SWALI: Matendo ya mitume 2:1 ″Hata ilipotimia “SIKU YA PENTEKOSTE” walikuwako wote mahali pamoja.Ndugu zangu hiyo Siku ya Pentekoste ilikuwa ni siku gani? Pentekoste ilimaanisha nini ndugu.?
JIBU: Pentekoste ni neno la kigiriki lenye maana “YA HAMSINI” . Hivyo kwa wayahudi walikuwa wanasherekea siku ya hamsini baada ya sikukuu ya pasaka (waliagizwa na Bwana wafanye hivyo) lakini wenyewe walikuwa hawaiiti kwa jina hilo la pentekoste, walikuwa wanaiita hiyo sikukuu kama “SIKU KUU YA MAJUMA”.
Bwana Mungu aliwaambia wahesabu majuma 7 yaani sabato 7 baada ya pasaka, yaani siku 49, na siku ya hamsini ( ndiyo pentekoste) wafanye sikukuu…Soma (Kumbu. 16:9 na Walawi 23:15).
Kwahiyo sasa kwasababu mambo yaliyokuwa yanafanyika agano la kale yalikuwa ni kivuli cha agano jipya, ilikuwa ni lazima sikukuu hizo ziwe na uhusiano mkubwa na mambo ya agano jipya,. Kwahiyo wayahudi pasipo kujua lolote walishangaa Roho Mtakatifu anashuka juu yao siku ile ile ya Pentekoste ambayo walikuwa wanasheherekea hiyo siku kuu yao ya Majuma, kama tu kusulibiwa kwa Bwana kulivyoangukia katika siku kuu yao ya pasaka kadhalika kumwagwa kwa Roho kuliangukia katika siku kuu yao ya majuma (yaani pentekoste). Na ilikuwa ni siku ya HAMSINI baada ya sikukuu ya Pasaka.
Ubarikiwe sana.
Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312
Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Mada Nyinginezo:
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
NINI MAANA YA KIPAIMARA?.NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
ITAFAKARI VEMA KAZI YA MUNGU
MAFUNUO YA ROHO.
Rudi Nyumbani:
Print this post
SWALI:Kama kijana mmoja yeye alimtuhumu muhubiri mmoja kuwa yeye ana KOSA HAWAONGOZI WATU SALA YA TOBA..Hilo ni kweli unaweza kumhesabia mhubiri kosa kwasababu hawaongozi watu sala ya toba ndugu zangu??Hiyo sala ya toba ikoje ndugu zangu?.
JIBU: Wokovu sio suala la kumsaidia mtu kufanya, wokovu ni jambo linalotoka katika moyo wa mtu…Kwasababu neno TOBA lenyewe linamaana ya KUGEUKA na sio KUZUNGUMZA…wapo watu wanasema hiyo sala usiku kucha lakini maisha yao hayageuki, kwasababu haitoki moyoni…na pia yupo asiyeisema hiyo sala lakini moyoni mwake akadhamiria kweli kugeuka na kuacha mienendo yake mibaya kuanzia huo wakati, Sasa mtu kama huyo mbele za Mungu ndiye aliyetubu.
Kumbuka ule mfano Bwana Yesu alioutoa juu ya wale wana wawili tukisoma katika
Mathayo 21: 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. 30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. 31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.”
Mathayo 21: 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.
30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.
31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.”
Unaona hapo?, mimi binafsi kabla sijatubu nilishaongozwa sala ya TOBA mara nyingi, lakini muda mfupi baada ya pale nilirudi katika maisha yangu ya kale ya dhambi…lakini siku moja nilipoona mwenyewe ubaya wa dhambi na kuona umuhimu wa mbingu na YESU KRISTO maishani mwangu, sikuongozwa sala ya toba na mtu yeyote, lakini yale ya nyuma yote nilidhamiria kuyaacha kwa kumaanisha kuyaacha na kuanza kumtazama Mungu, na tangu huo wakati na kuendelea Mungu akawa upande wangu kunishikilia mpaka hivi sasa nimesimama kwa neema zake.
Hivyo kazi ya muhubiri sio kumwongoza mtu sala ya TOBA, hapana bali kumjengea mtu mazingira ya yeye mwenyewe kuchukua uamuzi wa kutubia dhambi zake…kwasababu TOBA halisi inatoka moyoni.
