Je shetani anaweza kushusha moto kutoka mbinguni?

Je shetani anaweza kushusha moto kutoka mbinguni?

Swali: Ayubu alijaribiwa na shetani, iweje biblia iseme “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni kuteketeza kondoo zake”?.


Jibu: Tusome,

Ayubu 1:14 “Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari”.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe..

Ikumbukwe kuwa Ayubu pamoja na watumwa wake wote hapo mwanzo hawakujua kuwa ni shetani ndiye anayewajaribu.. Ayubu alijua ni Mungu ndiye kamletea majaribu yote yale, ingawa hakujua sababu.. Halikadhalika watumwa wake wote na marafiki zake wote walijua ni Mungu ndiye katuma moto kuwateketeza wale kondoo na kumpiga Ayubu kwa mapigo yote yale. Ndio maana tunaona hata hapo huyo mtumwa akitaja huo moto, kana kwamba ni kutoka kwa Mungu.

Ni baadaye sana, Mungu alipomtokea Ayubu katika upepo wa kisulisuli na kumfunulia jambo lililokuwa linaendelea rohoni, jinsi shetani alivyopeleka mashitaka mbele zake dhidi yake Ayubu. Ndipo Ayubu alipoelewa sababu ya matatizo yote ni shetani, na aliyewaua wanawe ni shetani, na aliyeleta moto ni shetani na si Mungu…Lakini hapo mwanzo wakati anajaribiwa hakujua hilo.. yeye alijua ni Mungu tu!, ndio maana utaona Ayubu naye alisema..

Ayubu 1:21 “akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA; jina la Bwana na libarikiwe”.

Umeona hapo anasema BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA!!.. Maana yake alikuwa anajua kabisa kuwa aliyewaua wanawe wote 10 ni Mungu, na si shetani!. Ambapo kiuhalisia ni shetani ndiye aliyewaua isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa Mungu.

Hiyo inatufundisha nini?.

Tunaweza kupitia majaribu fulani tukadhani ni Mungu kayaleta kumbe ni shetani?..isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa Mungu. Na majaribu hayo yamegawanyika katika sehemu kuu (2)

 1. Majaribu ya shetani kwa Mtakatifu.

Kama umesimama katika imani kama Ayubu na unajikuta unapitia majaribu mazito!, kama magonjwa, misiba, dhiki, n.k basi fahamu kuwa ni Mungu kamruhusu shetani akujaribu.. Hivyo simama usiogope kwasababu mwisho wako utakuwa ni mzuri kuliko mwanzo, Kama ulivyokuwa wa Ayubu.

 2. Majaribu ya shetani kwa Mtu ambaye hajaokoka!

Kama hujampokea Yesu, na ni mtu wa kiulimwengu, na unajikuta katika majaribu mazito mazito kama misiba, magonjwa, dhiki, mateso. Jua ni Mungu kamruhusu shetani akujaribu kwa kukuletea hayo matatizo ili utubu umgeukie yeye. Lakini usipoitii sauti ya Mungu na kutubu basi shetani atakumaliza kabisa kabisa. Maana lengo lake yeye(shetani) ni wewe ufe katika dhambi na mateso.

Hivyo suluhisho la haraka hapo ni wewe kumpokea Bwana Yesu, akusafishe dhambi zako na kukuosha na kisha atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu. Na hivyo ule ulinzi wa kiMungu utaongezeka juu yako.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba shetani ndiye aliyeuleta ule moto!, na si Mungu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments