Malaki 4:5 kama inasema “ angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”
Kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko ( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto.
Hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati pamoja na wote wanaoujia torati na kuifuatilia (ambao ndio mababa wa Torati) ili waiamini injili ya Kristo.
Na tonaona…Baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe Yohana, waliiamini Injili yake na baadaye hao hao wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, (mfano Andrea na Yohana) ambao walikuwa hapo kwanza wanafunzi wa Yohana Mbatizaji lakini wakaja kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu..na ndio sasa mababa wetu wa Imani ya Kikristo leo.Hivyo Yohana mbatizaji kazi aliyoifanya ni kuwageuza Mababa wa Torati kuwa Mababa wa Imani ya Kristo na mioyo ya watoto iwaelekee mababa.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
HOME
Print this post
Yohana Mbatizaji alizaliwa huko Uyahudi miezi michache kabla ya kuzaliwa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo, Baba yake mzazi aliitwa Zekaria aliyekuwa Mlawi, ambaye alikuwa ni kuhani, akihudumu katika Nyumba ya Mungu illiyokuwepo huko Yerusalemu…Mama yake aliitwa Elizabeth ambaye alikuwa ana undugu wa karibu na Bikira Mariamu mama yake Yesu.
Habari za kuzaliwa kwake kimiujiza, zinapatikana kwa urefu katika kitabu cha (Luka 1:1-60).
Maandiko yanasema Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni mwa mama yake (Luka 1:15). Na inasadikiwa kuwa miaka michache sana baada ya kuzaliwa kwake wazazi wake wote wawili walifariki. Na hivyo akaondoka na kwenda kukaa majangwani, mpaka siku alipotokea tena hadharani kuhubiri habari za msamaha na toba.
Aliitwa Yohana Mbatizaji kutokana na ufunuo alioupata wa ubatizo. Hapo kabla kulikuwa hakuna mwingine aliyekuwa anafanya ubatizo Zaidi yake, ndio maana alijulikana kama Yohana Mbatizaji, kumtofautisha na wakina Yohana wengine.
Yohana Mbatizaji sio Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo, aliyeandika kitabu cha Ufunuo ni Yohana aliyekuwa mwanafunzi wake Yesu. Yohana Mbatizaji hakuandika kitabu chochote katika Biblia
Yohana Mbatizaji, maandiko yanasema alikuwa ndiye Eliya aliyetabiriwa atakayekuja kumtengenezea Bwana Njia (Luka 1:17). Atakayeigeuza mioyo ya baba iwaelekee Watoto.
1. Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?
Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kuwa Nabii Eliya mwenyewe ndiye atakayerudi.Ili kuelewa vizuri juu ya jambo hilo hebu tafakari mfano ufuatao.
Ametokea kiongozi mmoja mashuhuri sana wa mambo ya kisiasa na akaleta mabadiliko makubwa sana katika taifa hilo, tuchukulie mfano Aliyekuwa Raisi wa Taifa la Tanzania, Hayati J. K. Nyerere baada ya kufa kwake, mwananchi mmoja akatabiri, Miaka ya huko mbeleni watazaliwa wakina Nyerere wengi ambao watafanya kama alivyofanya Baba wa Taifa.Je! kwa sentensi hiyo ni sawa na kusema, Nyerere atazaliwa tena yule yule aliyefariki na kuishi na kuja kuwa Raisi tena?..Ni wazi kuwa hiyo siyo tafsiri yake, tafsiri yake ni kwamba atazaliwa au watazaliwa watu ambao watakuja kuwa mashujaa kama NyerereNa ndivyo ilivyo kwa unabii wa ujio wa Eliya, sio kwamba ni Eliya yule yule atazaliwa tena hapana bali atakuja mtu au watu watakaobeba huduma inayofanana na ya Eliya. Na mtu wa Kwanza aliyeibeba huduma hiyo baada ya Eliya mwenyewe alikuwa ni Nabii Elisha na baada ya Elisha alifuata Yohana Mbatizaji..
1.Yohana Mbatizaji ni nani?
Historia inaonesha Nabii Eliya aliishi karne ya 9 kabla ya Kristo, Ni Nabii aliyeshindana sana na Utawala wa kipagani wa Mfalme Ahabu wa Israeli na mkewe Yezebeli.
kadhalika Biblia hairekodi kama alikuwa na mke wala Watoto. Wala haielezi huduma yake aliifanya kwa miaka mingapi.
Miujiza mingi iliambatana na Nabii huyu, Miujiza maarufu iliyoambatana na Nabii huyu ni ule wa KUSHUSHA MOTO na ule wa KUCHUKULIWA JUU NA MAJESHI YA FARASI.
Katika kitabu cha Malaki 4:5, biblia imeahidi kurudi tena kwa Nabii huyu.
1.Je! Ni Eliya mwenyewe atarudi au ni roho yake?
2.Je! Kazi ya Eliya atakaporudi itakuwa ni ipi?
3. Yezebeli ni nani?
Siku moja nilikuwa ninamsikiliza Mh.Raisi akizungumza na wafanyabiashara Ikulu, nikapata kitu ambacho kiuhalisi ndio kinachoendelea katika Ukristo isipokuwa tu ni katika upande mwingine wa shilingi. Kwa kawaida mimi sio mfuatiliaji wa mambo ya siasa, lakini siku hiyo nilijikuta ninasikiliza mahojiano kati ya Raisi na wafanyabiashara ikulu ni hotuba wakipeleka changamoto zao na malalamiko yao wanayokumbana nayo katika taasisi cha kiserikali hususani TRA….Wengi wao walipewa nafasi ya kutoa kilicho moyoni mwao..Na baadaye Raisi akasema hawa watu wa taasisi za umma, wanatumia kauli mbiu yake ya kuchapa kazi, ili kuwakandamiza wafanyabiashara na wananchi kwa kuwapa makadirio makubwa kushinda uwezo wao wa kulipa..Na wakishamaliza kuwakandamiza wanatumia kauli ya HAPA KAZI TU!, yaani kwa lugha nyepesi tunaweza kusema wanaongezea makali kile Raisi anachokiamini kwa kutimiza matakwa yao binafsi, ambayo hayalengi kujenga bali kubomoa ..Hilo ni jambo ambalo lilimuhuzunisha sana Mh Raisi.
Sasa ukiangalia, ni kweli kauli mbiu ya Raisi ni kuwa kila mtu achape kazi, lakini hakuwa na lengo la kumaanisha kuzidi mipaka hadi kuwakandamiza watu wenye nia njema ya kulijenga Taifa..Bali kanuni hiyo ilikuwa inalengo la kuwahamasisha wananchi wafanya kazi kwa bidii..
Leo hii ukirudi katika ukristo utakutana pia na hili neno maarufu, “Hatuishi chini ya Sheria, bali tupo chini ya neema”(Warumi 6:14)..Na hivyo Mungu haangalii matendo yetu bali Roho zetu…Ukiangalia ni kweli kabisa biblia inatuambia hivyo, lakini tunashindwa kufahamu Neno hilo lilikuwa linawahusu watu wa namna gani..
