Nini maana ya ufalme wa Mungu hauwi katika neno bali katika nguvu?(1Wakorintho 4:20).

Nini maana ya ufalme wa Mungu hauwi katika neno bali katika nguvu?(1Wakorintho 4:20).

Swali: Je, Mtume Paulo alimaanisha Nini kusema Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno Bali katika nguvu?.


Jibu: Turejee mstari huo..

1 Wakorintho 4:20 “Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu”.

Hapo anaposema kuwa Ufalme wa Mungu hauwi katika “neno” hamaanishi “Neno la Mungu”...kwasababu Ufalme wa Mbinguni unajengwa na NENO LA MUNGU kama nguzo ya msingi…na pasipo hilo hakuna ufalme wa Mungu…kinyume chake ni ufalme wa giza unajengwa.

Hivyo biblia inaposema ufalme wa Mungu hauwi katika neno, inamaanisha kuwa hauwi katika “MANENO MATUPU YASIYO NA NGUVU ZA MUNGU”...Bali unakuwa katika maneno yenye nguvu za Mungu.

Maana yake ishara na miujiza inafuatana na Neno la Ufalme…

Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alizidi kuliweka hilo vizuri katika 1Wathesalonike 1:5.

1 Wathesalonike 1:5 “ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika MANENO TU, bali na KATIKA NGUVU, na KATIKA ROHO MTAKATIFU, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu”.

Vile vile na sisi tunapaswa tuhubiri injili isiyo ya maneno matupu au yenye ushawishi wa maneno ili kuvuta watu… bali yenye dalili na udhihirisho wa Roho.

Maana yake ishara na miujiza vifuatane nasi…Na muujiza wa kwanza ni watu kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha…

1 Wakorintho 2:4 “Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments