JIBU: Tusome..
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu”.
Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu”.
Shalom!
Mfano huo Bwana aliutoa alikuwa anajizungumzia yeye na kanisa lake.
Huyo Mtu Kabaila aliyesafiri kwenda nchi ya mbali ni BWANA wetu YESU mwenyewe, (KABAILA maana yake ni MTU ALIYEZALIWA KATIKA FAMILIA YA JUU ZAIDI KATIKA JAMII inaweza kuwa familia ya kifalme au kichifu,nk) kama tunavyojua, Bwana Yesu asili yake ni Mbinguni ametoka katika familia ya kimbinguni, na ndio maana hapa anajifananisha na huyu Kabaila, tunaona na baada ya kumaliza tu kazi yake alipaa kwenda mbingu za mbingu..sasa hiyo ndiyo nchi ya mbali inayozungumiwa pale kwenye huo mfano, Na amekwenda kule kwa makusudi kabisa ili kutuandalia sisi makao ili arudi tena kuja kutuchukua. Na kama mfano unavyosema “akawaita watumwa wake kumi akawapa mafungu 10 ya fedha” maana yake ni kwamba Bwana wakati anaondoka duniani siku ile alituachia sisi Roho wake Mtakatifu..kisha akatugawia majukumu kama agizo kuu, akatuambia tukahubiri injili kwa kila kiumbe ili kuleta faida katika ufalme wa mbinguni, aaminiye na kubatizwa ataokoka, kwahiyo Roho Mtakatifu aliachiliwa juu ya kila mwamini kila mmoja kwa kiwango chake cha neema alichopewa, hilo ndio fungu la fedha kwenye huo mfano (Matendo 2:38)..
Ukichunguza pia utaona hawakuambiwa wakafanye biashara moja, hapana kila mmoja alikuwa na uhuru wa kufanya biashara yake, hii ikiwa na maana kila mmoja anayo karama yake Mungu kampa. Na kwa kupitia hiyo utaulizwa uliitumiaje katika mambo yahusuyo ufalme wa mbinguni.
Uwe ni mwinjilisti uwe ni mwalimu uwe ni mchungaji n.k. Na kama huo mfano unavyosema kwamba kuna siku moja yule kabaila alirudi, na kuanza kuwauliza wale watu aliowapa yake mafungu kila mmoja ameleta faida kiasi gani katika biashara, Ndivyo itakavyokuwa kwetu kila mmoja ataenda kutoa hesabu mbele ya Bwana wetu YESU siku ile. kaitumiaje neema aliyopewa duniani Ndipo atakapowakusanya watumishi wake wote, na kuanza kumlipa mmoja baada ya mwingine kulingana na jinsi alivyotumika katika huduma, katika nafasi yake ya kuhubiri injili..waliotumika kwa uaminifu watalipwa thawabu kubwa zaidi, lakini waliozembea au waliokuwa wanafanya kazi ya Mungu kwa ulegevu na uvivu, au kinyume cha Neno Bwana anasema atawanyang’anya na thawabu yao na kupewa watu wengine.
Kwahiyo hiyo ndio maana ya mfano huo, unatufundisha kuwa makini sana na Neema Mungu aliyotupa ya Roho wake Mtakatifu, na karama alizotupa, kwamba siku moja tutakwenda kuulizwa, kama umepewa karama ya kuhubiri, au kufundisha halafu haufundishi inavyopaswa au kulingana na Neno, au unakuwa mvivu na kuendelea na mambo yako mengine na kuidharau kazi ya Mungu…Basi siku za mwisho utakwenda kuulizwa..Kama ulipewa karama ya kuhubiri kwa njia ya uimbaji na uimbaji wako hauna tofauti na waimbaji wa miziki ya kidunia, kila mtu akutazamapo anaona kitu tofauti na unachoimba, utakwenda kuulizwa siku ile. Ndio maana Bwana anasema..
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja UPESI, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja UPESI, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?
NI KWASABABU YA YESU KRISTO.
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?
MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
JIBU: Biblia haijatueleza muda Ayubu aliokaa katika majaribu, Lakini tukisoma baadhi ya vipengele inatupa picha kukisia muda aliodumu, kwa mfano tukisoma ile sura ya Ayubu 7:2-6 Ayubu anasema..
“2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; 3 Ni vivyo nami NIMEPEWA MIEZI YA UBATILI iwe fungu langu, NAMI NIMEANDIKIWA MASIKU YENYE KUCHOKESHA. 4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. 5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. 6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.”
“2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake;
3 Ni vivyo nami NIMEPEWA MIEZI YA UBATILI iwe fungu langu, NAMI NIMEANDIKIWA MASIKU YENYE KUCHOKESHA.
4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.
5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.
6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.”
Unaona hapo Ayubu anajaribu kujifananisha na mtu aliyeajiriwa ambaye kwa uvumilivu mwingi anasubiri mshahara wake kila mwisho wa kipindi Fulani labda tuseme wiki, au mwezi au mwaka,.apate faraja ya taabu yake, vivyo hivyo Ayubu naye anaonyesha amekaa katika hali hiyo ya kusononeka na kutaabika kwa MIEZI na masiku mengi, kama ya mwajiriwa vile, akisubiria faraja yake kutoka kwa Mungu ni lini atamrehemu na kumtoa katika mateso yale na majonzi yale.. Tunaona hapo Ayubu katamka neno MIEZI na sio MWEZI, hiyo ikiwa na maana ni zaidi ya mmoja, inaweza ikawa ni miwili au mitatu, au mitano au 12, au 20, au 100 hatujui kwasababu biblia haijaeleza jambo lingine la ziada.
Halikadhalika Pia hatujui ni muda gani ilimchukua Ayubu kukaa na wale marafiki zake, ambao tunasoma pia waliwasili kwake na kukaa siku 7 bila kuzungumza naye chochote, hivyo tukijumulisha na siku ambazo ziliwagharimu kufika kwa Ayubu kutoka majumbani kwao baada ya kupata taarifa za msiba wake, pamoja na siku ambazo walikuwa wanazungumza naye.. tukijumuisha na wakati ambapo Mungu anamwagiza Ayubu awaombee rehema wale marafiki zake kwa kwenda kuchukua ng’ombe 7 na kondoo 7 kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, tunaweza kukisia ni muda unaoweza kuchukua zaidi ya mwezi.. Lakini pia hatujui, kipindi Mungu alichotumia kumrejeshea Ayubu vitu vyote na mali zote alizozipoteza, je ilikuwa ni mara moja au kidogo kidogo, kama ni kidogo kidogo basi ni muda mrefu ulipita, lakini tunachofahamu ni kuwa Mungu alimburudisha Ayubu mara mbili ya alivyokuwa navyo pale mwanzo. Lakini hiyo ilikuwa ni kwa kusubiri na kwa kustahilimili na kwa kuvumilia.
