Category Archive Home

ESTA: Mlango wa 3

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO aliye mkuu wa uzima wote litukuzwe.

Karibu katika kujifunza NENO la Mungu ili tukue toka utukufu hata utukufu mpaka tutakapofikia kile kilele cha kumjua sana huyu mwokozi wetu Yesu. Leo tukiendelea na ile sura ya 3 ni vizuri ukaipitia habari hii kwanza peke yako katika biblia ndipo tuende pamoja.

Kwa maelezo mafupi kitabu hichi kinaelezea unabii wa mambo yatakayokuja kutokea baadaye licha ya kwamba tunaisoma kama hadhithi iliyo nyepesi kuielewa lakini ndani yake imebeba maana kubwa zaidi ambayo kila mkristo ni vema akaifahamu kwa haya majira tunayoishi, kwa mfano laiti ile historia ya YONA ingeeleweka machoni pa watu wengi kwa wakati ule kwamba sio tu ilikuwa ni hadithi ya Yona kutokutii maagizo ya BWANA, bali pia ilikuwa inamwelezea Bwana wetu Yesu kufa na kufufuka kwake, kuwa atakuja kukaa siku tatu kaburini kama vile Yona alivyokaa siku tatu usiku na mchana katika tumbo la samaki. Unaona Hivyo hadithi hizi zote zinaelezea unabii wa mambo yanayokuja kutokea mbeleni na ndivyo ilivyo hata katika kitabu hichi cha Esta.

Katika sura ya 3 tunasoma habari ya HAMANI ambaye alikuja kupandishwa cheo na mfalme Ahasuero na kuwa juu ya maakida wote waliokuwa katika ufalme wake uliotawala dunia nzima, (Esta 3:1-2) Alitukuzwa sana kiasi kwamba watu wote waliokuwa chini yake waliamiriwa wamsujudie, Lakini tunasoma haikuwa hivyo kwa watu wote, alionekana mtu mmoja myahudi aliyeitwa Mordekai alikataa kuanguka chini yake na kumpa heshima yake. Na habari ilipomfikia Hamani alikasirika sana, na alipomjaribu tena aone kama atamwangukia amsujudie kama wale wengine wanavyofanya, msimamo wa Mordekai ulikuwa ni ule ule hakudhubutu kumsujudia..Hivyo Hamani tunasoma alizidi kuchukia zaidi akaona si shani kumwangamiza Mordekai peke yake bali hata na watu wake wote (yaani WAYAHUDI).

Esta 3:2 “Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia.
3 Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme?

Lakini swali la kujiuliza ni hili; kwanini Mordekai aliyahalifu maagizo ya mfalme juu ya kusujudiwa kwa Hamani angali tunamsoma Mordekai alikuwa ni mtu mkamilifu aliyemuheshimu mfalme na kumtii?. Kumbuka neno kusujudia linavyotumika hapo sio kumsujudia kama Mungu bali ni kuanguka na kumpa Heshima yake kama mkuu wa nchi, ni kama tu vile kwasasa mahali ambapo Raisi anapita watu wote mnapaswa kusimama ili kumpa heshima yake, ndivyo Mordekai alivyokuwa anafanya kwa mfalme na kwa wakuu wote waliokuwa juu yake..lakini haikuwa hivyo kwa Hamani yeye alienda kinyume na wengine, hakumsujudia.

Ni dhahiri kuwa kuna jambo Mordekai aliliona ndani ya HAMANI ambalo sio sawa na ndio maana hakumpa Heshima yake. Biblia haijaeleza moja kwa moja ni mambo mangapi aliyaona kwa yule mtu. Lakini tukichunguza biblia tunaweza tukapata dondoo za kwanini Mordekai asimuheshimu HAMANI kama wakuu wengine wa Uajemi.

Tukirejea nyuma kidogo katika ile ya sura ya pili mwishoni tunaona kulikuwa na watu wawili waliotaka kumfanyia hila mfalme Ahausero na kutaka kumuua. (Esta 2:21-23). Lakini Mordekai alipogundua ya kwamba madhara yamepangwa kinyume cha Mfalme alikwenda kumuarifu jambo hilo na wale watu wakauliwa. Hivyo tukichunguza tunaona kuwa katika ule utawala fitna nyingi zilikuwa zinapangwa dhidi ya mfalme na ufalme wake. Na Mordekai kwasasa tunaweza kusema alikuwa ni mtu wa USALAMA,

Hivyo alichunguza mambo yote waliyokuwa yanaendelea kwa siri pasipo hata wakuu wengine kujua. Hivyo kitendo cha kutokumpa heshima HAMANI ni kwasababu aliziona HILA zake mbaya tokea mbali. Pengine hata wale watu waliotaka kumuua mfalme walikuwa na mahusiano ya karibu na Hamani. Na Mordekai kwa kutokupenda UNAFKI alidhihirisha moja kwa moja kuwa huyu mtu hastahili heshima ya ukuu japokuwa amri imetoka kwa mfalme watu wote wamwangukie.

Lakini tunavyozidi kuendelea kusoma tunakuja kuona jinsi Hamani alivyoomba kibali cha Mfalme kuwateketeza hata watu wasiokuwa na hatia (WAYAHUDI). Aliwachukia mpaka akatenga siku rasmi kuwaangamiza wayahudi wote walioko duniani. Mpaka biblia inamtaja kama “Adui wa wayahudi”. Na japokuwa ni mfalme mwenyewe aliyemnyanyua lakini alikuja kuwa adui hata wa mfalme kwa kujaribu kuwaangamiza ndugu wa mke wake (Malkia Esta). Lakini utawala wake wa hila haukudumu kwa muda mrefu tutakuja kuona mbeleni tunavyozidi kusoma..

Habari hii inatoa picha halisi ya mambo yatakayokuja kutokea katika siku za mwisho. Kumbuka moja ya siku hizi atanyanyuka MFALME ambaye Mungu atamruhusu atende kazi kwa kipindi kifupi.

Tukisoma Ufunuo 13:5-7 ” 5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. AKAPEWA UWEZO wa kufanya kazi yake MIEZI AROBAINI NA MIWILI.

6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.

7 Tena AKAPEWA KUFANYA VITA NA WATAKATIFU na kuwashinda, AKAPEWA UWEZO JUU YA KILA KABILA NA JAMAA NA LUGHA NA TAIFA. “

Hamani ni mfano wa mpinga-kristo atakayeanza kufanya kazi moja ya siku hizi. Yeye alipewa amri kutoka kwa mfalme ahausero naye huyu vivyo hivyo atapewa uwezo kutoka kwa Mungu mwenyewe kutawala dunia kama biblia inavyosema. Na kama vile watu wote wa dunia nzima walimsujudia Hamani isipokuwa Mordekai peke yake. Vivyo hivyo mpinga-kristo atasujudiwa na watu wote wa dunia nzima pale atakapoanza kutenda kazi yake isipokuwa kikundi cha watu wachache sana watakaomdhihirisha maovu yake (miongoni mwao watakuwepo wale mashahidi wawili wa ufunuo 11, pamoja na wale wayahudi 144,000 watakaotiwa muhuri na Mungu katika Ufunuo 7&14.) kumbuka wakati huo kanisa litakuwa limeshanyakuliwa.

Jambo lile lile lililotokea kwa Hamani la kumchukia Mordekai kisa tu hajapendezwa naye na kukusudia kumwangamiza yeye pamoja na watu wake wote (wayahudi), vivyo hivyo MPINGA-KRISTO naye atawaghadhibikia wale MASHAHIDI WAWILI pamoja na wale 144000 na kutaka kuwaua na sio wao tu..bali mpaka wayahudi wengine waliozagaa duniani kote na baadhi ya masalia ya wakristo waliokosa unyakuo. Wote hawa atatafuta kuwaua kwa bidii (Ufunuo 12).

Wale mashahidi wawili wa ufunuo 11 watamhubiri kuwa huyu mfalme anayejitukuza sasa kana kwamba yeye ni Mungu sio rafiki wa Mungu bali ni MPINGA-KRISTO aliyetabiriwa, na watu waache kumwabudu wamgeukia Mungu wa mbinguni, wakithibitisha hilo kwa zile Ishara na yale mapigo yaliyoandikwa kule. Hivyo mpinga-kristo (PAPA kwa wakati huo) ataghadhibika sana na kufanya vita nao. Na kwasababu atakuwa ana nguvu duniani kote, atatoa amri kuundwe ustaarabu mpya wa dunia (NEW WORLD ORDER). Kwa kisingizio cha kuleta amani duniani lakini nia yake sio hiyo bali ni kuwakamata na kuwauwa watu wote watakaenda kinyume na uongozi wake na hawa watakuwa si wengine zaidi ya wayahudi na masalia ya waliokosa unyakuo. kama vile HAMANI alivyofanya.

Kumbuka sio watu wote watajua kuwa ni kiongozi mbaya kama vile Hamani sio watu wote waliojua kuwa ni kiongozi mbaya wengi walijua amepewa heshima na mfalme mpaka mwishoni kabisa walipokuja kujua kumbe alikuwa ni adui wa mfalme pia.

Vivyo hivyo na huyu MPINGA-KRISTO hatajulikana na watu wote, wengi watamwona kama kateuliwa na Mungu kama tu kivuli cha huyu wa sasa watu wasivyoweza kuona ni roho gani iliyopo ndani yake. Biblia inasema watu ambao hawakuandikwa majina yao tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaomsujudia (Ufunuo 17:8). Pale atakapotaka kukaa katika Hekalu la Mungu na kutaka kuabudiwa kama Mungu (2Thesalonike 2).

Hivyo atakuja kwa kivuli cha AMANI, na kuunda chapa yake itakayomtambulisha kila mtu IMANI yake. Vitu kama Micro-chips,lDS, N.k vitatumika kutakuwa hakuna “kujiajiri wala kuajiriwa” bila kuwa na vitambulisho maalumu, hivi vitatumika kutambulisha Dini/ dhehebu lililosajiliwa na UMOJA WAKE ALIOUUNDA (Ekumene). Kumbuka usajili huu hautakwepeka mahali popote usipokuwepo kwenye kitambulisho cha taifa utakutana nao kwenye leseni ya biashara au kitambulisho cha kazi au leseni au ATM card ..Hivyo lile neno hakuna atakayeweza kuuza wala kununua litatimia kwa namna hiyo. Sasa kwa wale ambao watakataa kupokea utambulisho wake ndio watakaopitia DHIKI ambayo haijawahi kuwepo.

Unaona hii roho ya shetani inavyojirudia rudia..ilianzia kwenye utawala wa Babeli wakati wa akina shedraki, Meshaki na Abednego, walipolazimishwa kuabudu ile sanamu, ukaja katika huu utawala wa Uajemi na Umedi, Hamani anataka kuwateketeza tena wayahudi, Ilitokea pia katika utawala wa Uyunani Antiokia IV Epifane alipowauwa baadhi ya wayahudi na kuwaondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima. Na utawala wa mwisho ambao ni RUMI ndio uliopo sasa uliohusika kwa mauaji mengi ya wakristo waaminifu kwa Mungu zaidi ya milioni 68. Umetabiriwa utapata nguvu tena katika siku hizi za mwisho utahusika na mauaji makubwa ambayo biblia inasema haijawahi kutokea mfano wake.

Hivyo ndugu majira haya sio ya kuchezea kabisa Bwana yupo mlangoni kurudi, kulinyakuwa kanisa lake, na siku atakapolinyakua watakaojua ni bibi-arusi tu, lakini wengine haitajulikana kwao. Je! umejiwekaje tayari, Bwana akirudi leo utasema sijasikia?. Mtafute Muumba wako angali muda unao tubu weka mbali uasherati, ibada za sanamu, nguo zisizo na maadili, ulevi, usengenyaji n.k. ukabatizwe upate ondoleo la dhambi zako. Umwishie Mungu ili uwe na uhakika wa maisha yako ya milele.

Ubaikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>>  ESTA: Mlango wa 4

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: MLANGO WA 14

CHAPA YA MNYAMA.

DANIELI: MLANGO WA 7

NINI MAANA YA ELOHIMU?

WALE MANABII 400 WALIOMTABIRIA MFALME AHABU WAKATI WA MIKAYA WALIKUWA NI MANABII WA MUNGU KWELI?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

ESTA: Mlango wa 1 & 2

MFALME wa WAFALME YESU KRISTO Bwana wetu, atukuzwe daima

Karibu kwa neema za Mungu tujifunze kitabu cha Esta leo tukianza na ile sura ya 1 na ya 2.Ni vizuri ukiwa na biblia yako pembeni uipitie habari hii kwanza ndipo tuende pamoja. Kama tunavyofahamu Agano la Kale ni kivuli cha Agano jipya hivyo kila habari inayozungumzwa katika agano la kale, inafunua jambo fulani linaloendelea katika roho kwa wakati tunaoishi sasa.

Kitabu hiki kwa ufupi kinaelezea habari ya Mfalme Ahasuero wa Ufalme wa Umedi & Uajemi aliyekuwa tajiri sana na mwenye nguvu ni mfalme aliyetawala mataifa 127, biblia inasema kuanzia India mpaka taifa la Kushi (Ethiopia), kote huku alimiliki na kwa wakati ule alikuwa ni kama Mfalme wa dunia. Kwasababu Umedi na Uajemi ndio zilikuwa zinatawala dunia kwa wakati huo.

Hivyo ilifika wakati mfalme Ahasuero aliandaa sherehe kubwa sana kwa wakuu wake wote, pamoja na watu wote waliokuwapo katika mji wake (huko Shushani ngomeni), wakubwa kwa wadogo walihudhuria, watu walikula na kunywa jinsi wapendavyo, na kwa fahari yake aliamua kumuwasilisha malkia aitwaye VASHTI, mbele za wakuu wote wauone uzuri wake, maana biblia inasema Vashti alikuwa ni mzuri sana wa uso, kwasababu hata tafsiri ya jina Vashti linamaanisha “mwanamke mzuri”.

Lakini mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa, Badala ya Vashti kumtii mume wake, na zaidi ya yote alikuwa ni MFALME, alikaidi amri ile kwa KIBURI cha Uzuri wake na kuamua kutokwenda, Jambo hili lilionekana kuwa ni aibu kubwa kwa Uajemi yote, kwasababu hakukuwa na desturi ya mwanamke kumvunjia heshima mfalme, Na tunasoma Vashti alikuja kuvuliwa umalkia wake na kutafutwa mwengine “ALIYE MWEMA KULIKO YEYE”.

 

Esta 1:19 “Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.”

Hivyo moja kwa moja, ikaanza kupangwa mipango ya kumtafuta malkia mwingine mahali pa Vashti, mbiu zikapigwa katika mataifa yote duniani (127) aliyokuwa anayamiliki, walikuja MABIKIRA vijana wengi na ESTA alikuwa mmoja wapo. Kumbuka wote hawa walitokea katika machimbuko tofauti tofauti, wengine katika familia za kitajiri, wengine katika koo za kifalme, wengine walikuwa mabinti za maakida, wengine familia za kisomi, wengine familia za mabinti warembo n.k. Kwahiyo walikusanyika wengi sana pengine mabinti 30,000 au zaidi.

Lakini tukiendelea kusoma habari tunaona kwamba kila mmoja alipewa uhuru wa kujipamba kwa jinsi atakavyo, apewe chakula atakacho, au lolote atakalolitaka apewe ili tu siku atakapopelekwa mbele ya mfalme Ahasuero isionekane kasoro yoyote kama walivyofanyiwa wakina Danieli, Shedraka, Meshaki na Abednego mbele ya mfalme Nebukadreza. Hivyo mabikira wote na Esta akiwa miongoni mwao waliwekwa chini ya msimamizi mmoja wa nyumba ya mfalme Ahasuero aliyeitwa “HEGAI”.

Kazi ya huyu HEGAI ilikuwa ni kuhakikisha kuwa anawahudumia na kuwapa mahitaji yao kwa jinsi watakavyo. Tukisoma;

 

Esta 2:1-4 “ 1 Baada ya hayo, hasira yake mfalme Ahasuero ilipotulia, alimkumbuka Vashti, na vile alivyotenda, na yale yaliyoamriwa juu yake.

2 Basi watumishi wa mfalme waliomhudumu walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira vijana wazuri;

3 naye mfalme aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Shushani ngomeni, kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa HEGAI, MSIMAMIZI-WA-NYUMBA WA MFALME, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe VIFAA VYA UTAKASO.

4 Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza mfalme, naye akafanya hivyo.”

 

LAKINI NI SIRI IPI ILIYOMFANYA ESTA AKUBALIKE KULIKO MABIKIRA WENGINE?.

Biblia haimtaji Esta kama alikuwa ni mwanamke mzuri kuliko wote waliohudhuria, hapana biblia inasema alikuwa na Uso mwema tu, wala hakutokea katika familia ya kitajiri kama wenzake, wala hakuwa na elimu kama wale wengine pengine ingekuwa chachu ya kumfanya mfalme Ahasuero avutiwe naye lakini vyote hivyo hakuwa navyo. Bali kuna jambo lingine lililomfanya mfalme avutiwe naye. Na hili tunalipata kwa HEGAI, YULE MSIMAMIZI WA NYUMBA YA MFALME na MORDEKAI mjomba yake.

Wakati wengine wakimwendea Hegai na kumlazimisha awape vitu wanavyotaka wao ili wamwendee mfalme, Esta hakuwa hivyo, bali alijinyenyekeza kwa Hegai, Huku akishikilia maagizo aliyopewa na mjomba wake Mordekai kuwa ASIJIONYESHE KABILA LAKE HUKO AENDAKO, hivyo kwa jambo hilo tu ilimpelekea Hegai avutiwe naye sana kwasababu hakupeleka sifa yoyote imuhusuyo yeye mbele zake, na kwa kuwa Hegai alikuwa ni msimamizi wa nyumba ya mfalme Ahasuero, kwa uzoefu wa miaka mingi aliokuwa nao kule alitambua mfalme huwa anapenda msichana wa tabia gani au huwa hapendi msichana wa tabia gani, kwasababu yeye ndiye aliyekuwa msimamizi wa Vashti kabla hajawa malkia. Kwahiyo alitambua tabia ya mfalme kuwa anapenda mwanamke katika mwonekano upi, na katika tabia ipi. Na siri hiyo HEGAI alimfunulia Esta peke yake.Akamtenga Esta na wale wengine na kumpa matunzo ya kipekee kwa msaada wa vijakazi wengine saba.

Esta 2:8-9 “Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.

9 Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake.

10  Walakini Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe.”

Kwahiyo baada ya ule muda wa utakaso kuisha ambao ulikuwa ni miezi 12 tu, Esta na wenzake waliingizwa mbele za mfalme kila mmoja akijionyesha ujuzi wake na uzuri wake, na utashi wake, kila mmoja kwa namna yake, pengine wengine walionyesha familia za kitajiri walizotokea, wengine tamaduni zao za kujua kucheza vizuri na urembo wao, wengine pamoja na uzuri wao juu ya hilo walionyesha elimu zao kubwa mbele ya mfalme, pengine wengine walionyesha kuwa wametoka kabila moja na mfalme, hivyo wangestahili, na mambo kadha wa kadha.

Lakini tukirudi kwa Esta yeye hakuonyesha chochote, isipokuwa vile tu alivyopewa na Hegai aende navyo mbele za mfalme. Na badala yake hakuonekana aliyekuwa mfano wa Esta mbele ya mfalme.

JE! BIBI-ARUSI WA KRISTO ANAPATIKANAJE?

Tunaposoma habari hii tunajifunza kwa Bwana Yesu jinsi alivyoanza kumtafuta BIBI-ARUSI wake bikira safi tangu vizazi vya kale hadi sasa, Kwahiyo mambo haya tafsiri yake kwa kanisa ni;

>Mfalme Ahasuero anamwakilisha BWANA YESU,

>malkia VASHTI ambaye baadaye alikuja kutolewa katika Umalkia wake anawakilisha taifa la ISRAELI,

>ESTA anamwakilisha BIBI-ARUSI wa kweli aliyekubaliwa na Kristo,

> Wale mabikira wengine ; Wanawakilisha MADHEHEBU.

>Hegai na Mordekai wanawakilisha NENO LA MUNGU na Roho Mtakatifu.