Neno hilo lilikuwa linawahusu watu waliokuwa ndani ya Kristo na wala sio walio nje ya Kristo, ikiwa na maana kuwa katika bidii yako ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ndani ya Kristo, Usihesabu kuwa hicho ndicho kinachokupa uhalali kwa kukubaliwa na Mungu au kwenda mbinguni..,Hapana, mbinguni ni mahali patakatifu sana, hakuna kinyonge kitakawezakuingia na kama hivyo hakuna mtakatifu yoyote ambaye angestahili kwenda mbinguni isipokuwa YESU KRISTO tu peke yake kwasababu yeye ndiye hakuwahi kutenda dhambi yoyote tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake..
Hivyo ili na sisi tuhesabiwe kama watakatifu basi neema lazima ichukue nafasi yake, lakini huku tukiwa bado ndani ya Kristo, na tukijitahidi kuishi maisha makamilifu na matakatifu kwa kadiri tuwezavyo..Lakini leo hii utakuta, mtu anatembea uchi barabarani, anavaa vimini na suruali kama soksi, na bado anajiita mkristo, ukimuuliza kwanini unafanya hivi . Anakwambia Biblia inatuambia hatuishi chini ya sheria bali chini ya neema, Mungu haangalii vya nje bali vya ndani.
Hata mtu aliye nje ya wokovu utamsikia akizungumza maneno hayo hayo, hatupo chini ya sheria bali chini ya neema. Nataka nikuambie, biblia inasema katika siku za mwisho maneno haya ..“lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. (2Timotheo 3:13)..
Usikubali kudanganyika, Maovu yanavyozidi kuongezeka shetani ndivyo anavyotumia silaha ile ile ya maandiko kudanganya watu wengi. Kama vile tu alivyojaribu kutumia silaha hiyo kumdanganya Bwana Yesu kule jangwani…Ukiendelea na mtazamo huo kuwa tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo na huku unafanya mambo maovu kwa makusudi, unawasababishia wengine watende dhambi ya kutamani kwa ajili yako, kuwa na uhakika tu siku ile utahukumiwa na Mungu kwa kushindwa kulipambanua Neno la Mungu ipasavyo.
Warumi 6:15 “Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! 16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.”
Warumi 6:15 “Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!
16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.”
Na Neno lingine lililo maarufu leo hii, utalisikia kila mahali ni hili ‘Usihukumu usije ukahukumiwa’..Na kwamba ikitokea mtu anahubiri kuwa walevi wote na waasherati wataenda motoni, kama biblia inavyosema anaambiwa kuwa anahukumu…Lakini mtu huyo huyo yupo tayari kumweleza kwa uwazi wote mtoto wake ikiwa anapotea mwisho wake utakavyokuwa, utasikia anamwambia usiposoma mwanangu, utaishia kuwa teja, au kuwa kibaka, au kuwa maskini…hilo kwake haoni kama ni hukumu, lakini yeye akihubiriwa kwamba endepo akiendelea kuwa mlevi ataishia jehanamu ya moto utasikia anakumbia unahukumu, mwenye uwezo wa kuhukumu ni Mungu tu!…Hiyo yote ni kutokana na kushindwa kulichambua vizuri neno la Mungu. Utakapokwenda mahali popote ukaanza kuwafundisha tu watu wadhara ya dhambi na mwisho wake ni upi, utasikia wakisema unawahukumu..
Na mambo mengine mengi tu, ya namna hiyo. Hivyo tunapaswa tukae mbali na misemo hiyo, ambayo inatumia kivuli cha maandiko kusitiri maovu na mabaya. Kwasababu siku ile Mungu hatakuwa radhi na sisi.
Kama bado haujafahamu thamani ya kuwa ndani ya Kristo, ni vema ufanya hivyo sasa kabla ya mlango wa neema haujafungwa..Unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha kufanya dhambi, kisha tafuta mahali wanapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa Jina la BWANA YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako kama bado hujafanya hivyo..kisha Uukulie wokovu mpaka siku ya kunyakuliwa..
Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
1.Angalieni Jinsi Msikiavyo
2. Umesikia inavyopaswa?
3. Je! Una masikio yanayosikia?
.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jina la Bwana Yesu Kristo, libarikiwe…
pamoja na kazi nyingine nyingi anazozifanya Roho Mtakatifu juu ya mtu aliyemwamini Yesu Kristo, nyingine ni kumwongoza katika kuijua kweli yote…Hilo tunalisoma katika..
Yohana 16:13“ Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”
Neno kuongoza halina tofauti sana na kuelekeza, yaani mtu anayekuelekeza jambo Fulani hatua kwa hatua, mpaka kufikia hitimisho analotaka yeye ufikie, hana tofauti na mwongozaji…na kazi ya mwelekezaji au mwongozaji, sio tu kuonesha njia pekee bali hata kurekebisha baadhi ya makosa..Kwamfano mtu anapotaka kukuongoza kufika mahali Fulani, halafu wewe unampa mashauri yako ya njia ya kuipitia, ni wazi kuwa kama hayo mashauri yako sio sahihi basi atakurekebisha kwa nia ya kukuelekeza njia iliyo bora zaidi.
Na ndivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu, yeye ni mwongozaji wetu, na Roho Mtakatifu ndio jambo la kwanza kabisa mtu aliyemwamini Kristo anapaswa kuwa naye…Biblia inasema mtu asiye na Roho Mtakatifu huyo sio wake (Warumi 8:9) Ikiwa na maana kuwa mtu asiye na Roho Mtakatifu, hakuna uongozi wowote wa KiMungu unaoendelea juu ya Maisha yake..Ni kupotea tu!.
Hivyo mtu aliyeamini, katika hatua za awali kabisa, anakuwa hajui vitu vingi, hiyo ni kawaida kabisa, anakuwa kama mtoto mdogo aliyezaliwa, ambaye hajui chochote katika maisha haya, na vivyo hivyo mtu aliyezaliwa mara ya pili anakuwa ni mdhaifu katika roho. Lakini pamoja na udhaifu huo kunakuwa na kitu ndani yake kinachomfanya aelewe mambo mengi kwa muda mfupi kwasababu anakuwa na moyo wa unyenyekevu wa kutaka kujua au kufahamu Zaidi kuhusu Mungu, kama mtoto mchanga… hiyo Kiu ni ambayo Roho Mtakatifu kaiweka mwenyewe ndani ya mtu, ili itumike katika mstari wa kuwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anaanza kumvuta, kidogo kidogo na kumtoa hatua moja hadi nyingine, aielekee njia ya utakatifu, ndio hapo mtu ataanza kutoka katika ulimwengu na kuona sababu ya kutafuta kanisa Fulani ambalo angalau ataweza kuipooza ile kiu iliyopo ndani yake ya kutaka kumjua Mungu…Atatoka kwenye dhambi na hatimaye kujiunga kanisa Fulani, atapata vitu ndani ya lile kanisa ambavyo vitamsisimua sana na kumfanya kukua kiroho kwa kiwango Fulani..na atakapofika mahali na kuona hali yake ya kiroho ipo pale pale, baada ya kukaa muda mrefu, kuna kitu kitamwambia hapo ulipo bado unahitaji kuwa na Mungu zaidi…..hiyo nguvu itamsukuma kutafuta hazina mpya ya chakula cha kiroho kwa hali na mali, utaona anazidi kutafuta mahali ambapo atapata chakula kilichobora zaidi…lengo lake sio kuhama kanisa au dhehebu hapana!.
Bali lengo lake ni kupata kuweka sawa hatima ya Maisha yake ya kiroho…Tofauti na wengi wanaohama makanisa sasahivi ni kwasababu tu wamesengenywa kidogo, au kwasababu wanahitilafiana na mchungaji wake kwa masuala ambayo hata sio ya kiimani, au kwasababu wanakemewa waache dhambi, au kwasababu wanataka kuolewa au kuoa, au kwasababu wamechoka tu kukaa pale na hivyo wanajaribu ladha mpya n.k…
Aliye na Roho Mtakatifu kweli haondoki mahali kwasababu kama hizo…Kinachomwondoa sehemu moja hadi nyingine ni ile kiu iliyopo ndani yake ya kutaka kumjua Mungu Zaidi, na anakuwa hana kiburi…Mahali alipokuwa anakaa hapo kwanza walikuwa hawana utaratibu wa maombi ya mfungo, hivyo anaona kuna kitu ndani ya roho yake kimepunguka anahitaji kuwa mwombaji zaidi na msomaji wa maandiko zaidi, kwahiyo anatafuta mahali ambapo atakuwa mwombaji Zaidi…Au mahali alipo kuna mchanganyiko wa Neno la Mungu na mambo ya ulimwengu huu hivyo anaondoka kwenda kutafuta mahali atakapoishibisha roho yake na Neno lisilochanganywa.
Au pengine mahali alipokuwa anakaa hakukuwa na desturi za kwenda kufanya uinjilishaji, na yeye anaona kuna kiu ndani yake ya kwenda kuwahubiria wengine habari njema popote pale, na hivyo mahali alipo haiwezekani kufanya hivyo, kwahiyo anaondoka kwenda mahali ambapo atatimiza agizo hilo la Bwana Yesu la kwenda kuhubiri injili kwa kila kiumbe..
Au pengine mahali alipokuwepo kunafanyika ibada za sanamu, na baada ya kuyachunguza maandiko vizuri anaona si sawa kufanya jambo hilo, na hivyo anaondoka kwenda kutafuta mahali ambapo hataabudu sanamu tena n.k.
Sasa katika hatua zote hizo utaona mtu huyu wa Mungu anaweza akawa ameshatembea sehemu nyingi zote akitafuta kukaa mahali salama….Na anavyozidi kusogea mbele ndivyo anavyozidi kuwa bora zaidi katika Imani. Na mtu anayekua kutoka sehemu moja hadi nyingine anakuwa hatamani tena kurudia yale ya nyuma…kwamfano mahali alipokuwepo ni mahali ambapo palikuwa hakuna utaratibu wa kusali au kuomba, wala palikuwa hakuna msisitizo wa kuishi maisha matakatifu akishatoka hapo hawezi tena kutamani kurudia hapo..
Sasa jambo hilo la kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa lengo la kutafuta Usalama wa maisha yako ya kiroho, na si sababu nyingine tofauti na hizo…sio dhambi! Bali ni kazi ya Roho Mtakatifu katika kukuongoza na kukuweka katika kweli yote…
Hiyo ndio kazi ya Roho Mtakatifu kutuhakikisha hatukwami sehemu moja kila siku bali tunakuwa kuufikia utimilifu,
Kosa moja linalofanyika na watu wengi, ni kujaribu kutafuta dhehebu Fulani la kuhamia na kutafuta lililobora zaidi ya lingine kwa kuangalia watu wengi wanakwenda wapi, au kwa kusikiliza ushauri wa watu, au kwa kuangalia uzuri wa kanisa….lakini hawasikilizi msukumo wa Roho Mtakatifu ndani yao, ambaye huyo ndiye angewaongoza katika kuwatia kwenye kweli yote…
Binafsi nimekutana na watu wengi, wakiniuliza nimeamini sasa nihame hapa niende kanisa gani?…Binafsi huwa nakosa jibu la hili swali..kwasababu Mungu hakuanzisha madhehebu, na Roho Mtakatifu hamwongozi mtu kwenda kwenye dhehebu lolote bali anamwongoza katika kuijua kweli…..Hiyo njaa na kiu ya Neno la Mungu ndio inayomsukuma mtu kutoka sehemu moja hadi nyingine kutafuta chakula, hivyo hata kama akikutana na chakula kilichochacha mbele yake atakula tu kwa huo muda ilimradi aweze kuishi..
Kanisa sio suluhisho la kuishi katika mapenzi ya Mungu, bali Roho Mtakatifu ndio suluhisho, unapokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuyasoma maandiko ndivyo unavyompa nafasi Roho Mtakatifu kukuonesha ni wapi ulikuwa unakosea, na ni wapi unapaswa urekebishe na ni wapi pa kukaa palipo salama…lakini sio kutafuta ushauri kutoka kwa watu, au kwa kuangalia ni wapi wengi wanakwenda. Wengi wanaofanya hivyo hakuna chochote katika maisha yao kitakachobadilika kwasababu ni sawa na wamehama dini moja na kujiunga na nyingine…huko wanakokwenda wanakwenda kuwa washirika wa dini tu na si wakristo halisi, na kuvamiwa na roho ya udhehebu ambayo ndiyo roho ya mpingakristo….roho ya kusema dini yangu inafundisha hivi, au dhehebu halisemi hivyo n.k Kumbuka madhehebu ya Mafarisayo na Masadukayo ndiyo yaliyoongoza kumpinga Bwana Yesu katika huduma yake…sasa roho hiyo hiyo ndiyo iliyopo katika madhehebu (yaani watu walioacha uongozi wa Roho Mtakatifu na kuwa washirika au washabiki wa dini)..Bwana alipokuwa anawaambia Mafarisayo hivi wenyewe wakawa wanasema Musa hakutufundisha hivyo, kwahiyo ikawafanya kuwa mbali na Mungu kuliko hata watu wa Ulimwengu wasio mjua Mungu, hiyo yote ni kutokana na Udhehebu na Udini uliokuwa ndani yao.
Ndio maana Biblia inatuambia tutoke huko (Ufu.18:4), Tunapomgeukia Roho Mtakatifu na kufuata uongozi wake ndio kutoka kwenyewe kunakozungumziwa hapo…yeye ndiye kiongozi wetu ambaye kila siku anarekebisha makosa yetu kulingana na Biblia na kutuweka katika mstari.
Usianze kutafuta kanisa la kwenda sasa, anza kutafuta maandiko yanasemaje kwanza…ndipo Roho atapokuongoza pa kwenda, Roho Mtakatifu anawaongoza watu wanaosoma maandiko sio wanaotafuta makanisa…
Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
MIISHO YA ZAMANI.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
Rudi Nyumbani:
Shalom, mtu wa Mungu natumai u buheri wa afya kwa pumzi unayopewa na mwenyezi Mungu. Leo kwa furaha ya Bwana nakukaribisha tuutafakari ukuu wa Mungu na matendo yake jinsi yalivyo makuu.
Tabia mojawapo ya Mungu ni kuwa, huwa hajisifii au kujionyesha moja kwa moja mbele za watu kuwa yeye ni mkuu, badala yake huwa anawaacha wanadamu wavumbue wao wenyewe kazi zake, na pale wanapoona mambo ya kutisha na kusema he! Kumbe na hili kalifanya yeye, kumbe na lile kalifanya yeye!, na yule mtu kumpa Mungu utukufu Sasa hapo ndipo Mungu anapoipokea sifa yenyewe. Tofauti na sisi wanadamu, Kwanza tunataka tusifiwe kwa kitu ambacho si chetu, pili tunapenda kuwaonyesha watu kuwa sisi tunacho, kwa lengo la kujitafutia utukufu bandia..
Sasa yapo mambo ambayo, laiti watu wa vizazi vya Nuhu wangeona, leo hii wasingeangamizwa, vile vile yapo mambo ambayo laiti watu wa Sodoma wangeyaona leo hii wangemuheshimu Munguna kumwogopa sana, Halikadhalika yapo mambo ambayo mitume wangeyaona kama tunavyoyaona sisi , leo hii wangemtukuza Mungu kwa nguvu zao zote..Vile vile yapo mambo ambayo Mfalme Daudi angeyaona leo hii angemwabudu Mungu Zaidi hata ya pale alipomwabudu alipodondokewa na nguo.
Sisi watu wa leo hii Teknolojia imeturahisishia mambo sana, na hivyo kwa kutumia simu zetu tu au computa au television tunaweza kuona uweza mwingi wa Mungu duniani kote.
Mfano zamani, watu walikuwa wakitazama juu, walikuwa wanaona nyota na mwezi tu peke yake, napengine walidhani kuwa kuvifikia hivyo sio mwendo sana lakini sisi tunaoishi kizazi hiki ndio tunajua, kumbe baadhi ya zile nyota tunazoziona ni Ma-Jua mengine mengi, kama tu jua letu hili, na kila nyota inayo sayari zake nyingi kama Jua letu hili lilivyo na sayari 9, Dunia yetu ikiwa ni mojawapo ya sayari hizo.
Sasa karibu kila kitu unachokiona angani, vyote hivyo ni kama punje moja kati ya nyingi. Kama vile punje moja ya mahindi katikati ya gunia, sasa punje yetu tuliyopo sisi ndio inaitwa Milky way galaxy(Giligili), ambayo inatengenezwa na mamilioni ya mifumo ya jua..Hivyo ukiendelea juu zaidi unakutana na punje nyingine ambayo pia inayo ma-jua yake mengi, na sayari zake mabilioni kwa mabilioni, kama hii yetu ya Milk-way nayo inaitwa Andromeda Galaxy, sasa jumlisha punje zote hizi za Magalaxy, katengeneza Mungu mmoja, inasemekana yapo magunia mengine kama hayo mabilioni kwa mabilioni, hapo bado haijasisha ukiyajumlisha magunia hayo yote unatengeneza tena rumbesa moja lijulikanalo kama Clusters, sasa hayo marumbesa nayo yapo mabilioni kwa mabilioni, nayo ukiyajumlisha utapata kitu kimoja kinachoitwa Super clusters, Hizi nazo zipo mabilioni kwa mabilioni, ukijumlisha unapata kitu kinachotwa Universe,…Na hizi Universe nazo zinaonekana zipo mabilioni kwa mabilioni ambayo hayo upeo wa wanasayansi wa sasa hawajaweza kugundua chochote kinachoendelea juu Zaidi ya hapo.
Sasa tukizungumzia kutoka kwenye mfumo wetu tu wa Jua, kutoka sayari moja hadi nyingine, yaani sayari iliyo karibu na sisi ujulikanayo kama Mars inaweza kukuchuka Zaidi ya miaka 57.4 kufika kama ukisafiri kwa gari lenye spidi ya juu sana..sasa jiulize kukatisha kutoka galaxy moja hadi nyingine inaweza kukuchukua miaka mingapi?
Inasemekana zipo sayari zenye mfano wa dunia hii, na nyingine Zaidi hata ya dunia hiii nazo hizo zipo Zaidi ya BILIONI 40, Yaana kama kila mwanadamu apewe dunia yake, atepewa amiliki dunia 6.
Hapo bado hatujazungumza kwa viumbe vya ajabu vilivyogunduliwa hivi karibuni duniani, nabado vinaendelea kugunduliwa, laiti mfano watu wa zamani wangeweza kuyaona haya au kuyasikia wasingemchukulia Mungu katika taswira iliyo bora zaidi. Ukirudi baharini vipo viumbe vingi vya ajabu ambavyo kila siku vinazidi kugunduliwa…
Lakini sasa ni kwanini tunajikumbusha haya?
Hiyo yote ni kuonesha kuwa Mungu ni mkuu na mwenye uweza kushinda sisi tunavyoweza kufikiri, hata kama uliwahi kumwomba kitu na hujakipata, hilo lisikufanye kumuona kuwa Mungu hawezi kukupa chochote, kumbuka ikiwa anamiliki matrilioni ya Sayari angani, atashindwaje kukupa wewe kipande cha mita 20 za ardhi,? Jaribu kufikira tu hayo mambo.
Ikiwa anamlisha tembo kila siku kilo Zaidi ya 200 na maji Zaidi ya lita 100 atashindwaje kukupa wewe chakula kilo 2 tu kwa siku?, ikiwa umemwomba chakula na hujaona kimekuja kwa muda huo, basi usinung’unike ujue kuwa anakuandalia kilicho bora Zaidi..
Hali yoyote unayopitia leo, uwe ni shida, au magonjwa visikuvunje moyo ukadhani kuwa Mungu hakuoni, au hawezi kukutoa katika hali uliyopo..Anao uwezo huo, wewe endelea kuyatafakari tu matendo yake.Poteza muda mrefu, kuuchunguza ukuu,wake na kumsifu kwa kila unachokiona, Nakuambia wakati utafika utasema asante Mungu kwa kuwa umenipa au umenitendea katika wakati huu, ambao ndio bora ziadi kuliko kama ungenipa wakati ule.
Hivyo ikiwa wewe ni mkristo, usiache kuishindani Imani yako, uliyokabidhiwa mara moja tu… Pia kama bado upo nje ya Kristo, acha kuyahatarisha Maisha yako, mgeukie yeye sasa atakuponya Roho na Mwili wako.
Zaburi 46:8 “Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. 9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. 10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.” Bwana akulinde,Bwana akufunike, Bwana akubariki.
Zaburi 46:8 “Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.”
Bwana akulinde,Bwana akufunike, Bwana akubariki.
Shalom. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
MJUE SANA YESU KRISTO.
YESU MPONYAJI.
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
KIFAA BORA CHA MATUMIZI.
