Swali: Kukaramkia ni nini?
Jibu: Tusome,
2Wakorintho 7:2 “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu. 3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja”
2Wakorintho 7:2 “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.
3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja”
“Kukaramkia” ni Kiswahili kingine cha neno “Utapeli” (ambao unahusisha kuchukua fedha kutoka kwa mtu kwa njia ya ulaghai wa maneno). Mfano wa watu wanaokaramkia watu ni manabii wa uongo, na makristo wa uongo!, ambao wanaweza kutumia chochote kile kudanganya nacho watu, ili lengo lao wapate fedha kutoka kwao. ( Na fedha hizo ndizo zijulikanazo Kama mapato ya aibu, ambayo yanatajwa katika kitabu Cha Tito 1:7)
Katika siku hizi za mwisho manabii wa uongo wanatumia maji, mafuta, udongo na vyote vijulikanavyo kama visaidizi vya upako kulaghai watu, hivyo wanawakaramkia watu na kuchukua fedha zao na mali zao, huku wakiwaaminisha kuwa matatizo yao yameondoka.
Watumishi hawa wa uongo, maandiko yanasema kuwa mungu wao ni tumbo!!..
Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi. 18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; 19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani. 20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”
Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.
18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”
Mitume wa kanisa la kwanza hawakumkaramkia mtu yeyote, ili kupata faida.. Zaidi walihubiri injili kamili yenye kumgeuza mtu kutoka katika dhambi kuingia katika haki kupitia Yesu Kristo.
Na sisi hatuna budi kuwa kama hao, tuifanye kazi ya Mungu bila kumkaramkia mtu yeyote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya ELOHIMU?
Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).
Je jina Eva na Hawa ni sawa?
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.
Rudi nyumbani
Print this post
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu, lihimidiwe.. karibu tujifunze biblia..
Neno la Mungu linasema..
Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”
Faida ya kumlea mtoto wako katika njia inayompasa ni kwamba atakapokuwa mzee hataiacha, na maana yake zaidi ni kwamba hawezi kufikia uzee kabla na yeye kuwa na watoto wake.. hivyo na wajukuu wako pia watanufaika kwa malezi yako wewe kwa mwanao, kwasababu kile mwanao alichokipokea kutoka kwako, na yeye atawafundisha watoto wake, hivyo kizazi chako chote hata cha tatu na cha nne au zaidi ya hapo kitakuwa kitakatifu na cha baraka.
Ukiona kuna shida kwa mjukuu, basi ujue kuwa shida ilianzia kwa bibi au babu, ikaingia kwa mtoto na kisha ikamalizikia kwa mjukuu.. Lakini kama babu au bibi alimlea mwanae katika njia inayompasa, ya kumcha Mungu na kumpenda Mungu, huyo mtoto naye pia ni lazima atawafundisha watoto wake njia hiyo hiyo, na hivyo wajukuu watakaozaliwa basi watakuwa wenye mwenendo mwema wa kumpendeza Mungu.
Tuangalie mfano mmoja wa kwenye biblia wa mtu aliyemlea vyema mtoto wake, na hata mjukuu aliyezaliwa akawa na mwenendo mzuri.
Mtu huyo si mwingine zaidi ya BIBI LOISI, ambaye alikuwa na binti yake aliyeitwa EUNIKE, ambaye ndiye aliyemzaa Askofu Timotheo, mtumwa wa Bwana..
2Timotheo 1:4 “Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; 5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo”.
2Timotheo 1:4 “Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha;
5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo”.
Hapa tunaona Paulo anamwandikia waraka Timotheo, na kukiri chanzo cha imani yake Timotheo, kwamba ilianzia kwa bibi yake Loisi, na hatimaye kwa mama yake aliyeitwa Eunike, na ndipo ikaja kwake, ikimaanisha kuwa msingi wa Timotheo kumpenda Mungu haukuanzia kwake, bali ulianzia kwa bibi yake huko.. Ndio maana ikawa hata vyepesi Timotheo kuiamini injili ya Bwana Yesu na hata kuja kuwa Askofu wa makanisa mengi, na ndiye aliyekuwa pamoja na Paulo mpaka hatua ya mwisho.
Timotheo hakuwa Mwisraeli moja kwa moja, bali mama yake ndiye aliyekuwa mwisraeli, lakini baba yake alikuwa myunani… pamoja na mchanganyiko huo lakini malezi ya bibi yake na mama yake yalimfanya awe mwenye mwenendo bora kuliko vijana wengi.
Matendo 16:1 “Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. 2 Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. 3 Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani”.
Matendo 16:1 “Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani.
2 Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio.
3 Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani”.
Je na wewe kama mzazi un akitu gani cha kuwarithisha watoto wako na wajukuu wako?… je ni elimu tu ndio unayoona ni ya muhimu kwao???….
Nataka nikuambie kama watakuwa na elimu ya kidunia halafu hawana Mungu, basi jua kuwa umewapoteza wanao, haijalishi watakuwa mamilionea huko mbeleni!!.. Bibi Loisi, aliona utukufu wa mjukuu wake mbeleni, na kwamba atakuja kuwa mtumishi wa MUNGU hodari katika kuwavuta watu kwa Mungu, hivyo akaanza kuweka msingi bora kwa binti yake Eunike, na Eunike akamfundisha mwanae Timotheo malezi bora.
Walikuwepo vijana wengi wenye elimu nyakati za akina Timotheo, lakini wapo wapi leo??..walikuwepo vijana mamilionea kipindi cha akina Timotheo, lakini hakuna hata mmoja habari yake tunaisoma leo, lakini Timotheo habari zake tunazisoma na zinawaponya mamilioni ya watu duniani hata leo. Bwana amempa Timotheo kumbukumbu lisilofutika..