Yakobo 5.10 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. 11Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”
Yakobo 5.10 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.
11Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”
Hivyo na sisi tunafundishwa tujifunze kuwa wavumilivu maadamu tunajiona bado tupo katika njia sahihi ya wokovu,hatuna budi kuwa hivyo kama Ayubu, tabu, shida, misiba, dhiki, mateso, kupungukiwa, n.k. visituzimishe roho tukamkufuru Mungu kama mke wa Ayubu, hata kama itachukua mwezi, au miezi, au miaka, au miongo, hilo lisituzuie kuangalia ahadi za Mungu, sisi tunachofahamu tu ni kuwa mwisho wa siku tutamwona Mungu jinsi alivyo mwingi wa rehema na huruma…kama alivyokuwa kwa Ayubu.
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:
DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.
SWALI: Shalom!
Luka 23:27 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata,na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua vyao na kumwombolezea.Yesu akawageukia,akasema,Enyi binti za Yerus’alemu,msinililie mimi,bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.29″KWA MAANA TAZAMA SIKU ZINAKUJA mtakaposema,HERI WALIOTASA,na MATUMBO YASIYOZAA,na MAZIWA YASIYONYONYESHA. Naomba kufahamu Siku hizo Kwanini hao walisema “Heri waliotasa..heri matumbo yasiyozaa..heri maziwa yasiyonyonyesha??
JIBU: Shalom! Hayo maneno a Bwana Yesu aliyazungumza kabla ya kupandishwa msalabani, Tunaona wale wanawake waliokuwa wanamfuata walimwonea huruma sana na kusikia uchungu mkubwa kwa mateso aliyokuwa anayapitia…lakini Bwana Yesu akawaambia msinililie mimi bali jililieni ninyi nafsi zenu na watoto wenu.. Kwanini alisema vile…
Kwasababu aliona kipindi kifupi sana kinachokuja mbeleni…kwamba mambo yaliyompata yeye yatakwenda kuwapata na wao pia, pamoja na watoto wao tena makubwa zaidi ya hayo…ambapo na wao pia watakatwa katwa na wanawake watachichwa kama kuku. Na kama unafuatilia unabii vizuri wa Biblia utakuja kuona kuwa kipindi kifupi tu baadaye AD 70 (yaani miaka 37 baada ya kusulibiwa kwa Bwana)..Jeshi la Rumi lilikuja na kuuzingira mji wa Yerusalemu na kuuchoma moto na kuwaaua watu wengi sana wakiwemo wanawake na watoto …historia inasema zaidi ya watu milioni moja na laki moja waliuawa…Mpaka ikaonekana kuwa ni heri mwanamke aliyetasa ambaye hakuzaa mtoto kuliko Yule aliyezaa na kuona mtoto wake anachichwa kama kuku mbele yake,Yerusalemu kulikuwa na maombolezo makubwa sana, hiyo ni kutimiza unabii alioutoa Bwana juu ya Mji huo katika..
Luka 19: 41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.
Mathayo 23.37 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! 38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa”.
Unaona hapo? Sababu ya Mji kuharibiwa na kufanywa ukiwa?..Ni kwasababu hawakujua saa ya kujiliwa kwao, ni kwasababu Masihi alikuja kwao na wao wakamkataa wakasema anapepo, anakufuru n.k hawakujua kuwa yeye ni mwokozi na ndiye aliyeteuliwa na MUNGU kuwa ukombozi kwa mwanadamu…Na kwasababu hiyo, Bwana akawaambia ule ulinzi na amani vimeondoka kwao siku zinakuja siku watakapoteketezwa na kuangamizwa na kutolewa kutoka katika nchi yao..Ndio maana Bwana akawaambia msinililie mimi, bali jililieni nyinyi na watoto wenu..kwasababu yatakayokuja kutokea mbeleni ni makubwa kuliko haya yangu.
Hiyo ilikuwa ni dhiki au adhabu kwa wayahudi (yaani waisraeli) kwa kumkataa Masihi, na kadhalika itakuja dhiki nyingine iliyo kubwa na isiyo na mfano kwa watu wa dunia nzima, kwa wale wote ambao wanamkataa Kristo sasa na kumsulibisha katika akili zao..Dhiki hiyo itakuwa ni kubwa isiyokuwa na mfano kuliko hiyo iliyowapata wayahudi..Biblia inaeleza hivyo. Kwahiyo tukiyajua hayo, sio wakati wa kuchezea hatima yetu ya milele, kabla dhiki kuu haijamiminwa duniani tunapaswa wakati huo tuwe tumekwenda na Bwana katika unyakuo. Je! Na wewe una uhakika utakuwepo miongoni mwao watakaomlaki Bwana mawinguni?
Bwana akubariki.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MAFUMBO YA MUNGU.
NGURUMO SABA
JUMA LA 70 LA DANIELI
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
SWALI : Ninatamani kwenda kusomea udaktari , lakini nina mashaka labda sio mapenzi ya Mungu kwangu, inanifanya nisiwe na maamuzi ya kueleweka..Naomba ushauri nifanyeje ili nijue masomo Mungu aliyoyakusudia nisomee katika maisha yangu.?
JIBU: Swali hilo linafanana na lile la mtu anayemwomba Mungu mpenzi sahihi wa kuoa/kuolewa katika maisha yake.. Mara nyingi tunatarajia Mungu atufunulie aidha kwa ndoto au maono au unabii au kwa njia nyingine iliyo dhahiri juu ya mpenzi wa kuoa, na hiyo inatufanya tufikiri labda pengine Mungu asipotumia njia kama hizo kabisa basi tumeoa mke/mume asiyesahihi, au tumeingia mahali pasipotupasa. Lakini kumbuka Mungu kujitambulisha kwetu kama MSHAURI WA AJABU,(Isaya 9:6) ni uthibitisho tosha kuonyesha kuwa Mungu sio dikteta wa mawazo ya mtu. Ikiwa na maana kuwa kama angekuwa hataki wewe uwe na uchaguzi wako binafsi, basi asingejitambulisha kwako kama mshauri badala yake angejiita “kamanda”..