Israeli kama taifa teule la Mungu, lilifananishwa na mke wa Mungu(Yeremia 3:14), na ndivyo lilivyokuwa kwa miaka yote, Lakini Mfalme wake (YESU KRISTO) alipokuja ili afanye nao karamu, walimkataa kwa kiburi na zaidi ya yote wakamzalilisha pale kalvari mbele ya dunia yote ni mfano tu wa Vashti alivyomwaibisha mfalme Ahasuero mbele ya dunia yote. Japo Bwana Yesu alikuja kwa upole kwa mke wake Israeli wao walimkataa na kumpinga, Na ndio maana tunaona Bwana Yesu aliwaambia Ee Yerusalemu, Yerusalem “Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!”

Mathayo 23:38 “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.

39 Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.”

Unaona hapo baada ya wayahudi kumkataa aliye mfalme wao na mume wao, walikuja kukatwa(Warumi 11) na kutolewa katika nafasi yao ya umalkia, na ndipo Mungu akaanza kutafuta malkia mwingine mahali pake, Ndipo NEEMA ikatugeukia sisi mataifa, akitafuta BIBI-ARUSI safi atakayekaa mahali pa Israeli.

Na kama vile tunavyoona walijihudhurisha mabinti wengi mbele za mfalme kutoka maeneo mbali mbali duniani kote. Hawa mabinti si wengine zaidi ya madhehebu mbalimbali na kila moja linajiona kuwa limestahili kuwa bibi-arusi wa BWANA YESU zaidi ya lenzake. Huoni leo hii Kanisa Katoliki linajiona kanisa pekee mama ambalo Mungu amelipokea?, walutheri nao vivyo hivyo, Waanglikana wanajiona wao ndio wapo sawa, wasabato nao vivyo hivyo wao ndio kanisa litakalokwenda kumlaki Bwana mawinguni, mashahidi wa Yehova nao vivyo hivyo, wapentekoste nao wanajiona kuwa wamestahili kuwa bibi-arusi wa KRISTO, na madhehebu mengine yote yanafanya ivyo hivyo..kumbuka leo hii duniani kuna madhehebu ya kikristo zaidi ya 40,000 na yote wanadai kuwa yapo sahihi zaidi ya mengine?. Lakini tujiulize je! Wote hawa watakuwa bibi-arusi wa Kristo??.

Jibu ni hapana bibi-arusi ni mmoja tu na ni ESTA basi. Yule tu atakayekidhi vigezo vya mfalme ndiye atakayekuwa malkia.

 

JE! ESTA NI MFANO WA DHEHEBU GANI SASA HIVI?

Tabia ya kwanza ya Esta aliyoonywa na Mordekai mjomba yake(aliye mfano wa Roho Mtakatifu) ni “KUTOKUFUNUA KABILA YAKE” mahali aendapo . Hiyo ni sifa iliyomfanya Esta apate kibali kwanza kwa HEGAI na kisha kwa Mfalme. Ukitaka kufahamu kwamba jambo la kujisifia, au kueleza chimbuko lako lilikuwa ni harufu mbaya mbele za mfalme, utaona kuwa japo Esta alikuwa ni malkia kwa muda mrefu mfalme alioishi naye hakuwahi hata siku moja kumuuliza Esta yeye ni kabila gani au jamaa zake ni nani?, au watu wake ni watu na namna gani!!, mpaka baadaye sana matatizo yalipotokea, hii ilionyesha kuwa mfalme alikuwa havutiwi na chimbuko la mtu unapokuja mbele zake, Yeye alimtaka Esta kama Esta tu katika unyenyekevu wake wote yeye kama alivyo, bila kujihesabia haki mbele zake. Na ndivyo Kristo anavyotaka watu wamwendee mbele zake.

Na jambo lingine lililomfanya Esta akubalike mbele za mfalme ni kumsikiliza HEGAI, ambaye ni Mfano wa mitume na manabii (yaani NENO LA MUNGU), Esta alipata ujuzi wa taratibu za kumwendea mfalme tofauti na wale mabinti wengine kwa kudumu katika maagizo ya HEGAI.

Na sasa hivi maana ya “KUFUNUA KABILA NI NINI?”. Pale unapomwendea Kristo na desturi za kimadhehebu; Ukatoliki, ulutheri, usabato, uanglikana, u-JW,n.k. pale unapoulizwa je! Wewe Ni MKRISTO? unasema mimi ni mlutheri, au mimi ni mbranhamite au mimi ni mpentekoste n.k…mpaka hapo hizo ni hatua za awali za wewe kutokidhi vigezo vya wewe kutokuwa bibi-arusi wa Kristo. Kwasababu pale utakapokwenda kukutana na HEGAI wako(yaani NENO LA MUNGU), na kuambiwa vitu visivyoendana na dhehebu lako.. utaishia kupinga na kujikuta unamfuata Bwana Yesu kwa desturi zako mwenyewe na sio desturi zilizopo katika NENO LAKE.

Hivyo ndugu ili uwe bibi-arusi aliyekubaliwa jambo la kwanza ondoa udhehebu ndani ya fikra zako, toka kwenye kamba za kidini na za kimadhehebu, halafu mfuate yeye kama ulivyo, unaona mafarisayo walimfuata Yesu na madhehebu yao wakaishia kukatwa, vivyo hivyo ukishikilia dhehebu na kumfuata YESU utakatwa kama wao. Mgeukie HEGAI wako yaani INJILI YA MITUME NA MANABII.. BIBLIA TAKATIFU.. mfuate MFALME YESU KWA NJIA HIYO ndipo utakapomwona.

Biblia inasema Tokeni kwake enyi watu wangu..kumbuka udhehebu ni chapa ya mnyama, alama hii ukiikumbatia itakusabibishia usimuone Bwana siku ile ya unyakuo itakapofika..bibi-arusi wa kweli wa Kristo ni mnyenyekevu aliyekaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu peke yake na kudumu katika kile NENO LINACHOSEMA na SIO KILE KANISA LINACHOSEMA.

Neno la Mungu linaposema “mwanamke avae mavazi ya kujisitiri(1Timotheo 2:9)” na wewe unasema haijalishi dhehebu letu halihimizi hivyo, ni sawa na kukataa maagizo ya Hegai na bado unataka uwe bibi-arusi hiyo haiwezekani..pia NENO linaposema “usijifanyie sanamu za kuchonga na kuziabudu (kutoka 20)” na wewe anaenda kuchukua sanamu ya mtakatifu Fulani na kuiabudu na kusema dhehebu letu linatufundisha hivyo..Na bado unasubiri siku ile uchaguliwe na Bwana uende mbinguni…Nataka nikuambie ndugu yangu siku ile utaikosa licha ya juhudi zako zote za kujionyesha kukubaliwa siku ile utalia na kuomboleza kama wale wanawali wapumbavu wa kwenye Mathayo 25 walivyokuwa. Kwasababu tu ya kuyadharau maagizo ya HEGAI (NENO LA MUNGU).

Hivyo maombi ni Bwana akupe kuliona hilo, na kuwa Bibi-arusi safi aliyestahili kwenda katika KARAMU YA MWANA-KONDOO. Mfuate Bwana kama ulivyo bila kuwa na utambulisho wowote unaokufuata hapo nyuma.

Mungu akubariki.Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> ESTA: Mlango wa 3


Mada Nyinginezo:

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

MAFUTA YA ZIADA WALIYOKUWA NAO WALE WANAWALI 10 YANAWAKILISHA NINI?

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).

MAJI YA UZIMA.

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU


Rudi Nyumbani:

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 7 & 11

Dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika wakati wa kumalizia, kurudi kwa YESU KRISTO mara ya pili kulinyakua kanisa na kuleta utawala mpya hapa duniani wa miaka 1000 umekaribia sana. Kama tukitazama unabii wa biblia tunaona kuwa baada ya Israeli kumkataa MASIA wao (YESU KRISTO), injili iliondoka kwao na kuhamia kwetu sisi mataifa.

Matendo 13:46 ” Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza(Wayahudi); lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. ” …

Matendo 28:28 ” Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!”

Tukiendelea kusoma mahali pengine mtume Paulo alisema kwenye (Warumi 11:17-24 ) kwamba Israeli kama mzeituni halisi, ulikatwa ukupachikwa mzeituni mwitu ambao ndio sisi mataifa. Hivyo kuanzia kile kipindi walichomkataa Masia, Bwana akawaacha na kuanza kushughulika na watu wa mataifa kwenye zile nyakati tofauti tofauti saba za makanisa kama tunavyosoma katika (Ufunuo 2 & 3). Na sasa ndio tupo katika lile kanisa la mwisho linaloitwa LAODIKIA.

Lakini kumbuka ukiendelea kusoma utaona pia NENO linasema..

Warumi 11 :24″ Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?

25 Kwa maana, ndugu zangu, SIPENDI MSIIJUE SIRI HII, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.

26 HIVYO ISRAELI WOTE WATAOKOKA; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 

Kwahiyo unaona hapo juu,Kuna SIRI imejificha, anasema pale UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI ndipo Israeli watarudiwa tena na kuokoka, pale ule mzeituni halisi utakapopachikwa tena na ule mwitu kuondolewa.

Swali ni je! huu utimilifu wa mataifa unawalisi wakati gani? utawasili pale zile nyakati za yale makanisa saba zitakapoisha, Kanisa la Laodikia likiwa kama la mwisho BWANA atakapomaliza kulinyakua kwenda mbinguni, sasa kuanzia wakati huo na kuendelea utakuwa ni wakati wa BWANA kushughulika na watu wake Israeli, na kitakuwa ni kipindi kifupi sana yaani MIAKA SABA tu! baada ya hapo ni hukumu ya mataifa na mwisho wa Dunia.

Tukisoma katika ufunuo sura ya pili na ya tatu, tunaona yale makanisa saba na malaika wake 7, utaona kuwa wale malaika ni wajumbe na ni wanadamu Mungu aliowanyanyua kuangaza NURU ya Mungu ambayo ilikuwa inakaribia kuzimika kwa kila nyakati, mfano Mtume Paulo alikuwa ni malaika wa kanisa la kwanza linaloitwa EFESO, Irenius-mjumbe wa kanisa la pili, Martin la tatu, …Luther la tano…William Branham la saba.

Na kama vile kila mjumbe alikuwa anamulika NURU ya wakati ule kwa kila kanisa, vivyo hivyo baada ya Mungu kuamishia INJILI Israeli kuna watu ambao Mungu atawanyanyua kuwahubiria INJILI ambayo itawafanya wao wamwamini YESU KRISTO waliyemkataa miaka 2000 iliyopita, Kumbuka leo hii Wayahudi hawamwamini YESU kuwa ndiye masia aliyetabiriwa juu yao atakayewakomboa wanasema “Kama huyu YESU ndiye Masia, na leo hii afanye zile ishara walizozifanya manabii nasi tutamwamini”, wakiwa na maana ishara kama vile za MUSA na ELIYA, Kushusha moto, bahari kuwa damu, n.k.

Kwasababu hiyo basi kwa kuwa wayahudi walikataa kumwona Mungu katika rehema na neema ya msalaba, Hivyo katika nyakati za mwisho Mungu atawapa ISHARA wanazozitaka wao. Na ukisoma biblia katika kitabu cha Ufunuo 11, utaona habari ya wale manabii 2 ambao Mungu atawanyanyua katika siku za mwisho, hawa ndio watakaoipeleka injili ya KRISTO aliye hai Israeli, zile ISHARA na yale MAPIGO yakifuatana nao..tusome 

                     **** UFUNUO 11****

1 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.

3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.

6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.

7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.

8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.

9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini.

10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.

11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.

12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.

13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.

Hawa manabii wawili watafanya kazi yao miaka mitatu na nusu ya kwanza kati ya ile saba ya mwisho, kumbuka wakati huo kanisa la Kristo litakuwa limeshanyakuliwa na wafu wameshafufuliwa neema haipo tena kwa mataifa mzeituni mwitu umeshang’olewa waliobaki ambao hawakunyakuliwa ni wale ambao walichezea neema waliyopewa wakati Kristo analia katika mioyo yao watubu, hao ndio watakaopitia DHIKI KUU na wengi wao ndio watakaoshirikiana na mpinga-kristo kuwaua wale wayahudi na wale ambao watakataa kuipokea ile chapa ya mnyama.

Kumbuka miaka 7 ya mwisho itakuwa imegawanyika katika vipindi viwili, nusu ya kwanza (yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza) injili itahubiriwa Israeli na wale manabii 2, na nusu ya pili itakuwa ni kipindi cha ile DHIKI KUU,mpinga-kristo atakaponyanyuka na kuwaua wayahudi na wale wote wasioipokea ile chapa ya mnyama, kutakuwa na mateso mengi yasiyoweza kuelezeka.

Hivyo WAYAHUDI baada ya kuona zile ishara na yale mapigo ya wale manabii 2, watagundua kuwa waliokosea, na kwamba yule waliyemsulibisha miaka 2000 iliyopita alikuwa ni MASIA wao,na hakuna mwingine, maandiko yanasema watatubu kwa kulia na kuomboleza..ukisoma

Zakaria 10:10-14″ Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.

12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;

13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.

14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao. “

Unaona hapo wayahudi watamwombolezea yule WALIYEMCHOMA(mkuki), pale KALVARI. Hivyo Mungu atawamwagia Roho ya kumwamini ndipo hapo watakapotiwa MUHURI WA ROHO MTAKATIFU, kama vile watakatifu wote wanavyotiwa muhuri kwa Roho Mtakatifu leo, kumbuka muhuri wa Mungu ni ROHO MTAKATIFU(waefeso 4:30, 1:13 ) .

Jambo hili tunaona katika kitabu cha Ufunuo 7, pale wayahudi 144,000 walipotiwa muhuri, kwahiyo kumbuka sio wayahudi wote waliotiwa muhuri bali ni wale 144,000 tu, kama vile sio wakristo wote watakaokolewa bali ni lile kundi dogo tu lilipokea Roho Mtakatifu muhuri wa Mungu, vivyo hivyo itakavyokuwa kwa wayahudi nao baada ya kanisa kuondoka

                                       *** UFUNUO 7 ***

1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.

4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.

5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.

6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.

7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.

8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. “

Umeona hapo yule malaika aliwapigia kelele wale malaika wengine akiwaambia wasiidhuru nchi mpaka watakapotiwa muhuri watumwa wa Mungu, ikiwa na maana kuwa baada ya wale wayahudi 144,000 kutiwa muhuri kitakachofuata ni mapigo ya GHADHABU YA MUNGU WENYEZI dhidi ya waovu wote walioko duniani walioipokea chapa na utawala wa mpinga-kristo.

Hivyo ndugu huu ni wakati wa kujiweka tayari hili ni kanisa la mwisho la LAODIKIA na mjumbe wa hili kanisa alishapitia (William Branham) akiwa na ujumbe wa kuwaita watu watoke katika mifumo ya madhehebu na ile dini ya uongo Katoliki, yule Babeli mkuu mama wa makahaba, Hivyo ndugu ni muhimu kufahamu saa unayoishi, na ujumbe wa wakati wako.

Angalia sasa hivi taifa la Israeli linanyanyuka biblia inasema kwa MTINI JIFUNZENI, pindi mnapoona unaanza kuchipua tena basi mjue wakati wa mavuno umekaribia, kumbuka Mtini ni Israeli na tunaona Israeli inazidi kuchipua kuonyesha kwamba neema inavyoanza kuondoka kwetu na kuhamia Israeli, Neema ikishageukia Israeli huku kwetu mlango utakuwa umefungwa na jambo hili lipo karibuni sana kutimia, Bwana Yesu alisema AMIN! AMIN! nawaambia KIZAZI HIKI HAKITAPITA, HATA HAYO YOTE YATAKAPOTIMIA, sasa kizazi kinachozungumziwa hapo sio kile kizazi cha akina Petro, bali ni KIZAZI HIKI KILICHOONA MTINI KUCHIPUA TENA (yaani ISRAELI).

Kumbuka waisraeli hakuwa na taifa huru kwa zaidi ya miaka 2500 hadi ilipotimia juzi mwaka 1948 walipopata uhuru wao (yaani kuchipuka tena). Hivyo kizazi hichi kilichoshuhudia Israeli kuwa taifa tena hakitapotea kabla ya YESU KRISTO Kuja mara ya pili. unaweza ukaona ujue ni wakati gani tunaishi!. Injili ipo karibuni kurudia Israeli ilipotokea, je! umejiweka tayari kwa unyakuo?, JE! TAA yako inawaka? Umepokea ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye MUHURI WA MUNGU.

Luka 13:23-28”

23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. “

FAHAMU KUWA PASIPO ROHO MTAKATIFU HAKUNA UNYAKUO. Kurudi kwa Yesu Kristo  kumekaribia.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mungu akubariki! Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 8

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

AMIN, NAWAAMBIA, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, HATA HAYO YOTE YATAKAPOTIMIA..!!


HOME

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 6

Katika kitabu cha ufunuo sura ya tano, tunaona Mungu akiwa ameketi katika kiti chake cha enzi akiwa na kitabu katika mkono wake wa kuume, kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba. Na hapakuonekana mtu yeyote mbinguni wala duniani aliyestahili kukifungua hicho kitabu wala kukitazama, Ni kitabu kilichobeba siri zote za ukombozi wa mwanadamu,kuanzia mwanzo wa mambo yote hadi mwisho wake, jambo lililomfanya Yohana alie machozi kwa kuwa hapakuona mtu yeyote aliyestahili kukifungua wala kukitazama. Lakini alionekana mmoja aliyestahili kukifungua hicho kitabu, naye ni BWANA YESU KRISTO haleluya!. (soma ufunuo sura ya tano yote.).

MUHURI WA KWANZA:

Ufunuo 6:1-2, “Kisha nikaona napo Mwana kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! nikaona na tazama, farasi mweupe na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.”

Tunaona kuna wenye uhai wanne na farasi wanne.Wale wenye uhai wanne walioonyeshwa katika sura hii, wanaashiria nguvu ya Mungu iliyoachiwa kwa watu wake, kupambana na uovu na njama za yule adui.Mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na wa pili alikuwa mfano wa ndama na wa tatu kama mwanadamu, na wanne kama tai arukaye.

Kwahiyo muhuri wa kwanza ulipofunguliwa, yule mwenye uhai wa kwanza aliposema njoo! akatoka farasi mweupe, na aliyempanda juu yake ana uta (upinde wa mshale). Na hiyo ni roho ya mpinga Kristo ikianza kutembea katika kanisa la Mungu kwenye kanisa la kwanza, 2thesalonike 2:3 ” Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yeyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu: akafunuliwa yule mwana wa kuasi, mwana wa uharibifu.” kwahiyo hapo tunaona kuwa mwisho wa yote usingefika kabla ya ule uharibifu( ukengeufu) kuja kwanza na kuingia katika kanisa.

hii roho ya shetani ilianza kuingia katika kanisa la kwanza baada ya mitume kuondoka hapa Paulo anasema matendo 20:29 ” najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.”

1Yohana 2:18 aliongezea kusema ” watoto ni wakati wa mwisho na kama vile mlivyosikia ya kwamba mpinga kristo yuaja, hata sasa wapinga kristo wengi wamekwisha kuwapo. kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wakwetu wangalikaa pamoja nasi.Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.”

Kwa hiyo hapa mitume walilionya kanisa juu ya mafundisho ya uwongo ambayo hayakuhubiriwa na mitume. Hivyo yule farasi mweupe ni roho ya mpinga kristo ikitembea katika kanisa la kwanza, na alionekana mweupe na aliyempanda ameshika uta (upinde) lakini hana mshale, kuashiria kutokuwa na madhara yoyote (yaani kuhusisha mauaji ya watakatifu) . roho hii ilanza kuingia kama mafundisho ya uwongo lakini Mungu aliachia Roho ya kuishinda iliyofananishwa na yule mwenye uhai wa kwanza ambaye ni Simba. Tabia ya simba ni mnyama asiyeogopa, mwenye ujasiri hivyo wadristo wa kipindi kile waliweza kuishinda ile roho ya mpinga kristo kwa ujasiri wa neno la Mungu.

Nyakati hii ilidumu kati ya kipindi cha 53AD-170AD. katika kanisa la kwanza ambalo ni Efeso.

Kristo alitoa pia angalizo kwa kanisa hili tunasoma katika kitabu cha ufunuo 2:2″ nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio ukawaona kuwa ni waongo……lakini unalo neno hili, ya kwamba wayachukia matendo ya wanikolai ambayo na mimi nayachukia.”.

MUHURI WA PILI:

Ufunuo 6:3-4 ” Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema Njoo!. akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyeimpanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.”

