SWALI: Ni vitu vipi hivyo tumekirimiwa vitupasavyo uzima na utauwa? (2Petro 1:3)
2 Petro 1:3
[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia “vitu vyote” vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
JIBU: Andiko hilo linatufundisha kuwa Mungu anao uweza wake, ambao una nguvu ya kumfanya mtu kuwa kama anavyotaka. Sasa hapo tunafunuliwa kuwa uweza huo ameuachilia katika maeneo mawili makuu la kwanza ni UZIMA la pili UTAUWA. Uzima ni maisha ya milele, na utauwa ni utakatifu.
Sasa swali linauliza ni vitu gani hivyo ambavyo Mungu ametukirimia vinavyozungumziwa hapo vitufanyavyo kuufikia huo uzima na utauwa, anaousema?
Vitu vyenyewe ni kama vifuatavyo
Bila Yesu Kristo kuja duniani, kuwa fidia ya dhambi zetu kwa kifo chake, tusingeweza kupokea uzima wa milele. Kwasababu ilihitajika kumwagika kwa damu isiyokuwa na dhambi ili kutuondolea sisi dhambi zetu tupokee uzima wa milele. Hivyo uweza huu wa uungu, umetukirima Yesu Kristo, kutuondolea dhambi ndani yetu.
Tuna kila sababu za kumshukuru Mungu sikuzote, kwa huruma zake hizi. Tunaye mkombozi ambaye kila amwaminiye tu. Uzima anao. (Yohana 3:16)
Roho wa Mungu ni msaidizi wetu, bila yeye, ni kweli tungesamehewa dhambi lakini tusingeweza kuwa watakatifu. Hivyo yeye anapokuja juu yetu na kujaa vizuri tunajikuta tunaweza enenda katika mwenendo wa utakatifu. Hivyo huu ni uweza wa Mungu mwenyewe.
Yohana 14:16
[16]Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Wagalatia 5:16
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Hichi ni kitu kingine ambacho Mungu ametukirimia kwa uweza wake, kwa kuisoma tunatambua wazo lote la Mungu, na hivyo kuturahisishia kuisikia sauti ya Mungu. Tusomapo biblia tunabadilishwa tabia zetu, kwa maonyo, mafundisho, faraja, shuhuda n.k.
2 Timotheo 3:16
[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Kanisa ni uweza wa Mungu kwetu, hekima ya Mungu ambayo aliibuni yeye mwenyewe siku ile ya pentekoste. Kuwakusanya watakatifu wake na kuwahudumia kwa karama mbalimbali. Kanisa humlinda mwamini, kanisa humwombea mwamini, humsaidia mwamini, humfariji mwamini na kumwongoza.
Sikuzote Uthabiti wa mwamini hutegemea kanisa. Mtu asiye na kanisa (ushirika), ameukana uweza huu wa Mungu, ambao Mungu huutumia kutukamilisha sisi.(Waebrania 10:25)
1 Wakorintho 12:27-28
[27]Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. [28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
[27]Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
Bwana huwatuma malaika wake, kumlinda mwamini asijikwae. Huu ni uweza wa Mungu pia.
Waebrania 1:14
[14]Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Zaburi 91:11-12 [11] Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. [12] Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
[14]Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Zaburi 91:11-12
[11] Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. [12] Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Kama si Mungu kutuagizia malaika zake, bila shaka adui angepata penyo nyingi sana za kutuletea majaribu na kutuangusha. Ukiwa ndani ya Kristo adui hana nguvu juu yako, kwasababu unalindwa na jeshi lake. Unapiganiwa kwa namna usiyojua wewe.
Na hivyo kuishi maisha ya utauwa kwako inakuwa ni vyepesi zaidi ya mtu mwingine yeyote aliye nje.
Ukipungukiwa kimoja wapo, ni lazima tu eneo lako la utauwa au uzima litakuwa na kasoro. Kumbuka Bwana ameshatukirimia ni sisi tu kukubali na kupokea.
Wokovu upo bure, biblia ipo wakaki wote, Roho yupo, kanisani lipo, malaika wapo. Amini tu na kutubu dhambi zako, kwa Kumaanisha kabisa kugeuka na kumfuata Yesu, akupaye ondoleo la dhambi. Kisha ukabatizwe, upokee Roho. Na baada ya hapo, shiriki sasa vitu hivyo vya ki-ungu kwasababu vimewekwa tayari kwa ajili yako na mimi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
Rudi Nyumbani
Print this post
Wazia jambo hili, raisi amepewa taarifa na wataalamu wake wa hali ya hewa kwamba kuna kimbunga kikubwa kinatokea bahari.