Tatizo linakuja ni pale ambapo hatumfanyi Mungu kuwa mshauri wetu, na ndio hapo tunaingia katika maamuzi yasiyo sahihi.. Lakini mtu atajiuliza je! Tunamfanyaje Mungu kuwa mshauri wetu?..Jibu lipo wazi , na mashauri yake yapo wazi kabisa na karibu kila mtu anayafahamu na ameshayasikia, na hayo si mengine zaidi ya MAANDIKO MATAKATIFU. Hivyo ikiwa tumefikiria kufanya jambo Fulani ambalo tumelipenda, pengine tunataka kuoa au kuolewa na mtu fulani, jambo la kufanya kwanza ni kutuliza akili, pata muda wa kutosha wa kuombea jambo hilo, kisha ukishamaliza hatua hiyo lichukue katika maandiko, uangalie je! Litapinga imani yako au la!..kwa mfano unaweza ukawa umetamani kweli kufanya biashara Fulani ya kuuza vinywaji,lakini ndani yake kuna pombe,..sasa hata kama uliiependa biashara hiyo lakini ushauri wa Mungu unakuambia hapana maandiko hayaruhusu pombe…
Hivyo moja kwa moja unapaswa uache , utafuate kitu kingine. Inawezekana pia binti umempenda mwanaume mzuri, lakini ni wa imani tofauti, na yeye anataka mfunge ndoa muishi pamoja,..Lakini ushauri wa Mungu unakukataza katika maandiko, kwamba ndoa inapaswa ifungwe katika Bwana tu!, hivyo ikiwa mtu huyo hatataka kuigekia imani ya kweli ya Yesu Kristo, basi unachopaswa kufanya ni kukataa jambo hilo hata kama ulikuwa unampenda kiasi gani.. Hiyo ni kwa faida yako mwenyewe.
Lakini ikitokea sasa umeshavipitisha vyote hivyo kwenye mizani ya ki-Mungu na kuona kuwa hakuna chochote kinachopingana na maandiko na ndani yako umekipenda kweli na unasikia amani kukifanya, kwamfano, unahitaji kwenda kusomea udaktari hapo hakuna ubaya wowote, maadamu tayari ulishatenga muda wa kumwomba Mungu akutangulie basi hiyo inatosha kukupa amani kuwa Mungu ameshakusikia..Hivyo usiogope kwenda kusomea.. Kwasababu biblia inasema.
Mithali 16:1 “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.”
Hivyo hata ikitokea hicho ulichomwomba Mungu kukifanya au kukitenda hakikuwa ni sawasawa na mapenzi yake, kwa kuwa ulishamshirikisha mawazo yako kabla ya kuingia basi yeye mwenyewe atahakikisha anakuepusha nacho, au atakuandalia mazingira mazuri ya kutimiza kusudi lake ndani yake. Kama hajakujibu kwa ndoto au maono vile vile atakuepushia nacho pasipo ndoto wala maono kama sio mpango wake..
Mungu wetu hatuweki kwenye mtego kwamba tumwombe akae kimya na aruhusu tufanye jambo fulani kimakosa ili kesho na kesho kutwa aje kutulaumu!..yeye hayupo hivyo wanadamu ndio wapo hivyo.. Kwahiyo Kikubwa tu hakikisha huchukui uamuzi wowote bila kuupeleka kwanza kwenye maombi kwa muda wa kutosha, (sio maombi ya chai, hapana walau tenga kipindi kirefu kidogo, kuonyesha umakini kwamba umekusudia kweli kumkabidhi Mungu njia zako, hata ikiwezekana funga siku kudhaa,) ,Na pili hakiki kama kinaathiri imani yako au kinapingana na maandiko..ikiwa vitu hivyo viwili umevizingatia ipasavyo na hakuna shida basi endelea mbele kufanya unachotaka kufanya kwasababu Mungu atakuwa pamoja na wewe kuyaonyoosha mapito yako. Usisubiri ndoto wala maono.
Mithali 16:3 Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.
Lakini kama unasubiria maono au ndoto, au malaika akutokee ndipo achukue hatua…nakushauri acha kwasababu unaweza ukavunjika moyo pale ambapo majibu yatakuja usivyotarajia kwa kutokuona chochote, na mwisho wa siku ukajikuta upo njia panda hujui lipi la kufanya.
Ubarikiwe sana.
Mada nyinginezo:
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO?
IMANI “MAMA” NI IPI?
JIBU: Kwanza kabisa hebu tujifunze juu ya hili.. “Ni kwanini Shule nyingi za bweni karibia zote, zinakataza watoto kuwa na simu au kucheza karata au magemu au kuangalia movie?”..unafikiri ni kwanini?..Jibu ni rahisi ni kwasababu vitu hivyo vinapotumiwa na wanafunzi vinawasababishia kwa namna moja au nyingine kutokuwa na kiasi na matokeo yake inawapelekea kusahau kilichowapeleka shule na mwisho wa siku ni kufeli tu, Kwani ule muda ambao mtoto angepaswa afikirie masomo yake anajikuta anafikiria ile movie aliyoiangalia jana usiku au zile karata alizokuwa anazicheza au atakazozicheza, na mwisho wa siku hiyo inabadilika na kuwa hasara kubwa kwa mwanafunzi, na kwa shule na kwa Taifa kwa ujumla…Sasa kama wanadamu wanauwezo wa kuwa na hekima kama hiyo ya kupambanua hayo mambo yanayofaa na yasiyofaa…unadhani kwa Mungu itakuaje?..Ni dhahiri kuwa itakuwa ni zaidi ya hapo. Biblia inasema tusiupende ulimwengu:
1 Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
1 Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Unaona? Kwanini biblia inasema tusiipende dunia?..sio kwamba dunia ni mbaya, sio kwamba michezo ni mibaya, wala sio kwamba kustareheka ni kubaya…hapana vitu vyote hivyo sio vibaya kama vikitumiwa ipasavyo…Ubaya ni kwamba tunaishi duniani kwa muda! tupo darasani kwa kipindi kifupi sana, tukiyafuata hayo mambo ya duniani basi tujue kuwa hatutazingatia mambo ya Mungu, na matokeo yake ni kufeli na hivyo kupata hasara ya nafsi zetu. na Mungu wetu hataki tupotee ndio maana anatuambia tukae mbali na mambo hayo ya ulimwengu… Sisi (watoto wa Mungu) Ni sawa na mwanafunzi walioko shuleni, tena shule za Bweni…Ni wasafiri tu wa hapa duniani, tunatengeneza maisha yetu sasa ili tuwe na maisha bora huko katika umilele unaokuja…
Hivyo kama ni starehe, basi tutazifanya sana katika hiyo mbingu mpya na nchi mpya inayotungojea huko mbeleni, kama ni kufurahi, kama ni kuzurura, kama ni kucheza na kujiburudisha kwa jinsi tupendavyo basi tutafanya sana katika hiyo Yerusalemu mpya ambayo Mungu ametuandalia huko mbeleni, ..…lakini sasa katika ulimwengu huu sio wakati wake…Hayo mambo ni ya wakati wa zamani zijazo za wakati wa ulimwengu ujao, ambapo huko kutakuwa hakuna kusoma tena biblia wala kuhubiri, wala kufunga, wala hakutakuwa na majaribu tena, wala maumivu wala kula kwa jasho, wala kujizuia…hayo mambo hayatakuwepo kule, kule itakuwa ni sehemu ya furaha, ya kufanikiwa na ya uhuru usio na kifani. Ndivyo maandiko yanavyosema.
Lakini Wengi wanasema ni ushamba kujinyima raha katika ulimwengu huu, lakini hao hao hawajui kuwa ni ushamba mkubwa zaidi kujinyima raha za umilele unaokuja huko mbeleni…jiulize ukifa leo huko utaenda kuwa mgeni wa nani?. Kumbuka Mwanafunzi mwenye busara ni yule anayezingatia kilichompeleka shuleni..sio ushamba mwanafunzi kujizuia kuangalia movie ili atumie muda wake vizuri katika masomo, wala si ushamba mwanafunzi anapojizuia kuzurura zurura huku na huko na badala yake muda wote unautumia kutafakari masomo ili mitihani aje kufaulu vizuri…anajinyima hivyo vyote kwasababu anajua ni kwa faida yake mwenyewe na ni kwa muda mfupi tu, ..anajua siku akimaliza shule na kufaulu, atayafanya hayo sana na zaidi ya hayo…
Na sisi tunapaswa tuzingatie kwasasa kile kilichotuleta duniani. Sio ushamba kuukataa ulimwengu, sio kila kitu kinachoja mbele yetu tukijaribu tu, vingine vinatupoteza muda, vingine vinatuondoa katika dira ya wokovu, vingine vinaturudisha nyuma… Ni wajibu wetu kuenenda katika hii dunia kwa werevu. Kwahiyo kwa kuhitimisha, mchezo wa karata haufai kwa mtoto wa Mungu, utacheza karata masaa mawili lakini kushika biblia dakika tano huwezi, utaangalia muvi series hata masaa nane lakini biblia dakika 10 huwezi…huoni kuna roho nyuma ya huo mchezo?..roho inayokufanya kutokuzingatia mambo ya msingi ya Imani. Hiyo ni roho inayokupeleka katika kufeli maisha. Hivyo tuwe makini sana.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?.
KISASI NI JUU YA BWANA.
JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.
MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.
TWEKA MPAKA VILINDINI.
SWALI: Shalom mtumishi wa Mungu; Naomba unisaidie kuelewa haya maandiko katika (matendo 9:3-7, 22:6-9, 26:12-14). Pale Mtume Paulo alipokuwa anatoka Yerusalemu kwenda Dameski kushika wakristo na kukutana na YESU njiani. Kama yanazungumzia habari moja mbona kama yanajichanganya yenyewe?.
JIBU: Mtafaruku mkubwa kwenye vifungu hivyo vitatu ni pale ile sauti ilipotoka mbinguni ikisema na Paulo. Watu wanajiuliza inakuaje sasa sehemu moja biblia inasema wale watu waliisikia sauti ya Yesu iliyosema na Paulo , na sehemu nyingine biblia inasema hawakuisikia?, Ni kwanini iwe hivyo?Kwamfano Tukisoma
Matendo 9:7 inatuambia…. “Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, WAKIISIKIA SAUTI, WASIONE MTU.”
Lakini tukirudi tena kusoma kwenye kitabu hicho hicho cha Matendo ile sura ya 22:9 Paulo anasema…
“Na wale waliokuwa pamoja nami WALIIONA ILE NURU, LAKINI HAWAKUISIKIA ILE SAUTI YA YULE ALIYESEMA NAMI”.
Unaona hapo kunaonekana kama kuna mkanganyiko fulani, inaonyesha kama maandiko yanajipinga hivi, huku yanasema wale watu waliisikia sauti, wakati huo huo tena mbeleni kidogo inasema wale watu hawakusikia ile sauti iliyosema naye. Ni kweli kabisa tukisoma kwa juu juu tu tunaweza kuona maandiko yanajipinga lakini kiuhalisia maandiko hayajichanganyi, badala yake ni sisi ndio tunakosa shabaha ya kuyaelewa..uelewa wetu ndio unaojichanganya. Na ndio maana Mtume Paulo kwa kuyaona mambo kama hayo alikuwa akimsisitiza Timotheo mara kwa mara, akimwambia afanye bidii katika KUSOMA (1Timotheo 4:13)..
Sasa Kusoma kunakozungumiziwa hapo sio kusoma kama mtu asomavyo gazeti, halafu basi, hapana bali ni kusoma kwa KUJIFUNZA..yaani Kwa kuchukua muda kutafakari na kuchambua kwa undani maandiko huku ukimwomba Roho Mtakatifu akuongoze kuyaelewa vinginevyo biblia inaweza kubakia kwako kuwa kama kitabu kisichoeleweka daima, na kinachojipinga siku zote. Sasa tukirudi darasani. Katika maandiko kumbuka Neno KUSIKIA linamaana kubwa zaidi ya “kusikia” tu peke yake..Kwa mfano Utaona Yesu alipofundisha mifano yake mingi alimalizia na kauli hii “mwenye masikio ya kusikia na asikie.”
Unaona hapo Hakumaanisha kuwa watu waliokuwa mahali pale walikuwa viziwi hawasikii alichokuwa anakizungumza, hapana bali alimaanisha “mwenye masikio ya kuelewa na akielewe kile alichokuwa anakimaanisha.”..
Hali kadhalika Mungu anaweza kuzungumza na mtu maneno yanayoeleweka kabisa na kumshushia ujumbe, lakini kwa mtu mwingine ujumbe ule ukamwasilia kama sauti tu ya ajabu, au ngurumo tu, au mlio wa ajabu usioeleweka,..tunalithibitisha hilo kwa Yesu siku ile aliponyanyua kichwa chake juu na kumwomba baba ndipo sauti ilipotoka juu na kusema naye.…,
Yohana 12: 28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu
Yohana 12: 28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.
29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.
