Category Archive Home

Zile tunu (Dhahabu, uvumba na manemane) Mamajusi walizozitoa kwa Bwana (Mathayo 2) . ziliwakilisha nini?

JIBU:

Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.

11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; DHAHABU na UVUMBA, na MANEMANE. 

Ukisoma hapo utaona zile zawadi wale mamajusi walizozipeleka ni tatu tu. Ndio tunu zenyewe nazo : (dhahabu, uvumba na manemane)…

Sasa hizi zawadi tatu kila moja ilikuwa na maana yake kubwa, Tukianza na dhahabu, wale mamajusi walifahamu kuwa aliyezaliwa ni mfalme na anastahili heshima ya kifalme na kitu chenye thamani kubwa kuliko vyote ambacho angestahili kupewa mfalme ni dhahabu, kwasababu dhahabu inaweza kubadilishwa na kuwa hata fedha na kutumiwa kwa matumizi mengine yeyote..kwahiyo hii zawadi ya dhahabu ilikuwa ni zawadi yenye manufaa kimaisha, tofauti na hizo zawadi mbili nyingine zilizobakia zenyewe zilikuwa na manufaa ya kiujumbe zaidi kuliko kimatumizi.. Kwa mfano zawadi ya UVUMBA.

Kwa kawaida uvumba sio zawadi tunaweza tukasema uzito wa kumfaa mtu kwa wakati wote, ni zawadi isiyokuwa na thamani kubwa sana,hivyo hatuwezi kivile kuiweka katika makundi ya zawadi kama zawadi , tuchukulie kwamfano Mtu kasafiri kutoka mbali tuseme Marekani halafu anakuletea zawadi ya msalaba au ufunguo..Kwa namna ya kawaida wewe unayoipokea huwezi kwenda kuiuza au kuitumia kwa matumizi yako yoyote, zaidi sana utafahamu moja kwa moja kuwa ni zawadi iliyobeba ujumbe Fulani wa ndani zaidi ya kinachoonekana, Mfano mwingine tunafahamu pale binti anapoagwa baada ya kuposwa na kwenda kuolewa huwa kuna baadhi ya zawadi zinaambatanishwa naye kutoka kwa watu wa nyumbani kwake, licha ya kupewa vitu vya ndani na mali..lakini kuna mambo madogo madogo utakuta anakabidhiwa pia na hayo ndio yana ujumbe mzito kuliko hata vile vitu vya thamani alivyopewa, kwamfano utakuta anapewa ufagio, au ungo,..Ikiwa na maana kuwa mwanamke anapaswa awe Msafi na awe anazingatia Mapishi n.k… 

Hivyo hivyo na wale mamajusi walipata ufunuo wa wanayemfauata ni nani, na ndio maana walikwenda na dhahabau lakini wakaongezea kubeba na Uvumba juu yake?.. 

Sasa Kumbuka katika hekalu la Mungu, uvumba ulikuwa unavukizwa tu na makuhani baada ya sadaka kutolewa sasa ile damu ilichukuliwa na kupelekwa katika madhabahu ya dhahabu iliyokuwa kule patakatifu, na hapo ndipo uvumba ulikochomwa kujaza ile nyumba ya Mungu harufu nzuri ya manukato na utukufu, na kumbuka kazi hiyo aliifanya kuhani mkuu peke yake. Hii ikifunua kuwa Huyu aliyezaliwa Yesu Kristo, licha tu ya kuwa mfalme atakuja kuwa KUHANI pia, kwasababu kila kuhani lazima awe na uvumba mkononi mwake wa kuvukiza mbele za Mungu…Na Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu wetu. Haleluya.

 Waebrania 4: 14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.

15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.

16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”. 

Kwahiyo wale Mamajusi walipata ufunuo huo kuwa Yule atakuja kuwa kuhani mkuu pia..Jambo ambalo wengi wa waliokuwa pale hawakulifahamu hilo, mpaka alipokuja kupaa mbinguni, mitume ndio wakamwandikia habari zake. Kadhalika MANEMANE, ni zao lililotoka katika miti likiwa na maana ya “Uchungu”, manemane ilitumika kutengenezea dawa, Hivyo zawadi kama ile isingeweza kuonekana inafaa sana kwa mazingira kama yale ya furaha ya kuzaliwa Mfalme duniani, lakini walifanya vile kwasababu ilikuwa inabeba ujumbe mwingine wa ndani zaidi..

Kama tafsiri ya jina lake lilivyo ilifunulia kuwa mtoto aliyezaliwa licha ya kuwa mfalme atapitia mateso na uchungu mwingi, na hilo lilikuja kujidhirisha alipoteswa na kusulibiwa kwa ajili yetu… Wakati akiwa katika safari yake ya kwenda msalabani wale askari walimchanganyia mvinyo na manemane na kumnyeshwa, lakini Bwana aliitema kwa jinsi ilivyokuwa chungu,(Soma Marko 15:23)..Gharama Bwana aliyoilipa kwa ajili ya dhambi zetu ni kubwa sana, mfalme kufa na kuteswa msalabani kwa ajili ya mtu mwenye dhambi asiyestahili kwa chochote, hakika ni jambo la neema sana.

 Hivyo wale mamajusi Mungu aliwapa kuona mbali zaidi ya zile hazina walizozipeleka. Kama mamajusi ambao hawakuwa wayahudi walisafiri kutoka nchi za mbali kwa muda wa miaka miwili, ili tu kumwona mfalme YESU akiwa mchanga, tutapataje kupona sisi tulioshuhudia matendo yake makuu ya neema kuu namna hii ambayo kila siku yanatuita tutubu dhambi?. Tutapate kupona tukidharau leo! 

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

NYOTA YA ASUBUHI.

WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.

UFUNUO: MLANGO WA 12

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?

JIBU: Hilo neno SHEHE lisikusumbue sana..kama tunavyofahamu lugha yetu ya Kiswahili maneno mengi yametoholewa kutoka katika lugha ya kiharabu..kwamfano neno shukrani, marhaba, salamu, sultani, sadaka, simba, msalaba,jehanamu, sheria, raisi,uasherati, hekalu, adhabu, adui, askari, lawama, dhamira,roho,damu, giza, tufani n.k. theluthi ya Lugha ya Kiswahili ni kiharabu.  (Hivyo kuna Neno shehe katika biblia pia)

Sasa kwasababu waarabu walikuwepo katika nchi yetu huku zamani zile na lugha yetu ilikuwa bado haijajitosheleza hivyo tukajikuta tunatumia maneno yao katika lugha zetu, na sio kiharabu tu hata na lugha nyingine za kigeni za watu waliotawala nchi yetu… Kwahiyo hilo neno SHEHE asili yake ni kiharabu, likiwa na maana ya Kiongozi, au mwalimu hususani anayehusiana na mambo ya kidini..na ndio maana ukisoma katika tafsiri nyingine za biblia mfano za kiingereza utaona linatumiwa neno Lords, or rulers badala yake…Neno hili unaweza ukaliona katika kitabu cha Yoshua 13:3,21, 17:7, 1Samweli 5:7,11, 6:4, Ezra 9:2 Nehemia 2:16.

Hivyo kwasababu ni Neno la kiharabu viongozi wa dini ya kiislamu walilitumia sana katika dini yao na ndio maana linaonekana kama ni neno la kiislamu lakini kiuhalisia sio..   kadhalika kama tu neno Rabi ni neno linalomaanisha mwalimu kwa kiyahudi, lakini kwasababu ni neno la lugha ya kiyahudi na linatumiwa sana na viongozi wa dini ya kiyahudi basi inachukuliwa hivyo mtu yeyote anayejiita Rabi yeye ni kiongozi wa dini ya kiyahudi lakini kiukweli sio hivyo hata kiongozi wa dini nyingine yoyote tofauti na ya kiyahudi anaweza kuitwa Rabi kwasababu maana halisi ya neno Rabi ni mwalimu…  

Kadhalika na Neno Mchungaji limezoeleka kutumiwa na viongozi wa dini ya kikristo, na halitumiwi na wengine lakini kiuhalisia hata kiongozi wa dini ya kibuddha anaweza kuitwa mchungaji.. Na ndivyo ilivyo hata kwa Neno shehe, kwahiyo pale katika maandiko neno hilo linasimama kama kiongozi wa imani wa dini husika kwa wayahudi na kwa wasio wayahudi.…  

Na pia katika agano jipya halijatumika sana hilo neno lakini badala yake yametumika maneno kama waalimu na wachungaji lakini kwa lugha ya kiharabu ndio hao hao.  

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?

IMANI “MAMA” NI IPI?

UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.

EPUKA KUTOA UDHURU.

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

UFUNUO: MLANGO WA 11


Rudi Nyumbani:

Print this post

SAYUNI ni nini?

JIBU: Tukirudi Mwanzo kabisa Daudi alipoenda kuiteka Yerusalemu,na kufanikiwa eneo lile liliitwa ngome ya SAYUNI (2Samweli 5:7).Hivyo Sayuni kwenye biblia imetumika kama Mji wa Daudi au Mji wa Mungu (YERUSALEMU).. 

Kadhalika na lile eneo la mlima ambalo hekalu la Mungu lilijengwa liliitwa pia mlima Sayuni, ambalo lipo hapo hapo Yerusalemu (Yeremia 31:6,12). 

Sehemu nyingine biblia imetaja Sayuni kama watu wa Mungu yaani wayahudi;

 Isaya 60: 14 “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako [Israeli] na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli” 

Unaweza kuona hapo. Kadhalika ukisoma pia (Zakaria 9:9, Sefania 3:14-19),biblia inamtaja Israeli kama binti Sayuni. Yote haya yanaonyesha pia Wayuhudi mbele za Mungu ni sawa na SAYUNI yake. Lakini tukirudi katika agano jipya neno Sayuni limezungumziwa kama ufalme wa watu wa Mungu wa rohoni. 

Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,” 

Hapo Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho anaonyeshwa Sayuni hasaa ambayo Mungu aliikusudia kwa watu wake tangu zamani yaani hiyo Yerusalemu ya mbinguni kanisa la Mungu. Mtume Petro pia aliandika katika…

 1Petro 2: 6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.”

 Habari hiyo nayo inathibitisha kuwa kanisa ndiyo Sayuni ya Mungu na ndio pia Yerusalemu ya mbinguni,..na tunafahamu Kanisa msingi wake ni Yesu Kristo, na hapo hiyo Sayuni jiwe kuu lake la pembeni linaonekana nI YESU KRISTO BWANA WETU. Kwahiyo na sisi pia tujitahidi tuwe na sehemu katika hiyo SAYUNI/ YERUSALEMU mpya ya Mungu ambayo Mungu alishaanza kuiandaa na anaendelea kuiandaa hapa hapa duniani. 

Ubarikiwe.

MLIMA WA BWANA.

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

Rudi nyumbani:

Print this post

Kwanini pale Bwana Yesu alichukua hatua ya kumsamehe dhambi kwanza kabla ya kumponya yule mtu mwenye kupooza?(Marko 2).

JIBU: Ubarikiwe dada tuisome kwanza habari yenyewe.. 

Marko 2: 1 “Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.

2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.

3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.

4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.

5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,

7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?

9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),

11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote,wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe” …

Kama ukichunguza utaona kuwa jambo la kwanza Bwana aliloliona ni ile Imani yao kwake, aliona ndani yao walikuwa na kitu cha ziada zaidi ya imani ya kuponywa, nayo ni Imani kwa Yesu Kristo…..Na tunajua kitu cha kwanza kilichomleta Bwana Yesu duniani ni kuokoa dhambi za watu, na vitu vingine baadaye…

Ukisoma Yohana 8:24 Bwana aliwaambia makutano ..“Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”….

Unaona hapo?…Inakupasa uamini kwanza. Na ndio maana jambo la kwanza alilolitamka yeye kama mkuu wa uzima wa roho za watu mara baada ya kuona Imani yao kwake, akamwambia yule aliyekuwa amepooza..UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO…..Ni Neno zuri na la neema kiasi gani!!! Lakini wale wengine mawazo yao yalikuwa tofauti, wao walitazamia tu, Bwana amponye yule mtu kisha amwambie nenda zako, halafu yule mtu akaendelee kuishi maisha ya dhambi kisha mwisho wa siku afe aishie kupata hasara ya nafsi yake!..na uponyaji wake wa mwili usimfaidie kitu baada ya maisha ya hapa. 

Sasa Ukiendelea kusoma pale utaona Bwana anawauliza tena wale watu, Marko 2:9 “Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?, Sasa kwa namna ya kawaida kwa mtu mwenye akili za rohoni atagundua kuwa ni afadhali usipone ugonjwa wako, lakini dhambi zako ziwe zimesamehewa…kuliko kuponywa halafu dhambi zako ziendeleee kubaki! Na ndio maana Bwana alimchagulia fungu lililo jema la kusamehewa dhambi zake kwanza, kisha baadaye amponye… 

Na ndivyo tunavyopaswa na sisi kama wakristo kufanya sasahivi, tunakimbilia kuwaombea watu magonjwa ,wapokee miujiza, na mafanikio na huku tunasahamu kuwafundisha watu habari za msamaha wa dhambi ambao ndio msingi wa Imani ya kikristo.. vyepesi ni vipi??? Ni heri tukamuhubirie mtu habari za msamaha na toba, aokolewe roho yake hata kama hatapokea uponyaji kuliko kuhubiri kila siku mimbarani miujiza na uponyaji na huku bado watu wanakufa katika dhambi zao.

Au ni afadhali kufanya vyote kuliko kutupilia mbali habari za msamaha wa dhambi, na kushikamana na miujiza tu. 

Ubarikiwe .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

HOME

Print this post

Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.

JIBU: Kujiliwa na Neno la Mungu ni sawa sawa na kufunuliwa ujumbe unaomuhusu mtu au jamii fulani, na ujumbe huu Mungu anamshushia mtu aidha kwa njia ya ndoto, au maono, au sauti, au kutembelewa na malaika, au njia nyingine yoyote ya ki-Mungu. 

Kwahiyo unaposoma mahali popote kwenye biblia,unakutana na sehemu inasema Neno la Mungu lilimjia Isaya, au Yeremia au Yona, hap ni sawa na kusema, ujumbe utokao kwa Mungu umemfikia Isaya, au Yeremia au Yona awapelekee watu. Kadhalika hata sasa hivi Neno la Mungu, huwa linawajilia watu kwa njia mbalimbali, mt anapofunuliwa Neno lolote kwa njia ya ndoto, au maono au kuzuriwa na malaika, au katika biblia, na Neno hilo limebeba ujumbe wa kwenda kuwapelekea watu wengine, hiyo ni sawa tu na Neno la Mungu limemjia mtu huyo. Kadhalika unaposikia ndani wito wa kwenda kuwashuhudia wengine habari njema, hapo ni sawa na lile Neno linalosema

Marko 16:15 “Enendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili kwa kila kiumbe”

limekujia, hivyo unapaswa ukauwasilishe huo ujumbe kwa wakati. Na kuna hatari za kutokutii Neno la Mungu linalokujia, na hatari zenyewe ndio kama zile zilizompata Nabii Yona na zile alizoonywa Nabii Ezekieli zikisema.. 

Ezekieli 3: 17 “Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.

18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

20 Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako”.

 Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

BIBLIA INASEMA USIONGEZE WALA USIPUNGUZE NENO LA MUNGU, HUKO KUONGEZA NA KUPUNGUZA KUKOJE?

WANA WA MAJOKA.

JIWE LA KUKWAZA

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

MADHAIFU.

WITO WA MUNGU


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

JIBU: Kwanza sio sahihi kwa mtu aliyeamini kwenda kutwaa mke au mume asiye wa imani yake ya kikristo, kwasababu moja tu! nayo ni KUEPUKA KUGEUZWA MIOYO!..   Kumbuka jambo mojawapo ambalo Mungu aliwakanya sana wana wa Israeli hata kabla ya kufika nchi ya Ahadi ni suala la kuoa/kuolewa na watu wa jamii nyingine tofauti na wayahudi, na sio kwasababu labda ni wabaya, au hawavutii hapana, ni kwasababu moja tu! Watageuzwa mioyo yao wasiambatane na Mungu wa Israeli kinyume chake wataambata na miungu migeni. Na Mungu siku zote ni Mungu mwenye wivu!.   Tukisoma;

Nehemia 13:25 “………… nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.

26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini WANAWAKE WAGENI WALIMKOSESHA HATA YEYE.

27 Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumhalifu Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni?”  

Unaona hapo?. Mfalme Sulemani pamoja na hekima zake zote nyingi za kuweza kupambanua mambo lakini aligeuzwa moyo, na wale wanawake wa mataifa mpaka kufikia hatua ya kuivukizia uvumba miungu migeni, Unadhani itashindanaje kwa mkristo mwingine yeyote wa kawaida?. Unaweza ukasema aa! Mimi nitaweza kumtawala, lakini hilo haliwezekani Mungu sio mwongo, akisema atakugeuza, ni kweli atakugeuza,.Mwanzoni utaona kama inawezekana lakini mwisho wa siku utajikuta unaangukia katika shimo kama Sulemani.   Vivyo hivyo ukimsoma Mfalme Ahabu alikoseshwa na Yezebeli mchawi, Samsoni naye alikoseshwa na Delila. Wote hawa wake zao walikuwa ni wanawake wa kimataifa n.k.  

Kwahiyo unapokuwa mkristo unapaswa umtafute mtu mwenye imani moja na yako ya kikristo, au kama sio basi umgeuze kwanza amgeukie Kristo ndipo umuoe au uolewe naye, vinginevyo utakuwa unajiweka mwenyewe katika hali ya hatari kubwa ya kumkosea Mungu, na kuishia katika majuto…   Lakini kama ikitokea mlishaoana tayari huko nyuma na mtu mwingine kabla wewe hujawa mkristo, na wewe baadaye ukaja kuamini na Yule mpenzi wako hajaamini lakini bado anaona vema kuishi na wewe hapo biblia inasema haupaswi kumuacha, unatakiwa ukae naye katika hali yake hiyo hiyo pengine wakati ukifika kwa matendo yako mema ya kikristo yatambadilisha na yeye naye aamini…

Lakini kama akichukizwa na uamuzi wako wa wewe kuwa mkristo na anataka kuondoka…Hapo haufungiki, anaweza kwenda, na biblia inaruhusu kutwaa mke/mume mwingine ila katika Bwana tu ambaye ni mkristo mwenye imani moja na wewe.   Soma.

1Wakoritho 7: 12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.

13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.

15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.

16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?”  

Kwahiyo hairuhusiwi kuoa mtu ambaye sio wa IMANI moja nawe kulingana na maandiko.  

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

NDOA NA TALAKA:

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?

NINI TOFAUTI KATI YA UZINZI NA UASHERATI ?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

NAPENDA KUJUA MAANA NA TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO.

UKWELI UNAOPOTOSHA.

DUNIANI MNAYO DHIKI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Wapendwa nini maana ya hili andiko “Ushuhuda wa YESU ndio ROHO YA UNABII” (ufunuo 19:10)?

JIBU: Biblia inaposema ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii…inamaanisha kuwa mtu yeyote ambaye anajiona kuwa anayo roho ya kinabii ndani yake au anayejiita nabii, kama maisha yake au mahubiri yake hayalengi katika kumshuhudia YESU KRISTO BWANA WETU..basi huyo ni nabii wa uongo ushuhuda wake ni wa uongo!..hata kama atakuwa anaona maono kiasi gani, au anatabiri na kutenda miujiza kiasi gani huyo bado sio nabii wa kweli, ni nabii wa uongo..

Biblia inasema katika..

1 Yohana 5:9-11“9 Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana USHUHUDA WA MUNGU NDIO HUU, KWAMBA AMEMSHUHUDIA MWANAWE.

10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ANAO HUO USHUHUDA NDANI YAKE Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.” 

Hivyo ili tumtambue kama huyu ni nabii kutoka kwa Mungu au la! …hatupaswi kukimbilia kuangalia miujiza anayofanya, au maono anayoona, tutampima kwa ushuhuda anaouhubiri (Neno la Kristo) je! anaturudisha kwa YESU? Anamuhubiri Yesu yule wa Kalvari? Yesu yule aliyesema mtu akinifuata ajikane nafsi yake ajitwike msalaba wake anifuate, Yesu yule aliyesema “itamfaidia nini mtu kupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yake” kama atamhubiri Yesu huyu basi hata asipofanya muujiza hata mmoja, au kutabiri huyo ni nabii wa kweli kwasababu anao ushuhuda wa Yesu Kristo ambayo ndio Roho ya unabii. Unamkumbuka Yohana mbatizaji, yeye hakuwahi kufanya muujiza hata mmoja, wala ishara yoyote..lakini ushuhuda wake ulikuwa ni nini?..ulikuwa ni kuwapeleka watu kwa YESU, na si kingine..lakini Bwana alimwambiaje?…yeye ni zaidi ya NABII..na hakuna aliyetokea kama yeye hata Musa hakuwa mfano wake. 

