JIBU: Ipo mitazamo mingi, ihusuyo eneo halisi la makaburi ya wazazi wetu wa kwanza, Kwamfano kwa mujibu wa hadithi za kiyahudi, wao wanaamini kuwa Adamu na Hawa walizikwa pale Israeli, mahali palipoitwa Hebroni katika pango lijulikanalo kama pango la Makpela. Ambalo baadaye Ibrahimu na Sara walikuja kulinunua likawa ni eneo la maziko yao ya kifamilia, (Mwanzo 49:29-31) kwa urefu wa habari hiyo fungua hapa usome >>> Pango la Makpela ni lipi,
Wengine, wanaamini kuwa pale Kristo aliposulubiwa Golgota, ndipo palipokuwa kaburi la Adamu, wakiamini kuwa kama Kristo alivyoitwa Adamu wa pili, maana yake ni alikuja kurudisha kile kitu ambacho Adamu wa kwanza alikipoteza, yaani uzima. Hivyo kama Adamu alileta kifo, Kristo alileta uzima kwa msalaba wake, na aliyafanya hayo juu ya kaburi la Adamu.
Lakini je! kuna usahihi kwa mitazamo hiyo.
Kwasababu biblia haijaeleza chochote, kuhusiana na kaburi la Adamu na Hawa, hii yote ni mitazamo, ambayo yaweza kuwa ukweli au uongo, tusiweke imani yetu moja kwa moja katika mitazamo. Kwasababu gharika ilipokuja ilivuruga ramani yote ya ulimwengu, isingekuwa rahisi kupatambua mahali sahihi alipozikwa Adamu, isipokuwa kwa ufunuo.
Na habari hiyo kutoandikwa ni kutuonyesha kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua Adamu alizikiwa wapi. Ushindi tulioupata kwa kifo cha Kristo, na kufufuka kwake, ni habari tosha tunayopaswa tuitafakari usiku na mchana, zaidi ya kaburi la Adamu.
Lakini swali ni Je! Yesu amefufuka ndani yako? Fahamu kuwa Ikiwa bado hujazaliwa mara ya pili, kifo kina nguvu juu yako, ukifa hakuna maisha kwako, ni mateso katika moto wa jehanamu. Lakini ukizaliwa mara ya pili uzima wa milele unao na hata ukifa, utakuwa unaendelea kuishi.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Unasubiri nini? Usiokoke leo.
Saa ya wokovu ni sasa, ni pale tu unapotubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kumwita Yesu ayatawale maisha yako, kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Hapo unakuwa tayari umezaliwa mara ya pili. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo wa Sala hiyo ya toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
JINA LAKO NI LA NANI?
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
Rudi Nyumbani
Print this post
Maelezo ya Mithali 28:20
“Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa”.
Mstari huo unatufundisha jinsi pupa (kutaka vya haraka), inavyokinzana na neno “Uaminifu”. Ikiwa na maana mtu ambaye anataka wingi kwa muda mfupi, ni lazima tu atatumia njia isiyo ya haki, ili avipate anavyovitaka. Kwamfano viongozi wa nchi au waajiriwa wenye tamaa ya mafanikio ya haraka, wanaotaka mwezi huo huo wajenge, au wawe na miradi mikubwa, mwisho wa siku huwa wanatumia njia za wizi, ili kufikia mafanikio yao. Hiyo ndio sababu inayowafanya wapoteze uaminifu katika kile walichokabidhiwa.
Na hatma ya hawa watu, ni kukutana tu na matatizo, aidha kufungwa, au kufukuzwa kazi, au kutozwa faini, n.k.. na kuangukia hasara tu sio faida.
Ndio maana ya hili Neno
Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Kwasababu mafanikio na pupa, havipatani kabisa. Bali achumaye kidogo-kidogo ndiye atakayefanikiwa(Mithali 13:11)
Yusufu alirekodiwa kuwa ni mwaminifu katika kazi yake. Na hivyo, akabarikiwa na Bwana mpaka akapewa nafasi ya uwaziri-mkuu wa taifa kubwa la Misri (Mwanzo 39:1-6). Danieli alirekodiwa kuwa muaminifu na hivyo akadumu katika falme zote mbili zilizotawala dunia wakati ule, yaani Babeli pamoja na Umedi na Uajemi (Danieli 6:4).
Lakini pia Neno hili linatafsirika rohoni.