30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu
Unaona? Wale watu waliisikia sauti kabisa, na wengine wakatambua ya kuwa ni Mungu ndiye aliyekuwa anasema naye, lakini Hawakuielewa …ilikuja kwao kama kitu kingine kama ngurumo tu, sauti isiyoeleweka.. “” kwahiyo waliisikia sauti lakini ni sawa na hawajaisikia maana hawajaielewa.
Na ndicho kilichowakuta kundi la watu hawa, walipokuwa wanatoka Yerusalemu kuelekea Dameski, wakiongozwa na kiongozi wao mkuu Sauli (Paulo), waliokwenda kuwakamata Wayahudi wote waliokuwa wakimtangaza Kristo hadharani ili kuwarudisha Yerusalemu waadhibiwe….Ndio katikati ya safari yao walipokutwa na tukio hilo la ajabu, njia mida ya adhuhuri ile nuru kuu kutoka mbinguni ikawaangazia wote, ndipo Yesu akaanza kuzungumza na Sauli kwa lugha ya Kiebrania. Sasa hapo wale watu waliokuwa na Sauli muda ule waliisikia kweli sauti fulani iliyotoka mbinguni, lakini kwao ilikuja kama sauti isiyoeleweka…kama mlio tu au mngurumo!..
Na ndio hapo sasa tukirudi kwenye vile vifungu kama kile cha kwanza mwandishi anasema..”
Matendo 9:7 …. “Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, WAKIISIKIA SAUTI, WASIONE MTU.”
Unaona, Hapa ni sawa na kusema walisikia ngurumo tu au sauti isiyoeleweka kutoka mbinguni mahali pale, hakukuwa kimya kabisa kulikuwa na sauti fulani mahali pale,.
Sasa Tukirudi kwenye kile kifungu cha pili inatuambia..Matendo 22.9 …”Na wale waliokuwa pamoja nami WALIIONA ILE NURU, LAKINI HAWAKUISIKIA ILE SAUTI YA YULE ALIYESEMA NAMI”. Hapo ni sawa na kusema Hawakuelewa, kile walichokisia..Hivyo maandiko yapo sawa, na wala hayajipingi na hata sasa biblia inatumbia Luka 8:18 “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo;”..
Tunapaswa tuwe makini na kile Mungu anachosema nasi, katika maandiko wakati mwingine tunaweza kujiona tumefika tunaelewa kila kitu, biblia tunaifahamu yote, hakuna hadithi tusioyoijua katika biblia, lakini kumbe hatujaielewa sauti ya Mungu iliyojificha nyumba yake. Bwana Yesu alisema..
Mathayo 13:14 “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.”
Mathayo 13:14 “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.”
Mungu aturehemu na atujalie kumjua zaidi..
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
MTUME PAULO ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA ″…NINAKUFA KILA SIKU?
KWANINI MTUME PAULO HAKUMSAMEHE MARKO, PINDI WALIPOTAKA KWENDA WOTE KAZINI?
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?
DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
JIBU: Wafu wote waliokufa kabla ya Kristo kuja duniani walikuwa makaburini, au sehemu za wafu, mahali pengine katika biblia panapaita Kuzimu, Daudi aliomba katika roho akisema “Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.” (Zaburi 16:10) Aliomba asiende sehemu za wafu iliyo njia ya wote, lakini tunasoma alikufa na akakusanywa na baba zake huko, Lakini kumbe Unabii huo ulikuwa haumuhusu yeye bali Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni yeye pekee nafsi yake haikubaki huko.
Hivyo biblia haielezi kwa mapana walikuwa wanaishije ishije huko..lakini ni mahali ambapo hatuwezi kusema palikuwa ni salama sana, kwa maana shetani naye kwa sehemu Fulani alikuwa anao uwezo wa kuwasiliana na hata watu wenye haki waliokuwa wamekufa zamani, tunalithibitisha jambo hilo kwa Samweli, (1 Samweli 28)…Na hiyo ni kwasababu ya kuasi kwetu ndipo kulipompa shetani baadhi ya funguo za kututawala sisi hata mpaka baada ya kufa kwetu..japo alikuwa hana uwezo wa kuwaondoa mahali walipokuwepo…Lakini Kristo alipokuja na kushinda vyote pale msalabani, ndipo akachukua funguo zote za kuzimu na mauti na sasa wafu wote anawamiliki yeye.
Ufunuo 1: 17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.
Ufunuo 1: 17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.
Hivyo leo hii hakuna mtu au pepo lolote, au shetani anayeweza kuwasiliana na mtu wa aina yoyote yule aliyekufa ile awe mwenye dhambi au asiye na dhambi isipokuwa YESU peke yake..Ukiona mtu anakuambia mzimu wa baba yangu, au bibi yangu umenijia basi ujue kuwa hilo ni PEPO lililojigueza na kuvaa sura ya yule mtu,na wala si yule mtu halisi..Sasa kukaa kwake Bwana kaburini zile siku tatu, kulikuwa ni kushuka kuzimu huko wafu wote walipo ili kuwatenga wale wafu waovu na wema kwa injili aliyokwenda kuwahubiria.
1Petro 3:18 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,19 AMBAYO KWA HIYO ALIWAENDEA ROHO WALIOKAA KIFUNGONI, AKAWAHUBIRI;20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
1Petro 3:18 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
19 AMBAYO KWA HIYO ALIWAENDEA ROHO WALIOKAA KIFUNGONI, AKAWAHUBIRI;
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Sasa wale wema ambao waliishi maisha ya haki duniani na ya kumcha Mungu walihamishwa na kupelekwa mahali pa raha zaidi, ambapo panajulikana kama PEPONI/PARADISO (Kule alipomwambia yule mwizi aliyesulibiwa kuwa atakuwepo naye siku hiyo hiyo peponi)…Lakini wale waovu waliosalia walisogezwa mahali pa shida zaidi huko huko kuzimu…. Na katikati yao kukawekwa SHIMO kubwa ili wa kule wasiweze kuja huku na wa huku kwenda kule katika Roho,..Wale wema walipandishwa juu, lakini waovu walizidi kukaa chini na ndio maana yule tajiri katika habari ya Lazaro utamwona akinyanyua macho yake na kumwona Lazaro upande wa pili kule kuzimu.