Ipo dhambi ya Mauti, Hiyo mtu aliye mkristo akiitenda kama Bado Neema ya Mungu ipo juu yake, atakufa lakini ataokolewa siku ya kiyama. Mfano Musa!, alimkosea Mungu, akasamehewa kosa lile lakini adhabu ya kifo haikuondolewa juu yake, Bwana alimwambia kwa kosa lile hataiona nchi ya ahadi na kufa atakufa…lakini baada ya kufa, alikwenda mahali pa watakatifu.Ndio maana utamwona akitokea tena na kuzungumza na Bwana Yesu, yeye pamoja na Eliya katika ule mlima Mrefu.
(Mathayo 17:1-9), Sasa hiyo ni dhambi ya mauti ambayo, unaadhibiwa mwili ili roho ipone (1 Wakoritho 5:5)..Kwa maelezo marefu juu ya dhambi hii ya Mauti, utaipata mwisho kabisa wa somo hili.
Lakini ipo dhambi ya isiyo na msamaha kabisa hapa duniani wala huko katika dunia inayokuja…Hiyo ni dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Dhambi hii watu wanaitenda na kadhalika mtu asipoielewa dhambi hii ni rahisi kupelekeshwa na shetani sana…Kwasababu shetani anamjua mwanadamu sana kwa miaka mingi, tangu Edeni, hivyo mojawapo ya njia anazotumia kumkandamiza mwanadamu asiye na ufahamu wa kutosha ni kumletea mawazo kwamba ana dhambi isiyosameheka mbele za Mungu, Tutakuja kuona hapo mbeleni kidogo, namna ya kukabiliana na hilo jaribu Kongwe la shetani!
Lakini sasa hebu tujifunze ni namna gani mtu anamkufuru Roho Mtakatifu.
Biblia inasema katika
Mathayo 12:31 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. 32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao”.
Mathayo 12:31 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao”.
Hapo Neno limewekwa moja kwa moja kuwa yeye atakayenena Neno juu ya Roho Mtakatifu na wala si mwana wa Adamu, haimaanishi kuwa Kuna Miungu watatu, hapana! Mungu ni mmoja tu…Ila Roho Mtakatifu ni Utendaji kazi wa Bwana Yesu Kristo mwenyewe katika mfumo wa Roho, kwasababu Roho Mtakatifu ndiye roho wa Yesu mwenyewe (Matendo 16:7) ndio maana ilimpasa yeye aondoke kwanza katika mwili ili arudi tena katika roho ( soma Yohana 16:16), kwasababu mtu anayefanya kazi katika roho, anakuwa na matunda Zaidi kuliko anayefanya kazi katika mwili, mchawi anayekwenda mahali katika roho anauwezo wa kuathiri kikundi kikubwa cha watu kuliko angekuwa mahali pale katika mwili…Kwahiyo utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndio utendaji kazi wa Mungu, ulio karibu Zaidi na wenye matunda Zaidi kuliko Mungu alivyokuwa katika mwili…ndio maana kuna hatari kubwa sana ukimkufuru….kwasababu nguvu ya kumshawishi mtu kuja kwa Mungu inatokana na Roho Mtakatifu.
Sasa endapo mtu ambaye hajawa mkristo kabisa, na ndani ya moyo wake anasikia kabisa kuna kitu kinamshuhudia kuwa Yesu ndiye njia, na kinampa uthibitisho wa kila aina kuwa hakuna njia nyingine nje ya Yesu Kristo, huyo ni Roho Mtakatifu ndani ya huyo mtu anayemlilia ageuke atubu na kumwamini Yesu, lakini mtu huyo pamoja na msukumo wote huo wa kiMungu ndani yake, na wenye kila aina ya uthibitisho, akaamua kwa idhini yake mwenyewe kuikataa na kutamka maneno ya kufuru wazi kwa kinywa chake dhidi ya ule ushawishi au dhidi ya mtu anayemletea injili ile, Roho Mtakatifu ndani yake anaondoka milele, kamwe mtu huyo hataisikia tena ile sauti ikimshawishi kuwa Yesu ni njia. Kamwe hatasikia tena kitu kikimvuta kutubu, atabakia kupinga injili Maisha yake yote…Hapo Mtu huyo anakuwa na dhambi ya Milele (amemkufuru Roho Mtakatifu)…haiwezekani tena yeye kutubu!…Kumbuka sio kwamba itafika kipindi atatamani kutubu na Mungu amkatae! Hapana! Hatasikia sababu wala hamu ya kutubu mpaka anakufa!..kwasababu anayeleta moyo wa Toba ndani ya mtu ni Roho Mtakatifu mwenyewe, kama mtu anahukumiwa dhambi zake na kutamani kutubu ina maana bado Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, lakini asiyetaka kabisa kutubu ni wazi kuwa Roho Mtakatibu hayupo kabisa juu ya Maisha yake.
Kadhalika kama mtu tayari ni Mkristo, na ameshawishika kabisa kumfuata Kristo, na kuonja mema yote na vipawa vyote vya kiMungu na kutambua kabisa ya kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zake na ameshajua utendaji kazi wa Roho Mtakatifu upoje, na kuamua kugeuka kuacha wokovu, na kugeukia shetani moja kwa moja, na kunena maneno ya kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu au dhidi ya mtu anayehubiria wengine Injili ya wokovu kwa uweza wa Roho, hapo mtu huyo Roho Mtakatifu anaondoka moja kwa moja juu yake, na harudi tena! Kamwe moyoni ile sauti iliyokuwa inamhukumu atendapo mabaya au iliyokuwa inamwongoza inakuwa haipo tena, huko alikokwenda ndio anakuwa wa huko huko moja kwa moja….hawezi wala hatakuwa na hana hamu ya kutubu tena, wala hatasikia kuupenda wokovu tena, kwasababu anayetupa sisi hamu ya kuendelea kuupenda wokovu ni Roho Mtakatifu.
Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. 7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.”
Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;
8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.”
Sasa kuna kitu kinaitwa kurudi nyuma, au kupoa! Hii inatokea pale, mkristo alikuwa moto sana, alikuwa anaomba na kusali lakini kapunguza kufanya hivyo, alikuwa anafanya kitu Fulani cha kiMungu lakini kakipunguza, alikuwa anahubiria wengine lakini kapunguza, …Kumbuka anakuwana anapoa sio anakuwa baridi!, Mtu anayekuwa baridi maana yake ametoka kwenye wokovu kabisa! Hivyo ni ngumu kurudi tena, yupo hatiani kupata dhambi ya mauti au dhambi isiyosameheka..Lakini aliyerudi nyuma, maana yake anaweza kurudi pale alipokuwepo akitubu na ndani yake, bado kuna kitu kinachomshuhudia kuwa anahitaji kumgeukia Mungu, na hofu ya kwenda kwenye ziwa la moto sasa huyo ni Roho Mtakatifu bado anafanya kazi ndani yake.
Lakini sasa, shetani akishajua kuwa mtu karudi nyuma, jambo la kwanza analokwenda kulifanya ni kwenda kumwekea ukingo asirudi alipokuwepo, na hiyo anaifanya kwa kumletea sauti inayomwambia UNA DHAMBI ISIYOSAMEHEKA! Au UMEMKUFURU TAYARI ROHO MTAKATIFU.
