Tunajua kuwa vya Kaisari tunavyopaswa tumpe ni “kodi” lakini je! Na Vya Mungu ambavyo tunapaswa tumpe ni vipi kulingana na Luka 20:25?
Tuanze kusoma mstari wa 21 ili tuelewe vizuri zaidi..
Luka 20:21 “Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli 22 Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo? 23 Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia, 24 Nionyesheni dinari. INA SURA NA ANWANI YA NANI? Wakamjibu, Ya Kaisari. 25 Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, NA VYA MUNGU MPENI MUNGU. 26 Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa”.
Luka 20:21 “Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli
22 Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo?
23 Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia,
24 Nionyesheni dinari. INA SURA NA ANWANI YA NANI? Wakamjibu, Ya Kaisari.
25 Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, NA VYA MUNGU MPENI MUNGU.
26 Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa”.
Nataka tujifunze ni vigezo gani Bwana Yesu alitumia hapo kuhalalisha kuwa Kodi ni haki ya Kaisari, hiyo itatusaidia na sisi kujua vilivyo vya Mungu ni vipi?.. Na tunaona hakutumia kitu kingine chochote isipokuwa ile “Sura” inayoonekana kwenye ile sarafu pamoja na ‘Anwani” inayosomeka pale. Kwani Dinari ile ilikuwa na sura ya Kaisari na Anwani ya Kaisari, hivyo ni haki kuwa mali ya Kaisari.
Sasa kama vya Kaisari vilitambulika kwa sura iliyokuwa inaonekana juu ya Sarafu, ni wazi kuwa na vya Mungu vitatambulika kwa njia hiyo hiyo, Maana yake chochote chenye Sura ya Mungu hicho ni cha Mungu, na anapaswa apewe.. Sasa hebu tusome maandiko yafuatayo..
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.
Umeona?..Kumbe! sisi tumeumbwa kwa Mfano wa Mungu, Nyuso zetu ni nyuso za Mungu, na kama tumeumbwa kwa mfano na Sura ya Mungu basi ni wazi kuwa sisi (yaani miili yetu na roho zetu) ni mali ya Mungu na si yetu! na hivyo ni LAZIMA TUMPE MUNGU VILIVYO VYAKE…Biblia inasema hivyo kuwa sisi si mali yetu wenyewe..
1Wakorintho 6:19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE”
Na tena inasema Miili yetu ni MALI INAPASWA ITOLEWE KWA BWANA..
1Wakorintho 6:13 “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. LAKINI MWILI SI KWA ZINAA, BALI NI KWA BWANA, naye Bwana ni kwa mwili”
Hiyo ikiwa na maana kuwa ni lazima tuitoe miili yetu kwa Bwana, ni lazima tumpe MUNGU vilivyo vyake, Tusipofanya hivyo tutakuwa tunafanya makosa makubwa sana..
Sasa tunampaje Mungu vilivyo vyake?
1.KWA KUOKOKA!
Kuokoka maana yake ni kumkabidhi Bwana roho zetu, kwa kutubu dhambi na kubatizwa kwa maji na kwa Roho.(Marko 16:16). Unapomwamini Bwana Yesu na kumkabidhi maisha yako, hapo umempa Mungu vilivyo vyake, na hivyo utakuwa umeyafanya mapenzi ya Mungu.. kwasababu Utu wako wa ndani umeumbwa kwa mfano wake.
2. KWA KUJITENGA NA DHAMBI.
1Wakorintho 6:13 “…LAKINI MWILI SI KWA ZINAA, BALI NI KWA BWANA, naye Bwana ni kwa mwili” Hapa maandiko yanaonesha dhahiri kuwa “mwili si kwa zinaa bali kwa Bwana ” maana yake mtu anayefanya zinaa inaiharibu mali ya Mungu, ambayo ni mwili wake.. Kwasababu mwili wake umeumbwa kwa mfano wa MUNGU, una anwani ya Mungu!!..
Hivyo si ruhusa kuuharibu kwa zinaa, au kwa pombe, au kwa sigara, au kwa kuuandika tattoo au kwa kuuvisha jinsi mtu atakavyo (nguo za kubana au zisizo za maadili) au kwa mambo mengine yote yanayofanana na hayo..
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba.. Vya Mungu anavyopaswa apewe ni ROHO ZETU, na MIILI YETU. Kwasababu vitu hivyo vina sura na anwani ya Mungu mwenyewe, kama vile dinari iliyokuwa na sura na anwani ya Kaisari.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu?
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
Naomba kufahamu maana ya “sura ya kijiti” katika Marko 12:26.
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Nuru yetu inapaswa iangaze au isiangaze kulingana na Mathayo 5:16 na Mathayo 6:1?
Rudi nyumbani
Print this post
Mwanzo 45:1 “Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. 3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake”.
Nakusalimu katika jina kuu sana la mwokozi wetu Yesu Kristo.
Yusufu baada ya kuuzwa na ndugu zake kwa watu wa mataifa, akidhaniwa kuwa ndio habari yake imeishia pale, lakini kama tunavyoifahamu habari, mambo yalikuwa ni kinyume chake, badala ya kuwa mtumwa akawa msaada na nguzo kubwa sana sio kwa wa-Misri peke yao bali pia kwa dunia nzima.
Lakini nachotaka tuone leo, ni ile siku alipojitambulisha kwa ndugu zake, ambao hawakumtambua siku zote ijapokuwa alikuwa ni ndugu yao kabisa wa damu, utaona siku hiyo Yusufu hakujidhihirisha mbele ya kila mtu tu ilimradi, hakujidhihirisha mbele ya watu wake Misri waliompokea, bali aliwaondoa kwanza wote, akabaki yeye kama yeye pamoja na wale ndugu zake 11 tu.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini iwe vile? Kwani kuna ubaya gani yeye kujifunua mbele ya kila mtu?..Kulikuwa hakuna ubaya wowote, lakini upo ufunuo mkubwa sana nyuma yake, kuhusiana na mpango wa wokovu wa Mungu.
Kibiblia habari ya Yusufu ni picha halisi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye alipokuja duniani kama mfalme, biblia inasema watu wake (Wayahudi), hawakumkubali, bali kinyume chake ndio wakamuua, ili tu asiwe mfalme wao.
Yohana 1:11 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea”
Lakini neema walioikataa ilipohubiriwa kwetu sisi (watu wa mataifa), tuliipokea kwa shangwe, na ndio maana tunaona mpaka sasa Bwana Yesu ndio msingi na ngome ya mataifa yote ulimwenguni. Lakini cha ajabu ni kwamba Yesu ambaye alitoka kwa wayahudi, mpaka sasa hawamtambui, ijapokuwa miaka 2000, inakaribia kuisha.. Bado hawaoni kuwa huyu Yesu ndiye tegemeo la dunia yote, wala hakutakuwa na masihi mwingine atakayekuja kuwaokoa zaidi ya huyo. Hilo hawalioni, ukienda kumuhubiria sasa Rabi wa kiyahudi habari za Yesu, anakuona kama wewe ni kafiri.
Lakini maandiko yanatabiri kuwa, wakati wao wa kurudiwa tena utafika, na Yesu atajitambulisha kwao kwa mara nyingine, macho ya mioyo yao yatatiwa Nuru, wakati huo, wayahudi wote, watalia na kuomboleza kwa maombolezo makuu pale Israeli, watalia sana ni kwanini walimsulibisha Bwana wao na mfalme wao, waliyekuwa wanamsubiria..
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. 12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; 13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. 12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Hapo ndipo neema itarudi Israeli, ambapo inafananishwa ni lile tendo la Yusufu kujifunua tena kwa ndugu zake na kumtambua..Wakalia pamoja.
Lakini kabla hayo yote hayajatokea, ni sharti kwanza, watu wa nyumbani mwa Yusufu “WAONDOLEWE”.
Yusufu hawezi, kuwahudumia wote wawili kwa mpigo..Alikuwa na utaratibu wake. Na ndivyo hata Kristo atakavyofanya pindi neema inarudi Israeli, sisi watumishi wake, (tulio katika mataifa), atatuondoa kwanza, kwa tukio lijulikanalo kama unyakuo, ndio ajifunue kwa Israeli.
Ndugu yangu, kama hujui mpango huu wa Mungu ni kwamba mpaka sasa Israeli imeshakuwa taifa tangu 1948, ni taifa huru linalojitegemea, na hivi karibuni neema hii ya injili itarejea kwao. Hivyo mimi na wewe hatuna muda mwingi, Unyakuo upo karibu, tunachokisubiria hapa ni parapanda tu, hakuna kingine, dalili zote Yesu alizozisema zimeshatimia,(hilo kila mtu anajua) Kama unadhani, dunia itaendelea kuwepo kwa miaka mingine elfu, hilo wazo lifute,
Ikiwa unyakuo utapita leo, maana yake ni kuwa hii dunia itakuwa imebakiwa na miaka saba(7) tu mpaka iishie, na ndani ya hicho kipindi, Israeli itampokea Kristo, kisha mpinga-Kristo atanyanyuka mahususi kupigana nao, na baada ya hapo, Mungu ataiadhibu hii dunia kwa wote watakaopokea chapa ya Mnyama. Kisha Bwana atawaokoa watu wake Israeli, kwa kurudi kwake mara ya pili duniani, na dunia itakuwa imeisha.
Ndugu yangu, angalia maisha yako, angalia unapoelekea, angalia mpango wa Mungu ulivyojidhihirisha wazi mbele yetu, utaendelea mpaka lini kudumu katika dhambi? Au katika maisha ya uvuguvugu?. Ikiwa hujazaliwa mara ya pili ni heri ufanye hivyo sasa katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho. Na mtu anazaliwa mara ya pili kwanza kwa kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha, na pili kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi, na kwa jina la Yesu Kristo, na mwisho kupokea Roho Mtakatifu.
Hivyo ikiwa utahitaji msaada ya Toba, au ubatizo sahihi wa maji mengi, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi nasi tutakusaidia.
Maran Atha.
WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MIHURI SABA
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
Mafundisho maalumu kwa ajili ya waajiriwa: Sehemu 1
“Wewe U Mungu uonaye“
Kwa kuwa tupo katika huu ulimwengu, na hivyo Bwana ametuagiza tufanye kazi za mikono (kwa sisi ambao hatuna huduma ya kudumu madhabahuni kwa Bwana). tumeona ni vema pia tuwe na madarasa, ambayo, yatatupa mwongozo, wa namna ya kuishi katika maisha ya kazi. Na kama tujuavyo, kazi imegawanyika katika makundi mawili
Lakini, watu wengi wameangukia sana katika hilo kundi la pili(Yaani kuajiriwa). Hivyo leo tutaangazia hapo. Kazi ya kuajiriwa maana yake ni kuwa ni sharti mtu awekwe chini ya mwajiri (Boss) wake. Tutatazama kimaandiko, migogoro inayotokea mara nyingi katika kazi za kuajiriwa.
Watu wengi ukiwauliza, shida ni nini? Mbona huna raha na kazi yako? Watakuambia shida ni boss wangu, mwingine atasema haniamini, mwingine atasema ananionea wivu, mwingine atasema ni mbinafsi sana, anawapandisha wengine cheo hanipandishi mimi, mwingine atasema hatujali wafanyakazi, n.k. n.k.
Lakini wewe kama mkristo hupaswi umfikirie kiongozi wako, kwa jicho hilo, kwasababu, hata kama kweli anazo hizo tabia zinazokukwamisha, bado hawezi kuzuia kufanikiwa yako, au maono ambayo Mungu amekuwekea mbele yako.
Embu tutafakari kile Kisa cha Sarai na kijakazi wake Hajiri..Biblia inasema Sarai mwenyewe ndiye, aliyemwambia mumewe Abramu, amwingilie kijakazi wake ili ampatie uzao.. Wazo hilo halikuwa la Hajiri wala Abramu,. Kwa namna nyingine tunaweza kusema, Sarai alikusudia kumpandisha cheo kijakazi wake Hajiri, aonekane na yeye kama ni sehemu ya wake wa Ibrahimu.
