakini tukikosa hekima kama aliyokuwa nayo Bwana tutajikuta tunaangamiza roho badala ya kuokoa.

Hebu mtafakari Musa, wakati wana wa Israeli wanamkosea Mungu kule jangwani…Mungu alimwambia Musa ajitenge na wale watu ili apate kuwaangamiza…na atamfanya Musa kuwa Taifa kubwa, atampa uzao utakaoirithi nchi….ingekuwa ni mmojawapo wa sisi tungesema asante Mungu, kwa kuwa umeteta nao wanaoteta nami, lakini tunaona Musa, alilipindua wazo la Mungu na kuanza kuwaombea msamaha ndugu zake na kuwatafutia upatanisho na Mungu, na Mungu akalisikiliza ushauri wa Musa na kughairi mawazo yake…

Sasa tuchukulie mfano Musa, angekubali kujitenga nao, unadhani, kulikuwa kuna kosa lolote pale? hapana Mungu kweli angewaangamiza wale watu na angeenda kumfanya Musa kuwa Taifa kubwa kama alivyomwahidia..Lakini Musa angekuwa hajatenda kwa busara mashauri yale yalitoka kweli kwa Mungu, angekuwa hajastahili kuwa kiongozi bora kwasababu hakuizuia ghadhabu ya Mungu juu ya watu wake. Kwahiyo pengine hata Mungu asingemtukuza Musa kwa kiwango hichi alichomtukuza sasa.

Kutoka 32:9 “Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu

10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.

11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?

12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.

13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.

14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake”.

Kwahiyo hiyo inatufundisha kuwa siyo kila fursa au mamlaka tunayopewa na Mungu, tuyatumie tu bila kutafakari vizuri..Mungu wetu hajatuumba kama maroboti kwamba yeye ni wa kusema na sisi ni wakufuata tu pasipo kutafakari..hapana! huo ni utumwa na sisi sio watumwa sisi ni wana, tunazungumza na Baba yetu na kushauriana naye…ametuumba tuzungumze naye, tusemezane naye, tupeane naye mashauri.

Isaya 1: 18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”.

Ndio maana Musa alisemezana na Bwana na akasafisha dhambi za wana wa Israeli zilizokuwa nyekundu kama bendera, na akazifanya kuwa nyeupe kama sufu. Haleluya!

Mungu anaweza kumweka mtu anayekuchukia, au anayekupiga vita mikononi mwako, au mtu ambaye alikufanyia visa Fulani, ukapata madhara fulani…Mungu anaweza kumweka mikononi mwako kiasi kwamba ukisema tu neno moja umemmaliza, au ukifanya jambo Fulani tu, habari yake imekwisha ikawa ni kweli Mungu kamtia mikononi mwako ili kumlipizia kisasi, kwa ubaya aliokufanyia….kama vile Mungu alivyomtia Sauli mikononi mwa Daudi..akajua kabisa hii ni fursa ya kummaliza lakini hakufanya hivyo…nasi pia huo usiwe wakati wa kummaliza, badala yake uitumie fursa hiyo kumgeuza kwa Kristo, huo ndio wakati wa kusemezana na Bwana juu ya dhambi zake zote, na kumwombea Msamaha…hakika ukifanya hivyo na kuigeuza hasira ya Bwana, Bwana atakupenda zaidi ya anavyokupenda sasa…atakutukuza zaidi ya anavyokutukuza sasa…

Utasema hiyo habari ya Musa na Daudi ilikuwa ni ya agano la kale, vipi kuhusu agano jipya, je! Kuna mtu yeyote alishawahi kufanya hivyo..Jibu ni ndio! Hata katika agano jipya tunayo hiyo mifano.

Tunasoma habari za Paulo na wenzake, wakati mmoja walipokwenda Makedonia kuhubiri, walikutana na mtu mwenye pepo na walipomtoa Yule pepo, ndipo wakuu wa mji wakawakamata na kuwachapa bakora na kisha kuwatupa gerezani.

Sasa lile jambo halikumpendeza sana Mungu, na hivyo Bwana akawatengenezea njia ya kutoka mule gerezani, akamtuma malaika wake usiku ule wakati Paulo na Sila walipokuwa wanamsifu Mungu, ghafla vifungo vikalegea na milango ya gereza ikafunguka…sasa Lengo la Yule malaika kufungua milango ya gereza haikuwa tu kuwafurahisha wale watu , hapana ilikuwa ni ili Paulo na Sila watoke!!, waondoke mule gerezani,..Kama vile Yule malaika alivyomtoa Petro gerezani wakati Fulani alipokuwa amefungwa.

Lakini tunasoma Paulo na Sila walilitengua agizo la Bwana, badala ya kutoka na kwenda zao, waliendelea kukaa mule gerezani japokuwa Mungu aliwafungulia mlango wa kutoka…lakini walitafakari mara mbili mbili, endapo tukitoka na kwenda zetu tutakuwa kweli hatujatenda dhambi lakini tutaacha madhara makubwa huku nyuma, tutasababisha kifo badala ya kuokoa roho, na zamani zile utawala wa Rumi, mfungwa yoyote akitoroka kinachobakia kwake ni kifo tu, na ndio maana Yule askari ilikuwa nusu ajiue, lakini Paulo na Sila wakamzuia.

kwahiyo wakaitumia ile nafasi sio kwa faida yao bali kwa faida ya wengine, ndio tunaona wakaenda kumwuhubiria Yule askari injili pamoja na familia yake wote wakaokoka, na mwisho wa siku kesho yake asubuhi wakatolewa gerezani, kwahiyo ikawa faida kwao mara mbili.

Matendo 16: 22 “Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.

23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.

24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.

25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

26 GHAFULA PAKAWA TETEMEKO KUU LA NCHI, HATA MISINGI YA GEREZA IKATIKISIKA, NA MARA HIYO MILANGO IKAFUNGUKA, VIFUNGO VYA WOTE VIKALEGEZWA.

27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia

28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.

29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.

33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.

34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.

35 Kulipopambauka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.

36 Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Makadhi wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani”.

Sasa hebu fikiri endapo Paulo na Sila wangeondoka usiku ule mule gerezani, na kusema safi sana! Mungu katupigania! Kawaaibisha maadui zetu!…. ni wazi kuwa wangeshampoteza Askari na kusudi la wao kwenda makedonia lingekuwa ni sifuri kwa maana wenyewe walikwenda kwa nia ya kuhubiri injili, na sasa hapa ni sawa na wamemsababishia wengine mauti.

Kwahiyo ndugu tunajifunza, sio kila fursa ya kumpiga adui yako ni mapenzi kamili ya Mungu, sio kila mlango Mungu anaokufungulia ni wa kuutumia pasipo kutafakari, aliyekutukana, aliyekuaibisha, aliyekupiga, aliyekunyima kazi wakati Fulani tena akakufanyia na visa juu, aliyekurusha, aliyekuharibia mipango yako na maisha yako, sasa Mungu kamleta mikononi mwako..huo sio wakati wa kuitumia hiyo fursa Mungu aliyokuwekea mbele yako pasipo hekima!! Itumie hiyo KUOKOA ROHO, BADALA YA KUANGAMIZA. Hicho ndio kitu Mungu anachotaka kuona kwetu!.

Kuna muhubiri mmoja, ambaye alikuwa ni Nabii, siku moja wakati anahubiri kanisani kwake malaika wa Bwana alimwambia atazame mwisho kabisa wa kanisa, na alipotazama akaona watu wawili kwa mbali mwanamume na mwanamke wanafanya kitendo kichafu cha kunyonyana ndimi na hiyo ilikuwa ni katikati ya ibada…Yule muhubiri akakasirika sana, akawa anawaendea…wakati yupo njiani anawaendea Yule malaika aliyemwambia atazame nyuma ya kanisa, huyo huyo akamwambia sema Neno lolote na mimi nitalitimiza hilo neno saa hivi hivi kama ulivyosema…yaani maana yake angesema “Bwana naomba waanguke sasa hivi wafe, wangekufa saa ile ile”..na alipofika pale Yule muhubiri..kitu fulani kikamwingia ndani yake, kama huruma Fulani hivi… akasema “nimewasamehe”…Baadaye alivyomaliza ibada, sauti ikazungumza ndani ya moyo wake na kumwambia..”hicho ndio nilichokuwa nataka kusikia kutoka kwako”…msamaha…

Ni wazi kuwa hao watu kwa msamaha huo, baadaye walitubu na kumgeukia Mungu kwa kumaanisha.

Umeona? Epuka injili unazohubiriwa kila wakati piga adui yako, usiposamehe kuna wakati nawe utafika utamkosea Mungu, naye Mungu hatakusamehe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Print this post

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!

Kutoka 20:7 “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure..”