Mwamini yule akisikia sauti ile ndani yake ikimwambia vile basi anavunjika moyo, na kuingia kwenye dimbwi kubwa la mawazo yasiyoisha. Hata hamu ya kuendelea mbele yote inaisha!..Sasa mtu wa namna hiyo hajamkufuru Roho Mtakatifu kwasababu bado anahitaji kurudi kwa Mungu, bado anataka kutubu, hiyo hamu au hitaji la kutubu linaletwa na Roho Mtakatifu, hivyo Roho Mtakatifu bado hajaondoka juu yake, ingawa shetani atamletea mawazo ya kwamba ana dhambi ya milele.
Kwamfano kuna mtu mmoja mwenye tatizo kama hilo alinitumia ujumbe inbox, akiwa na mashaka hayo na hajui afanyaje…Hebu fuatilia kidogo mazungumzo haya…
Shalom! swali langu ni kwamba je mtu akiokoka halafu akakengeuka ila akarudi tena kuomba toba madhabahuni, je mtu huyu anakuwa kasamehewa au atakuwa hajasamehewa? na jina lake litaendelea kuwepo kwenye kitabu cha uzima?
Nikamjibu swali hilo, nikamtumia na somo linalohusu swali hilo…na kisha akaendelea kuniambia…
“Asante sana Mtumishi wa Mungu…Yani mimi nimeokoka sasa kuna kipindi nikaanguka nikazaa kabla ya ndoa halafu pindi naishi na mwanaume wangu nlikuwa nashika mimba mwenzangu ananiambia nitoe nami nilikuwa nikifanya hivyo lakini badae nikaona amani ikawa inaisha kila kukicha kwa kitendo nlichofanya nikaamua kwenda kwa mchungaji nikamwelezea akanikemea na akanitenga kihuduma kwa muda na akanambia nisirudie tena kutenda dhambi Mungu ataniacha vibaya sana sasa wakati nahudhuria ibada kanisani kuna mpendwa akauliza nililokuuliza mchungaji akajibu akasema mtu huyu hasamehewi tena basi tu tunaendelea kufarijiana ila hakuna msamaha tena hapo basi toka siku hiyo mimi linaniumiza sana neno hilo sijui nifanyeje ili niweze kurudisha amani yangu katika kumwabudu Mungu”.
Baada ya kunitumia ujumbe huo, nikamwambia ni sahihi kabisa alichofanya mchungaji wako kukutenga kwasababu umestahili kutengwa kulingana na maandiko kwa kitendo ulichokifanya, (1 Wakorintho 5:9-13)..Na alikujibu pia sawa, kwamba usirudie tena kufanya hivyo akimaanisha ukatubu!…lakini siku nyingine alipojibu swali kama hilo kwa mwingine akasema mtu kama huyo hana msamaha,….Nikamwambia mchungaji wako sijui Ni kwanini alimjibu vile huyo mtu wa pili lakini naamini hakumjibu huyo mtu wa pili kwa kulinganisha na tatizo ulilonalo wewe, yeye alimjibu yule pengine akimaanisha mtu aliyeacha kabisa wokovu na kukengeuka na kuiacha njia ya msalaba, na kukufuru huyo ndiye mtu ambaye Roho Mtakatifu anaondoka ndani yake kabisa kabisa!…na hatuwezi kumfariji kwasababu hata hatatamani kufarijiwa wala kutamani kanisa..ataendelea kudanganyika na kutamani mambo maovu…
2 Timotheo 3: 13 “lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika”..
lakini sio wewe! Wewe bado kuna nguvu ya kutaka kutubu ipo ndani yako, kitu fulani kinachokusukuma kumrudia Mungu, ambacho ni Roho Mtakatifu…
Sasa hicho kitu cha kumsukuma kutubu endapo kisingekuwepo ndani ya huyu dada, na akawa anafurahia kuendelea na tabia hiyo, hapo ndio angekuwa pengine na hiyo dhambi isiyosameheka…kwasababu Roho Mtakatifu anayehusika katika kumvuta kutubu hayupo…(Yohana 6:44).
Tatizo hili limekuwa ni la watu wengi, hususani waliofanya dhambi za mauaji, ubakaji na utoaji mimba, mizaha iliyopitiliza katika madhabahu za Mungu…Unakuta mtu aliitenda dhambi hii sasa kasikia sauti ndani ikimshawishi kutubu lakini akikumbuka kwamba alishaua kuna kitu kinamwambia huwezi kusamehewa, hivyo anavunjika moyo moja kwa moja, mwingine alitoa mimba kadhaa, mwingine alifanya kitendo kibaya kiasi kwamba hawezi kukisema hata mbele za watu…Sasa mawazo kama hayo yanapokujia, wakati unapotaka kumgeukia Mungu, unapaswa UYAKATAE! Kwa nguvu na kuendelea kusonga mbele, kwasababu ni mawazo ya shetani!
Na pia jiepushe na kutenda dhambi hizo kwasababu madhara yake ndio kama hayo ya kuletewa mawazo ya mkandamizo kutoka kwa shetani!, usipotenda mambo hayo, shetani hawezi kukupata kwa mawazo yake. Na pia dhambi hizo ukizitenda baada ya kuamini, na kumkataa kabisa Roho Mtakatifu. kuna uwezekano mkubwa wa Roho Mtakatifu kuondoka kabisa ndani yake..usisikie tena hamu ya kumpenda Mungu na hivyo kuishia kuipinga injili na wokovu milele.
Bwana akubariki.
Maran atha!. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
DHAMBI YA MAUTI
DHAMBI ZINAZOTANGULIA HUKUMUNI NA ZINAZOFUATA
DHAMBI YA ULIMWENGU
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI?
Nyumbani
1Wakorintho10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.”
Shalom ndugu, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe milele. Nakukaribisha tuyatafakari kwa pamoja maneno ya uzima, maadamu rehema zake ni mpya kila siku asubuhi(Maombolezo 3:22-23). Leo tutajifunza hii miisho ya zamani inayozungumziwa kwenye mistari hiyo ni ipi na tutaitambuaje kama tumeifikia au kuikaribia..
Kama ukisoma mistari kadhaa ya juu kabla ya huo, utaona kuwa biblia imeandika mambo maovu na makosa waliyoyafanya wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani mpaka ikawapelekea wengi wao wa waliotoka Misri kutokuiona nchi ya Ahadi Mungu aliyowaahidia, kama tunavyofahamu ni watu 2 tu kati ya mamilioni waliotoka Misri ndio walioiona nchi ya ahadi, na mambo yaliyotajwa hapo kuwa yaliwakosesha ni pamoja na ibada za sanamu, uasherati, manung’uniko, na kumjaribu Mungu.
Lakini mfano Mungu angeyaacha tu hivyo hivyo bila kuyaandika kwa ajili ya vizazi vya mbeleni, ni wazi kuwa na sisi pia tungeyarudia yale yale na hiyo ingetupelekea watu wachache sana kuirithi mbingu mfano wa Yoshua na Kalebu.. Lakini Mungu aliyaandika sio tu kwa vizazi vya mbeleni bali pia kwa vile vya mbali zaidi vitakavyofikiwa na miisho ya zamani.
