Biblia inaposema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? ” Swali ni Je! sisi tutawahukumu vipi Malaika?.
1Wakorintho 6:2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
JIBU: Watakatifu wamefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO kwa sababu yeye aliitwaa asili ya mwanadamu na sio asili ya malaika wala kiumbe kingine chochote, maandiko yanamtaja yeye kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi (ambao ndio sisi),
Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.
Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.
Unaona hapo na kama vile Mungu alivyompa vitu vyote vya mbinguni, na vya duniani na vya kuzimu vivyo hivyo alimpa pamoja na hukumu yote (Yohana 5:22), na pia tukisoma:
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Kwahiyo kama Mungu amempa vyote ikiwemo na hukumu ya viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani, visafi na vichafu, vilivyopo na vitakavyokuja, hivyo ni dhahiri kuwa malaika wote watakatifu na walioasi wapo chini yake na watahukumiwa na yeye kulingana na njia zao, aidha ni nzuri au mbaya, kwa mfano ule ule atakavyowahukumu wanadamu wote watakatifu na waovu. Hivyo basi kama watakatifu watakuja kuketi pamoja na KRISTO (Ufunuo 3:21) ni wazi kuwa watahukumu pamoja na Kristo, maana wakati huo watasimama kama ndugu zake. Na ndio maana Mtume Paulo anaoujasiri wa kusema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika
Kwahiyo ndio ni kweli malaika wote watahukumiwa na watakatifu, wale malaika watakatifu watazidi kutukuzwa zaidi pamoja na Kristo katika umilele ujao, na wale waovu (shetani na malaika zake) watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto pamoja na wanadamu walioasi. kumbuka hizi hukumu zitafanywa na YESU pamoja na watakatifu wake tu!. Na ndio maana maandiko yanasema tutauhukumu ulimwengu na malaika wote.
Ufunuo 20:4 inasema…
” KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”
Kwahiyo wale tu watakaoshinda na KUKETI PAMOJA NAYE KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI hao ndio watakaohukumu ULIMWENGU na MALAIKA. Amina. Kumbuka watakaokuwa na mamlaka hayo ni wale watakaoshinda tu (watakaonyakuliwa).. Na mamlaka hayo tutayapata baada ya kumaliza maisha haya, lakini kwa sasa tumewekwa chini ya malaika, kama Bwana Yesu alivyowekwa chini yao kipindi yupo duniani (Waebrania 2:9 ) mpaka alipomaliza kazi na kutukuzwa..Kwahiyo tujitahidi tushinde maana biblia inasema..
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
JE! KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
Rudi Nyumbani:
Print this post
JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo kwa jamii fulani ya watu, Pia ni muhimu kufahamu utendaji kazi wa Mungu katikati ya wanadamu tangu kuumbwa kwao, Mungu alimchagua Ibrahimu na kumbariki yeye na uzao wake, kuanzia hapo Bwana Mungu aliliteua taifa moja pekee ambalo atashughulika nalo katika mpango wake wa wokovu kwa wanadamu (yaani taifa la Israeli), hilo pekee ndilo lililokuwa taifa la Mungu katikati ya mataifa yote ulimwenguni katika agano la kale.
Hivyo Wayahudi (au Waisraeli) kwa asili hawakuwa wazungu au watu wazuri nikiwa na maana kuwa “weupe sana” kuliko watu wa mataifa mengine duniani, walikuwa ni watu wa kawaida sana, na hata ngozi zao hazikuwa nyeupe kama za watu wa mataifa mengine mfano wa Ugiriki, Rumi, ambayo yalikuwa kando kando ya Israeli n.k ni jamii iliyokuwa inakaribia kufanana na Waarabu, na kama unavyojua Waarabu sio weupe kama wazungu au Wachina, hivyo Hao (waisraeli) ndio Mungu aliowateua sio kwa mwonekano wao bali kwa kusudi lake Mungu, ili baadaye aje kutimiza mpango wake wa wokovu alioukusudia kuja kuuleta kwa kupitia Bwana wetu Yesu Kristo kwa watu wa ulimwengu mzima na ndio maana utaona kuanzia mwanzo wa biblia hata mwisho huwezi kuona ngozi nyeusi au nyeupe ikitajwa, na sio tu ngozi nyeusi hutaweza pia kuona mzungu, au mchina yoyote, au mhindi yoyote akitajwa kama nabii halisi wa Bwana, kwasababu kwa wakati huo Mungu alikuwa anatenda kazi na wayahudi (waisraeli) tu. na sio na watu wa ulimwengu mzima,
Lakini ulipofika wakati wa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kudhihirishwa ulimwenguni kote, watu wote mbele za Mungu tumekuwa sawa hakuna tena cha myahudi, au mtu wa mataifa au mweusi, au mwarabu, au mchina n.k Bwana Yesu Mungu wetu alikiondoa kile kiambaza cha kati kilichotutenga sisi na jamii ya waisraeli, na kutufanya mbele za Mungu kuwa wamoja, na ndio maana leo utaona kuna manabii, waalimu, wakizungu, wakiafrika, wa-kichina, wa-kihindi, jambo ambalo hapo kwanza halikuwepo. Ilikuwa ni kwa wayahudi tu, na sio kwasababu eti wao ni weupe, hapana wakati huo wazungu walikuwepo wengi sana, wachina walikuwepo nao pia lakini hawakuruhusiwa hata mmoja kumkaribia Mungu wa Israeli katika shughuli zozote zinazohusiana na ibada..