Japo upo wakati mtu atakuuliza nifanye nini ili niokoke? Na hapo unaona kabisa mtu kama huyo amedhamiria kweli KUGEUKA kwa wakati huo, na hafahamu lolote kuhusu mambo ya wokovu, hapo unaweza kumwongoza Sala, na sala hiyo kiuhalisia ni kama tu kumwongezea IMANI, ya kile alichokiamua rohoni mwake..lakini sio tiketi kwamba kwa kupitia hiyo amesamehewa. Hapana alishasamehewa pale tu alipodhamiria kugeuka kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake. Hivyo kama ulihubiri na hukuongoza mtu yeyote sala ya Toba, maadamu umehubiri Neno lililohai la Mungu, haupaswi kuhukumiwa na mtu yeyote, kwasababu huwezi jua tangu huo wakai ni wangapi waliotoka hapo wamegeuka kwa Neno lile au la! hata kama hakukuwa na hata mmoja aliyejionyesha katubu mbele za watu.
AMEN.
Mada zinazoendana:
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
KISASI NI JUU YA BWANA.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
JAWABU LA MAISHA YA MTU.
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
SWALI: Maana yake ni nini Bwana anaposema (Mathayo 19) “Maana wako 1.MATOWASHI-waliozaliwa hali hiyo toka MATUMBONI MWA MAMA ZAO; Tena wako
2.MATOWASHI-waliofanywa na WATU kuwa matowashi; tena wako 3.MATOWASHI-WALIOJIFANYA KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI.Awezaye kulipokea neno hili,na alipokee”.
JIBU: Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa Mungu, wasiojihusisha na mambo ya wanawake,(yaani kuwa na mke au watoto), mfano wa matowashi katika biblia ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo,Barnaba, n huwenda pia Yohana mbatizaji, Danieli na Eliya Mtishbi.
Sasa wapo wa aina tatu, wapo ambao tangu kuzaliwa tumboni mwa mama zao Mungu aliwaumba hivyo, hawana uwezo wa kuzalisha, wengi miongoni mwa hao Mungu amewachagua wawe wakfu kwake…kwa ajili ya utumishi wake.
Kadhalika wapo wengine wamehasiwa, hao ndio waliofanywa na watu kuwa hivyo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni…
Na pia wapo ambao wameamua kujifanya wenyewe kuwa matowashi..hawa hawajahasiwa wala hawana shida yoyote isipokuwa wao wenyewe wameamua kubaki hivyo hivyo wasioe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni yaani wajishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni kwa uhuru zaidi..mfano wa hao ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo, Barnaba.
Na kama Bwana Yesu alivyosema mtu yoyote awezaye kulipokea neno hilo na alipokee alikuwa anamaanisha kwamba “mtu akitaka kuwa hivyo na awe” ila sio lazima kama kama Mtume Paulo pia alivyosema kwa uweza wa Roho katika 1 Wakorintho 7:26-40.
Na pia kumbuka hiyo ni KARAMA watu wa namna hiyo huwa wanaona mke/mume kwao si kitu cha thamani kubwa sana kama kuwa tu karibu na Mungu. Hawajilazimishi wala kutumia nguvu nyingi kufanya hivyo, tofuati na wengi wanavyodhani. Mwanamke aliyejitoa kwa Mungu, kaamua kutojishughulisha na mambo ya mume, huyo naye anatafsirika kama towashi.
Ubarikiwe.
Mada zinaendana:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?
BIBLIA INASEMA ASKOFU ANAPASWA AWE MUME WA MKE MMOJA! JE! WALE WASIOOA KWA AJILI YA INJILI HAWAWEZI KUWA MAASKOFU?
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
JIBU: Inategemea kama hapo kabla alishausikia ukweli au la, kwa mfano kama mtu alishaufahamu ukweli tangu zamani, na hataki kufanya hivyo au anapinga, huyo mtu atahukumiwa…Lakini kama huyo mtu ndio mara yake ya kwanza kuamini na kwa bahati mbaya akafa kabla ya kubatizwa, ataokolewa atafananishwa na yule mhalifu pale msalabani aliyekufa na Bwana.
Lakini Wapo watu baada ya kuujua ukweli, hawataki kuufanya uteule wao na wito wao imara kulingana na 2Petro 1: 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”
Kadhalika biblia inasema pia katika
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. “
Soma tena hapa..
Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”.
Hivyo masuala ya rohoni ni ya kuyatimiza kwa kuogopa na kutetemeka, na sio ya kuyachukulia tu kijuu juu.. Tunapoujua ukweli na mapenzi ya Mungu tunapaswa kuyafanya.
Wafilipi 2:12”…. utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka”.
MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
UCHUNGU WA KUIBIWA.
UAMSHO WA ROHO.
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
SWALI 1:Bwana Yesu aliposema huu mfano alikuwa anamaanisha nini?..
“Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na WATOTO wanaokaa SOKONI,WANAOWAITA wenzao,wasisema,Tuliwapigia FILIMBI,wala hamkucheza; TULIOMBOLEZA,wala hamkulia.MAANA YOHANA ALIKUJA,HALI WALA HANYWI,WAKASEMA,YUNA PEPO.MWANA WA ADAMU ALIKUJA,AKILA NA KUNYWA,WAKASEMA,MLAFI HUYU,NA MLEVI,RAFIKI YAO WATOZA USHURU NA WENYE DHAMBI!” NA HEKIMA IMEJULIKANA KUWA INA HAKI KWA KAZI ZAKE”.(Mathayo11:16-19).
JIBU: Mfano huo ni sawa ni kizazi cha sasa hivi tulichopo tuchukulie tu mfano, Mtu akitokea ni mtumishi wa Mungu kweli, maisha yake yote ameyachagua ni kukaa tu kanisani, au milimani kuomba, hafanyi kazi yoyote isipokuwa ni kuomba tu, na kuhudumu kanisani, hana pesa nyingi, nguo zake sio mpya sana, hana mke, wala marafiki, yeye kazi yake ni kumtumikia tu Mungu basi, kajikana maisha yake yote hataki chochote isipokuwa Mungu kajizuia kila kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni ..Unadhani watu huku nyuma watamchukuliaje mtu kama huyo??..Si ajabu watamwita mlokole masalia, au kalogwa, watasema Mungu hayupo hivyo, Mungu anataka watumishi wake wawe na maisha ya kujifurahisha, kama vile Sulemani, na sio kuwa kama vichaa wa barabarani wasiokuwa na malengo..watamwambia hakika wewe utakuwa umeingiliwa na roho nyingine ambayo si ya Mungu….hivyo hatutaweza kukusikiliza mtu kama wewe maskini wa roho na kimawazo…sisi tunawasikiliza wahubiri wenye malengo, na mafanikio.
Lakini watu hao hao, mfano wakimuona mtumishi wa Mungu kweli labda Mungu kampaka mafuta anahubiri Neno na Mungu katika kweli yote, kambariki na maisha mazuri ya duniani, labda kampa nyumba nzuri, nguo nzuri, kampa familia nzuri, kampa mali nyingi, analo kanisa kubwa, ..utashangaa watasema, watumishi wa Mungu huwa hawapo hivyo, watumishi wa Mungu hawawezi wakawa matajiri, huwa wanakaa tu milimani wanautafuta uso wa Mungu usiku na mchana, na sio kwenye majumba ya kifahari kama watu wa mataifa…..Kwahiyo kwao pia watasema hatuwezi kuwasikiliza nyie matapeli mnakula Fedha za waumini..
Na ndivyo ilivyokuwa katika mfano huo, Mungu alipojaribu kuwapeleka Israeli nabii aliyejikana kwa kila jambo, (Yohana mbatizaji) wakasema mtu wa kawaida hawezi kuishi maisha kama hayo ya kutokula wala kujichanganya na wengine, ni lazima atakuwa anao pepo, Lakini Bwana alipokuja anakula na kunywa pengine akidhani kuwa labda watamsikia na yeye wakamwambia ni mlafi na mlevi, manabii wa Mungu hawawi hivyo…….Ndio mithali hiyo inakuja, walipopigiwa filimbi ili wacheze wakakataa, pengine wanahitaji maombolezo, lakini pia walipoombolezewa hawakulia,..sasa waelewekeje! Kwenye raha hawapo kwenye huzuni hawapo..Na ndivyo ilivyo katika kizazi hiki..hata kipewe ishara gani ya nabii hakitaamini isipokuwa wale tu waliokusudiwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaoamini ..