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Sasa tukirudi kwenye swali wale wafu walikuwa wapi, ndio hapo siku ile Bwana aliyofufuka utawaona wafu watakatifu wakitoka makaburini, na kuhamishiwa Peponi,..Hivyo mtu akifa leo katika haki moja kwa moja anapanda peponi/paradiso akisubiria UFUFUO wa Haki siku ile ya unyakuo..lakini atakayekufa katika dhambi, naye moja kwa moja atateremka Jehanum, kwenye mateso makali akingojea naye kufufuliwa siku ile ya hukumu mbele ya kiti kile cheupe cha Enzi cha Mwanakondoo ahukumiwe kisha atupwe kwenye lile ziwa la moto
Hivyo huu ni wakati wa kuweka mambo yetu sawa, yasije yakatukuta kama yale ya yule tajiri, biblia inasema itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima na mwisho wa siku tupate hasara ya nafsi zetu.?. Kiburi cha mwanadamu ni maua leo kipo kesho kinanyauka, ikiwa leo utajikuta haupo tena duniani..Huko uendako utakuwa mgeni wa nani? Huko hakuna nafasi ya pili.
Wokovu unapatikana bure sasa, ukikupita leo kesho utautafuta kwa kilio na kusaga meno na hautauona.. Ni maombi ikiwa maisha yako yapo mbali na Kristo basi leo fanya uamuzi wa kumkabidhi yeye maisha yako na yeye ana upendo na ni mpole na ameahidi kukupokea, na kuwapokea wote wanaomkimbilia yeye.
UPONYAJI WA YESU.
HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
MNGOJEE BWANA
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?
SWALI: Tukisoma Matendo 19:13 Inasema pale “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, NAO NI WAPUNGA PEPO….” swali,Naomba kufahamu hawa Wapunga Pepo ni watu wa aina gani ndugu zangu?
JIBU: Tafsiri ya Neno kupunga pepo ni “kufukuza pepo”…hiyo ni lugha iliyotumika katika tafsiri yetu ya Kiswahili inayosimama badala ya kufukuza pepo…Kwahiyo zamani na hata sasa zilikuwepo njia nyingi za kuondoa pepo ndani ya mtu…
Watu wa Mungu wanao uwezo wa kufukuza mapepo kwa kutumia jina la YESU, kadhalika na watu wa shetani wanauwezo wa kufukuza pepo.Sasa njia wanayotumia watu wa Mungu kufukuza mapepo ni tofauti na njia wanazozitumia wachawi au waganga…
Wakristo wanafukuza pepo na kumfanya yule mtu kuwa huru kabisa kabisa, kwa kutumia jina la Yesu Kristo kwa Imani, mtu huyo anafunguka na kuwa huru..kama mtu alikuwa na pepo fulani lililomletea ugonjwa Fulani labda ugonjwa wa kuumwa tumbo, linapoondolewa kwa jina la Yesu linaondoka moja kwa moja pamoja na ule ugonjwa wake na madhara yake yote.
Lakini waganga wa kienyeji au wachawi wanavyofukuza mapepo ni tofauti kabisa kwao haiwi hivyo..wao hawayafukuzi bali wanaleta mapepo mengine juu ya yule mtu yenye nguvu zaidi ya lile pepo lililopo ndani ya yule mtu, kwahiyo kinachotokea labda yule mtu alikuwa na pepo fulani lililomletea ugonjwa fulani labda wa kuumwa tumbo, Yule mtu anapokwenda kwa mganga (mpunga pepo)… yule mganga anamtumia pepo lingine lenye nguvu kuliko lile la ugonjwa wa tumbo linamwingia labda tuseme pepo la utasa na lile pepo la ugonjwa wa kuuma tumbo nguvu zake zinafunikwa na lile lingine la utasa lililomwingia.
Kwahiyo yule mtu baada ya kuaguliwa na yule mganga anaweza akajisikia unafuu wa kupona tumbo kwa muda…lakini baada ya kipindi fulani anakuja kujigundua tena kapata utasa au ugonjwa mwingine mkubwa zaidi…sasa hiyo hali ya kupunguza pepo hili nguvu kwa kulileta lingine lenye nguvu zaidi ya lile la kwanza ndiyo inayoitwa “kupunga pepo”.
Ni sawa kuleta nyoka ndani ili ale panya wanaokula mahindi yako ghalani, atawapunguza tu na kufurahi kwa muda lakini hawezi kuwamaliza wote, na zaidi ya yote huyo nyoka siku moja atakuletea madhara na wewe…
Kwahiyo waganga hawana uwezo wa kutoa mapepo, wanaongeza pepo juu ya pepo, kwasababu shetani hawezi kujifitini kwenye ufalme wake mwenyewe kama Bwana Yesu alivyosema…
Mathayo 12:26 “Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?”.
SEHEMU ISIYO NA MAJI.
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
UTEKA ULIOGEUZWA.
Nini maana ya Kipaimara?..je watu wanaweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na kwa kupitia mafunzo fulani ya kipaimara?
JIBU: Kipaimara ni Neno lenye maana ya “uthibitisho”…Neno hili linatumika katika madhehebu baadhi kama vile Katoliki, Orthodoksi na Anglikana kama kanuni muhimu ya ukristo..Kwamfano Kanisa Katoliki lina kanuni saba za kufuata wanazoziita Sakramenti. Kwahiyo kipaimara Ni moja wapo ya hizo kanuni saba (sakramenti 7), ni kanuni ya Imani ambapo mtu anapaswa aipitie ili awe AMETHIBIKA MBELE ZA MUNGU. Na kanuni hiyo si nyingine zaidi ya KUWEKEWA MIKONO NA MAASKOFU WA KANISA… Madhehebu yanayotumia kanuni hii yanasimamia mistari kutoka katika kitabu cha..
Matendo 8: 14 “Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.17 NDIPO WAKAWEKA MIKONO YAO JUU YAO, NAO WAKAMPOKEA ROHO MTAKATIFU.”
Matendo 8: 14 “Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
17 NDIPO WAKAWEKA MIKONO YAO JUU YAO, NAO WAKAMPOKEA ROHO MTAKATIFU.”
Kwahiyo kinachotokea ni kwamba baada ya mtoto kubatizwa, atapaswa apitia mafunzo fulani yanayohusiana na kipaimara, na akishahitimu, ndipo atakusanyika kanisani na kuwekewa mikono na Askofu, na ndipo Roho Mtakatifu atashuka juu yake kama alivyoshuka juu ya hao wasamaria waliokuwa wamebatizwa tu lakini bado walikuwa hawajashukiwa na Roho Mtakatifu. Kwahiyo kwa lugha rahisi au nyepesi ni kwamba hao Wasamaria walipokea kipaimara kwanza kwa mikono ya akina Petro na Yohana, ndipo Roho Mtakatifu akashuka juu yao..ikiwa na maana kuwa kama wasingewekewa mikono na Mitume na Bwana Yesu Kristo kamwe wasingepokea kile kipawa cha Roho Mtakatifu.