Katika kazi ya Bwana, palipo na UAMINIFU, basi mwishowe Mungu huwa anabariki utumishi wa mtu huyo. Alisema maneno haya;
Luka 16:10 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. 11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
Umeona? Lakini ukikosa uaminifu, ndio utataka utumie njia zisizompendeza Mungu ili uone matokeo unayoyatarajia haraka, ndio hapo utaona mhubiri anatumia njia za undanganyifu kutengeneza shuhuda za uongo, ili watu wajue kuwa anao-upako wajae kwenye kanisa lake. Mambo kama haya hatma yake ni , uangamivu. Wengine, wanahubiri injili ya kisiasa, au vichekesho, wengine wanapachika staili za kidunia madhabahuni na kwenye kwaya, hawahubiri tena kweli, wala hawakemei dhambi, wakihofia watu kukimbia makanisa yao. Wanapoteza uaminifu ili wapate watu wengi kanisani. Hii ni hatari kubwa!
Hawajui kuwa ndani ya uaminifu, zipo Baraka. Na Mungu anaona, Mungu atamnyanyua tu mtu huyo.
Hivyo tupende kusimamia kweli, turidhike na nafasi zetu, tupinge mambo ya giza, TUWE WAAMINIFU katika yote na hakika tutaona Baraka za Bwana.
UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Maana ya Mithali 9:17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
THAWABU YA UAMINIFU.
Rudi nyumbani
Katika biblia mtu ambaye alipokea taarifa iliyofichwa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Kwa watu aliitwa mwonaji. Alipokea aidha kupitia, maono, ndoto, au kufunuliwa dhahiri, Mfano wa Hawa alikuwa ni Samweli…
1 Samweli 9:9-12
[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.) [10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu. [11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? [12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)
[10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.
[11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?
[12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
Lakini baadaye watu Hawa walikuja pia kuitwa Manabii kama tunavyosoma kwenye vifungu hivyo
Isipokuwa Maana ya Nabii ni Pana zaidi sio tu kupokea taarifa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Bali pia alisimama kufundisha na kuwarejesha watu, katika Sheria ya Mungu.ikiwemo kukaripia na kukemea, na kuonya. Mfano wa Hawa ni Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yona, Hosea, Mika, Hagai, Malaki na wengine.
Hivyo nabii ni lazima pia awe mwonaji, kwamba apokee pia taaarifa za Moja Kwa Moja kutoka Kwa Mungu, na kufichua Siri zilizositirika lakini mwonaji haikuwa lazima afanye kazi ya kinabii, Bali ni kusema tu kile anachoelezwa, au kufichua Siri zilizojificha, au kuomba mwongozo wa Roho wa Mungu, Kwa ajili ya jambo/tatizo Fulani.
Hivyo kuhitimisha ni kwamba Kuna maandiko mengine yanawataja waonaji, lakini yalimaanisha pia ni manabii, na mengine yanabakia kumaanisha walewale tu waonaji.
Mfano wake ni Samweli, ambaye alikuwa ni mwonaji lakini pia ni Nabii.
1 Mambo ya Nyakati 29:29
[29]Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
Soma pia vifungu hivi, kufahamu zaidi.
(2Samweli 24:11, 2Nyakati 16:7, 29:30,)
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA.
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?
Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?
Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake.
Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii.
Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.
Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.
Yohana 8:52-53
[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. [53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)
Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.
Yakobo 1:19
[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!
KUOTA UPO UCHI.
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;
Fahamu Maana ya;
Mithali 18:18 Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Kupiga kura ni Moja ya njia ambayo ilitumika kuleta suluhisho lenye utata, na wakati mwingine kuchagua viongozi/wamiliki. Pitia hapa ujue zaidi kuhusu kura zilivyopigwa zamani za biblia…>> Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;
Na Mungu wakati mwingine aliingilia kati na kuleta majibu yake sahihi kwa kupitia njia hiyo. Kwamfano wakati ule Yona anamkimbia Mungu, Hali ilipochafuka kule baharini, utaona wale watu walipiga kura, ili kujua sababu ya mambo yale ni nani na Ile kura ikamwangukia Yona.
Mitume wa Bwana baada ya kuomba, kuhusu mrithi wa nafasi ya Yuda wakapiga kura katika ya wale wanafunzi wawili, nayo ikamwangukia Mathiya, na likawa kweli ni chaguo la Mungu.(Matendo 1:15-19),
Hata wakati wa nchi ya Israeli kugawanywa . Kura zilitumika kuamua nani akae wapi, na nani arithi wapi (Hesabu 26:55).
Hivyo kupiga kura ilikuwa ni mojawapo ya njia kuleta jibu lisilokuwa na upendeleo. Au lililoegemea upande Fulani mmoja. Na kwa kufanya hivyo malalamiko mengii yalikomeshwa kwasababu maamuzi hayakuamuliwa na upande wowote ule.
Ndio maana ya hili andiko
Mithali 18:18
[18]Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Hata kipindi Cha sasa njia ambayo hutumiwa kuchagua viongozi wengi ulimwenguni Huwa ni ya kura. Isipokuwa hii siyo ya kurusha SHILINGI, au kete angani inayomwangukia mmojawapo ndio anakuwa kiongozi..hapana Bali ni kuruhusu Kila mmoja kutia maoni yake..Kisha zinahesabiwa na yule mwenye nyingi hupewa. Na hivyo hakuna malalamiko.
Tofauti na Ile mtu atawadhwe tu Moja Kwa moja kuwa kiongozi, Hiyo huleta ukakasi mwingi.
Hivyo ni kutufundisha kua Bwana anaouwezo wa kuingilia kura zipigwazo na kuleta majibu yake sahihi..hususani pale anaposhirikwa Kwa maombi, na kama hakusema Kwa njia nyingine ya Moja Kwa moja.
Bwana akubariki
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
MKUU WA ANGA.
Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
Hakuna namna utautenganisha “Moyo” na “hazina”.. vitu hivi vinaenda pamoja!.(ni sawa na miguu na mwili,..mahali miguu ilipo na mwili upo, miguu haiwezi kuwa mahali pengine na mwili mahali pengine) Vile vile Moyo wa mtu na hazina yake, vinaenda pamoja…Pale mtu alipojiwekea hazina, ni lazima (akili yake yote na fikra zake na hisia zake na mawazo yake yatakuwa huko).
Ndio maana mtu aliyejiwekea hazina kubwa ya mali za kidunia, halafu mali zile zikapotea zote ghafla, ni rahisi mtu huyo kuchanganyikiwa au kupoteza maisha maisha kabisa!.
Kwanini?..Kwasababu Moyo wake wote (fikra, mawazo, akili, malengo, uzima, hadhi) vilikuwepo katika mali zile, na sasa hana tena!, hata maisha kwake yanakuwa hayana maana tena!. Ndivyo ilivyo, kwamba Moyo siku zote unafuata hazina ilipo!, na unaishi kutokana na hazina mtu alizonazo. Ndivyo moyo wa mtu ulivyoumbwa!..
Vile vile mtu anayejiwekea hazina mbinguni, ni lazima fikra zake, mawazo yake, akili yake, malengo yake yote yatakuwa kule mbinguni hazina yake ilipo.
Sasa Bwana Yesu alitufundisha kanuni ya kuielekeza Mioyo yetu mbinguni, kwamba si kwa kuomba tu! Bali kwa kujiwekea hazina kule mbinguni,..kwanini?…kwasababu tutakapojiwekea hazina kule juu mbinguni basi mioyo yetu (yaani fikra, fahamu, akili, mawazo na hisia) zitaelekea kule Mbinguni, bila shuruti!.
Sasa swali, tunajiwekeaje hazina juu mbinguni?.. yeye mwenyewe (Bwana Yesu) alitufundisha kanuni katika Luka 18:18-22
Luka 18:18 “Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? 19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. 20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako. 21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu 22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, NAWE UTAKUWA NA HAZINA MBINGUNI; kisha, njoo unifuate”.
Luka 18:18 “Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?
19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.
20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu
22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, NAWE UTAKUWA NA HAZINA MBINGUNI; kisha, njoo unifuate”.
Na tena anarudia maneno kama hayo hayo katika Luka 12:32-34…
Luka 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. 33 Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, AKIBA ISIYOPUNGUA katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. 34 KWA KUWA HAZINA YENU ILIPO, NDIPO ITAKAPOKUWAPO NA MIOYO YENU”.
Luka 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.
33 Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, AKIBA ISIYOPUNGUA katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.
34 KWA KUWA HAZINA YENU ILIPO, NDIPO ITAKAPOKUWAPO NA MIOYO YENU”.
Umeona?.. Kumbe kanuni ya kujiwekea hazina mbinguni ni kumtolea Mungu!..
Kwanini?.. Kwasababu tunapomtolea Mungu vile tulivyo navyo, mawazo yetu yatakuwa siku moja kwenda kupata thawabu mbinguni!, fikra zetu zitakuwa siku moja kwenda kuona miji mizuri tuliyoandwaliwa, mawazo yetu yatakuwa siku moja kwenda kuvikwa taji……hivyo muda wote tutakuwa tunafakari tu yaliyo ya juu na huko ndiko mioyo yetu itakapokuwepo!.
Ndio maana utaona watu wanaojitoa kwa Mungu kuanzia miili yao, mpaka mali zao, muda wote wanawaza unyakuo utakuwa lini?, muda wote wanawaza Kristo anakuja lini?.. ni kwanini wanakuwa hivyo?, si kwamba wanajilazimisha kuwa hivyo, ni kwamba tayari mioyo yao ipo mbinguni kwasababu wamejiwekea hazina huko.
Hii ni kanuni rahisi kabisa ya kuhamisha mioyo yetu kutoka kutafakari MAMBO YA CHINI na kuanza kutafakari MAMBO YA JUU!.
Ukitaka uwe mtu wa kutafakari mambo ya mbinguni sana, mtolee Mungu kuanzia muda wako, akili yako, mwili wako, ufahamu wako na hata vitu vyako!.. Hapo moyo wako wenyewe tu utaanza kuelekea mbinguni bila hata kutumia nguvu nyingi!,. Utajikuta tu unaanza kutamani kumwona Yesu, utajikuta unatamani ile siku ya mwisho ifike n.k
Laakini kinyume chake usipofanya hivyo na ukajitumainisha katika kujiwekea hazina katika mambo ya ulimwengu, basi fahamu kuwa moyo wako utaelekea tu katika mambo ya ulimwengu hata kama hupendi!.
Wakolosai 3:2 “Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi”.
Maran atha!
Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
UKIOKOKA, JIANDAE KUPITISHWA USIPOPATAZAMIA.
Yeshuruni ni nani katika biblia?
Swali: Biblia inatufundisha katika Wagalatia 5:23 kuwa “tuwe wapole kiasi”, sasa napenda kujua mtu utakuwaje mpole kiasi.
Jibu: Tusome,
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 UPOLE, KIASI; juu ya mambo kama hayo hakuna sharia”.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 UPOLE, KIASI; juu ya mambo kama hayo hakuna sharia”.
Hapa biblia haisemi kuwa tunda la Roho Mtakitifu kuwa ni “Upole kiasi” kana kwamba “upole unapaswa uwe na kiasi”…. La! Bali inasema tunda la Roho ni “Upole”, halafu “Kiasi”… hayo ni maneno mawili yaliyotengenishwa na alama ya mkato.
Maana yake “Upole” ni kitu kingine na “Kiasi” ni kitu kingine. Ikiwa na maana kuwa Tunda la Roho “Upole ulio wote” na sio upole kiasi.
Biblia inatufundisha tuwe watu wapole kama Hua (Njiwa).
Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua”
Hua ni ndege mpole sana ndio maana Roho Mtakatifu alitumia umbile la Hua kushuka juu ya Bwana Yesu wakati ule alipobatizwa (Mathayo 3:16)... Na maandiko yanazidi kutufundisha kuwa Bwana Yesu ni Mpole..
Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.
Soma pia, Mathayo 11:29, utaona sifa hiyo ya Bwana ya upole ikitajwa..
Na sisi pia ni lazima tuwe na sifa hiyo ya “Upole” kama ishara mojawapo ya kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu… shetani kaligeuze Neno hili la Upole na kuweka “Upole kiasi” ili kuchochea ubaya ndani ya watu.. Kwamba ni vizuri kuwa wapole lakini tusiwe wapole sana, tuwe wapole tu kiasi!. Huo ni uongo wa adui!.
Na kumbuka kuna tofauti ya “upole” na “unyonge”. Biblia haitufundishi kuwa wanyonge, bali kuwa wapole, Mtu mpole ni yule ambaye ana uwezo wote wa kutumia ukali lakini hautumii!, kama alivyokuwa Bwana Yesu… Lakini mnyonge ni yule anayekuwa analazimika kuwa hivyo mpole kutokana tu na mazingira..na akitoka katika hayo mazingira basi tabia yake ya ubaya na ukali usio na maana na vurugu inajidhihirisha.
Bwana atusaidie .
Upole ni nini?
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).
Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?
Jibu: Tusome kuanzia mstari wa 5..
Zaburi 91:5 “Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, 6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri”.
Zaburi 91:5 “Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri”.
“Uele” ni janga linaloleta mauti linaloweza kumpata mtu.. ajali ya gari ni mfano wa Uele, Ajali ya kuzama kwenye maji ni mfano wa “Uele”, janga la kuungua moto mpaka kufa ni mfano wa “Uele”.
Maandiko yanatufundisha kuwa wote wamtumainio Bwana, na kumkimbilia na kumfanya kuwa ngome na msaada, hawatakuwa na hofu na majanga hayo, kwani Mungu ni ngome ya wote wanaomcha, naye ndiye awaokoaye na majanga.
Zaburi 121:4 “Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume. 6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. 7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. 8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele”.
Zaburi 121:4 “Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele”.
Je una hofu na UELE?..Mpokee Yesu kwa kutubu dhambi na kujazwa Roho Mtakatifu, naye atakupa furaha nawe utaishi maisha ya raha na ya utulivu.
Zaburi 127:2 “……Yeye humpa mpenzi wake usingizi”
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Fahamu Maana ya Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”.
Mara nyingi Sulemani kwa hekima ya Roho aliongozwa kuona uhusiano uliopo kati ya uvivu na umaskini. Kama tu kinyume chake, sehemu nyingine alivyoweka uhusiano kati ya bidii na utajiri(Mithali 10:4). Vivyo hivyo uvivu na umaskini havipishani.
Na kama anavyosema hapo, uvivu humpeleka mtu katika usingizi, lakini sio usingizi tu bali ule mzito, Kwasababu gani? Ni kwasababu mwili haupo katika hali ya kujishughulisha, na hivyo utalala tu, na Bado utaendelea kulala siku baada ya siku.. Na matokeo yake kutokuzalisha chochote kinachoonekana, hatimaye, umaskini unaingia.
Hivyo mstari huo unalenga Nyanja mbili. Ya kwanza ni ule uvivu wa mwilini, na ya pili ni ule uvivu wa rohoni.
Mungu katuumbia kufanya kazi, watu wote (ikiwemo watakatifu). Maana yake ni kuwa ikiwa huna huduma yoyote ya madhabahuni Bwana amekuitia, ambayo inakufanya utumike muda wote hapo. Ni sharti ufanye kazi. Mtume Paulo alilionya kanisa juu ya watu ambao hawafanyi kazi kwamba ni sharti wajishughulishe ili wapate na kitu cha kuwagawia na wengine (2Wathesalonike 3:10)
Lakini pia Uvuvi wa rohoni. Mtakatifu anapokuwa mvivu, kusoma Neno, yaani muda wa Neno anakwenda kutazama filamu, anakwenda kijiweni kucheza drafti,.Anakuwa mvivu kuomba, Unapofika huo muda tu anaona usingizi ni bora kuliko kuomba,.Au Mtakatifu hataki kushuhudia habari za Kristo kwa wengine, anasema jua kali. Sasa mtu huyo anajiandaa kuwa maskini kiroho. Yaani atakuwa katika wokovu usiokuwa na matunda, ukuaji wake wa kiroho utakuwa hafifu, Neema ya Mungu haitatenda kazi kwa wingi juu yake, na hivyo atakosa mema mengi ya Mungu katika safari yake wa wokovu hapa duniani.
Uvuvi wowote, una hasara, kwahiyo tuuweke katika orodha ya maadui zetu wa imani.
Bwana atusaidie.
Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Mstari huo unatufundisha mtu aliyejaa “Busara” moyoni ni mtu wa namna gani..
Anaeleza ni Yule ambaye anaouwezo wa kughahiri hasira yake, na pia kupenda kusemehe makosa. Ambayo ndio sifa ya Mungu, Aliyonayo, soma;
Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Hivyo na sisi hatuna budi kutokuwa watu wa kukasirika haraka, mpaka ikaleta athari nje, kwamfano umeumizwa na mke/mume wako, tunapaswa tujifunze kuachilia mara moja, lakini pia kusamehe, sio kuweka kinyongo, au uchungu moyoni. Au mtu amefanya kosa la kukuudhi ambalo anastahili adhabu, si vema kuwa wepesi wa kuadhibu bali kuahirisha hasira hizo kwasababu Mungu naye anatusamehe makosa yetu, hatuadhibu kila kosa.
Bwana alisema kusamehe kwetu hakupaswi kuwe na ukomo, alitumia lugha ya hata ‘saba mara sabini’ kwa siku(Mathayo 18:22). Kuonyesha kuwa kusamehe kwetu kunapaswa kuwe endelevu. Ili tufikie hatua ya Kuona ‘fahari’ katika uwezo wa kusamehe, zaidi ya kuona fahari katika uwezo wa ‘kupata vitu’. Yaani tuhesabu ni watu wangapi tumewasamehe, hapo ndio iwe furaha yetu. Na kwamba tuipime busara yetu kwa kiwango cha kuiharisha hasira zaidi ya uwezo wa ‘kuwa na maneno mengi ya hekima’.
NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?
Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?
TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?