Ubarikiwe!
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU?
WATU WASIOJIZUIA.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)
SWALI: Yohana hapa anasema Bwana ametufanya kuwa Ufalme na Makuhani Ufunuo1:6 …(Sasa hapa anamaanisha sasa hivi sisi ni wafalme na makuhani au ni katika ule umilele ujao?) na je! ni sahihi kumuita mwanamke kuhani??
JIBU: Ndio sasahivi sisi ni ufalme na makuhani wa Bwana katika roho,..kama vile Bwana Yesu alivyokuwa duniani tangu siku za kuzaliwa kwake mpaka siku za kuondoka kwake,,…tayari yeye alishakuwa mfalme,..Kama unakumbuka wale Mamajusi walimuuliza Herode yuko wapi mfalme wa wayahudi tunataka kumsujudia (Mathayo 2:3)? unaona hapo tangu alipokuwa mdogo tayari ni mfalme, pia Pilato tunaona baadaye siku chache kabla ya kuondoka kwake duniani alikuja kumuuliza Bwana …
Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.
Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?
35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.
Kwahiyo hata sisi tuliookolewa, na kuoshwa kwa damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, ni makuhani na ufalme. Lakini mambo hayo yatakuja kudhihirika katika ulimwengu unaokuja kama Bwana alivyosema ufalme wake ni wa ulimwengu unaokuja!…Na ukuhani wenyewe hautakuwa wa kuvukiza uvumba tena, ule ulikuwa ni taswira ya mambo yatakayokuja yanayofunua kumkaribia Mungu..
Vivyo hivyo na katika huo ulimwengu unaokuja hatutakuwa tu wafalme bali tutakuwa na uwezo kumkaribia Mungu kwa namna ya kipekee mfano wa makuhani, ambao sio watu wote watapewa uwezo huo bali ni wale watakaoshinda tu!.. Na thawabu hiyo itakuwa ni kwa wote…wanawake na wanaume.
Hivyo ukuhani wako mbele za Mungu unautengeneza ukiwa hapa hapa duniani, kwahiyo tunapaswa tukaze mwendo ili tusikose thawabu hizo.
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?
NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO?
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
JIBU: SALA ni neno la ujumla linalojumuisha maombi yote, iwe ya shukrani, mahitaji, ibada, sifa, toba,ulinzi, Baraka n.k…Kwamfano yale maombi ya Baba yetu uliye mbinguni Yesu aliyowafundisha wanafunzi wake….Ni mfano wa SALA.
Kwahiyo unaposhukurau ni sala, unapoomba toba ni sala, unapomba hitaji lolote Kwa Mungu kama chakula, mavazi, nyumba n.k. hizo zote ni sala, unapomshukuru Mungu kwa maombi ni sala, na pia unapomwimbia Mungu sifa kama Daudi alivyokuwa anafanya kadhalika ni sala.
Lakini maombi ya Dua ni tofauti kidogo na sala, kwasababu sala ni Neno la ujumla kama tulivyosema lakini DUA imeegemea sana katika maombi ya MAHITAJI..
Kumbuka pia kuna maombi ya kawaida ya mahitaji haya ni yale ambayo unamwomba Mungu akufanyie jambo Fulani, kama tulivyosema hapo juu kuomba riziki, chakula, pesa, n.k. lakini Dua ni maombi ya hitaji isipokuwa haya yanakwenda ndani zaidi, (na ya masafa marefu) ndiyo yanayohusisha na kuomba rehema, kumsihi Mungu akutendee jambo Fulani ambalo pengine usingestahili kulipata, na dua huwa inaambatana na kujinyenyekeza kwa hali ya juu, na wakati mwingine inahusisha pia na kufunga kwa muda mrefu. Kwamfano unapoomba toba juu ya Kanisa, nchi au familia yako, au ndoa yako kwamba Mungu airehemu kwa makosa Fulani yaliyofanyika, huwezi kwenda kwa maombi ya kawaida tu kama unavyokwenda kumwomba akupe chakula, au pesa, au mavazi, au kazi, hapana hapo utamwendea kwa unyenyekevu, kwa kuomboleza, wakati mwingine kufunga kumsihi Mungu juu ya uovu wa kanisa, au nchi au familia yako ausamehe, sasa hiyo ndio inayoitwa Dua.
Mfano ulio hai tunaweza kuuona kwa Danieli, pale alipoomba DUA juu ya makosa na uovu wa watu wake uliowasababishia mpaka kupelekwa Babeli,
Danieli 9: 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa MAOMBI NA DUA, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. 4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako…………; )
Danieli 9: 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa MAOMBI NA DUA, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako…………; )
Maombi ya namna hii tunaona pia yalifanyika kwa Nehemia, pale alipopata taarifa juu ya uharibifu wa Yerusalemu na maovu ya watu wake yaliyokuwa yametendeka Yerusalemu, aliomba Dua kwa Mungu kwa kuomboleza na kufunga kama Danieli alivyofanya. Soma (Nehemia 1).
Tunaona pia kwa malkia Esta na wayahudi wote walipotangaziwa kuuawa, walijinyenyekeza mbele za Mungu kwa kufunga na kuomboleza kwa ajili ya maangamizi yao, Mungu akasikia dua zako, akawaokoa na maangamizi.
Kadhalika na Daudi mara nyingi alipokuwa akipitia shida, aliingia katika maombi ya Dua kwa ajili yake mwenyewe na Mungu amwepushe na adui zake.(Zaburi 28:2, zaburi 30:8).
Bwana wetu Yesu Kristo pia alikuwa anaomba Dua. Waebrania 5: 7 “Yeye [YESU], siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, MAOMBI NA DUA pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;” Unaona hapo?
Hata sisi pia tunapaswa tuwe watu wa SALA na DUA kwa ajili yetu wenyewe kuomba rehema mbele za Mungu, na kwa ajili ya Kanisa, na kwa ajili ya Nchi ili Mungu aweze kufungua mambo mengine yaliyofungwa mbele yetu. Kwasababu biblia pia imetukumbusha hilo katika:
1Timotheo 2: 1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka DUA, na SALA, na MAOMBEZI, na SHUKRANI, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;”
1Timotheo 2: 1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka DUA, na SALA, na MAOMBEZI, na SHUKRANI, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;”
FAIDA ZA MAOMBI.
MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.
MAOMBI YA YABESI.
ELIYA ALIOMBA KWA BIDII, JE! KUOMBA KWA BIDII KUKOJE?
OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!
MKUU WA GIZA.
MJI WENYE MISINGI.
JIBU: Kuongoka maana yake ni kugeuka au kutubu..Katika habari hiyo tunasoma..
Luka 22: 31 “Akasema [YESU], Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe UTAKAPOONGOKA waimarishe ndugu zako.33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Luka 22: 31 “Akasema [YESU], Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe UTAKAPOONGOKA waimarishe ndugu zako.
33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.
34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Tunaona hapo Bwana alishafahamu kuwa wakati wa mamlaka ya giza umefika, kwa Bwana pamoja na wanafuzi wake katika muda mchache mbeleni watatiwa chini ya yule mwovu, na ndio maana kwa kulijua hilo kuwa wanafunzi wake watashindwa kustahimili majaribu pasipo msaada wake, alimwambia Petro maneno yale, “Nimekuombea wewe ili imani yako isitindike”, kwasababu shetani atakwenda kuwapepeta kama ngano, hivyo inaweza ikawapelekea kuikana Imani mara moja, na kurudi nyuma kuacha kabisa kuambatana na Bwana…
Tena Bwana akamwambia nimekuombea ili Imani yako isitindike pale utakapojaribiwa, na utaona jaribu lile lilikuwa ni kumkana Yesu mara tatu muda mchache baadaye, hivyo kama Bwana asingemuombea angeweza kujinyonga kabisa kama Yuda au kuacha kabisa kuambatana na njia ya Kristo badala ya Kuongoka(kutubu). Utakuja kuona Wale wanafunzi wengine walikuwa tayari katika mashaka ya kuiacha imani..Hivyo Bwana alimchagua Petro ili baada ya yeye kutubu (kuongoka) kwa machozi pale alipata nguvu ya kwenda kuwaimarisha na wale wanafunzi wengine waliokuwa wametawanyika.
Na ndio maana baada ya Bwana kufa Petro ndiye alikuwa anashughulika kuwakusanya wanafunzi wote, hata wakati wa kwenda kuvua samaki wanafunzi wengine walitaka kwenda nae, utaona pia yeye ndiye aliyetoa pendekezo la kuteuliwa mwanafunzi mwingine mahali pa Yuda kadhalika hata katika siku ile ya Pentekoste Petro ndiye alikuwa wa kwanza kufungua kinywa na kuwaeleza watu upya habari ya maneno ya wokovu kwa nguvu nyingi…Kwahiyo Petro alishughulika sana kuwaimarisha ndugu zake (mitume) waliokuwa naye.
Kadhalika hili neno KUONGOKA, limeonekana katika
1Timotheo 3: 2 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)6 WALA ASIWE MTU ALIYEONGOKA KARIBUNI, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.”
1Timotheo 3: 2 “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
6 WALA ASIWE MTU ALIYEONGOKA KARIBUNI, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.”
Sasa hapo neno hilo limetumika kwa mtu aliyetubu hivi karibuni (yaani kumpa Bwana maisha yake hivi karibuni)..Mtume Paulo alitoa maagizo kwamba kazi ya uaskofu inahitaji mtu aliyedumu kwa muda fulani mrefu katika Imani, ili isiwe rahisi kwa mtu huyo kunaswa na mitego ya ibilisi kiwepesi.
Tunajifunza nini?..Kama tu vile shetani alivyowataka mitume kuwapepeta kama ngano, na sisi vivyo hivyo anatutaka leo kutupepeta, na nia yake ni tuikane imani, hivyo wewe kama mkristo ni jukumu lako kudumu katika fundisho la mitume(biblia), na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali, kama maandiko yanavyotuagiza katika (Matendo 2:42 ). Ili uwe na nguvu ya kushinda mawimbi ya shetani.
NINI TOFAUTI YA HAYA MANENO. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
NOTI YA UFALME WA MBINGUNI.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
JIWE LA KUKWAZA
JIBU: Kwanza, ni vizuri kufahamu kubatizwa, ni tendo la rohoni, na linapaswa litoke rohoni, kitendo cha mtu kwenda kubatizwa kwanza anapaswa awe tayari kugeuka [kutubu], kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake, kuacha maisha ya dhambi, na kuanza maisha mapya katika Kristo…
Sasa mtu wa namna hiyo BWANA YESU KRISTO akishaona moyo wake kweli umedhamiria kugeuka, na hajafanya hivyo kama ni desturi za kidini tu ili kutimiza wajibu, sasa moja kwa moja mtu wa namna hiyo anapewa UWEZO WA KUSHINDA dhambi, kwasababu yeye mwenyewe hawezi. soma
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”
Sasa Uwezo huo hauji juu ya mtu kama hajadhamiria kabisa kuacha dhambi zake, ikiwa na maana kudhamiria kuacha ulevi, anasa, uasherati, utukanaji, uongo, wizi na mambo yote yanayofanana na hayo..
Hivyo kitendo cha Kubatizwa kama mtu akizingatia vigezo hivyo, ubatizo ule unakuwa na maana kubwa sana katika maisha yake kuanzia huo wakati na kuendelea, yeye anakuwa ni milki halali ya Kristo YESU. Ile hatia ya dhambi Bwana anaifuta juu yake, na UWEZO wa kushinda dhambi unaachiliwa juu yake..Kwahiyo, kitu anachopaswa kufanya sasa kuanzia huo wakati wa kubatizwa na kuendelea, ni KUTOKUMZIMISHA ROHO WA MUNGU NDANI YAKE….Na hii inakuja kwa kudumu katika usafi wa roho, na kujifunza Neno la Mungu, na kukaa karibu na ndugu wa kikristo wenye Imani moja na wewe.
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?
CHANZO CHA MAMBO.
SWALI: Naomba kufahamu kwanini Bwana wetu Yesu Kristo kwanini amesema “Waandishi na MAFARISAYO wameketi katika KITI CHA MUSA;” basi YEYOTE watakayo watakayowaambia,MYASHIKE na KUYATENDA;LAKINI KWA MFANO WA MATENDO YAO MSITENDE;maana wao hunena lakini hawatendi.Wao hufunga MIZIGO MIZITO na kuwatwika watu mabegani mwao;WASITAKE WENYEWE KUGUSA KWA KIDOLE CHAO.Kwakuwa hupanua HIRIZI ZAO,huongeza MATAMVUA yao”.(Mathayo23:1-5).?
JIBU: Kwanini alisema hivyo sababu ameshaitoa hapo…“hunena lakini hawatendi” hiyo ndiyo sababu akawaambia wanafunzi wake wasitende matendo kama yao.Na aliposema mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa anamaana mafarisayo na masadukayo, wameisoma sana torati ya Musa na ni wepesi kuhukumu kwa kupitia hiyo torati, hivyo wanakuwa kama wawakilishi wa Musa, jambo lolote likitokea mfano mwanamke kafumaniwa kwenye uzinzi ni rahisi kutumia torati ya Musa kuhukumu,.na hali wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanafanya hayo hayo.
Na aliposema wao WANAPANUA HIRIZI ZAO hakumaanisha wao wana hirizi, kama hizi wanazotumia wachawi, hapana! Neno hirizi zamani lilitumika kuwakilisha “kiboksi” kidogo kilichobeba maandishi Fulani madogo ambacho watu walikuwa wanatembea navyo, kama kumbukumbu kila waendapo wasisahau yale aliyoyakusudia kuyafanya au kuyatunza katika maisha yake. Mfano katika dunia ya sasa wanandoa wanavaa pete na kutembea nazo kila mahali,..zile ni hirizi za wakati huu wa sasa, kwamba mtu akiitazama inamkumbusha agano aliloingia yeye na mke wake mbele za Mungu siku ile walipofunga ndoa.
kwahiyo, wana wa Israeli waliamuriwa na Mungu waandike baadhi ya vifungu vya maneno ya torati katika viboksi Fulani vidogo kisha wawe wanatembea navyo popote waendapo, wavivae kama utepe katikati ya macho yao, au mkononi. sasa huo utepe waliokuwa wanauvaa katikati ya kipaji cha uso ndio unaoitwa hirizi.
Tukisoma
(kumbu 6:4-9) “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
Kwasasa jambo hili limezoeleka kuonekana likifanywa na wachawi, lakini asili ya neno hirizi sio uchawi. Kama vile neno kafara lisivyokuwa la wachawi, shetani anatabia ya kugeuza mambo na kuyafanya yawe yake. Isipokuwa sisi wakristo hatufungi hirizi mwilini bali hirizi zetu [sheria za Mungu] tunazifunga rohoni.
Sasa hawa mafarisayo, wenyewe badala ya kuweka utepe mdogo tu(mfano wa kiboksi kidogo cha nchi 2) katikati ya macho yao, wao waliongeza ukubwa wa utepe likawa ni li-boksi likubwa ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu sana,
kadhalika na MATAMVUA yao waliyaongeza, matamvua ni sehemu ya mwisho wa kanzu za wayahudi katika sehemu za mikono, hizo waliamuriwa wazishone wakichanganya na michirizi ya rangi ya samawi(yaani blue), lakini wao wakawa wanashona makubwa kupita kiasi ili waonekane na watu kuwa ni watakatifu zaidi.
Hivyo badala ya hizo hirizi zao kuwa ni za kiasi tu, wao wakaziongeza na kuwa kubwa ili waonekane na watu ni watakatifu zaidi na wanashika sheria zaidi, kadhalika na matamvua yao badala yawe ya madogo kiasi wao wakayafuma na kuwa mafundo makubwa kupita kiasi ili kila mtu atakapowaona waonekane kuwa wanaijua sheria zaidi, ili kuelewa vizuri tazama picha chini…
Huu ni mfano dhahiri, wa viongozi wa kidini na madhehebu na baadhi ya wakristo wa sasa, wanavaa majoho marefu, na misalaba mikubwa, na kubeba biblia kubwa na kujionyesha mbele za watu, nia yao hasaa sio kumtangaza Kristo, hapana bali waonekana na watu kuwa ni watu wa kuheshimiwa zaidi na kuogopwa katika kanisa, nia yao ni kuonyesha vyeo vyao, lakini ndani yao hawayashiki yale wanayoyaonyesha kwa nje.
Hivyo tunafundishwa na sisi pia tusiwe wanafki, kuigiza mambo ambayo sisi wenyewe hatuyatendi ni unafki mbele za Mungu..na itageuka kuwa OLE!! Katika siku ile.
CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!.
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
MELKIZEDEKI NI NANI?