Lakini kitu gani kilichopo sasahivi…watu wanajiita manabii wanatabiri lakini hawana ushuhuda wa Yesu Kristo ndani yao, mungu wao ni tumbo, wanahubiri tu mafanikio ya ulimwengu huu na kukwepa mafundisho ya kumpeleka mtu mbinguni na toba, kama biblia inavyosema katika

Wafilipi 3:18-21 “18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO;

19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI.

20 KWA MAANA SISI, WENYEJI WETU UKO MBINGUNI; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.” 

Kwahiyo roho yoyote isiyoturudisha kwa YESU KRISTO na maneno yake, hiyo ni roho ya Yule mwovu, ikivaa kinyago cha roho ya kinabii, hivyo ili ile Roho ya kinabii iwe juu yako inakupasa kumshuhudia YESU KRISTO katika maisha yako na katika huduma yako.

 Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinaendana:

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

MJUE SANA YESU KRISTO.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

CHAKULA CHA ROHONI.

SWALI LA KUJIULIZA!


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?

Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja KUITANGUA TORATI AU MANABII; La!, SIKUJA KUTANGUA, bali KUTIMILIZA.

18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.

JIBU: BWANA aliposema hakuja kuitangua torati wala manabii bali kuitimiliza…alikuwa ana maana kuwa yeye hakuja kuondoa neno lolote la torati lililosemwa bali alikuja kulifanya kuwa IMARA ZAIDI..kwa mfano torati iliposema usizini, haikuishia pale tu katika mwili…lakini Bwana Yesu alipokuja alisema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake…si umeona hapo.. hajaiondoa amri ile bali ndio ameikolezea..Ikiwa na maana sio tu kwenda kuchukua hatua ya kuzini ndio iwe kosa hapana bali kitendo cha kumtamani tu tayari ni kosa, hivyo haupaswi kutamani kabisa ili kuitimiliza torati… 

Kadhalika Torati pia ilisema usiue..lakini Yesu alisemaje? amchukiaye ndugu yake ni sawa na muuaji..umeona na hapo pia sio tu Kuua ndio iwe kosa, hapana! bali hata hilo wazo la kumchukia tu ndugu yako halitakiwi liwepo ndani ya mtu. Torati ilisema pia ikumbuke siku ya sabato uitakase, lakini Bwana Yesu alisema ..Yeye ndiye BWANA wa Sabato (Marko 2:28), ikimaanisha kuwa ukimpata Yesu umeishika sabato yako, kwasababu ndani ya moyo wako kila wakati unakuwa ndani ya pumziko lako na kila siku unakuwa katika ibada na sio tena siku moja maalumu. 

(Mathayo 11:28)…Unaona hapo? Hajaiondoa lakini ameifanya ieleweke zaidi. Na ndivyo ilivyo pia kwa maneno mengine yote yote ya torati Bwana hakuyaondoa bali aliyafanya kuwa imara zaidi. 

Ubarikiwe sana .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa njia ya maelezo unaweza kufungua video chini

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=RxbUfwts4fg[/embedyt]


Mada zinazoendana:

UTIMILIFU WA TORATI.

JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!


Rudi Nyumbani:

Print this post

Habari ile ya Pilato kuchanganya zile damu za wayahudi na pamoja na dhabihu zao,(Luka 13) ilihusu nini?

Tukisoma

Luka 13:1 “Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya DAMU YAO NA DHABIHU ZAO.

2 Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?

3 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

4 Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?

5 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.”  


JIBU: Kama ukiitazama kwa ukaribu habari hiyo picha utakayokujia hapo ni kwamba kwa wakati huo ambao Bwana aliokuwepo na hao watu, kulikuwa na habari iliyozagaa sana mjini kote, maeneo kadha wa kadha uko uyahudi,ni habari ya tukio ambalo sio la kawaida kutokea katikati ya jamii ya watu wa Israeli,nalo si lingine zaidi ya kuuawa kwa wayahudi kikatili tena kibaya zaidi na cha kushtusha ni kuchangwa damu zao na za wanyama.  