Hivyo akachukua hatua ya kuwatahadharisha wananchi wake wasifike maeneo yote ya pwani. akawaelekeza na namna ya kujilinda, na mazingira yote hatarishi, akawajuza na madhara ambayo tayari kimbunga hicho kimeshaleta, akawaonya sana wakae ndani mpaka hicho kipindi chote cha hatari kitakapokwisha.
Lakini cha kushangaza kesho yake wakaonekana watumishi wa raisi na mawaziri , pamoja na watumishi wote wa serikalini wakiwa ufukweni wakiogolea na kufurahi na kustareheka..kana kwamba hakuna hatari yoyote mbeleni.
Unadhani ni wazo gani litajengeka kwa wananchi juu ya raisi wao?
Watasema raisi ni mwongo. Ametulaghai, mbona mamlaka yake haichukui hatua ya janga lililotangazwa?
Lakini heri na hapo, unadhani raisi naye atajisikiaje moyoni, kwa wale watu waliomtendea hivyo?
Sasa hilo ndilo watu wanalolifanya kwa Mungu sasa mpaka anaonekana ni mwongo.
Neno la Mungu linasema…
1 Yohana 5:10-12
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. [11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. [12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
[12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Mungu alimtuma Yesu duniani, kuushuhudia ulimwengu kuwa una dhambi, Na mwana wake kuja duniani ni kwa lengo hilo kuu la kuwaokoa watu dhambini.
Hivyo Mungu akamshuhudia kwa sauti kutoka mbinguni, kwa ishara na miujiza mingi,.kwa Roho Mtakatifu aliyetuachia, lakini bado watu wakapuuzia, wakaendelea na mambo yao. Sasa huko ndiko kumfanya Mungu mwongo. Yaani kufikiri kuwa sisi hatukutenda dhambi, tunamfanya yeye kuwa mwongo.
1 Yohana 1:10
[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Hivyo mtu yeyote anayekataa injili, ni kwamba anamfanya yeye aonekane mwongo. Ushuhuda wake ni uongo, kazi aliyoifanya ni bure, ni kuthibitisha mtu anaweza kuishi tu mwenyewe apendavyo na akawa na maisha ya milele?
Je! umempokea Yesu, kama Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kama ni La! ndugu Kamwe usimfanye Mungu mwongo.
Amini ushuhuda wake kupitia mwana wake kwasababu ni kweli usipookolewa na yeye. Uzima wa milele haupo ndani yako. Dhambi ipo, na bado itaendelea kuwepo juu yako, hata kama utakuwa na matendo mazuri kiasi gani.
Fanya uamuzi sasa ya kuokoka. Hukumu ipo mbele na inatisha.
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.
NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?
NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU
Kitabu hiki kama kinavyoanza na utambulisho wake. Kiliandikwa na Yakobo aliye mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo. (Yakobo 1:1).
Yakobo huyu sio yule mmoja wa mitume kumi na mbili wa Yesu, (yaani ndugu yake Yohana wana wa Zebedayo)..Hapana bali ni mmoja wa ndugu za Yesu wa kunyonya aliozaliwa nao (kimwili) kupitia Mariamu. Na huyu ndiye baadaye aliyekuwa kama moja ya nguzo ya kanisa la Yerusalemu. Wengine wakiwa ni Petro na Yohana.
Inaonekana wakati Petro alipotoka na kwenda kusimamisha makanisa katika mataifa ya mbali, yeye ndiye aliyebakia kama msimamizi mkuu kwa kanisa la Yerusalemu,
Vilevile majaribu na dhiki mbalimbali zilizolikumba kanisa hili tukiachia mbali janga la njaa kubwa lililotokea wakati ule, mpaka wakapelekewa misaada kutoka kwa makanisa mengine (Matendo 11:28–30), lakini pia na dhiki walizozipata kwa wayahudi wasioamini, mtume huyu Yakobo alizifahamu sana.
Ndio maana katika sehemu kadha wa kadha za waraka huu Yakobo anayazungumzia majaribu,
Huku yeye akiyachukulia katika taswira nyingine, tofauti na kama yangepaswa kuchukuliwa, akielezea kwamba Majaribu na dhiki, sio jambo la kukaa na kuhuzunika, kinyume chake tuyaone kama ni fursa nzuri ya sisi kuimarishwa na kuthibitishwa kiimani.
Lakini Maudhui kuu ya waraka huu, ni kueleza mahusiano kamili yaliyo katika imani, na matendo yake. Kwamba hivi vitu viwili haviwezi kutenganishwa.
Waraka huu aliuelekeza kwa wayahudi wote waliotawanyika ulimwenguni kote (kwa wakati ule). Ambao kwasasa unatuhusu sote.
Huu ndio ufupisho wake katika maeneo makuu SITA (6).
Yakobo anaeleza.
Kwa ufupi mtume Yakobo kwa uvuvio wa Roho alilenga kuimarisha watakatifu katika eneo la utendeaji kazi imani. Na hiyo pengine ilidhaniwa au kufikiriwa kuwa wokovu ni kuamini tu, bila kuonyesha matendo yoyote. Lakini katika waraka huu analiweka sawa kwa kuonyesha matendo na imani hivitenganiki, kama mtu akijaribu kuacha kimoja, basi ni kifo mfano wa roho na mwili visivyoweza kutenganika.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA MATHAYO.
Uchambuzi na Mwandishi wa kitabu cha Wagalatia
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
WhatsApp
SWALI: Mitume walikuwa na maana gani kuwasihi wanafunzi kule Antiokia, waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? Ni maana ya hiyo kauli?
Matendo 11:22 Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia. 23 Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. 24 Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.
Matendo 11:22 Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.
23 Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.
24 Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.
JIBU: Kauli hiyo inamaanisha kwa “kusudi sahihi la moyo” sawasawa na imani waliyoipokea, Kwasababu Mitume walijua madhumuni ya wao kumfuata Yesu yakiwa sio sahihi, kusimama kwao kunaweza kusidumu. Kwasababu walijua wapo wanaomfuata Kristo kwa sababu ya fitna, wengine fedha, wengine watu, wengine vyeo, wengine kuajiriwa n.k.. Na hiyo haipaswi. Kwasababu Mungu huuchunguza kwanza moyo wako kilichokupelekea kumfuata ni nini?. Ikiwa sio kwa lile kusudi lake sahihi, hauwezi kusimama.
Sifa hizo za Mungu kuchunguza makusudi ya moyo tunazisoma kwenye vifungu hivi;
Waebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukataokuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Hivyo hata sasa, Mungu anataka tuipokee imani kwa kusudi la kweli la moyo, ili tuweze kudumu, na kuona utendaji kazi wake bora, katika maisha yetu ya rohoni, na pia tuweze kusimama hadi mwisho .
Kusudi sahihi la moyo ni kumfuata Yesu ili akuokoe dhambini, kumtazama Kristo kama dhabihu kamilifu ya Mungu iliyotolewa kwa ajili ya kuondoa dhambi zetu, na sio atupe utajiri, au atuponye magonjwa, au atupe mke/mume.
Kwanini iwe hivyo?
Kwasababu hayo yasipokuja kwa wakati utamwacha Kristo, au yakipatikana basi Kristo hawezi kuwa tena na thamani moyoni mwako, kwasababu kusudi lako moyoni lilikuwa utatuliwe tu changamoto yako, si zaidi. Na ndio maana ni rahisi leo kuona watu wengi makanisani, lakini wasiwe wote wameokoka.
Mitume waliliona hili kama ni jambo muhimu sana kufundishwa mwanzoni kabisa mwa imani kwa waongofu wapya. Vivyo hivyo na sisi tuige fundisho hilo pindi tunapowajenga waongofu wapya.
KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
Nini tofauti ya Majira na Wakati?
Mathayo 21:12 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; 13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Mathayo 21:12 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa;
13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Bwana aliwaagiza wana wa Israeli, kwamba waendapo mbele zake mahali patakatifu alipopachagua wakusanyike kwa ajili ya upatanisho. Kila mtu mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi atatoa nusu shekeli kama kodi, ambapo fedha hiyo ilitumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za hekaluni . Hivyo watu wote walipokwenda hekaluni kwa ajili ya ibada, walihakikisha wanabeba sadaka hiyo kwa ajili ya gharama za hekalu.
Utalisoma hilo katika vifungu hivi;
Kutoka 30:11 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 12 Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa Bwana kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu. 13 Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini;) nusu shekeli kwa sadaka ya Bwana. 14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya Bwana. 15 Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu. 16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Kutoka 30:11 Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
12 Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa Bwana kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu.
13 Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini;) nusu shekeli kwa sadaka ya Bwana.
14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya Bwana.
15 Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Lakini sasa kwa sababu fedha hiyo ilipaswa itolewe kwa fedha ya kiyahudi, na si za kigeni, ikizingatiwa kuwa watu walikuwa wanatoka mataifa mbalimbali ulimwenguni kote kuja kumwabudu Mungu pale Yerusalemu, Sasa hawa wanaoitwa wabadili fedha ndio wakapatia hapo fursa ya kuanzisha biashara hiyo pale hekaluni.
Lakini badala ya kufanya kama huduma, kuwasaidia watu kazi hiyo bila riba, wao wakageuza pale kuwa ni mahali pao pa kujipatia faida, pakawa kama kiini cha soko la fedha ukanda ule wote. Watu walipokuja na fedha zao, waliwageuzia kwa riba ya juu.
Hiyo ndio sababu Yesu kuchukizwa na wale watu, na kwenda kuzipindua meza zao, pamoja na wale wauza njiwa
Hata sasa, desturi hii ya adui inatenda kazi katika nyumba nyingi za Mungu duniani.
Watu hutumia mambo ya kiibada kama njia ya kujipatia faida. Si ajabu hata Mtume Paulo aliliona hilo akasema,
wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. (1Timotheo 6:5).
Utakuta mtu anafanya biashara ya biblia, kando kando ya kanisa. Atakuwa radhi kuzitoza bei zaidi ya kiwango stahiki ili ajinufaishe, kwasababu anajua watu wenye uhitaji wa vitabu hivyo kwa watu huo ni wengi. Mwingine atakuwa anauza maji au mafuta (wayaitayo ya upako), lengo sio kuwasaidia hao watu wapokee huduma, bali ni kujipatia faida.
Injili ya Kristo imekuwa biashara, kumwona mtumishi uombewe, ni lazima uandikiwe kuponi ya fedha, vinginevyo huwezi kumwona.
Sas watu kama hawa Yesu hawezi waonea huruma atazipindua meza zao, kama tu vile alivyozipundua za wale hekaluni. Maana yeye ni yeye Yule jana, na leo na hata milele.
2Timotheo 3:9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Je! Habari iliyo katika 1Nyakati 21:25, na 2Samweli 24:24, ya Daudi kununua kiwanja inajichanganya?
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.
SI KWA FAIDA YA MWENYEZI, BALI KWA FAIDA YETU.
SWALI: Kwanini wale wayunani, walimfuata Filipo na kumwambia tunataka kumwona Yesu, maudhui ya tukio lile ni nini, mpaka lirekodiwe?
JIBU: Kipindi cha Bwana Yesu hadi kipindi chote cha mitume, yalikuwepo makundi mawili ya watu ambayo yalijikita kwa umakini sana katika kutafuta uhalisia na ukweli wote kuhusu masuala ya Mungu.
kundi la kwanza lilikuwa ni wayahudi, na kundi la pili ni wayunani. Tofauti ya wayahudi na wayunani ni kwamba. Wayahudi walijikita kuthibitisha kwa njia ya ishara. Lakini wayunani kwa hekima.
1 Wakorintho 1:22-23
[22]Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; [23]bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
Hivyo Yesu ambaye ni jibu lao wote alipokuja, baadhi ya hawa wayahudi walipomwona Kristo wakaanza kumthibitisha kwa ishara kwa walivyotarajia, kwamba ndiye masihi na mkombozi waliyemtarajia la!.(wakitaka wafanyiwe matendo fulani ya ajabu mbele ya macho yao, waamini)
Ijapokuwa Mungu hathibitishwi kwa ishara, bado Kristo aliwapa ishara.. Na ishara hiyo ilikuwa ni ile ya Yona. kukaa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana na hatimaye kutoka mzima.
Mathayo 12:38 Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.
Mathayo 12:38 Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.
39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.
Hilo lilipokuja kutimia…tunaona wayahudi wengi waliamini, ikiwemo mitume (akina Tomaso). Na ndio ukawa mwanzo wa kumuhubiri Yesu aliyefufuka.
Lakini wale waliotazamia ishara walizoziwaza kwa akili zao, mfano za kushusha moto, kama Eliya, na kusahau ile ya kufufuka ambayo imezidi zote, bado Kristo akabakia kikwazo kwao.
Halikadhalika na kwa wayunani. Walimtafuta Mungu kwa njia ya hekima, ya elimu, ya maarifa, walimtafuta Mungu mwenye siri zote za uumbaji, na ujuzi, na utashi zaidi ya wanadamu wote na viumbe vyote.Ambaye atawazidi wanafalsa wao kama Plato, Socrates, Aristotle.
Kwa muda mrefu hawakufanikiwa mpaka baadhi yao, wakaishia kumwabudu tu, huku wakikiri hawamjui.
Matendo 17:22-23
[22]Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. [23]Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
[22]Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.
[23]Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
Yaani wakiwa na maana tunasikia miungu mingi,.lakini katika hiyo yote bado hatujaona mwenye hekima ya kuitwa Mungu wa ulimwengu. Wote akili zao ni kama za kibinadamu tu.
Sasa tukirudi kipindi cha Yesu, tunaona tukio jipya linajitokeza,
sio tu wayahudi walimwamini, bali hadi hawa wayunani watafuta-hekima wengi wao waliposikiliza maneno ya Yesu, na kupima kwa jicho la hekima, wakaona hakika hajawahi tokea anayeweza kuelezea ukweli wote wa uumbaji kama Yesu.
Hilo liliwashawishi na kuwafanya kukiri kuwa huyu ndiye suluhisho la utata wetu kuhusu Mungu na elimu.
Hivyo wakaamini, ndio sababu ya wao kumfata Filipo kumwomba wamwone Yesu. Hiyo ilikiwa ni heshima kubwa sana kwa Yesu (kidini) mbele ya macho makuhani na mafarisayo wote, kwamba Mungu kathibitishwa kifalsafa. Kumbuka wayunani hawa waliokwenda hawakuwa watu tu wa kawaida. Bali ni watu wenye heshima ya juu sana na hadhi.
Hiyo ndio sababu Bwana Yesu kusema saa imefika mwana wa Adamu atukuzwe.
Yohana 12:20-26
[20]Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. [21]Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. [22]Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. [23]Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. [24]Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. [25]Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. [26]Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
[20]Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.
[21]Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu.
[22]Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.
[23]Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.
[24]Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
[25]Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.
[26]Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Hata leo, Yesu anathibitika katika mambo yote endapo tu tutamaanisha kumwona katika namna hizo. Ndio maana katika makundi yote ya watu ni lazima utakuta waamini.
Katika ya wanasayansi utawaona, katikati ya wanajeshi utawaona, katikati ya watawala utawaona,katikati ya mamajusi utawaona, katikati ya matajiri utawaona, katikati ya maskini utawaona, kati ya wanazuoni utawaona, kati ya madaktari utawaona,
Ukiuliza imekuwaje katika hali zao/ nafasi zao ambazo ni mbaya, na nyingine zenye majaribu, au zenye kumkana Mungu waziwazi, lakini wao wamemwamini Mungu?.
Ni kwasababu YESU anathibitika kila mahali.
Mtu kutokuamini ni yeye mwenyewe kataka. Hakuna atakayekuwa na udhuru siku ya mwisho, kwasababu Yesu amefunuliwa kila mahali.
Swali ni je! umemwamini Kristo? kama ni la! unasubiri nini. Mwamini leo kwa kuikubali kazi aliyoikamilisha juu yako ya kuondoa dhambi kwa kifo na kufufuka kwake. Ambayo hiyo huambatana na toba ya kweli na ubatizo.
Baada ya hapo utakuwa umepokea ondoleo la dhambi zako bure, mpokee Yesu sasa
Mungu akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani.
Utawanyiko wa Wayunani ulikuwaje?
ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.
SAUTI NYUMA YA ISHARA.
Maandiko yanaonyesha kuwa kitu pekee cha asili kinachoweza kutenganisha watu wawili walio katika Ndoa ni KIFO.
Warumi 7:2 “Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. 3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.”
Warumi 7:2 “Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.”
Lakini inapotokea Mtu anachukua nafasi ya KIFO, yaani anaivunja ndoa yake mwenyewe au ya Mtu mwingine iliyo ya Halali, basi mtu huyo kibiblia ni MFU, au jina lake lingine ni KIFO/MAUTI..Sasa utauliza KIFO kinaweza kuwa MTU jibu ni Ndio!.
Ufunuo 6:8 “Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda JINA LAKE NI MAUTI, na Kuzimu akafuatana naye…”
Kwahiyo Mtu anayechukua nafasi ya KIFO, katika ndoa yake mwenyewe au ya mwingine, huyo jina lake ni MAUTI kibiblia, awe mwanamke au mwanaume, huyo ni MAUTI, ni Mfu anayetembea.
Utauliza ni wapi tena katika maandiko, panaonyesha mtu aliyeharibu ndoa ya mwingine aliitwa MFU?
Mwanzo 20:2 “Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, UMEKUWA MFU WEWE kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu”.
Mwanzo 20:2 “Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, UMEKUWA MFU WEWE kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu”.
Umeona hapo?.. MUNGU anamwambia Abimeleki kuwa yeye ni MFU kwa kitendo tu cha kumchukua mke wa Ibrahimu.
Hebu jiulize hapo kwanini Mungu hajamwambia Mfalme Abimeliki kuwa umekuwa Najisi, au umekuwa Mjinga, au umekuwa Mpumbavu.. badala yake anamwambia amekuwa MFU!!!.. Maana yake pale alipo alikuwa ni Marehemu anayeishi.. Siku yoyote anashuka kaburini, na kila atakachojihusisha nacho kitakufa pia.
Hiyo pia ni hali ya Mtu anayeharibu ndoa yake mwenyewe au ya mwingine, kiroho jina lake ni MFU/MAUTI.
Na kumbuka maandiko yanasema Mauti anafuatana na Kuzimu.. Ufunuo 6:8 “Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda JINA LAKE NI MAUTI, na Kuzimu akafuatana naye…”
Maana yake huyu mtu anayeitwa MAUTI, anakwenda sambamba na kuzimu, na mwisho ni ZIWA LA MOTO.
Ufunuo 20:14 “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto”.
Je Mke au Mume uliye naye ni wako? Au wa mtu mwingine?… Unajua ni maumivu gani unayasababisha kwa mwingine unapomchukua Mke wake au Mume wake??..
Labda ulimchukua pasipo kujua maandiko au enzi bado hujaokoka, lakini sasa umejua …Mrudishe huyo mwanamke/mwanamume kwa aliyewake wake hata kama una watoto naye, (weka naye tu mipango ya namna ya kuwatunza watoto), lakini usiendelee kuishi naye kwani unafanya UZINZI, mrudishe kwa mume wake/mke wake, akikataa Mwache aishi mwenyewe, wewe utakuwa umejifungua katika kifungo cha Mauti….Vunja agano na Mauti kwa namna hiyo…
Isaya 28:18 “Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo”.
Bwana atusaidie.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
MATESO YA KUZIMU.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya uzima. Leo napenda tujifunze tabia nyingine ya Bwana Yesu. Kwasababu yeye mwenyewe alituambia ‘tujifunze kwake’. Hivyo naamini tuna mengi ya kuyajua kuhusu yeye.
Habari hiyo tunaisoma katika vifungu hivi;
Luka 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; 52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. 53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. 54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? 55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Luka 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;
52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.
53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kuwa kuna wakati ulifika, ilikuwa wazi kwa watu wote, kuwa Yesu anatafutwa ili auawe, (hususani kule Yerusalemu). Na hilo lilimfanya mara kadha wa kadha asitembee kwa uwazi wote mbele ya makutano (Yohana 7:10), kwasababu, saa yake ya kuuawa ilikuwa bado haijafika.
Yohana 11:54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye, hilo halikuendelea kwa wakati wote. Alipoona sasa kazi aliyopewa na Mungu ameimaliza, alionyesha tabia nyingine ambayo haikuwa ya kawaida. Biblia inatuambia, “aliukaza uso wake kuelekea Yerusalemu”, kule kule alipokuwa anatafutwa auawe.
Jambo ambalo lilileta mshtuko hata kwa mitume wake;
Yohana 11:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Yohana 11:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.
8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Walishangaa, ujasiri huo ni wa namna gani? Ni sawa na wanajeshi waliokwenda vitani, halafu maadui wakawaua wanajeshi wote, akabakia mmoja tu, halafu huyo mmoja anasema nitakwenda kupambana na jeshi lote hilo peke yangu sitajificha. Ukweli ni kwamba inahitaji nguvu nyingine ya ziada ndani ya huyo mtu.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, aliukaza uso wake, kwenda kututetea sisi. Embu Fikiria kama angeulegeza, na kuendelea kuzunguka mahali pengine na sio kule uyahudi(Yerusalemu), wokovu wetu tungeupatia wapi?
Ilibidi, alazamishe mambo, japo mwili wake ulikuwa hautaki, ndio maana akiwa pale bustanini, anaomwomba Baba, akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, ni kuonyesha kuwa hata mwili wake ulikuwa unagoma kuwepo kule Yerusalemu, na si mwili tu, bado mazingira pia hayakutaka, alipokuwa anakatiza kwa Wasamaria wenyeje wa pale hawakutaka kumruhusu akae kwao, kwasababu waliona kama anawaletea matatizo, ikumbukwe kuwa watu hao hao ndio waliokuwa wanataka kumfanya mfalme hapo mwanzo. Kuonyesha kuwa mazingira yalimgomea. Si mazingira peke yake, hata mitume wake nao, walifanya kama kumsindikiza tu, lakini mioyo yao walishajiandaa kuchukua hatua yoyote lolote litakapotokea, ndio maana pale bustanini, wale watu walipokuja kila mmoja akakimbia na njia yake.
Kwa ufupi kila kitu kilikataa, isipokuwa roho yake tu. Ndio sababu ya kwanini maandiko yanatuambia ‘aliukaza uso wake’ kwasababu haikuwa rahisi, si jambo tena la kuomba, au kubembeleza, au kushawishi, au kusubiri msimu mzuri. Bali ni kujitoa tu wote wote, katika hayo. Watu wengi tunadhani Yesu aliuchukua msalaba wake siku ile alipobebeshwa ule mti, hapana, aliuchukua msalaba wake Kwa kitendo hichi cha kuamua kuukaza uso wake, kuelekea kifoni. Hata aliposema tujitwike misalaba yetu, alilenga, eneo hilo.
Ni nini na sisi tunapaswa tukipokee kwa Bwana Yesu?
Kwa kuwa Roho wake naye yupo ndani yetu, hatuna budi kufahamu kuwa yapo majira katika safari yetu ya wokovu, hatutahitaji mazingira yawe mazuri, ndio tulitimize kusudi la Mungu, au ndugu kutukubalia, au marafiki kuafikiana na sisi, au miili kutuambia sasa ndio wakati, hapana..bali ni kujitwika misalaba yetu, “kwa kukaza nyuso zetu” na kumfuata Yesu.
Tukingoja vikwazo viondoke, au viondoshwe, tutajidanganya, na tutangoja sana, kwani vita vitaendelea kuwepo mpaka mwisho, mapambano hayaishi, tutashinda tu kwa kukaza tu nyuso zetu. Na Bwana atakuwa pamoja na sisi, ijapokuwa itaonekana ni kujipoteza lakini mwisho wake utakuwa ni uzima kama ulivyokuwa kwa Bwana Yesu.
RABI, UNAKAA WAPI?
MFALME ANAKUJA.
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
Msingi ni chimbuko, au mwanzo au kiini cha kitu fulani.
Ni wazi kuwa kila jambo lina msingi wake. taifa lina msingi wake, taasisi ina msingi wake, kabila lina msingi wake vilevile pia imani ina msingi wake.
Hivyo tukirudi katika ukristo. Msingi wa imani yake ni upi?
Msingi wa ukristo ni YESU KRISTO mwenyewe, na kazi yake aliyoikamilisha ya kufa na kufufuka kwake. Na sio kanisa, au dhehebu, au mapokeo fulani, au kikundi fulani cha wanaharakati.
Pasipo Yesu hakuna ukristo.
Yeye anafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni, ambalo hakuna mjenzi aliyeweza kusimamisha jengo bila kuliweka hilo.
1 Petro 2:6
[6]Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Habari kamili za Yesu, na kazi yake aliyokuja kuifanya duniani unaipata katika kitabu kimoja tu kiitwacho BIBLIA. Hivyo huwezi kutenganisha biblia na Yesu Kristo.
Ili mtu ashawishwe kuipokea imani, ni sharti, aisikie kwanza injili yake ambayo hiyo utaipata katika Neno la Mungu yaani biblia..(Warumi 10:17)
Mpaka mtu aitwe mkristo ni lazima amtambue kwanza Kristo ni nani, na nini amekileta duniani, vinginevyo hawezi kuwa mkristo, hata kama atajiunga na kanisa, au dhehebu na kuyashika mapokeo yote aliyoyakuta huko, au kuisoma biblia yote, huyo bado hajawa mkristo.
Ni muhimu sana kumtambua Yesu ni nani kwetu. Kumtambua Yesu kama mwana wa Mungu bado inaweza isikupe wokovu, hata kumtambua Yesu kama Mungu bado inaweza isikupe wokovu (ijapokuwa vyote hivyo ni vyeo vyake). Lakini vyeo hivyo sio kiini cha ukristo.
Yesu ni nani na ni nini alikileta duniani?
Yesu ni MKOMBOZI, kama tafsiri ya jina lake linavyojieleza( Mathayo 1:21)
mkombozi wa nini?
Alikuja kutukomboa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu, Na kama ilivyo kanuni ya kiroho ili jambo hilo liweze kukamilika ilipasa itolewe kafara isiyo na kasoro yoyote(yaani dhambi). Na aliyeweza kukidhi vigezo hivyo ni Yesu pekee.
Ndio maana ilimgharimu afe, kama fidia ili sisi tupokee ondoleo la dhambi na msamaha wa dhambi kwa kifo chake. Hivyo yoyote anayeamini(yaani anayeupokea wokovu huo aliouleta).
kwa toba ya kweli na ubatizo, Basi anakuwa ameokoka, hivyo ile ghadhabu ya Mungu kwa wenye dhambi wote haiwi tena juu yake, tangu huo wakati anaitwa mbarikiwa, au mkristo, kwasababu dhambi zake zinakuwa zimefutwa kabisa.
Na zaidi ya hayo mtu huyu moja kwa moja anapewa zawadi ya Roho Mtakatifu, ambaye tangu huo wakati na kuendelea anakuwa ndani yake kama msaidizi, kumsaidia madhaifu yake, katika kuomba, kuijua kweli, kumkumbusha aliyoyasema Yesu, kumpasha habari ya mambo yajayo, na kumtia nguvu ya kumtumikia Mungu, pamoja na kumpa nguvu ya kushinda dhambi.
Huyu ndiye mkristo.
Swali ni je! umemwamini ipasavyo? au umempokea kwa namna ile ya kidini?
Usifikiri kuhama dini, wewe ni Kristo, au kuzaliwa kwenye familia ya kikristo wewe ndio mkristo, au kusomea theolojia, hapana hizo ni kampeni tu, ukristo halisi huja kwa kumwelewa Kristo ni nani na ni nini amekifanya kwako.
Ikiwa bado hujaokoka na unataka kumpokea leo ili upate ondoleo la dhambi zako. Basi uamuzi huo ni bora sana kwako. Wasiliana nasi namba uzionazo chini kwa mwongozo wa sala ya toba.
Ubarikiwe.
+255693036618/ +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
YESU NI NANI?
UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?
Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?
Biblia kitabu kikamilifu, na kitakatifu kimeandikwa na waandishi Zaidi ya 40 kwa Uvuvio wa Roho Mtakatifu. Ndani ya biblia kuna taarifa zinazohusu maisha ya watu zilizobeba sauti ya Mungu nyuma yake, pia kuna taarifa za Mataifa mbalimbali pia zenye kubeba sauti ya Mungu nyuma yake, lakini Zaidi sana kuna Nabii za wakati ujao.
Ifuatayo ni orodha ya waandishi 40 wa Biblia kuanzia Agano la kale hadi Agano jipya.
Agano la kale.
Agano Jipya.
Kwanini waandishi wapo Zaidi ya 40 na si 40 kamili?.. Ni kwasababu biblia pia imewataja wana wa Kora, ambao hatujui walikuwa ni wangapi, zaidi sana yupo mwandishi wa kitabu cha Waebrania, ambaye hajatajwa ni nani, huenda akawa ni Mtume Paulo, lakini kama si yeye bali ni mwingine, basi ataongezeka katika idadi ya walioiandika biblia.
Kumbuka tena, biblia ni kitabu cha Mungu kilichoandikwa na WATU, kwa uvuvio wa ROHO MTAKATIFU, Hivyo maneno yaliyoandikwa ndani ya Biblia, yana uzima.
2Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”.
2Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”.
KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.
Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume.
Je ni Mungu au Malaika?
Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.