Walikuwepo wamama wengi na wabibi wengi nyakati za akina Timotheo, lakini hakuna hata mmoja tunayezisoma habari zake, ila hawa wawili Loisi pamoja na mwanae Eunike, habari zao tunazosoma hadi leo..
Na Mungu ni yeye Yule, hajabadilika..ikiwa na sisi tutatembea katika kanuni zake atatupa kumbukumbu ambalo halitafutika. Ikiwa na sisi tutawalea watoto wetu katika njia zitupasazo basi kumbukumbu letu pamoja na watoto wetu, na wajukuu wetu, na vitukuu vyetu, na vilembewe na vilembwekeze litadumu milele na milele.
Anza kuwafunza watoto wako biblia, wafundishe wamjue Yesu zaidi ya Hisabati, wafundishe wazijue amri za Mungu, na kuwa waombaji na watu wa ibada zaidi hata ya shule za ulimwengu. Ukimfanya Mungu wa kwanza katika maisha yao, na Mungu atawafanya wa kwanza katika mambo yao.
Bwana atubariki sote.
Maran atha.
“Si watu wa kutumia mvinyo sana”, je tunaruhusiwa kutumia mvingo kidogo?(1Timotheo 3:8).
KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?
2Timotheo 1:6 “Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu”.
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.
Neno la Mungu linatufundisha kuzichochea KARAMA tulizopewa,.. Ikiwa na maana kuwa “Kuwa na karamaa pekee haitoshi kuifanya kazi ya Mungu vizuri”..bali inahitajika Karama iliyochochewa. Na anayeichochoea si Mungu, bali ni sisi ndio tunaoichochea.
Mtu anapomgeukia Kristo na kuokoka, tayari Mungu anakuwa ameiweka karama ndani yake, kama mbegu ndogo sana.. Lakini karama ile isipochochewa inaweza kufa ndani ya mtu, na hatimaye mtu yule akabaki kama mtu asiye na karama kabisa.
Hata wanaoshiriki michezo ya kidunia, ijapokuwa wanavyo vipaji vya michezo hiyo, lakini wasipovifanya mazoezi ya kutosha, haijalishi wana vipaji vikubwa kiasi gani, bado vipaji vyao hivyo vitakuwa si kitu. Na vipaji vina muda wake, mwanamichezo akifikia umri Fulani kama hajakitumia vizuri kipaji chake, basi kinapungua nguvu chenyewe, kwasababu tayari umri umeshaenda!.
Na karama za rohoni au vipaji vya rohoni ni ivyo hivyo.. visipochochewa vinakufa na visipotumika katika muda fulani, vinaisha thamani nguvu ndani yake..Ndio maana maandiko yanasema..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. 2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”
Na pia inasema..
1Yohana 2:14 “…..Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”
Sasa maandiko yanasema Bwana alitoa wengine kuwa mitume, wengine manabii, wachungaji, waalimu, wainjilisti, karama za kuponya, matendo ya miujiza, karama za lugha, karama za masaidiano, imani, hekima, maarifa n.k (kasome Waefeso 4:11-12, 1Wakorintho 12). Lakini wengi hawajijui kama wanazo hizo karama.. kwasababu wanadhani zinaanza katika ukubwa wanaotugemea wao.
Wengi sana leo hii ni wainjilisti tangu siku ile wanapookoka, lakini kwasababu hawajijui kama wao ni wainjlisti, pale wanapojiona kuwa hawafanani na mwinjilisti mmoja maarufu, basi moto unazima ndani yao, pasipo kujua kama wanamzimisha roho, wengi ni waalimu tangu siku ile wanapookoka, lakini kwasababu hawajui namna ya kuzitumia karama zao na wanapoona wao si kama waalimu Fulani maarufu wanaowajua basi moto unazima ndani yao, wanabaki kusubiria muujiza siku moja wajikute wamekuwa wahubiri wenye uwezo wa kuhubiri kama watu Fulani maarufu.
Wengi wamepewa karama za kumwimbia Mungu, tangu siku walipookoka lakini kwasababu wanajiona kama sauti zao bado zinakwaruza, kwa kujilinganisha na wengine ambao tayari wanamwimbia Mungu kwa muda mrefu, basi wanatulia huku wakisubiri muujiza mwingine uwashukie utakaowafanya wawe kama hao wengine.
Kungoja huko ndiko kunakuua karama za watu wengi ndani yao.
Leo tutatazama njia 3, za namna ya kuzichochea karama zetu ili zifanye kazi katika viwango ambavyo Mungu amevikusudia.
1.KUJIFUNZA NENO.
Msingi wa karama zote ni Neno la Mungu, mtu aliyepungukiwa Neno la Mungu ndani yake, tayari karama yake inazima yenyewe tu ndani yake.. Kwanini Neno la Mungu??… kwasababu Neno la Mungu linatia hamasa, linatia moyo, linatupa sababu ya kuzitumia karama zetu, linafundisha jinsi ya kuzitumia kupitia mifano mbali mbali ya watumishi wa Mungu ndani ya biblia, na pia linatuonya madhara ya kutozitumia karama zetu. Hivyo Mtu mwenye Neno la Mungu la kutosha ni lazima tu karama yake itanyanyuka.
2. MAOMBI.
Hii ni njia ya pili ya kuchochoe karama zetu, Maandiko yanasesema tuombe bila kukoma (1Wathesalonike 5:17), Na kuomba kunajumuisha pia na kufunga, vitu hivi viwili vinaenda pamoja..tunapoomba Bwana anatuongezea uwezo na upako katika karama zetu.
Mathayo 17:21 “Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.”