Kwahiyo Kanisa katoliki na mengine wakaichukulia hiyo kama ni kanuni ya MUHIMU SANA ya kufuata kwa kila mkristo, kwamba ili mtu athibitike kuwa mkristo kweli kweli na ili aweze kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ni lazima abatizwe kwanza na kisha awekewe mikono na maaskofu wa kanisa, Na akishapitia hizo hatua kikamilifu ndipo anaweza kukubalika kama ni mshirika halali wa kanisa, na zaidi ya yote ni Mkristo..Kabla ya hapo anakuwa hajulikani kama ni mkristo.Sasa kwa namna ya kibinadamu, hiyo inaweza ikaonekana ni sawa, inaweza ikaonekana ni utaratibu mzuri, au ni kanuni ya kufuata siku zote,..Lakini je! Ni sahihi kulingana na maandiko?.
Kwanza kabisa kabla ya kuelezea kipaimara, tuuzungumzie ubatizo kwa ufupi: ni muhimu kufahamu kuwa watoto wachanga hawabatizwi kulingana na Neno “Imani” lenyewe lilivyo, Ili iwe imani, ni lazima kwanza mtu aamini kitu fulani, sasa watoto wachanga hata kujielewa tu hawajajielewa, sasa wataaminije?..watamwamini vipi Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yao, na kwamba amekufa kwa ajili yao, na kwamba wanapaswa watubu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao, wakati hata fahamu za kujitambua wao wenyewe hazipo ndani yao?Kwasababu biblia inasema..
Warumi 10: 13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? TENA WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA? Tena wamsikieje PASIPO MHUBIRI?15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema”
Warumi 10: 13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? TENA WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA? Tena wamsikieje PASIPO MHUBIRI?
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema”
Kwahiyo Ubatizo wa vichanga sio sahihi kulingana na uhalisia wa mambo yote, haihitaji ufahamu mwingi sana kuelewa jambo hilo. Kumbatiza mtoto mchanga ni sawa na kwenda mtaani na kumchukua mtu asiyemjua Mungu kabisa pasipo kumhubiria, wala kumfundisha chochote na kwenda kumzamisha kwenye maji na kumwambia tayari umebatizwa!…Hiyo ni kazi bure. Na pili, kuhusu kipaimara, Mitume hawakutoa kanuni Fulani kwamba mtu akitaka kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu ni lazima awekewe mikono na viongozi wao kwanza?..Hapana hawakutoa hiyo formula hata kidogo..Petro Na Yohana waliwawekea mikono wale wasamaria kwa wakati ule tu kwasababu ndio njia waliyoongozwa na Roho waitumie kwa wakati ule tu! Mahali pengine watu walishukiwa na Roho pasipo kuwekewa mikono na mtu yoyote.
Kama tu siku ya Pentekoste watu walishukiwa na Roho pasipo kuwekewa mikono na mtu yoyote. Na pia tunaona huyo huyo Petro alipokwenda nyumbani kwa Kornelio kumhubiria injili yeye na nyumba yake, Roho aliwashukia wale watu wote pasipo hata Mtume Petro kuwawekea mikono..
Matendo 10: 43 “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 10: 43 “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Unaona hapo? Wakati Petro akiwa anazungumza tu! Roho aliwashukia juu yao, Na sehemu nyingine Petro alipowahubiria watu zaidi ya elfu 3, na walipoamini..aliwaambia namna ya kupokea Roho Mtakatifu pasipo kuwekewa mikono akawaambia..”
Matendo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Matendo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Unaona na hapo? Petro Hakuwaambia watu tubuni mkabatizwe na kisha njooni tuwawekee mikono ndipo mpokee kipawa cha Roho Mtakatifu badala yake maneno hayo yanaonyesha kuwa mtu anaweza kupokea Roho Mtakatifu pasipo hata kuwekewa mikono na mitume. Kwahiyo kuwekewa mikono sio kanuni ya kupokea Roho Mtakatifu, kanuni ya kupokea Roho ni kutubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu.Mwingine anaweza akapokea Roho kwa kuwekewa mikono, mwingine anaweza apokee pasipo kuwekewa mikono…Na kwa jinsi Roho atakavyochagua njia ya kushuka juu ya huyo mtu, baada tu ya mtu kutubu na kubatizwa.
Ni sawa na wakina Petro mahali pengine walikuwa wanatumia hata leso zao kuponya wagonjwa, na sehemu nyingine wanataja tu jina la Yesu pasipo kutumia chochote na watu wanafunguliwa..
kwahiyo ni njia tu ambayo Roho aliyokuwa anawaongoza kwa wakati husikia ndiyo waliyokuwa wanaitumia..lakini huwezi kuona Petro anatoa kanuni maalumu kuwa sehemu zote watu ili wafunguliwa lazima watumie leso, huwezi kuona jambo hilo.. Tofauti na ilivyo siku hizi za mwisho..Mafuta, chumvi, udongo ndio KANUNI ya kupokea uponyaji, kila tatizo linatatuliwa na maji ya maombezi, kila tatizo linatatuliwa na mafuta ya maombezi na chumvi…Inakuwa ni kanuni, jina la Yesu halitumiki tena…Ni roho hiyo hiyo iliyopo pia katika mifumo ya kipaimara na ubarikio. Kwahiyo kipaimara ni mfumo wa kimapokea ambao hausimami katika uhalisia wa kibiblia, ambao malengo yake ni kuwafanya watu waamini kuwa kuwekewa mikono na askofu, tayari wamekamilika na ndio tiketi ya kuthibitika mbele za Mungu..ni mfumo ambao unawafanya watu waridhike na kanuni za dini kuliko kanuni za biblia.
Utamwuliza mtu unauhakika wa kwenda mbinguni, atakwambia ndio nimebatizwa na nimepokea kipaimara…lakini mwulize nini maana ya Roho Mtakatifu na matunda yake ni yapi?..atakwambia sijui?, muulize nini maana ya unyakuo atakuambia sijawahi kusikia hata hicho kitu, muulize umeokoka atakwambia dini yangu haifundishi hivyo, mwambie kuwa Tunaishi siku za mwisho atakuambia sijui?..lakini atajisifia kipaimara chake kwa sherehe kubwa aliyoifanya siku hiyo. Utakuta mtu analijua dhehebu lake kuliko anavyoijua biblia. Kwahiyo kanuni za kipaimara sio kanuni zilizokatibiwa na Mungu bali wanadamu, Mungu hajatoa kanuni maalumu kuwa mtu lazima apitie kipaimara au apakwe mafuta ya maombezi, au atumie chumvi ndipo afunguliwe au akubaliwe na yeye..yote hiyo ni mipango ya ibilisi kuwafanya watu wasitafakari maandiko kwa kina bali wapate njia za mkato za kutatua matatizo yao. Na kujiridhisha katika hizo kama ndio sababu ya kukubaliwa na Mungu, kumbe sio.
NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
UNAFANYA NINI HAPO?
MSTARI HUU UNA MAANA GANI? “YUKO MWENYE HAKI APOTEAYE KATIKA HAKI YAKE”?
WAPUNGA PEPO WANAOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NI WATU WA NAMNA GANI?
JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?
Baba mmoja Ananisimulia akisema, “Mimi hapa huwa ninasikia watu wanaosema wanakuja kunikamata.akaniuliza je! Na wewe unawasikia? Nikamwambia hapana mimi siwaskii[saa hiyo ni yeye tu anawasikia]. Akanichukua akanishika mkono Akaniambia” Unasikia hiyo nyimbo yangu wanaimba? (Mimi siisikii yeye peke yake anasikia)” Nikamwambia hapana” ANAOGOPA SANA.
Sasa Juzi juzi Usiku nikamkuta amesimama hapa nje nyumbani kwetu Akiwa ameshika panga mkononi mwake akaniambia “Unamsikia bibi mmoja kule ng’ambo anasema nimebaka mjukuu wake[Kwa bibi huyo ni mbali na hapa kwetu]?” Nikamwambia hapana.Akarudi nyumbani na panga lake.[Wakati huo anaongea yuko siriazi kabisa].Wakati mwingine ananiambia aliowaona watu wamesimama mlangoni kwake. Sasa Swali:Ndugu kwa nyinyi Muonavyo Hicho ni kitu gani?? KARIBUNI [Nilijaribu kumueleza habari ya kumpa Bwana maisha akasema ATAPAMBANA KIJESHI[Nilijuwa anamaanisha kwa waganga],Lakini namuona sasa hawezi kupambana kijeshi alivyosema].Hali yake inazidi kuongezeka Ikifika mahali Si ajabu akawa kichaa kabisa.
JIBU: Shalom, Mambo yanayoendelea katika roho ni mengi, na shetani naye kila kukicha anaongeza mapana ya maarifa yake…mtu akizama katika maarifa ya shetani (mfano uchawi)..anakuwa anauwezo wa kufanya vitu ambavyo kwa namna ya kawaida haviwezekani kufanyika…sasa kwa mtu kama huyo aliyekuja kukusimulia kuwa anasikia sauti za nyimbo, na ana uwezo wa kusikia mtu akizungumza akiwa mbali, ni wazi kuwa kuna roho ipo ndani yake na hiyo ni roho ya yule adui. Kwanini ni roho ya adui, na si ya Mungu? kwasababu matunda ya hiyo roho ni ya yule adui, kumpeleka kwenye uovu na kumweka katika vifungo vya uoga,wasiwasi na mkandamizo… Kwasababu matunda ya Roho Mtakatifu sio hayo ingekuwa ni Roho Mtakatifu yupo ndani ya huyo mtu ungeona matunda ya Roho ndani yake kama yalivyoandikwa kwenye kitabu cha Wagalatia
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
Umeona hapo? Roho Mtakatifu akiwa ndani ya mtu hivyo vitu hapo juu lazima vionekane, amani, furaha,upendo n.k…Lakini roho iliyopo ndani ya huyo mtu haijamsukuma kwenye upole, wala haimpeleki kwenye furaha, wala uvumilivu, wala amani…zaidi ya yote umempeleka kwenye hofu, mashaka na ghadhabu…hivyo hiyo ni moja kwa moja roho ya yule mwovu ipo ndani yake. Sasa Roho Mtakatifu akiwa ndani ya mtu huwa ni lazima atoe na kipawa fulani juu ya huyo mtu, ndio hapo anawapa wengine vipawa vya unabii, wengine lugha, wengine miujiza,ishara,uchungaji, ualimu,uinjilisti n.k [kumbuka vipawa vya Roho ni tofauti na matunda ya Roho].
kadhalika na roho za mashetani ni hivyo hivyo, mtu akiwa na pepo fulani la utambuzi, ni lazima litampa uwezo fulani,(ni kama karama yake fulani hivi) watu wengine shetani anawapa uwezo wa kufanya utambuzi, wanakuwa na uwezo wa kutambua siri za watu, au kuona vitu vinavyoendelea sehemu nyingine mbali na mahali walipo, hata wakati mwingine wanakuwa na uwezo wa kusikia sauti na mazungumzo ya watu waliopo mbali kama huyo mzee, wengine wanakuwa na uwezo wa kufanya viishara ishara fulani (mazingaumbe mazingambwe) wengine wanakuwa hawana huo uwezo lakini wanakuwa wanauwezo mwingine mkubwa wa ushawishi…wanaweza kumshawishi mtu au jamii na wakafanikiwa kuleta vitu vyenye madhara kwa kutumia hivyo vipawa walivyonavyo vya nguvu za giza.
Kwahiyo kwa habari ya huyo mzee ni kwamba kafungwa na nguvu za giza, aidha kwa kujua au kwa kutokujua, na kwasababu hamjui Yesu Kristo, inawezekana yeye akajihisi anakipawa kutoka kwa Mungu cha uwezo wa kujua na kuwasikia maadui zake mahali walipo, lakini ni roho ya adui ipo ndani yake, pasipo yeye kujijua,hivyo nakushauri, tenga muda umhubirie injili, ili macho yake ya rohoni yafumbuke,umweleze uwezo uliopo katika Yesu Kristo, na tumaini lililopo ndani ya Yesu Kristo, na Bwana akimpa Neema ya kuamini injili na kuipokea, mwekee mikono na kumwombea kwa Jina la Yesu na hizo roho zitamwacha atakuwa huru kabisa.
Na akizingatia kutubu kwa kuacha dhambi zake kabisa na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, basi Bwana atampa kipawa cha Roho wake Mtakatifu kwasababu yeye mwenyewe alisema ahadi hiyo ni kwa watu wote waliompokea..Na akiisha pokea Roho Mtakatifu basi yale matunda ya Roho yataambata naye..atapata amani isiyokuwa ya kawaida, furaha ya ajabu, upendo wa ajabu, uvumilivu usioelezeka, upendo usiokuwa na mipaka na fadhili nyingi.
Bwana akubariki.
JE! UMECHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU?
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
VITA DHIDI YA MAADUI
“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”
NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!