Swali: Biblia inataja siri za Mungu katika 1Wakorintho 4:1, je hizi siri ni zipi na zipo ngapi?
Jibu: Turejee,
1Wakorintho 4:1 “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu”
Awali ya yote tujue maana ya uwakili unaozungumziwa hapo?…. Uwakili unaozungumziwa hapo sio mfano wa ule wa “mahakamani” La! bali unamaanisha “Usimamizi”… Kibiblia mtu aliyepewa usimamizi wa nyumba au kazi Fulani, aliitwa “Wakili”..soma Luka 12:43-48 na Luka 16:1-13…
Hivyo hapo Mtume Paulo, aliposema “.. sisi ni mawakili wa siri za Mungu” maana yake “wameweka kuisimamia nyumba ya Mungu kwa kuzifundisha siri za Mungu”….Kwa urefu Zaidi kuhusu Uwakili katika biblia fungua hapa >>> Wakili ni nani kibiblia? Uwakili ni nini?
Sasa tukirudi katika swali letu, SIRI ZA MUNGU NI ZIPI na ZIPO NGAPI?
Jibu ni kwamba “SIRI ZA MUNGU” zimetajwa MBILI TU (2), katika biblia. Ambazo ni 1)YESU NI MUNGU. 2) MATAIFA NI WARITHI WA AHADI ZA MUNGU… Tutazame moja baada ya nyingine.
1.YESU NI MUNGU.
Wakolosai 2:2 “ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, WAPATE KUJUA KABISA SIRI YA MUNGU, YAANI, KRISTO; 3 ambaye ndani yake yeye HAZINA ZOTE ZA HEKIMA NA MAARIFA ZIMESITIRIKA”.
Wakolosai 2:2 “ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, WAPATE KUJUA KABISA SIRI YA MUNGU, YAANI, KRISTO;
3 ambaye ndani yake yeye HAZINA ZOTE ZA HEKIMA NA MAARIFA ZIMESITIRIKA”.
Kwanini au kivipi “KRISTO” ni “SIRI YA MUNGU”?.. Kwasababu ndani yake hazina zote na hekima na maarifa zimesitirika..maana yake yeye ndio kila kitu, NDIYE MUNGU MWENYEWE katika mwili wa kibinadamu!!!!..Kiasi kwamba laiti Pilato angelijua hilo, asingeruhusu hukumu ipite juu yake, laiti wale makuhani na maaskari wangelijua hilo wasingepitisha misubari katika mikono yake na miguu yake, lakini walifumbwa macho ili tupate wokovu.
1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu KATIKA SIRI, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 8 AMBAYO WENYE KUITAWALA DUNIA HII HAWAIJUI HATA MMOJA; MAANA KAMA WANGALIIJUA, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU”.
1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu KATIKA SIRI, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 AMBAYO WENYE KUITAWALA DUNIA HII HAWAIJUI HATA MMOJA; MAANA KAMA WANGALIIJUA, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU”.
Siri hii ya kwamba KRISTO NI MUNGU, inaanzia katika Isaya 9:6, na kisha Yohana 1:1, Yohana 14:9, Yohana 20:28, Tito 2:13, 1Timotheo 3:16 na Ufunuo 22:13-13.
Siri ya Bwana YESU Kuwa MUNGU, inajulikana pia kama “Siri ya Utauwa/Uungu” ambayo Mtume Paulo aliitaja katika 1Timotheo 3:16..
1Timotheo 3:16 “Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.
Kwahiyo BWANA YESU KRISTO ni MUNGU ALIYEDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, na wote tunaomwamini tunapaswa tuwe mawakili wa SIRI HIYO, Maana yake “KUIAMINI na KUIHUBIRI KWA WENGINE, wasiofahamu” .
2. MATAIFA NI WARITHI WA AHADI ZA MUNGU.
Hii ni Siri ya pili (2) ambayo ilifichwa kwa vizazi vingi, lakini ikaja kufunuliwa baada ya KRISTO kupaa juu mbinguni.. Tangu wakati wa Musa mpaka wakati wa Yohana, manabii wote na wayahudi wote walikuwa wanajua na kuamini kuwa “hakuna namna yoyote, wala njia yoyote” itakayofanyika kwa watu wa mataifa wakubaliwe na MUNGU.
Wote walijua Taifa Teule la Mungu ni ISRAELI peke yake, na mataifa mengine yote ni watu najisi, lakini baada ya Bwana YESU kuondoka alianza kumfunulia Petro siri hiyo kuwa hata mataifa ni warithi sawa tu na wayahudi, kupitia msalaba wake (Bwana YESU).. Na alimfunulia siri hiyo wakati ule alipokwenda nyumbani kwa Kornelio aliyekuwa mtu wa mataifa (Matendo 10)..
Na baadaye Bwana YESU akaja kumfunulia Mtume Paulo siri hiyohiyo kuwa Mataifa nao ni warithi, tena wa ahadi moja na wayahudi, hivyo wanastahili injili, na kuhubiriwa habari njema..
Waefeso 3:5 “Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 6 YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, NA WA MWILI MMOJA, NA WASHIRIKI PAMOJA NASI WA AHADI YAKE ILIYO KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI; 7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake”.
Waefeso 3:5 “Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, NA WA MWILI MMOJA, NA WASHIRIKI PAMOJA NASI WA AHADI YAKE ILIYO KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI;
7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake”.
Na sisi lazima tuwe wahudumu (Mawakili) wa siri hii kwamba “Wokovu ni haki ya watu wote” na Mungu anawapokea watu wote, ikiwa tu watakubali kutii na kunyenyekea mbele zake.
Kwahiyo kwa hitimisho, ni kwamba “Siri za Mungu” Si zile siri za kanisa, au zile za watumishi, au wapendwa kanisani…La! Bali ni hizo zilizotajwa hapo katika maandiko…Na kumbuka, shetani naye ana siri yake ijulikanayo kama “Siri ya Kuasi” iliyotajwa katika biblia ambayo inafanya kazi kwa kasi sana nyakati hizi…
Je umempokea YESU?..Kumbuka kipindi tulichopo ni cha Neema, lakini hii neema haitadumu milele, itafika wakati itaisha.. baada ya unyakuo hakuna neema tena, vile vile baada ya kifo hakuna Neema tena. Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwa Bwana YESU maadamu unaishi, baada ya kifo hakuna nafasi ya pili.
Warumi 10:8 “Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. 9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. 11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika 12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; 13 KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA”
Warumi 10:8 “Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika
12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
13 KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).
SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.
UFUNUO: Mlango wa 10.
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Rudi Nyumbani
Print this post
Heshima ni kitendo cha kumpa mtu hadhi yake, au uthamani wake anaostahili. Kwa kawaida kila mwanadamu anastahili heshima. Na hivyo kama mwamini huna budi kujua jinsi ya kuigawanya heshima kulingana na mtu husika. Kwasababu ukosefu wa heshimu, kwanza ni zao la kiburi (Mithali 15:33), lakini pia hukuondolea Baraka na kibali popote pale uendapo. Lakini pia ukitoa heshima isiyompa mtu ni kosa pia.
Warumi 13:7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima
Kutii maelekezo yao.
Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
Kutowakwaza,
Waefeso 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Kutenda agizo lao.
Warumi 13:1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu
Kuwatumikia kwa uaminifu na adabu. (Waefeso 6:5-8)
Hivyo kwa hitimisho, ni kwamba kila mwanadamu anastahili heshima, haijalishi, tajiri, au maskini, mrefu au mfupi, mgonjwa au mzima, mwenye elimu au asiye na elimu, bwana au mtumwa, ameokoka au hajaokoka. Wote ni agizo tuheshimiane.
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!
JIWE LILILO HAI.
Swali: Tumekuwa tukisikia na kuona watu wakisema “Tunalibariki jina la Mungu” na wengine wanasema “tunambariki Mungu”.. Je mtu anaweza kubariki Mungu au jina lake?..au ni Mungu ndiye anayeweza kumbariki mtu na kulibariki jina la mtu?
Jibu: Mungu anaweza kulibariki jina la mtu na vile vile mtu anaweza kulibariki jina la MUNGU. Isipokuwa tafsiri ya neno “baraka” ndiyo inayoleta ukinzani kwetu!.
Neno “Baraka” maana yake ni “kukiongezea kitu au mtu thamani, au heshima au fursa” ambacho hakikuwa nacho au hakuwa nayo!… Na thamani hiyo/heshima hiyo inaweza kuwa ni zawadi, au nafasi, au hadhi.
Mtu anapompa mwingine zawadi, tafsiri yake ni kwamba “amembariki mtu yule” vile vile mtu anapompa mtu mwingine heshima ya juu au fursa ya juu “maana yake amembariki mtu yule”.
Vile vile na sisi Mungu anaweza kutupa fursa, au heshima au zawadi ya jambo Fulani tulitendalo..Na sisi pia tunaweza kumpa heshima Mungu wetu, au fursa au zawadi kwa jambo Fulani atutendealo,…sasa kitendo hicho cha kumheshimu Mungu kwa kumpa kitu Fulani, ndicho kinachoitwa KUMBARIKI BWANA.
Na zawadi kubwa ambayo tunaweza kumpa MUNGU ikawa ni Baraka kwake ni Maisha yetu, pamoja na SIFA za midomo yetu.
Pengine utauliza ni wapi katika maandiko watu walimbariki Bwana…
2Nyakati 20:25 “Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana. 26 Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la baraka; MAANA NDIPO WALIPOMBARIKIA BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo”.
2Nyakati 20:25 “Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
26 Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la baraka; MAANA NDIPO WALIPOMBARIKIA BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo”.
Umeona hapo mstari wa 26, biblia inasema “MAANA NDIPO WALIPOMBARIKIA BWANA”..Na walimbaki kwa njia gani??… si nyingine Zaidi ya SIFA…
2Nyakati 20:18 “Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.
19 Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, KWA SAUTI KUU SANA”.
Na pia katika Zaburi ya 63 tunazidi kulithibitisha hilo…
Zaburi 63:3 “Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. 4 NDIVYO NITAKAVYOKUBARIKI MAADAMU NI HAI; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.”
Zaburi 63:3 “Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.
4 NDIVYO NITAKAVYOKUBARIKI MAADAMU NI HAI; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.”
Kwahiyo SIFA, tuimbazo ikiwa tunaziimba katika roho na kweli basi zinalibariki jina lake..utalisoma hilo Zaidi katika Zaburi ile ya 96 na Ayubu 1:21.
Zaburi 96:1 “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote. 2 Mwimbieni Bwana, LIBARIKINI JINA LAKE, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku”.
Zaburi 96:1 “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.
2 Mwimbieni Bwana, LIBARIKINI JINA LAKE, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku”.
Ila kumbuka jambo moja!.. Wewe au Mimi tusipolibariki jina la Mungu kwa kumpa yeye utukufu kwa vinywa vyetu au maisha yetu.. hatumpunguzii chochote, kwani anao mabilioni ya Malaika mbinguni wanaomsifu… Zaidi sana ni kwa hasara yetu wenyewe!!.. YEYE DAIMA ATABAKI KUWA MUNGU, NA WA KUABUDIWA, NA KUPEWA UTUKUFU HATA PASIPO SISI!!.
2Timotheo 2:12 “Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; 13 KAMA SISI HATUAMINI, YEYE HUDUMU WA KUAMINIWA. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”.
2Timotheo 2:12 “Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;
13 KAMA SISI HATUAMINI, YEYE HUDUMU WA KUAMINIWA. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”.
Bwana atubariki.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
JINA LAKO NI LA NANI?
Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?
Je shetani anaweza kushusha moto kutoka mbinguni?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Swali: Je, Mtume Paulo alimaanisha Nini kusema Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno Bali katika nguvu?.
Jibu: Turejee mstari huo..
1 Wakorintho 4:20 “Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu”.
Hapo anaposema kuwa Ufalme wa Mungu hauwi katika “neno” hamaanishi “Neno la Mungu”...kwasababu Ufalme wa Mbinguni unajengwa na NENO LA MUNGU kama nguzo ya msingi…na pasipo hilo hakuna ufalme wa Mungu…kinyume chake ni ufalme wa giza unajengwa.
Hivyo biblia inaposema ufalme wa Mungu hauwi katika neno, inamaanisha kuwa hauwi katika “MANENO MATUPU YASIYO NA NGUVU ZA MUNGU”...Bali unakuwa katika maneno yenye nguvu za Mungu.
Maana yake ishara na miujiza inafuatana na Neno la Ufalme…
Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alizidi kuliweka hilo vizuri katika 1Wathesalonike 1:5.
1 Wathesalonike 1:5 “ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika MANENO TU, bali na KATIKA NGUVU, na KATIKA ROHO MTAKATIFU, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu”.
Vile vile na sisi tunapaswa tuhubiri injili isiyo ya maneno matupu au yenye ushawishi wa maneno ili kuvuta watu… bali yenye dalili na udhihirisho wa Roho.
Maana yake ishara na miujiza vifuatane nasi…Na muujiza wa kwanza ni watu kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha…
1 Wakorintho 2:4 “Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu”.
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Elewa maana ya mstari huu;
Mithali 10:12 Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
Mstari huu unalenga kutufundisha sifa za kipekee sana za upendo. Ambazo zinazungumziwa pia sehemu mbalimbali.
Kwamfano hapo anasema kuchukiana hakuzai kingine zaidi ya fitina,( yaani uchongezi, na kudhuriana), lakini upendano husitiri MAKOSA YOTE. Anaposema yote. Ni kweli yote. Endapo upendo utatoka kwelikweli katika kilele chake. Hiyo ndio sifa ya ajabu ya upendo ambayo kitu kingine chochote chema hakiwezi kutoa, kwamfano imani, nguvu, mamlaka, uweza n.k. haviwezi kusitiri “makosa yote”. Ni upendo tu peke yake.
Neno hilo hilo pia limerudiwa katika agano jipya.
1Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi
Ndio maana Bwana Yesu alisema Torati yote imelalia hapo, katika kumpenda mwenzako kama nafsi yako, alisema vile unavyotaka wewe utendewe watendee wenzako. Utashangaa tu, wivu unayeyuka wenyewe, hasira inakufa, vinyongo vinaondoka, mashindano yanapotea, wizi, uzinzi unafutika, kwasababu umegundua kuwa mwenzako ni kama hiyo nafsi yako mwenyewe, kama vile wewe unavyopenda kufanikiwa vivyo hivyo usichukie kuona mwenzako amefanikiwa.
Lakini Jambo hili linaweza kutoka ndani yetu kwa njia tatu. Ya kwanza ni kujazwa Roho Mtakatifu. Kwasababu tunda mojawapo la Roho Mtakatifu ni upendo (Wagalatia 5:22). Hivyo unapokuwa mwombaji sana, hususani wa “masaa” sio dakika, unajazwa Roho Mtakatifu vema. Na matokeo yake ni kuwa urahisi wa kuudhihirisha upendo unakuja.
Lakini hilo peke yake halitoshi, unapaswa uambatanishe na usomaji wa Neno kila siku. Neno ni njia nyingine ya Roho Mtakatifu kukukumbusha, yale unayopaswa kufanya, kwamfano ukidhihirisha hasira ukisoma Neno utajifunza uvumilivu, utajifunza unyenyekevu, kuachia, na madhara ya kutokusamehe. Hivyo litakufanya uweze kurejea kwenye mstari haraka pale unapokaribia kuteleza. Usipuuzie kusoma Neno kila siku.
Tatu, ni kutendea kazi. Lazima ujiwekee malengo. Kwasababu ukiwa mwombaji tu, na msomaji peke yake bado haitakusaidia sana , kama huna mikakati ya kukifanyia kazi. Ndio maana hapo anasema iweni na JUHUDI nyingi katika kupendana,.Juhudi ni lazima yaani unaanza kuchukua hatua ya kushindana na vipinga-upendo, na hapo hapo utaanza kuona, wepesi umekuja ndani yako,
Sisi kama watoto wa Mungu, tumeagizwa tukue kila siku kuufikia upendo wa ki-Mungu ndani yetu. Ndio ukomavu wetu na kilele cha imani yetu. Kwasababu hii ndio dawa ya dhambi zote.(2Petro 1:5-11)
Bwana atuongezee neema.
