JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu maana ya hili neno UBATIZO.Hili ni neno la kiyunani lijulikanalo kama (BAPTIZO), lenye maana ya”KUZAMISHWA”. Kwahiyo kama tafsiri ya jina lake ilivyo, mtu anapobatizwa ni lazima azamishwe mwili wake wote katika maji, Na kumbuka haisemi ni katika mto, bahari, ziwa, au kisima, n.k. La! Maagizo yametolewa ni kuzamishwa.
Kwahiyo Hakuna tatizo lolote mtu kubatizwa/kuzamishwa kisimani, ili mradi tu, maji yawe mengi ya kuweza kumzamisha mwili wote, hivyo iwe kwenye mto, kisima, chemchemu, pipa au baharini au kwenye dimbwi, popote pale la muhimu ni azamishwe mwili wote uzame usionekane na abatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Ubatizo mwingine wowote tofauti na huo ni Batili. Hivyo Mtu huyo anapaswa akabatizwe tena.Kumbuka Nyakati za mtume Paulo kulikuwa na watu waliokuwa wanaujua ubatizo tu wa Yohana wa Toba, hawakuufahamu ubatizo uletao ondoleo la dhambi, Lakini Paulo alipowahubiria na kuamini wakabatizwa tena kwa ubatizo sahihi soma..
Matendo 19: 1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”
Matendo 19: 1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
5 Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”
Na wewe pia unaweza ukawa umebatizwa kwa ubatizo usio sahihi, hivyo usione aibu kwenda kubatizwa tena, ili kufanya imara wito wako na uteule wako. Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna ubatizo wa kunyinyuziwa kulingana na maandiko…Na ubatizo sahihi ni muhimu mno haupaswi kuupuziwa kwa namna yoyote ile. Kadhalika hakuna chuo chochote cha kupitia ndipo ukabatizwe, pale mtu tu anapoamini na kutubu kabisa kwa kumaanisha kuziacha dhambi zake moja kwa moja anapaswa aende akabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake na kupokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Ukipata muda pia pitia mistari hii ,( Matendo 8:16, 10:48).
Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana:
MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?
NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?
MKUU WA GIZA.
UPONYAJI WA YESU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
JIBU: Kulingana na biblia zinaonekana Hukumu kuu Nne za Mungu mwenyezi zitakazokuja mbeleni.. HUKUMU YA KWANZA:..Ni hukumu ya watakatifu watakaonyakuliwa kwenda mbinguni, hukumu hii siyo ya kulaumiwa wala ya adhabu, bali ni ya thawabu, kila mtakatifu atalipwa kulingana na taabu na Uaminifu wake aliokuwa nao katika kuifanya kazi ya injili akiwa hapa duniani,
2 wakorintho 5:9-10 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.”
Pia tukisoma warumi 14:12 biblia inasema; “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.”
Tunajua nyaraka hizi mbili Paulo hakuziandika kwa watu wasioamini bali kwa wakristo kwahiyo hukumu hizi zinazozungumziwa hapa zinawahusu watakatifu tu ndipo taji la kila mtu litang’aa kulingana na kazi yake alipokuwa duniani. HUKUMU YA PILI: Hii itakuja baada ya ile siku kuu ya kutisha Bwana kupita, baada ya ile dhiki kuu, itawahusisha wale wakristo walioachwa katika unyakuo, ambao walikataa kuipokea ile chapa ya mnyama, na kuuliwa na mpinga kristo, sasa hawa nao watakufufuliwa tena, kulingana na..
Ufunuo 20: 4 “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu”.
Ufunuo 20: 4 “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu”.
Hivyo wote watakaoikata chapa ya mnyama watafufuliwa na kuhukumiwa na wale watakatifu watakaokuja na Bwana siku ile, kisha baada ya kuhukumiwa nao pia watapewa neema ya kuingia katika ule utawala wa Amani wa Bwana Yesu Kristo wa miaka 1000.
Japo hawatakuwa daraja moja na wale watakatifu wa Mungu waliokuja na Bwana. HUKUMU YA TATU; hukumu hii pia itakakuwepo katikakati hapo, kati ya siku ile Bwana atakapokuja, na kabla ya utawala wa miaka 1000 kuanza, hii itakuwa kwa watu wote waliowafanyia fadhila watakatifu wa Mungu walipokuwa duniani,pamoja na wayahudi katika kile kipindi cha dhiki kuu, ndipo Kristo atakapowatenganisha kondoo na mbuzi…..
Tunasoma.
Mathayo 25: 31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mathayo 25: 31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Kwahiyo hawa nao(Kondoo), watapewa neema ya kuingia katika utawala wa miaka 1000, Bali mbuzi (waovu), Watakwenda katika lile ziwa la moto.HUKUMU YA NNE:..Hii itakuwa baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha pale Kristo atakapokaa katika kiti chake cha enzi cheupe kuwahukumu mataifa ukisoma
Ufunuo 20:11“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”
Ufunuo 20:11“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”
Hii itakuwa ni hukumu ya mataifa kwa wale wengine wote waliobakia na wale waliozaliwa ndani ya ule utawala wa miaka 1000 na wale ambao hawakuwa katika ule ufufuo wa kwanza, Na wale wote walioipokea ile chapa ya mnyama watahukumiwa wote kulingana na matendo yao na baada ya hapo wataingia katika lile ziwa la moto wale wote ambao majina yao hayakuonekana katika kitabu cha UZIMA. huko kutakuwako na kilio na kusaga meno. Kisha mbingu mpya na nchi mpya zitafuata, ambapo huko dhambi, wala hukumu havitakuwepo tena, wala mateso, wala uchungu, wala shetani, wala waovu, wala shida, wala magonjwa. Mambo ya kwanza yatakuwa yamepita Bwana atayafanya yote kuwa mapya katika ile Yerusalemu mpya itakayokuja.Na tutakuwa huko milele na milele na BWANA. Amina.
Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?
JE NI KWELI TUTAWAHUKUMU MALAIKA? SAWASAWA NA 1WAKORINTHO 6:2
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
KITABU CHA UZIMA
KITABU CHA UKUMBUSHO
JIBU: Tunakosa maarifa tukidhani kuwa tunapowaombea watu maombi ya kufunguliwa kwa mfano kutoa Pepo.Ni kwamba tunawatoa kweli wale Pepo na hapo hapo mtu yule anakuwa ameshafunguliwa, Hapana ukweli ni kwamba hatutoi pepo moja kwa moja bali tunakuwa TUNAWAFUKUZA PEPO KWA MUDA TU wanakwenda mahali watakapokaa pale kwa kipindi fulani cha muda. Na baadaye wakisha tulia kwa muda,wana tabia ya kurudi kuangalia maskani zao za kwanza zikoje, Kwasababu kama ingekuwa ndio hivyo kirahisi rahisi tu Bwana asingesema tena maneno haya;
Mathayo 12: 43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. 44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”
Mathayo 12: 43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.
44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.
45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”
Unaona? Watu wengi wanaosumbuliwa na vifungo vya shetani au mapepo, kwa kudhani kuwa mtumishi yule anapomwombea na pepo kulipuka ndio kafunguka moja kwa moja, hapana hiyo ni hatua ya kwanza ya yule pepo kukuacha, ila bado yupo na wewe, bado ana hati zote za kukumiliki wewe.
Hivyo kwa wakati ule mfupi baada ya kuombewa kwa Imani huyo Pepo ataondoka, na baada ya hapo utaanza kuona unafuu mkubwa katika maisha yako kwa kipindi kifupi tu cha wakati. Lakini yule pepo aliyefukuzwa hawezi kuiachia milki yake kirahisi hivyo anachofanya, ni kurudi kuona je! yule mtu analo badiliko lolote katika maisha yake?. Na kama asipoona ndio anakwenda kuchukua mapepo mengine saba maovu kuliko yeye (anafanya hivyo ili kwamba siku nyingine asisumbuliwe kutolewa kirahisi), na ndio unakuta yule mtu yale matatizo aliokuwa nayo kwanza yanarudi na kuzidi kuwa mengi, hali yake ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
Zipo shuhuda nyingi ndio utasikia mtu anasema nilikwenda kuombewa na mtumishi fulani, nikapona ugonjwa uliokuwa unanisumbua pale pale lakini baada ya mwezi ile hali imenirudia tena, na safari hii ndio imekuwa mbaya zaidi kuliko hata ya mwanzo..Sasa wengi wa watu kama hawa hawajajua au hawajafundishwa utendaji kazi wa hizi roho ovu.
Kumbuka KUFUNGULIWA kwa mtu, kunaanzana na yeye mwenyewe, ikiwa mtu hataki kufunguliwa basi hata aombeweje hawezi kufunguka. Kadhalika watu hawajui kuwa vipo vifungo/mapepo mengine ambayo hayajidhihirishi kwa nje(yaani hayalipuki) kama mapepo mengine yanavyofanya. yamekaa ndani tu,na mengine yanakuja ndani ya mtu na kuondoka, hivyo haya yote huwezi kuyatambua kwa kutegemea kusubiria uombewe. Ni lazima ufahamu mtu yoyote ambaye hajazaliwa mara ya pili (yaani kwa kumwamini YESU KRISTO na kubatizwa katika ubatizo sahihi) kwa namna moja au nyingine kuna roho au vifungo vya uovu vinaambatana naye hatakama yeye anajiona yupo sawa.
Hivyo basi pepo linapofukuzwa ndani ya mtu, ni wakati wa mtu yule haraka sana kuchukua hatua ya kumkabidhi Bwana maisha yake yote kwa kumaanisha kuacha maisha ya dhambi na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo atakuwa ameondoa hati miliki zote za pepo lile kurudi, na sio tu mapepo yale yanayojidhihirisha bali hata na yale yasiyojidhihirisha yanakuwa hayana nafasi ya kurudi na hivyo mtu yule anakuwa UMESHAFUNGUKA KIKABISA KABISA. Na ndio maana Bwana alipokwisha kuwafungua watu aliwaambia wasitende dhambi tena, maana ya kutokutenda dhambi ni kumwamini yeye (Bwana Yesu, kwa kutubu na kuzaliwa mara ya pili). Hivyo deliverance ambayo itaweza kumfungua mtu MOJA KWA MOJA ni kuzaliwa mara ya pili, na sio kuombewa tu na pepo kulipuka halafu basi.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
FAIDA ZA MAOMBI.
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:
1Wakorintho 3:10-15 Inasema.. 10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. 11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. 15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto. 16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”
1Wakorintho 3:10-15 Inasema..
10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.
13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”
JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa wanaozungumziwa hapo ni watenda kazi (yaani watu wote wanaojiita watumishi wa Mungu), na kila mtu anapofanya kazi ya kuhubiri na kuwavuta watu kwa Kristo ni sawa na kama anajenga nyumba yake mwenyewe ya mbinguni. Kwahiyo wale watu anaowazaa kwa injili yake hiyo ndio kazi yake na ndio itakayojaribiwa kwa moto. Sasa moto ni nini, na unaijaribuje kazi ya mtu?.
Moto ni majaribu ya imani, misukosuko, adha, dhiki, au mateso shetani atakayoyaleta juu ya watu wako uliowazaa katika kazi ya kuhubiri injili.
Kwahiyo kama wale watoto wako uliowaowazaa uliwakuza katika mafundisho madhaifu wasiyowafanya wawe imara, itakapokuja dhiki, au misukosuko,au majaribu, watashindwa kusimama na mwisho wa siku wataanguka na kuteketea na kupotea kabisa. Hivyo katika siku ile Kazi yake mtu huyo itaonekana kama ni ya hasara kwasababu watu aliowazaa wote wameteketea na moto(majaribu misukosuko n.k.), Kwa mfano unakuta muhubiri injili yake siku zote imejikita katika mafanikio ya kimwilini tu,haweki mambo katika usawa hafundishi watoto wake kumjua Mungu zaidi na utakatifu na uweza wa Mungu na iMANI,na Upendo wa Mungu au mambo yahusuyo ufalme wa mbinguni, yeye mafundisho yake ni mafanikio tu ya kimwilini basi na mtumishi huyo utakuta yupo na maelfu ya wafuasi anawalea chini yake,
Sasa kipindi kitakapofika shetani naye atataka kuwajaribu wale watoto aliowazaa,..atawaletea aidha mtikisiko wa kiuchumi kidogo tu, au magonjwa, au vifungo, au wakati mwingine mafanikio makubwa kupita kiasi ili apunguze muda wake na Mungu ajikite katika mambo ya kidunia n.k. sasa kwasababu wale watoto hawakufundishwa uvumilivu, saburi na Imani, kiasi n.k.. haraka sana wataiacha ile Imani na kurudi nyuma. Na ndio hao wanafananishwa na zile mbegu zilizodondokea nyingine njiani, ndege wakapita wakazila, nyingine kwenye miamba zikakosa mizizi na kufa(Hawa ndio wale wakati wa kujaribiwa wanajitenga na Imani), wengine kwenye miiba(shughuli na udanganyifu wa mali vinawasonga, wanakuwa hawazai chochote) n.k.. Kwa namna hiyo basi safari yao ya Imani wanajikuta imeishia ukingoni.
Hivyo kazi ya yule muhubiri mwisho wa siku yote aliyojisumbukia yanakuwa ni hasara tupu kwasababu hakuijenga nyumba yake(kondoo wake) katika ubora unaotakiwa… Kadhalika biblia inaposema yeye naye ataokoka lakini kana kwamba kwa moto, inamaanisha pia na yeye atapitia majaribu yale yale, na kama akiweza kuyastahimili yeye ataokoka lakini kazi yake itakuwa ni ya hasara, atakuwa kama mtu tu ambaye hajawahi kumtumikia Mungu kwa namna yoyote ile.
Kwahiyo habari hiyo inatufundisha kuwa tufanye kazi ya Mungu kwa malengo, tukijua ya kuwa kazi zetu zitaenda kupimwa siku ile. Itatufaidia nini tupate maelfu wa washirika katika makusanyiko yetu kwasababu tu tunawahubiria injili laini, na siku ile tunakwenda kuonekana hatufanya chochote?. Ni heri awepo mmoja lakini chombo cha thamani chenye kumfaa Mungu kilichojengwa kwa dhahabu.kuliko kuwa na mabunda ya nyasi.
Hivyo Tusihubiri tu ilimradi kuwaburudisha washirika ili washirika waendelee kukaa katika makusanyiko yetu, hapana bali tuwajenge wawe kama mawe ya thamani ambayo moto utakapokuja kuyajaribu ndio yanazidi kuwa imara badala ya kuwa dhaifu.
UBATIZO WA MOTO
JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?
ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.
UPUMBAVU WA MUNGU.
IMANI NI KAMA MOTO.
JIBU: Biblia haijatoa masharti yoyote ya kufuata katika kufunga kwamba ufunge masaa 12 au 26 au 36 au mwezi,nk.. hapana. Kwasababu kitendo chenyewe cha kufunga ni kitendo kinachotoka rohoni na sio mwilini. Hivyo kwa jinsi mtu atakavyoguswa moyoni au atakapoona yeye mwenyewe umuhimu wa kufunga kwa muda fulani, pengine kutokana na ugumu wa hali fulani anayopitia kiroho ama haja fulani anataka kupeleka kwa Mungu, ndipo anapolazimika kujichagulia mwenyewe aina ya ufungaji wake utakaoendana na haja zake, (isipokuwa labda awe ameagizwa na Mungu mwenyewe aina ya mfungo anaopaswa afunge). Mfano tunaweza tukamwona mtu kama Danieli ukisoma katika
Danieli 10: 1 “Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danielii, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo. 2 Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. 3 SIKULA CHAKULA KITAMU, WALA NYAMA WALA DIVAI HAIKUINGIA KINYWANI MWANGU,WALA SIKUJIPAKA MAFUTA KABISA, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.
Danieli 10: 1 “Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danielii, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
2 Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.
3 SIKULA CHAKULA KITAMU, WALA NYAMA WALA DIVAI HAIKUINGIA KINYWANI MWANGU,WALA SIKUJIPAKA MAFUTA KABISA, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.
Hivyo kulingana na habari hiyo Danieli kwa kuona vita kubwa mbele yake na kutaka kufahamu mambo gani yatakayokuja kutokea huko mbeleni, ikamlazimu afunge wiki tatu, pasipo kula chakula kitamu wala kujipaka mafuta, Kadhalika na Musa, kwa kuwa alifahamu anakwenda kukutana na uso wa Mungu na kupokea amri za Mungu kule mlimani ilimlazimu afunge siku 40 usiku na mchana bila kula chochote, Pia wakati wa Esta wayahudi walipoona wanapitia hatari ya kuuawa walifunga siku tatu usiku na mchana bila kula chochote, kadhalika na wengine mfano Nehemia, Daudi, Mitume Pamoja na Bwana wetu YESU KRISTO hata yeye wakati wa kwenda kujaribiwa na shetani nyikani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote. n.k.
Hivyo unaona hapo inategemea na sababu ya mtu kuingia katika mfungo huo, ndio kinachopelekea aina ya kujinyima nafsi. wapo watu wengine wanafunga saa 24 au zaidi kwa kunywa maji tu pasipo chakula na wanaweza kwenda hivyo kwa siku tatu au zaidi,.Wapo wengine wanaweza kufunga pasipo kula chakula wala maji kwa siku kadhaa, wapo wengine wanafunga kwa kutokula chakula walichokizoea, mfano walikuwa wanakula nyama mara mbili kwa siku, wanaamua kujinyima kwa kutokula chakula kitamu kama nyama kwa muda wa labda mwezi mmoja hivi au zaidi wanakuwa wanakula tu pengine maji na mkate basi.n.k. Vyovyote vile nawe ukiamua kufunga kwa kutokunywa maji saa 24, au kwa kunywa maji tu katika ufungaji wako wote, ni uamuzi wako, lakini kumbuka kwa jinsi unavyojinyima zaidi ndivyo unavyoongeza nguvu zako za kiroho, Biblia inaonyesha wengi walikuwa wanafunga pasipo kula wala kunywa kwa kiwango cha chini ni saa 12 (yaani jua linapochomoza mpaka linapozama). Hivyo kufunga kokote kule utapata thawabu kama kama ukizingatia yale Bwana aliyosema katika Mathayo 6:16.
Hivyo unapofunga kumbuka kuzingatia pia viwango vya rohoni kama usafi, utakatifu,(kwa kujitenga na dhambi) n.k. vinginevyo mfungo wako utakuwa ni sawa na bure kama wapagani wanavyofanya, Kwa kulijua hilo zaidi soma mistari ifuatayo. Bwana akiwaambiwa watu wake;
Isaya 58:3 ” Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. 4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu, 5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana? 6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? 8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. 9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. 11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. 12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia. 13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; 14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.
Isaya 58:3 ” Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu,
5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;
14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
BWANA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI KUSEMA MARKO 2:19″WALIOALIKWA HARUSINI WAWEZAJE KUFUNGA MAADAMU BWANA-ARUSI YUPO PAMOJA NAO?”
MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.
NINI MAANA YA HUU MSTARI ” NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?(2TIMOTHEO 4:7)
MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
SWALI: Shetani kwa sasa ni mzuri wa umbo kama malaika watakatifu au ni mwenye mapembe na makwato na makucha marefu ya kutisha?
JIBU: Udanganyifu mkubwa uliopo duniani leo hii, ni pale watu wanapodhani kuwa shetani ni kiumbe chenye mapembe ya kutisha tu na kinakaa makaburini na kuzimu, hivyo wanadhani endapo mtu akikutana na kitu kama hicho kinachotisha sana ndio wamemuona shetani, Lakini hawajui kuwa yule alikuwa ni malaika kama wale wengine na alipoasi yeye na malaika zake, ndipo akawa shetani(Kumbuka maana ya neno shetani sio mapembe hapana bali ni MSHITAKI.
Hivyo mara baada ya kuanguka ndipo akageuka na kuwa mshitaki wetu akitushitaki mbele za Mungu ..na biblia inaposema amelaaniwa haimaanishi kalaaniwa kimaumbile(ya nje) hapana, bali katika roho, na ndio maaana hata leo hii wanadamu wakilaaniwa na Mungu hawabadilili maumbile yao na kuwa vitu vya kutisha vyenye mapembe au viumbe visivyoeleweka, hapana bali roho zao ndio zinazobadilishwa. Kwahiyo shetani na malaika zake vivyo hivyo, wapo vilevile na ndio maana wanao uwezo wa kujigeuza jinsi wapendavyo hata kijifanya kama malaika wa Nuru wa Mungu, kadhalika pia hawajaondolewa ujuzi wao wote waliokuwa nao, isipokuwa hawana uwezo wowote wa kumshinda mtu aliye ndani ya Kristo.. Ukisoma;
2Wakorintho 11:3 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
2Wakorintho 11:3 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Kwahiyo unaona hapo?..Hawa watu wote waasi pamoja na viumbe vilivyolaaniwa(malaika waovu), wapo tu kama walivyoumbwa, isipokuwa tabia za roho zao ndio zinazowatofautisha kwasababu hao tayari wameshalaaniwa wakiongejea mauti ya pili katika lile ziwa la moto..(Na tabia zao ndio zinazofananishwa na vitu vya kutisha). Kwahiyo ndugu kumbuka ni vita kubwa inayopigwa sasa hivi, haupigani na vibwengo, au majinamizi, n.k. bali unapigana na malaika na vita kubwa ni kukufanya wewe Uache Imani yako usiende mbinguni.Tujitahidi tufanye Imara wito wetu na uteule wetu, kwasababu shetani ni kama simba angurumaye..
1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.
1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.
Ubarikiwe sana. Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye namba hizi: +255789001312/ +255693036618 . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:
KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI, JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?
JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?
TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
Kwa kuwa Bwana Yesu alipitia katika tumbo la Mariamu je! Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
JIBU: Mariamu alimzaa BWANA kwa namna ya mwili, hivyo wakati Bwana alipokuwa duniani ndio Mariamu alijulikana kama mama wa Yesu, na sio mama wa Mungu. Bwana Yesu alipokuja hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili lakini hakuja kutafuta kuabudiwa na ndio maana hakuna sehemu yoyote alijiita yeye ni Mungu, zaidi sana alikuwa anawarudisha watu wamuabudu Baba. Kumbuka Mungu alipouvaa mwili ilimpasa afananishwe na mwanadamu kwa namna zote, azaliwe, ale chakula, asikie maumivu, alie, aone huruma, n.k. kama mwanadamu mwingine yeyote, si ajabu kumuona akiwa na Baba au bibi, au babu au mjomba, lakini haimaanishi kuwa yeye (YESU) yupo chini ya hao wote hapana..
Mathayo 22:41 Bwana Yesu alizungumza maneno haya;
“41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena”.
“41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?
42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,
44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?
46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena”.
Unaona hapo? jibu litakuwa pia hivyo hivyo kwa Mariamu kwamba Yesu atakuwaje mwanawe na wakati bado ni Bwana wake? na yeye ni binti wa Mungu (Kwasababu kama Daudi alikuwa mkubwa kuliko Mariamu aliambiwa hivyo je! si zaidi yeye?).
Hivyo sisi wote tunaomwamini YESU KRISTO mbele zake ni ndugu na dada, Na yeye akiwa kama Baba yetu. Kwahiyo ni muhimu tujue kutofautisha jinsi Mungu anavyotenda kazi katika ofisi zake tofauti, Mungu anapoonyesha unyenyekevu (kuzaliwa kibinadamu) haimaanishi kuwa mwanadamu yupo juu yake. Hapana anafanya hivyo kutuonyesha sisi njia bora kama watoto wake.
MARIAMU
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.
UDHAIFU WA SADAKA!
SHUKURU KWA KILA JAMBO.
KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?
JIBU: Ni kweli Yohana alibatiza kwa maji na alisema Bwana YESU atakapokuja atatubatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto..Sasa huu ubatizo wa moto ni upi?, kama tunavyofahamu moto hufanya kazi kuu tatu:
Ya kwanza: ni kuteketeza vitu dhaifu vyote visivyostahili. Kwamfano takataka..Vivyo hivyo Hatua hii ni ile Mungu anaichoma dhambi yote ndani ya mtu, hapo ndipo utakuta mtu tamaa ile ya kutenda dhambi aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma inakufa yote, alikuwa anavuta sigara ghafla kiu ya sigara inakufa, alikuwa anakunywa pombe ghafla kiu ya pombe inakata, alikuwa ni mzinzi ghafla hata ile hamu ya kwenda kufanya uzinzi inakufa, alikuwa mtukanaji,ghafla anaanza kuona uzito tena kufungua kinywa chake na kutukana watu, alikuwa ni mwizi anajikuta hapendi tena uwizi, alikuwa msengenyaji ghafla dhamiri inamsuta akitaka kusengenya, alikuwa anatembea nusu uchi, ghafla anaanza kuona aibu hata kuzivaa hizo nguo n.k.
Ya pili: ni kuimarisha vitu vilivyo vigumu ili viwe vigumu na imara zaidi. kama vile dhahabu inapopitishwa kwenye moto.
Hatua hii Roho Mtakatifu anapitisha mtu kwa lengo la kumuimarisha, Kama wafuaji wanavyofanya huwa wanayeyusha madini kwenye moto mkali ili baadaye yakishaganda yawe na mng’ao mzuri zaidi. , japo kwa nje yataonekana kama yanapitia dhiki ya hali ya juu kwa kuwekwa kwenye tanuru lakini yakishamalizwa kuchomwa matokeo yake yanaonekana kuwa bora zaidi kuliko yalipokuwa pale mwanzoni (Na ndio maana tunaona matofali ya udongo huwa yanachomwa kwanza, na ndipo yapelekwe kwa matumizi ya kujengea nyumba nzito,)..Hivyo kadhalika na kwa watoto wa Mungu..Tunapopokea Roho Mtakatifu..Mungu mwenyewe anaruhusu tupitie moto wa majaribu, ili kuzihimarisha IMANI ZETU zisiwe dhaifu, hata tutakapopitia mambo magumu tusiweze kuanguka kirahisi.
Na ndio maana tunaona pale tu mtu anapoanza kuamini! mara anaanza kuona mambo ya nje yanabadilika, ghafla anachukiwa na ndugu au kutengwa, mwengine atapitia misiba, mwingine magonjwa, mwingine vifungo, mwingine mapigo, mwingine anadorora kiuchumi, mwingine atatengwa n.k. mfano kama walivyopitia akina Ayubu, Yusufu n.k….Lakini Mungu kumpitisha mtu hivyo huwa sio kwa ajili ya kumwangamiza hapana bali ni kumuimarisha hivyo mtu kama huyo Bwana huwa anampa neema ya ziada kuyashinda hayo majaribu, kwasababu Mungu hawezi kuruhusu tujaribiwa kupita tuwezavyo
1Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.
Na pia Ukisoma…
1Petro 1: 6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba KUJARIBIWA KWA IMANI YENU, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”
Hivyo huo ndio ubatizo wa Moto unaozungumziwa hapo..Kwahiyo mtoto yoyote wa Mungu ni lazima aupitie huo(Mitume walipitia, manabii walipitia na Bwana wetu Yesu Kristo alipitia kadhalika na sisi pia)..yaani ubatizo wa Maji pamoja na ubatizo wa Roho na wa moto .
Na Hatua ya tatu: Ni kuchochea. Kwamfano moto ukiwashwa ndani ya bunduki, ile risasi iliyo ndani yake ni lazima ifyatuke. Moto ukiwekwa chini ya sufuria yenye maji, yale maji ni lazima yatokote, Vivyo hivyo na moto wa Roho ukiachiliwa ndani ya mtu..Ni lazima atatoka na kwenda kuwahubiria injili wengine, hawezi kutulia..Na hicho ndicho kilichotokea ile siku ya Pentekoste mitume walipopokea ubatizo huu, muda huo huo walianza kuhubiri kwa kasi sana.
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
MELKIZEDEKI NI NANI?
SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.
JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kwamba ziwa la moto waliandaliwa shetani na malaika zake,(wale walioasi pamoja naye), kutokana na makosa waliyoyafanya huko nyuma kabla ya mwanadamu kuumbwa, ambapo shetani pamoja na kuonywa na Mungu abaki katika kweli lakini hakutaka, akaandaliwa adhabu hiyo,Na vivyo hivyo wanadamu ambao hawataki kukaa katika ile kweli, wao pia watatupwa katika lile ziwa la moto.
lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hamchomi shetani au mwanadamu kwenye ziwa la moto kama kuwakomoa au kuwakomesha au kuwalipizia kisasi, hapana! bali Bwana anafanya vile ili kuondoa uovu karibu naye kwasababu yeye ni mtakatifu, ili kuelewa zaidi tafakari mfano ufuatao, Wewe ni msafi hupendi uchafu halafu inatokea kuna uchafu umejitokeza pembeni yako au karibu na makazi yako, uchafu huo unakuletea harufu mbaya, na kichefuchefu, na kukufanya ujisikie vibaya sana, dawa pekee ya kuutoa uchafu huo ni lazima itakuwa ni kuukusanya pamoja na kwenda kuutupa au kuuchoma moto? swali ni je! umeuchoma uchafu huo kwasababu unakisasi nao? au kwasababu unataka kuukomoa? jibu ni hapana!! unauchoma uchafu kwasababu umekaa mahali pasipo stahili na wewe huwezi kuchangamana na uchafu, kwahiyo itabidi utengeneze tanuru ili kuundoa uchafu huo. Kadhalika na Mungu pia, yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu, biblia inasema tutakuwa watakatifu kwasababu yeye Mungu ni mtakatifu
1 Petro 15: 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU. 17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
1 Petro 15: 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.
17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
Unaona hapo sababu pekee ya Mungu kuuteketeza Roho zote zilizoasi katika ziwa la moto ni kwasababu yeye ni MTAKATIFU na hawezi kuchangamana na uchafu, hawezi kukaa mahali pamoja na uchafu, watu waovu hawawezi kuzirithi ahadi za Mungu, hawawezi kuketi pamoja naye, na kama unavyojua takataka ngumu ndiyo inayochelewa kuteketea zaidi kuliko ile laini kadhalika nafsi iliyojichafua sana na mambo maovu ndiyo itakayoadhibiwa sana kuliko ile iliyojichafua kidogo.
Luka 12: 47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. 48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.
Luka 12: 47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.
Hivyo adhabu ya shetani haiwezi kuwa sawa na ya mwanadamu, yeye atapigwa zaidi, na adhabu ya aliyeua watu 100 haiwezi kuwa sawa na aliyeua watu 10 n.k Lakini mwisho wa yote roho zote zilizoasi(shetani na wanadamu walioasi) zitakufa katika lile ziwa la moto, kwasababu hazina uzima wa milele, hiyo ndiyo mauti ya pili biblia inayoitaja katika (ufunuo 2:11,ufunuo 20:14). Kwahiyo tujitahidi tumwishie Mungu, tukijua kuwa ipo hukumu mbeleni inatungojea.
Ubarikiwe sana. . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=DaH7IK-F324[/embedyt]
MBONA MUNGU ANARUHUSU WATU WAPATE SHIDA, ILHALI ANA UWEZO WA KUTUEPUSHA?
JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?
NI NANI ANAYETAWALA DUNIA KATI YA MUNGU NA SHETANI?
MUNGU MWENYE HAKI.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
JIBU: Neno Malkia wa mbinguni limeonekana mara mbili katika biblia
18 Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi. 19 Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe? 20 Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.
18 Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
19 Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?
20 Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.
Yeremia 44:17-23 ” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba MALKIA WA MBINGUNI, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo? 20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema, 21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake? 22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo. 23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. ”
Yeremia 44:17-23 ” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba MALKIA WA MBINGUNI, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.
19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema,
21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?
22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. ”
Tunaona habari hizo zote mbili zinaelezea juu ya miungu ya kipagani iliyowasababishia Israeli kuingia matatizoni kwa kwenda kuifukizia uvumba, na kumbuka haina uhusiano wowote na ukristo, kwahiyo mbinguni Mungu anapoishi hakuna malkia, biblia inamtaja MFALME TU!, Naye ni mmoja na si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA yeye peke yake.
Hivyo Mariamu sio malkia wa mbinguni, alikuwa ni mwanamke kama wanawake wengine waliokuwa wanamcha Mungu na kupewa neema ya kipekee ya kumzaa Bwana wetu Yesu, lakini hilo halina uhusiano wowote na yeye kuwa malkia, desturi za kuabudu miungu wake ni za kipagani na zilikuwepo tangu zamani AShtorethi/Semiramisi/Artemi mungu mke alikuwa anaabudiwa zamani zile na ndiye aliyekuwa anajulikana kama malkia wa mbinguni. Kanisa katoliki ndilo lililobeba tamaduni hizi za kipagani kumwabudu Mariamu na kuwa kama kipatanishi kati yetu na Mungu ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Kwahiyo mkristo yoyote hapaswi kujihusisha na ibada potofu zinazotaja kuabudu miungu “wake”. Ni YESU KRISTO pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.
Mada zinazoendana
YESU KRISTO NI MUNGU NA KAPITIA TUMBONI KWA BIKIRA MARIAMU SASA NI SAHIHI KUMUITA MARIAMU MAMA WA MUNGU?
ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA (MATHAYO 2) . ZILIWAKILISHA NINI?
NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?
JE! NI SAHIHI MTU KUNING’INIZA PICHA NYUMBANI MWAKO KAMA YA YESU?
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
MAVAZI YAPASAYO.