Lakini mambo yalikuja kubadilika mbeleni, Hajiri alipoonekana ana mimba, Sarai akaanza kumtesa mama Yule. Na sababu ya kumtesa sio kwamba alimwonea wivu, hapana, bali aliona tabia za Hajiri zimebadilika ghafla hataki tena kuishi kama kijakazi bali anataka kuishi kama mke-mwenza, akiambiwa na Sarai aoshe vyombo anasema embu, niache hujui kama mimi ni mzazi!.
Hivyo Sarai kuona vile akaanza kumtesa, na kufadhaisha, mpaka uzalendo ukamshinda,Yule binti, ikabidi akimbilie jangwani huko akafie mbali. Lakini akiwa njiani, malaika alimtokea, akamwambia unakwenda wapi, akasema ninamkimbia bibi yangu Sarai kwasababu ananitesa nusu aniue,..Malaika akamwambia, Rudi kwa boss wako UKANYENYEKEE..
Tuisome habari..
Mwanzo 16:1 “Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. 2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. 3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. 4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. 5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe. 6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. 7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. 8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. 9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, UKANYENYEKEE CHINI YA MIKONO YAKE. 10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi. 11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako. 12 Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote. 13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, WEWE U MUNGU UONAYE, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye”?
Tafakari kwa umakini hiyo habari..
Rudi ukanyenyekee, Mungu anajua kuwa unateswa, lakini wakati mwingine ni kwasababu ya kukosa kwako unyenyekevu..Rudi, kwasababu Baraka zako haziwezi kuzuiliwa na mtu yeyote kama mtoto utazaa tu, naye atakuwa taifa kubwa..Na kweli Hajiri akatii, japo hapo mwanzo alidhani kuwa Mungu haoni mateso yake..lakini hapa mpaka akasema, hakika “Wewe U Mungu uonaye”
Ndugu uliyeajiriwa, hakuna mtu anamchukia “mnyenyekevu”, usishindane na boss wako, hata kama ni mkali, wala usimkimbie, ukaacha kazi kwasababu za chuki, na fitina n.k., unaweza usipate nyingine nzuri kama hiyo.. bali kuwa tu mtulivu, kwasababu “Yupo aonaye”..Ukidhulumiwa mshahara “Yupo aonaye”.. Baraka zako zipo palepale. Yusufu alinyanyuliwa visa na boss wake wa kike, akawekwa gerezani, lakini mwisho wake tunaujua.
Hivyo zingatia hilo kama mkristo, katika maisha ya kuajiriwa,kuwa mnyenyekevu, ili uifurahie kazi yako.
na Bwana atakubariki.
Shalom.
Biblia inasemaje kuhusu Kazi?
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 3)
Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?
USIISHI BILA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KABISA..
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume, maana yake nini?
Maji ya Zamzam yapo kibiblia?
JE! UNAMPENDA BWANA?
MIEZI 13 YA KIYAHUDI.
Je unajua kwamba kuikaribia dhambi ni “DHAMBI”, Hata tu kabla ya kuifanya?.
Mungu hakumpa tu Adamu maagizo ya kutokula yale matunda ya mti wa katikati…bali pia alimwambia “Asiyaguse yale matunda”..asije akafa. Wengi wetu tunaona tu habari ya “kula” kama kosa, lakini hatujui kuwa Mungu aliwaagiza kwamba hata kuyagusa wasiyaguse, (maana yake wakae mbali nayo).
Mwanzo 3:2 “Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala MSIYAGUSE, msije mkafa”.
Mwanzo 3:2 “Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala MSIYAGUSE, msije mkafa”.
Kumbe hata wangeyagusa tu yale matunda bila hata ya kuyala, bado Wangekufa!!.
Hii ni hatari sana..na inatupa fundisho kubwa sana..
Kwanini Mungu akataze wasiyaguse?..Je kuna ubaya wowote katika kuyagusa???… Jibu ni ndio!… kwasababu chanzo cha dhambi ya kula tunda ni kulishika lile tunda kwanza, (Hawa asingeweza kulipeleka mdomoni kabla ya kulishika) kabla ya kulichunguza chunguza kwanza, kabla ya kulidadisi dadisi, ndipo akaangukia katika ushawishi wa kulila.
Hivyo Mungu aliona chanzo cha dhambi kuwa ni “kushika” ndipo akatoa maagizo kwamba WASIYAGUSE!! Wasije wakafa… lakini wenyewe (Waligusa, na tena wakala) Hivyo ikawa ni makosa mawili yaliyozaa Mauti kamilifu.
Na hata leo Bwana anatuonya tukae mbali na dhambi, tusiikaribie kabisa dhambi, tusiiguse dhambi licha ya kuitenda!!..
Tukae mbali na Wizi kama ya wizi wenyewe kutendeka,…tukae mbali na Ulevi kabla ya ulevi wenyewe kutendeka… tukae mbali na Utukanaji, Uadui, Kiburi, Uasherati, kabla ya kufanya mambo hayo (Wagalatia 5:19-20)… Tusizikaribie kabisa hizi dhambi!!.. tukae nazo mbali maili nyingi sana, kwasababu kitendo cha kuzikaribia tu tayari ni kosa..
leo hii utaona mtu anasema hazini, wala hafanyi uasherati lakini katika simu yake kumejaa picha zinazochochea mambo hayo, kumejaa miziki inayochochoea mambo hayo, kumejaa filamu zi kidunia zenye maudhui hayo ya kiasherati, simu yake imejaa magroup ya mizaha, na uhuni, unaochochea mambo hayo…pasipo kujua kuwa anafanya makosa makubwa kuisogelea dhambi kwa namna hiyo..
Neno la Mungu linasema kwamba tuikimbie zinaa, sio tuishi nayo, au tuikemee!..bali tuikimbie (Soma 1Wakorintho 6:18 )...kama vile Yusufu alivyoikimbia mbele ya mke wa Potifa, na sisi tunapaswa tuikimbia hivyo hivyo Yusufu hata hakukubali kuzungumza na Yule mwanamke..
Lakini ni kinyume chake katika siku hizi za mwisho, utaona binti anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno na mwanaume anayemtaka, kijana anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno ya kidunia na binti anayemtamani, na hata kufanya naye mizaha..Hii ni hatari kubwa!, kumbuka ushawishi wa Hawa kula tunda haukuanzia mdomoni bali mkononi!..baada ya kulishika ndipo ushawishi ukamwingia..
Na sisi tukijishikamanisha na dhambi, basi ni lazima tutazitenda tu!, haijalishi itachukua muda gani ni lazima tutazitenda tu!…Hauwezi kusema umeacha utukanaji, lakini kila kukicha kampani zako ni za watu wanaotukana…ni lazima tu na wewe utatukana, haijalishi itakuchukua muda gani kudumu bila kutukana lakini mwisho wa siku utaishia kurudia matukano tu.
Hauwezi kukaa unasikiliza usengenyaji na wewe usiwe msengenyaji..ni suala la muda tu!, utajikuta na wewe upo kama wao.. Kumbuka Adamu na Hawa waliambiwa “wasiukaribie kabisa ule mti, na hata kuugusa”.. Vile vile na sisi leo hii tunapaswa tusiikaribie miti ya dhambi…wala tusiguse mashina yake wala matawi yake.. maana kugusa ndio chanzo cha kula..
Bwana atusaidie na kutuwezesha katika yote.
Maran atha!
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
MUME / MKE BORA KUTOKA KWA BWANA UTAMWONA UKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,
Nini tofauti kati ya Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:8) na bustani ya Adeni (Ezekieli 28:13 na Yoeli 2:3)
Jibu:Tusome
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa EDENI, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.
Isaya 51:3 “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama BUSTANI YA EDENI, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba”.
Hapa tunaona ikitajwa bustani ya “Edeni” lakini tukisoma mahali pengine tunaona ikitajwa bustani nyingine ya “Adeni”
Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya ADENI, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari”
Yoeli 2:3 “Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na BUSTANI YA ADENI mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao”.
Na pia katika Ezekieli 31:9, Ezekieli 31:16-18, na Ezekieli 36:35 utaona ikitajwa Adeni na si Edeni, swali je kuna utofauti wowote?
Jibu ni la! hakuna utofauti wowote iliyopo kati kati ya “Adeni” na “Edeni”, hayo ni maneno mawili yenye maana moja, sehemu moja biblia imetaja Edeni, sehemu nyingine Adeni lakini maana ni ile ile..Na maana ya neno Edeni au Adeni ni “paradiso ya raha”.
Mungu alipoiumba dunia, alimweka mwanadamu wa kwanza katika bustani ya Edeni, na alikusudia mahali pale pawe Paradiso yake ya milele. Dunia yote ilikuwa ni nzuri, lakini pale Edeni palikuwa ndio kitovu cha utukufu wa mwanadamu.
Lakini baada ya shetani kumdanganya Hawa, ndipo Uovu ukaingia na kusababisha mwanadamu kuondolewa katika bustani ile, na Mungu kuitowesha kabisa!
Lakini Bwana ameahidi kuumba Mbingu Mpya na Nchi mpya (Isaya 65:17), ambayo itakuja baada ya utawala wa miaka elfu kuisha hapa duniani. Katika mbingu mpya na nchi mpya, Bwana ametuandalia mambo mazuri kuliko yaliyokuwepo Edeni, maandiko yanasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Mungu kawaandalia wale wampendao..(1Wakorintho 2:9).
Lakini ahadi hiyo kulingana na Neno lake ni kwa wale waliomwamini Yesu Kristo na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake.
Je umempokea Yesu?..kama bado unasubiri nini?. Mwamini leo na ukabatizwe katika ubatizo na ujazwe Roho Mtakatifu kulingana na Matendo 2:38.
Maran atha.
Bustani ya Edeni ipo nchi gani?
EDENI YA SHETANI:
Je! Ni kweli Yesu alirejesha kila kitu kama pale Edeni?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
MIGAWANYO MINNE (4), YA HUDUMA YA YESU.
Mwanazuoni ni mtu aliyejikita katika utafiti au usomi wa ndani katika tasnia Fulani, lengo lake likiwa ni kupata uvumbuzi wa yale magumu yenye utata au yaliyojificha.. Hivyo mwanazuoni wa biblia ni mtu anayeingia ndani kujifunza Biblia, ili kuieleza katika urahisi zaidi au katika ufasaha zaidi kwa jamii au kutoa majibu ya mambo magumu yaliyo ndani ya biblia.
Mwanazuoni anajitofautisha na mwana-theolojia, kwa namna ya kwamba mwanatheolojia yeye yupo kisomi zaidi, kusoma kanuni na taratibu za kidini, hivyo anapohitimu, anakuwa amepata maarifa yale yale yaliyokwisha kuandaliwa. Lakini mwanazuoni, ni mtu ambaye hafungwi na taratibu, anaweza jitenga, kuchunguza, kusoma kwa ndani na kujua maana ya mambo.
Si kila mwanazuoni lazima apitie vyuo vya biblia.. Mtu akijikita katika kusoma biblia kwa undani na kujua siri nyingi zilizo ndani yake, huyo huitwa pia mwanazuoni.
Vilevile si kila mchungaji ni mwanazuoni. Mchungaji kazi yake ni kulichunga kundi la kulilisha, lakini ni vizuri pia mchungaji yeyote awe mwana-zuoni wa biblia. Kwasababu katika siku hizi za hatari zenye mafundisho mengi potofu, na udanganyifu mwingi wa dini za uongo, kila mmoja wetu hana budi kuwa mwanazuoni(mwanafunzi) wa biblia, ili awasaidie na wale ambao, hawajui kweli ya Neno la Mungu.
Lakini..
Kuna aina mbili za wanazuoni;
Mfano wa hilo kundi la kwanza, ndio wale waandishi na mafarisayo, waliokuwa kipindi cha Bwana Yesu, hawa waliipokea torati kama vitabu vya kidini tu, na kuvikariri, na kutunga hata na taratibu zao nyingine ambazo Mungu hakuwaagiza kabisa.
Walikuwa wanayachunguza maandiko, lakini wanamweka Mungu nyuma, Matokeo yake wakashindwa hata kumwona Kristo katika kila kipengele cha torati walichosoma, badala ya kumpokea wakampinga..Ndipo hapo Yesu akawaambia..
Yohana 5:39 “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. 40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima”
Lakini kundi la pili la wanazuoni ni lile ambalo lina nia ya kuujua ukweli, na kiu yao ni wokovu na sio mashindano au usomi, mfano wa hawa ni wale watakatifu wa Beroya, ambao tunawasoma katika..
Matendo 17:10 “Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. 11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. 12 Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache”.
Mfano tena wa hawa, ni Nabii Danieli.. ambaye pia biblia inatuonyesha alikuwa ni mtafiti (mwanazuoni) aliyekuwa anasoma sana vitabu, na matokeo yake akagundua hesabu ya miaka ambayo wangekaa Babeli, hivyo akajinyenyekeza mbele za Mungu akaomba dua na rehema, na Mungu akamsikia, na kumfunulia zaidi..
Danieli 9:1 “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; 2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini”.
Mwingine ni mtume Paulo ambaye mpaka uzee wake alikuwa anasoma vitabu, soma (2Timotheo 4:13), na ndio maana hatushangai ni kwanini Mungu alimjalia mafunuo mengi namna ile.. mpaka akamuasa na Timotheo naye awe vilevile..
1Timotheo 4:13 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha”.
Zipo faida nyingi za kila mmoja wetu kuwa mwanazuoni, Kama Apolo asingekuwa mwanafunzi mzuri wa maandiko, asingeweza kuwashinda wayahudi ambao walilisumbua sana kanisa la kwanza kwa imani zao potofu..(Soma Matendo 28:24-28).
Hivyo kuwa mwanazuoni huchangiwa na; kwanza kwa kuwa na bidii ya kusoma biblia binafsi, pili kuhudhuria mafundisho ya biblia kanisani, tatu kusoma vitabu mbalimbali vya Kikristo, Nne kusikiliza mafundisho yenye maudhui ya biblia kwenye radio, televisheni na bila shaka, kwenye tovuti kama yetu hii www.wingulamashahidi.org.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyotuhimiza kuwa wasomi/wanafunzi wa biblia..wenye lengo la kujifunza kumjua Mungu, (lakini sio mfano wa waandishi na mafarisayo, ambao lengo lao lilikuwa ni vyeo na ukubwa, na heshima waonekane wanayajua maandiko mengi, wasomi, wakubwa waogopwe). Lakini tukiwa na kiu ya kujua mapenzi ya Mungu katika maandiko, ni bora kwetu na kwa wengine..
Wakolosai 4:6 “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.
Mathayo 4: 4 “Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu”.
Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.
Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?
UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
Biblia ni nini?USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
Gombo ni nini?
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
Wakati ambapo Israeli inapitia manyanyaso makali kutoka kwa wakaanani kwa miaka 20, mpaka yakawafanya wamlilie Mungu kwa nguvu ili awaokoe..Tunasoma kwenye biblia Mungu alisikia kilio chao akawanyanyulia mwamuzi Debora pamoja na baraka..
Hivyo Mungu akawaagiza wana wa Israeli wapange majeshi, ili wakapigane na adui zao, na hakika Bwana atawashindia..makabila mengi yalikubali kupeleka majeshi yao, lakini yapo makabila mengine hayakutaka kujishughulisha na jambo hilo..na hayo si mengine zaidi ya Dani, Asheri, na nusu ya kabila la Manase na Gadi. Haya yote yalikuwa mbali kidogo na eneo la vita, Yaliona kama vile vita haviwahusu wao, hivyo yakawa bize kuendelea na mambo yao..
Waamuzi 5:17
[17]Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake.
[17]Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani,
Na Dani, mbona alikaa katika merikebu?
Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari,
Alikaa katika hori zake.
Kwamfano kama hapo maandiko yanasema Dani alikaa katika merikebu, maana yake ni kuwa alikuwa ni mfanya biashara, aliona kuacha biashara zake za melini, za uchukuzi, na kwenda kujishughulisha na vita, ni upotezaji wa muda, kupigania taifa la Mungu ni kazi kichaa, wacha niendelee na biashara zangu..Na ndivyo hata hayo mataifa mengine yalivyokuwa, yalichowaza ni biashara, na mahangaiko ya hii dunia mpaka Agizo la Mungu likawa halina maana tena kwao, hata utumwa wa taifa lao hawakuuona, mateso na dhihaka taifa lao lilipokuwa linapitia hawakuona kama ni kitu zaidi ya biashara.
Ndipo Debora akaongozwa na Roho kutunga wimbo huo wa kuwashutumu ambao mpaka sasa tunausoma..
Hata sasa, tabia za makabila haya kama Dani zipo miongoni mwa wakristo wengi, ni mara ngapi utamwambia mkristo twende tukashuhudie, kwasababu tumeamuriwa kufanya hivyo na Kristo..lakini atakuambia sina muda, nipo buzy, sina mtu wa kumuacha kwenye biashara yangu…
Anaona biashara yake ni bora kuliko kuokoa roho za watu wanaopotea, huyu ni Dani anayekaa merikebuni..kipaumbele chake ni shughuli za huu ulimwengu, kazi, pesa, ndizo anazozitaabikia kutoka Januari mpaka Disemba, mwaka kwa mwaka, hana rekodi ya kufanya chochote kizuri kwa ajili ya ufalme wa Mungu, lakini yupo tayari kujenga majumba, na mahoteli, na ma-meli ili kutanua wigo wake wa kibiashara..
Ni kweli Mungu anaweza kuokoa watu wake pasipo wewe, lakini vilevile kumbuka Mungu anaweza kubaki na mbingu yake pasipo wewe..usipokwenda mbinguni hakumpunguzii yeye kitu.
Hatushangai hata ni kwanini hili kabila la Dani halionekani miongoni mwa makabila ya Israeli yatakayookolewa siku za mwisho (Ufunuo 7:1-8). Sababu mojawapo ni hii..Na sisi tujichunguze tutambue kipaumbele chetu kwa kwanza ni kipi. Je siku ile tutakuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya Kristo?
Bwana atupe kuliona hili.
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
Hori ni nini kibiblia (Waamuzi 5:17, Luka 2:7)?
Tarshishi ni mji gani kwasasa?
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.
NYOTA ZIPOTEAZO.