Hii ni moja ya amri tulioizoea sana, Na tumekuwa tukidhani kulitaja jina la Mungu bure ni pale tu tunapo muhusisha na mambo yasiyo na maana, au pale tunapo apa, lakini hiyo ni sehemu mojawapo ya kulitaja bure jina la Mungu, ipo sehemu nyingine ambayo ni kuu zaidi, na inamuudhi Mungu sana, pengine na wewe ulishawahi kuifanya bila kujua na pengine ndio imekuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio ya roho yako.

Pale unaposema leo nimeamua kuwa Mkristo nimeamua kumfuata Mungu kwa moyo wangu wote, pale unaposema maisha yangu ya kale basi, hapo ni sawa na umemwita Mungu aje kuyaongoza maisha yako kuanzia huo wakati na kuendelea, au kwa lugha ki-kibiblia tunasema umeliitia jina la Mungu lije kukuokoa, lakini pale unaposema Nimeokoka, mimi ni mkristo halafu, unaendelea kuyafanya yale yale uliyoyaacha kule nyuma, unaendelea kuiba,unazidi kuzini, unatazama pornography, unasengenya n.k. Hapo ni sawa kabisa na umemdhahaki Mungu kwamba ulimwita akuokoe na kumbe haupo tayari kuokolewa, Hapo umelitaja JINA LA MUNGU wako bure!.. Ni heri usingedhubutu kuujaribu wokovu kabisa maishani mwako ..

Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona watu walioanza kumtafuta Mungu, biblia imetafsiri kama “waliliita au wanalitaja Jina la Mungu”

Mwanzo 4: 25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.

26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA”.

Utaona pia katika maandiko BWANA akitangaza jina lake yeye mwenyewe…utaona halitaji jina lake kama YEHOVA, bali analitaja jina lake kama TABIA..Tunalisoma hilo katika kitabu cha Kutoka.

Kutoka 34: 5 “Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, AKALITANGAZA JINA LA BWANA.

6 Bwana akapita mbele yake, AKATANGAZA, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; WALA SI MWENYE KUMHESABIA MTU MWOVU KUWA HANA HATIA KAMWE; MWENYE KUWAPATILIZA WATOTO UOVU WA BABA ZAO, NA WANA WA WANA WAO PIA, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE”.

Unaona mstari wa saba hapo?…tafsiri ya jina lake sio tu Mungu mwenye huruma bali pia ni MUNGU asiyeacha kumwesabia mtu mwovu kuwa hana makosa kamwe. Kwahiyo unapompokea Kristo maishani mwako halafu maisha yako yapo vilevile hayabadiliki…Hapo ni sawa na umelitaja jina Bwana Mungu wako Bure na atakuhesabia kuwa na hatia kwa hilo.

Embu tafakari mfano huu halafu wewe uhukumu, ni sawa na leo mtu ameagiza gari nje ya nchi labda tuseme Japan kwa makubaliano ya kuwa siku litakapofika ndipo atalilipa..Lakini siku linafika ili akabidhiwe gari lake afanye malipo biashara iishe, anageuka na kusema mimi sina haja na hilo gari kwanza nilikuwa ninawatania tu, labda siku nyingine nikiwa tayari.

Wewe unadhani, wale watu watamfanyaje?. Ni dhahiri kuwa hawawezi kumwacha hivi hivi waingie hasara kwa ajili ya uzembe wake, hivyo hapo kama hatatozwa faini, basi atafunguliwa mashtaka mahakani, na mwisho wa siku lazima atajikuta analipa mpaka senti ya mwisho kwa njia yoyote ile,…Na ndivyo ilivyo kwa Mungu, tunapolitaja jina lake, (JINA LA YESU ambalo hakuna jingine zaidi ya hilo ambalo litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo 4:12) lije lituokoe, tuonyeshe kweli kweli kutaka kuokolewa vinginevyo , Bwana hatutacha hivi hivi bila kutuhesabia kuwa wenye hatia..wakati mwingine mapigo au vifo vinatukuta kwa sababu hiyo.

Na ndio maana mtunzi wa Mithali alisema.. 30:8 “Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. 9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana NIKAIBA, NA KULITAJA BURE JINA LA MUNGU WANGU”.

Unaona huyu mtu alijua kabisa dhambi za wizi ni sawa na kulitaja jina la Mungu wake bure.

Na sisi pia kama tunalitaja jina la YESU mwokozi wetu kuwa ndio jina pekee linalotusababisha kuwa hivi tulivyo leo ndani ya wokovu basi na tuuweke ulimwengu mbali na sisi tumfuate Mungu wetu kweli kweli kwa kumaanisha..ili tujiepushe na laana, Kwasababu maandiko ndivyo yanavyotuonya.

2Timotheo 2:19 “..KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU”.

Jina la Kristo lisitamkwe kinywani mwako kama haupo tayari kuuacha ouvu..Na unaacha uovu kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutokuzifanya tena, na kisha kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO na lihimidiwe daima..

Amen.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312


Mada Zinazoendana:

JINA LA MUNGU NI LIPI?

JINA LAKO NI LA NANI?

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

KANUNI JUU YA KANUNI.


Rudi Nyumbani

Print this post

UTEKA ULIOGEUZWA.

Ukisoma kitabu cha Ayubu utagundua kuwa jaribu kubwa shetani alilomshambulia Ayubu halikuwa Kufiwa na wanawe au kupoteza mali zake zote ndani ya siku moja! Hayo kweli yalimuumiza sana…lakini utaona Ayubu hakuongea lolote kuhusu hayo…Alisema tu BWANA ALITOA na BWANA AMETWAA…Jina la Bwana libarikiwe. Basi akaishia hapo! Ndio maana unaona mpaka sura ya Pili habari ya Ayubu inakuwa imeshaisha…

Lakini kuanzia sura ya 3 hadi ya 42…utaona ni habari nyingine zinaanza kuzungumziwa hapo…utaona ni mazungumzo kati ya watu watatu mpaka wane…Ayubu, Sofari, Bildadi na Elifazi…akitoka huyu anaongea huyu, akitoka huyo sofari anaongea bildadi, akitoka bildadi anaongea Ayubu hivyo hivyo mpaka mpaka sura ya 40.

Sasa wengi wetu tunapenda kusoma tu ile sura ya kwanza na ya Pili tukidhani kuwa ndio lengo la kile kitabu cha Ayubu, lakini hiyo sio kweli..Ufunuo mkubwa wa kitabu cha Ayubu upo kuanzia ile sura ya 3 na kuendelea…kuanzia ile sura ya 3 na kuendelea ndio utaona jinsi gani shetani alivyokuwa anampepete Ayubu kwa kupitia vinywa vya wale marafiki zake watatu.

Utaona jinsi gani wale marafiki zake Ayubu, walivyokuwa wanatumia maandiko kuivunja imani ya Ayubu. Nakushauri ndugu kama hujakipitia kitabu cha Ayubu kuanzia hii sura ya 3 na kuendelea kafanya hivyo leo..Kuna mambo mengi sana Bwana atakuonyesha ambayo ulikuwa huyajui.

Shetani anakawaida ya kuwa..akishindwa kumjaribu mtu kwa njia ya kawaida ya nje! Huwa anabadilisha mbinu na kuja kwa njia nyingine ya kutumia maandiko, atawaingia hata wapendwa au hata wachungaji kukuhakikishia jambo Fulani ambalo sio sahihi, nia na madhumuni ni kukuangusha tu!. Ili kulielewa hili vizuri chukua mfano ufuatao.

Tuseme shetani anataka kumwangusha mtu anayeitwa Amelia aanguke kwenye dhambi ya uasherati. Atakachokifanya kama kawaida atatafuta kwanza kibali kutoka kwa Mungu, akishakipata ataanza kutikisa kwanza uchumi wake..ili amweke katika mazingira ya uhitaji wa fedha, wakati yupo katika hayo mazingira ya kuhitaji fedha anatokea mtu mwenye fedha nyingi kidogo na kumshawishi. Na atakaposhinda vile vishawishi na kumkataa Yule mtu…Shetani atamjaribu kwa njia nyingine, atamletea mpaka magonjwa ilimradi tu! Atafute njia mbadala ya kupata fedha kwa kuutoa mwili wake….Na endapo akimwona bado huyo mwanamke kasimama…atamjaribu kwa njia nyingine mbalimbali..Na mwishowe ataacha na kuingia kwenye mbinu yake ya mwisho na kuu kuliko zote ya kumwangusha.

Katika hiyo mbinu yake ya mwisho hatatumia tena watu wa nje kumshawishi, kwasababu anajua huyu dada Amelia amesimama hawezi kutikiswa na watu wasiomjua Mungu, atakachokifanya atamfuata kule kule kanisani kwasababu imani yake yote ipo katika nyumba ya Mungu na anawaamini watu wa Mungu.

Kwahiyo siku moja ataingia kanisani na kusikia mahubiri yafuatayo…. “kuna watu humu ndani wanachezea bahati, utakuta mtu anashida, Mungu anamfungulia mlango wa fedha anakataa, unakuta mtu ni mgonjwa, hana hela anakuja mtu anataka kumsaidia anakataa, kwa njia hiyo hata kuolewa hutaolewa..dada! na watu wote kanisani wanajibu Ameen!” Na huyo mtumishi atasoma mistari kadha kadhaa kwenye biblia kuthibitisha mahubiri yake.

Sasa kwa mahubiri kama hayo..huyu dada atatoka kanisani huku kuna kitu kinamuhukumu ndani,…anaanza kujitathimini pengine lile Neno lilikuwa linamhusu yeye…Ni watu wangapi wamekuja kumjaribu akawakataa…pengine kweli anachezea bahati! Akijiangalia ni kweli ana matatizo ya fedha, sasa Kidogo kidogo anaanza kushawishika na kuhisi alikuwa anafanya makosa kujiepusha na wale watu waliokuwa wanakuja kumjaribu, anaanza kufikiri pengine hata alikuwa anamkosea Mungu, hivyo baada ya siku kadhaa akitokea mwingine anaanza kumsikiliza na mwishowe kuanguka kwenye dhambi ya uasherati na kushindwa na shetani.

Hizo ndizo njia shetani anazozitumia kuwaangusha wengi waliosimama…Na ndio Ayubu naye yalimkuta hayo hayo…shetani alipoona hatetereki hata kwa msiba wa wanawe..akawaingia marafiki zake Ayubu watatu ambao nao pia walikuwa tunaweza kusema ni watumishi kama Ayubu, walikuwa wanamtafuta Mungu pamoja naye na kusali pamoja naye. Wakaanza kumwambia Ayubu, tatizo haliko kwa Mungu, tatizo lipo kwako, haiwezekani yakupate haya yote wewe tu na si mtu mwingine, lazima utakuwa umetenda dhambi kwahiyo nenda katubu! Ubadilishe na njia zako. Na walitumia maaandiko kumshawishi Ayubu ageuke aiache njia yake. Lakini tunaona Ayubu alisimama thabiti mpaka Mwisho na hatimaye Bwana akageuza uteka wake..

Sasa leo kwa Neema za Bwana hatutazungumzia sana juu ya huduma za hawa rafiki zake watatu Ayubu, kama utahitahi somo kwa urefu kuhusu huduma zao unaweza ukawasiliana na mimi inbox nikutumie somo hilo.

Lakini leo tutazungumzia ni kwa namna gani Bwana alimrejeshea Ayubu mali zake zote maradufu na familia yake. Kwa namna hiyo hiyo na sisi tunaweza kuzipata Baraka zetu maradufu endapo tukifanya kama Ayubu alivyofanya.

Ukisoma Mwishoni mwa kitabu cha Ayubu ile sura ya 42 tunasoma..

Ayubu 42: 7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.

8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.

9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu.

10 KISHA BWANA AKAUGEUZA UTEKA WA AYUBU, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; BWANA NAYE AKAMPA AYUBU MARA MBILI KULIKO HAYO ALIYOKUWA NAYO KWANZA.

11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.

12 Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu.

13 Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu.

14 Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu.

15 Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume.

16 Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne.

17 Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku”.

Nataka uuone huo mstari wa 10 unaosema.. “ kisha bwana akaugeuza uteka wa ayubu, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; Bwana naye akampa ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.

HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE”…hilo ndilo Neno la Msingi la leo. Pamoja na kwamba shetani aliwatumia rafiki zake kumjaribu yeye, pamoja na kwamba rafiki zake walimchukiza sana Mungu, mpaka hasira za Bwana zikawaka juu yao, akataka kuwaua…Lakini Ayubu hakuwahukumu wala kuwachukia aliwahurumia…akaenda akapiga magoti akawaombea toba! Na msamaha! Akatubu kwa ajili yao kwa dhabihu na machozi…Akawaombea rafiki zake Baraka badala ya Laana, heri badala ya shari..Na Mungu akawasamehe.. Na Bwana akapendezwa sana na AYUBU kwasababu hiyo ya kuwaombea rafiki zake…ndipo UTEKA WAKE UKAGEUZWA.. Akapewa vile vitu mara mbili..Bwana akamrudishia vyote alivyopoteza HALELUYA!!

