Swali: Maandiko yanasema KRISTO ameketi kutuombea, hata tufanyapo dhambi?
Jibu: Tafadhali soma taratibu na kwa umakini…
Warumi 8:34 “Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; TENA NDIYE ANAYETUOMBEA”.
Ni kweli Neno la Mungu linasema BWANA WETU YESU KRISTO, katika mstari huo na linazidi kututhibitishia tena katika 1Yohana 2:1.
1Yohana 2:1 “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi TUNAYE MWOMBEZI KWA BABA, Yesu Kristo mwenye haki”
Lakini ni vizuri kuzijua lugha za kiroho na namna ya kuzitafsiri, vinginevyo itatuwia vigumu sana kuielewa biblia na hata wakati mwingine kujikuta tunaabudu sanamu kwa kushindwa kuzipambanua lugha za kiroho,
Kwamfano kuna mahali Bwana YESU alisema Mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake (soma Yohana 6:53), sasa tukiuchukua huo mstari kama ulivyo na kwenda kutafuta mwili wa Bwana kama nyama, na Damu yake kama ilivyo na kuinywa, tutakuwa tumeshindwa kutafsiri vyema lugha ya biblia, na hivyo tutakuwa tumefanana na waganga na wachawi walao nyama na kunywa damu!.
Lakini kama tukiweza kuelewa maana ya mwili wake Bwana Yesu na damu yake kuwa ni ule mkate na kile kikombe, sawasawa na (Mathayo 26:26-27) tutakuwa tumeenda sawasawa na Neno la Mungu.
SASA KWA MSINGI HUU, TUTAKUWA TAYARI KUJIFUNZA NI KWA NAMNA GANI KRISTO ANATUOMBEA KWA BABA.
Katika hiko kitabu cha Warumi mlango wa 8:34 tuliposoma kuwa KRISTO ndiye anayetuombea, hebu turudi mistari kadhaa nyuma mpaka ule mstari wa 26, tuone jambo..
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA kuugua kusikoweza kutamkwa. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”
Angalia hapa; Katika ule mstari wa 34 tumesoma kuwa ni BWANA YESU ndiye anayetuombea, lakini tena katika mstari wa 26 ndani ya sura hiyo hiyo, tunasoma kuwa ni ROHO MTAKATIFU ndiye anayetuombea.. Sasa swali ni yupi kati ya hawa wawili anayetuombea kwa Baba?… ni Roho Mtakatifu au ni Bwana YESU??.
Sasa jibu la swali hili ni rahisi sana na ndio tunaelekea katika kiini cha mada hii.
Jibu la swali hili tunalipata katika kitabu kile cha 2Wakorintho 3:17, sikiliza Neno la Mungu linavyosema…
2Wakorintho 3:17 “Basi Bwana ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru”.
Hapo anasema lakini “Bwana” (yaani YESU)..ndiye “Roho”(yaani Roho Mtakatifu).. kumbuka hapo Roho imeanza kwa herufi kubwa kuwakilisha Roho Mtakatifu. (Popote pale Roho inapoanza kwa herufi kubwa inamaanisha Roho wa Mungu).
Hivyo kulingana na hayo maandiko, ni sahihi kabisa kusema BWANA YESU ndiye ROHO MTAKATIFU, na Roho mtakatifu ndiye Bwana YESU.. Kwahiyo mahali popote asemapo Roho Mtakatifu ni Bwana YESU ndiye kasema..
Ndio maana utaona katika kile kitabu cha Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3 katika jumbe za yale makanisa saba, utaona ujumbe unaanza YESU ANASEMA, na unamaliza ROHO AYAAMBIA MAKANISA, ikiwa na maana kuwa Roho ndiye huyo huyo Bwana.
Vile vile Roho Mtakatifu akiomba ni Bwana ameomba.
Sasa swali la mwisho ambalo litahitimisha Mada hii, ni je!, Kama Bwana YESU ndiye Roho Mtakatifu, je huyo Roho Mtakatifu anatuombeaje sawasawa na huo mstari wa 26?
Roho Mtakatifu (ambaye ndiye Bwana mwenyewe) hatuombei kama sisi tunavyoombeana!.. La! Yeye anaomba ndani yetu.. Maana yake tuombapo sisi, basi yale maombi yetu anayachukua na kuyapeleka mbele za Baba katika lugha nzuri Zaidi, katika maelezo mazuri Zaidi.
Lakini si kwamba tumelala au tunacheza, au tunafanya mambo yetu mengine basi wakati huo huo yeye kule anatuombea, hapana! Hiyo si tafsiri yake kabia..
Kwa urefu jinsi Roho Mtakatifu anavyotuombea fungua hapa utapata kuelewa vizuri sana >>ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba jinsi Bwana YESU anavyotuombea ni kwajinsi ya Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu anachukua yale maombi yetu na kuyapeleka kwa Baba kwa lugha kamilifu Zaidi.. Hivyo kamwe usiwaze kuwa Bwana YESU yupo mbinguni mbele za Baba, akisali kwaajili yetu, bali ni kwa njia ya Roho wake mtakatifu ndani yetu, ndipo anapotuombea.
Kwanini tunajifunza haya?.
Ni kwasababu zipo Imani zilizoanzishwa na ibilisi mwenyewe zisemazo kuwa “hatuna haja ya kuomba, kwasababu Bwana YESU yupo mbinguni anatuombea usiku na mchana”…
Kamwe usidanganyike na hayo mafundisho kwani ni mafundisho ya Adui, ibilisi… Tusipoomba na Roho Mtakatifu hawezi kuomba, na Roho Mtakatifu asipoomba ni Bwana hajaomba.. Lakini tuombapo, Roho Mtakatifu ni kipaza sauti chetu kwa Baba..kwahiyo maombi ni lazima… (Pitia tafadhali somo la jinsi Roho Mtakatifu anavyotuombea).
Na mwisho kabisa, hakuna mtakatifu yoyote aliyekufa au aliyenyakuliwa anayetuombea… NI YESU TU PEKE YAKE, kwa NJIA YA ROHO WAKE MTAKATIFU, ndiye anayetuombea.. Hivyo Mtakatifu Mariamu, hawezi kutuombea, wala Eliya, wala Musa, wala Henoko, wala mtu mwingine yoyote aliye hai wala aliyekufa…(Hawana na hatuna hivyo vigezo).
Kwahiyo lililo kubwa na la msingi sana, ni kutafuta Roho Mtakatifu kwasababu kwa kupitia huyo ndio maombi yetu yatafika na kukubaliwa, na tena mtu asiyekuwa na Roho Mtakatifu huyo si wake kulingana na biblia (Warumi 8:9)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)
NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Roho Mtakatifu ni nani?.
Rudi Nyumbani
Print this post
Kwanza ni vema kufahamu uzazi wa mpango ni nini na kama ni dhambi au la!.
Uzazi wa mpango ni kuzaa kwa mpangilio ulioutaka wewe, kwamfano ukijiwekea malengo ya kuzaa watoto 30, huo ni uzazi wa mpango maadamu yalikuwa ni malengo yako, au ukijiwekea malengo ya kuzaa mmoja maisha yako yote huo pia ni uzazi wa mpango. Kinyume chake uzao usio wa mpango, ni ule wa kutojali idadi ya watoto utakaouzaa, wala kutojali muda wa uzaaji wako.
Ukweli ni kwamba uzazi wa mpango si dhambi. Kwasababu gani?
Licha ya kwamba Mungu ameweka maagizo yake kupitia biblia takatifu, lakini pia, ameweka hekima yake kupitia mambo ya asili (1Wakorintho 11:14, Warumi 1:20), Hivyo mambo ya asili yanatufundisha pia agizo la Mungu .
Si kila wakati mama atashika ujauzito, bali upo wakati wa hatari na wakati usio wa hatari. Sasa kwa hekima huo tayari ni utaratibu Mungu kamwekea mtu, atambue majira yake, achukue tahadhari. Umeona? Kwa namna nyingine Mungu anasema, kuna majira utapata mtoto, na kuna majira hutapata mtoto. Hivyo uamuzi ni wako, ukitaka kuzingatia mazunguko huo, ni wewe, usipojali pia ni wewe.
Sasa mtu ambaye anayechagua kuzingatia mzunguko huo wa asili wa Mungu, huyo tayari yupo katika uzazi wa mpango. Na pia ni agizo la Mungu tuwe na uwezo wa kuwatunza wale wa nyumbani kwetu (1Timotheo 5:8)
Lakini je! Vipi ambao wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango je na wao wapo sawa?
Tukisema njia za kisasa, ni kama zile za kutumia vidonge, kutumia sindano, kutumia vizuizi kama mipira (kwa wanaume na wanawake), kuweka kitanzi, na kuweka vipandiki/vijiti. Zote hizi ni njia za kisasa.
Hapa ni lazima tufahamu pia lengo ni nini?. Bila shaka lengo ni lile lile moja la uzazi wa mpango kwa wanandoa, na si vinginevyo. Lakini mwanadamu ameamua kutumia njia zake za kisasa, ili kufanikisha hilo?
Je! Ni kosa?
Ili kujibu swali hilo, tufikirie pia mambo mengine ya kisasa, leo hii tuna vitu vingi vya kisasa vimebuniwa na wanadamu, kwamfano kuna kuku wa kienyeji lakini pia wapo wa kisasa, kuna mchicha wa kienyeji lakini pia ipo ya kisasa, kuna matunda ya kienyeji lakini pia yapo ya kisasa. Je! Ni dhambi kutumia vitu hivyo, kwasababu vimebuniwa na mwanadamu?
Jibu ni hapana.
Lakini vinaweza kuwa na madhara yake, kwasababu mwanadamu hawezi kuumba kitu kiukamilifu. Ndio maana asilimia kubwa ya vitu hivi vya kisasa, huwa si vizuri kiafya. Vivyo hivyo katika matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Yaweza isiwe dhambi kwako kutumia. Lakini madhara ya kiafya, pia waweza kukumbana nayo. Wengine hupata shida ya vizazi, wengine ugumba kabisa kulingana na njia iliyotumika, lakini wengine hawapatwi na madhara. Hivyo amani ya Kristo iamue ndani yako.
Lakini ile y asili ni bora zaidi. Ukitumia njia ya kalenda, ni salama lakini pia Mungu ametubunia hiyo, ukijizoesha kuifuatilia utaweza tu kupangilia uzazi wako.
Lakini fahamu pia uzazi wa mpango, maadamu amani ya Kristo imeamua moyoni mwako, si dhambi mbele za Mungu.
Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?
JE! KUBET NI DHAMBI?
Je Kutoa Mimba ni dhambi?
Jibu: Miti ya Misunobari tunaisoma katika kitabu cha Isaya 55:13 na sehemu nyingine baadhi katika biblia.
Isaya 55:13 “Badala ya michongoma utamea MSUNOBARI, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali”
“Misonubari” ni jamii moja na miti ya “Mierezi”. Tofauti ya Msonubari na mwerezi ni kwamba Misonubari yenyewe haiwi mirefu kama mierezi, na pia ina matawi myembamba kuliko mierezi, lakini kwa sehemu kubwa inafanana kimatumizi na mierezi, ndio maana sehemu karibia zote panapotajwa miti ya Mierezi basi na Misunobari pia inatajwa..
Zekaria 11:2 “Piga yowe, MSUNOBARI, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia”.
Soma pia 2Wafalme 19:23, Isaya 14:8, Isaya 37:24, Ezekieli 27:5 na Ezekieli 31:8.
Miti ya Misonubari na Mierezi ilitumika katika ujenzi wa nyumba za thamani na ilipatikana sana katika nchi ya Lebanoni..
Sasa kwa urefu kuhusu miti ya Mierezi na matumizi yake fungua hapa >>>Mwerezi ni nini?
NI LAZIMA KUISHIKILIA IMANI MPAKA MWISHO.
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).
Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;
FAHAMU SEHEMU NNE (4) APANDWAPO MWAMINI.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
SWALI: Nini tafsiri ya Mithali 27:22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
JIBU: Kama tunavyojua mtwangio na kinu ni vyombo vinavyotumika kuponda-ponda nafaka ngumu kuwa unga, au wakati mwingine mimea migumu kuwa milaini. Mfano wa kisamvu ambacho ili kiweze kulika, majani yake huwezi yapika hivyo hivyo huna budi kuyatwanga twanga kidogo, yalainike ndipo upike ule.
Na vivyo hivyo, nafaka kama mahindi, au ngano, ili viweze kulika zamani vilikuwa vinatwangwa kwenye vinu ,tofauti na sasa vinasagwa na mashine.
Sasa katika mithali hiyo, Mungu anatoa, asili ya mtu mpumbavu, kwamba hata akitwangwa, mfano wa ngano kinuni, huo upumbavu hauwezi kumtoka. Yaani njia gani ya lazima itumike bado hawezi kuacha upumbavu.
Sasa ni vizuri kufahamu, mpumbavu ni nani?
Mpumbavu kibiblia sio mtu Fulani mjinga tu hapana, bali ni Neno pana, linalolenga kuanzia
mtu anayesema hakuna Mungu (zaburi 14:1)
Mtu mgomvi (Mithali 9:13),
Mtenda maovu (Mithali 10:23)
Anayejiona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)
Mwenye kiburi (Mithali 14:3)
Mwenye dharau (Mithali 15:5)
Yaani kwa kifupi mpumbavu ni mtu ambaye hana Mungu ndani yake. Kwasababu dhambi ndani ya mtu ndio chanzo cha Upumbavu wote.
Sasa mtu kama huyu, hakuna kitu kinachoweza kuutoa upumbavu huo ndani yake, waweza kusema elimu, lakini ni watu wangapi wameelimika, lakini walevi, watukanaji, mashoga. Hata atwangwe vipi kinuni hawezi lainika, ikiwa hajui ni kipi sahihi kinachoweza kutoa upumbavu huo.
Kumfunga mwizi, hakumfanyi wizi au tamaa ya kuiba itoke ndani yake, mara ngapi unasikia mwizi katoka jela, karudia wizi wake, au ni kiongozi ambaye anaaminiwa awe kielelezo cha kupambana na ufisadi, lakini yeye ndio anakamatwa katika ufisadi, au teja ametolewa hospitalini karudia, tena madawa la kulevya. Ndio maana jamii ijapojaribu kudhibiti vitendo viovu, bado haviishi, bali hubadilika tu maumbile. Kwasababu mpumbavu hata atwangwe kinuni, hawezi geuka, hakuna nidhamu inayoweza mbadilisha. Huwezi acha mwenendo wake mbovu kwa semina za kijamii, au kuwekewa sheria
Je! Ni kipi kinachoweza kumgeuza?
Ni Yesu Kristo tu. Yeye ndiye aliyetiwa mafuta, na Mungu kuwaokoa watu wa Mungu na kuwafungua. Amwaminiye na kudhamiria moyoni mwake kumfuata, basi atageuzwa moja kwa moja na kuwa mtu mwingine, huo ni uhakika.
Alisema.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Ni ahadi yake kuwa Ukimwamini jambo la kwanza ni kukusamehe dhambi zako, kwasababu ndio jambo lililomfanya aende msalabani kwa ajili yako miaka elfu mbili iliyopita,. Unakuwa huhesabiwi dhambi tena, unahesabiwa haki bure kwa neema yake. Lakini sambamba na hilo anakupa UWEZO wa kuwa kama yeye kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu atakayemwachia ndani yako, pindi tu unapoamini.
Na baada ya hapo utashangaa tu unavyoanza kubadilika moyoni mwako.
Zingatia tu toba ya kweli, pamoja na ubatizo sahihi (kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo). Na kumtii yeye.
Upumbavu utakutoka.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
SWALI: Nini maana ya Mithali 26:2
Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
JIBU: Mungu anafananisha laana isiyo na sababu na ndege wanaotanga-tanga angani.
Kama tunavyojua ndege hawa aina ya shomoro na mbayuwayu, kila siku tunawaona wanaruka angani, kila siku tunawaona wapo hari-hari, wanaonekana kama wapo buzy, lakini katika kazi zao zote, na juhudi zao zote, na mikakati yao yote, kamwe huwezi ona yanaleta madhara yoyote kwa mwanadamu. Hata kama utawaharibia viota vyao, hata kama watakauwa na hasira na wewe, huwezi ona wanamshambulia mwanadamu, kwasababu uwezo huo hawana. Huwezi wafikiria na kila wanapokuona wanakimbia. Wewe mwenyewe ukiwaona huwezi kuwaogopa, tofauti na ukimwona nyoka, utajidhatiti asikuume. Lakini ndege huvai ‘chapeo’ kichwani kujilinda naye asikuume, kwasababu hana madhara.
Ndivyo Mungu anavyotufundisha, laana zisizo na sababu, haziwezi kukupata ni kama ndege tu angani, zitapita, na kuendelea na shughuli zake, kamwe haziwezi kukupata ikiwa wewe ni mtakatifu, Hii ni kutufundisha kuwa hatupaswi kuwa waoga wa maneno ya watu (laana) ambayo hayana sababu.
Ukiona laana imekupata basi ujue kulikuwa na sababu nyuma yake, (lakini sio tu maneno matupu mtu anayoyatoa), mfano wa laana hizi ni ile ya Elisha aliyowalaani wale vijana 42, walioraruliwa na dubu. Kwasababu walimdhihaki. (2Wafalme 2:22-25)
Lakini mfano wa laana zisizo na sababu, ni ile Goliathi aliyomlaani Daudi kwa miungu yake, ambayo ilikuwa ni kazi bure..
1Samweli 17:42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake
Ni mfano mwingine ni ile Balaamu mchawi alivyojaribu kuwalaani Israeli ikashindakana, kwasababu huwezi laani vilivyobarikiwa. (Hesabu 23)
Hata leo, ikiwa wewe umeokoka, hupaswi kuogopa, maneno yoyote iwe ya waganga au wanadamu. Kwasababu wewe tayari ni mbarikiwa. Ni ajabu sana kuona mkristo, analia na kutetemeka, eti! Mchawi kamwambia mwaka huu hautaisha atakuwa watoto wake wote watakuwa wamekufa!!. Mzee wa mila kamwambia atapata ajali kwasababu hakutambika kijijini mwaka huu.
Mwingine anawaza, mzazi kamwambia hatafanikiwa kwasababu kaamua kuokoka. Haa! Unaogopa nini hapo?. Hizo ni laana zisizo na sababu. Ishi kwa amani zione tu kama ndege wa angani ambao hukai kuwafikiria kama watakushambulia siku moja.
Ukiokolewa na Kristo umebarikiwa, wewe sio wa kunenewa maneno ovyo ovyo tu, na yakatokea. Wewe ni uzao wa kifalme usiotetemeshwa, ngome imara isiyoangushwa. Mwamba mgumu usiogharikishwa. Yatambue mamlaka na nguvu ulizopewa ndani ya Kristo. Usiogope!
Elewa maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,
Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,
Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)
NUHU WA SASA.
Swali: Napenda kujua Daudi alikuwa na wake wangapi na je na sisi tunaruhusiwa kuwa na wake wengi?
Jibu: Mfalme Daudi alikuwa na wake nane (8), waliotajwa katika biblia, ambao ni..
Wake wengine aliokuwa nao hawakutajwa katika biblia, lakini alikuwa nao wengine wengi, pamoja na masuria (nyumba ndogo), aliowatwaa kutoka katika mji wake YERUSALEMU.
2Samweli 5:12 “Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli. 13 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. ”
2Samweli 5:12 “Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli.
13 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. ”
Lakini swali ni je!, kama Daudi alioa wake wengi, basi na sisi ni halali kuoa wake wengi?..
Jibu ni la!, ikiwa ni halali sisi kuoa wake wengi kwa kumwangalia Daudi, basi ni halali pia na sisi kuua kwasababu Daudi pia aliua!..lakini kama si halali kuua basi vile vile si halali kuoa wake wengi, kama Bwana wetu YESU KRISTO alivyotufundisha…
Mathayo 19:4 “Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”
Mathayo 19:4 “Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”
Hivyo ndoa ni ya mke mmoja na mume mmoja, kwa urefu Zaidi fungua hapa >>>JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
Vyemba ni nini kama tunavyosoma katika 2Samweli 18:14
JE! UNAWEZA KUWA NA GEUKO KAMA LA DAUDI?
Swali: Biblia inasema wakrete walikuwa ni waongo na walishuhudiwa na nabii wao, je walikuwaje waongo (walidanganya nini), na huyo nabii wao alikuwa nani?
Jibu: Wakrete ni jamii ya watu waliokuwa wanaishi mahali paitwapo “Krete” na Krete ni kisiwa kilichokuwepo katika nchi ya Ugiriki.
Sasa Mtume Paulo alimwandikia Tito waraka huu kumpa maagizo na maelekezo machache kuhusu kanisa na viongozi (katika uteuzi).. Kwa urefu kuhusiana na kitabu hiki cha Tito na maaelekezo Paulo aliyompa Tito kwa uongozo wa Roho Mtakatifu fungua hapa >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Lakini kwa ufupi ni kwamba tabia mojawapo waliyokuwanayo watu wa Krete, ni UONGO, Walikuwa wanasifa ya kusema Uongo katika viwango vikubwa, kiasi kwamba mpaka mtu wa kwao, ambaye ni nabii wao wenyewe aliandika kuhusiana na tabia hiyo waliyonayo waKrete ya Uongo, pamoja na ulafi na uvivu.
Biblia haijamtaja huyo Nabii ni nani, na wala haijaandika kuhusu huo waraka, lakini hapa tunaona Mtume Paulo ana unukuu…”
Tito 1:12 “..MTU WA KWAO, NABII WAO WENYEWE, AMESEMA, WAKRETE NI WAONGO SIKU ZOTE, HAYAWANI WABAYA, WALAFI WAVIVU”
Sasa tukirudi katika historia, alikuwepo mwana filosofia wa KRETE aliyeitwa “EPIMEDINES”.. Huyu alikuwa ni Nabii wa mungu wa kigiriki aliyeitwa “zeu”..ambaye anatajwa katika Matendo 14:12-13.
Huyu Epimedines pamojana na kuwa alikuwa ni nabii wa mungu huyo wa kigiriki, lakini pia alikuwa ni mwandika mashairi. Moja ya shairi lake aliloliandika (ambalo aliliandika kwa kumtukuza huyo mungu wao wa kigiriki aliyeitwa zeu) lilikuwa linasema hivi..
…“Walikutengenezea kaburi, takatifu, uliye juu (zeu), Wakrete, waongo siku zote, wanyama wabaya, wavivu wa tumbo. Lakini wewe hukufa: unaishi na unakaa milele. Kwa maana ndani yako tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu”…
Ni shari la kumtukuza mungu wao (zeu), lakini lilikuwa maarufu Krete kote kwani huyu Epimedines aliaminika na wakrete wote kuwa ni nabii. Na Paulo kwasababu ni msomaji, aliujua huu ushairi, na hivyo katika kusisitiza dhambi ya wakrete ya Uongo kuwa ni kweli, ndio ananukuu hayo maneno ya nabii wao aliyewashuhudia kuwa ni waongo.
Lengo la Mtume Paulo si kumthibitisha nabii wao huyo La!.. bali kuthibitisha Uongo wa wakrete ambao watu wote wanauona hata walio wa Imani ya mbali… Hivyo ndio anamwonya Tito aukemee huo!.
Tunachoweza kujifunza ni kuwa UONGO ni mbaya, kwani biblia inashuhudia kuwa ibilisi ndiye baba wa Uongo, hivyo wote wadanganyi wote ni watoto wa ibilisi.
Yohana 8:44 “ Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.
Bwana atusaidie tushinde dhambi.
Maran atha!
WANNE WALIO WAONGO.
Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
SWALI: Kwanini katika agano la kale Mungu aliwazua walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake? Ikiwa Mungu hana upendeleo kwanini aliliagiza hili litendeke?
Mambo ya Walawi 21:16-24
[16]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, [17]Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. [18]Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili, [19]au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono, [20]au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu; [21]mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. [22]Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu. [23]Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye. [24]Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.
[16]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
[17]Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
[18]Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,
[19]au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,
[20]au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;
[21]mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
[22]Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.
[23]Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.
[24]Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.
JIBU: Agano la kale lilikuwa ni taswira ya agano jipya (la rohoni) jinsi litakavyokuwa baadaye (Wakolosai 2:17).
lile lilikuwa ni agano la mwilini, hivyo mambo mengi yalipaswa yadhihirishwe kwanza ki-mwilini ili kufunua au kufundisha kwa urahisi mambo ya rohoni yatakayokuja baadaye, lakini kiuhalisia haikuwa mpango wa Mungu mkamilifu yachukiliwe vilevile kwa majira yote.
Kwamfano mtoto mdogo anapoanza kujifunza hesabu, huwezi kumwambia moja jumlisha na tatu ni nne. hatakuelewa. Bali utachukua kitu chenye umbo, (labda vijiti). utampa kimoja, kisha utachukua tena vijiti vingine vitatu utampa. halafu utamwambia avichanganye avihesabu atoe jumla. atavihesabu vyote..na hapo hapo anakuambia nimepata vinne.
Sasa yeye atadhani hesabu ni vijiti. Lakini anapokuwa mtu mzima anagundua alipewa tu maumbo ili aelewe vizuri. Lakini hesabu ni uelewa wa akilini sio vijiti.
Vivyo hivyo na sisi tulipoanza kuelezwa makusudi makamilifu ya Mungu, tulifananishwa na watoto (Wagalatia 4:1-6). Mungu hakutaka kumleta Kristo moja kwa moja afe, amwage damu yake, ndipo sisi tuondolewe dhambi zetu kwa hiyo damu. Ukweli ni kwamba tusingemwelewa Mungu, vema.
Hivyo alitanguliza agano la kale kwanza, la mwilini, la mambo ya nje. Tuelewe kitaswira jinsi ilivyo sawa na isivyo sawa. ndipo baadaye atumie mifano hiyo kueleza ya rohoni.
kwamfano walikatazwa kula nguruwe, sababu alikuwa hacheui, mnyama asiyecheua ni yule asiyeweza kurejesha chakula akakitafuna na kukimeza tena kama ng’ombe. Sasa lengo la Mungu sio kwasababu nguruwe alikuwa ana magonjwa. kiuhalisia nguruwe ni mboga nzuri tu, lakini ni kwasababu ya ile sifa, ya kutocheua, ambayo rohoni sisi tunafundishwa hatupaswi kuwa nayo. maana yake ukishindwa kutafakari, yale uliyotendewa na Mungu nyuma, au uliyofundishwa na Mungu, wewe ni sawa na kiumbe najisi, mfano wa nguruwe. kwasababu hutaweza kuwa mtu wa shukrani, hutaweza kuwa mtu wa imani. Wana wa Israeli walionyesha tabia hii, wakati wanavuka habari ya shamu. walimnung’unikia Mungu wakisema unatuua, kwasababu hawana chakula. hawakukumbuka miujiza mikubwa aliyowatendea kipindi kifupi nyuma. Lakini Daudi alipokutana na Goliati hakulia wala kuogopa alisema yule Bwana aliyeniokoa na dubu na simba ataniokoa na mfilisti huyu asiyetahiriwa. alicheua akala tena akapata nguvu ya kuendelea mbele, kumshinda adui. Hakutaka kuwa nguruwe.
sasa tukirudi pia katika mambo ya madhabahuni kufuatana na swali letu. Kumbuka waliopewa nafasi ya kuhudumu hekaluni walikuwa ni jamii ya makuhani tu, wazao wa Lawi. Mtu mwingine yeyote hakuruhusiwa. Vilevile hata yule mlawi ikiwa ni mlemavu wa aina yoyote pia hakuruhusiwa.
Kuonyesha kuwa hawakutengwa wao tu, hata watu wa kabila nyingine, haijalishi ni manabii au wanamtumikia Mungu kiasi gani ikiwa wewe si mlawi hukuruhusiwa hata na wanawake wote, hawakuwa tofauti na vilema katika suala la kuhudumu. Kwahiyo hawakutengwa walemavu tu. Bali na makundi mengine yote.
Sasa kwanini Mungu akataze walemavu na wenye madhaifu wasihudumu. Kwasababu Mungu alikuwa.anaonyesha picha ya rohoni ni jinsi gani watumishi wake, wahudumu.wa madhabahuni wanavyopaswa wawe, kwamba wasiwe watu wenye kasoro mbele zake. Yaani wawe watu wakamilifu sio walemavu rohoni.
Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Mungu, hakuwa na Neno lolote baya na walemavu. Wala hakuwachukia.
Na ndio maana tunapokuja agano jipya tunaona vipofu, viwete, mabubu wanamjia Mungu, anawaponya. Na isitoshe Yesu alikuwa anakwenda kukaa kwao na kula nao (Marko 14:3).
Mungu hashughulika na ulemavu wa mwilini, bali ule wa rohoni. Ambao ukiwa mdhaifu huko, wewe ni najisi mbele zake. pitia somo hili ufahamu zaidi juu ya ulemavu wa rohoni upoje.
>>> UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?
wapo walemavu wengi, ambao wengine Mungu mwenyewe ameruhusu wawe vile kwa ushuhuda wake, na wanamtumikia kwa namna isiyo ya kawaida na wanafanya miujiza mikubwa, wanaponya watu na kuwafungua, utauliza kwanini Mungu asiwaponye? mawazo ya Mungu si mawazo yetu, Elisha alikufa na ugonjwa wake, lakini mifupa yake ilifufua wafu.
fuatilia ushuhuda huu ukujenge…. >>> USHUHUDA WA RICKY:
Hii ni kutuonyesha kuwa, wakati wa sasa mbele za Mungu hakuna mwanamume, au mwanamke, au mlemavu au mtumwa wote ni makuhani wake na tumestahilishwa na Yesu Kristo kuingia patakatifu pa patakatifu kwa damu yake sisi tuliomwamini….
Haleluya. Upendo wake ni wa ajabu kwetu.
Shalom
Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?
CHAKULA CHA ROHONI.
Swali: Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu kwa mgonjwa aliye katika uhitaji huo, kwaajili ya kuokoa maisha yake?
Jibu: Biblia inasema maneno yafuatayo…
1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU. 17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”
1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU.
17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”
Maadamu mtu akiondolewa damu kiasi kidogo mwilini mwake, Hafi!!.. na vile vile mtu anayepokea damu mwilini mwake pia Hafi!, kinyume chake ndio anapata UZIMA! (wa mwilini).. basi ni wazi kuwa si dhambi kuchangia damu kwa mtu mwingine…..Zaidi sana ni jambo la upendo, ikiwa hakuna njia nyingine ya kumsaidia mhitaji huyo zaidi ya hiyo ya kumchangia damu.
Kwanini si dhambi!.. ni kwasababu hata sehemu ya damu tulizonazo tumepokea kutoka kwa wazazi wetu!…HAKUNA MTU ANAYEZALIWA DUNIANI NA DAMU YAKE MAALUM (Special), wote tunazipokea kutoka kwa wazazi wetu ndio maana zinamfanano na hao!, na zinamfanano na ndugu zetu tuliozaliwa nao familia moja.
Kwahiyo kumchangia damu mgonjwa si dhambi!… Maana utamchangia atapona!, na kwa njia hiyo yaweza kuwa sababu ya kumvuta kwa KRISTO, (akiona upendo wako namna hiyo).. lakini kama ukimnyima na akifa katika hali yake ya kutokuamini hakuna faida yoyote wewe unayoipata…
Kwahiyo ni afadhali utafute namna ya kuokoa roho kwa njia hiyo, kwasababu hakuna hasara yoyote unayopata katika mwili wako utoapo kiasi kidogo hiko cha damu na kumpatia mwingine!.. ni lita ngapi za damu umepoteza wakati wa mzunguko wako (wewe mwanamke) na bado unaendelea kuishi.
Ni lita ngapi za damu umepoteza wewe mwanaume ulipopata majeraha au ulipofyozwa na hao mbu kutandani mwako siku zote za maisha yako?.. Kwa kutafakari hayo yote hakuna sababu ya kumnyima damu ndugu yako, ikiwa kuna ulazima huo, na wala hakuna sehemu yoyote kwenye biblia iliyokataza kuchangia damu.
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
Swali: Tukisoma Mwanzo sura ya kwanza tunaona Mungu akimaliza kazi yote ya uumbaji kwa zile siku saba, lakini tukirudi kwenye Sura ya pili tuona ni kama tena Mungu anarudia uumbaji anamuumba mwanadamu, na pia mimea, je kulikuwa na uumbaji wa aina mbili ulitokea pale. Na ni nini tunajifunza pale?
JIBU: Jibu ni hapana, uumbaji wa Mungu ulikuwa ni ule ule mmoja, tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani. isipokuwa Sura ya kwanza Mungu anaeleza ‘kwa taswira ya ujumla’, lakini katika sura ya pili anaeleza jinsi ‘utaratibu wa uumbaji wake ulivyokuja kutokea’, mpaka kuileta hiyo picha ya ujumla.
Kwamfano katika Sura ya kwanza anasema Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume..
Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Lakini katika sura ya pili anaonyesha jinsi alivyoanza kumuumba kwa kumtoa ardhini mpaka alivyompulizia pumzi ya uhai, hadi utaratibu wake wa kutawala.
Mwanzo 2:4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi 5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; 6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. 7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. 8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Mwanzo 2:4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi
5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. 7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Umeona,? Vilevile ukisoma Mwanzo 1:11&12, utaona Mungu anaumba mimea yote . Lakini hapo kwenye sura ya pili anaonyesha jinsi mime hiyo inavyokuja kutokea, anaeleza kwanza inaanza katika mbegu, kisha inyeshewe mvua, ikue baadaye ndio iwe mche kamili wenye matunda.
Hivyo, Kulikuwa na umuhimu wa kuwekwa sura zote mbili, ili tuelewe kanuni za Mungu za utekelezaji wa mipango yake. Maana kama tungeishia tu sura ya kwanza tusingeelewa ni kwa namna gani mambo yanaendelea kama yalivyo leo.
Hata sasa Mungu anasema jambo. Lakini pia huna budi kuelewa mpango wake wa utekelezaji wa hilo jambo! Ili usiudhike, au usikate tamaa, au usijikwae, au usiwe na mashaka. Unatafakari ni kweli Mungu alimuumba mwanamke tangu awali, lakini kutokea kwake kulikuja baadaye sana, tena sio ardhini bali ubavuni mwa Adamu. Kama hilo tusingelifahamu, tusingeelewa kwanini tunaambiwa sisi wote ni mwili mmoja.
Kama tusingejua kuwa ili mti ufikie matunda, kama Mungu alivyoukusudia, ni lazima uanze kwanza kama mbegu, ioze ardhini, kisha ipate mvua, imee, itoke katika jani, hadi shina, hadi mti. Tungesema hii si sawa, kuna shida, mbegu kuoza ardhini, hakuna mmea hapo?.
Halikadhalika hata sasa Mungu amekuahidi pengine, atakupa jambo Fulani. Sasa usitarajie lije ghafla tu, pengine litapitia hatua Fulani, huwenda likaonekana kama limetoweka kabisa,kama vile mbegu inayooza ardhini, lakini mwishowe itakuja kutokea tu, kama tu Yusufu alivyoonyeshwa kuwa ndugu zake watamwinamia, Au Ibrahimu kuonyeshwa atakuwa baba wa mataifa mengi, lakini mapito yao unayajua, Yusufu kuuzwa utumwani, kutupwa gerezani, Ibrahimu kuwa tasa. Lakini mwisho utaona yale waliyoahidiwa yalikuja kutokea vilevile.
Tunapaswa tumwelewe sana Mungu ili tuwe na amani, Neno la Mungu linaposema, kwa kupigwa kwake sisi tumepona, amini kuwa umepona kwa kifo cha Yesu, hata kama utahisi maumivu mengi kiasi gani leo, daktari atakuambia huwezi kupona ugonjwa wako hautibiki. Wewe amini, tu hilo jambo litatokea, haijalishi litachukua wakati gani, utapitia mateso mengi kiasi gani leo, mwisho wa siku utakuwa tu mzima.
Usiishi tu na mwanzo sura ya kwanza, ishi pia na sura ya pili. Utamwelewa Mungu.
NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI
Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)
Ni maneno gani Bwana Yesu aliyokuwa anayaandika ardhini? (Yohana 8:7).