3. MAZOEZI.
Hii ni njia ya tatu na ya muhimu sana, chochote kisichofanyiwa mazoezi hakiwezi kuwa bora.. hata karama isipofanyiwa mazoezi haiwezi kuwa bora, maana yake ni kwamba kama wewe una karama ya kuimba, kamwe usitegemee utakuwa bora, bila kuifanyia mazoezi karama hiyo, ni lazima uwe na vipindi vya kuinoa sauti yako, kutafuta na kujifunza jinsi ya kuzipangilia sauti kupitia waliokutangulia au waalimu, huku wewe mwenyewe ukifanya mazoezi ya kurudia rudia mara kadhaa… hivyo ndivyo karama yako itakavyoongezeka nguvu, lakini ukiiacha tu na kujiona tayari unajua kila kitu, basi hutaweza kupiga hatua..
Vile vile kama umepewa karama ya kiualimu, au kiinjiilisti..kama utaketi tu kusubiri kufundishwa, basi kamwe hutaweza kufundisha wengine..unapaswa utenge muda wa wewe kwenda kufundisha wengine, hata kama bado hujui vitu vingi,.. wewe kafundishe hivyo hivyo, Bwana atakufundisha huko mbele ya safari, makosa utakayoyafanya ndiyo yatakuwa darasa lako la kufanya vizuri katika matukio ya mbele..hivyo usiogope, nenda kahubiri..
Vile vile kama umepewa karama ya matendo ya imani, au karama za kuponya, usingoje ngoje.. nenda mahospitalini, nenda sehemu mbali mbali kafanye maombezi huku ukiwahubiria habari za njema za wokovu, usiogope wala kuvunjika moyo, unapoona umeombea watu 10, na hakuna aliyepona hata mmoja.. wewe endelea mbele, hizo ni hatua za awali, katika matukio yanayokuja Bwana atakutumia kwa maajabu mengi.
Na karama nyingine zote ni hivyo hivyo, ni lazima UZICHOCHEE!!..kama vile moto unavyochochewa.
Na ulingo mzuri wa kuiona karama yako ikifanya kazi ni ndani ya KANISA, yaani unapokuwa katika kusanyiko la Kristo ni kipindi kizuri cha kuiona karama yako kuliko unapokuwa nje ya kusanyiko, kwasababu Biblia inasema karama hizi lengo lake la kwanza ni kuujenga mwili wa Kristo, maana yake kulijenga kanisa (Waefeso 4:11).
Ichochee karama yako!
Bwana akubariki.
Nini tofauti kati ya Kipawa na Karama?
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
USINIE MAKUU.
Uzima wa milele ni nini?
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
Mungu kamwe hajatuweka hapa duniani tutafute “dunia njema”, Dunia ambayo tutaishi mbali na hatari, mbali na majanga, mbali ni watu wabaya au waovu, hapana, hili ni jambo ambalo kila mtu aliyempokea Kristo au aliyeokoka anapaswa alijue, hata tujitahidi vipi kutafuta mahali ambapo patakuwa pazuri kwetu bado hatutapaona…
Kwasababu duniani hii ilishaharibika tangu Adamu alipoasi, na iliendelea kuwa hivyo hivyo, na hata sasa itakuwa hivyo hivyo ya hatari hadi mwisho wake, hakuna mahali utaenda au utakaa na kusema hapa hakuna ukinzani, hakuna masumbufu.., ni kitendo cha muda tu, ukiyashazoelea hayo mazingira mapya utavumbua shida nyingine nyingi na hatari zilizopo hapo,ambazo kule hukuziona, nenda kote ulimwenguni ndio uhalisia ulivyo..
Kitu Mungu anachokifanya ni kutufanya tuwe salama katika mazingira haya mabaya, lakini sio kubadili mazingira yawe mbingu kwetu. Anachofanya ni kutuandalia meza, tule tunywe, katikati ya watu waovu, katikati ya wachawi, katikati ya waganga, katikati ya wauaji, katikati ya wapagani.. Lakini tusidhuriwe na wao..Na anafanya hivyo ili tumaini letu liwe kwake tu.
Daudi alilijua hilo akasema maneno haya katika Zaburi..
ZABURI 23
1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. 2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. 3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji 5 WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji
5 WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Umeona, anasema waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu.. Machoni pa wafanyakazi wenzangu wanaonionea wivu, machoni pa wafanya-biashara wenzangu wanaoniendea kwa waganga, machoni pa majirani zangu wanaoniundia visa kila kukicha..Hapo ndipo Mungu anapokuletea chakula chako, anapokuchunga, anapokupa faraja..Kamwe usitazamie atakupeleka mbinguni, kukupa rizki, au Baraka zako.
Usihangaike kumwomba Mungu akubadilishie mazingira akupe mengine, au akubadilishie watu akupe wengine, au akubadilishie majirani, au wafanyakazi, au akuhamishe mahali ulipo akusogeze kwingine kwasababu hapo ulipo ni pabaya sana.. Mungu atakusogeza wakati wake ukifika, lakini fahamu kuwa hata huko uendako, hata hao watu wengine uwakutao, matatizo yanaweza kuzuka hata makubwa kuliko ya kwanza.. Lakini mwombe Bwana katika mazingira yoyote akusaidie,, Hilo linatosha yeye awe mchungaji wako, awe mwamba wako, awe jemedari wako wa vita, ndio maombi anayotaka kuyasikia, na huwa anayajibu upesi, maombi ya namna hii. Mwombe akufanikishe hapo hapo ulipo, akupe amani na faraja hapo hapo ulipo..
Bwana Yesu alimwomba Mungu maneno haya..
Yohana 17:15 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu”.
Si mapenzi ya Bwana, wewe ukae mbali na walimwengu, bali katikati yao, mpaka wakati wa Bwana utakapofika ndio akuondoe na kukupeleka pengine. Wakristo wengi wameathiriwa na mazingira yanayowazunguka, wanapoona hatari nyingi mbele yao au nyuma yao. Badala waweke tegemeo lao kwa Bwana awasaidie watimize mapenzi ya Mungu, wanabakia kuyalaumu mazingira, wakisema, ni kwasababu ya hiki, ni kwasababu ya kile..Yule ananipiga vita ndio maana sina muda na Mungu..Laiti ningeondoka hapa na kwenda kule ningetumika vizuri zaidi n.k…
Ndugu, Dunia hii iliyoanguka haina mahali utakuta pana unafuu, zaidi ya pengine, hapatakuwa na wachawi lakini patakuwa na magonjwa, hapatakuwa na magonjwa lakini patakuwa na uzito kiroho, au mwitikio wa watu kwa Mungu ni mdogo, hapatakuwa na maskini lakini patakuwa na majanga,..Hivyo hatari zipo na zitaendelea kuwepo kwasababu mkuu wa ulimwengu huu yupo kote.
Lakini tukiegemea kwa Bwana, na kumlilia yeye atembee nasi, atulinde, atuokoe, atupe amani, atupe faraja,atupiganie, na sio kuyalaumu mazingira, tutakuwa salama.
Wakati Fulani Mungu alinionyesha usiku katika ndoto, nilijikuta nimeingia katika jumba Fulani, lakini sikufahamu kama ni milki ya adui..Hivyo nikiwa kule nikawa kuzungumza na mama mmoja ambayr alikuwa kama kafungwa, lakini ghafla, mahali pale palibadilika,nikaanza kuwaona watu wanaotumiwa na ibilisi ndani ya mazingira yale, nikagundua uwepo wa pale sio wa ki-Mungu, bali ni milki ya ibilisi, basi nikawa natafuta mlango wa kutoka niondoke, lakini milango yote ilikuwa imepotea, basi nikawa nazunguka zunguka kwenye lile jumba lenye mazingira ya kutisha, kutafuta mlango wa kutokea sioni, kila nikiingia kwenye mlango mmoja, nakutana na chumba kingine, nikifungua kile huku nikitazamia ndio mlango wa kutoka nje, ndio kwanza nazama katika vyumba vya ndani zaidi..
Lakini nikiwa huko ndotoni, nikajikuta Napata hisia nyingine, nikasema Bwana ndiye ngome yangu ninahofu ya nini..Nikasema sitahangaika tena kutafuta mlango wa kutokea, nitatulia tuli, niendelee kumwangalia Bwana wangu, nikasema hapa nitatoka tu nisiwe na hofu..Na muda huo huo ghafla , nikawaona wenzangu wakiwa katika chumba kimoja wapo ndani ya hilo jumba, tukakutana wote tukiwa na amani sana kana kwamba pale sio ndani ya jumba la shetani, tukawa tunakula na kunywa, halafu tukaanza kuimba nyimbo nzuri za kumsifu Mungu, nakumbuka mahali pale niliona uwepo mzuri wa Bwana kana kwamba tulikuwa kanisani,
Na ghafla nikashutuka, ndipo Mungu akanifundisha neno hili..
Zaburi 23:5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Zaburi 23:5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Hivyo tuondoe hofu ya watu, tumtazame Bwana. Na yeye atatuokoa.
Shalom.
Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
YESU ANAKWENDA KUIBADILISHA OFISI YAKE.
SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
Ni miaka mingapi ya njaa Daudi aliyoambiwa achague? Ni miaka 7 au miaka 3?
karismatiki maana yake nini?
Karismatiki ni neno la kiyunani lenye maana ya “Zawadi za neema”.. Au kwa lugha nyepesi zaidi, tunaweza kusema, “vipawa vya neema”. Ambavyo hivyo hutolewa na Roho Mtakatifu mwenyewe na sio mwanadamu. Neno hili utalisikia sana vinywani vya madhahebu mbalimbali ya kikristo.
Ni mkondo ambao ulianza, mwanzoni mwa karne ya ishirini, (1906), kule Azusa Marekani, wakati ambapo dhehebu la Pentekoste lilipoanza. Lililoamini kuwa uthibitisho wa Mungu kuwepo katikati ya watu basi ni kuonekana kwa zile karama za Roho Mtakatifu, ambazo zinazungumziwa katika kitabu cha 1Wakorintho 12.
Kwamba kanisa ili liwe hai, ni sharti vipawa vya Roho kama vile Kunena kwa lugha, kutoa unabii, uponyaji na miujiza, vidhihirike ndani yake. Ikumbukwe kuwa tangu kanisa la kwanza la mitume kupita, vipawa hivi vilionekana kama vimekufa, havipo tena, lakini, viliibuliwa tena na Roho Mtakatifu mwanzoni mwa hiyo karne ya ishirini, ambapo baadhi ya wakristo walikaa chini na kufunga na kumwomba Mungu ajifunue kwa namna hiyo kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume. Na kweli wakiwa katika maombi hayo, Roho Mtakatifu alishuka, watu wengi wakaanza kunena kwa lugha, na karama mbalimbali kuonekana.
Ni jambo ambalo lilikuwa gheni, kwa madhehebu mengi makongwe, ambayo yalikuwa tayari yameshajikita katika mifumo ya kidini kwa muda mrefu. Kama vile Katoliki, Lutheran, Angalican, Moravian n.k.
Hivyo basi mvuto wa vipawa hivi, ulivyoendelea kuwa mkubwa, mpaka kufikia miaka ya 1980, madhehebu mengine mengi yakaanza kurithi mfumo huu wa karismatiki, ikiwemo dhehebu kama Katoliki, ( wakaitwa Karismatiki Katoliki), mengine ni Lutheran, na Anglikana, n.k. ijapokuwa yamekuwa na upishano kati ya wao kwa wao katika mifumo ya imani hii .
Hivyo kwa ufupi tunaweza kusema kanisa lolote linalosisitiza udhihirisho wa vipawa/karama za Roho, kama vile uponyaji, unabii, kunena kwa lugha, huitwa Kanisa la Karismatiki.
Ni nini tunapaswa tufahamu kuhusu vipawa vya Roho(Karismatiki).
