Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia.
Leo nataka tujifunze umuhimu wa kuchunguza mambo, kwani tusipokuwa watu wa kuchunguza mambo basi tunaweza tusiuelewe uweza wa Mungu.
Asilimia kubwa ya watu wanaobarikiwa hawajui kuwa mafanikio yao ni kutokana na maombi ya watu wengine (ambao wanawaombea wao pasipo kujua), hivyo ni muhimu sana kufikiri wakati wa kufanikiwa.
Hebu tujifunze katika ile habari ya Kana ya Galilaya pale Bwana Yesu alipofanya muujiza wake wa kwanza wa kugeuza maji kuwa divai.
Maandiko yanasema baada ya Bwana Yesu kubadili yale maji kuwa divai, yule Mkuu wa meza, aliyeteuliwa kuandaa vinywaji vya wageni wa kawaida na mgeni rasmi, hakujua kama ile divai mpya imetoka kwa Bwana, badala yake alidhani mwenye sherehe ndiye aliyeinunua, na ndipo akaenda kumfuata mwenye sherehe (Bwana harusi) na kumpongeza akidhani kuwa yeye ndiye kainunua ile divai mpya na kuwapa watu wote wanywe.
Na yule Bwana harusi naye akashangaa kupewa sifa ambazo si zake, huenda na yeye akadhani kuna mtu tu katikati ya sherehe kajitokeza na kujitolea kununua divai mpya ili kuimeza aibu.. kwamaana divai kuisha katikati ya sherehe na bado kuna watu wa muhimu hawajapata, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa wenye sherehe. Hivyo mpaka mwisho wa sherehe ni wachache sana ndio waliojua siri ya ile divai, kuwa na Bwana Yesu ndiye aliyeitoa.
Tusome,
Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.
5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.
6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa”.
Sasa nataka tuone nyuma ya Baraka hizo alikuwa nani?, Nyuma ya muujiza huo alikuwa nani, na nyuma ya aliyetoa aibu alikuwa ni nani?.. kisha na sisi tutapata akili wakati wa kufanikiwa.
MWOMBAJI/ WAOMBAJI.
Kulipoonekana tatizo, Marimu alienda kumwomba Bwana na kumsihi sana. Huyu ndiye aliyekuwa mwanzo wa muujiza wa divai. Kama sio Mariamu watu wangeabika kwenye sherehe hata kama sherehe hiyo Kristo alikuwepo ndani.
Vile vile hata leo, ukiona jambo Fulani la heri limetokea mbele yako lililoziba aibu yako, hebu tafakari sana, usijivune wala usikimbilie kusema wewe ni mwenye bahati, huna bahati yoyote, hayo ni matokeo ya wengine kuomba kwaajili yako..haijalishi Kristo yupo na wewe.. Hata katika ile harusi Kristo alikuwepo ndani, alikuwa ni mwalikwa, lakini bado kama pasingekuwepo mwombaji, hakuna kitu kingefanyika.
Ukiona umebarikiwa kwa jambo Fulani au mambo yako fulani fulani yameenda sawa usikimbilie kujisifu, wala kujivuna, kwamba una bahati!!…fahamu kuwa hayo ni matokeo ya wengine kuomba kwaajili yako, na hao huenda unawajua au huwajui.
Mtoto ukifanikiwa jua wakati mwingine ni matokeo ya maombi ya wazazi wako na si kwasababu wewe una akili sana au una ujanja mwingi, kijana ukifanikiwa jua ni matokeo ya maombi ya ndugu zako, au wapendwa wenzako wanaokesha kwaajili yako pasipo wewe kujua.
Unapoona unapiga hatua kimaisha au kiroho, fahamu kuwa ni matokeo ya wanaokuongoza kiroho kukuombea, wala usidhani ni kwa nguvu zako au una bahati..
Waebrania 13:17 “Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi”
Ukilifahamu hili siku zote utakuwa mnyenyekevu na kumshukuru Mungu kwa kila jambo na pia kufikiri sana kuwaheshimu wanaokuombea na hata wewe kutenga muda kuwaombea!.. Laiti yule mkuu wa Meza na yule Bwana arusi wangejua kitu Mariamu alichowafanyia, kwenda kuwaombea kwa Bwana wangeshangaa sana, na kunyenyekea sana.
Laiti ungejua mambo watu wanayomwambia Bwana kuhusu wewe, usingebaki kama ulivyo..
Amani ya familia yako, Amani ya jamii yako, Amani ya nchi yako, ni matokeo ya maombi ya watu wengine wa Mungu wanaolia mbele zake usiku na mchana.. wala si kwasababu nyingine?, kama si hao ni kitambo sana mambo ya ulimwengu yangeshaharibika..(2Thesalonike 2:7).
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?.
Nakusalimu katika jina kuu sana na lenye nguvu la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima ya Mungu wetu.
Sisi kama Wanadamu Kila mmoja wetu haijalishi ameokoka au hajaokoka, ndani yake ameumbiwa kiwango cha “kusahau”. Hii ni karama ya Mungu na ni vizuri kumshukuru Mungu Kwa jambo hili, kwasababu kama tungeikosa wanadamu wote tusingeishi hivi tulivyo Leo.
Lakini kusahau kukisimama Mahali pasipo-papasa, inageuka kuwa hatari kubwa sana, Tena dhambi yenye matokeo mabaya sana rohoni.
Kuna aina ngapi za kusahau?
Sasa kusahau kunaweza kuwa aidha kupoteza kumbukumbu ya lile jambo au tukio, Moja Kwa Moja akilini mwako, uwe kana kwamba hujawahi kulipitia.
Au kunaweza kuwa kulipoteza tu Kwa muda katika kumbukumbu lakini utakapokumbushwa unalikumbuka Tena.
Kusahau kwenye madhara ni kupi?.
Kabla ya kutazama ‘kusahau’ kwenye hasara tuone kusahau kwenye faida kukoje.
Kusahau kwenye faida kunatimia katika mambo yasiyo na maana, au yenye maudhui hasi kwako. Kwa mfano pale mtu unapotukanwa, au unapopigwa kikumbo barabarani na mtu usiyemjua, unaposikia miziki isiyokufaidia huko nje, unapofiwa, unapodhulumiwa, unaposemwa, unapovunjiwa heshima, unapoaibishwa, unaposingiziwa n.k… Mazingira kama haya ambayo ni hasi…kusahau Kunahitajika sana na ni lazima ujifunze kuruhusu jambo hili liumbike ndani Yako ili uponyeke kwa haraka,.maana ndio sehemu yake hiyo inapopaswa itumike.
Lakini kusahau kusikokujenga ni pale unaposahau Matendo mema, au mambo chanya yakupasayo kutenda. Kwamfano Sheria inasema ” usitupe taka hapa” Halafu inapita wiki Moja umesahau agizo hilo, unarudia tena kutupa taka pale pale ulipokatazwa..Hapo utakuwa hujitafutii jambo lingine zaidi matatizo?
Vivyo hivyo katika Neno la Mungu pale unaposahau sahau Neno la Mungu hapo ndio pabaya sana. Wakristo wengi hatujui kuwa Mungu “anayorudia kutuambia ni mengi kuliko Yale mapya anayotaka kusema nasi”..Ni Kwanini? ni kwasababu tumekuwa wepesi wa kusahau Sheria zake.
Mambo yamekuwa kinyume chake, badala tusahau yaliyo mabaya tukumbuke yaliyo mema, tunasahau mema tunakumbuka mabaya sikuzote.
Ni shambuliko kubwa sana ambalo ibilisi amelipanda mioyoni mwa wanadamu. Ndio sababu uchungu haukomi, masengenyo hayaishi, vita vinazuka Kila siku, fitna, unafki, na uongo havina mwisho ni kwasababu Hali Ile Ile tuliyokuwa nayo nyuma mpaka sasa tunairuhusu ikae kwenye akili zetu.
Wakati nguvu hiyo tungepaswa tuitumie kulihifadhi Neno la Mungu mioyoni mwetu ili Matendo chanya yaendelea kutokea ndani yetu, hatufanyi hivyo.. maandiko yanasema..
Yakobo 1:22-25
[22]Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
[23]Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
[24]Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
[25]Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Tuweke mfano, tunaweza kusoma kwenye biblia kwamba Upendo hauhesabu mabaya, Wala haujivuni, Wala hauoni uchungu n.k(1Kor 13).. Sasa wakati uliposoma hili neno, moyoni mwako unasema nitaliishi hili Neno, lakini inapita siku mbili unashangaa umerudia kule kule, unaanza ishi maisha ya namna Ile ya kwanza,. Tatizo lipo hapo kwenye kusahau. Laiti.hilo Neno lingekuwa limeganda viizuri kwenye moyo wako, ingekuwa breki pale tu mambo mabaya yanapojaribu kuvuka mipaka.