Tunajifunza nini hapo?…kuna watu watatumiwa na shetani kutujaribu, hususani wanaotumia biblia..pengine ni marafiki zetu au ndugu zetu, na kwasababu Neno la Mungu linakaa ndani yetu, tunazitambua fikra za shetani ndani yao..Na mambo wanayofanya ukaona kabisa yanamchukiza Mungu na Mungu kawakasirikia, sasa huo sio wakati wa kupiga maadui yako!! Sio wakati kusema walaaniwe maadui zangu, wafe maadui zangu, waanguke!! Hapana! Biblia haitufundishi hivyo hata kidogo…inatufundisha kwenda kwenye magoti kutubu kwa ajili yao, kuwaombea msamaha, kulia hata ikiwezekana kutoa sadaka kwa ajili yao…hivyo ndivyo Bwana naye atakavyogeuza UTEKA WETU! Ndugu jitenge na injili za kupiga maadui si za kimaandiko hata kidogo…ukifanya hivyo Mungu hatageuza uteka wako hata kidogo. Tujifunze kwa Ayubu hakuna mtu aliyeumizwa moyo kama Ayubu, kapata msiba na wakati huo huo rafiki zake wanamwambia ana dhambi nyingi…inaumiza kiasi gani, lakini hakuwalaani bali aliwaombea..

Biblia inasema katika Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;

18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.

Unaona! Ndio maana Bwana alisema “ombea adui yako”..kwasababu unavyomwombea ndivyo Bwana anavyogeuza uteka wako.

Bwana akubariki sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada, Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312


Mada Zinazoendana:

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).

MNGOJEE BWANA

AYUBU ALITESEKA KATIKA MAJARIBU KWA MIAKA MINGAPI?.

NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:

AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Karibu katika mwendelezo wa kujifunza vitabu vya biblia.

Kwa ufupi tumeshapitia vitabu vinne vya kwanza yaani kitabu cha Mwanzo, kutoka,Mambo ya Walawi na Hesabu na leo Kwa Neema za Bwana tutasogea mbele na vitabu vingine vinne vinavyofuata.

5) KUMBUKUMBU LA TORATI:

Kitabu hichi cha kumbukumbu la torati kiliandikwa na Musa, katika hatua za mwisho kabisa karibia na wana wa Israeli kuingia nchi ya Ahadi, Musa alipewa maagizo na Mungu aandike kitabu hichi kwaajili ya ukumbusho wa Torati..Kama jina lake lilivyo “kumbukumbu la Torati”..kwahiyo ni wazi kuwa kilikuwa ni kitabu cha kumbukumbu ya vitu ambavyo walikuwa tayari walishapewa au kuagizwa.

Mungu aliruhusu kitabu hichi kiandikwe kwaajili ya kizazi kipya cha wana wa Israeli, waliozaliwa katikati ya safari. Kwasababu wengi wa waliotoka nchi ya Misri walikufa njiani, kutokana na manung’uniko yao kwa Mungu ndio wale waliyoyaona matendo yote makuu Mungu aliyowatendea kwa macho yao lakini hawakutaka kumwamini na hiyo ikapelekea Mungu kuchukizwa nao, Mpaka kuwaahidia kuwa hakuna hata mmoja aliyetoka nchi ya Misri atayaeiona nchi ya Ahadi isipokuwa Kalebu na Yoshua tu! Ndivyo ilivyokuja kutimia kama ilivyo, wote walikufa wakabaki watoto wao..na hawa watoto waliozaliwa jangwani walikuwa hawamjui Mungu wa Israeli vizuri, hawakuyaona matendo Mungu aliyoyafanya wakiwa kule Misri,

kwahiyo ililazimika Kitabu kiandikwe ili kuwakumbusha TORATI ya Mungu aliyowapa wakiwa jangwani…ili wasije wakakengeuka na kumkosea Mungu kama baba zao na mama zao walivyofanya.

Kumbukumbu la torati 6: 4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.

5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;

7 NAWE UWAFUNDISHE WATOTO WAKO KWA BIDII, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo”.

Kwahiyo kwa maagizo ya kitabu hichi cha kumbukumbu la torati, watoto wote waliozaliwa katikati ya safari kiliwasaidia kuwakumbusha matendo ya Mungu yote aliyoyafanya tangu alipowatoa wana wa Israeli katika nyumba ya utumwa, Kwahiyo kilibeba kumbukumbu ya sheria na amri zote za Mungu kuanzia Amri kumi mpaka sheria za Makuhani (Walawi). Kwahiyo kwa ufupi tunaweza kusema ni kama kitabu cha marudio ya sheria, hukumu, na baraka..Mungu alizowawekea wana wa Israeli wakiwa njiani kuelekea Nchi ya Kaanani.(Ndio maana kikaitwa kumbukumbu la Torati)

6) KITABU CHA YOSHUA:

Kitabu cha Yoshua kiliandikwa na Yoshua mwenyewe, baada ya Musa kufa…Yoshua ndiye aliyekabidhiwa gurudumu na Mungu mwenyewe, kuwaongoza wana wa Israeli kuingia nchi ya Kaanani, baada ya kuzunguka miaka 40 jangwani..Kwahiyo Yoshua na Kalebu ndio waliosalia miongoni wa waliotoka Misri, hawa wawili ndio waliobebeshwa jukumu kukiingiza kizazi kipya cha wana wa Israeli katika nchi ya ahadi.

Kusudi kubwa la kuandika hichi kitabu cha Yoshua ni kuonyesha jinsi Wana wa Israeli walivyoshindana katika kutwaa urithi wao walioahidiwa…Hatua kwa hatua, jinsi walivyopigana vita na kuyatoa yale mataifa saba yaliyoshikilia urithi wao..Ni kitabu cha Vita, chini ya amiri jeshi wao Yoshua, Bwana aliyemtia mafuta kwa kuwashindania Israeli.

Yoshua 1: 1 “Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,

2 Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.

3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.

4 Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.

5 Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha”.

Kwahiyo rekodi yote ya vita, iliandikwa ndani ya hichi kitabu cha yoshua, ni sawa kipindi kile Rais Nyerere amwagize aliyekuwa mkuu wa Majeshi, aandike kitabu cha jinsi walivyovamia majeshi ya Uganda na kuyaangusha, kwenye vita dhidi ya Idd Amin, hatua kwa hatua jinsi walivyoteka jimbo moja baada ya lingine, na hatimaye jinsi walivyofanikiwa kuiteka Uganda yote na kuuangusha utawala wa Idd Amini. Ndivyo kitabu cha Yoshua kilivyo kinaelezea hatua kwa hatua namna Israeli walivyoteka na kuyatwaa maeneo ambayo Mungu aliwaahidia yatakuwa urithi wao katika nchi ya Ahadi.

Na hichi kitabu cha yoshua  pia kiliandikwa kwa dhumuni ya kuonyesha mipaka ya wana wa Israeli katika nchi mpya ya Kaanani waliyoiingia..kwamba kila Kabila liligawiwa sehemu yake..

Kumbuka vitabu hivi pia, havikuandikwa kama hadithi tu, kutufurahisha sisi tunaosoma wa vizazi hivi..hapana bali kila kitabu kina kimebeba maana kubwa sana na ujumbe mzito katika roho. Vitabu hivi vina maudhui makubwa sana katika kutufundisha sisi watu wa siku za mwisho. Hivyo nakushauri unaposoma vitabu hivi, omba Roho wa Mungu akusaidie kupata uelewa ya ujumbe kwa wakati wako husika. Na hakika utafurahia na kujifunza mengi sana.

7) KITABU CHA WAAMUZI:

 Kitabu kinachofuata ni kitabu cha Waamuzi kitabu hichi kiliandikwa na nabii Samweli. Kama jina la kitabu lilivyo “waamuzi” maana yake ni kitabu kinachozungumzia watu fulani ambao wamewekwa kutoa “suluhisho la mwisho la mambo yahusuyo nchi” au kwa lugha rahisi tunaweza kuwaita mahakimu.

Sasa Nabii Samweli ndiye aliyeagizwa na Bwana akiandike hichi kitabu cha Waamuzi, miaka mingi sana baada ya waamuzi wote kupita…aliagizwa aandike mambo waliyoyafanya hawa waamuzi moja baada ya lingine, kwani matendo yao yamebeba ufunuo wa KiMungu mkubwa sana ambao ungekuja kueleweka na vizazi vya mbeleni..ambao ndio sisi tunaosoma sasa.

Waamuzi walikuwa ni watu waliokuwa wanatoa maamuzi ya mwisho katika Israeli, baada tu ya wana wa Israeli kuingia katika nchi ya Kaanani..Mungu hakuwahi kuweka muamuzi katika nchi, lakini kwasababu ya kukengeuka kwa wana wa Israeli na kuiacha sheria na maagizo yake, Ndipo Mungu aliwatupa kwenye mikono ya maadui zao wateswe lakini walipomlilia Mungu, ndipo Mungu akawatumia mwokozi ili awaokoe kutoka kwenye shida zao, na huyo mwokozi Bwana aliyewatumia baada ya kuwaokoa katika shida zao ndio anakuwa kama MWAMUZI wa Taifa hilo kwa wakati huo.

Kitabu cha Waamuzi 2: 8 “Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi.

9 Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.

10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.

11 WANA WA ISRAELI WALIFANYA YALIYOKUWA NI MAOVU MBELE ZA MACHO YA BWANA, NAO WAKAWATUMIKIA MABAALI.

12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.