Kuna tofauti gani kati ya ‘Mungu’ na ‘Mola’?
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
Tofauti na Kalenda ya Kirumi ambayo ndiyo tunayoitumia sasa yenye miezi 12, Kalenda ya kiyahudi yenyewe inakuwa na miezi 13 kwa mara saba kila baada ya miaka 19. (Yaani katika kipindi cha miaka 19, miaka 7 inakuwa na miezi 13, na miaka 12 iliyosalia inakuwa na miezi 12 kama kawaida), Na miaka yenye miezi 13 ni inakuwa ni mwaka wa 3, 6,8,11,14, 17 na 19 na mzunguko wa miaka 19, unapoisha na unapoanza mzunguko mwingine, basi mgawanyo wa miezi unakuwa ni huo huo, wa baadhi ya miaka kuwa na miezi 13 na mingine 12.
Sasa mwezi wa 13, unaoongezeka juu ya miezi 12 ya kiyahudi ni mwezi ujulikanao kama Adari II, Sasa kabla ya kwenda kuutazama huu mwezi wa 13 wa Adari, hebu tuitazame miezi 12, na rejea zao katika biblia.
Mwezi wa 1: Abibu au Nisani.
Mwezi wa Abibu au Nisani ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiyahudi, mwezi huu unaanza katika mwezi Machi katikati na kuisha mwezi Aprili katikati katika kalenda yetu ya kirumi tunayoitumia..
Mwezi wa Abibu ndio mwezi ambao wana wa Israeli walitoka Misri..
kutoka 13:3 Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa. 4 Ninyi mwatoka leo katika MWEZI WA ABIBU.
kutoka 13:3 Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
4 Ninyi mwatoka leo katika MWEZI WA ABIBU.
Na wakati ambapo Hamani ananyanyuka kutaka kuwaangamiza Israeli yote katika ufalme wote wa Ahasuero, tunasoma wazo hili lilimjia katika Mwezi wa Nisani/ Abibu..
Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio MWEZI WA NISANI, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.
Na pia tunausoma huu mwezi ukitajwa wakati Nehemia alipoingiwa na wazo la kwenda kuujenga Yerusalemu..
Nehemia 2:1 “Ikawa katika MWEZI WA NISANI, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote.”.
Mwezi wa 2: Zivu au Ayari
Mwezi huu unaangukia kati ya mwezi Aprili na mwezi May kwa kalenda yetu tunayoitumia, na ni mwezi wa pili katika kalenda ya kiyahudi.
Mwezi huu ndio mwezi ambao Mfalme Sulemani alianza kulijenga Hekalu la Mungu katika Yerusalemu..
1Wafalme 6:1 “Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika MWEZI WA ZIVU, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana. 2 Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini”.
1Wafalme 6:1 “Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika MWEZI WA ZIVU, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana.
2 Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini”.
Mwezi wa 3: Siwani
Huu ni mwezi wa tatu kwa kalenda ya kiyahudi, lakini kwa kalenda yetu ni mwezi unaoangukia kati ya mwezi Mei na mwezi Juni.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Mfalme Ahasuero, enzi za malkia Esta alitoa ruksa kwa wayahudi kujilipizia kisasi juu ya adui zao.
Esta 8:9 “Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio MWEZI WA SIWANI; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao”.
Mwezi wa 4: Tamuzi
Huu ni mwezi wa Nne katika kalenda ya kiyahudi, lakini kwetu sisi unaanguka katika ya mwezi Juni na mwezi Juni na mwezi Julai.
Mwezi huu katika bibli unaonekana kutajwa mara moja tu katika kitabu cha Ezekieli.
Ezekieli 8:14 “Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia TAMUZI”.
Mwezi huu wa nne umetajwa sehemu nyingine kama kwa namba na si kwa jina (Soma Yeremia 39:1-2, na Yeremia 52:6-7).
Mwezi wa 5: Avu
Huu ni mwezi wa tano kwa wayahudi na kwetu sisi unaangukia kati ya mwezi wa Julai na Mwezi Agosti.. Mwezi huu katika biblia haijatajwa kwa jina bali kwa namba..
Kwamfano tunasoma Ezra aliwasili Yerusalemu katika mwezi wa 5
Ezra 7:8 “Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme”
Na pia katika (2 Wafalme 25:8-10, Yeremia 1:3 na Yeremia 52:12-30)
Mwezi wa 6: Eluli
Huu ni mwezi wa 6 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi wa Agosti na Septemba katika kalenda yetu.
Katika biblia mwezi huu ndio mwezi ambao Nehemia alimaliza kati ya kuukarabati ukuta Yerusalemu..
Nehemia 6:15 “Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa ELULI, katika muda wa siku hamsini na mbili”
Mwezi huu pia umetajwa kwa namba katika kitabu cha Hegai 1:14-15.
Mwezi wa 7: Ethanimu
Huu ni mwezi wa 7 kwa kalenda ya kiyahudi na kwa kalenda yetu unaangukia katika ya mwezi wa Septemba na Oktoba.
Hekalu la Sulemani liliwekwa wakfu katika mwezi huu wa Ethanimu
1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 2 Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika MWEZI WA ETHANIMU, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku”
1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.
2 Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika MWEZI WA ETHANIMU, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku”
Unaweza kuusoma pia mwezi huu katika..(1Wafalme 8:2, Walawi 23:24, Nehemia 8:13-15).
Mwezi wa 8: Buli.
Mwezi huu ni mwezi wa 8 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi Octoba na mwezi mwezi Novemba katika kalenda yetu ya kirumi.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Sulemani alimaliza kuijenga nyumba ya Mungu (Hekalu).
1Wafalme 6:38 “Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika MWEZI WA BULI, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Unaweza kusoma pia habari za mwezi huu katika (1Wafalme 12:32-33, 1Nyakati 27:11).
Mwezi wa 9: Kisleu
Huu ni mwezi wa 9 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi wa Novemba na Disemba katika kalenda yetu ya sasa ya kirumi.
Katika mwezi huu Nabii Zekaria alioneshwa maono juu ya Yuda na Israeli.