Shalom.
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Malaika watakatifu waliopo mbinguni, wanaompa Mungu utukufu usiku na mchana, ni WAALIMU wazuri wa SIFA, na KWAYA kwetu!.. Hao wamewekwa ili kutufundisha sisi namna ya kumwimbia Mungu katika viwango vya kimbinguni. Huenda wasitufundishe namna ya kuhubiri, lakini katika kusifa, wanayo mafunzo kwaajili yetu.
> FUNZO LA KWANZA: Wanajisitiri!.
Malaika wa Sifa, (yaani Maserafi na Makerubi) sehemu kubwa ya mbawa walizopewa wanazitumia kujisitiri.. na wanajisitiri kuanzia kichwani mpaka miguuni…wanaposimama mbele za MUNGU KUMPA UTUKUFU..
Isaya 6:1“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. 2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; KWA MAWILI ALIFUNIKA USO WAKE, NA KWA MAWILI ALIFUNIKA MIGUU YAKE, NA KWA MAWILI ALIRUKA”
Isaya 6:1“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; KWA MAWILI ALIFUNIKA USO WAKE, NA KWA MAWILI ALIFUNIKA MIGUU YAKE, NA KWA MAWILI ALIRUKA”
Ikimaanisha kuwa kabla ya kupeleka sifa mbele za MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi, kigezo cha kwanza ni KUJISITIRI!!. Lakini leo hii watu watasimama mbele za MUNGU kumwabudu na kumsifu, vifua vikiwa wazi, mgongo ukiwa wazi, mapaja yakiwa wazi, mauongo yakiwa wazi..na wanawake vichwa vikiwa wazi..
Swali la kujiuliza je ni nani amewafundisha hayo????.. kuabudu, na kusifu wakiwa nusu uchi, je wamefundishwa na nani?..na Malaika watakatifu wanaomwimbia Mungu au nani?..jibu rahisi ni kwamba wamefundishwa na shetani, na wanayempa sifa si MUNGU wa Mbinguni bali ni shetani wa duniani na kuzimu!.
> FUNZO LA PILI: Wanahubiri utakatifu.
Malaika wa Sifa mbinguni, (Maserafi na Makerubi) wanaonekana “wakiitana” (maana yake wakiambiana) Mtakatifu…Mtakatifu… Mtakatifu…
Na zingatia hili: si kwamba walikuwa wanamwambia Mungu, kwamba ni Mtakatifu!!.. la! Walikuwa wanaambiana wao!.. maana yake wanakumbushana wao kwa wao!, wanajitangazia na kuwatangazia wengine kuwa Bwana ni mtakatifu, hivyo “kila mmoja adumu katika huo utakatifu”..kwasababu Mungu ni mtakatifu na hakai katika uchafu..
Ufunuo 6:3 “Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”.
Huo ndio wimbo wa MALAIKA mbinguni usiku na mchana!!… UTAKATIFU, UTAKATIFU, UTAKATIFU…
Na ndizo zinazopasa kuwa NYIMBO za watakatifu waliopo duniani… Sio kumwambia Mungu MTAKATIFU!!, Kana kwamba tunampa taarifa asiyoijua!!… yeye tayari ni mtakatifu na atabaki kuwa hivyo daima… bali tunapaswa tujikumbushe na kujitangazia sisi kuwa MUNGU NI MTAKATIFU, NA HIVYO TUZIDI KUJITAKASA… SIFA ZA NAMNA HIYO NDIZO ZINAZOMPENDEZA MUNGU!!..
Na sio mtu unaimba huku una mambo mengine ya kando kando!!.. sio unaimba huku unaishi na mke/mume ambaye si wako, sio unaabudu na kuimba kwaya huku ni mzinzi na mwabudu sanamu na unafanya mambo mengine yaliyo machukizo.
Neno la Mungu linasema pasipo huo utakatifu, hakuna mtu atakayemwona MUNGU…
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Nyimbo au Mahubiri yasiyohubiri utakatifu ni “Ngojera za ibilisi:”.. zinazotoa thawabu za kishetani, haihitaji kuwa mchawi ndio uwe wa shetani… kumwimbia tu ibilisi tayari wewe ni wake!..kuhubiri huku unasifia na kuzitenda dhambi wewe ni wa shetani.
Kama una karama ya uimbaji acha usanii, kazi ya MUNGU lebo!!, si brand! Ni huduma..kwahiyo usijitengeneze na kuwa mfano wa wasanii wa kidunia ambao wamepewa lebo na brandy na shetani ili wafanye mapenzi yake. (Hao wanahitaji kusaidiwa waokoke, na sio kuigwa).
Ukiamua kumwimbia MTAKATIFU aliye juu, VAA NGUO KAMILI!!!, HUBIRI UTAKATIFU, ISHI UTAKATIFU..
BWANA ATUSAIDIE!
NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)
MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.
UTUKUFU WA MUNGU NI KITU GANI?
Jibu: Turejee..
Yohana 12:3 “Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya NARDO SAFI yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu. 4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, 5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa DINARI MIA TATU, wakapewa maskini”
Yohana 12:3 “Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya NARDO SAFI yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,
5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa DINARI MIA TATU, wakapewa maskini”
“Nardo” ni jamii ya mmea mdogo ujulikanao kama “Nardostachys”. Mmea huu hutoa maua madogo ya rangi ya “Pinki” (Tazama picha juu), na vijimatunda vidogo vyeusi ambavyo ndivyo chanzo cha mafuta aina ya “Nardo” yanayotumika kutengenezea madawa ya asili pamoja na marhamu (yaani Perfumes/pafyumu) iliyo ya gharama kubwa kuliko nyingine nyingi.
Pafyumu iliyotengenezwa kwa “Nardo”, ilikuwa ni ya gharama kubwa na hata sasa ni ya gharama kubwa kutokana na upatikanani wa mimea hiyo.
Mimea ya Nardostachy, inapatikana katika safu za milima ya Himalaya, iliyopo nchini Nepali, na sehemu chache za “nchi ya India” pamoja na “Uchina”. Na inamea kuanzia kwenye kimo cha Mita 3,000 mpaka mita 5,000 kutoka katika usawa wa bahari (Mita 5,000 ni karibia na kimo cha Mlima Kilimanjaro).. Hivyo upatikanaji wake ni mgumu sana, kutokana na sehemu chache unazomea na kimo unapopatikana!.
Kutokana na sababu hizo, ndizo zinazoifanya Marhamu ya Nardo kuwa ya gharama. Mpaka hapo tutakuwa tumeshafahamu kuwa ile Marhamu yule mwanamke aliyompaka Bwana iliagizwa kutoka mbali sana (maana yake nje ya Israeli) na ilikuwa ya gharama sana… Dinari 300 ni sawa na shilingi Milioni 6 za kitanzania.
Mistari mingine inayozungumzia Marhamu ya Nardo ni pamoja na Wimbo ulio bora 1:12, na 4:13-14
Sasa kufahamu kwa urefu ni nini tunajifunza kupitia tukio la mwanamke yule kukivunja kile kibweta fungua hapa >>AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.
AKAZIDI KUENDELEA KATIKA HEKIMA NA KIMO.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.
Wimbo 2:9 “Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani”.
“Kimiami” ni dirisha kubwa lililo katika “ghorofa”..
Madirisha makubwa yaliyo katika maghorofa tofauti na yale yaliyo katika nyumba za chini ndiyo yaliyoitwa “kimiami”.
Mfano wa dirisha la Kimiami ni lile ambalo mfalme Ahazia aliloanguka na kuugua..
2Wafalme 1:2 “Na Ahazia AKAANGUKA KATIKA DIRISHA la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu”.
Na lile ambalo Yezebeli alianguka, baada ya kuangushwa na wale matowashi..
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani. 31 Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako? 32 AKAINUA USO WAKE KULIELEKEA DIRISHA, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia. 33 Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga”.
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
31 Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako? 32 AKAINUA USO WAKE KULIELEKEA DIRISHA, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia.
33 Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga”.
Tazama pia shubaka hapa >>>Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
TOA HUDUMA ILIYO BORA.
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
MUNGU HAJARIBIWI NA MAOVU BALI MEMA.
Swali: Je ni kwamba Mungu anafurahia Mauti ya watu wake mpaka aseme hivyo?
Jibu: Turejee mstari huo…
Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”
Sasa ili tupate vizuri maana ya huu mstari hebu tuweke msingi kwa kusoma tena mstari ufuatao…
Ezekieli 33:11 “Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, SIKUFURAHII KUFA KWAKE MTU MWOVU; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?”
Kama Bwana hakufurahii kufa kwake MTU MWOVU, basi kinyume chake ni kweli!! kuwa “KUFA KWAKE MTU MWENYE HAKI ikiwa amemaliza kusudi lake duniani NI JAMBO LINALOMPENDEZA MUNGU”… Na Ndio hapo kwenye Zaburi 116:15 anasema “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”.
Sasa kwanini MAUTI YA WENYE HAKI NI YA THAMANI MACHONI PA MUNGU?
1. DUNIANI NI MAHALI PA DHIKI.
Hii ndio sababu KUU..Duniani si mahali pa raha kwa “Wanaomcha Mungu”.. Kwa wengine wasiomcha Mungu panaweza kuwa mahali pao kwa raha ya kitambo..lakini kwa wacha Mungu si sehemu ya faraja hata kidogo..
Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. ULIMWENGUNI MNAYO DHIKI; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.
Kutokana na kwamba ulimwenguni ni mahali pa dhiki, na tena pa mapito, ni mahali pa kutaabika kupambana na dhambi na kutaabika kuhubiri injili.. hivyo MAUTI ni sehemu ya mapumziko kwa wanaomcha Mungu kutokana na taabu hizo za ulimwengu…ndivyo maandiko yanavyosema..
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA TANGU SASA. NAAM, ASEMA ROHO, WAPATE KUPUMZIKA BAADA YA TAABU ZAO; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Hiyo ndiyo sababu kwanini KIFO ni sehemu bora kwa WANAOMCHA MUNGU KULIKO KUENDELEA KUSHI DUNIANI. Na Mkristo yeyote yule wa kweli, ni lazima atamani kuondoka katika haya maisha kuliko kuendelea kubaki hapa!!, ni lazima atamani kila siku ile siku ya unyakuo ifike, au siku ya kulala kwake (kufa) ifike akamwone Bwana.
Kitu pekee ambacho kinapaswa kutufanya tuendelee kutaka kubaki duniani ni “kuimaliza kazi yake”, (maana yake tusiondoke kabla ya kuimaliza kazi yake aliyotuitia, kwani kuna hatari ya kufa bila kuifanya kazi yake au kuimaliza).. na hakuna sababu nyingine tofauti na hiyo…
Ukiona unatamani uendelee kubaki duniani, ili uwe milionea, au ili uendeshe na kumiliki magari, au utengeneze majumba kwa fahari yako, kuna shida katika Imani yako!..(Ni muhimu kujipambanua upya).. wewe utakuwa wenyeji wako ni hapa duniani, sio mbinguni.
Walio wa mbinguni wanatamani ya mbinguni, na walio waduniani wanatamani, na kuwekeza, na kusifia vya duniani…
Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”
Soma pia 1 Petro 2:11 utaona jambo hilo, hivyo jihakiki ni nini kinakupa sababu ya wewe kuendelea kubaki hapa duniani?..ni vitu vya dunia hii au vile vijavyo?.
Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho aliandikia kuwa “kuishi kwake ni Kristo na kufa ni faida”,..Maana yake kusudi lake kuu la kuendelea kubaki duniani ni Kristo (yaani kufanya kazi Kristo aliyomuitia na kuimaliza)..Nje na hapo kufa ni FAIDA KUU!
Wafilipi 1:21 “Kwa maana kwangu mimi kuishi ni KRISTO, NA KUFA NI FAIDA. 22 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. 23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; 24 bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu”.
Wafilipi 1:21 “Kwa maana kwangu mimi kuishi ni KRISTO, NA KUFA NI FAIDA.
22 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui.
23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;
24 bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu”.
Hapo anasema kudumu katika mwili (yaani kuendelea kuishi) kwahitajika kwaajili yao, na si kwaajili yake (maana yake kwaajili ya kuwahubiria wao injili).
Je mimi na wewe kubaki kwetu katika mwili kwahitajika kwaajili ya nini??…je ni kwaajili ya matumbo yetu, na tamaa, na anasa au kwaajili ya Bwana?..
Kumbuka pia, ni hasara kubwa sana kufa katika dhambi!.. na hakuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kutoka katika mateso ya moto wa jehanamu na kumingiza paradiso. (Hayo maombi hayapo usidanganyike).
Hakuna maombi yoyote ya Mchungaji, au Askofu, au Nabii, au Mtume, au Papa, au Padre, au Kadinali, au Mwalimu, au Rabi, au Mwinjilisti, au Kuhani au Malaika wa mbinguni…. yatakayomtoa mtu kwenye mateso ya moto wa jehanamu na kumwamisha kumwingiza peponi, Mtu akifa katika dhambi!, habari yake ndio imeishia hapo..
Bwana YESU Kwa kinywa chake mwenyewe ametupa tahadhari hiyo katika kitabu cha Yohana..
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU”.
USIFE NA DHAMBI ZAKO!
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU
Mistari ya biblia kuhusu kibali.
Amosi 5:23 “Niondoleeni KELELE ZA NYIMBO ZENU; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.
Je ni kwamba Mungu wetu hapendezwi na nyimbo tunazomwimbia??
Jibu ni la! Yeye anapendezwa na nyimbo na tena anaketi katika SIFA.
Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli”.
Lakini kwanini aseme “niondoleeni kelele za nyimbo zenu?”… Ni wazi kuwa kuna nyimbo ambazo kwa Mungu ni kama kelele.
Sasa ni aina gani za nyimbo ambazo kwa Mungu ni kelele?.
1. NYIMBO ZA UNAFIKI.
Nyimbo za kinafiki ni zile mtu anazoimba kwa kupaza sauti, lakini maisha yake hayaendani na kile anachokiimba, kuanzia, uzungumzaji, uvaaji, utendaji na maisha yake yake siri. Mtu mwenye tabia hiyo halafu akasimama na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu, iwe ni nyimbo alizozitunga yeye, au za mwingine, mtu huyo anapiga kelele mbele za Mungu na hivyo anafanya dhambi.
2. NYIMBO ZENYE MIDUNDO YA KIDUNIA.
Kuna nyimbo ambazo zinafanana sana na za kidunia, kiasi kwamba mtu akisikiliza anafananisha na nyimbo Fulani ya kidunia ambayo alishawahi kuisikia mahali fulani. Nyimbo za namna hiyo ni kelele, na si kelele tu, bali pia ni machukizo… mfano wa hizo ni nyimbo aina ya rege, rap, pop, taarabu na nyingine zinazofanana na hizo, Nyimbo za namna hii zinajulikana kama nyimbo za upuuzi (Amosi 6:5). Hivyo wakristo hatupaswi kutumia midundo hiyo kumwimbia MUNGU.
3. NYIMBO ZINAZOSHIRIKISHA WASANII WA KIDUNIA.
Wasanii wa kidunia ni watu wanaoimba nyimbo za zinazotukuza na kusifia mambo ya ulimwengu huu, na ulimwengu upo chini ya shetani, sasa mtu anayewashirikisha waimbaji hao wa kidunia, waliozoea kumwimbia shetani, kisha wakapewa mashairi ya kumsifu Mungu pamoja na watu wa kiMungu, hizo ni kelele na machukizo mbele za Mungu, haijalishi nyimbo hiyo itakuwa na beti nzuri kiasi gani na ujumbe mzuri kiasi gani, au zenye kumsifia MUNGU kwa kiasi gani, bado ni kelele mbele za Mungu na hazina matunda yoyote.
Nyimbo zenye kumtukuza Mungu ni zile zilizobeba ushuhuda wa Neno kuanzia kwa MWIMBAJI, beti na mdundo. Na zinapoimbwa zinamtukuza Mungu na kuwabariki wasikiao.
MAONO YA NABII AMOSI.
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
Fahamu maana 1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu msiwe watoto katika akili zenu;
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.