Sasa tunawezaje kuishinda Hali hii ya kusahau sahau?
Ni kama vile mwanafunzi darasani, mara nyingi anakuwa ni mtu wa.kurudia rudia kusoma na kufanyia sana mazoezi kile alichofundishwa..lengo la kufanya vile ni kulazimisha akili yake inakili Yale mafundisho kwa muda mrefu ili atakapoingia kwenye mtihani asisahau chochote…Lakini kama akisema Mimi ni ‘genius’ sina muda wa kurudia nilivyofundishwa..ni wazi kuwa mambo mengi yatamruka, na atafeli.
Hivyo na sisi sote ni wanafunzi wa Biblia. Soma biblia Kila siku ifanye kuwa rafiki Yako, usiwe mtu wa kusoma Leo, Tena wiki ijayo au mwezi ujao, ndio unakuja kusoma tena..SoMo tafakari mambo uliyoagizwa mule na Mungu Kila siku..Ndivyo itakavyokuwa rahisi kuliishi Neno la Mungu, kinyume na hapo usijidanganye Utasahau…kwasababu mwisho wa siku yatatoka moyoni mwako, na hivyo dhambi yoyote itakayokatisha mbele Yako, utashindwa kukabiliana nayo mapema. Mungu hapendi tuwe na tabia hii ya kusahau sahau Neno lake.
Kumbukumbu la Torati 6:6-9
[6]Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; [7]nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. [8]Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. [9]Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
Piga vita kusahau Neno la Mungu.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu? Na je ni dhambi kuwa na Wivu?
Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
JE NI KUTII AU KUPATA KWANZA MAARIFA?
Haya ni Mafundisho maalumu Kwa ajili ya watumishi, ikiwa wewe ni kiongozi, askofu, mwalimu, mchungaji, mtume, mwinjilisti, unayesimama mahali fulani katika kulitazama kundi la Bwana, au jamii ya watu waliookoka, basi mafundisho haya ni maalumu kwako.
Biblia inasema;
Mithali 27:23
[23]Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.
Mchungaji Bora sikuzote anatambua ni wajibu wake kuwa karibu na mifugo yake wakati mwingi. Ili Kuhakikisha Mahali wanapolala ni salama, wanaogeshwa Kila wakati, wanapata chakula Bora, afya zao pia ni njema na wanachungwa Mahali salama.
Kwamfano kama mchungaji akiwa Hana desturi ya kwenda zizini. Tunajua mifugo Kwa kawaida Huwa Haijui kujisafisha yenyewe, matokeo yake ni kwamba lile zizi litajaa vinyesi na mwisho wa siku watapata magonjwa na kufa, na hasara inaangukia kwa mchungaji?
Vilevile akiiachia mifugo yake ianze kujichunga yenyewe, inaenda popote iwezavyo kujitafutia chakula, bila shaka itapotea, kama sio kuibiwa, au kuliwa na wanyama wakali, au kula vitu visivyostahili.
Hivyo utaona ni sharti Mahali palipo na mifugo, hapapaswi kukosekana mchungaji hata kidogo. Hii inatufundisha sisi tulio watumishi, kuhakikisha tunafahamu Hali mbalimbali za watu wale tunaowaongoza.
Tunawajibu wa kuwapa chakula kizuri kitakachowakuza (yaani Neno la Mungu lisiloghoshiwa), tuna wajibu wa kuwalinda kiroho, dhidi ya mafundisho potofu na mitego ya ibilisi, Kwa kuwaonya na kuwakemea pale inapobidi wavukapo mipaka.
Tuna wajibu wa kuwaombea, tunawajibu wa kuwafariji na kuzijali Hali zao za mwilini katika maisha Yao ya kawaida.
Hivyo wewe kama kiongozi ikitokea upo mbali na kundi lako, usikawie sana, ukaliacha kundi lako ma-miezi na ma-miaka,bila kujua maendeleo yao, ukadhani kwamba litaweza kujichunga lenyewe, hiyo ni hatari..ni heri uwe mtu wa kwenda na kurudi, kwenda na kurudi… lakini pia ukiwa karibu nalo usiwe mlegevu kupeleka jicho lako Kila eneo la maisha Yao ya kiroho na ya kimwili, kuangalia ni wapi Pana mapungufu au shida..ili kuondoa kasoro hizo, Ili kundi la Bwana listawi kama vile yeye atakavyo.
Ndio maana ya hili andiko Mithali 27:23 “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako”.
Ni wajibu wako kufanya hivyo, kwa hiari yako mwenyewe na sio kama unalazimishwa;
1 Petro 5:2
[2]lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
Kwanini Nuhu alimlaani Kaanani badala ya mtoto wake Hamu,
EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.
Je mgongo kuuma kunasababishwa na nini?
Kama maumivu ya mgongo si kutokana na umri, au ugonjwa uliopo ndani ya mwili wako sasa, au si kutokana na ajali uliyoipata au hali uliyopo sasa kama Ujauzito n.k?. Na umejaribu kutafuta kila suluhisho kwa madaktari bila mafanikio yoyote..basi fahamu kuwa huenda kuna ujumbe kutoka kwa Bwana unaopaswa kuujua nyuma ya huo ugonjwa, na ukisha ujua na kuchukua hatua basi ugonjwa wako huo utaondoka mara moja.
Tusome maandiko yafuatayo..
Mithali 10:13 “Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu”
Mithali 19:29 “Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu”
Mithali 26:3 “Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu”.
Yatazame maisha yako je! Yamejaa mizaha?, yamejaa udunia? Je maneno yako yamejaa upumbavu?.. Kama hekima imepungua ndani yako, na mizaha imezidi katika maisha yako, basi huenda maumivu ya mgongo wako ni ujumbe kutoka kwa Mungu kwamba utubu na kugeuka. Na ukishatubu kwa kumaanisha kabisa kubadili njia zako, basi BWANA atakuponya mara moja!
Lakini kama njia zako na midomo yako ni ya hekima, basi fahamu kuwa ni mashambulizi umepokea kutoka kwa adui, lakini habari njema ni kwamba Yupo Mkuu wa uzima aliyeteswa kwaajili yetu, YESU KRISTO, mwombe huyo kwa Imani naye atakuponya kikabisa kabisa. Au wasiliana nasi kwa namba tajwa hapo chini, tuweze kukuombea kwa jina la Bwana Yesu Kristo naye atakuponya.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Tatizo la Bawasiri kibiblia
Tatizo la kuvimba miguu kibiblia
TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA
JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Jibu: Turejee.
Walawi 11:29 “Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake,
30 na GURUGURU na kenge, na mjusi na GOROMOE, na lumbwi.
31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni”
Guruguru ni jamii ya mijusi wanaishi katika miti, tazama picha juu, na Goromoe ni mijusi wanaishi katika miamba au mchanga, tazama picha chini.
Kumjua Lumbwi ni mnyama gani fungua hapa >> Lumbwi ni nini katika biblia?
Viumbe hawa, Bwana Mungu aliagizwa wasiliwe katika Agano la kale, si kwasababu vilikuwa na sumu au madhara katika mwili, bali vilikuwa vimebeba tabia zinazowakilisha tabia za jamii/ aina Fulani ambayo haikuwa inampendeza Bwana Mungu.
Na tulipoingia katika Agano jipya hakuna sheria tena ya kula au kutokula wanyama hao, maadamu hawana sumu kwenye mwili.
Kwahiyo Guruguru na Goromoe ni halali kuliwa kibiblia , ingawa si chakula kifaacho sana kwa jamii zote, ikiwa na maana kuwa kama ukiona havikufai vitu hivyo pia si dhambi kutovila, ingawa ni halali kuliwa.
1Wakorintho 10:23 “Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo”
Maran atha
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini samaki wasio na mapezi na magamba hawakuruhusiwa kuliwa?
Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?
Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)
Mafundisho maalumu Kwa ajili ya watumishi wa Mungu.
Huu ni mwendelezo wa mafundisho maalumu Kwa ajili watumishi wa Mungu, ikiwa wewe ni Mchungaji, mwalimu, mtume, askofu,Nabii, au mtu yoyote unayemtumikia Mungu katika nafasi yoyote kanisani au kwenye huduma basi mafundisho haya yatakufaa sana.
Wakati ule Yakobo alipodhamiria kwenda kukutana na ndugu yake Esau baada ya kutengana naye Kwa muda mrefu..maandiko yanasema walifurahi sana walipoonana kule nyikani. Na baada ya mazungumzo Yale kuisha, sasa ikiwa ni wakati wao wa kuondoka pale nyikani walipokutana waelekee Kaanani.
Na kama tunavyosoma habari tunaona ndugu yake Esau alimshurutisha wasafiri pamoja naye. Ndipo Yakobo akamwambia Esau kuwa jambo hilo ni gumu kwake..kwasababu ya Hali ya makundi mbalimbali na watu na mifugo aliyokuwa nayo..Tusome..
Mwanzo 33:12-17
[12]Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia.
[13]Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng’ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.
[14]Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.
[15]Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu.
[16]Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri.
[17]Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.
Ni nini cha kujifunza hapo?
Yakobo alilitambua kundi analolichunga, alijua kuwa wapo watoto wachanga ndani yake, na mifugo pia michanga, Ambayo haijazoezwa kupelekwa mkiki mkiki, kwani ikilazimishwa kufanywa hivyo itakufa yote njiani. Hivyo akaomba muda wa kusafiri wake uongezwe, kusudi kwamba ayakokote taratibu taratibu mpaka yatakapofika kule Shekemu alipokuwa anapakusudia. Pengine mwendo wa siku moja tu ikamgharimu mwezi.
Tofauti na Esau yeye alikuwa na watu wa vita tu,watu walio hodari, Lakini Yakobo alikuwa na makundi yote. Na hivyo kwenda nayo taratibu taratibu ilimgharimu .
Hii ni kutufundisha asili ya msimamizi wa kweli, kwanza hulijali kundi lake, pia anakuwa tayari kuchukuliana na vile vyombo dhaifu. Kwasababu sio wote katika kanisa watakuwa na mwendo kama wa kwao, SI wote watakuwa wepesi kustahimili vishindo kama baadhi yao. Hivyo wewe kama kiongozi ni lazima ujifunze kuendana na makundi yote kama Musa kule jangwani, ili kisipotee chochote. Maana yake ni kuwa usiwe na haraka ya kufikisha kundi Mahali Fulani Kwa jinsi utakavyo, vinginevyo utawaua wengine.
Yakobo alipaita mahali pale Sukothi, kwasababu ndipo alipowajengea makundi yake vibanda. Na wewe pia jenga Sukothi yako.
Bwana akubariki.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
TOFAUTI YA MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU NI IPI?
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
MIGAWANYO MINNE (4), YA HUDUMA YA YESU.
Biblia inasema nini kuhusiana na kuvimba miguu na miguu kuuma?
Kama miguu imevimba na hujui chanzo, wala madaktari hawaoni tatizo…basi huenda ni Mungu anataka kusema na wewe jambo, ambalo ukilirekebisha basi tatizo hilo linaweza kukuisha moja kwa moja..
Hebu tusome maandiko yafuatayo katika biblia..
Nehemia 9:19 “hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; NGUZO YA WINGU haikuwaondokea wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala NGUZO YA MOTO haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonyesha njia watakayoiendea.
20 Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.
21 Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala MIGUU YAO HAIKUVIMBA”
Wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Nguzo ya Wingu, Na nguzo ya Moto ambayo ni ufunuo wa ROHO MTAKATIFU juu yao, ambaye aliwaongoza kama ROHO MWEMA, katika njia yao..
Ikiwa na maana kuwa njia waliyokuwa wanaiendea ilikuwa ni njia sahihi waliyoongozwa na Roho wa Mungu ndio maana miguu yao HAIKUVIMBA!, lakini wangeenda njia nyingine tofauti na hiyo ya Roho Mwema, basi ni wazi kuwa miguu yao Ingevimba, hata kama wangekuwa hawatembei, wamekaa tu, bado ingevimba.
Kwahiyo na wewe kama unaona miguu yako imevimba, na hujui chanzo na wala huoni dalili ya kupona, huenda upendo wa Mungu unakukumbusha kuwa umtafute Roho Mtakatifu, kwani yeye ndiye atakayeyaongoza maisha yako ya kiroho, maumivu hayo ni ishara ya upendo wa Mungu kwako kutaka kukupa zawadi ya Roho wake Mtakatifu, akuongoze katika njia sahihi.
Sasa utampataje Roho Mtakatifu?
Utampata kwa kanuni ifuatayo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.
Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TATIZO LA VISIGINO KUUMA KIBIBLIA
TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
Vihekalu vya fedha vya Artemi vilikuwaje? (Matendo 19:24).
Jibu: Turejee
Matendo 19:24 “Kwa maana mtu mmoja, jina lake Demetrio, mfua fedha, aliyekuwa akifanya vihekalu vya fedha vya Artemi, alikuwa akiwapatia mafundi faida nyingi”.
Mahekalu yalikuwa ni majengo maalumu kwaajili ya ibada za miungu.. Lilikuwepo hekalu moja tu duniani la Mungu wa kweli, ambalo lilitengenezwa Yerusalemu, hilo pekee ndilo Mungu wa kweli wa mbingu na nchi alikuwa akiabudiwa ndani yake kipindi cha agano la kale. Lakini mahekalu mengine yote yaliyojenga tofauti na hilo yalikuwa yanamuabudu shetani kupitia sanamu.
Sasa kipindi Mtume Paulo na wanafunzi wengine wamefika mji wa Efeso, walikuta jamii ya watu wa pale wanamwabudu mungu mke waliyemwita Artemi.
Na katika huo mji wa Efeso walikuwa wamemtengenezea Hekalu kubwa, na ndani ya hilo hekalu kulikuwa na sanamu ya huyo mungu mke, Artemi ambayo wanaamini haikutengenezwa na mtu bali ilishushwa/ilianguka kutoka mbinguni (jambo ambalo halikuwa la kweli). Na watu kutoka pande zote za dunia walikuwa wanakuja hapo Efeso lilipo hekalu la huyo Artemi kumwabudu..
Matendo 19:35 “Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa HEKALU LA ARTEMI, aliye mkuu, NA WA KITU KILE KILICHOANGUKA KUTOKA MBINGUNI?”.
Sasa kwasababu walikuwa wanamwamini huyo mungu waliyemwita Artemi kuwa ni mkuu na aliye na wafuasi wengi, wale wageni walikuja kutoka mataifa ya mbali walipata changamoto ya kumwabudu wakiwa makwao (huko katika mataifa yao ya mbali),
Hivyo ili kutatua hiyo changamoto..baadhi ya mafundi waliokuwepo pale Efeso wakaanza biashara ya kutengeneza vijihekalu vidogo vidogo vinavyobebeka vinavyofanana kabisa na lile hakalu lenye sanamu ya huyo Artemi, ili watu wanaotoka mbali wakiisha kumwabudu wakiwa Efeso waweze kuondoka na vijihekalu hivyo na kwenda navyo huko walikotokea na kuendeleza ibada zao, ambapo wengine waliviweka kwenye vyumba vyao, wengine katika vimilima na sehemu mbali mbali.
Vihekalu hivyo vilitengenezwa kwa madini ya “fedha”, ambapo mafundi wakiongozwa na fundi mkuu aliyeitwa Demetrio waliyeyusha madini hayo ya fedha na kuyatengeneza kwa muundo wa hilo hekalu.
Lakini Paulo pamoja na wanafunzi wengine wa Bwana walijua uongo huo wa shetani, na hivyo walipoingia huo mji wa Efeso waliupindua kwa injili ya kweli, na wengi wakamwamini Mungu wa kweli na kumpokea Yesu na kuacha ibada hizo za miungu, ambayo nyuma yake ni shetani anaabudiwa.
Ukisoma mistari ya juu utaona matokeo ya injili ile iliwafanya maelfu ya watu waache uchawi waliokuwa wanaufanya, na kumgeukia Mungu.
Matendo 19:18 “Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.
20 Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu”.
Na hata sasa uweza wa Mungu upo, Injili ya Kristo ina nguvu nguvu kuliko uchawi!. Sawasawa na Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.
1Wakorintho10:4-5 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”
Usiionee haya (aibu) injili.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?
Karibu tujifunze biblia,
Mathayo 6:22 “Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.
23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo”
Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani “Jicho” limefananishwa na “Taa ya mwili”?
Siku zote taa ikiwa inaangaza basi nyumba yote inakuwa na Nuru na ndipo vitu vyote vilivyomo ndani vinaweza kuonekana, lakini ikizima nyumba yote inakuwa giza na hakuna kitakachoonekana.
Hali kadhalika na jicho likiwa halioni, au likiwa limefumbwa basi kinachoonekana ni giza, huwezi kuona chochote, huwezi kuona mikono yako, wala miguu yako, wala kiungo kingine chochote, huwezi kuona mbele wala nyuma wala kitu kingine chochote. Kwa ufupi unakuwa ni kipofu!. Hayo ni matokeo ya jicho kuharibika!.
Sasa Bwana Yesu analinganisha Nuru iliyopo ndani yetu na jicho.. Kwamba Nuru iliyopo ndani yetu, kazi yake ni kutuongoza njia, kama vile Jicho linaloona linavyoongoza njia na kuusaidia mwili wote kusonga mbele, vile vile Nuru iliyopo ndani yetu kazi yake ni kuongoza maisha yetu katika njia sahihi.
Sasa Nuru iliyopo ndani yetu au inayopaswa uwe ndani yetu ni nini?.
Mathayo 5:16 “Vivyo hivyo NURU YENU NA IANGAZE mbele ya watu, wapate kuyaona MATENDO YENU MEMA, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Umeona hapo?.. kumbe Nuru ni “Matendo yetu mema” .. kwamba matendo yetu yanapokuwa mema, basi ni sawa na macho yanayoona!.. Kumbe matendo yetu yakiwa mabaya sisi ni sawa na vipofu!, wala hatujui tunapokwenda!…kama Bwana Yesu alivyosema katika…
Mathayo 15:14 “Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili”.
Je unataka kuona mambo yaliyopo mbele yako? na njia unayoielekea? kama ni salama?.. je! Unataka kuona hatari inayokuja na kuepukana nayo?.. Basi fanya matendo mema!!…usiende kwa waganga wala wasoma nyota wala manabii, wewe yasafishe matendo yako tu!, na utaona mambo yajayo!..
Hiyo ndio siri nyingine iliyopo nyuma ya “Matendo yetu mazuri”.. sio tu yanaupendeza moyo wa Mungu na kutupa baraka.. bali pia yanatuongoza na kutufanya tuone mambo yajayo (yaliyopo mbele yetu).
Na unayasafishaje matendo yako?.. Si kwa nguvu zako bali kwa Neema iliyopo ndani ya damu ya Yesu, ambayo hiyo inakuja kwa njia ya kutubu dhambi na kumaanisha kuziacha pamoja na kupata ubatizo sahihi..
Hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukupa uwezo wa wewe kufanya matendo yampendezayo Mungu, na hivyo macho yako ya kiroho yatakuwa angavu… Utakuwa na uwezo wa kuona hatari zilizopo mbele yako na kuepukana nazo, utakuwa na uwezo mkubwa wa kuona hasara zilizopo mbele yako na kuzikwepa, utakuwa unauwezo wa kuona mema yaliyopo mbele yako na kuyafuata na vile vile utakuwa na uwezo wa kuona hatari inayokufuata nyuma yako n.k
Lakini kanuni ni hiyo moja tu!..Ifanye Nuru yako (matendo yako) yaangaze!
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TWAENENDA KWA IMANI NA SI KWA KUONA.
Kama ulimwengu ujao utakuwa na watakatifu tu, sasa hao watakaotawaliwa watatoka wapi?
RUHUSU TOHARA IPITE JUU YA KARAMA YAKO.
ITII SAUTI ILIYOPO NYUMA YA KILA ISHARA YA MUNGU!
Wivu ni nini kibiblia na kuna aina ngapi za Wivu unaowapata watu? Na je ni dhambi kuwa na Wivu?
Katika kitabu cha Wagalatia biblia imetaja “Wivu” kuwa ni mojawapo ya tunda la mwili. Sasa swali ninapopata wivu wa kimaendeleo nafanya dhambi? Au ninapopata wivu wa mwanandoa mwenzangu kukosa uaminifu je nayo ni dhambi?
Jibu: Tusome,
Wagalatia 5:19-21
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi..20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira……….. ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”
Ni kweli Wivu ni mojawapo wa matendo ya mwili ambayo ni dhambi mtu kuwa nayo, lakini kama ya kuingia ndani zaidi katika andiko hili..ni vizuri kuzijua kwanza aina za wivu..
Upo “Wivu wa kiMungu” na vile vile upo “wivu wa kidunia”, ni kama tu “hasira” au “hofu”. Ipo hasira ya kiMungu na vile vile ipo hasira ya kidunia au ya kiulimwengu.
Hasira ya kidunia ni ile inayoyoishia au inayompelekea mtu kutenda dhambi, kama kutukana, kuua, kuonea, kuiba n.k.. kwaufupi matunda yake ni mabaya daima… Lakini hasira ya kiMungu ni ile inaiyoishia katika kumjenga mtu na kumtengeneza zaidi, na kumrudisha kwa Mungu au katika njia sahihi kwa upendo.
Mfano wa hasira ya kiMungu ni ile Bwana Yesu aliyokuwa nayo juu ya Mafarisayo na Masadukayo.
Utaona Mafarisayo na Masadukayo walikuwa wanamwudhi sana Bwana lakini hasira ya Bwana haikuishia katika kuwatukana, au kuwashushia moto na kuwaangamiza ingawa alikuwa na uwezo huo, au kuwaharibu kwa njia yoyote ile… bali katika kuwahurumia..
Marko 3:1-5 “Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;
2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.
3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.
4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
5 AKAWAKAZIA MACHO PANDE ZOTE KWA HASIRA, AKIONA HUZUNI kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena”.
Hasira ya namna hii biblia imesema tuwe nayo ila tusitende dhambi, jua lisizame tukiwa nayo bado mioyoni..(Waefeso 4:26).
Sasa tukirudi katika Mantiki ya hofu na wivu ni hivyo hivyo, ipo hofu ya kiMungu na ya ipo hofu ya kidunia, vile vile upo wivu wa kiMungu na upo wivu wa kidunia.
Wivu wa kidunia ni ule unaoishia kutenda dhambi.. Mfano mtu atamwonea mwingine wivu kwasababu kapata kitu fulani ambacho yeye hajakipata, hivyo atatamani au atatafuta njia yule mtu akipoteze kile kitu ndipo atulie.
Mfano wa wivu huu ni ule aliokuwa nao Kaini, alipoona sadaka ya ndugu yake imekubaliwa na kwake imekataliwa. Badala atafute njia ya kuboresha sadaka yake ikubalike mbele za Mungu kama ya ndugu yake, yeye akatafuta kumwua ndugu yake, (wivu unaoish kuleta chuki, masengenyo, vinyongo, visasi ni wa kishetani)..ambao ni dhambi mtu kuwa nao sawasawa na hiyo Wagalatia 5:20.
Wivu wa kiMungu ni ule unaomfanya mtu atamani kuwa mwema kama mwingine alivyo mwema, unaomfanya mtu atamani kufanya vizuri kama mwingine anavyofanya vizuri pasipo kumtakia madhara yule mwingine, (kwa ufupi haufurahii kuanguka wala kupunguka kwa mwingine)..zaidi sana mafanikio ya mwingine yanakuwa siku zote ni darasa kwake….
Wivu huu sio mbaya na si dhambi mtu kuwa nao, kwasababu matunda yake ni mazuri..
Mfano wa huu ni ule Mtume Paulo, aliojaribu kuutia kwa ndugu zake Waisraeli ili wamgeukie Mungu zaidi.
Warumi 11:14 “nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao”.
Lakini pia upo Wivu mwingine wa KiMungu ambao unaishia kuharibu vitu vya kishetani lakini si kimharibu mtu..
Mfano wa wivu huu ni alikuwa nao Bwana Yesu juu ya Hekalu la Mungu, alipoingia na kukuta watu wanafanya biashara ndani ya hekalu, maandiko yanasema Bwana alizipindua meza zao, na kuharibu biashara zao lakini si kuwaharibu wao.. Na wanafunzi wake wakakumbuka andiko la wivu wa nyumba ya Mungu utamla (Yohana 2:17).
Wivu huu pia na sisi tunapaswa tuwe nao tunapoona kazi ya Mungu inachafuka, ni lazima tusimame kuziharibu hizo kazi za shetani kwa maombi na kwa mafundisho sahihi, lakini si kwa kuwadhuru watu au kuwatukana, au kuwaletea madhara yoyote ya kimwili.
Wivu wa namna hii pia upo katikati ya wanandoa na wanafamilia, kama kuna kiashiria chochote cha mwanandoa au mwanafamilia kutoka kwenye mstari wa uaminifu, au nidhamu, au maadili au heshima…Wivu wa namna hii huwa unanyanyuka!, sasa vibaya yule aliyemwaminifu, au aliye imara katika ndoa au familia kusimama na kuharibu au kuziba upenyo wowote ambao shetani anataka kuchukua nafasi ndani ya hiyo familia au ndoa…lakini kwa hekima pasipo kumdhuru mtu.
Lakini wivu wa wanandoa au wanafamilia unaoishia kuua huo hautokani na Mungu!.
Je na wewe unasumbuliwa na dhambi ya Wivu wa kidunia ambao unaishia kusengenya, kuona hasira, kuua, kutukana n.k Na hujui utatokaje katika hilo shimo?.
Bwana Yesu amekuja kwaajili ya kututoa katika hayo mashimo, kwa nguvu zetu hatuwezi kutoka huko wala kujitoa.
Nguvu pekee ya kututoa huko ni kwa njia kwa ya Roho Mtakatifu, kwa somo kamili kuhusiana na Roho Mtakatifu, jinsi ya kumpomea na jinsi.atakavyokuwezesha kushinda yale usiyoweza kuyashinda basi tutumie ujumbe inbox ili uweze kupata somo hilo.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.
USHUJAA WA ROHONI HAUANGALII UZOEFU WAKO.