Zekaria 7:1 “Ikawa katika mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi wa kenda, yaani, KISLEU”
Mwezi wa 10: Tebethi
Huu ni mwezi wa 10 kwa Wayahudi na kwa kalenda ya kirumi unaangukia kati ya mwezi Disemba na January.
Katika biblia mwezi huu ndio mwezi ambao Esta aliingizwa katika nyumba ya kifalme..
Esta 2:16 “Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake. 17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti”.
Esta 2:16 “Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.
17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti”.
Na ndio mwezi ambao Nebukadreza aliuhusuru Yerusalemu (2Wafalme 25:1, Yeremia 52:4).
Mwezi wa 11: Shebati
Mwezi huu unaangukia kati ya mwezi Januari na mwezi Februari kwa kalenda ya kirumi na katika kalenda ya kiyahudi ni mwezi wa 11.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Zekaria aliona maono tena juu ya Yerusalemu..
Zekaria 1:7 “Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani, mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, nabii, kusema, 8 Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe”.
Zekaria 1:7 “Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani, mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, nabii, kusema,
8 Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe”.
Mwezi wa 12: Adari I.
Huu ni mwezi wa 12 na wa mwisho kwa kalenda za kiyahudi, ambapo kwa kalenda ya kirumi unaangukia kati ya Mwezi Februari na mwezi Machi.
Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.
Kutokana na kuwepo na miaka mirefu na mifupi, Marabi wa kiyahudi katika karne ya 4, wakiongozwa na Rabbi Hillel II, waliongeza mwezi mmoja wa 13, katika kalenda ya kiyahudi ambao waliuita mwezi ADARI II (Adari wa pili).
Lengo la kuongeza mwezi huu ni ili kuziweka sikukuu za kiyahudi katika majira halisia, vinginevyo sikukuu za kiyahudi zingeangukia misimu ambayo sio, kwamfano sikukuu ya pasaka ambayo kwa wayahudi inaseherekewa katika mwezi wa March au April kwa kalenda yetu, kama kusingekuwepo huu mwezi wa 13, basi huenda miaka mingine sikukuu hii ingeangukia mwezi wa 8 kwa kalenda yetu, jambo ambalo lingekuwa halina uhalisia hata kidogo.
Lakini swali ni je!, sisi wakristo tunapaswa kuifuata kalenda ipi?, ya kiyahudi au hii inayotumika sasa ya kirumi?
Jibu ni kuwa Kalenda hazitusogezi karibu na Mungu wala hazipeleki mbali na Mungu, tukitumia kalenda ya kiyahudi, au ya kirumi au ya kichina au hata ya kichaga haituongezei chochote, kilicho cha muhimu ni kuishi kwa kuukomboa wakati kama biblia inavyosema katika..
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”
Na tunaukomboa wakati kwa kufanya yale yanayotupasa kufanya, ikiwemo Kujitakasa, kufanya ibada, kuomba, kusoma Neno, kuifanya kazi ya Mungu kupitia karama iliyo ndani yako kabla ya ule mwisho kufika na mambo mengine yote yanayohusiana na hayo.
Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
Nini maana ya wokovu watoka kwa Wayahudi? (Yohana 4:22)
Yesu alipokuwa nyumbani kwa Yule Simoni mkoma, alitokea mwanamke mmoja na kufanya jambo ambalo lilizua malalamika mengi sana kwa wale waliokuwa pale, kama tunavyoifahamu habari, mwanamke Yule alikuwa na kibweta (kijagi), kilichojaa marhamu(pafyumu), na thamani yake ilikuwa ni kubwa sana, ni sawa na pesa za kitanzania, milioni 6, Mshahara wa mwaka wa mtu anayelipwa vizuri.
Lakini maandiko yanatuambia, mwanamke Yule hakufungua tu kile kifuniko cha kibweta ili aimimine pafyumu kichwani pa Yesu hapana, bali “ alikivunja kabisa”, kwa namna nyingine aliharibifu kijagi hicho, kuonyesha kuwa hii pafyumu haitatumiwa tena sehemu nyingine yoyote, itaishia yote hapa, na hilo ndio lililowafanya wale watu waliokuwa pale walalamike, na kusema upotevu wote huu wa nini?..
Anaimwaga pafyumu yote kama maji, lakini Yule mwanamke hakujali, aliimaliza yote, mpaka nyumba yote ikiwa inanuka pafyumu.
Tusome kidogo..
Marko 14:3 “Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake. 4 Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii? 5 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke. 6 Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;7 maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote. 8 Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. 9 Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake”
Marko 14:3 “Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.
4 Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii? 5 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.
6 Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;7 maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.
8 Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. 9 Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake”
Nachotaka tuone juu ya habari hii, ni kwamba tunaweza kudhani kuwa ni huyu mwanamke tu, ndiye aliyekuwa na kibweta kile cha thamani,..Ukweli ni kwamba wale wote walikuwa na vibweta vyao, isipokuwa tu katika maumbile tofuati.. kuna mahali walivivunja au watavivunja, na kutumia kwa ajili ya vitu watakavyoviona vya thamani..
Hata sasa, kila mmoja wetu anachokibweta chake, ni suala tu la muda.. Utajiuliza, unamtazama msanii Fulani kwenye tv, anamwaga pesa, na kuwapa makahaba, au ananunua gari la kifahari, halafu wewe unaanza kulalamika na kusema upotevu wote huo wa nini, si ni heri angewasaidia maskini, kuliko kutumia kwa anasa.. Usimlaumu kibweta chake ndio amekivunjia hapo.
Leo hii, utaona, mtu kumtolea Mungu, au kusapoti huduma ambazo zinamsaidia kiroho ni ngumu, hata halifikirii.. Lakini mwanawe akitaka kwenda shule, atahangaika kila mahali kumtafutia ada, au akiumwa, anahitaji kwenda kutibiwa India, atauza, gari mpaka shamba, kusudi kwamba aokoe maisha ya mwanawe..Hicho ni kibweta chake amekivunja.
Kuonyesha kuwa kumbe anaweza kupoteza chochote cha thamani kwa ajili ya kitu cha muhimu. Tujiulize, Utasema mimi sina kibweta cha thamani..Ukweli ni kwamba unacho, bado hujaona mahali pa muhimu pa kukimwaga. Wakati utafika tu,.