Neno “Miisho ya zamani”, kwa lugha rahisi ni sawa na kusema mwishoni wa nyakati, au majira,..Au ni sawa na kusema pia utimilifu wa nyakati…..au kilele/ukingoni mwa nyakati….Sasa ukisikia mahali popote katika biblia inasema tunaishi katika siku za mwisho,/wakati mwa mwisho , Huo wakati kibiblia haujaanza leo wala jana bali ulianza rasmi takribani miaka 2000 iliyopita,..
1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.”
Na Mambo hayo kwa mara ya kwanza yalianza kuhubiriwa na Yohana Mbatizaji pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo wakisema, TUBUNI kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia…Kwasababu walijua tayari wameshaingia katika majira ya siku za mwisho.
Lakini swali unaweza ukajiuliza kama ni hivyo, kwanini basi Bwana Yesu akiwa katika mlima wa Mizeituni alianza kuwaeleza tena dalili za siku za mwisho ikiwa tayari anafahamu kuwa yupo katika siku za mwisho, dalili nyingine za nini tena?
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Bwana Yesu alikuwa hazungumzii habari za SIKU za mwisho kwani tayari wakati ule ilishajulikana kuwa zile ni siku za mwisho…Bali alikuwa anazungumzia habari ya SIKU ya mwisho jinsi itakavyokuwa…dalili zitakazoonesha kuwa ule mwisho wa yote utavyokuja ..
Ni sawa tu na kusema mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi, lakini uchaguzi wenyewe utafanyika mwezi wa 10, hivyo kwa namna ya kawaida mwaka wa uchaguzi unapoanza, kunakuwa na vuguvugu la kampeni, vyama vinajiweka tayari, vinaanza kufanya kampeni za nyuma ya mgongo, dalili ndogo ndogo zitaonekana kwa tabia zao, sera zao n.k. lakini kampeni rasmi hazijafunguliwa bado.. hivyo ule wakati ukifika miezi 2 kabla ya uchaguzi wenyewe kufika, ndipo Kampeni rasmi zinafunguliwa na hapo ndipo utaona mambo yanavyofanyika kwa kasi na kwa nguvu ambazo hujawahi kuziona ni kwasababu wanajua muda waliopewa na waliobakiwa nao ni mchache sana kabla ya siku yenyewe kufika..
Na ndivyo Bwana Yesu alivyokuwa anafanya, ni kueleza dalili rasmi za kukaribia kwa “siku” ile ya mwisho na sio kukaribia kwa “siku za mwisho”…akasema mtakapoona wimbi kubwa na manabii wa uongo limejitokeza, wanafanya kampeni ili kukusanya magugu matita matita basi mjue ule mwisho ule umekaribia….hayo mambo hayakuwahi kuonekana katika wakati wowote katika historia tangu kipindi cha mitume hadi kizazi hichi cha karne ya 21, kutokea kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo namna hii, yaani kuanzia mwaka 2005 kupanda juu mambo haya ndio yameanza kujitokeza kwa kasi….hii inaonyesha kuwa tunaishi ukiongoni kabisa mwa wakati,.. kipindi cha utimilifu wa wakati.
Alisema watakuja wengi kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo,.yote hayo tunayaona kila kukicha.. Hizi ni dalili za kukaribia kwa siku ile kuu ya kuitisha,
Alisema kutaongeza maasi, na upendo wa wengi kupoa,..Leo hii tunaona jinsi teknolojia ya simu na mitandao jinsi ilivyoleta maovu karibu na watu kuliko kipindi chochote cha nyuma, ndani ya simu ndogo tu mtu anaweza akapata mambo yote maovu yanayoendelea ulimwenguni kote, mpaka watoto wadogo sasa hauna jambo lolote la siri kwao. Mambo hayo yameanza kukolea kuanzia kipindi cha mwaka 2005 kupanda juu wala hata sio siku nyingi….Ulimwengu umeshajua kuwa siku zake zimebaki chache hivyo unafanya kampeni kwa nguvu kuielekea ile siku yake kuu ya kuangamizwa.
Na dalili nyingine kubwa Bwana Yesu aliyoizungumzia katika (Mathayo 24:32)ni kuchipuka kwa “mtini” ambao huo unawakilisha taifa la Israeli..Alisema jambo hilo likishaanza kuonekana basi tujue kuwa kizazi hicho hakitapita mpaka hayo yote yatakapotimia…
Kwa upana wa somo hili bofya link hili la kuchipuka kwa Israeli bofya hapa ⏩ Amin! Amin! nawaambia.
Hivyo unaweza kuona hapo kuwa sisi ndio watu tuliofikiliwa na miisho ya zamani.. ndio watu ambao sio tu tunaishi katika siku za mwisho, bali pia ni watu tunaoishi katika ukingo kabisa wa siku hizo…
Je! Bado mambo ya ulimwengu yanakusonga?. Bado upo njia panda? Bado unazini na mke ambaye si wako au mume ambaye si wako?, bado ni mlevi, bado ni mfanyaji mustarbation, bado ni mtazamaji pornography? Bado ni mfanyaji anasa?,bado ni mtoaji mimba, bado mla rushwa? bado tu upo buzy huna muda na injili za wokovu?… Hizi ni nyakati mbaya..Kama bado upo nje ya Kristo jitahidi uingie kabla mlango haujafungwa.
Anasema..
“20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”(Ufunuo 3:20-22)
“20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”(Ufunuo 3:20-22)
Shalomsana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
Rudi Nyumbani
Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu
Kama inavyojulikana na wote kuwa Divai ina kilevi…Lakini swali linakuja kama ina kilevi kwanini Bwana Yesu aligeuza maji kuwa Divai, na kwanini Divai ilitumika katika kushiriki?..hata wakati wa kanisa la kwanza, ilitumika katika kushiriki meza ya Bwana?..Na je! Mpaka leo ni sahihi kuitumia kwa kushiriki?
Divai ni kinywaji ambacho kilikuwa na matumizi mengi zamani, Kwamfano Divai iliweza kutumika kama dawa…Ndio maana Mtume Paulo, alimwambia Timotheo asitumie maji peke yake bali atumie mvinyo…
1 Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara”..
Unaona hapo? Aliambiwa atumie kwa ajili ya magonjwa yanayompata mara kwa mara, kumbuka Wakati ule, Mitume walisafiri umbali mrefu wakati mwingine wakiwa wamefunga kwenda kuhubiri injili, hivyo ile hali ya kukaa na njaa muda mrefu, utumbo ulikuwa unajisokota, kwahiyo suluhisho la hayo, ilikuwa mtu anakunywa kiasi kidogo cha Divai na ndipo ale chakula kingine…Zingatia hilo Neno ‘kidogo’…biblia inasema hapo kidogo sio sana!..ikiwa na maana kuwa ni kiwango ambacho hakiwezi kuleta madhara ya nje kama kulewa. Ingesema kunywa mvinyo wa kutosha kwa ajili ya tumbo, tungeelewa kuwa maandiko yamehalalisha ulevi. Na pia zingatia dhumuni la kunywa divai hapo sio kulewa, au kujiburudisha, au hamu…hapana! Bali kwaajili ya tumbo, ikiwa na maana kuwa kama afya yake itakuwa vizuri hana sababu ya kuinywa hata kidogo!!