Hapa tunaona shetani (mpinga kristo), baada ya kuona ameshindwa kuwazuia wakristo wa kweli kumwabudu Mungu katika Roho na kweli wakisimamia neno wakiongozwa na ile nguvu ya Mungu kwa mfano wa simba ambayo ndiyo ile Roho ya Mungu aliyoiachia kwa watu wake kumshinda shetani, Hivyo shetani akabadilisha mbinu zake za kuwashambulia wakristo, kwa kubadilika kutoka farasi mweupe kwenda kuwa farasi mwekundu, na runaona aliyempanda ni yule yule aliyekuwa anamwendesha yule farasi wa kwanza. Tunasoma kuwa alipewa mamlaka ya kuiondoa amani na upanga mkubwa, kuashiria kuleta dhiki za mauaji kwa wale watu wanaomwamini Mungu na kuzishika amri zake.

Katika utawala wa Roma, Historia inaonyesha kuanzia mwaka 354AD hadi kufikia kipindi cha matengenezo ya kanisa utawala wa Rumi chini ya kanisa katoliki ulifanikiwa kuwauwa wakristo zaidi ya milioni 68, kwa dhumuni la kuimarisha itikadi za dini yao. kwa mtu yeyote kuwa na imani nyingine nje ya dini ya kikatoliki adhabu ilikuwa ni kifo. Wakristo na wayahudi wengi waliuawa kwa kusimamia imani yao. damu nyingi za watakatifu zilimwagika.

lakini Mungu aliachia Roho ya kuweza kuikabili hiyo nguvu ya mpinga kristo nayo ni nguvu iliyofananishwa na ndama, Ndama ni mnyenyekevu sana yupo tayari kwenda kuchinjwa na anaandaliwa kwa ajili ya kutolewa sadaka, hivyo wakristo wengi kwa kutaka wenyewe walijitoa maisha yao kwenda kuuawa kwa ajili ya imani yao bila kuogopa kwani Mungu ndiye aliyeachia hiyo Roho juu yao, walichinjwa, walisulibiwa, waliliwa na simba, waliburutwa lakini jinsi walivyozidi kuwauwa ndivyo walivyozidi kujitoa. warumi 8:36 ” …..kwa ajili yako tunauwa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa” kipindi cha huyu farasi mwekundu kilidumu mpaka mwishoni mwa kanisa la pili.

Na hii roho ya mauaji dhidi ya wakristo bado inatenda kazi hata leo, katika baadhi ya nchi.


MUHURI WA TATU:

Ufunuo 6:5 “na alipoifungua muhuri ya tatu,nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wa nne, ikisema, kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”

Baada ya shetani kuona anawaua wakristo na bado wanaendelea kukubali kwenda kuuawa kwa kuishikilia imani yao akaamua kubadili mbinu ya kulivamia kanisa la Mungu kwa namna nyingine kwa kubadilisha rangi kutoka kuwa farasi mwekundu kwenda kuwa farasi mweusi

Hichi ni kipindi kinachojulikana na wanahistoria wengi kama kipindi cha giza (dark age) kilidumu kwa zaidi ya miaka 1000 kuanzia karne ya 5 mpaka karne ya 16. Ni kipindi ambacho utawala wa kipapa ulianza kuuza kile wanachokiita neno la Mungu kwamfano mtu akitaka kuoa au kuolewa ni lazima atoe fedha, ibada za kuwaombea wafu (ambazo ni kinyume na neno la Mungu) ni lazima utozwe pesa, kushiriki meza ya Bwana ni lazima utoe pesa, ukitaka kusamehewa dhambi unapaswa kutoa pesa, ukitaka kuombewa kama unaumwa ni lazima utoe pesa n.k ndio maana tunasoma yule mpanda farasi alikuwa amebeba mizani mkononi mwake hii inamaanisha kuwa ukitaka kitu lazima utoe kitu. Kwa njia hii kanisa katoliki likiongozwa na utawala wa papa lilijikusanyia utajiri mkubwa sio ajabu hata leo hii tunaona jinsi taifa la Vatican lilivyo na utajiri mkubwa na halifanyi biashara yoyote ya kuliingizia kipato.

Lakini pamoja na hayo Mungu aliachilia nguvu ya kulishinda hilo giza kwa watu wake,na ile sauti iliyosikika ikisema usiyadhuru mafuta wala divai. Mafuta yanaashiria Roho Mtakatifu na divai inaashiria ufunuo wa neno la Mungu, hivyo basi lile kundi dogo la Mungu lililopitia kwenye hichi kipindi kirefu cha giza Bwana aliachia Roho ya ufunuo juu yao kwa mfano wa uso wa mwanadamu ikiashiria hekima ya kibinadamu

Katika hichi kipindi cha giza hadi kwenye matengenezo ya kanisa Mungu alinyanyua watu waliotumia hekima kama Martin Luther alihubiri (mwenye haki wangu ataishi kwa imani) ambapo hapo mwanzo ilikuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufundisha au kusoma biblia isipokuwa kwa viongozi tu wa kanisa katoliki tu!.hivyo Mungu aliendelea kunyanyua wengine wengi kama, Zwingli, Calvin, Knox,Bucer n.k kwa ajili ya matengenezo ya kanisa.

MUHURI WA NNE:

Ufunuo 6:7-8 “Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu ikafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.”

Tunaona hapa shetani ambaye ndiye mpinga Kristo alipoanza kubadilika kutoka kwenye farasi mweupe akaenda kwenye farasi mwekundu, akaenda tena kuwa farasi mweusi na sasa amekuwa farasi wa kijivu jivu. Rangi ya kijivujivu inaashiria mchanganyiko wa rangi zote tatu yaani nyeupe, nyekundu na nyeusi. ambayo pia inaashiria udanganyifu na mauti.

Hii ni roho ya mpinga kristo inayotembea sasa katika kanisa hili la mwisho (laodikia), farasi huyu amechanganyikana na anazo tabia zote tatu. Ameitwa kuzimu na mauti inamfuata kwasababu katika hichi kipindi cha mwisho anaonyesha rangi zake zote na kujifunua yeye ni nani kwa kuwaua watu na kuwapeleka kuzimu kwa mafundisho yake ya uongo, akiyaleta makanisa yote pamoja (world council of churches) na kuunda ile chapa ya mnyama. Na bado hazina yote ya dunia ipo Roma hii inaonyesha yule farasi mweusi pia bado anatembea katika utawala wa kanisa katoliki, na ni mwekundu kwasababu anawaua watu katika roho walewe kwa mvinyo wa uasherati wake na kuwafanya watu wengi wawe vuguvugu na bado pia atakuja kuwaua wakristo wengi na wayahudi katika kipindi cha dhiki kuu ambacho kiko mbioni kutokea pale mpinga kristo atakaponyanyuka kwa kupitia utawala wa kiPapa chini ya kanisa katoliki.

Pamoja na hayo Mungu ameachia nguvu ya kupambana na roho hii ya mpinga kristo nayo imefananishwa na Tai. Tai ana uwezo wa kuona vitu vya mbali na Bwana aliwafananisha manabii wake na Tai, hivyo basi katika kanisa hili la Laodikia ambalo ndio la mwisho Bwana ameachia Roho ya kinabii kuweza kuzitambua hila za yule adui, na kuturudishwa katika imani ya mababa na nguvu Mungu aliyoiachia ni ufunuo wa kumtambua Mpinga Kristo na chapa yake na ujumbe wa kutoka kwake na kutokushiriki mafundisho yake ya uongo..ufunuo 18:4 “…tokeni kwake, enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ikiwa wewe ni mkristo na hauna ndani yako Roho ya ufunuo ya kuona mbali kama Tai huwezi kamwe kumshinda shetani, utaangukia kumezwa na yule mnyama kwa mafundisho yake ya uwongo na unajua ni jambo gani linaambatana naye, biblia inasema ni MAUTI NA KUZIMU, hakuna namna yoyote utakayoweza kumshinda shetani kama upo kwenye mifumo ya madhehebu, umekwisha pokea chapa ya mnyama pasipo wewe kujijua, Kama hauna Roho Mtakatifu mwombe Mungu akupe na Roho ya ufunuo ya kulielewa neno lake.Amen!

MUHURI WA TANO:

Ufunuo 6:9-11 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”

Hapa tunaona hakuna mwenye uhai yeyote akitangaza kufunguliwa kwa muhuri huu, hivyo hatuoni kanisa la mataifa likihusishwa. lakini ulipofunguliwa muhuri wa tano zilionekana roho nyingi chini ya madhabahu zikimlilia Mungu. Hizi roho ni wayahudi waliouawa kipindi cha utawala wa kimabavu wa Hitler (Holocaust), waliuliwa kwa sababu moja tu kuwa wao ni wayahudi, historia inasema Hitler aliwaua wayahudi zaidi ya milioni 6 katika kipindi cha vita ya pili ya dunia.

wana theolojia wengi wanasema kuwa hizi roho xilizo chini ya madhabahu ni wakristo waliouawa katika kipindi cha kanisa la kwanza chini ya utawala wa Roma, lakini hiyo sio kweli, hapa tunaona kuwa hawa walikufa kwa ushuhuda wao, na sio ushuhuda wa Yesu Kristo, na pia hawa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, kwani kulingana na torati kulipiza kisasi ni desturi ya wayahudi. kwamfano tunaona kuna maandiko yanayosema jino kwa jino, jicho kwa jicho,n.k kwahiyo hatuwezi tukashangaa kwanini hapa walikuwa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, lakini hiyo siyo desturi ya wakristo. Wakristo hawalaani wala hawaombi kisasi, bali wao husema baba uwasemehe, tunaona mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo na Stefano walivyofanya.Hivyo hizi roho zinazozungumziwa hapa ni wayahudi na sio wakristo.

Pia tunaona walipewa nguo ndefu nyeupe, hizi zinaashiria kupewa neema ya wokovu kwa ushuhuda wao wenyewe walioushikilia, kwa lile agano Mungu alilomuahidia Ibrahimu na uzao wake,hawa ni wale wayahudi waliokuwa waaminifu na dini yao ya kiyahudi wakiishikilia torati kikamilifu hata kufa na sio wayahudi wote walio waliouliwa na Hitler walikuwa waaminifu na imani yao warumi 9:6 “Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. ”

wakaambiwa tena wangojee kwa kipindi kifupi mpaka idadi ya wajoli wao itimie ambao watakufa kama wao.hii inamaanisha katika kipindi cha ile dhiki kuu. Ambayo mpinga kristo atawaua wayahudi wengi na kulivunja lile agano atakalofanya na wayahudi ambalo limezungumziwa katika kitabu cha Danieli sura ile ya tisa.

(Wayahudi wakiwa katika kambi za mateso chini ya utawala wa Hitler,Nazi)

MUHURI WA SITA:

Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu na majemedari na matajiri, na wenye nguvu na kila mtumwa, na mungwana wakajificha katika pango la chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye akitie juu ya kiti cha enzi, na hasira ya mwanakondoo kwa maana siku iliyokuu ya hasira yao imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.”

Hapa tunaona muhuri huu ulipofunguliwa dunia nzima iliathirika na ndiyo ile siku kuu ya kuogofya ya Bwana kama Yesu Kristo alivyoizungumzia katika katika mathayo 24:29-30 ” Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”. Hii siku ya Bwana itakuja mwishoni mwa miaka mitatu na nusu baada ya kumalizika ile dhiki kuu

Siku hii ya Bwana itadumu kwa kipindi cha siku 75 ikianzia kwa kumimina ghadhabu ya Mungu katika dunia, ambayo itahusisha vita vya harmagedoni (ufunuo 19-21, zekaria 14:1-4, 12).ndani ya siku hizi 75 kutakuwa pia na kufufuliwa kwa watakatifu waliouawa katika kipindi cha dhiki kuu (ufunuo 11:18, 20:4), itamalizia na hukumu ya mataifa (mathayo 25:31-46) kabla ya kuingia katika matengenezo ya utawala wa miaka 1000 wa Bwana Yesu Kristo (mathayo 19:28).

hizi siku 75 zinapatikana kutoka katika zile siku 1335 zilizozungumziwa katika kitabu cha daniel 12:12. siku hizi 1335 ukitoa siku 1260 (au miezi 42) ambayo mpinga kristo atatawala baada ya kuikomesha sadaka ya kuteketezwa ya daima daniel 9:24-27″……Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”

MUHURI WA SABA:

Ufunuo 8:1 “Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.

Mstari wa pili unaelezea juu ya wale malaika waliojiweka tayari kupiga baragumu ambayo ni habari nyingine isiyohusiana na muhuri wa saba, Huu ukimya mbinguni unaashiria kuna jambo linakwenda kutokea ambalo ndilo tunaloliona katika ufunuo sura ya kumi.

katika sura ya kumi. Ufunuo 10:1-4 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi. Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.”

Malaika huyu anayeonekana hapa si mwingine bali ni Bwana Yesu Kristo akiwa ameshika kile kitabu kidogo. Na ndani ya muhuri huu wa saba ambao bado haujafunuliwa kwetu kwa sasa lakini utakapokuja kufunuliwa utampa bibi arusi wa Kristo imani ya kwenda katika unyakuo(ambayo siri hii imejificha katika zile ngurumo saba Yohana alizoambiwa asiziandike).Na muhuri huu wa saba utatimia kabla ya muhuri wa sita kutimia, kwasababu muhuri wa sita unaelezea siku kuu ya Bwana ambayo ni mwisho wa mambo yote.

kulingana na 1thesalonike 4:16-17 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.

Kuja kwa Bwana kutafuata hatua tatu, ya kwanza ni Bwana atakuja na mwaliko(shout) na ya pili ni sauti ya Malaika Mkuu na ya tatu ni parapanda ya Mungu. Hatua ya kwanza ya mwaliko ndiyo tuliyopo sasa hivi iliyoletwa na Mjumbe wa kanisa la saba (William Branham) yenye ujumbe wa kutuandaa sisi kumpokea Kristo na kuturudisha katika ukristo wa biblia.mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki” Mjumbe wa kanisa la saba alikuja kututangazia ujio wa Bwana Yesu Kristo ni wakati wa sisi kuzitengeneza taa zetu na kuwa tayari kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Hatua ya pili ni sauti ya Malaika mkuu. na ndiye tunayemwona katika ufunuo 10 na si mwingine zaidi ya Yesu Kristo, na ujumbe wake utakuwa kwa yule bibi arusi aliyekwisha kujiweka tayari kumlaki, bikira safi ambaye taa yake inawakaa, huyu ni mkristo aliyebatizwa na Roho Mtakatifu aliyejitenga na uasherati wa yule kahaba(katoliki na madhehebu yote) yasiyofanya neno la Mungu kuwa mwongozo wao na kushikilia mafundisho ya wanadamu na ibada za kipagani. Huyu bibi arusi pekee ndiye atakayeisikia sauti ya malaika mkuu ambayo itahubiriwa na zile ngurumo saba tunazoziona katika kitabu cha ufunuo 10:3-4 Yohana alizoambiwa asiziandike lakini mwingine yoyote asiye bikira mwenye busara hatoweza kuisikia sauti ya hizo ngurumo saba.

Ngurumo saba ni Sauti za watu saba ambao Mungu atawanyanyua katika kipindi hichi cha mwisho na kuleta uamsho duniani kote, ambazo kupitia hizi sauti saba tutapata imani itakayotuwezesha sisi kwenda katika unyakuo. Na hizi ngurumo saba zipo karibuni kutoa sauti zake..je? umejiweka tayari? unaye Roho Mtakatifu? watakaoweza kuupokea ujumbe wa ngurumo saba ni bibi arusi tu mwenye Roho wa kristo. Na wakati huo ukifika kutakuwa hakuna muda tena, ni wakati wa wewe kutengeneza mambo yako sasa vizuri kwa Bwana.

Hatua ya tatu na ya mwisho ni parapanda ya Mungu. katika kipindi hichi kila mmoja wetu aliye mkristo ataisikia sauti ya Mungu ikimwita na gafla tutaona mabadiliko ya miili yetu na kuchukuliwa juu mbinguni kwa Bwana milele na milele haleluya!.

Shalom! Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 7

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

AMIN, NAWAAMBIA, KIZAZI HIKI HAKITAPITA

MAONO YA NABII AMOSI.


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO:Mlango wa 6-( Maelezo ya Muhuri saba)

Tukisoma kitabu cha ufunuo sura ya tano, tunaona Mungu akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi akiwa na kitabu katika mkono wake wa kuume, kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kikiwa kimetiwa mihuri saba. Na tunasoma hapakuonekana mtu yeyote mbinguni wala duniani aliyestahili kukifungua hicho kitabu wala kukitazama, kwani Ni kitabu kilichobeba siri zote za ukombozi wa mwanadamu,kuanzia mwanzo wa mambo yote hadi mwisho wake, jambo lililomfanya hata Yohana alie machozi kwa kuwa hapakuona mtu yeyote aliyestahili kukifungua wala kukitazama. Lakini  mmoja  tu aliyeonekana amestahili kukifungua hicho kitabu, naye ni BWANA wetu YESU KRISTO haleluya!. (soma ufunuo sura ya tano yote.) utaona habari hiyo.

Kisha nikaona napo Mwana kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! nikaona na tazama, farasi mweupe na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

Lakini tukiendelea ile  sura ya 6 tunaona Bwana Yesu akivunja mihuri ya kile kitabu. Kumbuka kile kitabu sio kama hivi vitabu tunavyoviona leo, bali ni vitabu vya kuzunguka (scroll), na mihuri yake ni kama vifungo, tazama picha chini..

Na kila muhuri ulipofunguliwa ulikuwa unaambatana na tukio fulani, moja baada ya lingine, mpaka mihuri yote 7 imalizike ndipo kitabu kifunguliwe. Ni vema kama hujafahamu bado juu ya NYAKATI 7 ZA KANISA (ufunuo 2&3), ukasome kwasababu mihuri hii inaendana sana na zile nyakati saba za kanisa. kama utahitaji fuatilia link hii


MUHURI WA KWANZA:

Ufunuo 6:1-2, “Kisha nikaona napo Mwana kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! nikaona na tazama, farasi mweupe na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.”

Tunaona hapo kuna wale wenye uhai wanne na wale farasi wanne.Wale wenye uhai wanne walioonyeshwa katika sura hii, wanaashiria nguvu ya Mungu iliyoachiwa kwa watu wake, kupambana na uovu na njama za yule adui.Mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na wa pili alikuwa mfano wa ndama na wa tatu kama mwanadamu, na wanne kama tai arukaye.(Ufunuo 4:6-8). Vivyo hivyo na kwa wale farasi: farasi wa kwanza alikuwa ni mweupe, wa pili mwekundu, watatu ni mweusi na wanne ni wa rangi ya kijivujivu. Embu tuangalie ufunuo wa mambo haya kwa ufupi.

 Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema Njoo!. akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyeimpanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

Kwahiyo muhuri wa kwanza ulipofunguliwa, yule mwenye uhai wa kwanza aliposema njoo! akatoka farasi mweupe, na aliyempanda juu yake ana uta (upinde wa mshale). Huyo farasi mweupe na aliyempanda  ni roho ya mpinga Kristo ikianza kutembea katika kanisa la Mungu kwenye kanisa la kwanza Kabisa (EFESO) ,Lilidumu kwa kipindi cha kati ya AD 53- AD 170.

Mtume Paulo akiwa kama mjumbe wa kanisa hilo alisema hivi..2thesalonike 2:3 ” Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yeyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu: akafunuliwa yule mwana wa kuasi, mwana wa uharibifu.” kwahiyo hapo tunaona kuwa mwisho wa yote usingefika kabla ya ule uharibifu( ukengeufu) kuja kwanza na kuingia katika kanisa. Na huo ukengeufu ndio ulipoanza na huyo farasi mweupe, kumbuka rangi nyeupe inaashiria usafi hivyo shetani alikuwa anajigeuza kama malaika wa nurukatikati ya kanisa lakini kwa ndani alikuwa ni mbwa mwitu mkali.(2 Wakoritho 11:13-15)

Hii roho ya shetani ilianza kuingia katika kanisa la kwanza baada ya mitume kuondoka hapa Paulo anasema matendo 20:29 ” najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.” 1Yohana 2:18 aliongezea kusema ” watoto ni wakati wa mwisho na kama vile mlivyosikia ya kwamba mpinga kristo yuaja, hata sasa wapinga kristo wengi wamekwisha kuwapo. kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wakwetu wangalikaa pamoja nasi.Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.”

Kwa hiyo hapa tunaona mitume walilionya kanisa lililokuwa kipindi kile juu ya mafundisho ya uwongo ambayo hayakuhubiriwa na mitume. Hivyo yule farasi mweupe ni roho ya mpinga kristo ikitembea katika kanisa la kwanza, na alionekana mweupe na aliyempanda ameshika uta (upinde) lakini hana mshale, kuashiria kutokuwa na madhara yoyote (yaani kuhusisha mauaji ya watakatifu) . roho hii ilanza kuingia kama mafundisho ya uwongo lakini Mungu aliachia Roho ya kuishinda iliyofananishwa na yule mwenye uhai wa kwanza ambaye ni mfano wa SIMBA aliyesema Njoo!. Tabia ya simba ni mnyama asiyeogopa, mwenye ujasiri hivyo wakristo wa kipindi kile waliweza kuishinda ile roho ya mpinga kristo kwa ujasiri wa neno la Mungu.


Kumbuka Nyakati hii ya mpanda farasi wa kwanza ilidumu kati ya kipindi cha 53AD-170AD. katika kanisa la kwanza ambalo ni Efeso.

Kristo alitoa pia angalizo kwa kanisa hili tunasoma katika kitabu cha ufunuo 2:2″ nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio ukawaona kuwa ni waongo……lakini unalo neno hili, ya kwamba wayachukia matendo ya wanikolai ambayo na mimi nayachukia.”.

MUHURI WA PILI:


Ufunuo 6:3-4 ” Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema Njoo!. akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyeimpanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.”

Hapa katika muhuri huu tunaona shetani (roho ya mpinga kristo), baada ya kuona kwamba ameshindwa kuwazuia wakristo wa kweli kumwabudu Mungu katika Roho na kweli wakisimamia neno wakiongozwa na ile nguvu ya Mungu kwa mfano wa simba ambayo ndiyo ile Roho ya Mungu aliyoiachia kwa watu wake kumshinda shetani,

Hivyo shetani akaamua  kubadilisha mbinu zake za kuwashambulia wakristo, kwa kubadilika kutoka farasi mweupe kwenda kuwa farasi MWEKUNDU, na tunaona aliyempanda ni yule yule aliyekuwa anamwendesha yule farasi wa kwanza. Tunasoma kuwa alipewa mamlaka ya kuiondoa amani na upanga mkubwa mkononi mwake, kuashiria kuleta dhiki za mauaji kwa wale watu wanaomwamini Mungu na kuzishika amri zake, Kumbuka shetani huwa hafanyi vita na watu wote bali na watakatifu wa Mungu wanaolishika NENO lake.

Hii roho ya uovu(mpinga kristo) ilianza kama mafundisho yasiyohusisha mauaji, (ndiyo yale matendo ya wanikolai), baada ya kudumu muda mrefu yakatengeneza DINI, Na hii dini kumbuka ilianzia Roma kwasababu wakati ule RUMI ndio ilikuwa inatawala dunia, Wakati huo kulitokea makundi mawili, kundi lilishikilia mafundisho ya mitume tu! na lile lilichukua mafundisho yaliyochanganyikana na uongo. Ikapelekea kutokea mizozano kati ya haya makundi mawili, hivyo Rumi wakaunda dini moja chini ya mtawala(costantine), inayoitwa UNIVERSAL(CATHOLIC) CHURCH (AD 315), yaani DINI YA ULIMWENGU MZIMA. Hapo ndipo upagani wa kirumi ulipochanganyikana na Ukristo. Na ilipitishwa sheria yoyote atakayeonekana anaenda kinyume na DINI hiyo sheria ilikuwa ni moja tu! KIFO!!

Katika utawala wa Roma, Historia inaonyesha kuanzia mwaka 354 AD hadi kufikia kipindi cha matengenezo ya kanisa utawala wa Rumi chini ya kanisa katoliki ulifanikiwa kuwauwa wakristo zaidi ya milioni 68, kwa dhumuni la kuimarisha itikadi za dini yao. kwa mtu yeyote kuwa na imani nyingine nje ya dini ya kikatoliki adhabu ilikuwa ni kifo. Wakristo na wayahudi wengi waliuawa kwa kusimamia imani yao. damu nyingi za watakatifu zilimwagika.

Huu ndio ule upanga wa yule FARASI MWEKUNDU, alikuwa na kazi moja kuondoa amani katikati ya watakatifu. Na wakati huu wa farasi mwekundu ulitembea katika makanisa mawili yaani SMIRNA na PERGAMO. kati ya mwaka 170 AD -606 AD.

lakini pamoja na hayo Mungu alijua namna gani ya kuwashindia watueule wake hivyo aliachia Roho ya kuweza kuikabili hiyo nguvu ya mpinga kristo nayo ni nguvu iliyofananishwa na NDAMA (yaani YULE MWENYE UHAI WA PILI aliyesema njoo!), Ndama ni mnyenyekevu sana yupo tayari kwenda kuchinjwa na siku zote anaandaliwa kwa ajili ya kutolewa sadaka, hivyo wakristo wengi kwa kutaka wenyewe walijitoa maisha yao kwenda kuuawa kwa ajili ya imani yao bila kuogopa kwani Mungu ndiye aliyeachia hiyo Roho ya WEPESI juu yao, Kama vile tu BWANA wetu alivyokuwa mnyenyekevu akatii mpaka mauti ya msalaba, walichinjwa, walisulibiwa, waliliwa na simba, waliburutwa lakini kwa jinsi walivyozidi kuwauwa ndivyo walivyozidi kujitoa nafsi zao ziwe dhabihu .

 na alipoifungua muhuri ya tatu,nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! nikaona, na tazama, FARASI  MWEUSI, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wa nne, ikisema, kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai."

warumi 8:36 ” …..kwa ajili yako tunauwa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa” kipindi cha huyu farasi mwekundu kilidumu mpaka mwishoni mwa kanisa la pili.


MUHURI WA TATU:

Ufunuo 6:5 “na alipoifungua muhuri ya tatu,nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! nikaona, na tazama, FARASI  MWEUSI, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wa nne, ikisema, kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”

Sasa baada ya shetani kuona anawaua wakristo na bado wanaendelea kukubali kwenda kuuawa kwa kuishikilia imani yao iliyoanzishwa na mitume na si vinginevyo wakipinga mafundisho ya dini ya uongo(yaani ya kikatoliki), akaamua kubadili mbinu ya kulivamia kanisa la Mungu kwa namna nyingine kwa kubadilisha rangi kutoka kuwa farasi mwekundu kwenda kuwa farasi mweusi.

Hichi ni kipindi kinachojulikana na wanahistoria wengi kama kipindi cha giza (dark age) kilidumu kwa zaidi ya miaka 1000 kuanzia karne ya 5 mpaka karne ya 16. Ni kipindi ambacho utawala wa kipapa chini ya dini ya kikatoliki ,ulianza kuuza kile wanachokiita neno la Mungu kwamfano mtu akitaka kuoa au kuolewa ni lazima atoe fedha, ibada za kuwaombea wafu (ambazo ni kinyume na neno la Mungu) ni lazima utozwe pesa, kushiriki meza ya Bwana ni lazima utozwe pesa, ukitaka kusamehewa dhambi unapaswa kutoa pesa, ukitaka kuombewa kama unaumwa ni lazima utoe pesa n.k ndio maana tunasoma yule mpanda farasi alikuwa amebeba mizani mkononi mwake hii inamaanisha kuwa ukitaka kitu lazima utoe kitu.

Kwa njia hii kanisa katoliki likiongozwa na utawala wa kipapa lilijikusanyia UTAJIRI MKUBWA SANA USIO WA KAWAIDA, sio ajabu hata leo hii tunaona jinsi taifa la Vatican lilivyo na utajiri mkubwa na halifanyi biashara yoyote ya kuliingizia kipato, linadhamini pesa za kujenga maseminari, na mashule, pamoja na miradi mingi mikubwa duniani kote inayogharimu mabilioni ya dola na bado halifanyi biashara yoyote. Utajiri huu ulianza katika kile kipindi mpanda farasi mweusi. Kwa kuwa hii dini ya uongo ilikuwa imeshaenea duniani kote, NURU ya Mungu ilififia sana, ikasababisha GIZA nene kulikumba dunia kwasababu hakuna mafundisho ya kweli yanayohubiriwa tena. Uchawi na ushirikina vilienea sana wakati huo.

Lakini pamoja na hayo Mungu aliachilia nguvu ya kulishinda hilo giza kwa watu wake wachache waliokuwa wanashikilia mafundisho ya mitume,na ile sauti iliyosikika ikisema usiyadhuru mafuta wala divai. Mafuta yanaashiria Roho Mtakatifu na divai inaashiria ufunuo wa neno la Mungu, hivyo basi lile kundi dogo la Mungu lililopitia kwenye hichi kipindi kirefu cha giza Bwana aliachia Roho ya ufunuo juu yao kwa mfano wa USO WA MWANADAMU ikiashiria hekima ya kibinadamu, ndipo kuanzia huo wakati Mungu akaanza kuwanyanyua wana-matengenezo kuirejesha ile Nuru ya Mungu iliyokuwa inakaribia kutoweka.

Hivyo basi Katika hichi kipindi cha giza hadi kwenye matengenezo ya kanisa, Mungu alinyanyua watu kama Martin Luther na fundisho la (mwenye haki wangu ataishi kwa imani) ambapo hapo mwanzo ilikuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufundisha au kusoma biblia isipokuwa kwa viongozi tu wa kanisa katoliki!.hivyo Mungu aliendelea kunyanyua na wengine wengi kama, Zwingli, Calvin, Knox,Bucer, John Wesley na ujumbe wa (Pasipo utakatifu hakuna yoyote atakayemwona Mungu) n.k .Kwa ajili ya matengenezo ya kanisa na kulirejesha katika yale mafundisho ya mitume ya mwanzo ambayo shetani alijaribu kuyafukia.

Wakati huu wa FARASI MWEUSI, ulidumu katika makanisa matatu, yaani ; THIATIRA, SARDI, na FILADELFIA. Kuanzia mwaka AD 606-1520 AD.. ndipo ukaja wakati wa matengenezo ya kanisa.

MUHURI WA NNE:

Ufunuo 6:7-8 “Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu ikafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.”

Tunaona hapa yule MPANDA FARASI ambaye ndiye mpinga Kristo alipoanza kubadilika kutoka kwenye farasi mweupe akaenda kwenye farasi mwekundu, akaenda tena kuwa farasi mweusi na sasa kwa FARASI WA KIJIVUJIVU. Rangi ya kijivujivu inaashiria mchanganyiko wa rangi zote tatu yaani nyeupe, nyekundu na nyeusi. ambayo pia inaashiria udanganyifu na mauti.

Hii ni roho ya mpinga kristo inayotembea leo hii katika kanisa  la mwisho la saba, (LAODIKIA), farasi huyu amechanganyikana na anazo tabia zote tatu za wale farasi wa kwanza. Ameitwa kuzimu na mauti inafuatana naye kwasababu katika  kipindi cha mwisho anaonyesha rangi zake zote na kujifunua yeye ni nani kwa kuwaua watu na kuwapeleka kuzimu kwa namna mbili:

1) KWA KUWAUWA WATU KIROHO kwa  mafundisho yake ya uongo, akiyaleta makanisa yote na dini zote pamoja (WORLD COUNCIL OF CHURCHES) Kwa ulaghai wake kama ilivyotabiriwa katika kitabu cha Daniel ili kuunda ile chapa ya mnyama, ambapo hakuna mtu atakayeweza kuuza wala kununua pasipo hiyo.

2) Na namna ya pili ni kwa kuwaua wakristo wote aidha kwa wazi au kwa siri wale wanaoenda kinyume na yeye, zaidi sana atakuja kuonyesha rangi yake katika kile kipindi cha ile dhiki kuu.

Kumbuka hazina yote ya dunia ipo Roma hii inaonyesha yule farasi mweusi anatembea katika utawala wa dini ya katoliki. Na tabia zote za wale farasi wa kwanza amezibeba huyu wa kijivujivu. unaweza ukaona tunaishi katika kipindi cha hatari kiasi gani.

Lakini pamoja na hayo Mungu ameachia nguvu ya kupambana na roho hii ya mpinga kristo nayo imefananishwa na yule MWENYE UHAI WA NNE, (Aliyefananishwa na TAI). Tai ana uwezo wa kuona vitu vya mbali sana na Bwana aliwafananisha manabii wake na Tai, hivyo basi katika kanisa hili la Laodikia ambalo ndio la mwisho Bwana ameachia Roho ya kinabii kuweza kuzitambua hila za yule adui, na kuturudishwa katika imani ya mababa(yaani mitume wa Kristo) na nguvu Mungu aliyoiachia ni ROHO YA UFUNUO ya kumtambua Mpinga Kristo na chapa yake na ujumbe wa kutoka kwake na kutokushiriki mafundisho yake ya uongo..

Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu ikafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi."

 

Ufunuo 18:4 Inasema “…tokeni kwake, enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ikiwa wewe ni mkristo na hauna ndani yako Roho ya ufunuo ya kuona mbali kama Tai huwezi kamwe kumshinda shetani, utaangukia kumezwa na yule mnyama kwa mafundisho yake ya uwongo na unajua ni jambo gani linaambatana naye,

biblia inasema ni MAUTI NA KUZIMU, hakuna namna yoyote utakayoweza kumshinda shetani kama upo kwenye mifumo ya madhehebu na DINI ya uongo. umekwisha pokea chapa ya mnyama pasipo wewe kujijua, Kama hauna Roho Mtakatifu mwombe Mungu akupe na Roho ya ufunuo ya kulielewa neno lake.Amen!


Na huu wakati wa FARASI WA KIJIVUJIVU ulianza, mwaka 1906- Hadi mwisho wa dunia utakapofika pale utawala wa mpinga-kristo utakapohukumiwa na YESU KRISTO, BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME.


MUHURI WA TANO:

Ufunuo 6:9-11 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”

Hapa tunaona hakuna mwenye uhai yeyote akitangaza kufunguliwa kwa muhuri huu, hivyo hatuoni kanisa la mataifa likihusishwa wala mpanda farasi yoyote habari yao imeshakwisha.. lakini ulipofunguliwa muhuri wa tano zilionekana roho nyingi chini ya madhabahu zikimlilia Mungu. Sasa hizi ni roho za wayahudi waliouawa kipindi cha utawala wa kimabavu wa Adolf Hitler (Holocaust), watu hawa waliuliwa kwa sababu moja tu kuwa wao ni kwasababu wayahudi na si kingine!, historia inasema Hitler aliwaua wayahudi zaidi ya milioni 6 katika kipindi cha vita ya pili ya dunia.

Tunafahamu licha ya kwamba wayahudi wengi hawamwini YESU kuwa ni MASIA wao lakini bado ni watu wa Mungu na shetani anawachukia, kwasababu wanashika NENO la ushuhuda wao waliopewa na Mungu, (ambayo ni TORATI). Kwahiyo hapa tunaona kuwa hawa walikufa kwa ushuhuda wao, na sio ushuhuda wa Yesu Kristo, na pia hawa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, kwani kulingana na torati kulipiza kisasi ni desturi ya wayahudi.

Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao."

(Haya ni mateso ya wayahudi chini ya utawala wa dikteta Adolf Hitler)

kwamfano tunaona kuna maandiko yanayosema jino kwa jino, jicho kwa jicho,n.K ,Hivyo hatuwezi tukashangaa kwanini hapa walikuwa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, lakini hiyo siyo desturi ya wakristo. Wakristo hawalaani wala hawaombi kisasi, bali wao husema baba uwasemehe, tunaona mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo na Stefano walivyofanya.Hivyo hizi roho zinazozungumziwa hapa ni wayahudi na sio wakristo.

Na pia tunaona walipewa nguo ndefu nyeupe, hizi zinaashiria kupewa neema ya wokovu kwa ushuhuda wao wenyewe walioushikilia, kwa lile agano Mungu alilomuahidia Ibrahimu na uzao wake,hawa ni wale wayahudi waliokuwa waaminifu na dini yao ya kiyahudi wakiishikilia torati kikamilifu hata kufa , wakaambiwa tena wangojee kwa kipindi kifupi mpaka idadi ya wajoli wao itimie ambao watakufa kama wao.hii inamaanisha katika kipindi cha ile DHIKI KUU  ambayo mpinga kristo atawaua wayahudi wengi na kulivunja lile agano atakalofanya na wayahudi ambalo limezungumziwa katika kitabu cha Danieli sura ile ya tisa.


MUHURI WA SITA:

Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Hapa tunaona muhuri huu ulipofunguliwa dunia nzima iliathirika na ndiyo ile siku kuu ya kuogofya ya Bwana kama Yesu Kristo alivyoizungumzia katika katika mathayo 24:29-30 ” Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”. Hii siku ya Bwana itakuja mwishoni mwa miaka mitatu na nusu baada ya kumalizika ile dhiki kuu.

Siku hii ya Bwana itadumu kwa kipindi cha siku 75 ikianzia kwa kumimina ghadhabu ya Mungu katika dunia, ambayo itahusisha vita vya harmagedoni (ufunuo 19-21, zekaria 14:1-4, 12).ndani ya siku hizi 75 kutakuwa pia na kufufuliwa kwa watakatifu waliouawa katika kipindi cha dhiki kuu (ufunuo 11:18, 20:4), itamalizia na hukumu ya mataifa (mathayo 25:31-46) kabla ya kuingia katika matengenezo ya utawala wa miaka 1000 wa Bwana Yesu Kristo (mathayo 19:28).

hizi siku 75 zinapatikana kutoka katika zile siku 1335 zilizozungumziwa katika kitabu cha daniel 12:12. siku hizi 1335 ukitoa siku 1260 (au miezi 42) ambayo mpinga kristo atatawala baada ya kuikomesha sadaka ya kuteketezwa ya daima daniel 9:24-27″……Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”


MUHURI WA SABA:


Ufunuo 8:1 “Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. “

Mstari wa pili unaelezea juu ya wale malaika waliojiweka tayari kupiga baragumu ambayo ni habari nyingine isiyohusiana na muhuri wa saba, Huu ukimya mbinguni unaashiria kuna jambo linakwenda kutokea ambalo ndilo tunaloliona katika ufunuo sura ya kumi.

Kumbuka kulingana na mtiririko wa matukio yatakayotokea siku za mwisho, ni dhahiri kuwa Muhuri wa Saba utatimia kabla ya Muhuri wa sita kutimia.

katika sura ya kumi.

Ufunuo 10:1 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.

2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.

3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.

4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike”

Malaika huyu anayeonekana hapa si mwingine bali ni Bwana Yesu Kristo akiwa ameshika kile KITABU KIDOGO. kumbuka kitabu hichi ndio hicho kilichokuwa kumefungwa na mihuri 7, Na ndani ya muhuri huu wa saba ambao bado haujafunuliwa kwetu kwa sasa lakini utakapokuja kufunuliwa na upo mbioni kufunuliwa, UTAMPA BIBI ARUSI WA KRISTO IMANI YA KWENDA KWENYE UNYAKUO (ambapo ukisoma utaona siri hii imejificha katika zile ngurumo saba Yohana alizoambiwa asiziandike Ufunuo 10:4). Na muhuri huu wa saba utatimia kabla ya muhuri wa sita kutimia, kwasababu muhuri wa sita unaelezea siku kuu ya Bwana ambayo ni mwisho wa mambo yote.

kulingana na 1thesalonike 4:16-17 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.

Kuja kwa Bwana kutafuata hatua tatu, ya kwanza ni Bwana atakuja na mwaliko (shout) na ya pili ni sauti ya Malaika Mkuu na ya tatu ni parapanda ya Mungu.

Hatua ya kwanza: ya mwaliko ndiyo tuliyopo sasa hivi iliyoletwa na Mjumbe wa kanisa la saba (William Branham) yenye ujumbe wa kutuandaa sisi kumpokea Kristo na kuturudisha katika ukristo wa biblia.

Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki” Mjumbe wa kanisa la saba alikuja kututangazia ujio wa Bwana Yesu Kristo ambao ni wakati wa sisi kuzitengeneza taa zetu na kuwa tayari kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Hatua ya pili: ni sauti ya Malaika mkuu. na ndiye tunayemwona katika ufunuo 10 na si mwingine zaidi ya Yesu Kristo, na ujumbe wake utakuwa kwa yule bibi arusi aliyekwisha kujiweka tayari kumlaki, bikira safi ambaye taa yake inawakaa, huyu ni mkristo aliyebatizwa na Roho Mtakatifu aliyejitenga na uasherati wa yule kahaba (dini ya katoliki na madhehebu yote) yasiyofanya neno la Mungu kuwa mwongozo wao na kushikilia mafundisho ya wanadamu na ibada za kipagani. Huyu bibi arusi atakuwa bikira ndiye pekee atakayeisikia sauti ya malaika mkuu ambayo itahubiriwa na zile ngurumo saba tunazoziona katika kitabu cha ufunuo 10:3-4 Yohana alizoambiwa asiziandike lakini mwingine yoyote asiye bikira safi hatoweza kuisikia sauti ya hizo ngurumo saba.

NGURUMO SABA zitakuwa ni Sauti saba(watu,au huduma,) ambazo Mungu atazinyanyua katika kipindi hichi cha mwisho na kuleta uamsho mkuu duniani kote, ambazo kupitia hizi sauti saba tutapata imani itakayotuwezesha sisi kwenda katika unyakuo. Na hizi ngurumo saba zipo karibuni kutoa sauti zake..je? umejiweka tayari? unaye Roho Mtakatifu? kumbuka watakaoweza kuupokea ujumbe wa ngurumo saba ni bibi arusi tu mwenye Roho wa kristo. Na wakati huo ukifika kutakuwa hakuna muda tena, ni wakati wa wewe kutengeneza mambo yako sasa vizuri kwa Bwana.


Hatua ya tatu
: na ya mwisho ni parapanda ya Mungu. katika kipindi hichi kila mmoja wetu aliye mkristo ataisikia sauti ya Mungu ikimwita na gafla tutaona mabadiliko ya miili yetu na kuchukuliwa juu mbinguni kwa Bwana milele na milele haleluya!.

Kwahiyo kwa kuelewa Ufunuo wa MIHURI SABA, utaweza kufahamu kalenda ya Mungu na wakati unaoishi kwamba tunaishi katika siku za mwisho..


Mungu akubariki.!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 5

Shalom! Karibu katika mwendelezo mfupi wa uchambuzi wa kitabu cha ufunuo, kwa neema za Mungu tulishatazama sura zilizotangulia tukaona ile sehemu ya kwanza ya maono Yohana aliyoonyeshwa katika sura ya kwanza, ilihusu sana sana ujumbe wa yale makanisa saba ambayo tunayasoma katika ile sura ya 3 na ya 4, hivyo kama haujafahamu bado ufunuo wa yale makanisa 7 katika wakati wetu tunaoishi sasa, ni vema ukapitia kwanza kule, ili tuende pamoja katika sura hii.

Katika hii sura ya tano, tunaona Yohana akionyeshwa mfululizo wa maono mengine tofauti na yale ya kwanza ambayo alionyeshwa katika sura ile ya kwanza, sehemu hii ya pili ya maono haya yalianzia katika ile sura ya nne, yakaendelea mpaka sura ya 5, ambapo tunaona Yohana alichukuliwa juu mbinguni na kuonyeshwa kiti cha enzi cha Mungu katika roho, na wale wazee 24 wakiwa wamekizunguka kiti cha enzi, na wale wenye uhai 4, kadhalika na zile Taa saba za moto ambazo ndio Roho 7 za Mungu, na mbele ya kiti cha enzi kulikuwa pia na bahari ya kioo kama bilauri ikifunua weupe na usafi wa watakatifu, na bahari ikifunua wingi wa watakatifu, tutakuja kuona vizuri katika ile sura ya 15 inaonekana bahari nyingine ya kioo isipokuwa hiyo imechanganyikana na moto, ikifunua watakatifu waliosafishwa kwa moto katika dhiki kuu,.

Tukirudi kwenye sura ya tano, tunaona mkazo umewekwa kwa yule aliyeketi katika kiti cha enzi, na kile alichokuwa amekishika katika mkono wake wa kuume..Tusome hapo.

Ufunuo 5: 1 “Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba”.

Kumbuka hapo biblia inasema “yeye” ikimaanisha ni mmoja ambaye alishazungumziwa katika sura ya 4:2, ameshika KITABU kilichoandikwa NDANI na NYUMA. Na huyu si mwingine zaidi ya Elohim katika ofisi yake ya ubaba, ambaye yeye kabla ya kuumba ulimwengu vitu vyote vilikuwa ndani yake, yeye ndiye mjenzi wa vitu vyote vilivyokuwepo na vitakavyokuwepo, asiyekuwa na mwanzo wala asiyekuwa na mwisho, na kama yeye ndiye aliyebuni maisha na dunia na wanadamu, na malaika na viumbe vyote kama ni hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye ndiye mwenye siri na misingi ya vitu vyote. Kuanzia mwanzo wao mpaka mwisho wao, Na hakuna yeyote atakayeweza kuvumbua jambo lolote kwa uweza wake au nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwanza kafunuliwa na Mungu (Elohimu).

Kama vile tunafahamu leo hii mtu akibudi chombo chake labda tusema ni gari, siku akitaka kwenda kumpa mtu mwingine labda kumuuzia au kumrithisha hawezi kumpa hivi hivi tu bila kuambatanisha na mwongozo (MANUAL) fulani, ili kumsaidia yule anayepokea kuweza kukifahamu na kukitumia chombo hicho kwa ufasaha zaidi sawa sawa na jinsi kilivyokusudiwa kiwe. Kwa kupitia mwongozo ule atafahamu uwezo wa usafiri wa chombo chake, atafahamu wakati unaopaswa kukifanyia marekebisho, atafahamu aina ya nishati itakachotumia, atafahamu tahadhari za kuchukua wakati wa matumizi ili kisimletee madhara yoyote kwake bali faida n.k..

Vivyo hivyo na Mungu (Elohimu) kama muumbaji wa kila kitu alipoiumba dunia kwa hekima zake nyingi, na kuamua kumpa mwanadamu hakumpa pasipo mwongozo, wa jinsi ya kuindesha hii dunia na kuitunza ili iweze kumuhifadhi mtu milele asipatikane na madhara yoyote na aishi kwa amani na furaha siku zote alizowekewa mbele yake, Hivyo huu mwongozo (MANUAL) alianza kupewa mtu wa kwanza Adamu pale Edeni, Mungu alianza taratibu taratifu kumpa maarifa na kanuni za kuishi na kuitawala dunia milele.

Lakini tunaona Adamu mwanzoni kabisa mwa maagizo yale aliharibu mpango mzima, kwa kutokutii na kufuata yale aliyoambiwa ikapelekea ule mwongozo kutokuwa na maana tena mbele yake (ukafichwa) kwasababu mambo yote ameshayaharibu tangu mwanzo.

Kwamfano wewe unalo gari lako, umelibuni kwa utashi mwingi, na umekusudia kumrithisha mwanao liwe lake moja kwa moja, lakini wakati unaanza tu kumwonyesha gari kwa nje, matairi, vioo, milango, site mirrors n.k. yeye unashangaa tayari kashafungua mlango na kupiga ufunguo kasha kukanyaga mafuta na kuanza kuondoka,kumbuka na hapo hajawahi kuendesha gari hata siku moja, ni mara yake ya kwanza, ila amesikia tu! Ukishawasha gari weka “D” kisha kanyaga mafuta gari litaenda..wewe unadhani ni jambo gani litatokea hapo kwa mtu kama huyo? Ni dhahiri kuwa atasababisha ajali?? Na mwisho wake ni mauti??. Hicho Ndicho kilichomtokea Adamu, pale Bwana alipomwonyesha kuwa hii dunia ni urithi wake, hakusubiria ule mwongozo ambao alikuwa anapewa taratibu taratibu, siku baada ya siku na Baba yake…yeye alikimbilia moja kwa moja kusikiliza mwongozo bandia wa Shetani, wa jinsi ya kuiendesha hii dunia kama Mungu anavyoiendesha, Biblia inasema..

Mwanzo 3:4 “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya”.

Unaona hapo ni kweli ulikuwa ni mpango wa Mungu Adamu kufahamu mema na mabaya, lakini ilikuwa sio kwa wakati ule, bali Mungu alikusudia kumpa mwongozo kidogo kidogo, lakini yeye kwa maneno machache tu ya shetani alidhana kuwa angeweza kuiendesha dunia kama Mungu, matokeo yake maarifa yale yalimsababishia KIFO. Hivyo Mungu asingeweza kuendelea kumpa mwongozo ule mtu ambaye yupo katika hali ya mauti. Kuanzia hapo Mungu AKAUFUNGA ule mwongozo kwa MIHURI asiweze mtu yeyote kuifungua mpaka atakapoonekana anayestahili.

Kwahiyo Huu mwongozo ni kitabu cha MAARIFA ya Mungu juu ya mwanadamu na urithi aliopewa, kimebeba siri zote za uumbaji wa ulimwengu, misingi yake ilipo, namna ya kuifanya idumu milele, namna ya kuifanya iwe na amani,furaha, namna ya kuifanya mwanadamu asiishi kwa taabu, shida, maumivu, kero, adha n.k..kimebeba siri zote zinazohusiana na sayari na magimba mengine huko angani, na mambo mengine mengi sana ambayo hata sasa hivi hatuyajui..Hayo yote yapo ndani ya hicho kitabu na ndio hicho tunakuja kukiona tena katika Ufunuo sura ya 5 kimeshikwa na yeye (ELOHIMU) mwenyewe katika kiti chake cha enzi kikiwa kimefungwa kwa mihuri saba huku kikiwa kimeandikwa NDANI na NYUMA.

Tukiendelea kusoma.

Ufunuo 5: 2 “Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?

3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi”.

Unaona hapo? Hakuonekana mtu aliyestahili kukifungua hicho kitabu wala kukitazama, mara baada ya Adamu kuasi tu,tangu huo wakati hakuonekana mtu yeyote aliyestahili, na sio tu kikifungua bali hata kukitazama,! Hivyo Yohana alivyoona alilia sana, kuona kuwa dunia itaendelea kubaki vile vile katika hali yake ya ubovu, kama ilivyokuwa zamani, majanga, magonjwa, vifo, dhiki, taabu, shida, vitaendelea kuwepo, dunia itaendelea kuyumba yumba kama mlevi hivyo hivyo mpaka itakapofikia uharibifu wake.

Jaribu kifikiria hata ingekuwa ni wewe katika hali kama ile kuona hata malaika wa mbinguni hakuna aliyeonekana amestahili,..hakika ungevunjika moyo sana na kulia, ungeona hakuna tumaini tena, maisha hayana maana tena, …Lakini ashukuriwe Mungu wa mbingu na nchi, kwani alionekana MMOJA aliyestahili kukifungua kile kitabu na kuvunja mihuri yake naye si mwingine zaidi ya Simba wa Yuda, Bwana wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme, YESU KRISTO Bwana wetu, sifa na utukufu vina yeye milele na milele Amina..yeye pekee ndiye aliyestahili kukitwaa kile kitabu, hivyo basi tumaini la marejesho lipo! Limeinuka tena! Haleluya!!.

Na ndio maana ilimpasa aje duniani kwanza ajaribiwe kama sisi tulivyojaribiwa, aishi kama sisi tulivyoishi, bila kutenda dhambi yoyote, afe msalabani bila shutumu lolote kisha aongezee kuwakomboa wanadamu kwa damu yake, ili siku ile asiwe peke yake bali pamoja na ndugu zake (yaani mimi na wewe) na ndipo apande mbinguni akajionyeshe mbele za Mungu kuwa amestahili yeye kukitwaa hicho kitabu na kuvunja mihuri yake..Lakini kama asingeyapitia hayo yote kuishi na kufa kwa ajili yetu, kadhalika yeye naye asingestahili hata kikutazama kile kitabu.Lakini alishinda ili sisi nasi tushinde pamoja naye, Utukufu na heshima anastahili yeye peke yake milele na milele amina.

Lakini kumbuka pia usisahau jambo hili Yesu Kristo ni Elohimu mwenyewe katika mwili,( soma 1Timetheo 3:16) na ndio maana utaona pale katikati ya kile kiti cha enzi anatoka mwanakondoo, ambaye ni Yesu Kristo, Ni Elohimu Yule Yule akijidhihirisha katika ofisi ya mwana (Ufunuo 5:6), Na ndio maana tukiendelea, kusoma tunaona viumbe vyote mbinguni na duniani vyote vinatambua kwamba amestahili yeye pekee kukifungua kile kitabu..

Ufunuo 5:8-14“8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.

14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.”

Kumbuka Bwana Yesu alivyokuwa duniani, hakufahamu mambo yote, na ndio maana alisema siku ile hakuna mtu aijuaye, hata mwana bali Baba, lakini alipopaa juu mbinguni, alipewa funguo zote, ikiwemo funguo za mauti na kuzimu, pamoja na mamlaka yote ya mbinguni na duniani, na ukuu, na ufalme,kuteka vipawa na URITHI wote, n.k. mambo haya yote yalikuwa ndani ya kile kitabu cha mwongozo kilichokuwa katika mkono wa Mungu mwenyezi.

Hivyo alipopaa mbinguni ndipo alipokwenda kutwaa kile KITABU, na hapa Yohana anaonyeshwa katika maono siku aliyopokea Kitabu kile, Kumbuka kitabu kile kimeandikwa NDANI na NYUMA,. Ikimaanisha kuna mambo ya nje na ya ndani,..Ya nje! Ndio hayo tutakayoyajua tukiwa hapa duniani, bali ya ndani tutayafahamu vizuri tukifika mbinguni..ndio siku hiyo tutafahamu vizuri maana ya yale maneno Bwana aliyotuambia

Yohana 14: 1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

4 Nami niendako mwaijua njia.”
Makao yanayozungumziwa hapo ni miili yetu ya utukufu, urithi wetu wa milele unaokuja.

Ndani ya kile kitabu kumeandikwa urithi wote umuhusuo mwanadamu na mambo anayopaswa kuyafanya ili dunia iwe katika hali ambayo Mungu aliikusudia tangu mwanzo, kuna siri nyingi na maarifa mengi Mungu ameyasitiri ambayo sehemu ya hayo yatakuja kufunuliwa kwa Bibi-arusi wa Kristo pekee! Tukiwa hapa hapa duniani itakuwa ni karibia sana na nyakati kufungwa (karibia na unyakuo), ndio zile ngurumo saba, ambazo hazijarekodiwa mahali popote katika biblia, hizo zitampa Bibi-arusi imani ya kunyakuliwa, na sehemu iliyobaki ya ndani ya kitabu hicho tutaijua tukifika mbinguni mara baada ya kubadilishwa miili yetu,

Kumbuka mbinguni tutaenda kwa kitambo tu! Urithi wetu ni hapa DUNIANI, Mungu ndio aliotupa,.Tutaenda mbinguni kisha tutarudi, na ndio maana maandiko yanasema Kristo atarudi tena, moja ya kusudi la sisi kwenda mbinguni, si tu kufunuliwa uzuri wa kule bali pia kufunuliwa siri za urithi wetu tuliopewa na BABA na mikakati ya kuiunda tena kulingana na ule mwongozo ambao Bwana Yesu aliutwaa katika mkono wa ELOHIMU. Na baada ya hayo Kristo atashuka na watakatifu wake kutoka mbinguni, kuisafisha dunia.(urithi tulioahidiwa na baba)

Ndugu yale mambo yote ambayo tulikuwa hatuna majibu nayo, kwanini hivi?..kwanini vile?..ingekuwa hivi..ingekuwa vile..n.k…yote haya tutapata majibu yake siku ile tukifika mbinguni. Na ndio maana ukisoma Ufunuo 20:5-7, utaona kuna utawala wa MIAKA 1000 wa Bwana wetu Yesu Kristo unazungumziwa pale..Sasa hii miaka 1000 itakuwa ni miaka ya matengenezo kwa hekima ya ki-Mungu, kuirejesha dunia katika viwango vya ule urithi unaopaswa uwe, kuanzia hali iliyokuwepo pale Edeni na kuendelea..bahari itaondolewa, uovu utadhibitiwa, majangwa yatabadilishwa na kuwa kama Edeni, wanyama watarejeshwa katika hali yao ya asili, samba atakula majani kama ngo’ombe hawatadhuriana n.k dunia itajaa Amani (soma Isaya 65:17-25 na Isaya 11:1-9) Na baada ya ile miaka 1000 kuisha ya Kristo kuijenga dunia pamoja na watakatifu wake, kwa wakati huo dunia sasa itakuwa tayari kustahimili UMILELE. Wakati huo wale waovu wote watahukumiwa katika kiti cheupe cha enzi cha Mungu, pamoja na shetani na malaika zake kwa pamoja watatupwa katika lile ziwa la moto.

Huko katika UMILELE kusikokuwa na muda, ni kuishi tu, kuishi tu, kusikokuwa na mwisho, raha isiyokuwa na kifani, kila siku kutakuwa na uvumbuzi wa mambo mapya kumuhusu Mungu, itatuchukua umilele kumaliza kumjua Mungu, kila siku tutamwona Mungu ni mpya kwetu,hakutakuwa na dhambi tena wala waovu, wala machozi wala magonjwa,wala uchungu, wala shida,wala njaa wala mateso..Ni raha isiyokuwa na kifani..Na siku hiyo ndipo tutakapojua maana ya mstari huu.

Isaya 55: 8 “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.

9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”. Na Maana ya mstari huu Yeremia 29: 11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”.

Tutampenda Mungu kwa viwango vingine, tutakapojua kuwa hakuumba kitu kinyonge wala kidhaifu bali kikamilifu ni sisi wenyewe ndio tuliojiharibu.

Ufunuo 21: 1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7 YEYE ASHINDAYE ATAYARITHI HAYA, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Tukiyajua hayo ndugu na mambo mazuri ambayo Mungu ametuandalia, hatutataka tupoteze URITHI huu ambao Mungu ametuandalia kwa mambo ya kitambo tu yapitayo,.Itakufaidia nini leo hii upate kila kitu, uwe wa kisasa kuliko watu wote, uwe wa kidunia kuliko watu wote, uwe maarufu kuliko watu wote halafu siku ile unakuwa hauna sehemu katika ule urithi wa watakatifu, Kama sasa hivi unaona uchungu kukosa utajiri tu wa kitambo itakuaje kule utakapoona unakosa URITHI NA UTAJIRI wa milele usioisha, hapo ndipo kutakuwa na majuto yasiyokuwa na mwisho, uchungu hautakuwa sana kwasababu unakwenda kuteketea katika ziwa la moto, uchungu utakuja utakapoona wenzako ndio wanaanza kuona maana ya maisha kwa kurithi yote hayo na wewe huna kitu haupo.

Bwana anasema Zaburi 147:4-5 “[Yeye] Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.
5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka”.

Kila nyota ya mbinguni inayo jina, ikimaanisha kuwa zimepewa uhai, hazijawekwa kama urembo tu! Na kuna mabilioni ya nyota mbinguni na kumbuka kila nyota ina mfumo wake wa sayari, hivyo kuna mabilioni na mabilioni ya sayari na magimba angani ambayo hayo yote yana makusudi yake, ambayo yatapata kazi huko mbeleni (kwenye umilele), huo wote ni urithi wa watoto wa Mungu, Unaweza kuona ni jinsi gani itatuchukua umilele kummaliza Mungu na utajiri mkuu ulioko huko mbeleni.

Kwanini usitamani uwepo huko? Mpe Kristo leo maisha yako ayakomboe, ukabatizwe na umaanishe kabisa kumuishia Kristo naye ameahidi atakupa uwezo wa kushinda dhambi, na kuwa pamoja nawe siku zote.

Ubarikiwe

Katika sura ya sita tutaona hatua za awali kabisa wa kile kitabu kufunuliwa kimeshaanza, na sasa hivi tupo katika hatua ya mwisho ya kufunuliwa kwa muhuri wa saba, na siku yoyote utafunuliwa,

Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki.Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 6

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 4

Shalom! Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tukiendelea na ile sura ya 4, tulishakwisha kuona katika sura zilizotangulia jinsi Mungu alivyotembea katika yale makanisa 7 yaliyokuwa Asia ndogo, yaliyowakilisha makanisa 7 katika nyakati saba tofauti tofauti kuanzia wakati wa Pentekoste hadi wakati wa kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili, na tuliona pia sisi tunaishi katika kanisa la mwisho, linalojulikana kama Laodikia, na kwamba baada ya hili hakutakuwa na kanisa lingine la nane, kadhalika pia kila kanisa lilikuwa na mjumbe wake, na kanisa hili la mwisho mjumbe wake alikuwa ni Ndugu.William Branham ndiye Mungu aliyemnyanyua kubeba ujumbe wa nuru ya wakati huu wa mwisho. Hivyo ukiwa haujapitia sura zilizotangulia ni vizuri ukazipitia kwanza , ili tuende pamoja.

Sasa katika sura hii ya nne tunasoma..“1 Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo”.

Hapa tunaona Mtume Yohana ambaye anamwakilisha bibi-arusi wa Kristo (Kanisa), akisikia sauti ambayo ndio ile iliyokuwa inazungumza naye hapo kwanza kutoka mbinguni, na sauti hiyo sio ya mwingine zaidi ya sauti ya Bwana wetu YESU, ikimwambia “Panda hata huku nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo “. Unaona hapo kabla Yohana hajajua lolote mlango ulimfungukia kwanza mbinguni, ikimaanisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayeweza kupokea ufunuo wowote ule wa Roho kama mlango wa mbinguni haujamfungukia,.Kanisa/mtu ni lazima awe wa rohoni kwanza ndipo liweze kuelewa mambo ya mbinguni, vinginevyo halitaweza kuyaona yaliyo juu likitegemea mifumo au mapokeo ya kibinadamu peke yake.

Na tunasoma pia ile sauti ikamwambia “Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi KUWAKO BAADA YA HAYO”. Ikiwa na maana kuwa, yale maono aliyoonyeshwa kwanza, kama tulivyotangulia kusoma huko nyuma, Yohana alivyomwona YESU KRISTO katika ule mwonekano mwingine, mwenye uso kama jua, macho kama miale ya moto, miguu kama ya shaba n.k. alimwona akitembea katika vile vinara saba, pamoja na nyota saba katika mkono wake, n.k. haya yote yalifunga sehemu ya kwanza ya maono…Na sasa hapa anafungua sehemu ya pili ya maono mengine ambayo yatakuwa pia ni msingi wa mambo mengine tutakayokuja kuyaona huko mbeleni yahusuyo mihuri saba, kama tu vile yale maono ya kwanza yalivyokuwa msingi wa kufahamu tabia za makanisa saba. Na ndio maana hapo anasema ” Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. “..Hivyo ni muhimu kuyazingatia haya maono pia kwasababu tusipoyaelewa hapa mwanzoni basi sehemu zinazofuata za kitabu cha Ufunuo zitakuwa ni ngumu kuelewa,..

Tuliona kila kitu Yohana alichoonyeshwa katika lile ono la kwanza linalohusu mwili, tabia na mwonekano wa Kristo (Ufunuo 1) vilikuwa na maana kubwa katika yale makanisa 7 yaliyofuata (Ufunuo 2&3), Kwamfano ile miguu ya shaba ilikuwa na sehemu yake katika ujumbe wa kanisa husika, kadhalika na yale macho kama mwali wa moto, na ule upanga utokao kinywani mwake, na vile vinara saba na zile nyota saba zilizokuwa mkononi mwake n.k. yote haya tuliona jinsi yalivyokuwa na mahusiano makubwa sana katika kuelezea nyakati saba za kanisa..Vivyo hivyo na hapa pia katika hii sehemu ya pili ya maono, ambayo Yohana aliitwa juu kuonyeshwa mambo mengine tofauti na aliyoyaona hapo kwanza..Tusome;

Ufunuo 4:2 “Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;

3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.

5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.

7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.

8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.

9 Na hao wenye uhai wanne wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,

10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,

11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”.

Mstari wa pili unasema..Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;

3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi”.

Hapa Yohana anaonyeshwa kiti cha Enzi na “MMOJA” Kumbuka sio watatu, ameketi katika Kiti hicho, na anaonekana pia mithili ya jiwe la yaspi na akiki,. Sasa kumbuka mawe haya kwa wakati wa agano la kale yalikuwa ni mawe yenye uzuri wa kipekee na ya thamani kubwa sana,yalitumiwa na makuhani katika kifuko cha kifuani (Kutoka 28:15), ni mawe 12 yaliyotumika kama Urimu na thimimu na mojawapo ya hayo mawe ndio Yaspi na akiki, Hivyo hapo mawe hayo yanafunua UZURI wa Mungu, na thamani ya Uzuri wake kwetu sisi wanadamu pia Yohana aliona kile kiti kimezungukwa na upinde wa mvua ikifunua rehema na neema za Mungu pamoja na uthabiti wa maagano yake, Kumbuka baada ya Gharika Mungu kwa rehema zake aliuweka ule upinde wa mvua kama Ishara ya kughahiri hasira yake itakapokuja kutokana na maovu ya watu.

Tukiendelea tunaona pia, Yohana alionyeshwa wazee 24 wamekizunguka kile kiti cha Enzi, wamevikwa mavazi meupe na juu ya vichwa vyao walikuwa na mataji ya dhahabu, pamoja na taa 7 mbele ya kile kiti cha enzi ambazo ndio Roho 7 za Mungu, Kadhalika pia alionyeshwa wale wenye uhai wanne wamekizungu kiti cha enzi wote kwa pamoja wakimpa Mungu utukufu

Kwahiyo Mungu alikuwa anamuonyesha Yohana, mahali kiti chake cha enzi kilipo,kwamba ni lazima kiwe kimezungukwa na wale wazee 24, pili kiwe kimezungukwa pia na wale wenye uhai wanne Na tatu kiwe na Taa saba mbele yake…Hapo kiti cha enzi cha Mungu kimekamilika..hakuonyeshwa kama kimezungukwa na miji au makasri na magorofa ya dhahabu hapana.

Sasa huyu aliyeketi katika kiti cha enzi ni nani?

Kwa maelezo yake marefu tutakuja kumuona vizuri katika sura inayofuata ya tano.

Lakini sasa tuwatazame wale wazee 24 ni akina nani?.

Kwanza ni vizuri kufahamu mbinguni hakuna wazee 24, walioketi kando kando ya Mungu hapana, kumbuka yale ni maono, na wale wazee 24 ni ROHO 24 za Mungu zinazotengeneza ufalme wake katikati ya wanadamu, na ndio maana zimechukua taswira ya mwanadamu. Sasa hizo roho 24 ziliachiwa ulimwenguni kulitengeneza taifa la Mungu katikati ya wanadamu,.Na tunafahamu kuwa ufalme wa Mungu (KANISA) umeundwa na mataifa mawili,nayo ni Wayahudi na Wakristo.

Hivyo mwanzo kabisa Bwana alipoanza kuunda ufalme wake alianza na taifa la mwilini (yaani Israeli), na tunajua taifa la Israeli limegawanyika katika makabila 12, Mungu aliruhusu hivyo makusudi ili kulitengeneza taifa lake. Hivyo Bwana aliachia hizi roho 12 za kwanza kukaa juu ya kila kabisa ili kulijenga taifa la Israeli ambalo ni sehemu moja ya ufalme wake. Ndipo hizi roho zikaanzia kwa wana 12 wa Yakobo na kuendelea.

Lakini baadaye Mungu alipokusudia kuunda sehemu ya pili ya ufalme wake, ndipo akawajia watu wa mataifa (sisi), hivyo kama tu alivyoanza na misingi 12 katika taifa la Israeli kadhalika na huku pia alianza na misingi 12, kujenga sehemu ya pili ya ufalme wake, hivyo akaachia Roho nyingine 12 zilizokuja kukaa juu ya wale mitume 12 wa Bwana Yesu. 

Wefeso 2: 20 ” Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”.

Ile injili tuliyoipokea sisi kwa mikono ya mitume wa Bwana ndio imekuwa chachu mpaka leo hii ukristo umeenea duniani kote, Hizo ndio zile Roho 12 nyingine zilizoifanya hiyo kazi, kwahiyo kwa ujumla watakatifu wote wa agano la kale na wa agano jipya ndio wanaokizunguka kiti cha enzi cha Mungu katika roho, ndio wale wazee 24…Na ndio maana utaona wamevikwa mavazi meupe kuashiria usafi na weupe wa watakatifu na mataji kuashiria mamlaka ya kifalme kwa ushindi waupatao kutoka kwa yule adui.

Kadhalika na wale wenye uhai wanne, ni Roho nne za Mungu zinazowakilishwa na tabia za wale wanyama wanne. Utaona pia walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma, ikiashiria kuwa wapo kwa kazi ya ulinzi, wanaona vitu vitakavyokuja kabla hata havijawasili, wanaona mambo yaliyopita na yanayokuja.

Kwamfano mwenye uhai wa kwanza alionekana akiwa na mfano wa simba, inamaanisha kuwa ni Roho ya Mungu iliyokuwa ikililinda (Kanisa la Mungu), kwa wakati husikia ikijifunua kama tabia ya Simba. Tunajua simba siku zote sio mwoga, ni jasiri, hivyo tutakuja kuona huko mbeleni ni wakati gani hii Roho ilijidhihirisha hivyo katikati ya watu wa Mungu.Kadhalika na yule mwenye uso kama wa ndama, na yule mwenye uso mfano wa Tai arukaye n.k. wote hawa wanabeba tabia fulani inayoendana na maumbile yao..hizi roho zimechukua mfano wa malaika zina mabawa na kupaa tofauti na wale wazee 24, zenyewe zilikuja kwa mfano wa wanadamu,..

Kadhalika tunaona pia Taa saba za moto mbele ya kile kiti cha enzi. Hizo ni roho saba za Mungu, ambazo tulishakwisha kuziona zenyewe kwenye sura zilizotangulia zikitembea katika yale makanisa saba ya Mungu.

Kwahiyo kwa ujumla katikati ya vitu hivyo vyote ndipo kiti cha enzi cha Mungu kilipo, yaani ndani ya kanisa lake (Israeli na Mataifa), linaloongozwa na hizo Roho saba, na Roho za wenye uhai wanne, Hivyo ni muhimu kufahamu ni roho gani inayoliongoza kanisa ulilopo sasa, kadhalika na ni Roho ya mwenye uhai yupi aliye juu yako na juu ya wakati wa kanisa ulilopo vinginevyo hutaweza kukiona kiti cha enzi cha Mungu au kumshinda shetani kwa namna yoyote ile katika wakati huu unaoishi.

Kumbuka shetani naye anacho kiti chake cha enzi, na chenyewe pia kimezungukwa na roho chafu nne, ndio wale wapanda farasi wanne ambao tutakuja kuwaona katika sura ya 6, na anazo roho nyingine chafu saba, ndizo zilizokuwa zinatembea pia katika makanisa saba ya Mungu kulichafua kanisa la Mungu na kupoteza watu Ndio zile Bwana Yesu alizozizungumzia katika..

Mathayo 12: 43 ” Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye PEPO WENGINE SABA walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa KIZAZI HIKI kilicho kibaya. “

Unaona hapo katika ile siku ya Pentekoste Bwana alilijenga tena kanisa kwa kulitakasa kwa Roho wake, kwa wakati ule Kanisa lilikuwa kamilifu lakini mitume wa kweli walipoondoka,mitume wa uongo wakanyanyuka kuunda misingi ya kanisa lingine la uongo na kuanza kuchanganya kweli ya Mungu na mafundisho ya kibinadamu, hivyo ikapelekea ile roho (pepo) ambalo Bwana Yesu alilitoa pale Kalvari kurudi tena katika kanisa la Mungu kwa taswira mbaya zaidi, lilirudi katika mwishoni wa kanisa la kwanza, kadhalika na katika kanisa la pili likaongezeka lingine la pili, na katika kanisa la tatu, na la nne, mpaka kanisa la saba, mapepo yote saba maovu yakalivaa kanisa, na ndio maana hali ya kanisa hili la Laodikia ni mbaya kuliko makanisa yote yaliyotangulia…Lakini siku zote mbegu halisi haiwezi changanyikana na ya uharibifu Bwana alishalianza kuwatenga watu wake na kanisa hilo la uharibifu tangu zamani.

Hivyo ni muhimu kufahamu pia kiti cha enzi cha shetani kilipo, kwasababu yeye naye anachokiti chake cha enzi Soma Ufunuo 2: 13 ” Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; ….” Unaona hapo?

Ikiwa na maana kuwa hata yeye naye analo kanisa lake aliloliunda ndipo aketipo yeye. Na kanisa hilo ni Kanisa Katoliki. Hilo ndilo linaloongozwa na (mapepo) yale saba maovu, na wale wapanda farasi wanne, ambao kwa ujumla roho hizi zilishughulika sana kupambana na uzao wa Mungu na kuuharibu kama tutakavyokuja kuona katika sura ya sita.

Kama vile Mungu alivyotwaa mwili na kuishi katikati yetu na kufanyika mfalme wa kanisa la Mungu, kadhalika shetani naye amemtia mtu mafuta akae badala yake katika kiti chake cha enzi, na si mwingine zaidi ya mpinga-kristo (PAPA atakayekuja) aliye kichwa cha kanisa hilo la uongo.

Hivyo ndugu jiulize je! umeketi katika kiti cha enzi cha Mungu au cha shetani??..Kama unadai umeketi katika kiti cha enzi cha Mungu, na bado haupo katika misingi ya mafundisho ya mitume 12(BIBLIA), na haufahamu kanisa unaloishi!, na hauifahamu Roho inayoliongoza kanisa lako? basi ni dhahiri kabisa kwamba unaketi katika kiti cha enzi cha shetani pasipo hata wewe kujijua, kwasababu ile roho ya uhai yenye macho mbele na nyuma ambayo ingepaswa ikuongoze haipo juu yako ambayo ingekupa wewe uhai na macho ya kuweza kuona mambo ya mbele na ya nyuma na kukuwezesha wewe kuzijua fumbo za shetani imeondoka. Na pia kumbuka viti vyote vya enzi (cha MUNGU na cha shetani) vinaundwa hapa hapa duniani..Hivyo jitathimini maisha yako. je! umeoshwa kwa damu ya YESU KRISTO na kujazwa Roho Mtakatifu? Huyo tu ndiye atakayekuongoza katika kweli yote na sio dini au dhehebu. Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako kabla haijakaribia miaka utakayosema sina furaha katika hiyo (Mhubiri 12).

Ubarikiwe. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 5

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana..

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

MKUU WA GIZA.


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Sehemu ya tatu:

Jina kuu la Bwana wetu YESU KRISTO litukuzwe. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tukimalizia sehemu ya mwisho ya sura hii ya tatu. Ambapo tutaona kanisa lile la LAODIKIA. Tulishatazama makanisa mengine 6 yaliyotangulia pamoja na wajumbe wao, na jumbe walizopewa kutoka kwa Bwana.Kama haujayapitia unaweza ukayapitia kwanza ili tuende pamoja katika kanisa hili la mwisho, Tunasoma…

Ufunuo 3: 14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”.

Kama tulivyotangulia kujifunza tunaona ule utambulisho wa kwanza Bwana anaoutoa kwa kanisa, huwa una uhusiano mkubwa sana na ujumbe wenyewe wa kanisa husika. Hapa Bwana anasema ” yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu “. Na hasemi “yeye aliye na ule ufunguo wa Daudi, au yeye mwenye uso ung’aao kama jua. au yeye aliyekuwa amekufa kisha akawa hai” kama alivyokuwa anasema katika makanisa yaliyotangulia, hapana bali anasema “anenaye yeye aliye Amina, SHAHIDI MWAMINIFU na wa Kweli”. Ikiashiria kuwa katika kanisa hili anatazamia kuona UAMINIFU, kama aliokuwa nao yeye tangu mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

Kwa ufupi kanisa hili la Laodikia lilianza kati ya kipindi cha mwaka 1906 WK na litaisha na siku ya ujio wa Bwana mara ya pili (yaani Unyakuo). Na mjumbe wa kanisa hili ni WILLIAM BRANHAM. Na tafsiri ya neno LAODIKIA ni “HAKI ZA WATU”. Katika Asia ndogo ambapo haya makanisa 7 yalikuwepo, Mji wa Laodikia ndio uliokuwa umeendelea kuliko miji mingine, kama efeso, smirna, pergamo n.k. Ni mji uliokuwa tajiri kuliko yote, ulikuwa upo juu kibiashara na kiuchumi na kiusomi, hivyo ikapelekea na watakatifu waliokuwa katika mji huo kuwa na hadhi ya kitofauti na watakatifu waliokuwa katika miji mingine. Na ndio maana hatushangai kwanini Bwana Yesu kutoa ujumbe ufuatao;

“15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.

Unaona hapo? kutokana na mafanikio makubwa yaliyokuwepo katika ya hao watu, Ikawafanya watakatifu waridhike na kupoa sana kiroho pasipo hata wao kujitambua. Watu wa mji ule (wasiomjua Mungu) wakaanza kuweka mambo kwenye mizani, kila kitu nusu kwa nusu, kama tafsiri ya jina lake lilivyo “HAKI ZA WATU” Mambo kama haki sawa, yakazaliwa wanaume kwa wanawake,

Sasa hii roho ya haki sawa nayo ikapenyeza mpaka kwenye kanisa la Mungu.. Kwamba kwa Mungu kuna haki sawa, nusu kwa nusu, Mungu kidogo na Ulimwengu kidogo, Unasali kidogo unafanya anasa kidogo, unakuwa mtakatifu leo kesho unaendelea na mambo mengine, unatenda mema leo, baadaye unakula rushwa, leo unakuwa wa rohoni kesho wa mwilini, hivyo hivyo leo moto kesho baridi (Yaani vuguvugu). Na kibaya kibaya zaidi kutokana na utajiri wake wa nje waliokuwa nao kanisa hili lilikuwa Laodikia, shetani akalipiga UPOFU mkubwa juu yake, likawa halijitambui tena kama linakwenda mbali na ukweli. Jaribu kutengeneza picha upo uchi, na hujitambui kama upo hivyo..Hiyo ni hatari kubwa sana.

Kwa kuwa Bwana anaona mbele alilifanya kanisa hilo kuwa unabii wa watu wa nyakati fulani itakayokuja miaka mingi huko mbele nao sio wengine zaidi ya sisi watu wa kizazi hichi tunachoishi leo ambacho kilianza tangu kipindi cha miaka ya 1906, Hivyo ndugu ni muhimu sana kufahamu kuwa tunaishi katika kanisa linalofanana na lile la Laodikia.

Kama vile mji ule ulivyokuwa tajiri kuliko miji mingine yote sita, kadhalika na dunia ya sasa tunayoishi ndio dunia iliyoendelea na iliyotajirika kuliko nyakati nyingine zote zilitangulia, kiuchumi, kiteknolojia na kielimu n.k.. Kiasi kwamba dunia leo hii ni kama kijiji, utandawazi umefikia viwango vya juu sana. Sayansi imefika hatua ya kwamba mwanadamu anaweza akaenda mwezini, mambo mengi sana yamevumbuliwa kuanzia karne ya 20, yaani kuanzia mwaka 1901 na kuendelea uvumbuzi wa mambo mengi ulitokea tukianza kueleza moja moja hatutamaliza. Mambo ambayo hayakuonekana katika karne zote zilizotangulia. Hii ni kuonyesha kwamba dunia ya sasa tunayoishi inafanana kabisa na mji ule wa LAODIKIA.

Kadhalika “haki za binadamu”, agenda za haki sawa kati ya wanawake na wanaume zilizuka katika karne hii hii ya 20, kwamba chochote mwanaume anachoweza kufanya hata mwanamke anaweza akafanya, hata mavazi mwanaume anayovaa hata mwanamke pia anaweza akayavaa, haki za watu kuoa mtu anayemtaka aidha mwanaume kwa mwanaume, au mwanamke kwa mwanamke haina shida n.k. mambo ambayo hayakuonekana katika karne zote za nyuma zilizotangulia.

Hivyo hiyo roho iliyokaa katika ulimwengu ikajiambukiza tena katika kanisa la KRISTO kama ilivyokuwa kwa wakati wa Laodikia. Kwa kuwa tunaishi katika kipindi cha mafanikio makubwa ya kielimu, kiuchumi na kiteknolojia, watakatifu wa wakati huu wakaanza kuendana pia na watu wa ulimwengu huu, na wao pia wakaanza kuiga mambo ya ulimwengu na kuyaleta katika kanisa la Mungu.

Kutokana na kwamba kuwa na utajiri wa vitu vingine vya nje, kama makanisa makubwa, vitendea kazi vya kisasa vya ibada kama vyombo vya muziki, vipaza sauti vikubwa vya kuwafikia watu wengi mambo ambayo hayakuwepo katika makanisa ya nyuma, vitu kama televisheni, radio na internet vimekuwa nyenzo rahisi za kuwafikia watu, kadhalika vyombo vya kisasa vya usafiri kama ndege, magari n.k. tofuati na hapo zamani watakatifu walikuwa wakitumia miguu, na punda kwenda kuhubiri injili, Ikawasababishia shabaha yao ihame kutoka katika mambo ya rohoni zaidi na kuhamia kwenye mambo ya mwilini. n.k. watakatifu wakaanza kujiona kwa vitu walivyonavyo Mungu anapendezwa nao,

Hivyo nguvu ile ile inayoiendesha dunia, ndio hiyo hiyo inayoiendesha kanisa, mambo yale yaliyotukuka katika dunia ndiyo yanayotukuka ndani ya kanisa la leo, Badala utakatifu utukuzwe ndani ya kanisa, inatukuzwa elimu, kwamba kipimo cha kuwa mchungaji au umekubaliwa na Mungu ni kiwango cha elimu na sio utakatifu, kadhalika utajiri wa Fedha imetukuzwa zaidi kuliko utajiri wa Rohoni, kiasi kwamba kipimo cha mtu kubarikiwa na Mungu sio kukua kiroho hapana bali kuwa na fedha nyingi..Injili inayoweza kumfaa mtu kwasasa ni injili ya mafanikio na sio injili ya toba.

Kadhalika vyeo vilivyotukuka duniani vinavyotumika kuongozea ustaarabu wa kidunia vimepewa heshima kubwa zaidi kanisani kuliko vyeo Mungu alivyovikusudia viwepo kwa uongozo wa kanisa. Kiasi kwamba ili uonekane umekubaliwa na Mungu ni lazima Uwe Raisi wa dhehebu fulani, M/kiti, Katibu/ Papa/ Mkurugenzi, Dokta, Profesa n.k. na sio Karama fulani ya rohoni kama unjilisti, uchungaji, ualimu, mitume na manabii, au karama nyingine za Roho kama miujiza,lugha, unabii uponyaji n.k. zimewekwa nyuma na hazina nafasi yoyote katika kanisa la sasa.

Dunia tunayoishi leo hii ni ya “HAKI ZA KIBINADAMU”, kadhalika na kanisa nalo limechukua hizo tabia, kwamba hata mavazi anayovaa mwanaume hata mwanamke wa kikristo anaweza kuyavaa, kwamba karama za uongozi ambazo Mungu aliziweka kwa wanaume tu, kulingana na (1Timotheo 2:12) kama vile uchungaji, ualimu na utume, hata mwanamke anaweza akazifanya; Imefikia hatua kwamba ndoa za jinsia moja zinazofungishwa na watu wa ulimwengu zinafungishwa pia Kanisani..Na bado watu hao wanajiita wakristo na kibaya zaidi shetani amewapiga upofu hawajijui kwamba wapo uchi, vipofu, maskini, na wanyonge….Ni uvuguvugu wa hali ya juu sana. Kristo ametupwa nje.

Kumbuka katika kila nyakati kulikuwa na mjumbe wa kanisa hilo ambalo Mungu alimnyanyua kutoa nuru ya wakati huo, Tuliona katika kanisa la Tano Bwana alimnyanyua Martin Luther na wengine kama wakina Calvin na Zingwli, kadhalika katika nyakati ya sita Bwana alimnyanyua John Wesley na wenzake. Vivyo hivyo na katika hili kanisa la mwisho Bwana alimnyanyua mjumbe wake WILLIAM BRANHAM na ujumbe wa kuwarudisha watu katika NENO na watoke katika hali ya uvuguvugu iliyopo sasa katikati ya madhehebu na kutoka katika mifumo ya yule mwanamke kahaba (Kanisa Katoliki) na pia Bwana alimpa ujumbe wa kutangaza kuja kwa pili kwa Kristo.

William Branham ni nani?.

William Branham alizaliwa huko Kentucky, Marekani mwaka 1909alizaliwa katika familia ya kimaskini sana, baba yake alikuwa ni mtengenezaji wa pombe, hivyo aliishi katika mazingira ya kushawishika na ulevi, alipofikisha umri wa miaka 7 anasema siku moja wakati anatoka kuteka maji kisimani alisikia sauti juu ya mti ikimwambia, “Usikae unywe pombe, wala kuvuta sigara,kwani kuna kazi ya yeye kufanya utakapokuwa mtu mzima”, aliogopa sana lakini maneno hayo aliyaweka moyoni, kwani aliogopa kuwaeleza watu maono aliyokuwa anayaona kwasababu wengi miongoni mwa wachungaji walikuwa wakimwambia hayo ni maono kutoka kwa shetani, lakini ilifika kipindi akampa Kristo maisha yake, na kukata shauri kumtumikia Mungu, ndipo Bwana akaanza kumtumia kwa namna ya kipekee, Siku moja wakati anabatiza umati mkubwa wa watu katika mto mmoja huko Marekani unaitwa Ohio, alipokuwa anambatiza mtu kama wa 17, nyota kubwa ilishuka juu yake akiwa pale mtoni, watu wote wakaishuhudia na ndipo akasikia sauti ikimwambia “Kama vile Yohana mbatizaji alivyotumwa kutangaza kuja kwa kwanza kwa Kristo, vivyo hivyo ujumbe wako utatangaza kuja kwa pili kwa Kristo”. Habari ya tukio hilo ilisambaa sana na kuchapishwa katika magezeti na vyombo vya habari vya Marekani.

Na alipofikisha umri wa miaka 37, siku moja alipokuwa anasali usiku malaika wa Bwana alimjia na miongoni mwa maneno aliyoambiwa ni; “Kama akiwa mwaminifu atakapoomba hakuna kitachoweza kusimama mbele yake hata kansa, aliambiwa pia atawaombea wafalme na ujumbe wake utafika duniani kote,” . Hivyo kuanzia huo wakati Ishara na miujiza ya kupita kawaida viliambatana naye, mambo ambayo hapo nyuma yalikuwa hayaonekani, karama za upambanuzi wa roho ziliambata naye siku zote za huduma yake, siku moja wakati anahubiri Mungu kutaka kuithibitisha huduma yake NGUZO YA MOTO ambayo ilikuwa ikimfuata tangu kuzaliwa kwake, ilitokea hadharani na kukaa juu yake, mamia ya watu waliokuwa pale waliiona, na ikapigwa picha, hiyo ilikuwa ni mwaka 1950, Picha hiyo upesi ilipelekwa kwa George J. Lacy, Mchunguzi Mweledi wa Hati Zinazoshukiwa wa F.B.I. ya Marekani, ambaye aliihakiki picha hiyo kwa maoni yake ya kitaalamu. Hati rasmi iliyotolewa na Bw. Lacy kuhakiki kuwa ile ilikuwa ni picha ya kwanza ya kimiujiza iliyothibitishwa kisayansi. Hii ilikuwa ni mapema zaidi kabla ya kompyuta na kamera za tarakimu, wala haingeweza kuelezewa kwa njia zozote zinazojulikana na sayansi, mbali na kwamba kulikuwa na Nuru halisi juu ya kichwa cha William Branham. Leo hii picha hiyo hiyo inaweza kuonekana kwenye Maktaba ya Bunge la Marekani, katika makao makuu ya taifa, Washington DC. (Tazama picha chini).

Kwahiyo historia ya maisha na huduma ya William Branham ni ndefu kidogo hatuwezi kuielezea yote hapa ila kama utahitaji utaipata mwisho wa ukurasa huu.

Hivyo ishara zote na miujiza Mungu aliyomjalia William Branham viliambata na ujumbe, Na ujumbe wenyewe ulikuwa ni Kuwarudisha watu kwenye misingi ya Neno la Mungu, Kuwarejesha watu katika Imani ya kanisa la mwanzo, na kwamba watu wa Mungu watoke katika mifumo ya dini na madhehebu ambayo Mungu ameikataa, na kujiandaa kwa kuja kwa pili kwa Kristo, Kadhalika Bwana aliwanyanyua na wengine kama ORAL ROBERT, TL OSBORN, na BILL GRANHAM na wengine baadhi. Wote hawa ni ili kuangaza nuru ya Mungu katika kanisa la mwisho tunaloishi sasa. Hivyo uamsho wa Roho ulikuwa ni mkubwa sana katikati ya karne ya ishirini, tofuati na tunavyoona sasa hivi, kuzuka kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo na waalimu wa uongo, na miujiza bandia kama tunavyoona sasa.

Sasa turudi katika kanisa hili la LAODIKIA Bwana anasema;

“15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.

Unaona hapo, kanisa tunaloishi ni vuguvugu, kwa wingi wa vitu tulivyonavyo tumejikinai, Na Bwana anasema atatupika kama tusipotubu.. Bwana anasema..

“18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.

Ujumbe huo unajieleza wenyewe kwamba ni wakati wa kurudi na kufahamu ujumbe wako wa saa wa nyakati unayoishi.. unaweza ukajiona ni moto kumbe ni baridi kwasababu umeshindwa kufahamu ni nyakati gani unaishi. na ujumbe wa wakati huu ni kurudi kwenye misingi ya NENO LA MUNGU ambayo tumeiacha ili tuwe moto na sio vuguvugu, tuache kuchanganya neno la Mungu mapokeo ya kidini, tuache kuchanganya Neno la Mungu na mambo ya ulimwengu huu kama kanisa la Laodikia lilivyokuwa (Kwani ni sawa na kufanya uasherati wa kiroho)..Leo hii unafanya ibada, kesho upo disco, jumapili unavaa vizuri, jumatatu unavaa vimini, leo unakuwa mwaminifu kesho unakula rushwa, leo unazungumza ukweli kesho unadanganya na kutukana, n.k.huko ndio kuwa vuguvugu, au KUTOKUWA MWAMINIFU na Kristo katika kanisa hili anataka kuona UAMINIFU kama yeye alivyojitambulisha hapo mwanzo kuwa YEYE NI MWAMINIFU TANGU MWANZO.

Na Bwana anamalizia kwa kusema..

“21 Yeye ashindaye, nitampa KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Unaona hapo? Kanisa hili ndilo lililopewa thawabu kubwa kuliko makanisa yote yaliyotangulia, kwamba kwa yeye atakayeshinda kwa kuwa mwaminifu kama yeye alivyokuwa atapewa nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake cha Enzi” Je! hupendi thawabu kama hiyo?..Wote tunaipenda hivyo tukizijua thawabu hizi njema Mungu alizotuandalia huko, tutaishi maisha ya kujilinda sana asije mwovu akalitwaa taji letu katika nyakati hizi za hatari.. Kumbuka pia hakutakuwa na kanisa linguine zaidi ya hili. Hatua iliyobaki ni unyakuo tu.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Huu ndio mwisho wa ujumbe Bwana alioutoa kwa yale makanisa saba. Kwa neema za Mungu tutazidi kuzitazama sura zinazoendelea. Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 4

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 3 part 2

Sehemu ya pili:

Bwana wetu YESU KRISTO atukuzwe. Karibu katika kujifunza kitabu cha Ufunuo, leo tukiendelea na ile sehemu ya pili ya sura hii ambapo tutajifunza juu ya kanisa la sita linalojulikana kama FILADELFIA. Tulishayatazama makanisa matano ya kwanza na tukaona kila moja ujumbe wake, thawabu zake pamoja na wajumbe au Malaika zake. Hivyo kama bado hujazipita ni vema ukazianza hizo kwanza kisha tuendelee kwa pamoja na kanisa hili la sita.

Tunasoma…

Ufunuo 3: 7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”.

Kama tulivyokuwa tunajifunza katika sura zilizopita kuwa ule utambulisho wa kwanza wa Bwana kabla hajatoa ujumbe unakuwa na mahusiano makubwa sana na ujumbe wenyewe wa kanisa husika..Kwamfano hapa anaanza kwa kusema ” Haya ndiyo anenayo yeye aliye MTAKATIFU, aliye wa kweli, aliye na UFUNGUO WA DAUDI, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”.

Unaona hapo anasema yeye “aliye mtakatifu” hajasema “yeye aliye na hizo Roho saba” kama alivyofanya katika kanisa lililopita la Sardi, au “yeye aliye na huo upanga mkali utokao kinywani mwake kama alivyosema katika kanisa la tatu” hapana! Bali hapa anasema “yeye aliye mtakatifu na mwenye UFUNGUO wa Daudi”. Ikiashiria kuwa “Anategemea kuona UTAKATIFU kama yeye alivyo katika hilo kanisa”..Kadhalika na ufunguo pia alionao inaamaanisha “Anakwenda kufungua au kufunga kitu fulani katika hilo kanisa”. Hivyo tutakuja kuona hizo funguo za Daudi alizonazo ni zipi?..

Kwa ufupi kanisa hili la FILADELFIA lilianza mwaka 1750WK na kuisha mwaka 1906WK. Lilidumu kwa kipindi cha miaka 156, na Mjumbe/Malaika wa kanisa hili aliitwa JOHN WESLEY. Na tafsiri ya neno Filadelfia ni “UPENDO WA NDUGU”..Hivyo hili ni kanisa lililoonyesha utofauti mkubwa na makanisa mengine yote. Baada ya ule uamsho wa Luther wa kuwahubiria watu watoke katika ule mfumo wa yule mwanamke Yezebeli (Kanisa Katoliki). Bwana alimnyanyua tena Mjumbe wake mwingine mwaminifu, John Wesley na nuru ya ziada kwamba pamoja na “kuhesabiwa haki kwa imani kwa Mungu”, mtu anapaswa aongezee juu yake “UTAKATIFU

1Petro 1: 15 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. “

Na tena inasema… Waebrania 12: 14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”

Mambo ambayo Kanisa la Sardi halikuonekana wala mjumbe wa kanisa lile Martin Luther hakulifundisha sana, yeye alitilia mkazo sana kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani”. Hivyo mjumbe wa hili kanisa la FILADELFIA John Wesley alianza kuhubiri UTAKATIFU kwa nguvu, na kwamba usafi katikati ya maisha ya waumini ni jambo la muhimu sana.

Wesley alizaliwa huko Epworth, nchini Uingereza mwaka 1703 na alipokuwa chuoni Oxford ndipo Bwana alipoanza kubadilisha maisha yake, yeye na kaka yake aliyeitwa Charles waliunda kikundi pamoja na wengine kinachosimamia itikadi ya “Kuishi maisha kama ya Kristo aliyoishi”, kuliko maisha ya kidini, walianza kwenda kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, na wafungwa, na kuwahurumia maskini, n.k na kujifanya wao wenyewe kuwa vielelezo(njia ya kufuata) hivyo wakajiundia uongozi wa kiroho wakauita “(METHOD yaani NJIA”)..na kuanzia huo wakati wakaitwa WAMETHODISTI. Baada ya hapo Wesley na wenzake Bwana aliwagusa kwa namna ya kipekee, wakaona umuhimu wa kwenda kufanya kazi ya umishionari duniani kote. Hapo ndipo injili ikaanza kupelekwa duniani kote kwa nguvu, kasi na kwa bidii hata zile sehemu ambazo zilikuwa ngumu kufikiwa kama Afrika zikafikiwa na nuru ya neno la Mungu, ndio wakati wamishionari wengi wakaanza kufika sehemu za Afrika,Asia na Marekani ya kusini.

Wesley alikuwa ni mtu aliyeimarika kiroho sana, anasema hakumbuki kama alishawahi kupunngua nguvu rohoni hata kwa robo saa tangu siku aliyozaliwa. Alisema hakuwahi kulala zaidi ya masaa 6 siku zote za huduma yake, kila siku alikuwa akiamka saa 11 alfajiri, na kwenda kuhubiri zaidi ya mara nne kwa siku, ili kwamba kwa mwaka afikishe kwa wastani wa mafundisho 800. Alikuwa akisafiri maelfu ya maili kwa farasi kwenda kuhubiri. Kwa mwaka inakadiriwa alikuwa anasafiri zaidi ya maili 4,500 kwenda kuhubiri.

Tukiendelea na mistari inayofuata…

Ufunuo 3:8 “Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu”.

Bwana anasema amewapa mlango uliofunguliwa mbele yao.? Sasa huu mlango ni upi?.

Kumbuka hapo awali BWANA alijitaja kama “yeye aliye na ufunguo wa Daudi“. Na ni kwanini aseme funguo za Daudi na asiseme funguo za Musa, au Ibrahimu?. Ni kwa nini Daudi?. Hii inatupa picha halisi kuwa upo ufunguo ambao alikuwa nao Daudi na Bwana naye akawa nao. Hivyo ni vizuri tukaufahamu huu ufunguo kwanza ni nini ili tupate msingi mzuri wa huko tunapoelekea?..

Kumbuka Baada wa Wana wa Israeli kutoka Misri na kuingia katika nchi yao ya ahadi, watu wote baada ya kuiona ile nchi ni nzuri walitawanyika na kila mtu kwenda kukaa sehemu yake, walijenga na kupanda na kufanikiwa wakamsahau Mungu, Wao walifanikiwa lakini Mungu katikati hao hakuwa na nafasi yoyote, wao walikaa kwenye makasri lakini Mungu alikaa kwenye mahema ya giza. Na iliendelea hivyo kwa kipindi kirefu cha zaidi ya mamia ya miaka, na hakukuwa na mtu yeyote kutia moyo wake ufahamu kuona kwamba kwanini sanduku la Mungu linakaa kwenye mahewa yenye giza leo huku kesho kule, Mungu mkamilifu anayetujali hapaswi kukosa sehemu ya kukaa, Ndipo Daudi siku moja akatia moyo wake ufahamu na kusema nimtengenezee Mungu wangu mahali pa kukaa, haiwezekani yeye akae kwenye jumba la kifahari wakati, Bwana Mungu wake hajamjengea nyumba, ndipo Daudi kwa bidii akaiteka ngome ya Sayuni (YERUSALEMU), Kisha akakusudia kuanzia huo wakati amjenge Mungu wake nyumba ( yaani HEKALU). Na ndipo Mungu akamwambia Daudi.

2 Samweli 7: 2 “Mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.

3 Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.

4 Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema,

5 Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, JE! WEWE UTANIJENGEA NYUMBA, NIKAE NDANI?

6 Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.

7 Mahali mwote nilimo kwenda na wana wa Israeli wote, JE! NIMESEMA NENO LOLOTE NA MTU YO YOTE WA WAAMUZI WA ISRAELI, NILIYEMWAGIZA KUWALISHA WATU WANGU ISRAELI, NIKISEMA, MBONA HAMKUNIJENGEA NYUMBA YA MIEREZI?

8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;

9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.

10 Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza;”

Unaona hapo sababu kubwa iliyomfanya hata Bwana Yesu kuitwa mwana wa Daudi, ni tabia aliyoionyesha Daudi ya kumuundia Mungu wake mji wa kukaa pamoja na Hekalu la kuweka Jina lake, katika ya makuhani, kati ya wafalme, kati ya waamuzi, kati ya manabii, ni Daudi pekee ndiye aliyeliona jambo hilo?. Na Mungu alikaa kimya makusudi aone ni nani atakayekuwa na akili ya kufanya hivyo. Na akaonekana Daudi peke yake. Na huo ndio UFUNGUO Daudi aliokuwa nao KUFUNGUA ukimya wa Mungu.

Kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo aliposema “yeye mwenye Ufunguo wa Daudi” alimaanisha na yeye pia anaunda Yerusalemu yake na Hekalu kwa Mungu wake. Isipokuwa yeye YERUSALEMU yake ni ya rohoni sio ya mwilini,na hekalu kwa Mungu wake ni la rohoni sio la mwilini. Daudi hasaa asingeweza kabisa kumwandalia Mungu mji utakayomfanya ashuke yeye mwenyewe na kukaa katikati ya watu lakini Bwana Yesu anaandaa mji utakaoleta makao ya Mungu katikati ya watu..na huu “MJI” anaoundaa ni watakatifu wake. Tukisoma…

1 Wakorintho 3: 16 ” Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, AMBALO NDILO NINYI “.

Tutakuja kuona vizuri juu ya mji mtakatifu wa Mungu (Yerusalemu mpya) ni nini, tutakapofika katika Ufunuo sura ya 21.

Hivyo alipoliambia hili kanisa la Filadelfia “Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako”, Alimaanisha kuwa ni mlango wa kuujenga mji wake pamoja naye. Hivyo wale watu walipoanza kwenda huku na huko kufanya umishionari wa kuwaleta watu wengi (Ikiwemo) wapagani kwa Kristo, ndio ulikuwa mlango uliofunguliwa mbele yao. JOHN WESLEY na mamisionari wengine waliifanya kazi hiyo duniani kote, kipindi hicho pia ndio biblia kusambazwe duniani kote, hakuna nchi ambayo haikufikiwa na nuru ya Neno.

Tukiendelea ..

“9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.

Sinagogi la shetani halikuanzia tu kwenye hili kanisa la sita, bali lilikuwepo pia katika makanisa ya nyuma, lilitajawa pia katika kanisa la pili (Ufunuo 2:9), Hili ni kanisa la uongo ambalo walikuwepo watu waliojifanya kama kanisa la kweli la Mungu na kuiga mambo yaliyokuwa yanafanywa na watakatifu lakini ndani yao walikuwa ni mbwa-mwitu wakali, wanaliharibu kundi, ni tabia ya shetani popote palipo na nuru ya kweli ya Mungu, atanyanyuka na kupanda magugu yake katikati yao. Lakini katika hili kanisa kwa kuwa walilishika Neno la subira ya Mungu kwa uaminifu wote, Mungu akayadhoofisha hayo makundi mengine ya uongo shetani aliyoyanyanyua katikati yao na kumtukuza sana bibi-arusi wake zaidi yao.

Bwana anaendelea na kusema…

“10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Unaona hapo Kanisa hili liliahidiwa pia kulindwa kutoka katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguni wote (Na hii saa ya kuharibiwa itakuwa ni kipindi cha dhiki kuu), Ikiwa na maana kuwa dhiki hii kuu ingepaswa itokee tangu wakati wa hili kanisa la Filadelfia lakini kwasababu ya Subira na uaminifu wao, Bwana akawaepusha, hivyo itatokea katika kanisa linalofuata la mwisho la Laodikia. Na kama anavyosema saa hiyo itakuwa ni ya “kuwajaribu hao wakaao juu ya nchi”, ina maana kuwa ulimwengu mzima utapitia jaribu moja zito la “aidha kupokea chapa ya mnyama uishi au kuikataa ufe” litakuwa ni jaribu kubwa sana kwa wale watakaoachwa kwenye unyakuo. Ndugu Unaona wakati tunaoishi?, ni hatari kubwa sana ipo mbele yetu kama tusipokuwa waangalifu?.

Na anazidi kusema 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Hapa anasema “naja upesi” ikiwa na maana kuwa “hakawii” biblia inasema waebrania 10: 37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, YEYE AJAYE ATAKUJA, WALA HATAKAWIA”.

Na pia anasema “shika sana ulicho nacho” ikiwa na maana kuwa, kile ulichokipokea ukiihifadhi, kwa kuwa “mtakatifu” na kujiepusha na “mafundisho yadanganyayo” asije “MTU”, akatwa taji yako, kumbuka ni “mtu” na sio “malaika” ikifunua kuwa mataji tunapewa hapa hapa duniani, mbinguni tukifika ni kuvikwa tu. Na tukiwa hapa duniani kuna mtu anaweza akatwaa mataji yetu, SASA huyu “MTU” atafutaye kutwaa mataji yetu (au THAWABU) zetu ni nani??

2 Wathesalonike 2: 3 ” MTU awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule “MTU WA KUASI”, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? “

Unaona hapo huyu MTU anayezungumziwa hapo ni mpakwa mafuta wa shetani (yaani MPINGA-KRISTO ndani ya cheo cha UPAPA), na mifumo yake yote,na mitume wote wa uongo wajigeuzao kuwa mitume wa Kristo, ambao kwa kipindi hichi cha siku za mwisho wamezagaa kila mahali, wasiofundisha toba na msamaha wa dhambi wala wasiofundisha ujio wa Bwana bali mungu wao ni tumbo..Mtume aliwataja katika…

Wafilipi 3: 17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO;

19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI.

20 Kwa maana sisi, WENYEJI WETU UKO MBINGUNI; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

Na mwisho kabisa Bwana anamalizia kwa kusema…..

” 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa NGUZO katika HEKALU LA MUNGU WANGU, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “

Bwana aliwaahidia watu wa kanisa hili la Filadelfia, wale ambao waliokuwa watakatifu, na kujiepusha na mafundisho ya uongo na kujitoa kwa bidii yote kupeleka injili huku na kule duniani kote, na kuusimamisha mji wa Bwana Yerusalemu yake ya rohoni, na hekalu ndani yake, kama Daudi alivyoadhimia kumjengea Bwana nyumba, hata BWANA kuuchagua Yerusalemu kuwa makao yake makuu, na mji wake mtakatifu, kadhalika hawa wa Filadelfia Bwana aliwaahidia kuwafanya kama nguzo, katika ule mji uliotukuka Yerusalemu mpya ambao tutakuja kuuona habari zake katika sura ile ya 21..

Tukiyajua hayo, ni wakati wa kuzifanya taa zetu ziwe zinawaka, kwa kumuamini, Bwana Yesu Kristo, na kutubu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa na kwa JINA LA YESU na kupokea Roho Mtakatifu, na kuishi maisha yanayolingana na wokovu,(yaani maisha matakatifu), na zaidi ya yote kuipeleka habari njema kwa watu wote ulimwenguni kote, na kujihadhari “mtu” asije akayatwaa mataji yetu.

Ubarikiwe na Bwana Yesu, aliyetoa maisha yake kuwa dhabihu hai, kwa Mungu kwa ajili yetu.

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 3 Part 3

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

MPINGA-KRISTO


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 3 part 1

Sehemu ya kwanza.

Bwana na mwokozi wetu YESU KRISTO atukuzwe daima. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tukiliangalia lile kanisa la TANO kati ya yale makanisa SABA, na Ujumbe aliopewa Mtume Yohana ayapelekee. Kanisa hili linaitwa SARDI. Tunasoma.

Ufunuo 3:1 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa”.

Kumbuka hapa Bwana anajitambulisha kama “yeye mwenye hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba”. Katika kanisa hili hakujitambulisha kama “yeye mwenye macho kama mwali wa moto au yeye mwenye huo upanga mkali utokao kinywani mwake n.k.” bali alijitambulisha kama yeye mwenye hizo Roho saba, akifunua asili yake ya ndani, Sasa Hizi Roho saba, sio kwamba Mungu anazo Roho 7 na kila moja inajitegemea kivyake hapana, bali ni Roho ile ile moja isipokuwa inatenda kazi katika nyakati tofauti tofauti saba. Mfano tuna siku 7 katika juma, na kila siku tunaona jua likichomoza na kuzama, sasa hatuwezi tukasema kwa wiki tuna ma-jua 7, hapana tunafahamu kuwa jua ni lile lile moja isipokuwa limetenda kazi katika siku saba tofauti, na ndivyo ilivyo kwa Roho wa Mungu. Kwanza ni vizuri kufahamu Mungu ni Roho, na ni mmoja, na Roho yake ni moja, kadhalika na nafsi yake ni moja. Kwahiyo hapo ni ile ile Roho moja ikitenda kazi katika nyakati tofauti tofauti saba za Kanisa.

Kwahiyo kwanini Bwana alijitambulisha kama yeye mwenye Roho 7, ni kwasababu “Roho ndiyo inayotia uzima”. Na ndio iliyokuwa inatia UZIMA kwa makanisa yote 7 kuanzia la kwanza mpaka la mwisho. Ikiwa na maana kuwa kanisa hilo la SMIRNA lilihusiana na kupungukiwa na Roho wa Mungu. Hivyo kama tunavyofahamu mtu akikosa Roho wa Mungu ni sawa na kakosa uzima,na Kinachobakia ni kifo. Wakati fulani Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika

Yohana 6: 63 “ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA”.

Unaona hapo anasema ni Roho tena ni uzima. Hivyo kanisa hili limehusiana na kuacha maneno ya Bwana ambayo ndio Roho yenyewe itiayo uzima kwao. Na ndio maana Bwana anasema anayajua matendo yao ya kwamba “wana jina lililohai lakini WAMEKUFA”.

Tulichunguze kidogo hili kanisa la SARDI; Tafsiri ya neno SARDI ni “WALE WALIOTOROKA”..Na kanisa hili lilianza mwaka 1520WK na kuisha mwaka 1750WK, Kanisa hili halikudumu kwa muda mrefu sana kama Kanisa lililopita la Thiatira ambalo lenyewe lilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka 900. Kipindi hichi cha kanisa hili kinajulikana maarufu kama “wakati wa matengenezo ya kanisa”, Ni wakati ambao lile giza ambalo lilikuwa limetanda duniani kutoka katika nyakati za kanisa la nne lilianza kumezwa na Nuru ya kweli ya Mungu kidogo kidogo baada ya kanisa kuharibiwa kwa muda mrefu na mafundisho ya dini ya uongo (Katoliki).

Hivyo Mungu akaanza kunyanyua watumishi wake waaminifu ambao waliyashika yale maneno ya Bwana aliyosema katika lile kanisa la Nne lililotangulia kwamba “wanamridhia yule mwanamke YEZEBELI”. Hivyo hawa baada ya kuzijua fumbo za shetani na kwamba makao yake makuu yapo katika dini ya uongo inayofanana sana na ukristo (Katoliki), hawakumridhia kama watu wa kanisa la nne walivyofanya.. Hivyo wakaanza kunyanyuka na kwenda kinyume na kuyapinga mafundisho yake kwa kuhubiri UKWELI WA NENO kwa watu wote pasipo kumwogopa. Ndipo tunakuja kuona Mungu akamnyanyua mtu kama “MARTIN LUTHER”, Ambaye yeye ndiye aliyekuwa mjumbe/Malaika wa kanisa hilo (SARDI), na wengine pia kama wakina Calvin, Zwingli, na wengineo..Wote hawa kwa pamoja hawakumridhia yule mwanamke YEZEBELI. Na kama vile tafsiri ya jina la Kanisa hili lilivyo (Sardi=wale waliotoroka), hivyo hawa wakristo wa nyakati hii walifanikiwa kutoroka kwa sehemu kutoka kwa yule mwanamke Yezebeli.

Tunaona Martin Luther ambaye mwanzoni alikuwa ni kasisi wa kikatoliki, baada ya kuona njia ya kanisa Katoliki haiendani na kweli ya Mungu, aligeuka na kuyapinga mafundisho ya kanisa hilo, siku moja katika safari yake ya kuutafuta ukweli, alisikia sauti ikimwambia..“Mwenye haki ataishi kwa Imani” (Warumi 1:17). Hivyo baada ya kupokea ufunuo huo akaanza kuyakataa mafundisho yote ya “wanikolai” ya “Balaamu” na ya “Yezebeli” kwamba mtu hatapitia kwa kuhani fulani au Padre fulani au Papa ili amfikie Mungu, Bali kwa IMANI kwa Mungu kila mtu atamfikia yeye na kumpendeza..kwamba mtu anasamehewa dhambi zake kwa IMANI kwa Mungu, na sio kwa kupitia mwanadamu yoyote, kadhalika na uponyaji na mahitaji na mambo mengine yote…

Hivyo kuanzia huo wakati Martin Luther alizidi kupinga kwa Nguvu mifumo ya kanisa Katoliki siku moja aliandika HAYA 95 zinazopinga mfumo wa kipapa na kuzigongelea kwenye mlango wa ngome ya kanisa kubwa la kiKatoliki lililokuwepo huko wittenberg Ujerumani mwaka 1517. Na ndipo uprotestant ulipoanzia ikasababisha uamsho mkubwa wa roho, watu wengi wakaanza kutoka kwenye hiyo dini ya uongo kwa kupitia injili za hawa wana matengenezo.

Biblia zikaanza kutafsiriwa jambo ambalo hapo kwanza zilikuwa zinasomwa tu na makuhani wa kikatoliki, Hivyo ndivyo nuru ya kweli ilivyoanza kurejeshwa kidogo kidogo.

Lakini ilifikia wakati miaka kadhaa baada ya wale wajumbe kuondoka, watu wakaanza kujisahau, na kuanza kujiundia dini badala ya kuuendeleza uamsho wa Kweli ya Mungu, badala ya kuendelea kujitakasa kutoka katika yale mafundisho ya uongo zaidi na zaidi wakajiundia ngome, nao pia wakaanza kujiita Walutheran, wacalvism, wabrownist, wamennonite n.k. watu wakaanza kujivunia wanadamu na dini, badala ya kujivunia Kristo hivyo ikawafanya wasahau kabisa ule msingi wa uprotestant ambao haukuwa na lengo la kuanzisha dini nyingine bali ulikuwa na lengo la kuwatoa katika uongo wa yule mwanamke Yezebeli (Katoliki) na kuwarejesha watu kwenye NENO LA MUNGU.

Jambo ambalo Mtume Paulo alilikemea pia kwa nguvu katika…

1wakorintho 1: 11 “Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.

12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.

13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? “

Hivyo mbele za Mungu hawa watu wa Sardi ambao mwanzoni walianza vizuri kwa nje walionekana kama wapo hai, lakini kwa ndani walikuwa WAMEKUFA kwasababu Roho ya uhai, na UZIMA haikuwa tena ndani yao, ya kuwafanya waweze kuuendeleza ule UAMSHO walioanzana nao hapo mwanzo.

Tukiendelea kusoma tunaona…

“2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”.

Unaona hapo waliambiwa wakeshe, na wayaimarishe mambo yaliyoyasalia, (yaani kumalizia kuondoa mafundisho yote ya Yezebeli ndani ya Kanisa), na kwamba wasipofanya hivyo (yaani kukesha) atakuja kwao kama mwivi na wala hawatajua hiyo saa atakayokuja.

Swali ni saa gani hiyo anayoizungumzia atalijilia hilo kanisa? Angali wakati wa hilo kanisa ulishapita na unyakuo haujatokea?

Ni muhimu kufahamu kwamba kila kanisa Bwana alikuwa na wakati wake wa kulijilia kanisa hilo, na kujiliwa huko kulikuwa ni UAMSHO fulani wa kipekee ambao ni mahususi kwa kuwavusha watu katika hatua nyingine ya kiimani inayofuata na huo Uamsho huwa unakuja karibu na mwishoni kabisa mwa nyakati wa kanisa husika..Hivyo kwa kanisa la kwanza baada ya kuacha upendo wao wa Kwanza Bwana aliwajilia kwa kupitia uamsho wa Irenio mjumbe wa kanisa la pili hivyo kwa ile jamii iliyoweza kumtii Kristo kwa ujumbe wa wakati waliokuwa nao(Wa mtume Paulo) waliweza kuchukuliana na ujumbe wa nyakati iliyofuata..Hivyo kwao Bwana anakuwa amewajilia lakini sio kama mwivi kwasababu Roho wa Mungu hajazimishwa ndani yao, lakini wale waliokataa, kwao inakuwa kama mwivi ndio unakuta watu wanaishia kuupinga ule ujumbe wa kuwaua, Na kuishia kuchukuliwa na mafundisho ya shetani.

Kadhalika na kwa nyakati ya pili, kujiliwa kwao kulikuwa ni mwishoni kabisa mwa nyakati, jamii ya watu waliodumu na mafundisho ya Irenio (Mjumbe wa kanisa la pili) waliweza kuchukuliana na uamsho wa mjumbe anayefuata..Vivyo hivyo na kwa kwani la nne, la tano.

Sasa katika hili la tano saa ya kujiliwa kwao ilikuwa ni wakati wa uamsho wa kanisa lililofuata ambalo Bwana alimtumia Mjumbe wa Kanisa lile JOHN WESLEY kuja na ujumbe wa UTAKASO KWA DAMU YA YESU, na utakatifu Hivyo kwa wale wachache ambao waliruhusu Roho wa Mungu awatoe kutoka hatua moja hadi nyingine ya IMANI, na kukaa mbali na mifumo ya yule kahaba Yezebeli walipewa neema ya kuuamini na kuupokea ujumbe wa John Wesley na huko ndiko kulikokuwa kujiliwa kwao. Lakini wale wengine waliokuwa wanaonekana wapo hai lakini wamekufa kwa kujiundia “majina” na kutengeneza madhehebu, Bwana alipokuja na uamsho wa Roho wa Wesley hawakujua chochote Sasa hiyo ndiyo kujiliwa kama mwivi, walibaki na dini zao na madhehebu yao.wakawa hawataki kufahamu jambo lingine la ziada ya ulutheri, ucalvinism, umennonite n.k. wakati lile kundi dogo ambalo lilikuwa tayari kwenda na Roho wa Mungu lilipokea uvuvio mpya wa Roho. Kwamba kuhesabiwa haki kwa Imani peke yake hakutoshi bali pia na Utakatifu ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokua nao (Waebrania 12:14)

Kadhalika na kwa kanisa la sita Filadelfia vile vile Bwana alilijia na wale waliokuwa wanadumu katika mafundisho ya mjumbe wa kanisa la sita John Wesley ilipofika wakati kujiliwa waliweza kupewa neema ya kuonja Uamsho uliofuata lakini wale ambao waliridhika na kuchukulia ujumbe wa Wesley kama dini, walibakia katika madhehebu yao wakajifungia katika Umethodisti na wakati wa Pentekoste ya Bwana ulipokuja mwaka 1906 huko Asuza Marekani, hawakujua chochote, wengine waliishia kupinga na kusema hicho kitu ni cha shetani na wengine hawakuelewa ni kitu gani.. Kwamba kuhesabiwa haki kwa imani pamoja na utakaso havitoshi bali pia Ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wa mambo yote. (Waefeso 4:30) kwamba huo ndio muhuri wa Mungu.

Vivyo hivyo na kwa kanisa la mwisho tunaloishi linaloitwa Laodikia, wale wote watakaoupokea ujumbe wa mjumbe wa kanisa hili WILLIAM BRANHAM wakidumu katika kujitenga na mafundisho ya yule kahaba mkuu YEZEBELI na kuruhusu Roho ya Mungu ya uhai ifanye kazi ndani yao, Na kukua kutoka hatua moja kwenda nyingine kila siku, Sasa hawa Bwana atakapokuja watajua kwasababu Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yao, na taa zao zinawaka, lakini wale wengine hawatajua chochote, wataishia aidha kupinga, au kutokuelewa juu ya huo uamsho wa mwisho unaokuja. na kwa vile hakuna nyakati nyingine zaidi ya saba..Umsho huo utakuwa ni kwa ajili ya unyakuo wa kanisa. Na zile ngurumo 7 kwenye ufunuo 10 (zilizobeba siri ambazo hazijaandikwa mahali popote ), hizo ndizo zitakazoleta uamsho wa mwisho zitakazomvusha bibi-arusi wa Kristo kutoka katika nyakati ya saba, na kuingia katika umilele. Na ndio maana Bwana alisema…

Marko 13: 33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.

34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.

35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;

36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.

37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”.

Na utaona maneno haya haya aliliambia hili kanisa la SARDI…

Ufunuo 3: 3 “Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”. …

Lakini pamoja na hayo walikuwepo wachache katika kanisa hilo, walioweza kuenenda kwa uongozo wa Roho na kujitenga na yule mnyama hao ndio Bwana aliowaambia wataenda naye katika uvuvio wa Roho utakaokuja wa John Wesley.

“4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Anasema yeye ashindaye jina lake halitafutwa katika kitabu cha uzima, na zaidi ya yote yale mavazi meupe yanawakilisha usafi wa hali ya juu, ‘heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu (Mathayo 5:8) inasema hivyo”..Hivyo kundi hili katika umilele unaokuja watakuwa na nafasi ya karibu sana na Mungu kuliko watu wengine.

Hivyo ndugu Ujumbe huo pia unatuhusu hata sisi watu wa kizazi hichi tunachoishi, wa kanisa hili la mwisho la laodikia. Je! unakesha? na taa yako inawaka? je! Roho wa Mungu bado yupo hai ndani yako?. au una jina lililo hai lakini ndani yako umekufa?..Kumbuka huu ni wakati wa jioni, ondoka katika madhehebu na vifungo vya dini kama umeupokea ujumbe wa wakati wako halafu unaugeuza kuwa kama dini au dhehebu huu ni wakati wa kugeuka. Hivi karibuni Bwana ataenda kuachilia uvuvio wa mwisho nao utakuwa ni wa kipindi kifupi sana, utakaompa bibi arusi imani ya kwenda kwenye unyakuo.

Luka 12: 35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara”.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali share ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 3 Part 2

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

YEZEBELI NI NANI?

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA

NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?


Rudi Nyumbani.

Print this post