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; 12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. 13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. 15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. 16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”.
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.
16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”.
Na Pia papa hatuwezi kumweka katika kundi la Mitume au Manabii, kwasababu mfumo wa anachokiamini ni kinyume na mfumo wa maandiko unavyoagiza..
Mada zinazoendana:
UZAO WA NYOKA.
JIRANI YAKO NI NANI?
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
UNYAKUO.
JIBU:Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Wakristo hawahesabiwi haki mbele za Mungu katika siku, miezi au miaka ya kuabudia, aidha uabudu jumapili, jumatatu, jumamosi au jumatano huo ni utaratibu wa mtu tu! haimuongezei mtu chochote katika uhusiano wake na Mungu. Biblia inasema..
Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”
Na Pia inasema tena katika
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”
Hivyo Maana ya NENO sabato ni “Pumziko”, na pumziko kwa wakristo lipo rohoni, na mwokozi wetu Yesu yeye alituambia kuwa ndiye BWANA wa sabato (soma Mathayo 12:8), hivyo tukimpata YESU tumeipata SABATO au “pumziko letu la rohoni” na ndio maana anasema..
Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Kwahiyo wanaoabudu jumamosi, au jumapili au jumatano hawafanyi makosa, ni utaratibu wao tu, mbele za Mungu wote wapo sawa, kwa mfano tunasoma katika biblia wakristo wakwanza waliiteua siku ya kwanza ya juma ( yaani JUMAPILI) kwa ajili ya kukusanyika na kufanya changizo pamoja na kumega mkate, ukisoma Matendo 20:7 na 1Wakoritho 16:1-2 utaona jambo hilo, hivyo kuteua siku fulani na kusema hiyo ndio Mungu anairidhia kuabudia zaidi ya siku nyingine, ni kutokuyaelewa maandiko. kwasababu ibada halisi ipo rohoni na Mungu anaabudiwa katika roho na kweli, na sio katika siku maalumu au miezi maalumu au miaka maalumu bali ni kila saa na kila wakati mahali popote.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
EPUKA MUHURI WA SHETANI
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi
JIBU: Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake, Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake, kama wengi tunavyodhani Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.
Hivyo tukisema Mungu ana nafsi tatu kwa kuusimamia mstari huu sio kweli, pale Bwana alikuwa anazungumza na malaika zake ambao walikuwa wameshaumbwa kabla yetu sisi, Tunaona pia jambo hili linajirudia sehemu nyingine nyingi katika biblia Bwana akizungumza na malaika zake, Ukisoma
Mwanzo 3:22″Bwana Mungu akasema basi huyu mtu amekuwa kama MMOJA WETU, kwa kujua mema na mabaya”…,
pia,
Mwanzo 11:6 “Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.”
Unaona hapo sehemu zote hizi mbili Bwana alionekana akijadiliana na malaika zake. Mungu huwa anatenda kazi na malaika zake. Tukisoma pia
Isaya 6:8 Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, nimtume nani? naye ni nani atakayekwenda KWA AJILI YETU? Ndipo niliposema mimi hapa nitume mimi. Naye akaniambia enenda ukawaambie watu hawa fulizeni kusikia lakini msifahamu; fulizeni kutazama lakini msione…”
Unaona tena hapo Bwana alimuuliza nabii Isaya ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu (yaani Mungu na jeshi lake la mbinguni)?. Kwahiyo Mungu kujadiliana na malaika zake sio jambo jipya tunaweza tukaliona pia kwenye ile habari ya mfalme Ahabu na nabii Mikaya ukisoma
2 nyakati 18:15-22” utaona jinsi Bwana alivyokuwa anashauriana na malaika zake juu ya hatma ya mfalme Ahabu.
Kwahiyo pale katika mwanzo 1:26 aliposema Na tumfanye mtu kwa mfano wetu Mungu alikuwa hazungumzi na YESU wala Roho Mtakatifu bali na malaika zake waliokuwepo kabla yetu sisi. (Lakini kumbuka sio kwamba malaika ndio waliokuwa wanaumba, hapana Mungu peke yake ndiye aliyekuwa muumbaji.)
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
JINSI EDENI ILIVYOKUWA.
Rudi Nyumbani
JIBU: Biblia inasema kuna ufufuo wa aina mbili,
Ufufuo wa kwanza, umejumuisha wale watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu ukisoma (Mathayo 27:52) utaona..,pamoja na watakatifu watakao fufuka katika unyakuo, na watakao fufuliwa wakati wa kuingia kwenye ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 20:4) haya ni makundi matatu yanayotengeneza aina ya kwanza ya ufufuo.
Ufunuo 20:6 “….Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza, juu ya hao mauti ya pili haina nguvu…”
Na ufufuo wa pili utakuja mara tu baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha..ambapo wafu wote ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza watafufuliwa na kuhukumiwa na Kristo mwenyewe katika hukumu ya kile kiti cheupe cha Enzi cha Yesu Kristo tukisoma
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”
Kwahiyo ndugu biblia inasema wana heri wale watakaokuwepo katika ule ufufuo wa kwanza. kwasababu mauti ya pili haitakuwa na nguvu juu yao. Na mauti ya pili ni ziwa la moto. Hivyo tujitahidi hata kama Bwana atakupokuja akatukuta tumelala(tumekufa), basi tuwe na nafasi katika ule ufufuo wa kwanza.
KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI.
Miriamu alikuwa ni dada yake Musa na Haruni, wa damu (Hesabu 26:59), Miriamu ndiye aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa katika famila ya Yokebedi na Amramu. Biblia inasema naye pia alikuwa ni nabii. Hawa watatu Bwana aliwaita kipekee kuhudumu katika hatua ya kuwaongoza wana wa Israeli. (Mika 6:4)
Huduma ya Miriamu ilikuwa ya kipekee na kielelezo kwa wanawake, kwani baada ya Bwana kulipiga jeshi la Farao kwa kulitosa kwenye Bahari ya Shamu, Miriamu alisimama na jeshi kubwa pamoja na wanawake wenzake, wakamwimbia Bwana kwa MATARI na kucheza! (Kutoka 15:20-21).
Wakiwa jangwani katika safari yao ya kwenda nchi ya Ahadi. Miriamu pamoja na Haruni walianza kumnenea Musa, na kumlaumu, kwasababu ya Mwanamke wa kiKushi aliyemwoa. Jambo hilo likamchukiza sana Bwana na hatimaye Bwana kumpiga Miriamu kwa ukoma. Lakini baadaye alikuja kupona baada ya Musa kumwombea. (Kutoka 12:1-6).
Miriamu alikufa kabla ya kuiona nchi ya Ahadi, alikufa katika Bara la Sini, huko Kadeshi, na huko ndiko alikozikiwa.(Kutoka 20:1).
1.Musa ni nani?
2. Haruni ni nani?
3. Fimbo ya Haruni ilikuwaje?
HOME
Haruni alizaliwa miaka mitatu kabla ya kuzaliwa Nabii Musa, alikuwa ni ndugu wa damu kabisa wa Musa. Na walikuwa na dada yao aliyeitwa MIRIAMU. Bwana alimwita Haruni katika huduma baada ya Musa kusita-sita wito wake wa kwenda kwa Farao, na baada ya kutoa vijisababu. Mungu alimwita Haruni ndugu yake awe kama msemaji wake katika safari yao ya kwenda kuwafungua wana wa Israeli dhidi ya mateso ya Farao. (Kutoka 4:10-15).
Haruni pamoja na Musa walikuwa ni wa kabila la LAWI. Bwana aliwapa maagizo kwamba kwa kutumia ile FIMBO wakafanye ajabu zote mbele ya Farao. Fimbo ndiyo iliyokuja kujulikana kama FIMBO YA HARUNI.
Kutokana na utumishi wa Haruni, Bwana alimteua awe KUHANI MKUU, Yeye na wanawe milele. Na kabila la Musa na Haruni, (kabila la Lawi) ndilo lililokabidhiwa shughuli zote za kikuhani, yaani shughuli za kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zote za wana wa Israeli.
Kutokana na upingamizi mkali wa wana wa Israeli dhidi ya uongozi wa Mtumishi wa Mungu, Haruni mara kadhaa alijaribu kuvutwa na ushawishi wao. Na hivyo wakati Fulani kufikia hatua ya kukubali kuwatengenezea sanamu ya ndama (Kutoka 32:1-5).
Haruni naye hakufika nchi ya Ahadi, kutokana na dhambi waliyoitenda wao na Musa ya kujichukulia utukufu mbele ya Wana wa Israeli.(Hesabu 20:10,24) Hivyo alikufa akiwa jangwani akiwa mzee sana.
Pamoja na mambo mengi yasiyofaa tusiyoweza kujifunza kutoka kwake, kama kuungana na Wana wa Israeli kutengeneza ile sanamu ya ndama… lakini bado Haruni alikuwa ni mtu mwenye ujasiri mwingi kuliko Musa..Wakati Musa anasita sita kwenda kuzungumza na Farao..yeye alichukua nafasi yake kwa kuuvaa ujasiri uliotoka kwa Mungu..
Na jambo lingine la Muhimu ni nafasi ya ukuhani aliyopewa na Mungu..Musa hakupewa nafasi ya ukuhani isipokuwa Haruni na wanawe..Nafasi ya ukuhani inafananishwa na nafasi ya YESU KRISTO, Kama Kuhani Mkuu…Hivyo alisimama kama Kuhani Mkuu wa Mungu kwaajili ya wana wa Israeli. Na Yesu Kristo kama Kuhani mkuu wa wanadamu wote.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
1. Fimbo ya Haruni ilikuwaje?
1.Miriamu ni nani?
2. Musa ni nani?
Musa alizaliwa huko Misri, miaka mingi kidogo baada ya Yusufu mwana wa Yakobo kufariki. Wakati wa kuzaliwa kwake, mama yake alimhifadhi mtoni kutokana na hofu ya amri ya Mfalme juu ya kuuawa kwa wazaliwa wote wa jinsia ya kiume.
Jina la Baba yake Musa ni Amramu na Mama yake ni Yokebedi. (Hesabu 26:59).
Musa alikuwa na Kaka yake wa damu aliyeitwa Haruni waliokuwa wamepishana miaka 3, Haruni alikuwa mkubwa kwa Musa, na ndiye yule aliyekuja kuwa Kuhani Mkuu, pia alikuwa na dada yake aliyeitwa Miriamu ambaye naye pia alikuwa ni Nabii wa Bwana.
Bithiani aliyekuwa Binti wa Farao alimwokota akiwa kwenye kijisafina kidogo, pembezoni mwa mto wakati akiwa anaoga. Musa aliishi katika Nyumba ya kifalme mpaka alipofikisha umri wa miaka 40, Baadaye aliasi nyumba ya Farao kutokana na kumsaidia mmoja wa ndugu zake wa Kiebrania, akakimbilia nchi ya Midiani. Huko alipata mke kutoka kwenye nyumba ya kuhani mmoja wa Midiani aliyeitwa Yethro.
Alikaa miaka 40 nyumbani kwa Yethro, akichunga mifugo yake, mpaka siku moja Bwana alipomtokea katika mwali wa moto, ndani ya kile kijiti, alipokuwa anachunga kundi la Yethro, Alipewa maagizo ya kuwaokoa Israeli waliokuwa wanateswa chini ya utawala mkali wa Farao.
Kwa Ishara nyingi na miujiza mingi Musa aliwaongoza wana wa Israeli miaka 40 mingine, na Alifariki akiwa na miaka 120, akiwa na nguvu zake zote. Macho yake hayakupofuka wala mwili haukupungua nguvu (Kumbukumbu 34:7)
Musa pekee ndiye Nabii aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, wala baada yake hakuinuka nabii mfano wake yeye (Kumbukumbu 34:10-12)
1.Utaji uliokuwepo juu ya uso wa Musa ulikuwa unaashiria nini?
2.Haruni ni nani?
3. Miriamu ni nani?
Yezebeli, alikuwa ni Binti wa Mfalme wa Wasidoni aliyeitwa Ethbaali (1 Wafalme 16:31). Sidoni ilikuwa ni nchi iliyokuwepo Kaskazini mwa Taifa la Israeli, kwasasa nchi hiyo ni nchi ya LEBANONI.
Desturi za Wasidoni zilikuwa ni kuabudu miungu, waliabudu mungu wao maarufu aliyeitwa BAALI.
Mfalme wa Israeli aliyeitwa Ahabu alimwoa Binti huyo wa kifalme na kumleta katika Taifa la Israeli na kuwa Malkia. Na hivyo kuingiza ibada za miungu migeni ndani ya Taifa la Mungu.
Yezebeli licha tu ya kulichafua Taifa la Israeli kwa kumshawishi sana Mumewe Ahabu, alikuwa pia ni mchawi (2 Wafalme 9:22). Aliwaua manabii wengi wa kweli wa Mungu, na aliikosesha Israeli kwa sehemu kubwa sana. Mahali pengine Inamtaja Yezebeli kuwa ni Nabii wa Uongo. (Ufunuo 2:20)
Yezebeli pia ndio mwanamke pekee kwenye Biblia nzima aliyekuwa anapaka WANJA usoni na kupamba uso. Desturi za wanawake makahaba.(2 Wafalme 9:30). Mwanamke huyu ndiye Mwanamke pekee aliyeshindana na maagizo ya Mungu kuliko wanawake wote kwenye Biblia, ndiye aliyemsumbua sana Eliya na hata kufikia hatua Nabii Eliya kumkimbia, kuogopa madhara atakayoyapata kutoka kwake.
Yezebeli alikuwa na mtoto wa kike, aliyeitwa ATHALIA ambaye naye alirithi tabia zote za mama yake ambaye naye pia alikuwa anaabudu Baali, Athalia alikuwa muuaji na aliutwaa umalkia kwa nguvu ndani ya kabila la YUDA.
Yezebeli hakudumu muda mrefu kwani alikufa sawasawa na unabii uliotolewa juu yake, kwamba atakufa na mbwa watalamba damu yake. Siku ya kufa Yezebeli aliangushwa kutoka juu ya ghorofa refu na kuchuruza damu ukutani mwote, na alipofika chini farasi alimkanyaga kanyaga..na Mbwa walikumla na kubakisha viganja tu vya mikono na kifuvu (2 Wafalme 9:35)
NABII ELIYA NI NANI?
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
Shetani ni nani?…Tafsiri ya Jina shetani ni ‘mshitaki’ au ‘mchongezi’. Kazi yake ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu.
Jina lingine la shetani ni “LUSIFA” Maana yake ‘NYOTA YA ALFAJIRI’. (Isaya 14:12) Jina hili Lusifa aliitwa kabla hajaasi, baada ya kuasi ndio akawa shetani.
Alikuwa ni Malaika wa Sifa (Kerubi) huko mbinguni, alikuwa ni Mzuri kwa mwonekano na mkamilifu katika njia zake zote, aliishi katika taratibu za Mungu, na katika njia za Mungu, na hivyo akapata heshima kubwa mbinguni zaidi ya Malaika wengi (Ezekieli 28:14).. Alikuwa mkamilifu mpaka siku uovu ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15).
Kwasababu ya uzuri wake Moyo wake ukainuka, akataka kujiinua awe kama Mungu, aabudiwe kama Mungu na kwa ujuzi wake mwingi akawashawishi theluthi ya Malaika mbinguni (1/3) waambatane naye.
Vita, vikali vikatokea Mbinguni kati ya Malaika waliokataa kuungana na Lusifa na malaika waliokubali kuungana naye. Biblia haisema vita hivyo vilipiganwa kwa muda gani, lakini inasema mwisho wa siku lusifa pamoja na malaika wake walishindwa vita vile, na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:7).
Na vita hivyo bado havijaisha, vita vya kwanza vilipiganwa mbunguni, kati ya Malaika walio upande wa shetani na wale walio upande wa Mungu na Malaika waliokuwepo Upande wa Mungu wakavishinda, lakini vita vya pili na vya mwisho vinapiganwa hapa duniani na hata sasa bado vinaendelea..Na vitaisha mwisho wa dunia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP 1. Je! Ni nani aliyemdanganya shetani?
2. Huduma 10 za shetani sasahivi duniani ni zipi?
3. Mpango wa shetani kwa watoto katika siku hizi za mwisho.
4. Agenda kubwa ya shetani kwa kanisa hili la siku za mwisho
5. Mafundisho ya Mashetani ni yapi katika siku hizi za mwisho?
6. Kazi ya Malaika watakatifu sasa ni nini?