Tujiulize, vipi kuhusu Mungu wetu..Yesu wetu aliyetuokoa, twaweza kudhubutu kuwa kama huyu mwanamke? Ambaye alikivunjia kwa Bwana?..Hakujua kwa kufanya vile, injili yake itahubiriwa kizazi baada ya kizazi.. Na Yesu ni yeye Yule jana na leo na hata milele.. Kama alimfanyia huyu, anaweza pia akakufanyia na wewe, kwa namna yako..Lakini ni lazima ukivunje kibweta chako kwake..Kumbuka Bwana anasema maskini manao siku zote,..Unafurahi vipi, Bwana akuhudumie, halafu wewe umuhudumii?
Tafakari.
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
1.) DUNIANI (miaka 33 na nusu)
2) KUZIMU (Siku tatu)
3) MBINGUNI (Miaka elfu mbili na …)
4) DUNIANI TENA (Miaka 1000)
Ni vema tukaifahamu hii migawanyo kwa kina ili tujue huduma ya Bwana wetu Yesu sasa ni ipi kwa watu wake.
Bwana aliposhuka duniani, aliishi miaka thelathini na tatu na nusu, ndani ya miaka hii alikuwa na lengo la kuwafundisha na kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika laana ya dhambi na mauti. Na siku ile alipokwenda msalabani, ndipo akakamilisha kusudi hili. Ndio pale aliposema IMEKWISHA. Akiwa na maana kuwa kuanzia huo wakati na kuendekea kila mwanadamu atakayemwamini yeye ni lazima aokolewe.
Kusudi lake la kwanza likawa limekwisha.
Kusudi la pili lilikuwa ni kuzimu.
Pindi tu alipokufa hakwenda mbinguni moja kwa moja bali alishuka kuzimu. Kuzimu ni mahali pa wafu. Hivyo zamani wafu wote waliokuwa wema na waovu, wote walikuwa wapo makaburini, isipokuwa waovu walitengwa mahali pao mbali na wema. Waovu walikuwa katika vifungo vya hukumu. Lakini wema walikuwa sehema salama.
Sasa Bwana Yesu aliposhuka kuzimu, alifanya huduma kwa makundi yote mawili. Kwamfano lile Kundi la waovu alikwenda kulihubiria makosa yao, ni kwanini wamestahili hukumu, Soma..
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Maana yake ni kuwa hata sasa, ikiwa utakufa katika dhambi, ni moja kwa moja utakwenda huku wafu hawa walipo ambapo hapana raha, ndio Jehanamu yenyewe iliyopo chini ya dunia.
Lakini walio wema Bwana Yesu aliwachukua na kuwafungua kutoka katika vifungo vya kaburi, na kuwahamishia mahali pazuri sana pajulikanapo kama peponi.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;”
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;”
Hivyo ikiwa wewe ni mtakatifu ukifa sasa, hutajiona ukishuka makaburini, bali utajiona ukichukuliwa juu, mbinguni. Lakini sio kule Kristo alipokwenda,(huko tutafika baadaye) bali katika mbingu ya katikati, ambayo hiyo utakaa huku ukisubiria ule ukombozi wa miili yetu, Siku ile ya Unyakuo. Ambapo kwa pamoja utaungana na watakatifu walio hai, na moja kwa moja kwenda mbinguni kule Kristo alipo kwenye karama ya mwana-kondoo. Hivyo hudumu hii ya Yesu iliishia pale siku ile alipofufuka.(1Wakorintho 15:51-55)
Hii ndio huduma ambayo mpaka sasa inaendelea ya mwokozi wetu. Alisema mwenyewe maneno haya..
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.
Mpaka anasema ninakwenda kuwaandalia makao, maana yake ni kuwa hapo kabla sisi hatukuwa na makao yoyote mbinguni. Hivyo makao haya ndio ile Yerusalemu mpya, ambayo itashuka kutoka kwa Mungu mbinguni, baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha.
Haya ni makao ya milele, hivyo hatushangai ni kwanini hadi sasa Bwana anatuandalia. Bwana atusaidie tusiikose ile mbingu mpya na nchi mpya ambayo Yerusalemu mpya ipo ndani yake. Ni makao ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Huko tutamashangaa Mungu sana, kwa kipindi kisichokuwa na mwisho.
Huu ndio wakati wa ule utawala wa miaka elfu moja, ambao Kristo atakuja kutawala na watakatifu wake, hapa duniani, ndio kule kurudi kwa pili kwa Yesu Duniani, akiwa kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa Mabwana. Ni wakati wa sabato ya watakatifu wote. Utajiuliza kulikuwa na umuhimu gani Mungu kuipitisha kwanza hii miaka 1000, na sio tuingie moja kwa moja kwenye Yerusalemu yake iliyo ndani ya mbingu mpya na nchi mpya?
Ni kwasababu Bwana anataka kuwahakikishia watu wake kuwa hakuna chochote walichokipoteza pindi walipokuwa wanataabika kwa ajili yake hapa duniani, pindi walipojikana, kwa kuacha kila kitu, na kudharauliwa,.hivyo ili kuwaonyesha hakuna walichokipoteza, atawarudishia hiyo miaka ya raha, na wenyewe watakuwa wafalme na Mabwana duniani. Wakati huo dunia haitakuwa kama hii tena, bali itarejezwa hata zaidi ya Edeni, na amani itakuwepo duniani.(Soma Ufunuo 20:1-4). Watatawala pamojanna Kristo kwa amani na furaha isiyoelezeka.
Ndugu, tukiyaona haya, tunatambua sasa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana. Siku yoyote unyakuo utapitia, mlango wa neema utafungwa, dalili zote zimeshatimia Jiulize Je, umejiandaaje? Au umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu. Na hata kama hatarudi wakati wako. Ukifa leo hii, huko uendako utakuwa ni mgeni wa nani?
Yesu yupo mlangoni kurudi, tubu dhambi zako ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako. Hizi ni siku za mwisho. Tunachokisubiri sasa ni unyakuo tu, dalili zote zimeshatimia.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 3)
Je mbinguni itakuwa ni kuimba tu wakati wote?.
KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.