Tuchukulie kwamfano hapa Tanzania wakati ule tulivyosikia ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent kule Arusha, jambo lile liliwashutusha watu wengi sana, mpaka kupelekea tukio kama lile kuzungumziwa mara kwa mara katika vyombo vya habari Tanzania nzima, na tunajua habari za matukio kama hayo huwa kwa namna ya kawaida zinachua muda mrefu kidogo kuacha kuzungumziwa, Na ndio maana unaona hapo wale watu walimwendea Bwana Yesu kumuuliza ili waone kama na yeye anazo hizo taarifa au la! na kama anazo je! yeye naye analizungumziaje suala hilo? Ni kwanini Pilato aamue kufanya kitendo cha kikatili kama kile cha kuchanganya damu za wale wagalilaya na dhabihu zao wenyewe?. Hilo ni swali lililokuwa ndani ya vichwa vya watu wengi sana kwa wakati ule.

Lakini kama tunavyofahamu kwenye biblia Pilato alikuwa ni Liwali (Governor) wa Uyahudi,(Luka 3:1) chini ya utawala wa kikatili wa Rumi (Kumbuka kwa wakati ule Bwana akiwa duniani Dola ya Rumi ndio ilikuwa inatawala Dunia) Hivyo yeye kama Liwali aliyeteuliwa na Kaisari mkuu wake huko kutoka makao yao makuu Rumi, aiongoze Yudea, alikuwa na jukumu la kuhakikisha Maeneo aliyowekwa ayaongoze yanatulia kikamilifu chini ya utawala . kwahiyo jambo lolote ambalo lingeonekana kujitokeza aidha usaliti, au vurugu, au mapinduzi, au uvunjaji wa amani katika uyahudi lisingevumilika kwa namna yoyote chini ya utawala wa Pilato kwasababu naye pia alikuwa ni mkatili…tunamwona baadaye alikuja kuhusika hata na kifo cha Bwana Yesu.   Kwahiyo biblia haijaeleza sababu hasaa ya Herode kutaka kuwaua wale Wagalilaya waliokwenda kuabudu Yerusalemu wakati wa sikukuu. Inaeleza tu waliposhuka kutoka Galilaya kwenda kuabudu ghafla kikosi cha Pilato kiliwadondokea na kuwachinja na si mahali pengine zaidi ya Hekaluni kwasababu huko ndiko dhabihu zilikuwa zinatolewa , kisha kuchukua damu zao na kuzichanganya na damu za wanyama waliokuja nao kutolea dhabihu kwa Mungu wao..

Pengine Pilato alihisi kuna tukio la usaliti au uvunjaji amani lilipangwa na hao watu au vinginevyo hatujui lakini inaelekea itakuwa ni sababu ya kiusalama zaidi.   Na tunaona pia na wale{makutano} nao hakuwajua sababu hasaa ya Pilato kufanya vile, Wao WALIKISIA TU! mioyoni mwao, labda wale watu watakuwa na laana kutoka kwa Mungu na ndio maana wamekutwa na mambo kama yale, au walimkufuru Mungu katika mioyo yao,na ndio maana Mungu akaruhusu Pilato aje kuwaua, au walikuwa na dhambi sana zisizovumilika na ndio maana yakawapatwa mambo kama yale n.k.,  

Lakini Bwana akifahamu mawazo yao, akawaongezea kuwakumbusha kisa kingine cha kushtusha kinachofanana na hicho kilichowatokea pengine miezi michache tu! nyuma huko huko Israeli kabla ya tukio hilo, nacho ni kuhusu wale watu walioangukiwa na mnara kule Siloamu..,kwamba wasidhani na wale yaliwapatwa na yale mambo eti kwasababu walimuudhi Mungu kupita kiasi? jibu lake lilikuwa ni hapana.. … Na ndio maana ukiendelea kusoma utaona Bwana anawaambia sivyo kama wanavyofikiri..   Soma tena hapo hiyo habari utaona mawazo ya wale watu yalikuwa ni nini?…

Luka13:1 Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.

2 Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?

3 Nawaambia, SIVYO; lakini MSIPOTUBU, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.  

Unaona hapo Bwana Yesu alijua mawazo yao kwamba wanadhani kuwa yale mambo yaliyowakuta wale watu ni kutokana na dhambi zao kuwa nyingi sana. Lakini yeye aliwambia sivyo kama wanavyofikiri.   Bwana aliwaambia hata wao pia wasipotubu yatawapatwa na mambo kama hayo hayo. Kadhalika, tetemeko la ardhi lililotokea Kagera, tunadhani wale watu walikuwa na laana sana kuliko sisi??..Ile mvua ya mawe iliyouwa makumi ya watu kule Geita tunadhani wale watu walimkosea sana Mungu kuliko sisi?? ajali ya MV BUKOBA wale watu walikuwa waovu zaidi yetu sisi?..hapana Hakika na sisi pia tusipotubu yatatukuta kama hayo hayo.. Tsunami iliyotokea 2004 huko Indonesia na kuua maelfu ya watu duniani, na sisi kunusurika, tunadhani zile nchi zilimkosea Mungu sana zaidi yetu sisi …Sivyo, tusipotubu na sisi yatatukuta kama hayo..   Huyo jirani yako aliyekufa na ajali wiki chache zilizopita unadhani alikuwa anayo bahati mbaya sana kuliko wewe?..Sivyo lakini usipotubu siku moja yatakukuta na wewe kwa ghafla na kujikuta umeenda kuzimu.  

Hivyo tujichunguze kwanza sisi mioyo yetu, kisha tujue kuwa uvumilivu wa Mungu ni kutuvuta sisi tufikie toba. Mungu amekupa uhai na pumzi, sio kwasababu wewe ni mwema sana zaidi ya yule aliyekufa jana hapana..lakini fahamu kama usipomzalia matunda ya uhai wako sasa, yatakukuta hata pengine makubwa zaidi ya hayo yaliyowakuta hao wengine. Je! Umeokolewa? Je! Una uhakika wa kwenda mbinguni ukifa leo kifo cha ghafla?… yahakiki maisha yako tena, na umgeukie Mungu maadamu muda upo.  

Ubarikiwe sana .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya ELOHIMU?

JIBU: Kwanza kumbuka katika lugha ya kiswahili hilo neno ELOHIM, halionekani likitajwa katika biblia yetu kwasababu halipo katika lugha ya kiswahili. Hili ni neno la Kiebrania linalomaanisha Mungu, Kama tukisoma katika sura ya kwanza kabisa ya kitabu cha mwanzo biblia inasema “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”..Hii ni katika lugha yetu ya kiswahili lakini kwa kiebrania inatafsiriwa hivi; Hapo mwanzo ELOHIM aliziumba mbingu na nchi.

Unaona tofauti hapo? na neno hili limetokea kwenye agano la kale mara 2500 katika biblia yao ya kiyahudi, lakini kwetu limetafsiriwa kama Mungu. Wakati mwingine hili neno ELOHIM limefupishwa kama “EL” ..Na ndio maana sehemu nyingine anajulikana kama EL’Shadai ikiwa na maana kuwa yeye ni “Mungu mwenyezi” kwa lugha yetu ya kiswahili (Mwanzo 17:1, kutoka 6:3 )..Sehemu nyingine anatajwa kama EL ROI, ikimaanisha “Mungu anayeona”(Mwanzo 16:13)..

Kadhalika sehemu nyingine anatajwa kama El Elyoni ikimaanisha “Mungu aliye juu”…Haya majina yote utayakuta katika nakala za biblia ya kiebrania. mahali pengine tuliomwona Bwana Yesu akilitamka hili jina kama lilivyo, pale alipokuwa msalabani tunaona alisema..EL’OI ELOI lama Sabakthani…tafsiri yake ni Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?.. 

Kwahiyo jina Elohimu ni Mungu ikimaanisha kwamba ni Mungu asiyekuwa na mwanzo, wala mwisho, Mungu mwenyezi, muweza yote, muhukumu, muumba, n.k. kwa ufupi hilo jina Elohimu linabeba tabia zote za Mungu. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JINA LA MUNGU NI LIPI?

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

MUNGU MWENYE HAKI.

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.


 

Rudi Nyumbani

Print this post