13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.

14 HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA ISRAELI, NAYE AKAWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WALIOWATEKA NYARA, AKAWAUZA NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA ADUI ZAO PANDE ZOTE; HATA WASIWEZE TENA KUSIMAMA MBELE YA ADUI ZAO.

15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.

16 KISHA BWANA AKAWAINUA WAAMUZI, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.

17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo.

18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.

19 Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi”.

Katika Israeli walipita waamuzi 16 Samsoni akiwa mmoja wao, na Gideoni na Debora, na Yefta n.k. Hawa wote waliiamua Israeli kwa vipindi tofauti tofauti walikuwa wana madaraka karibia yafanane na ya kifalme lakini hawakuwa wafalme..Na Samweli mwandishi wa kitabu hichi ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Mwisho katika Israeli, ni sharti mwamuzi wa Mwisho ndiye awe mwandishi kwasababu yeye ndiye atakayekuwa na rekodi ya matukio yote ya waamuzi waliomtangulia…Mwamuzi wa kwanza haiwezekani apewe jukumu la kuandika historia ya mbeleni, ni lazima yule wa mwisho ndio awe muhasisi….

Kwahiyo hichi kitabu cha WAAMUZI, unapokisoma kimebeba siri nyingi Mungu alizozificha ndani ya hawa waamuzi, ukimsoma Gideoni utaona ufunuo wa ajabu sana, Vivyo hivyo Samsoni, vivyo hivyo Debora, vivyo hivyo Yeftha na wengine wote.

8) KITABU CHA RUTHU:

Hichi kitabu cha Ruthu ni kitabu cha Nane katika Biblia..Kitabu hichi kiliandikwa na Nabii Samweli yule yule aliyekuwa mwamuzi wa Mwisho wa Israeli, na aliyeandika kitabu cha Waamuzi, Bwana alimwongoza Nabii Samweli akiandike kitabu hichi kwani kimebeba maudhui makubwa sana katika mwili na katika Roho kwa kanisa lake..katika siku za mbeleni.

Kama jina la kitabu lilivyo RUTHU, Ikimaanisha kuwa ni kitabu kinachomwelezea mtu anayeitwa Ruthu. 

Kinaelezea maisha ya Ruthu, na kinaelezea jinsi Mungu alivyomlipaji wa thawabu kwa wote wenye haki, jinsi alivyomlipa Ruthu kwa uvumilivu wake na upendo wake..Mpaka kufanyika kuwa mama wa Bibi wa Mfalme Mkuu atakayekuja kutokea miaka michache mbeleni (yaani Mfalme Daudi)…

Mwana wa Mjukuu wa Ruthu ndiye Mfalme Daudi. Yaani katika uzao wa tumbo lake ukawa uzao wa kifalme. Jinsi gani Mungu anawapa thawabu hata watoto wa watoto wetu endapo sisi tukimcha yeye na kumpendeza na kuwa wavumilivu na wenye upendo kama wa Ruthu…Kumbuka Ruthu hakuwa hata mwisraeli alikuwa ni mtu wa mataifa lakini kwa upendo wake na uvumilivu wake…katika uzao wa tumbo lake akatoka Mfalme Mkuu Daudi, aliye Baba yake Suleimani…na katika Mnyororo huo ndio MFALME WA WAFALME, YESU KRISTO KATOKEA!! Ni Baraka kiasi gani…

Kwahiyo  hichi kitabu cha Ruthu kimebeba maudhui makubwa sana ya kutufundisha sisi watu wa siku za mwisho, tukianza kuzungumzia jambo moja baada ya lingine na kulitolea ufafanuzi tutamaliza kurasa na kurasa hapa…lakini wewe mwenyewe chukua nafasi ya kukisoma hichi kitabu cha Ruthu na Bwana atakupa ufunuo wa kipekee..na Pia utahitaji maelezo marefu juu ya kitabu hichi cha Ruthu unaweza kubofya hapa kwa uchambuzi zaidi >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:

Bwana akubariki sana..

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

 

Tutaendelea na sura zinazofuata Bofya hapa >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 3


Mada Nyinginezo:

BWANA ALIMPA FARAO MOYO MGUMU, ASIMTII, JE! HAPO BWANA ATAMHUKUMU KAMA MKOSAJI SIKU ILE?

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

RAHABU.

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)

SANDUKU LA AGANO LILIKUWA LINAWAKILISHA NINI KATIKA AGANO JIPYA?

YATAFUTE YALIYO JUU SIKU ZOTE.


Rudi Nyumbani:

Print this post