Ni kweli kanisa linalokosa vipawa hivi, ni kanisa lililo nusu-mfu, au mfu kabisa. Kwasababu Mungu sio sanamu, ambaye anapokea tu ibada, lakini hatoi vipawa/zawadi kwa watu wake. Hayupo hivyo. Lakini pia ukengeufu mkubwa umeingia na kuvichafua vipawa vya Mungu, ikiwa na maana, kuwa mkristo usipokuwa makini utajikuta unapokea Roho nyingine na sio Yule wa Mungu.
Ni kuwa makini katika siku hizi za mwisho, wimbi kubwa la manabii wa uongo, linazukia huku, mafunuo yasiyo ya ki-Mungu yanaibuka na kuwapoteza watu kutoka huku, matumizi ya visaidizi kama maji, na chumvi za upako, vimewapoteza wengi,..Hivyo kumetokea mvurugano mkubwa sana. Mtu atanena kwa lugha leo, kesho atakwenda kuzini, jiulize ni roho gani ameipokea huyo?
Ni nini tunapaswa tufanye?
Nyakati hizi za mwisho, Tujitahidi sana kuitegemea BIBLIA kwa kila kitu tunachokitenda, au tunachoongozwa kukifanya, Ikiwa ni karama hakikisha haikinzani na kanuni za msingi za Neno la Mungu, hiyo ndio njia pekee ya kuthibitisha kuwa kipawa hicho ni cha ki-Mungu. Lakini nje ya hapo utapotea. Ikiwa utapokea ufunuo, au unabii, usiupokee tu, ilimradi ni fulani kasema, kisa kaona maono, hakikisha kwanza katika biblia, Je! Ndivyo ilivyo? Au La!. Kwasababu shetani ameingilia sana mikusanyiko mingi, ajaribu kuiangusha kwa namna hii.
Haiwezekani, useme mimi nimepokea Roho Mtakatifu, ninanena kwa lugha, ninaimba kwa Roho, Halafu anakuacha uendelee kuabudu sanamu la mtakatifu Fulani,sanamu la Mariamu au uombe sala za wafu. Huyu sio Roho Mtakatifu, haijalishi atajiita ni Karismatiki namna gani.
Hivyo ni kuwa makini, tusije pokea roho nyingine isiyokuwa ya Mungu. Hizi ni zama za uovu.
1Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
SEMA KWA LUGHA NYINGINE.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.
Jina kuu la Bwana na Mwokozi wetu Yesu KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia.
Sarepta ulikuwa ni mji mdogo uliokuwepo nje kidogo mwa nchi ya Israeli, katika Taifa la Lebanoni.
Katika biblia tunasoma kipindi Nabii Eliya amefunga Mbingu miaka mitatu na nusu kwa Neno la Bwana, aliongozwa aende mpaka mji huu wa Sarepta ambapo kulikuwepo na Mwanamke ambaye Bwana alikuwa amemwandaa ili amlishe.
Mungu angeweza kumshushia Nabii Eliya mana kutoka mbinguni na akala akashiba, lakini hakufanya hivyo, bali alitumia watu na viumbe kumlisha wakati dunia nzima inapitia njaa. Mara ya kwanza alitumia kunguru (1Wafalme 17:4), na mara ya pili akatumia Mtu (ambaye ndiye huyu mwanamke wa Sarepta).
Sasa huyu mwanamke wa Sarepta alikuwa na tabia ya kipekee ambayo kupitia hiyo tunaweza kuvuna hekima ya mafanikio ya kimwili na kiroho.
Inawezekana mambo yako hayaendi sawa, inawezekana unapitia kipindi kigumu sana cha mbingu kufungwa juu yako, kila mahali unapogusa hapaendi, kila unalojaribu halifanikiwi, kila mahali ni ukame!!
Kama unapitia hii hali, basi usiende kutafuta kuombewa! Bali fanya kama alivyofanya huyu mwanamke wa Sarepta.
Ukifanya kama alivyofanya huyu mwanamke wa Sarepta, basi kipindi ambacho wengine watakuwa wanalia matatizo na dhiki, wewe hutakuwa katika hayo matatizo wala hizo dhiki..
Sasa ni kitu gani alichokifanya huyu mwanamke mpaka kufikia hatua ya yeye kuishi vizuri katikati ya vipindi vya shida na njaa na mauti?
Hebu tusome habari yake kwa ufupi kisha tujifunze tabia aliyokuwa nayo.
1Wafalme 17:7 “Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi. 8 Neno la Bwana likamjia, kusema, 9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe 10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi. 15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya”.
1Wafalme 17:7 “Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
8 Neno la Bwana likamjia, kusema,
9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe
10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.
12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.
14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.
15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.
16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya”.
Umeona tabia ya huyu mwanamke?.. alikubali kutoa chakula chake kipindi ambacho amebakiwa nacho kidogo!!.. kipindi ambacho hajui kesho itakuwaje.. Alikubali kuweka sababu zake kando ilimradi tu aone Neno la Mungu linazidi kusambaa kupitia mtumishi wake, aliona mtu wa Mungu, au kazi ya Mungu ina thamani mara nyingi zaidi ya kazi zake yeye au uwepo wake yeye na mwanae.
Hivyo akajitoa sadaka maisha yake.. akijua kuwa hata kama atakufa na njaa yeye na mwanae lakini atakuwa na thawabu kubwa mbinguni, atakuwa hajaifanya kazi ya Mungu isimame… Hicho ndicho kilichomfanya Mungu ayaangalie matatizo yake, na kumfungulia Mbingu wakati wengine bado mbingu zimefungwa.
Na Mungu ni yeye Yule jana, leo na hata milele hajabadilika (Waebrania 13:8).. Ukitaka Bwana ayaangalie mambo yako, basi wewe weka kando mambo yako na shida zako, na anza kujishughulisha na mambo yake..
Hii ndio shida kubwa inayowakabili wakristo wengi, huwa wanatanguliza matatizo yao mbele za Mungu na huku hawataki kumjali Mungu katika maisha yao.. wanatafuta kuombewa mambo yao yakae sawa, lakini kutafuta kuyaweka sawa mambo ya Mungu hawataki..
Watamwambia Mungu, tazama mwanangu hajala, mwanangu hana ada ya shule, mwanangu yuko hivi yuko vile, mimi sina chakula, mimi sina kazi, mimi sina hiki au kile..(wanakuwa ni watu wa kujijali wao) na hawana habari na mambo ya Mungu au kazi ya Mungu, wakidhani kuwa kwasababu Mungu ni muweza wa mambo yote, hivyo hahitaji kupewa chochote au kufanyiwa chochote.
Ni kweli yeye ni mweza wa yote, na hahitaji kufanyiwa chochote, lakini wakati mwingine anafanya hivyo kutujaribu upendo wetu kwake,.. angeweza kumshushia Eliya Mana kama alivyowashushiwa wana wa Israeli jangwani lakini hakufanya hivyo kwa Eliya, bali alimpeleka Eliya kwa huyu mwanamke, ili aujaribu upendo wake kwake.
Wengi wetu hatujui kuwa Mungu anafurahiwa sana na matoleo yetu kipindi ambacho hatuna kitu zaidi ya kipindi ambacho tuna kila kitu. Utasema hilo tunalithibitisha vipi kimaandiko?… Rejea ile habari ya Yule mwanamke mjane aliyetoa riziki yake yote katika sanduku la hazina…Utaona baada ya kutoa Bwana Yesu anamsifia, na tena anasema katoa zaidi ya wote, kwasababu hao wengine walitoa katika sehemu zilizowazidi…
Marko 12:41 “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; 44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia”
Marko 12:41 “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia”
Kwaufupi huyu mjane, hakubakiwa na kitu, huenda alijua baada ya kutoa vile atakaa siku kadhaa na njaa… lakini akiwa katika hiyo hali, Bwana Yesu alimsifia.. huenda baada ya pale, alishangaa kwa milango ya Baraka iliyofululiza mbele yake.
Na wewe ukitaka Mbingu zifunguke juu yako, usianze kutoa visababu katika kumtolea Mungu, usianze kusema sijalipa kodi, usianze kusema sina chakula, sijalipa ada, sijafanya hiki, sijafanya kile, ngoja nikusanye kidogo nitakapopata nitatoa.. Ni kweli siku ukipata na kutoa basi Bwana atakubariki, hataacha kukubariki!!!… lakini hujui tarehe wala siku mambo yako yatakapokuwa sawa..
Walikuwepo wanawake wengi sana kipindi cha Eliya wenye matatizo ya chakula kama huyu wa Sarepta, ambao na wenyewe pengine walikuwa wanafunga na kuomba Mungu awape riziki kwasababu ya ukame…lakini Eliya hakutumwa kwao kwasababu hizo hizo, huenda angeenda kwao na kuwaambia wampe yeye kwanza mkate, wangemfukuza kwa mawe, tena wangemtukana…
Wangesema hatuwezi kuona watoto wetu wanakufa njaa halafu tukupe wewe mzee chakula chao, wangetumia hata na maandiko kuthibitisha hilo.. Kwaufupi kila mmoja angeeleza shida zake na sababu zake kwanini asingempa Eliya mkate.. Ndicho Bwana Yesu alichokisema katika Luka 4:25.
Luka 4:25 “Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni”.
Luka 4:25 “Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima;
26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni”.
Na sisi pia tukitaka mbingu zifunguke juu yetu kabla ya wakati wake, hatuna budi kumjali Mungu zaidi ya kujijali sisi, hatuna budi kuyatazama mambo ya Mungu zaidi kuliko mambo yetu. Hii ni moja ya kanuni za Mafanikio.
Bwana Yesu atubariki.
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
Makanda ni neno lingine la KAPU.
Ambalo hutumika kuhifadhi au kubebea vitu mbalimbali hususani vyakula au nafaka.
Katika biblia Neno hilo utakutana nalo katika vifungu kadha wa kadha, mfano wapo ni hivyo ni hivi;
Mathayo 15:37
[37]Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.
Marko 8:8
[8]Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.
Luka 16:6-7
[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. [7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini.
[7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
Luka 16:5-7
[5]Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? [6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. [7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
[5]Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?
Ni nini twapaswa kujua nyuma ya makanda ya mikate waliyoyakusanya wanafunzi wa Yesu ambayo baadaye waliyasahau mpaka wakaanza kulalamikiana na kulaumiana..Hadi Yesu akawakemea..(Marko 8:14-21)
Ni kwamba waliweka mioyo yao katika makapu yao, katika hazina zao, hata waliposahau wakapaniki.
Ni hali iliyopo sasa miongoni mwetu sisi, tuliookolewa. Tunafikiri sana makapu yetu yana nini, kwa miezi 10 mbele, kwa miaka 3 ijayo..na pale tunapopungukiwa hata uhusiano wetu na Mungu unakufa..Lakini Bwana Yesu anatuambia tusiwe wasiwasi, wala tusiyasumbukie hayo..bali tuutafuta kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine atatuzidishia..kwasababu maisha ni zaidi ya chakula.
Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)
JE! UNAMPENDA BWANA?
Mtu akizaa watoto mia, lakini nafsi yake haikushiba mema;
MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA- Sehemu ya 2.
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
Ulishawahi kujiuliza ni nini Mungu anafundisha wana wa Israeli nyuma ya agizo hili? Tunalolisoma katika Kumbukumbu 22:6
“Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.
Bwana aliwapa agizo, endapo mtu yeyote akipita, njiani au karibu na kichaka, kisha akakutana na kiota cha ndege koo kimelala pale karibuni, kinatekeka kirahisi, kiasi kwamba unaweza kuwachukua wote, bila nguvu yoyote.Basi hapo, walipewa sharti, wasiwe na tamaa ya kuwachukua wote, bali wamwache koo aende zake akaendeleze uzao, lakini wale makinda anaweza kuwachukua na kuwafanya wake. Hivyo kwa kitendo hicho tu, mtu anajiongezea siku za kuishi duniani.
Ufunuo wake ni upi Katika Ukristo na katika maisha?
1) Katika Maisha.
Ni mara ngapi tunaona watoto wa jamaa zetu, wamekuwa mayatima, au wazazi wao wapo katika hali ya kutojiweza kupitiliza, mpaka wanashindwa kuwamudu watoto wao, lakini sisi tunapita hatuna muda nao kisa tu sio sisi tuliowazaa . Tunawaona watoto wale wakiangamia pamoja na wazazi wao. Bwana anatushauri, tusifanye hivyo, ni heri tusiwajali wale wazazi, tuwaache, tusiwape kitu chochote, lakini wale watoto tuwahurumie, kwani tukifanya hivyo, Mungu atatubariki na kutuongezea siku za kuishi duniani.
Watu wengi tunadhani, kuwaheshimu tu wazazi, ndio tunapata siku nyingi za kuishi, lakini ukweli ni kwamba, ukiwajali pia watoto wa asiyejiweza, utajiongezea siku pia za kuishi duniani.
2) Katika ukristo.
Vilevile katika ukristo. Ipo mikusanyika mingi, Yapo makanisa mengi, zipo huduma nyingi, ambazo haziwaweki watu katika mstari wa wokovu wa kweli, viongozi wao ni vipofu, hivyo na wale wanaoongozwa pia watakuwa ni vipofu, na mwisho wa siku wote watatumbukia shimoni. Sasa ikiwa wewe ni mchungaji au mkristo, na unaona mwenzako mahali alipo anapotezwa..Usikae kimya, na kusema wale sio washirika wangu, au wale sio wa dhehebu langu, au wale sio wa dini yetu..Bali unapaswa kuwaeleza ukweli, uwavute katika mahali sahihi ili uokoe roho zao..
Yawezekana ikawa ni ngumu kumgeuza kiongozi, hivyo usihangaike naye sana ikiwa utashindwa kumfikia, lakini wale makinda hakikisha unawajuza njia sahihi. Hiyo itakuongezea siku zako za kuishi hapa duniani.
Katika siku hizi za mwisho, watu wengi wamewekwa sehemu za hatari, wengine wameaminishwa katika watu, wengine vitu, wengine katika dini, wengine taasisi..lakini Kristo hayupo kabisa mioyoni mwao. Hawamjui, hawalifahamu Neno, hawajui nyakati wanazoishi, dini walizopo ni za kipagani. Sasa hii ni hatari sana, tunapoona wakiendelea katika kudanganywa na viongozi wao ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao. Hivyo sisi tuwe wa kwanza kulihubiria hili kundi la Mungu, litoke huko lirudi kwenye Neno.
Bwana atusaidie shalom.
KOIKOI ANGANI AJUA NYAKATI ZAKE ZILIZOAMRIWA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Thenashara ni nini? (Marko3:16)
Biblia ina Aya ngapi?
Jibu: “Sura, na Mlango” ni Neno moja. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66, na kila kitabu kina milango yake (sura zake), na kila sura zina aya zake, na kila aya ina mistari yake.
Kwamfano kitabu cha kwanza cha Mwanzo kina Sura hamsini (50), na kila Sura ina mistari yake.. Kwamfano Sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo ina mistari 31.
Kwahiyo tukiuliza biblia ina Sura ngapi, jibu lake ni kuwa ina sura nyingi kufuatana na Vitabu vyake. Jumla ya sura zilizopo katika vitabu vya Agano la kale ni 929, na sura zilizopo katika vitabu vya Agano jipya ni 260, Hivyo jumla ya milango/sura zote za vitabu vyote vya biblia ni 1,189.
Je unafahamu kuwa huwezi kuielewa biblia kama hujapokea Roho Mtakatifu?.. Ili uielewe biblia ni lazima umpate Roho Mtakatifu na kanuni ya kumpokea Roho Mtakatifu ni kumwamini Yesu Kristo kwanza kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kisha kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha kabisa, na baada ya hapo kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo na hapo Roho Mtakatifu atakuja juu yako.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
Kuna Mbingu ngapi?
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
Nini maana ya tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu?
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Shalom
Hii ni sehemu ya pili ya maswali na majibu yahusuyo ndoa.. Sehemu ya Kwanza unaweza kuisoma kupitia link hii >> MASWALI-NDOA
SWALI 01: Je Mkristo anaruhusiwa kuoa mtu wa Imani nyingine? Yaani akafunga naye ndoa tu, na kila mmoja akaendelea na imani yake.
Jibu: Ndoa ya kikristo ni ndio inayohusisha Imani moja, Bwana mmoja, Roho mmoja, tumaini moja, Ubatizo mmoja na Mungu mmoja..
Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”
Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”
Kwahiyo kabla ya Ndoa ni lazima wawili hao wafikie kuwa na imani moja, na ubatizo mmoja na Roho Mmoja na Mungu mmoja, wasipofikia huo umoja basi hiyo sio ndoa ya kikristo.
Sasa nini cha kufanya endapo ikitokea mmoja si wa imani ya kikristo?, Jibu: Huyo ambaye tayari kashaokoka anapaswa amhubirie mwenzake habari za Wokovu kwanza, na aamini na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu (kwaufupi awe mkristo aliyesimama kweli kweli) na baada ya hapo ndipo wafunge ndoa, lakini kumbuka, si abadilike kwasababu tu anataka kuoa au kuolewa!, hapana bali anapaswa apate badiliko la kweli kiasi kwamba hata kama asipoolewa na huyo basi bado Kristo atabaki kuwa Mwokozi wake siku zote za maisha yake.
SWALI 02: Je kuna umuhimu wowote wa kupima afya kabla ya kufunga Ndoa?
Jibu: Ndio upo umuhimu wa kufanya hivyo kama kuna huo ulazima. Kuhakikisha afya zenu zipo sawa kabla ya kufanya lolote, maandiko hayajakataza kufanya hivyo. Na endapo ikitokea mmoja kakutwa na maradhi ambayo yatawafanya wawili hao wasiweze kukutana kimwili!.. Basi hapo ni uchaguzi wa Yule aliye salama, kama upendo wake ni mwingi kama ule wa Kristo, anaweza kuishi na huyo anayemchagua, lakini kamba si hawezi basi yupo huru kutafuta mwingine aliye chaguo lake hafanyi dhambi.
Lakini kama tayari wameshafunga ndoa na mmoja akapata maambukizi ya maradhi hayo basi Yule aliye salama hapaswi kumwacha huyo aliye na maradhi, wataendelea kubaki pamoja siku zote. Vile vile kama mmojawapo kapata ulemavu ambao utamfanya asiweze kabisa kukutana na mwenzake basi Yule aliye mzima pia hapaswi kumwacha mwenzake aliye na udhaifu, siku zote za maisha yake.
SWALI 03: Je wakristo wanaruhusiwa kutoa Ujauzito (Mimba)?
Jibu: Mkristo haruhusiwi kutoa ujauzito (mimba), kwasababu yoyote ile isipokuwa ya kiafya kwa maelezo ya madaktari:
Kwamfano Ikitokea mtoto kafia tumboni hapo ni lazima ile mimba changa iondolewe ili kuokoa maisha ya mama, vile vile ikitokea itilafu katika tumbo la mama, ambayo ili mama awe salama (asipoteze maisha) na kama mama huyo hana imani ya kutosha ya kuamini kuwa anaweza kuishi bila kuitoa na akawa salama, na hivyo akakubali itolewe kufuatia maelezo hayo ya daktari, mama huyo hafanyi dhambi!, kwasababu ya usalama wake mwenyewe.
Lakini sababu nyingine yoyote ya kutoa mimba tofauti na hiyo ya kiafya, ni dhambi!..Kwamfano mwanamke kapata ujauzito bahati mbaya na alikuwa hana mpango wa kuipata hiyo, hapo hapaswi kuutoa huo ujauzito, au kapata ujauzito kwa njia ya ukahaba, hapo hapaswi kuitoa hiyo mimba, atabaki nao mpaka hatua ya kujifungua.
SWALI 04: Ni nani mtu sahihi wa kumpelekea matatizo ya ndoa? Endapo kukitokea kutokuelewana?
Jibu: Endapo kukitokea kutoelewana, ni vizuri kuomba kwa Bwana suluhisho na kurejea biblia kujua ni nini biblia inasema kuhusu hali hiyo, lakini kama bado mwanandoa anahisi anahitaji msaada zaidi basi anapaswa ayafuate makundi yafuatayo.
1: MCHUNGAJI WA KWELI WA BWANA:
Si wachungaji wote ni waaminifu, lakini pia wapo walio wa kweli na waaminifu, watu hao ni kituo bora cha kupata ushauri wa kiMungu na maombezi.
2. MZAZI:
Kama unaye mzazi aliyeokoka basi hicho pia ni kituo bora sana cha kupokea mashauri bora..na yenye msingi mkubwa.
Kamwe usitafute ushauri kwa marafiki, majirani, ndugu wa mbali, au watu usiowajua kuhusiana na mambo ya kindoa.
SWALI 05: Endapo nikagundua baada ya kufunga ndoa Mwenzangu ana matatizo katika uzazi wake (hana uwezo wa kuzaa au kuzalisha)..Je naweza kwenda kupata mtoto nje na kuendelea kuwa naye?
Jibu: Kama mwanandoa mmoja anamatatizo ya uzazi yanayomfanya asiweze kuwa na mtoto, hapo mwanandoa mwingine asiyekuwa na matatizo hayo hapaswi kumwacha Yule mwenye matatizo, wala kuondoka na kwenda kupata mtoto wa kando, atabaki naye huyo huyo siku zote za maisha yake, huku wakimwomba Bwana awafungue!.
Na kama ni mapenzi ya Bwana wao kuwa na watoto, basi Bwana atawapa mtoto haijalishi ni miaka mingapi itapita (Ibrahimu na Sara walipata watoto katika uzee), na Mungu ni Yule Yule hajabadilika.
Lakini pia kama wanaona ahadi za Mungu bado zipo mbali wanaweza ku-adopt mtoto/watoto na kuwalea kama watoto wao.. Vipo vichanga vingi visivyo na wazazi, na mtu akiwalea hao mbele za Mungu ni zaidi hata ya Yule mwenye watoto 100 waliotoka katika uzazi wake.
SWALI 06: Je mkristo anaruhusiwa kupanga uzazi?
Jibu: Ndio wakristo wanaweza kupanga idadi ya watoto wanaotaka kuwa nao!. Biblia haijatoa amri ya kuzaa idadi ya watoto 10 au 50, ni kila mtu atakavyotaka yeye. Lakini imetoa tu angalizo kuwa tuwe watu wenye uwezo wa kuwatunza wakwetu (1Timotheo 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.)
Kwahiyo ni lazima Mkristo awe na uwezo wa kuwatunza watoto wake, hivyo ni lazima awe na uzazi wa mpango.
MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA-1
MAFUNDISHO YA NDOA.
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
TOFAUTI YA MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU NI IPI?
Je ni viatu gani Musa aliambiwa avivue? Vya mwilini au vya rohoni? (Kutoka 3:5).