Kadhalika Divai hiyo hiyo haikutumika tu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa au madhaifu ya Tumbo, bali pia ilitumika kwa matibabu ya nje! Kama kutibu vidonda n.k..Tunaona jambo hilo katika ule mfano Bwana Yesu alioutuoa wa Msamaria mwema…
Luka 10:30 “Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. 32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.
Luka 10:30 “Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.
31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.
Umeona hapo?..alimpaka Mafuta na kutia Divai katika majeraha ya yule mtu. Ikionesha kuwa Divai ilikuwa na kazi pia ya kutibu vidonda!..
Sasa tukirudi katika nyakati zetu, tuna dawa zinazotibu vidonda, hatuwezi kutumia tena divai…ingawa sio dhambi wala kosa kuitumia, lakini zipo dawa zinazofanya kazi nzuri Zaidi ya divai, kwamfano kuna dawa inayoitwa SPIRIT wengi wetu tunaijua, dawa hii ni maalumu kwa kusafishia vidonda na kuua vijidudu visivyoonekana kwa macho, dawa hii inakiwango kikubwa sana cha KILEVI kuliko hata DIVAI….kilevi kilichopo ndani ya dawa hiyo ambayo wengi wetu tunaitumia pasipo kufahamu, ni kiwango kikubwa kiasi kwamba mtu akiinywa kwa bahati mbaya anayo hatari ya kuwa kipofu…Hakuna pombe yoyote duniani inayonywewa na mwanadamu yenye kiwango cha kilevi kikubwa kama hicho kilichopo kwenye Spirit.
Kadhalika, zipo pia dawa zinazotumika na wengi zenye kiwango cha kilevi ndani yake, Kwamfano kuna dawa ya kuongeza vitamin kwa kwa Watoto na watu wazima, inayoitwa SSS TONIC Dawa hii ina kiwango cha kilevi asilimia 12, kiasi kwamba mtu anayeitumia akinywa nyingi pamoja na madhara mengine atakayopata lakini pia atalewa!..ndio maana inatumika kwa kiwango kidogo sana kilichothibitishwa na madaktari kwamba hakitaweza kuleta madhara, wala kumlewesha mtu, kijiko kimoja au viwili vya chai, inatosha….sasa kwa njia hiyo iyo ndio Mtume Paulo alimshauri Timotheo atumie Mvinyo (Divai) kidogo kwa ajili ya tumbo..
Pia zipo dawa nyingi za kutuliza maumivu zimetengenezwa na kiwango fulani cha kilevi, ambazo mtu akinywa analewa… na kuna dawa za kuoshea midomo zenye kiwango cha kilevi ndani yake…
Kadhalika dawa nyingi za maji maji zinazotumika kutibu matatizo ya kifua na kukohoa, zimetengenezwa kwa kiwango Fulani cha kilevi ndani yake, kwamfano dawa kama expectorant, Chlorintmeton n.k hizi ni dawa za kifua za chupa zina kiwango cha kilevi ndani yake… kilevi hicho kimewekwa ndani yake kusaidia kuihifadhi dawa hiyo ikae kwa muda mrefu…Hivyo kwa namna moja au nyingine, watu wote wameshakunywa au kutumia kilevi pasipo kujijua kwa malengo mbali mbali kama tiba ya ndani au ya nje…lakini si kwa lengo la kulewa, wala kujiburudisha..
Sasa Divai hiyo zamani ilitumika katika kushiriki meza ya Bwana, na si kwa kulewa.. ambayo inawakilisha damu ya Yesu Kristo, na wakristo wa kanisa la kwanza walikuwa wanaitumia kwa kiasi kidogo sana katika kushiriki meza ya Bwana, na si kwa kulewa…kama tu vile mtu anayetumia mojawapo ya dawa hizo hapo juu kwa kiwango kidogo sana cha tiba, na kisiwe na madhara ya kumlewesha…Kadhalika na katika meza ya Bwana Divai ilikuwa inatumika kwa kiwango kidogo sana, kisichoweza kumfanya mtu alewe kabisa, mtu alikuwa anakunywa kiwango kidogo sana hata robo glasi inaweza isifike, kama ishara tu ya kushiriki DAMU YA YESU…Ingawa walikuwepo watu wachache waliokuwa wanakunywa kwa kiwango kikubwa mpaka kulewa! Hao ni wale ambao walikuwa ni walafi na walevi ambao… hawawezi kuupambanua vyema Mwili wa Kristo na Damu yake, na Mtume Paulo aliwakeme vikali na kuwaonya….kasome (1Wakorintho 11:21-34).
Kwahiyo Divai kama wakristo wa kanisa la kwanza walivyoitumia kwa lengo la kushiriki, na sisi tutafanya kama wao, kwa lengo hilo hilo,tunaitumia katika kushiriki meza ya Bwana katika kiwango kidogo sana kitakachotufanya tusilewe kama wao walivyofanya…na hatunywi divai hiyo kwa hamu, wala kwa kiu, wala kwa kujiburudisha, wala hatuitumii kwa matumizi mengine yoyote ya tamaa wala ulafi..tunatumia kama ishara ya Damu ya Yesu isiyoharibika, kama Damu ya Yesu yenye matumizi mengi, kutibu mambo yote ya rohoni na mwilini, ndivyo ilivyo divai.
Kinachotokea kwenye baadhi ya makanisa yasiyokuwa ya kiroho yanatumia mistari hii ya Biblia kuhalalisha unywaji wa pombe, hivyo mtu yeyote akijisikia tu hamu, au haja ana kwenda kunywa pasipo sababu yoyote, na kulewa kwasababu Mtume Paulo kasema..’usitumie maji peke yake bali mvinyo pia’…Ndugu hiyo sio kazi ya divai kwa Mkristo, na pia pombe nyingine zozote hazijatengenezwa kwa lengo la matibabu, pombe kama hizi zinazouzwa madukani, zimetengenezwa kwa lengo la mtu kulewa, na ulafi, na kujifurahisha, hazijashauriwa hata na daktari yoyote zitumike, na wala hakuna daktari yoyote anayemshauri mtu akanywe pombe…kwahiyo ulevi wa aina yoyote ule ni dhambi…Hakuna mkristo yeyote katika agano jipya aliyelewa kwa pombe hakuna! Na wala maandiko hayajahalalisha ulevi..(Kwa maelezo marefu juu ya ULEVI, Tutumie ujumbe inbox tutakutumia somo hilo).
Vile vile kuna watu wanaotumia juisi ya mzabibu katika kushiriki, lakini ukweli ni kwamba hakuna maandiko yoyote yanayoonyesha kilichokuwa kinatumika ni pombe, bali ni Divai kama divai yenye kilevi ndio iliyokuwa inatumika.
Bwana akubariki sana.
Maran atha! .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
JE! ULEVI NI DHAMBI?
MABALASI VILIKUWA NI VYOMBO VYA KUWEKEA NINI?
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU