Je! mtu anaweza kumbariki Mungu au kulibariki jina lake?

Je! mtu anaweza kumbariki Mungu au kulibariki jina lake?

Swali: Tumekuwa tukisikia na kuona watu wakisema “Tunalibariki jina la Mungu” na wengine wanasema “tunambariki Mungu”.. Je mtu anaweza kubariki Mungu au jina lake?..au ni Mungu ndiye anayeweza kumbariki mtu na kulibariki jina la mtu?


Jibu: Mungu anaweza kulibariki jina la mtu na vile vile mtu anaweza kulibariki jina la MUNGU. Isipokuwa tafsiri ya neno “baraka” ndiyo inayoleta ukinzani kwetu!.

Neno “Baraka” maana yake ni “kukiongezea kitu au mtu thamani, au heshima au fursa” ambacho hakikuwa nacho au hakuwa nayo!… Na thamani hiyo/heshima hiyo inaweza kuwa ni zawadi, au nafasi, au hadhi.

Mtu anapompa mwingine zawadi, tafsiri yake ni kwamba “amembariki mtu yule” vile vile mtu anapompa mtu mwingine heshima ya juu au fursa ya juu “maana yake amembariki mtu yule”.

Vile vile na sisi Mungu anaweza kutupa fursa, au heshima au zawadi ya jambo Fulani tulitendalo..Na sisi pia tunaweza kumpa heshima Mungu wetu, au fursa au zawadi kwa jambo Fulani atutendealo,…sasa kitendo hicho cha kumheshimu Mungu kwa kumpa kitu Fulani, ndicho kinachoitwa KUMBARIKI BWANA.

Na zawadi kubwa ambayo tunaweza kumpa MUNGU ikawa ni Baraka kwake ni Maisha yetu, pamoja na SIFA za midomo yetu.

Pengine utauliza ni wapi katika maandiko watu walimbariki Bwana…

2Nyakati 20:25 “Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.

26 Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la baraka; MAANA NDIPO WALIPOMBARIKIA BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo”.

Umeona hapo mstari wa 26, biblia inasema “MAANA NDIPO WALIPOMBARIKIA BWANA”..Na walimbaki kwa njia gani??… si nyingine Zaidi ya SIFA…

2Nyakati 20:18 “Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.

19 Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, KWA SAUTI KUU SANA”.

Na pia katika Zaburi ya 63 tunazidi kulithibitisha hilo…

Zaburi 63:3 “Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.

4 NDIVYO NITAKAVYOKUBARIKI MAADAMU NI HAI; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.”

Kwahiyo SIFA, tuimbazo ikiwa tunaziimba katika roho na kweli basi zinalibariki jina lake..utalisoma hilo Zaidi katika Zaburi ile  ya 96 na Ayubu 1:21.

Zaburi 96:1 “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.

2 Mwimbieni Bwana, LIBARIKINI JINA LAKE, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku”.

Ila kumbuka jambo moja!.. Wewe au Mimi tusipolibariki jina la Mungu kwa kumpa yeye utukufu kwa vinywa vyetu au maisha yetu.. hatumpunguzii chochote, kwani anao mabilioni ya Malaika mbinguni wanaomsifu… Zaidi sana ni kwa hasara yetu wenyewe!!.. YEYE DAIMA ATABAKI KUWA MUNGU, NA WA KUABUDIWA, NA KUPEWA UTUKUFU  HATA PASIPO SISI!!.

2Timotheo 2:12 “Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;

13  KAMA SISI HATUAMINI, YEYE HUDUMU WA KUAMINIWA. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”.

Bwana atubariki.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINA LAKO NI LA NANI?

Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?

Je shetani anaweza kushusha moto kutoka mbinguni?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments